Nguruvi3,
1. Mkuu unajua unachekesha sana maana huelewi tunazungumza nini.. sasa kama wahisani wamezuia misaada hiyo Miundombinu yetu inajengwa kwa fedha gani? Barubaru kakuonyesha mapato yetu yote kuwa ni trillioni 12, lakini matumizi ya kawaida tu ni trillioni 13, ina maana hazitoshi hata kwa kula na kulalal.. jiulize wewe hizo fedha za ujenzi wa miundombinu yetu inatoka wapi kama wamezuia?
2. Kuhusu Ulipaji. Jina na nchi inayokopa ni JMT, iweje Zanzibar walipe kwa jina lao? umeona wapi imeandikwa Dar es salaam au Mbeya walichangia kulipa madeni kiasi kadhaa! Mnasema wenyewe zanzibar sio nchi halafu unauliza! Kinachokuchanganya ni hii kuwepo kwa Tanzania bara ndani ya JMT basi laa sivyo huna hoja ya msingi kabsa. Na ajabu ya Firaun mnakubali kabisa Zanzibar wasipewe mamlaka ya kujiamulia mambo yao kwa sababu Zanzibar sio nchi, sasa kama hawana mamlaka hayo kwa nini unauliza mchango wa malipo ya Zanzibar !badala ya kuitazama serikali ya JMT (mdaiwa) ambaye ndiye mkopaji.
3. Duh kama Zanzibar wanapewa 4.5, Dar wanapewa ngapi?
Labda nikujibu kihuni tu ni kwamba karibu fedha zote za maendeleo zinaitazama Dar kwanza kwa barabara zake, miradi yake iwe ujenzi wa bandari, uwanja wa ndege, na hata fedha za maendeleo kwa mashirika ya Umma yote yapo Dar ukiacha hizo Escrow, bomba la gas, vyanzo vya kufua umeme kina Richmond na ufisadi mwingine wa Chukua chako mapema. Yaani bora ungeuliza mikoani wanapewa ngapi maana bara hubakiwa na asilimia 95.5, hii hutumikaje? leo wende kuniulize mimi zinagawanywa vipi na hao CCM sidhani kama hoja yako ni Zanzbar tena. Mpango wa maendeleo hautazami wingi wa watu, mji au mkoa isipokuwa mahitaji yetu kama taifa ktk kuzalisha na kukuza uchumi wa nchi nzima, hii ndio kazi ya serikali kuu
4. Labda wewe nambie katika mambo ya muungano ni mapato yapi yaliorodheshwa kuwa ni ya muungano halafu waulize wakusanyaji huzitenganisha vipi. Nachokisoma mimi ni muundo wa Serikali 2 ambao mapato ya kodi yapo ktk mambo ya muungano, ni utaratibu gani unafanyika ktk kukusanya na kuzigawa hilo sii somo langu miye!
Hamjaweza kusema 4.5% inatoka wapi.
Ndiyo maana niliwauliza, kwanza wekeni sawa, je, ni kutoka bajeti ya JMT, ni kutoka mapato ya Trilioni 12 ya Tanganyika au ni kutoka katika misaada na mikopo?
Hapa ndipo pa kuanzia na si kukimbilia deficit kati ya trilioni 13 na trilioni 12.
Pili, elezeni, je kama ni mikopo na misaada mnayosema, wadhamini wamezuia kwa kipindi sasa.
Znz inapata 4.5 kwa utaratibu wa kila mwezi na kwa jumla ya mwaka.
Je, katika kipindi ambacho misaada imezuia, znz imepata pungufu ya 4.5%? Simple!
Hoja kwamba miundo mbinu inajengwa na pesa zipi, ni nyanya na isiyo na mashiko.
Kama ni msomaji utaelewa miradi mingi imesimamishwa kutokana na kukosa fedha za wafadhi walizozuia.
Lakini pia lazima uelewe, ile imayoendelea pesa zilitolewa mwaka uliotangulia.
Na baada ya kuisha ndiyo sasa tunaona miradi imezuiwa. Hilo halina mjadala tena kwa mwenye uelewa.
