Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

https://www.youtube.com/watch?v=PCwc-W8mIuA

https://www.youtube.com/watch?v=P5t_842bXCs

https://www.youtube.com/watch?v=0HfChC3Uric

https://www.youtube.com/watch?v=LQLMhaNY7x0

https://www.youtube.com/watch?v=FlECaPDYzVQ

Wanaamvi

Tuliwahidi kuweka video za mkutano wa kamati ya maridhiano Bwawani znz dec 23 2014. Video zipo katika link hizo hapo juu
Pia kuna video ya CCM na jinsi walivyojadili katiba pendekezwa ya Chama chao iliyoandikwa na Chenge
Naomb mpitie video hizo ili mjadala ukiaendelea tuwe pamoja
 
YALIYOJIRI MKUTANO WA KAMATI YA MARIDHIANO, BWAWANI ZNZ 23 NOVEMBER

Yote yaliyojitokeza katika mkutano huo yapo katika uzi huu (video zitawekwa)

Waliokuwa wasemaji ni Mzee Hassan Moyo, Mzee Salim Rashid (Katibu wa kwanza wa baraza la mapinduzi), Mansour Himid, Jusa Ismail, Ali Salehe(Mjumbe wa iliyokuwa tume), Eddy Riyami na mshereheshaji Bimani.

Katika wazungumzaji wote, hakuna hata mmoja aliyesimama na kusema 'wazanzibar hawataki muungano''
Walichokuwa wanapigania ni kuwa na muungano wenye masilahi kwao.

Kuna sehemu moja Eddy Riyami alisema ''.... katiba ya Chenge ni kuendeleza ukoloni wa Watanganyika''

Nilimshangaa kama nilivyomshangaa Sheikh katika bandiko hapo juu.
Haiwezekani Wazanzibar watambue kuwa Tanganyika ni mkoloni, lakini waendelee kutafuta njia za kuishi na mkoloni huyo huyo.
Ingalikuwa vema kama wangeamua kuachana na mkoloni kuliko kubaki na duku duku mioyoni.

Mzee Salim Rashid,alifananisha ZNZ na ya Mauritius na Seychelles.
Akasema ZNZ inaweza kuwa na kipato cha mtu kikubwa kama nchi hizo mbili.

Alitaja idadi kama watu milioni 1.2.
Ninamshangaa Mzee Rashid kwasababu, hakuna sababu ya muungano na Tanganyika ikiwa znz inaweza kuendeleza watu wake.

Mzee Rashid hakueleza ukweli kuwa kati ya hao 1.2 nusu yao wamekimbilia Tanganyika wanakoishi bila tatizo.

Mzee Rashid aelewe mazingira ya Seychelles au Mauritius ni tofauti na ya znz.

Kijiografia znz inabaki kuwa katika kivuli cha Tanganyika kwa hiari au kwa lazima.
Si hiari au lazima ya mtu, bali mazingira yaliyotengenezwa na mwenyezi mungu.

Hata hivyo, badala ya kulalamika, alikuwa na wajibu wa kuhamasisha wznz wakatae muungano kabisa ili wawe kama Mauritius.

Mansour Himid, aliongelea sana kuhusu maridhiano. Alionyesha kuwa wapo watu wanaotaka znz kamili lakini hawawezi kusema kwa woga. Akasema, watu hao wakisikia jambo wanapanda ndege na kukimbia wakiacha msala kwa wenzao.

Hapa alikuwa anamsema Shemeji yake ambaye ni Karume kwa namna ya kiungwana sana.

Jusa alitumia muda mwingi kulinganisha katiba ya 1977, ya Chenge na ya ZNZ.
Alitumia taaluma yake kuonyesha jinsi katiba ya Chenge ilivyochukua nafasi ya ile ya 1977.

Na alionyesha ugumu uliopo hata pale katiba ya Chenge itakapolzimishwa. Ugumu huo unatokana na kubadili katiba ya znz ambayo ina masharti magumu.

Pamoja na umahiri wa kuelezea, Jusa aliacha ukweli na kuzungumzia mambo yasiyo na maana katika kuwapendeza wazanzibar.
Hapo ndipo tunasema, muungano upo katika matatizo makubwa.
Viongozi hawazungumzii ukweli, bali kupotosha watu wao pengine wakitaraji kupigiwa makofi.

Kwa mfano, badala ya kuongelea wingi wa viongozi wa katiba ya Chenge kwa kulinganisha na rasimu ya Warioba, Jusa aliongelea madaraka ya Rais wa znz katika katiba ya Chenge.

Tulidhani kuwa wananchi walitakiwa waelezwe, ile hoja ya gharama kubwa kwa S3 iimejibiwa vipi na rasimu ya Chenge.
Na hapa wznz walitakiwa waelewe zaidi kwani wao ndio wenye malalamiko na wao ndio hawaelewi hasa wanataka nini.

Kwanini hawawelewi!
Mansour kaonyesha picha ya wa kaskazini na kusini, waarabu na waswahili.
Kwasasa wanalaumiana, kwamba wale waliotengeneza katiba ya znz ya 2010 ndio wameenda kutengeneza katiba ya Chenge. Kwamba, kuna kusalitiana na kuisaliti znz.

Hoja hizo zimeungwa mkono na kauli za mzee Moyo, Eddy.

Lakini pamoja na kutojielewa na kutojua nafasi yao, wznz wanaficha ukweli kwa kumtuhumu Mtanganyika.
Mtanganyika wameshaelewa ni mkoloni, vipi wznz wamuunge mkono kama walivyofanya kwa Chenge?

Kuanzia leo tutakuwa na mjadala wa video za mkutano wa Bwawani kwa kila mzungumzaji.

Tutabainisha ukweli na kuonyesha upotoshaji.

Tusemezane

Nguruvi3,

Mimi siku zoote nawasifu sana waZnz kwa sababu ni wawazi na hawaogopi kitu. Wameweza na kudiriki mchana kweupeeeee KUUCHANA muungano na kama utaweka kumbukumbu zako vizuri Mh Sitta alipopeleka Rasimu ya muswada wa Katiba mpya pale Bwawani ilichukuliwa rasimu ile na kusiginwa bila kificho.

Nafikiri sote tuwape heko waZnz kwa uwazi wao.

Tukigeuza upande wa majirani zao TANGANYIKA.
1. Je wanaweza au kuwa na uthubutu wa kufanya kongamano kama hilo.
2. Je kuna MTanganyika UKIWEMO WEWE MWENYEWE mwenye uwezo wa kusema HAUUTAKI MUUNGANO? Mimi naona wengi kazi KUNUNG"UNIKA tu lakin hamuwezi kusema hadhwarani.
3. Hata Taasisi ya Nyerere ilipoandaa tu kongamano la kuzilinganisha KATIBA uliona wenyewe mlifanya fujo.

Sasa suala la kujiuliza HIVI HAIWEZEKANI KABISA TANGANYIKA KUSIMAMA BILA ZNZ? Kwanini Tanganyika inajificha nyuma ya PAZIA na kujitwika Utz.

Plz tafakur na fanya maamuzi.

Waachwe Znz wapumueeeee kwa raha zao

https://www.youtube.com/watch?v=PCwc-W8mIuA

https://www.youtube.com/watch?v=P5t_842bXCs

https://www.youtube.com/watch?v=0HfChC3Uric

https://www.youtube.com/watch?v=LQLMhaNY7x0

https://www.youtube.com/watch?v=FlECaPDYzVQ

Wanaamvi

Tuliwahidi kuweka video za mkutano wa kamati ya maridhiano Bwawani znz dec 23 2014. Video zipo katika link hizo hapo juu
Pia kuna video ya CCM na jinsi walivyojadili katiba pendekezwa ya Chama chao iliyoandikwa na Chenge
Naomb mpitie video hizo ili mjadala ukiaendelea tuwe pamoja

Nguruvi3,

Naona sasa ya Tanganyika yamekushinda na kuanza kudandia ya Znz. Hakika mambo ya Znz ni makubwa sana na yanataka mtu mwenye upeo wa juu wa uelewa na aliyeenda skuli sio kama wewe.

Labda nikudadavulie kidogo hapa. Kinachofanywa na Znz na kuilimishana na kubainishana MUUNGANO na mapungufu yake katika kuinua uchumi wa Znz.

Nitakupa kitu kidogo sana hapa kinacho wakwaza Znz hususan katika suala la UCHUMI WA NCHI hiyo. Najua inaweza kuwa darsa kubwa sana kwako kutokana na ilmu yako lakin nitaweka kiduchu kwa faida ya wasomaji wengine wenye ilmu na walioilimika.

Ikumbukwe kuwa miongoni mwa mambo ambayo yanachangia kukuza uchumi katika nchi ni UWEKEZAJI WA MOJA KWA MOJA KUTOKA NJE (yaani tunaita FOREIGN DIRECT INVESTMENT- FDI)

uwekezaji huu wa makampuni ya nje ni muhimu katika uchumi wa kileo chini ya biashara huru na utandawazi. Uwekezaji huu unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi husika.

Ukitazama kwa huko Tanzania SUALA LA UCHUMI SIO SUALA LA MUUNGANO lakin kwa sababu za mfumo wa Muungano uliopo suala hilo linatekelezwa kama suala la muungano.

Ikumbukwe kuwa Znz haimiliki sera za KIUCHUMI na hivyo inakuwa vigumu sana kuwashawishi wawekezaji wakubwa wa FDI kuwekeza maana wawekezaji wenye miradi mikubwa wanahitaji kwanza uhakika wa miradi yao kulindwa, mazingira mazuri ya kuwavutia, sera za fedhwa na kodi ambazo zote HAZIMO KATIKA MAMLAKA YA ZNZ.

mazingira ya Sasa yaliyopo ZNZ chini ya mfumo wenu wa Muungano yanampa ugumu muwekezaji kuvutika na kuwekeza Znz hasa akitazama utitiri wa kodi, kuna TRA, ZRB. Je ni mwekezaji gani atakwenda kuwekeza katika utitiri wa kodi namna hiyo.

