Nguruvi, unarudia rudia argument za gharama over and over wakati tangu mwanzo niliweza kuweka side by side matumizi ya serikali ya Zanzibar na Tanzania, nikakwambia kwamba argument ya gharama haina sababu the cost is insignificant na hata ufanye IF analysis yoyote huwezi kuwa na significant cost.
Nimekwambia kwamba from security standpoint benefit outperform the cost. Na hapa ndio wengi hawapendi kupazungumzia lakini that is a fact.
Kwanza, elewa hakuna gharama za znz na Tanzania. Unapoongelea Tanzania unaongelea Tanganyika na Zanzibar. Huwezi kuwa na gharama za znz halafu za Tanzania. Logic inalazimisha usema gharama za Tanganyika na Zanzibar
Pili, ni makosa sana kutoangalia gharama za znz na kusema ni insignificant.Mifano kidogo
Zanzibar kama sehemu nyingine ya Tanzania inapata 4.5% ya pato la Tanganyika kwa jina la Tanzania.
Ukiacha mambo mengine, pato la Tanganyika tu ni Trilioni 12 kwa mwaka.
4.5 ya Trilioni 12 ni takribani Bilioni 400.Pato la znz ni bilioni 400 kwa mwaka.
Hivyo znz inaweza kuishi bila kufanya kazi kutegemeana na pato la Tanzania.
Ndio maana hawakusanyi kodi kwasababu mjomba Tanganyika atafidia uzembe wao
Kiasi hicho ni kikubwa kuliko pesa za wizara moja ya Tanganyika katika bajeti. Unawezaje kusema ni insignificant
2. Katika mikoa inayochangia pato la taifa Sumbawanga inachangia takribani Trilioni 1 kwa mwaka.
Pesa za maendeleo kwenda Sumbawanga ni chini ya bilioni 20, wakati znz inachukua zaidi ya bilioni 300.
Hayo yote yanatokea wakati znz ikiwa haichangii chochote katika muungano. Unawezaje kusema ni insignificant
3. Gharama za ulinzi na usalama, znz haijui. Ukichukua mfano mmoja tu wa kikosi kimoja cha jeshi kinachotumia bilioni 50 kwa mwaka, kwa znz hiyo ni sawa na asilimia 7. Yaani asilimia 7 hutoka Tanganyika.Ndivyo ilivyo kwa shughuli nyingine na wizara.
In short znz inachukua nusu ya bajeti ya wizara ya mambo ya ndani ya Tanganyika.
Unawezeje kusema ni indignificant.Hebu jiulize ni mkoa gani katika Tanganyika unaochukua kisasi hicho.
Mfano rahisi sana, Znz inaleta wanafunzi 1700 kwa jina la Tanzania,hudhaminiwa bure.
Kwa hesabu za mjadala, kama gharama ya mwanafunzi mmoja ni milioni 5 tu kwa mwaka hiyo ni sawa na 8.5 Bilioni.
Kumbuka hizi ni gharama za kodi, Tanganyika inabeba.
Watanganyika wanarudisha mikopo. Kwa wanafunzi 1,700 wa Tanganyika hilo ni deni na inabidi walipe.
Unawezaje kusema ni insignificant wakati haijawa insignificant kwa Tanganyika.
ZNZ haina uwezo wa kudhamini wanafunzi 1000,wanaokota mitaani 1,700 kwa kuwa hawana gharama, unawezaje kudharau kiasi hicho. Kama si kuokota kwanini SMZ idhamini wazanzibar tu 800 na kuleta 1,700 kwa gharama za kodi za Mtanganyika
Endapo kijana, ndugu au jamaa yako wa Tanganyika amekosa mikopo kwasababu pesa zimeelekezwa kwa wanafunzi 1.700 wa znz hiyo ni 100% maumivu na huwezi kusema ni insignificant.
Kwamba mwanafunzi amekosa masomo kwa haki ya mkopo, wakati yule wa nchi jirani ya zanzibar amepewa buree ikiwa ni kodi za mzazi wa Tanganyika. Insane!
Fikiria, mbunge mmoja tu wa znz asiye na manufaa yoyote Dodoma analipwa milioni 15.
Wapo wabunge 84, Kwa mwezi tu, achilia posho na gharama nyingine, ni takribani milioni 120.
Hawa wamekuja kuwakilisha znz si Tanganyika hivyo walipaswa kulipwa na SMZ.
Leo kuna Hospitali haina X-ray ya milioni 50 tu kwa mfano wakati pesa zinaelekezwa kwa watu 84 wasiotuhusu.
Unawezaje kusema ni gharama ndogo. Kwanini wasilipiwe gharama zao za matibabu na wake zao na SMZ iliyowaleta kutetea znz tu
Mwezi January, JMT ambayo ni Tanganyika imetoa bilioni 11 kupeleka umeme nchi jirani ya znz kule Pemba.
Fikiria, kiasi hicho kingeweza kudhamini wanafunzi wangapi wa Tanganyika wasio na mikopo.
Unawezaje kusema ni kiasi kidogo sana.
Gharama za bajeti ya SMZ anazibeba Mtanganyika, kwa tune ya bilioni zaidi ya 300.
Jiulize kiasi gani kinakwenda hospitali ya Muhimbili kwa miezi 3 halafu utumabie ni insignificant.
Orodha ni ndefu sana, ninachoweza kusema ni kuwa wakati znz haina machango wowote wa maana kiuchumi, uchukuaji wake umekuwa mkubwa kuliko mkoa wa DSM.
Leo unatuambia kiasi hicho ni kidogo. Halafu angalia idadi ya watu kama laki 600 tu wanapewa kiasi hicho huku wengine wakiishi bara na kuleta social constrains katika services kama Watanzania, ukweli ukiwa Mtanganyika ndiye mbeba mzigo huo.
Hivyo jaribu kuangalia kutoka kona mbali mbali uone jinsi watu 1.2M wanavyochota tu bila kuchangia halafu utazame watu milioni 45 wanaochangia jinsi wanavypopata. Hili unasema ni dogo sana! real
Kutoka security point of view, labda utueleze kwa dunia ya sasa ni security gani unayozungumzia.
Hatuna sababu za kuficha mambo, weka hadharani kwanini unadhani znz ni muhimu kwa security ya nchi.
Kama ni muhimu, huo umuhimu kwa katiba ya Chenge umelindwa vipi.
Tunachotaka wengine, kwanza, znz iwajibike kuchangia muungano.
Znz iache kudai misaada kutoka Tanganyika kama haki yao.
Na pili Tanganyika ipate fiscal autonomy yake bila kufungwa mikono na uwepo wa znz.
Tunataka znz iwajibike kwa gharama zinzaowahusu, kwa mfano wabunge wao walipwe na kodi zao kwa ajili yao.
Hatutaki kuwa na muungano ambao znz inatumia jina la Tanzania inapohitaji kukidhi dhiki zao.
Hilo sasa lazima lifike mwisho. Na pia watambue kuwa muungano wa dunia ya leo ni kiuchumi si kuchota na kulilia hovyo.
Hebu tuambie kuhusu security, nini kinachokutisha.