Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #241
MTAZAMO WA UPANDE WA PILI WA WAZANZIBAR
Video za awali zimeonyesha kundi moja linalotaka uwepo wa serikali 3.
Hili ni la kamati ya maridhiano Kwa upande wa pili, lipo kundi la wazanzibar wanaotaka muundo wa sasa wa muungano uendelee
Kundi la pili halina hoja ya wazi kwanini wanaotaka serikali .
Hoja zao zimejificha katika ukweli kuwa Zanzibar inahitaji muungano kuliko ilivyokuwa inadai na watu wa kundi hilo hilo siku za nyuma.
Hoja zao zimesaidia kuelewa madai ya wazanzibar kuhusu kuonewa au kupunjwa katika muungano
Hoja zaio zimesadia pia kuwaeleza Watanganyika, ni wapi na kwanini Zanzibar ni mzigo katika muungano
Tuangalie video hizi za mkutano tukiwanukuu wasemaji bila kuwawekea maneno kama tulivyoangalia upande wa kwanza. https://www.youtube.com/watch?v=YthCo16Bx-0
https://www.youtube.com/watch?v=k6qUyt7dMLA
Video ya kwanza, Muongeaji kwa jina la Najma ni mwanasheria.
Najma anasema iliyokuwa rasimu ya Warioba iliacha suala la Elimu kama suala la muungano.
Najma akasema, uwepo wa Polisi wa nchi shirikishi utatengeneza mvutano.
Kwamba, Rais wa shirikisho atakuwa na nguvu sawa na za washirika na hivyo maamuzi kuwa magumu.
Najma anasema, rasimu ya Warioba ilipendekeza iwapo jambo linaongezwa au kupunguzwa ni lazima iwepo kura ya maoni, na hilo litaongeza gharama
Hoja zetu:
Katika video ya pili, wazungumzaji wafuatao walizungumzia suala la elimu ya juu .
Dakika ya 5, mzungumzaji amesema faida za muungano ni elimu ya juu inayodhaminiwa na Tanganyika.
Kasema bila hivyo wanafunzi 6,000 wa znz hawatapata nafasi.
Hamis Hajidakika ya 12 anasema, mikopo wanapata kupitia muungano.
Hata kozi zisizotolewa znz bado wanapata bara kwa mikopo ya bara.
Dakika ya 22 Machano kaongelea HESLB kama bodi inayotoa mikopo kwa wznz na ni faida kwao
Wazungumzaji wote wameongelea mikopo na elimu ya juu kama suala la muungano.
Na ni wznz waliolalamika mambo ya muungano kuongezwa kinyemela. Elimu halijawahi kuwa suala la muungano.
Pamoja na hao, kwa upande mwingine wznz wanalalamika kuwa muungano umedumaza elimu znz.
Haya kayasema mzee Maulidi katika video hii https://www.youtube.com/watch?v=PCwc-W8mIuA dakika ya 50
Hivyo, wznz wanaposema elimu ya juu ni kero ni makosa. Wznz wanapodai muungano umevuruga elimu ya znz ni makosa.
Elimu si jambo la muungano, na wao wanalitaka liwe la muungano,nyuma ya pazia wanalipiga vita.
Hapa hoja kubwa ya wznz ni nini?
Elimu ya juu ni ufadhili tu wanaoupata kutoka Tanganyika .
Ndiyo msingi wa tume ya Warioba kuliondoa suala hilo katika mambo ya muungano kama walivyodai wznz.
Ni vema kama wangeangalia hoja za tume ya Warioba kwa kuzingatia matakwa yao bila malalamiko yasiyo na uhahidi
Kwanini tunasema ni ufadhili. Majibu wanayatoa wznz wenyewe katika video hii https://www.youtube.com/watch?v=k6qUyt7dMLA Katika dakika ya 12 Haji Hamis anasema, iwapo kutakuwa na serikali 3, znz itaweza kuchangia nini?
Na akahoji, je wakishindwa si muungano utavunjika.
Hams akasema huko nyuma serikali ya Mkapa ililipa madeni ya SMZ, sasa kukiwa na serikali 3 nani atalipa madeni hayo?
Mchangiaji Machano katika dk ya 22 anasema, znz ikiambiwa ichangie asilimia 25 tu ya muungano, katika bajeti ya Bilioni 600 watachangia nini?
Zuberi katika dk 45 anasema, katika mwezi mzuri wa makusanyo znz inakusanya bilioni 14, anasema hata kama znz itaambiwa ichangie wanajeshi wastaafu tu kuwalipa, haitaweza.
Hayo ni maoni yao, lakini yana maana sana yakitazamwa kwa jicho la pili
Usawa wa muungano unapatikanaje kama hakuna usawa katika kuhudumia muungano huo?
Lakini muhimu zaidi, ni wznz kutambua kuwa kile wanachokiita kero, si kero ni madai.
Hapa pa la kujiuliza, inawezakanaje uombe halafu udai kama haki?
Itaendelea..

- Ile hali ya madai kuwa znz inapunjwa, sasa inajijibu yenyewe. Kwamba, wao ndio wafaidika wa huu muungano.
Hakuna hata mzungumzaji mmoja aliyeonyesha wapi wanapunjwa na kwa njia zipi,
- Inatoa fursa kwa Watananyika kuelewa ni kwa jinsi gani huu muungano unavyokuwa mzigo kwao.
Tunaona wakidai huduma ambazo hawana mchango nazo.
Katika dakika ya 45 Omar Zuber anasema ''sisi tunaweza kwenda kupata ardhi Tanganyika kwa kutumia Utanzani, lakini wao hawawezi kuja kupata ya znz kwasababu si wznz'' Hoja ya Utanzani wameitumia pia katika suala la elimu.
Hapa inaeleza kuwa wznz ni Watanzania pale wanapohitaji kukidhi haja zao.
Wote kwa pamoja ni wznz pale wanapokuwa na masilahi yao wenyewe.