Kumbuka kuwa FDI ina aina mbili za uwekezaji ambazo ni ULE WA FIXED ASSET na ule WA PORTFOLIO INVESTMENT ambazo zote zinachangia kukuza uchumi wa nchi husika.
( Darsa hili nitalichambua kwa kina katika forum ya uchumi).

Nisikuache hivi hivi nikupe kiduchu tena faida za FDI. ni kuongeza fursa za ajira, mapato kuongezaka, na kubadilishana technologies,utaalamu na kuongeza fedhwa za kigeni katika nchi.

Nguruvi.

najua ni darsa kubwa kwako lakin kiduuuchu nimekufumbua mambo uone KWANINI ZNZ WANATAKA UHURU KAMILI WA UCHUMI. Na darsa kama hizo za akina Jussa na wenzake ni kuwaandaa wananchi wajitambua na kuchukua hatua stahiki wakti unapotimu

POLE SANA.

Ahsante, wakati ukichambua katika forum ya uchumi yutakuja kujadiliana. Nausubiri huo uzi wako kwa hamu.

Mara nyingi napata taabu sana kujadiliana nawe. Mada iliyopo mbele ni video za wazungumzaji wa kongamano.
Hakuna aliyesema kongamano ni haramu, na hakuna anayesema maoni yao yana makosa.

Kinachozungumzwa hapa ni jinsi gani walivyogawanyika katika suala zima la muungano.
Kwa mfano, ukiangalia video, Bimani, Jusa na Ali Swalehe wanahimiza wananchi wajiandikishe ili kuweza kupiga kura ya hapana katika mchakato.

Kwa upande mwingine Mansour anaongelea kutoijadili kabisa katiba na kuiacha kama ilivyo.

Hapa kuna two school of thought.
Ya kwanza ni ya akina Bimani wanaotaka kura ya hapana. Kama umemsikiliza, Bomani amerudia mara nyingi ''haikubaliki, haipiti''

Ya pili, ni kuhusu Mansour anayetaka katiba ya Chenge isijadiliwe kabisa.

Hapa ndipo watu wanaotumia vichwa vyao wanapaswa kuvishgulisha ili kuleta maana kwa wasomaji na watu wengine.

Hakuna sababu za kuanza kuongelea mambo ya nje ya mada. Utaratibu wako wa kuvuruga mada unbakera kwa kweli.

Ningekushauri uanzishe uzi wako kuhusu yale unayodhani yanapaswa kujadiliwa.

Midhali unaingia katika nyuzi za wengine, nadhani kiustarabu na weledi unapaswa kuelewa na kuheshimu mawazo ya wengine.

Lakini pia ukumbuke kuwa kwavile unasoma na unachangia, basi darsa ni kubwa. Vinginevyo ungekuwa na darsa lako lenye akili zaidi na kuacha hili la wengine wajadiliane. Kinyume chake, kama unasoma na unachangia basi unakubali darsa

Narudia tena, vipi kama utaanzisha uzi wako na kusema unayotaka? Hili ni jukwaa huru.

Wanajamvi, tutaendelea kuziangalia video zote za kongamano na mkutano wa CCM

Nawataka radhi kwa usumbufu unaowapata. Hii ni jamii na tupo watu wa kila aina na mitazamo tofauti.

Barubaru ahsante sana kwa michango yako, tunaomba nafasi tujadili mada bila usumbufu usio wa lazima.
 
Nguruvi3.

Ndio maana kila wakti nakuhimiza ahali yangu kuwa skuli ni muhimu sana katika kupambanua mambo.

Unajuwa wewe umejikita kwa KUAMINI KUWA MAWAZO YAKO NI SAHIHI NA WENGINE HAWANA MAANA. Kumbuka kuwa katika majadiliano yoyoye laazima kuwe NA MGONGANO WA MAWAZO AU FIKRA na hicho ndio kinaitwa majadiliano. Kila Upande uinapata nafasi ya kutoa mawazo, fikra na mtazamo wao na kuwaachia wananchi wapime.

Kumbuka hata katika hiyo KATIBA PENDEKEZWA ya Chenga/ Sitaa wananchi watatakiwa KUIKUBALI AU KUIKATAA. Na sio wananchi kulazimishwa kuikubali au kulazimishwa wote waikatae hiyo ndio demokrasia.

Nimebainisha toka mwanzo kuwa SIASA ZA ZNZ zinataka mtu awe na uelewa wa hali ya juu sana na nikabainisha ZINATAKA UENDE SKULI na kuilimika bila hivyo utakwenda halijojo au mchomo kama ulivyokwenda wewe.

Makundi yote katika katika VIDEO hizo yana mitazamo yao na kila mtu anajaribu kushawishi lakin mwisho wa siku watafikia muafaka wa nini cha kufanya. Ikumbukwe kuwa waZnz ni waelewa na wamekwenda skuli sio wa kusukumwa kikondoo kama walivyo wengi katika majirani zao.

Kwa hiyo katika hiyo KATIBA pendekezwa laazima kutakuwa na makundi
1. wanaosema mkaipigie kura ya SIO na watakupa reasons zao.
2. Wanaosema mkaipigie kura ya NDIO na watakupa reasons zao.
3. Watakaosema msiende kabisa kupiga KURA na watakupa sababu zao.

Hiyo ndio inayoitwa demokrasio.

Na hata huko Tanganyika mkianza kampeni laazima yatajitokeza makundi kama hayo na ndio maana kunatolewa kipindi maalum cha kuilimishana kabla ya kufanya maamuzi.

Lakin kikubwa kinachonishangaza kwa sasa ni namna ulivyobadili upepo kwa kasi saaaana na kuacha yale manung'uniko yako
1. Wa TGK wanaibeba Znz kwa kuwalipia umeme, mishahara kwa wizara zote za muungano n.k
2. Wa TGK wanaipa pesa SUK Znz kulipa mishahara wafanyakazi wake na kuchangia bajeti ya Znz
3. Znz haichangii muungano na hivyo muungano kuchangiwa na Bara.

Na sasa umehamia kwa kulalamika.
KWANINI ZNZ HAWASEMI hatuutaki muungano?
Suala la kujiuliza manung'uniko hayo yamekwisha mpaka umegeuka hivyo? au ndio sarakasi za mjini ikijumlishwa na darsa tulizokupa zimekuingia na kuona ukweli kwanini pamoja na kufadhwiliwa kote Znz na bara (kwa jinsi ulivyokuwa unaamini) lakin baada waZnz wanadai uhuru zaidi wa kiuchumi?

Pole sana kwa sarakasi zako. Lakin ukisikia waZnz wanavyosasambua mambo bila shaka utajifunza mengi sana na utarudi katika mstari.

Mgongano wa mawazo within the paremeter and in sensible and logical way.

Tuna wachangiaji wengi tu tunaoyofautiana kimawazo na hilo tunalitamani sana litokee.

Kwa bahati mbaya, michango yako mara nyingi huacha mada, haisimami katika hoja , ni hafifu na dhalili.
Kwa mtu asiyekufahamu aghalabu hawezi kuamini kiwango chako cha elimu.Ulishaambiwa '' kila unapoingia kwenye mada, mada huchafuka''

Tunakushauri uache uzi huu wale wasio na shule wajadili, wewe mwenye skuli anzisha uzi wako.
Ni wakati sasa uanzishe uzi wako tutakuja kujadili.

Vinginevyo ukiwa katika mada za watu jadili yanayohusu mada, siyo matusi na kashfa.

Tunakushauri anzisha uzi, fanya counter argument tutachanngia.

Tunapoteza muda mwingi kujadili barubaru badala ya mada husika.

Lazima ifike mahali uone wajibu wako kwa jamii na kwamba unapaswa ujitambue jinsi unavyokera umma.

Tumekuambia ahsante kwa michango yako na hatuhitaji zaidi unless uanzishe uzi. Too low
 
https://www.youtube.com/watch?v=PCwc-W8mIuA

https://www.youtube.com/watch?v=P5t_842bXCs

https://www.youtube.com/watch?v=0HfChC3Uric

https://www.youtube.com/watch?v=LQLMhaNY7x0

https://www.youtube.com/watch?v=FlECaPDYzVQ

Wanaamvi

Tuliwahidi kuweka video za mkutano wa kamati ya maridhiano Bwawani znz dec 23 2014. Video zipo katika link hizo hapo juu
Pia kuna video ya CCM na jinsi walivyojadili katiba pendekezwa ya Chama chao iliyoandikwa na Chenge
Naomb mpitie video hizo ili mjadala ukiaendelea tuwe pamoja
Tutajaribu kuzipitia video hizi ili kubaini nakutafakari hali ya kisiasa Zanzibar

Tutaendelea....
 
Nguruvi3 swali kwako.

Mara kadhaa umekuwa ukiwakandamiza sana Wazanzibar kwamba wanabebwa na TGK sie wengine tulikuambia kwamba hawa wapeni nchi yao tuone kama watalalamika. Kwanini wewe usitumie nguvu hii ikubwa unayotumia katika kuwabeza badala yake ukawaelimisha wenyewe pamoja na TGK wajitoe katika muungano ambao wao wanaona wanadhulumiwa na ni kweli! Wakati wewe ukisema twawabeba? Yaani why wewe unatumia nguvu kubwa kuungana na CCM kuulinda muungano kwa kuwatisha na maneno kuwa nyie twawasaidia kwahyo mkiondoka katika muungano mtakuwa mmeumia?
 
Last edited by a moderator:

Sijui kama umedhamiria kusema hayo kwa ushahidi au ni kwa hisia.Tafadhalisana pitia rekodi zangu ili ujiridhishe na msimamo wangu kuhusu suala lamuungano.

