Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Hapana Mtanganyika, sisi wote ni watu wazima hivyo ni vizuri tujiepushe kudanganyana iwe kwa makusudi ama bahati mbaya. Wanaounga mkono mapendekezo ya Tume ya Merekebisho ya Katiba ndio kidogo wanaweza kuwa na utetezi unao make sense kwamba maoni yao hayafungamani na chama chochote na sio vinginevyo. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu wengi wao ndio pekee hawakuiamini tume toka mwanzo kwamba ingeweza kuendesha zoezi kwa weledi kama ilivyokuja kutokea. Sababu ya kutoiamini tume ni kwamba kundi kubwa la wajumbe waliteuliwa na kiongozi mkuu wa chama tawala chenye sera ya muundo wa serikali mbili na awali waliunga mkono sera hiyo.Mag3, nitakupa majibu kutokana na maono yangu ambayo kwa kukupa ufafanuzi hayaambatani na CCM wala hayafungamani na chama chochote bali ni maono huru.
Really? Mtanganyika unajua mantiki ya Raisi wa nchi kutakiwa kuzindua kikao muhimu kama cha Bunge Maalum La Katiba kabla ya kuanza shughuli zake? Hilo ni jukumu lake kama Raisi...kufungua rasmi shughuli za Bunge hilo. Labda nikuulize swali dogo tu, je wakati Mwenyekiti wa Tume, Mh. Jaji Warioba Tume anawakilisha mapendekezo ya rasimu, kikao hicho cha Bunge Maalum la Katiba kiliishaanza rasmi?1. Nadhani utakubaliana na mimi haingii akilini kwamba Jaji Warioba apewe kiti kuzungumza baada ya Raisi, ukiangalia leadership protocol boss ndio anakuwa mzungumzaji wa mwisho. So, hili likuwa na more logical lakini wana siasa wame spin kuonyesha kwamba intention ilikuwa kuvunjavunja katiba ya jaji warioba.
Jakaya Mrisho Kikwete kama sehemu ya jamii alikuwa na haki zote za kusema yake ya moyoni lakini kwa wakati muafaka; huo ni wakati tume inakusanya, kuchambua na kuratibu maoni ya wananchi, kwa nini asubiri hadi rasimu inawakilishwa BMLK? Je wakati Tume inaendesha zoezi lake alikuwa hapewi ripoti na kama kuna maeneo ya mapendekezo yalimkera kwa nini hakuishauri tume aliyoiteua yeye mwenyewe mapema?2. Jakaya kama sehemu ya jamii alikuwa na haki ya kusema yake ya moyoni. Kwani Azimo la Arusha si lilikanwa mwalimu akiwa hai?
Huu utetezi unaoutoa hapa ndio kwanza unakuumbua na pili unaonesha ni wewe ndio umezama kwenye unachoita medieval age playbook ya CCM kwa kutetea yale yale. Tume ilipewa kazi ya kusikiliza, kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi na kazi hiyo waliifanya bila kutanguliza itikadi ya vyama vyao wala matakwa yao binafsi kama wajumbe.3. Tatizo la namba za serikali limeigawa Tanzania katika makundi, nadhani Jaji Warioba na kundi lake walishindwa kutumia utashi kuangalia njia mbadala ya kuridhisha pande zote yaani serikali mbili, tatu na sisi wa serikali moja. Kama warioba angejua hilo leo tusinge kuwa hapa tulipo. Instead wao walichotumia ni kuja na statistics ambazo mungu ndio anajua walipo zitoa na kutaka kusokomeza mzigo wa serikali ambao ungejaa mabwanyenye. Nadhani cha muhimu ingekuwa kutengeneza reconciliation panel ambayo ingefanya maridhiano kati ya wanao taka tatu na wale wa mbili na sisi wa moja. Hii ingepunguza makali, instead wamekwenda kwenye Medieval age playbook na kurudi na yaleyale,
Insanity: doing the same thing over and over again and expecting different results - Albert Einstein.
Sasa hapo ndipo mimi huwa nawapuuza watu kama wewe na awali sikutaka kabisa kujibu huu upuuzi uliouandika hapa; Mtanganyika tunaongelea rasimu ya katiba kama ilivyowasilishwa Bungeni na mwenyekiti wa Tume, rasimu haikutolewa na Chadema, CUF wala NCCR- Mageuzi. Wahafidhina ambao toka mwanzo hawakutaka mabadiliko na hata hiyo Katiba mpya hawakuona umuhimu wake wakala njama kwa kumtumia Raisi wao asiye na msimamo kuteka ajenda nzima ya Katiba mpya. Imedhihirika wazi kuwa wakati tume inazunguka ikikusanya maoni ya wananchi, hawa wahafidhina walijifungia wakaamua kuandika Katiba mafichoni.4. CCM wanatumia political tactique sababu wao sera yao kichama ni serikali mbili, sasa kama vile Ukawa wavyotumia mchezo wa kwamba serikali tatu ndio suluhu. Tofauti ni kwamba CCM wapo more organized, wanajua nini wanataka na UKAWA ni genge tuu ambalo bado halijajua linataka nini. That is a difference, hawa wako more organized na hawa wengine wapo wapo tuu. Leo wanaitwa TCD wanakwenda behind doors wanakubaliana na mchakato uendelee wakija kwenye majukwaa wanasema tumegomea, wapo kama kuku aliyekatwa kichwa, focus less. So, CCM wanatumia old playbook ambayo ni dirty politics always works.