Kuhusu hoja ya znz kutolipa deni kwasasababu Dar na Mbeaya hawana mahali walipoonyeshwa kuwa wanalipa deni, hoja hii inafungua mambo mengi.
Kwanza,Dar es salaama na Mbeya hazina mgao wa 4.5% kama znz. Hazina 21% ya ajira kama znz, hazina advantage ya exclusive jurisdiction kama znz.
Hivyo, ikiwa znz inadai 4.5%, kulinganisha znz na Dar ni kujichanganya, hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa.
Kwavile znz inadai kama nchi, ina wajibu wa kulipa kama nchi.
Sisi wengine tunasema znz ni nchi na ni dola kwasababu ina kila kitu tofauti na sehemu nyingine ya Tanzania.
Haina sababu za kuwa sehemu ya Tanzania wakati wa dhiki na kuwa znz wakati wa faraja. Kigoma na Singida ni Tazania, hazina hadhi ya nchi au dola kama znz. Huwezi kulinganisha vitu hivyo. Tanga na Arusha hazina katiba yao kama znz na wala hazina bunge kama znz. Hivyo, znz haiwezi kukwepa majukumu kwa kujificha katika kivuli cha Utanzania. Ni ima wawe mkoa kama Dodoma au wawe nchi wabebe majukumu. Hakuna 'half a glass''
Ni kwa msingi huo, ndiyo maana tunataka Tanganyika. Wewe hutaki Tanganyika(ushahidi upo).
Na umeeleza kuwa nje ya muungano znz watapa hasara(ushahidi upo ukihitaji).
Sisi wengine tunasema, Tunataka Tanganyika ili tuamue na kupanga namna ya kushughulika na umasikini, ufisadi na wizi bila kuzongwa na znz ambayo hakuna anAyeeleza katika muungano huu inafaida gani kwa Tanganyika zaidi ya kelele
Kama znz wanAona wanaonewa, wana hiari ya kuacha muungano ili waendele kukopa na misaada kama wao.
Na kwa taarifa yako, katika katiba ya Chenge, wznz wameshinikiza wapewe haki ya kikatiba ya kudhaminiwa wakitaka misaada na mikopo. Hili tu linaonyesha wazi kuwa hakuna uonevu, bali wanapata fadhila.
Ni fadhila kwasababu katika huu muungano hakuna mahali inaonyeshwa wanachangia nini.
Hoja yao ya kutochangia eti ni kwasababu hakuna account ya pamoja.
Well, account ya pamoja wanayochota pesa zao za bajeti ni ipi?
Account ya pamoja wanayochukua bilioni 1.75 kwa mwezi kama kodi ni ipi?
Account ya pamoja wanayopata 4.5% ni ipi?
Account ya pamoja wanayolipa mishahara ya wafanyakazi wa muungano ni ipi?
Account ya pamoja inayowapa ulinzi ni ipi?
Account ya pamoja ya taasisi na wizara za muungano wanayochangia ni ipi?
Account ya pamoja inayolipa wale watalii 84 wanaokuja kulala Dodoma kwa jina la wabunge ni ipi?
Huwezi kuwa na kikapu cha kujichotoea halafu udai huna kikapu cha kuweka. Insane.
Ni haya ndio Watanganyika wanayaona sasa na mbele ya safari kila mmoja atabeba mzigo wake.
Tanganyika inabeba sijui znz itakuwaje. Huoni mada ya kuvunjika kwa muungano inaleta mantiki zaidi kuliko njia za kuficha ukweli!
Hoja yako ya nne, nakubaliana nayo kabisa. Hakuna mapato ya muungano na yale ya Tanganyika.
Jiulize, znz katika pato la bilioni 400 kuna ni hapo. In other words, Tanganyika wana disadvantage, chao kinatumika kote na znz wanachukua chao na kutumia wao.
Hivyo basi unatakiwa uunge mkono uwepo wa Tanganyika ili kila mmoja aonekane wazi katika kuchangia, na si kuchota.
Hapa ndipo hoja ya Tanganyika inapokuwa na mantiki sana na ahsante kwa hoja yako.
Msikwepe hoja kwa maneno mengi, jibuni hoja kwa hoja,