Nadhani nivema ungeonyesha wapi nimewebeza katika video walizotengeneza wenyewe.

Nitawebezavipi ikiwa sijaanza hata kuzijadili hizo video.
Usiongozwe na prejudice,ongozwa na ukweli. Nimeweka video tu, unasema nimewebeza, ni wapi

Nyuz izipo wazi , chukua muda uzipitie.

Hatahivyo, kuna hoja moja kubwa wengi hawaielewi. Wenye malalamiko ya muda mrefu niwznz kuhusiana na muungano.
Watanganyikawachache waliokuwa na ufahamu kuhusu namna gano muungano ni mzigo kwao.

Ninazungumziasuala la muungano kwa pande zote sawia.
Kwabahati mbaya au nzuri, wznz wamejitokeza sana katika suala hili kama historiainavyoeleza.

Wakatiwote wa malalamiko hakuna kiongozi wa znz aliyesimama kuonyesha msimamo Zaidi yamsimamo wa pamoja wa znz huru yenye mamlaka kamili.

Leounasikia video kama ya Sheikh akilaani muungano halafu anadai haki ya muungano.Hapo hakuna la kujadili kweli.

Ukiziangaliavideo hizo, utaona hoja zinazokinzana. Kamati ya maridhiano ikisema hili, CCMznz wakisema lile. Hakuna la kujadili kweli.

Tatizola wengi hawataki kujadili mada, wanataka kusikia wanachotaka kusikia. Sisitunasema, hapana!
Kama ipo video ya Tanganyika iletwe, na tumeshaweka nyingi tu

Sasa kuonyesha udhaifu wa wznz katika kutafuta nchi yao, jambo ninaloliunga mkono kwa dhati kabisa, imekuwa dhambi kweli!

Nimalizie kwa kusema, rekodi zipo. Msimamo wangu ni ZNZ huru, Tanganyika huru.

Kama,narudia kama ipo haja ya kuisadia znz basi uwepo muungano. Nasema hivyokwasababu sijawahi kuonyeshwa kwa mantiki na hesabu, Tanganyika inanufaika vipina uwepo wa znz.
 
Waarabu tuna usemi (nitauweka katika lugha ya kiswahili) '' UKIWA MUONGO BASI USIWE MSAHAULIFU ''

Maneno haya ndio yanayojidhihirisha hapa. Wewe umekuwa kinara sana katika mtandao hoo wa JF katika kuibeza na kuisemea Znz vibaya kuwa

1. Wa TGK wanaibeba Znz kwa kuwalipia umeme, mishahara kwa wizara zote za muungano n.k
2. Wa TGK wanaipa pesa SUK Znz kulipa mishahara wafanyakazi wake na kuchangia bajeti ya Znz
3. Znz haichangii muungano na hivyo muungano kuchangiwa na Bara.

Leo naona unaruka na kuyakana maneno yako? Ahali yangu ogopa sana FASIHI ANDISHI kwani kila mtu anakusoma au unataka tukuwekee mada zako zinazoikashifu na kuibeza Znz kwa mtiririko wake hapa wote waone kuthibitisha maneno yangu?

Naomba jibu hapa ili nikubainishia na kukukumbusha kuwa umesahau uliyoandika mwanzo au uyakane maandiko yako.

Nilipo RED.
Rais wa Nchi ya Znz Mh Ali Mohd Shein msimamo wake na kundi lake wanataka Serikali mbili au mfumo kama ulivyosasa bali walitaka uboreshwe tu. makamo wa kwanza wa Rais wa nchi ya Znz maalim Seif Sharrif Hamad na kundi lake wanatetea Serikali Tatu kwa maana Serikali huru ya Znz, Serikali huru ya TGK na Serikali ya Muungano.

SASA TUBAINISHIE NI LINI ZNZ AU WAZNZ WALIKUWA NA MSIMAMO WA PAMOJA ?kama sio kuwalisha kauli waZnz na Znz kijumla?

Nguruvi3 swali kwako.

Mara kadhaa umekuwa ukiwakandamiza sana Wazanzibar kwamba wanabebwa na TGK sie wengine tulikuambia kwamba hawa wapeni nchi yao tuone kama watalalamika. Kwanini wewe usitumie nguvu hii ikubwa unayotumia katika kuwabeza badala yake ukawaelimisha wenyewe pamoja na TGK wajitoe katika muungano ambao wao wanaona wanadhulumiwa na ni kweli! Wakati wewe ukisema twawabeba? Yaani why wewe unatumia nguvu kubwa kuungana na CCM kuulinda muungano kwa kuwatisha na maneno kuwa nyie twawasaidia kwahyo mkiondoka katika muungano mtakuwa mmeumia?

Ahali yangu umenena.

Unajuwa Nguruvi3 siku zote anaamini kuwa analoandika anajuwa watu hawalisomi na kama wakisoma basi wanasahau mapema. LAKIN baya zaidi kwake ni kuamini kuwa anajuwa na anachobainisha hataki kiwe kihojiwe na kujadiliwa kwa mawazo tofauti na yake. NDIO MAANA KILA WAKTI NAMWAMBIA SKULI NI MUHIMU SANA KATIKA MIJADALA.

Mara zote nimekuwa nikimbainishia kuwa TGK ina watu zaidi ya 45 Milioni na Znz chini ya watu 1.5 Milioni. TGK ina area ya 885,800 sq Km na Znz chini ya 2,000 Sq Km. Na TGK ndio iliyojitwika Joho la TZ kwa maana kuwa Serikali ya TGK ndio hiyo hiyo Serikali ya JMTz.

Ukija Bunge Maalum la Katiba la Mh Sitta walikuwepo wajimbe zaidi ya 68% kutoka TGK na Wajumbe wote kutoka Znz walikuwa chini ya 32% . sasa kwanini walikataa kupitisha rasimu ya kutaka uwepo wa Serikali ya TGK? Je wa TGK wanaogopa nini kudai serikali yao ndani ya Muungano?

Kuna masuala meeengi sana katika huo muungano na uanzishwaji wa Serikali ta TGK kuliko majibu yake.

Ahali yetu sasa baada ya kushindwa ya TGK sasa yupo visiwani anajadili tofauti ya mitazamo yao bila kujua hiyo ndio demokrasia. nAJIULIZA MBONA HAJATUPA MTAZAMO WA WATGK KUHUSU MUUNGANO? Anasema tu mtazamo wangu ni Znz huru na TGK huru. Mbona hilo halikufanikishwa katika Katiba iliyopendekezwa?

Kwa lugha nyepesi tunaweza kumuita "ASHKI MAJINUUN" . Tafsiri ya neno hili ilitolewa na Mh Chombo , mbunge wa magomeni Znz wakti wakijadili kadhwia ya Escrow mjengoni.

Tumhurumie.

Tuwaache Znz wapumue kwa mijadala yao ya kuilimishana baila kubezwa wala kubanwa banwa. wajinafasi kwa raha zao.

Barubaru, umesema unaanzisha uzi, tafadhali kaanzishe tutakuja. Lau kana unajadili nyuzi za watu wengine basi ziwe katika viwango. Napata taabu baadhi ya watu wanaposema nikupuuze at the same time unaingia na kuharibu mjadala.
Please ahsante kwa mchango wako, tunasubiri uzi wako wa uchumi.

Hapa tumeshatosehaka na hoja zako dhaifu. Jasusi aliwahi kukuambia, hakuna mjadala unaochangia la maana zaidi ya kuharibu.
Hivi kwanini hujitambui hata unapopuuzwa! unaonekana kituko katika jamvi.

lengo lako ni kuharibu uzi ili tUsIjadili gizo video. Kama huwezi kuwa katika mada, basi usituondoe wengine kwa kuingiza hoja zisizo na maana. Please anzisha uzi kama ulivyosema, kama utabaki hapa uwe na adabu ya darsa. Too low PhD
 
Last edited by a moderator:
HOJA KINZANI

Kwa muda mrefu wzn wa pande zote wamekuwa mtsari wa Mbele kudai znz huru yenye mamlaka kamili.

Aliyekuwa waziri kiongozi Shamsa Vuai(CCM) aliwahi kukaririwa na TV star akieleza jinsi muungano usivyoitendea haki znz
Katibu mkuu wa zamani wa CUF na makamu mwenyekit Hamad Rashid aliwahi kuwa kiongozi wa serikali 3 zenye mamlaka kamili. Chama cha CUF kimegwanyika, Seif Hamada akitaka mkataba wakati Lipumba akitaka S3

Tume ya Warioba imekuja na pendekezo la S3 zilizoungwa mkono na wznz wengi kuliko 1 au 2 kwa kuangalia mkataba pia.

Wazanzibar waliungana kutengeneza katiba yao ya 2010 bila kujali vyama.
Lengo ni kuhakikisha znz inakuwa na mamlaka kamili.Hilo lilifanyika bila SMZ kukemea ukiukwaji wa katiba ya JMT

Hivyo ni haki kusema msimamo wa znz ni kutaka S3 na wala si kuvunja muungano.

Hakuna mahali ambapo kiongozi yoyote wa siasa wa znz amewahi kutamka vunja muungano.

Wakati wanaelekea Dodoma, mwanasheria mkuu wa znz aliwauliza wenzake kuhusu msimamo wao.

tuliona akina Kificho wakijiondoa taratibu na kusahau walikuwa na makubaliano katika BLW hata kama hayakuwa ya maandishi.
Kificho alisimamia katiba ya 2010 iliyodharau katiba ya JMT. Hivyo msimamo wake na wenzake ni znz yenye mamlaka. Fair enough

Watanganyika ambao wengi hawakujali muungano taratibu walifuatilia malalamiko ya znz.
Kubwa lililojitokeza, muungano ni wa Tanganyika katika kuendesha na wa Tanzania pale panapohitaji mafao kwa wazanzibar.