Are you for real? Hebu nieleze niweze kuelewa maana ya kampeni, je kusambaza Katiba ya CCM siyo kampeni? Je wanayofanya viongozi wa CCM na redio TBCCM siyo kampeni? Kwa nini tunakuwa na kampeni wakati wa uchaguzi? Kwa nini watu wasiandike vipeperushi tu wakasambaza kwa wananchi? Kwa nini upande moja usambaze Katiba yao kwa wananchi lakini upande wa pili zitafutwe njia za kuwanyamazisha wasiwafikie wananchi?5. Mkuu kampeni za nini tena? Katiba isambazwe wananchi wasome mwenye kuipenda aseme ndio ambae anaikataa aseme hapana. Unataka tena kampeni za nini?
Unazikumbuka kampeni za orange na banana kwa jirani zetu Kenya? CCM inaogopa nini wananchi kulezewa mabaya ya Katiba iliyoandikwa na wahafidhina/mafisadi waliokubuhu kulinda malahi yao?
Duh! UKAWA ni muungano wa watu wenye vyama tofauti itikadi tofauti, sera tofauti, mitizamo tofauti n.k. lakini kama wameweza kushirikiana pamoja na kukataa hongo ya laki tatu kwa siku wakipigania kuheshimiwa kwa maoni ya wananchi wanastahili pongezi na si dhihaka. Wanapoamua kukutana na Raisi wanaonesha dhamira ya kutafuta maridhiano lakini mara zote na kwa bahati mbaya Raisi wetu hakuna alichoweza kuonesha zaidi ya udhaifu na mabadiliko ya msimamo mithili ya kinyonga.6. Tatizo kubwa ni moja mkuu walio upande wa pili wa sarafu ambao wana tetea serikali tatu wapo very disorganized, hawafamiki nini wanataka, mara wanagomea mara wanakutana na JK, hawajitambui. Sidhani tatizo lipo kwa vyombo vya usalama.
Waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2010 walikuwa 20,000,000. Kikwete alitangazwa mshindi kwa kura 5,000,000 sawa na asilimia 25%. Rasimu ya Katiba mpya kama ilivyowasilishwa na Tume ilikuwa izibe mianya kama hii inayotoa nafasi kwa matokeo ya kura kuchakachuliwa na kuruhusu kuhoji hali kama hiyo ikitokea. Waliozoea kuchakachua wameipiga teke rasimu yenye maoni ya wananchi na kuteua wezi na walaghai kutuandikia Katiba wakitanguliza maslahi kwa kulinda vya haramu walivyovichuma.nakataa kabisa kusema kwama kunaitajika ujasiri wakati unapiga kura ya siri. Hakuna ujasiri katika kusimama katika yale unayo amini. Mkubwa nadhani katika mikoa ya watu wenye uweleo na utashi Dar es Salaam iko juu sana, jee unaweza kuniambia kwa nini CCM wanashinda Dar es Salaam. Hawa watu wapo more inform labda kushinda mikoa yote ya Tanzania, lakini bado CCM wanaweka magoigoi na wanashinda. Unataka kuniambia kwamba hapa tusiseme kwamba sumu yetu ni sisi wenyewe.
Wachache wenye kuhoji uhalisia walikuwepo tangu wakati wa Mwalimu Nyerere, watu kama Kambona na wengine. Tatizo lilopo ni moja mfumo wa elimu na maisha unajenga wananchi wasio jitambua. Labda tufanye mapinduzi ya kifikra ndio tunaweza kushinda, vinginevyo hizi ni sauti za mwangu hazimtishi mpiga mbiu.
Stuart Silverstein - To come up with a new approach to an old problem, we often need to look at the problem differently. If we do the same things, we will get the same results. If we use our same bag of tricks, we will end up with the same magic show. In my experience, when a new solution was required, the best thing I could do (whether I was stuck or not) was to change my perspective on the problem. This could mean looking at new visuals, asking different questions or simply refining my language. Once you have explored new angles of a problem, be they visual, functional or strategic, you will often see something new, which will set you off on the road to creativity and true innovation. When all you see is the ear and leg, you usually just need the trunk to complete your view of the elephant.
Please take note Mtanganyika...CCM have run out of tricks, they are bound to end up with the same magic show.