Hoja za wznz zilikuwa kurudi katika mambo 11 ya mkataba wa muungano wa 1964.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Watanganyika baada ya kubaini kuwa mambo 22 hayakuwa na mafao kwao bali mzigo wa huduma.
Hivyo walipendekeza kupitia tume ya Warioba yabakizwe machache.

Katika hali ya kawaida ilitegemewa wznz wakubali mambo kupunguzwa hadi 11.
Tume ya Warioba ikapunguza hadi mambo 7 ikitoa unafuu kwa kila upande kubeba mzigo wake.

Hilo likawashtua wznz ambao kiuchumi wanategemea JMT.

Ukisiliza video zote za CCM na kamati ya maridhiano, hakuna anayeongelea jinsi ya kuendesha muungano.
Hakuna anyeongelea muungano kwa faida ya pande zote.Hakuna anyeongelea gharama za muungano bali wote wanaongelea vyeo

Kinyume chake, wznz wamegeuka na kuwa waumini wa mfumo ule ule wa kikoloni walioulaani miaka mingi.

Wamegeuka na kukiri Nyerere waliyemwita laanatullah ni makosa. Mawazo yake ni muhimu kwao kuliko wakati mwingine.

Pengine tuangalie hoja moja baada ya nyingine.

Katika video ya CCM, waziri wa SMZ amekiri wznz wanapata nafasi za elimu ya juu nyingi kuliko SMZ inavyotoa, na hilo kalisema kama neema.

Hakueleza Watanganyika wanafadika na nini katika utaratibu wa S2 anaouelezakutoka znz. Ikumbukwe hizi ni nchi sawa na hivyo zinapaswa kuhudumiana na si moja kuwa mgongoni kwa nyakati za dhiki na kudai usawa wakati wa faraja.

Lakini waziri alikuwa na hoja muhimu sana. Kwamba, katika muungano huu znz ni tegemezi na kilichopatikana ni neema kwa maana ya mgongo wa Mtanganyika utagharamia. Waziri ameonyesha kuwa znz inanufaika na muungano na wala si Tanganyika kwa hoja yake moja tu rahisi sana.

Waziri wa muungano, Samia suluhu amesema, upo utaratibu na formula imepatikana kupata ajira za BoT na TPDC.

Wakati huo huo Rais na waziri wa nishati na ardhi wa znz wanasema, mafuta na gesi si ya muungano kwa mujibu wa katiba ya Chenge wanayoipigia debe.

Hapa kuna maswali ya kujiuliza. Hivi kama mafuta na gesi si ya muungano, wapi wznz wanapata mtima na nguvu za kudai ajira TPDC ambayo haina masilahi na wala haiwahusu?Hoja hii inaeleza tatizo walilo nalo wznz la umimi.

Ndiyo hoja aliyozungumza sheikh katika video nyingine.
Sheikh kaita muungano Dubwana baya sana. Halafu kaomba uwepo unafuu wa makontena ya znz kuingia katika Tanganyika kwa sababu ni muungano. Hapa inakuwaje, kwamba anaomba fadhila kutoka kwa dubwana baya sana. Je, alielewa anaongelea nini.

Sheikh kasema elimu ya juu si suala la muungano na halipaswi kuwa hivyo kwasababu linadumaza znz kielimu.
Waziri wa SMZ anasema wznz wananufaika sana na nafasi za elimu ya juu kuliko SMZ inazotoa.
Hapa wanajamvi mnaelewa nini !

Ndivyo waziri Samia, Sheina na waziri Abdallah wanavyojichanganya.
Kama mafuta na gesi si ya muungano, wapi wanaingia katika maeneo kama TPDC?

Wakati huo huo, kamati ya maridhiano inasema suala hilo bado halijapata ufumbuzi.
Rais wa Tanzania ndiye mwenye ardhi na mafuta yapo ardhini. Hivyo kuna utegemezi wa Rais wa JMT katika kutafuta mafuta.

Hoja kama hizi zinachanganya na kujiuliza endapo wznz wanaelewa hasa nini wanataka.
Mgaongano wa mawazo si jambo baya, lakini lazima uwe katika mantiki.

Haiwezekani mtawaliwa akashangilia zawadi kutoka kwa mkoloni(CCM), na anayepinga ukoloni akataka kuwepo na muungano na mkoloni yule yule asiyemtaka(KAMATI YA MARIDHIANO)

Kuna mgongano wa mawazo, kinachoonekana kwa wenzetu ni zaidi ya hapo.

Hoja zaidi za wasemaji zinachambuliwa kutoka katika video zao wenyewe

Tutaendelea
 
Barubaru, umesema unaanzisha uzi, tafadhali kaanzishe tutakuja. Lau kana unajadili nyuzi za watu wengine basi ziwe katika viwango. Napata taabu baadhi ya watu wanaposema nikupuuze at the same time unaingia na kuharibu mjadala.
Please ahsante kwa mchango wako, tunasubiri uzi wako wa uchumi.

Hapa tumeshatosehaka na hoja zako dhaifu. Jasusi aliwahi kukuambia, hakuna mjadala unaochangia la maana zaidi ya kuharibu.
Hivi kwanini hujitambui hata unapopuuzwa! unaonekana kituko katika jamvi.

lengo lako ni kuharibu uzi ili tUsIjadili gizo video. Kama huwezi kuwa katika mada, basi usituondoe wengine kwa kuingiza hoja zisizo na maana. Please anzisha uzi kama ulivyosema, kama utabaki hapa uwe na adabu ya darsa. Too low PhD

Nguruvi3,

Labda nikukumbushe kwa mara nyingine tena Binafsi huwa nilishakupuuza toka zamani mara baada ya kuona mtazamo wako na kukuweka katika watu wenye uchache wa ilmu LAKIN MARA ZOTE NASUKUMWA NA WATU KUKUJIBU HOJA ZAKO HUSUSAN UNAPOJARIBU KUPOTOSHA MAMBO HUSUSAN YANAYOKHUSU ZNZ.

Mimi naamini wazi na mara zooote nakukhusia kuwa USIJADILI JAMBO KAMA HUNA UJUZI NALO. na kama umenisoma katika mada zangu kukujibu wewe huwa natanguliza neno SKULI NI BORA KATIKA MAJADILIANO kwa maana kuwa ongeza ilmu ili uongeze ufahamu wako.

HITIMISHO langu kwako ambalo mara zote nakwambia ACHANA KABISA KUZUNGUMZIA MAMBO YA ZNZ ambayo huna ujuzi nayo UONE KAMA UTAKUTANA na mimi katika majailiano yoyote.

Kama hu muelewa mada zote tunazokumbana na wewe ni zile unapojaribu kuzua maneno na kuwalisha waZnz kwa nia ya kujipatia umaarufu. Kumbuka kuwa kwalo hatutarudi nyumba tutakujibu na kubainisha ukweli japo wewe utakuuma kama unavyokuumiza huu ukweli ninaokupa.

Discuss mambo ya Bara utakuwa salama , ukigusa Znz basi hapo ni moto hatutakuacha.

Narudia tena skuli ni muhimu sana. Nakushangaa unaposema Low PhD Mmh kumbuka pia imepitia Udsm (Tz), Carleton Univ (Canada) na Sophia Univ (Jpn) sio vyuo vya st.. st.. st..
 
HOJA KINZANI

Kwa muda mrefu wzn wa pande zote wamekuwa mtsari wa Mbele kudai znz huru yenye mamlaka kamili.Hapa ungeweka wazi ni pande gani hizo. maana CCM wanataka muundo huo huo wa muungano uboreshwe na Upinzani wanataka Znz yenye mamlaka kamili . sasa kuna misimamo ya CCM na CUF. tufafanulie hiyo pande zote unazodai weye?

Aliyekuwa waziri kiongozi Shamsa Vuai(CCM) aliwahi kukaririwa na TV star akieleza jinsi muungano usivyoitendea haki znz
Katibu mkuu wa zamani wa CUF na makamu mwenyekit Hamad Rashid aliwahi kuwa kiongozi wa serikali 3 zenye mamlaka kamili. Chama cha CUF kimegwanyika, Seif Hamada akitaka mkataba wakati Lipumba akitaka S3. hizo zote ni tofauti ya mitazamo na ndio inayoitwa demokrasia lakin mwisho wa siku wanakuja na wazo moja tu ambalo ni S3

Tume ya Warioba imekuja na pendekezo la S3 zilizoungwa mkono na wznz wengi kuliko 1 au 2 kwa kuangalia mkataba pia.

Wazanzibar waliungana kutengeneza katiba yao ya 2010 bila kujali vyama.
Lengo ni kuhakikisha znz inakuwa na mamlaka kamili.Hilo lilifanyika bila SMZ kukemea ukiukwaji wa katiba ya JMT.Hapa nafikiri Bunge la JMTz walitakiwa wafanye kama walivyofanya kuhusu issue ya Znz kujiunga na OIC. kwanini walishindwa kukemea hilo na kuufyata. Jeulize Bunge la JMTz lilipata kigugumizi gani kukemea uvunjwaji huo wa sharia?

Hivyo ni haki kusema msimamo wa znz ni kutaka S3 na wala si kuvunja muungano.huu ni msimamo wa upinzani mara bada ya kujadiliana kwa kina kuhusu aina ya muungano. Na msimamo huu hata TGK wanao pia CHADEMA, NCCR na CUF na vyama vingine vya upinzani. HAKUNA UPINZANI AU CHAMA TAWALA KINACHOTAKA KUVUNJA MUUNGANO SIOTU KUTOKA ZNZ BALI HATA TANGANYIKA. NIELEZE KAMA KUNA MSIMAMO HUO KUTOKA BARA?

Hakuna mahali ambapo kiongozi yoyote wa siasa wa znz amewahi kutamka vunja muungano.

Wakati wanaelekea Dodoma, mwanasheria mkuu wa znz aliwauliza wenzake kuhusu msimamo wao. JE UNAWEZA KUTUELEZA MSIMAMO WA TANGANYIKA ULIKUWA NINI?

tuliona akina Kificho wakijiondoa taratibu na kusahau walikuwa na makubaliano katika BLW hata kama hayakuwa ya maandishi.
Kificho alisimamia katiba ya 2010 iliyodharau katiba ya JMT. Hivyo msimamo wake na wenzake ni znz yenye mamlaka. Fair enough . KUMBUKA PIA HATA AFISI YA WAZIRI MKUU PINDA AMBAYO NAYO ILITAKA S3 ILIIKANA HABARI HIYO ACHILIA MBALI BUNGE LA MUUNGANO?

Watanganyika ambao wengi hawakujali muungano taratibu walifuatilia malalamiko ya znz. HATA WAzNZ NAO WALIFUATILIA MALALAMIKO YA JIRANI ZAO TGK YALIYOBAINISHWA NA AKINA MH KESSY, TUNDU LISU NA WENGINE
Kubwa lililojitokeza, muungano ni wa Tanganyika katika kuendesha na wa Tanzania pale panapohitaji mafao kwa wazanzibar.

Hoja za wznz zilikuwa kurudi katika mambo 11 ya mkataba wa muungano wa 1964. JE UNAWEZA KUTUDADAVULIA HOJA YA TANGANYIKA ILITAKA MRUDI KATIKA MAMBO MANGAPI YA MUUNGANO?

Hoja hiyo iliungwa mkono na Watanganyika baada ya kubaini kuwa mambo 22 hayakuwa na mafao kwao bali mzigo wa huduma.JE INAINGIA AKILINI ANAEBEBWA AOMBE YAPUNGUZWE LAKIN ANAYEBEBA ASIWE NA MAWAZO. HUO SI UZUZU KWELI AU NDIO UZEZETA?
Hivyo walipendekeza kupitia tume ya Warioba yabakizwe machache.

Katika hali ya kawaida ilitegemewa wznz wakubali mambo kupunguzwa hadi 11. JE WATANGANYIKA WALITAKA YAONGEZWE AU KUPUNGUZWA MPAKA MANGAPI?
Tume ya Warioba ikapunguza hadi mambo 7 ikitoa unafuu kwa kila upande kubeba mzigo wake.

Hilo likawashtua wznz ambao kiuchumi wanategemea JMT. SASA KAMA LILIWASHTUA WA ZNZ, KWANINI ILE KURA YA MAAMUZI YA KATIBA YA SITTA/CHENGE ILIPATA WAKTI MGUMU ZNZ NA SIO TGK?NAFIKIRI MAJIBU YA ILE KURA ILITAKIWA KUWA DARSA KUBWA KWAKO IMA WA TGK VIGEUGEU KIMSIMAMO KAMA ALIVYO MB KESSY AU ...

Ukisiliza video zote za CCM na kamati ya maridhiano, hakuna anayeongelea jinsi ya kuendesha muungano.
Hakuna anyeongelea muungano kwa faida ya pande zote.Hakuna anyeongelea gharama za muungano bali wote wanaongelea vyeo. SKULI MUHIMU SANA. SI TU BUNGE LA KATIBA YOTE HAYO YALISASAMBULIWA NA MH JUSSA NA HATA TUNDU LISSU ALIBAINISHA NA MH JUMA DUNI. NAOMBA PITIA ANSARD ZA BUNGE HILO USIKILIZE VIZURI BADALA YA KUZUA MAMBO HAPO BARZANI

Kinyume chake, wznz wamegeuka na kuwa waumini wa mfumo ule ule wa kikoloni walioulaani miaka mingi. MFUMO GANI HUO?

Wamegeuka na kukiri Nyerere waliyemwita laanatullah ni makosa. Mawazo yake ni muhimu kwao kuliko wakati mwingine. HILO LIPO WAZI ZNZ NA MAWAZO YAKE YALIPINGWA KILA KONA. Pitia kadhia ya Mzee Jumbe.

Pengine tuangalie hoja moja baada ya nyingine.

Katika video ya CCM, waziri wa SMZ amekiri wznz wanapata nafasi za elimu ya juu nyingi kuliko SMZ inavyotoa, na hilo kalisema kama neema. WACHUMI TUNASEMA HAKUNA NEEMA NI UDHALILI TU NA NDIO WANADAI UHURU KAMILI WA KIUCHUMI NA HUO NDIO MSIMAMO WA UPINZANI WOTE HUKO TANZANIA (TGK na ZNZ) NDIO MAANA WANATAKA S3

Hakueleza Watanganyika wanafadika na nini katika utaratibu wa S2 anaouelezakutoka znz. Ikumbukwe hizi ni nchi sawa na hivyo zinapaswa kuhudumiana na si moja kuwa mgongoni kwa nyakati za dhiki na kudai usawa wakati wa faraja.

Lakini waziri alikuwa na hoja muhimu sana. Kwamba, katika muungano huu znz ni tegemezi na kilichopatikana ni neema kwa maana ya mgongo wa Mtanganyika utagharamia. Waziri ameonyesha kuwa znz inanufaika na muungano na wala si Tanganyika kwa hoja yake moja tu rahisi sana. NILIWAHI KUULIZA HUKO AWALI KUWA KWANINI SERIKALI YA JMTz INAPATA KIGUGUMIZI KUTEKELEZA SHARIA YA BUNGE LA JMTz YA KUUNDWA ACCOUNT YA PAMOJA YA UCHUMI NA FEDHWA (JOINT FINANCE COMMISSION) WACHUMI TUNAJIULIZA KUNA SIRI GANI HUKO TGK

Waziri wa muungano, Samia suluhu amesema, upo utaratibu na formula imepatikana kupata ajira za BoT na TPDC. SIO TU BOT NA TPDC KINACHOTAKIWA NI KUWA NA FORMULA KATIKA WIZARA NA IDARA ZOOOOTE ZA MUUNGANO. KWANI MUUNGANO SIO TU TGK NA ZNZ WAMO. NJE YA ZNZ HAKUNA TZ.

Wakati huo huo Rais na waziri wa nishati na ardhi wa znz wanasema, mafuta na gesi si ya muungano kwa mujibu wa katiba ya Chenge wanayoipigia debe.

Hapa kuna maswali ya kujiuliza. Hivi kama mafuta na gesi si ya muungano, wapi wznz wanapata mtima na nguvu za kudai ajira TPDC ambayo haina masilahi na wala haiwahusu?Hoja hii inaeleza tatizo walilo nalo wznz la umimi. NDIO MAANA NIKASEMA USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA KIZA. TPDC SIO CHOMBO CHA MUUNGANO , NI VIPI WAINGIE MKATA WA KWENDA KUTAFUTA MAFUTA KWENYE ENEO LA NCHI YA ZNZ? MAMBO HAYA PIA YALIKUWA YANAFANYWA NA BODI YA WAHANDISI (ERB), BODI YA MAKANDARASI (CRB) BODI YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA MAHISABU etc. kuweza ku operate mpaka Znz wakti wao sio vyombo vya muungano

Ndiyo hoja aliyozungumza sheikh katika video nyingine.
Sheikh kaita muungano Dubwana baya sana. Halafu kaomba uwepo unafuu wa makontena ya znz kuingia katika Tanganyika kwa sababu ni muungano. Hapa inakuwaje, kwamba anaomba fadhila kutoka kwa dubwana baya sana. Je, alielewa anaongelea nini. NAFIKIRI HILI NILILIFAFANUA KIDOGO HUKO JUU NA NIKABAINISHA NITASASAMBU KWA KINA KUHUSU MFUMO WA MUUNGANO WA SASA UNAVYOIGANDAMIZA NA KUINYONYA ZNZ KATIKA MADA MAKHSUS

Sheikh kasema elimu ya juu si suala la muungano na halipaswi kuwa hivyo kwasababu linadumaza znz kielimu.
Waziri wa SMZ anasema wznz wananufaika sana na nafasi za elimu ya juu kuliko SMZ inazotoa.
Hapa wanajamvi mnaelewa nini ! HIYO NI MITAZAMO TOFAUTI TU NA KILA MTU AMEBAINISHA HOJA ZAKE ALIZOSIMAMIA

Ndivyo waziri Samia, Sheina na waziri Abdallah wanavyojichanganya.
Kama mafuta na gesi si ya muungano, wapi wanaingia katika maeneo kama TPDC?

Wakati huo huo, kamati ya maridhiano inasema suala hilo bado halijapata ufumbuzi.
Rais wa Tanzania ndiye mwenye ardhi na mafuta yapo ardhini. Hivyo kuna utegemezi wa Rais wa JMT katika kutafuta mafuta. UKISOMA KATIBA PENDEKEZWA NA ILE RASIMU YA PILI YA WARIOBA UTAPATA DARSA KUBWA SANA HAPA. KWANI WARIOBA AMEDADAVUA VIZURI SANA NA UTAONA UCHAKACHUWAJI ULIOFANYWA NA BUNGE LA KATIBA LA CHENGE/SITTA. YAPO MENGI LAKIN HILO NDIO TUNASEMA NI MUSWIBA MKUBWA SANA KWA TGK

Hoja kama hizi zinachanganya na kujiuliza endapo wznz wanaelewa hasa nini wanataka.
Mgaongano wa mawazo si jambo baya, lakini lazima uwe katika mantiki.NI MANTIKI GANI HIYO UNAYOITAKA WEWE. MBONA MGONGANO HUO HATA TGK UPO BAINA YA UPINZANI NA TAWALA. UPINZANI UNATAKA SERIKALI ZA MAJIMBO WAKTI TAWALA WANATAKA MFUMO WA MIKOA? AU UKITOKEA ZNZ BASI IMEKUWA NONGWA?

Haiwezekani mtawaliwa akashangilia zawadi kutoka kwa mkoloni(CCM), na anayepinga ukoloni akataka kuwepo na muungano na mkoloni yule yule asiyemtaka(KAMATI YA MARIDHIANO)

Kuna mgongano wa mawazo, kinachoonekana kwa wenzetu ni zaidi ya hapo.LABDA UTUWEKE WAZI NI KIPI HICHO? BARZANI HAPA WE FUNGUKA TU NA KAMA ITAKUPURUCHUKA TUTAKUWEKA SAWA.

Hoja zaidi za wasemaji zinachambuliwa kutoka katika video zao wenyewe

Tutaendelea

Nguruvi3,

Nimejitahidi kukuweka sawa katika MANUNG'UNIKO yako mbali mbali uliyobainisha hapo juu.

Lakin kwa mtu timamu akikusoma BASI ATAGUNDUA NI CHOYO NA KHUSDA tu zinakusumbua kuhusu Znz na waZnz. kwani umepata makengeza katika kuangalia hoja zako na kutazama upande wa Znz tu bila kuangalia na upande wa TGK.

Waswaili wanasema JITAKASE KABLA KUMNYOOSHEA MWENZAKO KIDOLE.

ZNZ HURU ILEEEEEEEEE. Waachwe ZNZ wapumue na kujinafasi kwa raha zao.

MHESHIMIWA JUSA AONGELEA UMAKAMU WA RAIS

Katika video za maridhiano six, mh Jusa ameongelea umakamu wa pili wa Rais kwa umakini, lakini pia kwa kupotosha
Mtakumbuka Jumbe alikuwa makamu wa kwanza wa Rais. Yaliyomkuta tunayajua.

Kuondolewa kwake ni kutokana na nafasi yake kama makamu wa Rais na wala si Rais wa Zanzibar
Jumbe aliitwa Dodoma na yaliyoendelea ni hadithi

Kabla ya BMK kuvugika, tulizungumzia hili. Warioba/tume walifanya busara kutenga muungano, Tanganyika na Zanzibar
Kutenga nafasi hizo kulilenga kutoa mamlaka kamili ya nchi hsuika bila kuingiliwa.
Kwa mujibu wa video, WanaCCM wa znz wanashangilia Rais wa znz kuwa makamu wa Rais

Jusa anasema, umakamu wa Rais kwa mujibu wa katiba ya Chenge inayopigiwa upatu na CCM znz, Rais wa znz atakuwa makamu daima. Hili linahakikisha kuwa hakuna siku znz itakuwa na Rais wa JMT. Hoja ya Jusa ni ya kweli

Pili, Jusa amesema, kwa itifiki Rais wa znz ambaye ni makamu hatashika wadhifa wa Urais ikitokea Rais hayupo.
Atakayekaimu nafasi hiyo ni makamu wa pili wa Rais ambaye ni waziri mkuu wa Tanganyika.

Jusa kasema, hilo ni kumuondolea Rais wa znz hadhi, kwani kikao cha baraza la mawaziri, waziri mkuu wa Tanganyika ndiye atakuwa mwenyekiti na Rais wa znz mjumbe.
Jusa anaendelea, Rais wa znz anachaguliwa, hivyo anapokuwa chini ya waziri mkuu wa Tanganyika wa kuteuliwa ni kumdhalilisha. Hilo lina ukweli.

Hata hivyo anapotosha kwa kutoangalia kwa umakini na mantiki.
Kwanza, Rais wa znz anachaguliwa na watu chini ya laki 5. Mbunge wa Tanganyika anachaguliwa na watu zaidi ya milioni.

Mfano, Jimbo la ubungo wapiga kura tu ni zaidi ya milioni moja. Hivyo, mbunge wa Tanganyika anapochaguliwa kuwa waziri mkuu, bado ana uhalali wa kidemokrasia kluliko Rais wa znz kwa mambo mengi.

  1. Kachaguliwa na watu wengi kuliko Rais wa znz
  2. Ana wajibu mkubwa kwa watu milioni 41 na uchumi unaonedesha muungano. Hivyo, hadhi yake katika msingi wa demokrasia, ulinzi na usalama pamoja na uchumi ni kubwa kuliko Rais wa znz
  3. Rais wa znza anachaguliwa na wznz,anpo kuja kutawala Tanganyika ni kama kuazima kiongozi.
  4. Makamu wa Rais ambaye ni mgombe mwenza ana uhalali zaidi ya Rais wa znz ambaye Watanganyika hawajui kapatikana kwa njia zipi. Hapa ndipo Watanganyika wanatakiwa wajiulize, hivi imefika mahali kiongozi wa taifa anaweza kupatikana kutoka popote tu bila kujali kapatikana vipi.
    Ukimsikiliza Jusa kwa makini, ana hoja za msingi ambazo sijui kama wzn wanaweza kuzitazama kwa jicho mujarabu.

    Rais wa znz anapokuwa makamu, tayari hadhi yake inapungua.
    Rais huyo atakuwa ni makamu wa Rais wa JMT na hivyo uwezekano wa kwenda kinyume na matakwa ya JMT haupo.
    Hatakuwa na nguvu za katiba ya znz bali atawajibika kwa katiba ya JMT aliyoapa kuitetea. Katiba ya znz itakuwa ni muongozo tu kama Standard operatig procedure kwake, sheria atakayosimama nayo ni ile ya JMT

    Na endapo atajaribu kinyume na katiba ya JMT, historia ya Jumbe itajirudia. Ataitwa na kukabidhi funguo za ofisi.

    Je hayo ndiyo mamlaka wanayozungumzia? Je, Warioba aliwaonea au aliwasadia?

    Tusemezane
 
https://www.youtube.com/watch?v=PCwc-W8mIuA

MZEE SAID SALIM RASHID MAULID (Video 2/5)

KAWATUKANA WATANGANYIKA ''HAWA WA SIKU HIZI SI WASTAARABU KAMA WALE WA MIAKA YA 50'' !!!

Mzee Maulid ni katibu mkuu wa kwanza wa baraza la mapinduzi
Ameongea mambo mengi katika mchanganyiko, wa ukweli, upotoshaji na hata dharau na aina ya tusi

Mzee Maulid, ansema znz imekuwepo miaka zaidi ya 600 iliyopita,akonyesha lini Waingereza walikuja na hadi ilopifikia.
Hapa mzee maulid kasema, Tanganyika haikuwepo tena akisisitiza miaka 100 iliyopita.

Haieleweki alizungumzia katika mantiki gani, hata hivyo inatosha kusema hakuna taifa duniani lililojitokeza kuanzia siku ya kwanza ya uwepo wa dunia. Hiyo znz anayoongelea wakazi wake ni Watanganyika waliohamia.
Ndio maana kuna vurugu za akina ASha Bakari wakidai wao ndio wznz (video ya CCM) na Waarabu aliyozungumzia Mansour (3/5) na Eddi Riyami

Mzee Maulid hajatambua hitilafu ya rangi iliyopo, anawadanganya wznz kuzaliwa hapo dunia ilipoanza.

Nchi kama Australia, Marekani, Afrika kusini n.k. ziliundwa tu kutokana na nyakati.
Tanganyika ilikuwepo pengine si kwa jina bali kwa uwepo kama pande la ardhi na viumbe wake.
Historia inazidi kuonyesha mwanadamu wa awali kuishi Tanganyika pengine kwa umri zaidi kuliko maeneo mengine.

Mzee Maulid anasema kwa mara ya kwanza alifika Tanganyika mwaka 1950 na kukuta watu watulivu na wastaarabu.

Mahali anaposhangaza ni pale anaposema watu hao si kama wanaonekana siku hizi.
Haijulikani tofauti za miaka ya 50 na sasa ni zipi na tofauti za Watanganyika ni zipi.

Hili ni tusi, kwasababu Watanganyika ni wale wale na haieleweki mzee alilenga nini anaposema wale wa zamani si hawa wa siku hizi

Hata hivyo, hawa wa ''siku hizi'' ndio walipa kodi, walinzi wa usalama wa znz na wala mzee Maulid hajaliongelea hilo

Hakuna shaka, mzee Maulid alilenga kauli chafu ya kuwatukana Watanganyika, wale wastaarab aliowakuta na hawa wasio wastaaraba wa siku hizi. Inasikitisha mzee wa umri wake kuishi katika dunia ya aina hiyo

Hili ni tusi zito sana kwa Watanganyika kutoka kwa mwanapinduzi Salim Said Rashid.

Mzee Maulid anapswa kuomba radhi kwa tusi lake dhidi ya Watanganyika. Muungano si sababu ya kuwatukana na kuwadhililisha Watanganyika kama wanayama wa porini, wale wa miaka ya 50 na hawa wa siku hizi! Hili ni tusi zito sana

Na Watanganyika wanapswa kuona jinsi muungano wanaoumenyekea unavyowalipa kauli za matusi kama za mzee Maulid
Kauli ya mzee Maulid, inaonyesha uhalisia wa wznz na jinsi wanavyowaona Watanganyika, pengine kama viumbe tofauti duniani

Mzee Maulid anaonyesha uchumi wa nchi za Mauritius, Seychelles na Tanzania.
Hapa alilenga kuonyesha kuwa znz inaweza kuwa sawa na nchi hizo katika hali za kimaisha akimaanisha maisha bora.
Huo unaweza kuwa ukweli na unaweza kuwa upotoshaji.

Mzee Maulid hakuongelea COmoro, Haiti, Vanuata, Trinidad and Tobag, st Lutia ambavyo ni visiwa kama znz.

Endapo alimaanisha znz inaweza kuwa na Seychelles, bila shaka alipaswa kueleza uwezekano wa kuwa kama Comoro.

Hivyo hoja ya Mzee Maulid wala isingekuwa muungano, ingekuwa kuvunja muungano ili znz iwe kama Mauritius.

Hoja yake inapangina na ya msemaji aliyemtangulia Ali Salehe
Kimantiki Ali amesema, znz inahitaji autonomy, hakusema muungano uvunjike.

Akatolea mfano wa visiwa vya New Zeland,Macao na Hongkong.
Hii maana yake ni kuwa Ali anasimama katika muungano na wala si kuuvunja ili znz iwe kama Seychelles kama alivyosema mzee Maulid.

Jambo aliloongea Ali Salehe ni kuhusu sheria ya kujiandikisha kupiga kura lina mantiki.
Sheria inayopendekezwa ni ile ya kuruhusu wznz wanaosihi Tanganyika kupiga kura.
Mantiki yake ni kutengeneza uwezekano wa kuiba kura kwa kutumia njia haramu.

Hilo ni kweli kabisa. Hatuwajawahi kuwa na kura za watu nje ya maeneo yao. Vipi leo CCM ione ipo haja ya kufanya hivyo?
Je, wale wznz walioko nje ya nchi, barani Afrika, Ulaya, Asia na Marekani wao haki yao uipo wapi? Mbona sheria inawabagua na sheria hiyo hiyo inawapa uhuru wale wanaoishi Tanganyika kupiga kura?

Ule Mchezo wa Zahia Meghji kupiga kura znz akiwa ametajwa upande wa Tanganyika ndio unatengenezewa mazingira.

Kama watu wa pande zote wangekuwa makini, hakukuwa na haja ya kujadili rasimu kabisa achilia mbali kupiga kura ya maoni.
Kura ya maoni maana yake ni kuhalalisha uhuni, na hapo ndipo Mansour Himid katika video ya 2/5 anapokuja na hoja nzito sana.

Hoja ya Mansour tulishaijadili hapa. Hakuna sababu za wananchi kuzungumzia kura ya maoni.
Kura ya maoni ni kuhallaisha uhuni kwasababu kilichofanyika Dodoma ni uhuni uliokithiri.

Vyama vya upinzani vinapaswa kusimama na agenda yao ya kuandika katiba mpya. Hakuna sababu za kujdaili kama mzoga wa Sitta na Chenge unasehemu zinazofaa kupigiwa kura. Mzoga ni mzoga, na katiba pendekezwa ni ya CCM.
Wananchi wanadai katiba yao inayotokana na wao kwa maoni yao.

Tusemezane
 
MHESHIMIWA JUSA AONGELEA UMAKAMU WA RAIS

Katika video za maridhiano six, mh Jusa ameongelea umakamu wa pili wa Rais kwa umakini, lakini pia kwa kupotosha
Mtakumbuka Jumbe alikuwa makamu wa kwanza wa Rais. Yaliyomkuta tunayajua.

Kuondolewa kwake ni kutokana na nafasi yake kama makamu wa Rais na wala si Rais wa Zanzibar
Jumbe aliitwa Dodoma na yaliyoendelea ni hadithi

Kabla ya BMK kuvugika, tulizungumzia hili. Warioba/tume walifanya busara kutenga muungano, Tanganyika na Zanzibar
Kutenga nafasi hizo kulilenga kutoa mamlaka kamili ya nchi hsuika bila kuingiliwa.
Kwa mujibu wa video, WanaCCM wa znz wanashangilia Rais wa znz kuwa makamu wa Rais

Jusa anasema, umakamu wa Rais kwa mujibu wa katiba ya Chenge inayopigiwa upatu na CCM znz, Rais wa znz atakuwa makamu daima. Hili linahakikisha kuwa hakuna siku znz itakuwa na Rais wa JMT. Hoja ya Jusa ni ya kweli

Pili, Jusa amesema, kwa itifiki Rais wa znz ambaye ni makamu hatashika wadhifa wa Urais ikitokea Rais hayupo.
Atakayekaimu nafasi hiyo ni makamu wa pili wa Rais ambaye ni waziri mkuu wa Tanganyika.

Jusa kasema, hilo ni kumuondolea Rais wa znz hadhi, kwani kikao cha baraza la mawaziri, waziri mkuu wa Tanganyika ndiye atakuwa mwenyekiti na Rais wa znz mjumbe.
Jusa anaendelea, Rais wa znz anachaguliwa, hivyo anapokuwa chini ya waziri mkuu wa Tanganyika wa kuteuliwa ni kumdhalilisha. Hilo lina ukweli.

Hata hivyo anapotosha kwa kutoangalia kwa umakini na mantiki.
Kwanza, Rais wa znz anachaguliwa na watu chini ya laki 5. Mbunge wa Tanganyika anachaguliwa na watu zaidi ya milioni.

Mfano, Jimbo la ubungo wapiga kura tu ni zaidi ya milioni moja. Hivyo, mbunge wa Tanganyika anapochaguliwa kuwa waziri mkuu, bado ana uhalali wa kidemokrasia kluliko Rais wa znz kwa mambo mengi.

  1. Kachaguliwa na watu wengi kuliko Rais wa znz
  2. Ana wajibu mkubwa kwa watu milioni 41 na uchumi unaonedesha muungano. Hivyo, hadhi yake katika msingi wa demokrasia, ulinzi na usalama pamoja na uchumi ni kubwa kuliko Rais wa znz
  3. Rais wa znza anachaguliwa na wznz,anpo kuja kutawala Tanganyika ni kama kuazima kiongozi.
  4. Makamu wa Rais ambaye ni mgombe mwenza ana uhalali zaidi ya Rais wa znz ambaye Watanganyika hawajui kapatikana kwa njia zipi. Hapa ndipo Watanganyika wanatakiwa wajiulize, hivi imefika mahali kiongozi wa taifa anaweza kupatikana kutoka popote tu bila kujali kapatikana vipi.
    Ukimsikiliza Jusa kwa makini, ana hoja za msingi ambazo sijui kama wzn wanaweza kuzitazama kwa jicho mujarabu.

    Rais wa znz anapokuwa makamu, tayari hadhi yake inapungua.
    Rais huyo atakuwa ni makamu wa Rais wa JMT na hivyo uwezekano wa kwenda kinyume na matakwa ya JMT haupo.
    Hatakuwa na nguvu za katiba ya znz bali atawajibika kwa katiba ya JMT aliyoapa kuitetea. Katiba ya znz itakuwa ni muongozo tu kama Standard operatig procedure kwake, sheria atakayosimama nayo ni ile ya JMT

    Na endapo atajaribu kinyume na katiba ya JMT, historia ya Jumbe itajirudia. Ataitwa na kukabidhi funguo za ofisi.

    Je hayo ndiyo mamlaka wanayozungumzia? Je, Warioba aliwaonea au aliwasadia?

    Tusemezane

Kila wakti narejea kusema ILMU ni muhimu hususan unapotaka kusherehesha mambo ya kitaalamu kama haya yanayowekwa na wataalamu waliobobea kama Ismail Jussa.

hata siku moja huwezi kufananisha chumvi na sukari kwani kila kitu ni muhimu katika sehemu yake husika.
Suala la kujiuliza hapa kabla kurukia hapo nilipo BLUE ni:
Je kwanini katika kupitisha mabadiliko yoyote ya katiba ya JMTz ni laazima ipatikane 2/3 ya kura za Ndio toka Tgk na 2/3 ya kura za ndio toka znz. isipotimia kwa upande wowote basi mabadiliko hayo hayawezi kufanyika.

Lakin suala lingine iweje nchi yenye population ya zaidi ya 45 milion ikaungane pasu kwa pasu na nchi yenye watu wasiozidi 1.5 milion. je kuna uhalali au mantiki ya kuingia akilini hapo
?
 
WALIYOSEMA WASEMAJI WA MKUTANO-KIBANDA MAITI

https://www.youtube.com/watch?v=FlECaPDYzVQ

Katika video, wasemaji wa CCM walipangwa kupitia vifungu vya katiba ya Chenge/CCM
Kilichoonekana ni kuzungumzia masilahi ya Zanzibar.
Pale yanapotajwa ya Tanganyika, Tanganyika haisemwi bali Jamhuri ya muungano.

Hilo linaeleza ile hoja ya Tanganyika kuvaa koti la muungano bado ni tatizo.
Rais Shein aliwahi kusema'' Kwa mkataba wa 1964 hakuna mamlaka kamili''

Pengine amesahau kwa namna yoyote Tanganyika ni kubwa kwa znz kwa kila hali, hivyo kulivaa koti la muungano kupo tu midhali hakuna serikali ya Tanganyika.

Jamhuri ya muungano kwa katiba ya 1977 na pendekezwa ya CCM/Chenge Tanganyika haipo.
Kwa maana kuwa Jamhuri ndiyo Tanganyika, na hilo ni koti ambalo znz itabidi walikubali bila hiari.

Katika video hiyo saa 1.22 waziri wa fedha wa muungano amethibitisha,hakuna mapato ya znz yanayokuja muungano.
Huyu ni waziri wa fedha wa JMT ambaye pia ni mbunge kutoka znz na ni mzanzibar.

Ile hoja ya znz kunyonywa na Tanganyika kimapato inajieleza vema.
Lakini hoja ya Saada Mkuya itasaidia sana kuelewa hoja za wachangiaji wengine kadri tunavyosonga mbele.

Waziri Saada anasema, kwa mujibu wa katiba ya Chenge, znz ni huru kupata mikopo na misaada kutoka nje.

Katika muda wa saa 1.26 Makamu wa kwanza wa Rais, Seif Idd Ali anasema ''Katiba ya Chenge imeweka ndani ya katiba sharti la JMT kuidhamini znz katika mikopo''

Hapa ndipo Watanganyika wanatakiwa waone hatari inayokuja machoni mwao.
Kwa mujibu wa wznz, kukopa na misaada kutoka nje ni ruksa. Hiyo ni haki yao.

Lakini pia kwa mujibu wa wznz, kila wanapokopa basi JMT itawadhamini.
Kwa maneno mengine, mikopo na misaada ya znz italipwa na Watanganyika wasiofaidika hata senti moja.

Kibaya zaidi, SMZ inaweza kwenda kukopa maandazi na pili pili manga, na kisha kugoma kulipa.
Atakayelipa ni Mdhamini Tanganyika. Ndivyo walivyokopa michele kule Kenya na sasa ubalozi wa JMT upo katika wakati mgumu kulipa mchele uliokopwa na SMZ kwa ajili ya wazanzibar lakini bili analipa Mnyakyusa, Mpogoro, Mbondei na Mhaya.

Endapo znz wanataka kukopa na misaada kwanini wadhaminiwe na Watanganyika?
Kwanini Mtanganyika abebe mzigo wa znz usiomhusu kwa namna yoyote.

Ndipo naibu katibu mkuu CCM znz aliposema '' SMZ inadhamini wanafunzi 824 katika mwaka 2012/12, na JMT imedhamini wznz 1040'', sikiliza katika dakika ya 53 ya mkutano (video)

Kwa maana kuwa, znz isiyochangia pato katika JMT kwa mujibu wa waziri wa fedha Saada Mkuya, imepewa wanafunzi wengi kuliko SMZ inayochukua mapato yake kutoka kwa wznz.

Hapa ni kuwa wanafunzi wa walipa kodi wa Tanganyika wameachw mitaani wakihangaika, ili hali kodi za baba zao zinakwenda kudhamini wanafunzi wa znz waiochangia lolote katika JMT kwa mujibu wa saada Mkuya, na gavana wa benki kuu ya Tanganyika
Kodi za Watanganyika ndizo zimedhamini wanafunzi wengi kuliko kodi za wznz zinazobaki znz kwa mujibu wa Saada Mkuya

Tena bila aibu Vuai anasema, wazanzibar sasa ubwedo maana wana bodi mbili, ya ZHESLB na JMT ambayo ni HESLB.
Hapa wznz wana haki kwasababu wao ni Tanzanznia na wznz, wewe Mtanganyika ni Mtanganyika tu, huna haki ya kupata huo mkopo wa ZHESB pengine ni kwa kuosa ustaarabu kama alivyosema katibu wa baraza la mapinduzi mzee Maulid

Makamu wa Rais Seif Idd anasema kwa mujibu wa Chenge, znz imepewa haki ya kukopa.
Hapa anajaribu kueleza kuwa znz ikikopa kwa udhamini wa kodi za Mtanganyika, pesa hizo zitatumika katika mambo kama elimu ambayo Mtanganyika hahusiki kwasababu ni Mtanganyika.

Tanzania ikikopa, mkopo huo itabidi uende znz kwasababu znz ni sehemu ya JMT na hivyo ina haki.

Waziri wa Muungano Samia Suluhu anasema, kodi za wafanyakazi wa muungano sasa hivi zinakwenda znz
Kaungwa mkono na waziri Saada Mkuya aliyesema sh 1.2B kila mwezi zinakwenda SMZ kama kodi ya wafanyakazi wa muungano.

Watanganyika, hii maana yake ni kuwa ninyi mnalipa gharama za kuendesha muungano ikiwa ni pamoja na misharaha ya wafanyakazi wa muungano.

Halafu mnawazadia wznz Bilioni 1.2 kila mwezi kwa ajili ya kupunguza tatizo la ajira znz.

Wafanyakazi wa SMZ ni chini ya 10,000. Wznz wanaofanya kazi katika muungano ni 20,000.
Katika akili nzuri, wznz walitakiwa si kuchangia muungano bali pia kulipa kwa kuondoa tatizo la ajira znz.

Kinyume chake, ninyi walipa kodi wa Tanganyika, mnaendesha muungano wenyewe, mnalipa wznz mishahara na kisha mnawalipa zaidi kwa ajili ya kuwasaidia. Hapa ndipo wabunge wa CCM kutoka Tanganyika walipowafikisha.

Waziri Samia anasema formula ya kugawana idadi ya wafanyakazi kama BoT na TPDC imepatikana.
Kumbukeni wznz wameondoa mafuta na gesi hivyo TPDC haiwahusu. Swali, wafanyakazi wa znz ndani ya TPDC inawahusu nini?

Ukitazama maelezo yote, ni wznz wznz wanashangilia kupata tu.

Hakuna yoyote kuanzia Rais wa znz Shein, Makamu wa Rais Idd au mawaziri aliyesimama na kusema muungano unachangiwa vipi na wazanzibar. Hakuna aliyethUbutu kusema hilo.

Si kwamba hawajui, bali ni ile roho ya umimi na dharau kuwa wznz ni bora na wanapaswa kupewa na si kutafuta.

Lakini pia wameongelea sana mafuta na gesi, ajira mikopo na misaada.
Hakuna hata mmoja, si Rais wa znz, makamu au waziri aliyezungumzia usalama na ulinzi wa nje na ndani.
Mbona hatuwasikii wakiongelea wizara ya ulinzi, au mambo ya ndani?

Si kwamba hawajui, wanajua, lakini ni dharau tu kuwa hilo ni zigo la Mtanganyika na anapaswa kulibeba.

Hiyo ndiyo taswira nzima ya wenzetu ambao, kwao katiba ya Chenge inawafaa na Wtaanganyika ni wa siku hizi si wastaarabu pengine akisitiri kinyume cha kauli hiyo

Ni kwa mtazamo huo, na kwa kujua Watanganyika hawahoji, katibu mkuu wa kwanza wa baraza la mapinduzi, amenena katika video ya 1/5 kuwa 'Watanganyika wa siku hizi si wastaarabu''

Kwa lugha za pwani, kama mtu si mstaarabu huyo ni mshenzi.

Watanganyika mnapoona mambo kama hayo na kukaa kimya, kwanini akina Mzee Maulidi wasiwaite Washenzi!

Tusemezane
 
KAMPENI CHAFU ZA VYOMBO VYA HABARI
VIONGOZI WA DINI MLIKUWA WAPI?

Baada yakususiwa na kupoteza mvuto, kampeni za vyombo vya habari za katiba ya Chenge zimeanza.

Pitia habarihii kwa uangalifu
http://www.touch.dailynews.co.tz/index.php/local-news/39837-christians-urged-to-accept-new-constitution

Kichwa chahabari kinaonyesha Askofu Juda Tuwaichi akiwataka waumini wakubali katibapendekezwa ya CCM/Chenge

Ukisomamaelezo kwa undani, alichosema Ruwaichi ni kutaka wananchi kusoma kwauangalifu kabla ya kura ya maoni. Aliitaka serikali isambaze kopi za kutoshaili wananchi waweze kuisoma katiba ya Chenge

Ruwaichi aliwashauriwaumini wake umuhimu wa kura ya maoni.

Gazeti laDaily News ni la serikali. Msimamo wake tunaufahamu ni wa serikali.
Inapotokea maudhui yakaandikwa katika hali iliyopo, gazeti linapotezahsehima na kudharauliwa.

Hilo nigazeti kongwe kwa bahati mbaya sasa linachukua hadhi ya magazeti ya mitaani yaudaku

Viongozi wadini
Kwa kiasikikubwa viongozi wamekuwa sehemu la tatizo la taifa katika maadili

AlichosemaRuwaichi ni kuwataka wananchi washiriki kura ya maoni. Askofu anafahamumchakato ulivyoharibiwa na CCM, wizi wa kura hata CCM walipobakiwenyewe na anafahamu wananchi walivyodharauliwa.

Askofu anafahamukatiba ya Chenge ni ya CCM na haikuwa wala haikuzingatia maoni ya wananchi.
Kila jambo limefanyika kihuni kinyume na maadili ya kiroho ya Imani yoyote.

Ruwaichianaposimama na kuhimiza kura ya maoni inatia shaka sana.
Hivi askofu anatakawananchi wapigie kura ya maoni kitu gani.

Anachoshauri askofu ni kwenda kupigakura ya maoni ya dhambi. Pengine askofu ana maana ‘dhambi ndogo''

Endapoaaskofu anaamini dhambi ni dhambi na hakuna dhambi ndogo, hatudhani angesimamana kuhamasisha kura ya mzoga. Katiba ya Chenge ni kama mzogaambao wananchi na askofu wanataka kupiga kura ya maoni kama ni mzoga mzurikidogo au ni mbaya. Je, hilo ndilo analotaka askofu Ruwaichi?

AFAFANUE

Kutokana nahabari ya Daily news ambayo inachanganya kuhusu kauli ya askofu Riwaichi,pengine ni vema angeweka wazi kama aliyosema ndiyo yaliyonukuliwa auamenukuliwa vibaya.

Tukizingatia kuwa Askofu Ruwaichi aliwahi kuwa kiongozi wangazi za juu wa kanisa, na tukizingatia mwadhama Pengo alikutana na KikweteIkulu, ni rahisi kwa wanananchi kuunga dot hata kama hazina ukweli

WALIKUWAWAPI ?

Hivi viongoziwa dini walikuwa wapi wakati Samwel Sitta akivuruga mchakao kujiibia kura na CCM?
Mbona hatukuwasikiawakikemea hayo, eti leo wanaongelea kura ya maoni.

Katikamabandiko ya nyuma, tuliwahi kusema mbinu za serikali ni kuwatumia waandishi wahabari(Hilo limetokea), kuwatumia wasomi(limetokea) tena kwa kuthibitishwa nakurugenzi ya mawasiliano Ikulu.

Kundi la mwishotulisema ni viongozi wa dini. Hatuna uhakika kama kazi ndio imeanza au nikutetereka.
Hata hivyo, mabandiko yaliyopita tulisema hili ndilo kundi lenyematatizo makubwa.

Tusemezane
 
Back
Top Bottom