Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

HAKI YA WAZANZIBAR KAWAPA NANI KATIKA MUUNGANO?

Katika video zilizopita na zitazaokuja, tumeona maswali yasiyo na majibu. Wazanzibar hawawezi kueleza kwa kina kwanini wana haki juu ya muungano dhidi ya mshirika mwenza Tanganyika.

Watanganyika watambue kuwa wao ndio muungano. Ndio wamebeba muungano kwa kila kitu. Znz haina uzito na wala haikubeba uzito wa aina yoyote. Hivyo, inapotokea znz kusema wanataka hiki au kile ni dharau. Na dharau hiyo inatokana na ukweli kuwa Tanganyika haipo. Hivyo znz ipo na Tanzania ambapo imo ndani yake.

Haiwezekani kukawa na znz na Tanzania zikaa meza moja kuamua hatima ya Tanzania. Kwa mfano, katika tume zilizoundwa kushughulikia muungano yupo makamu wa Rais wa pili wa znz na timu yake. Kwa upande wa Tanzania yupo makamu wa pili wa JMT. Hlafu humo ndani ya kamati wapo mawaziri wa fedha. Waziri wa fedha ni mzanzibar lakini ndiye anasimamia fedha za nchi wanayoita jirani ya Tanganyika.

Vikao hivyo huishia znz kujipangia kile wanachotaka. Wao ndiio Tanzania na wao ni znz.
Mwisho wa siku Mtanganyika anasukumiwa bili zisizomhusu. Mtanganyika analipa asilimia zisizo na hesabu kama 4.5, Bilioni 1.75, gharama za muungano na taasisi zake.

Watanganyika wanafanya makosa sana kukaa kimya bila kcuhukua hatua. Na wasipoangalia mambo haya ya kubeba na kutoa sadaka yataandikwa katika katiba na watakaolipia gharama ni Watangnyika. Tayari Zzn wamefanikiwa kujenga hoja kuwa wakienda kukopa michele, mbatat na kashata, deni hilo alipe adhamini na kulipa Mtanganyika ikibidi.

Tatizo kubwa la Watanganyika n kukosa uzalendo na nchi yao. Ni wao kutokuwa tayari kusimamia masilahi yao wakidhani wana haki ya kutendewa lolote. Hakuna hata siku moja, waziri au mtumishi wa SMZ atakuwa Mtanganyika.
Lakini waziri wa fedha za Tanganyika ni mzanzibar, waziri wa afya na watendaji wengine wengi tu ni wznz.
Hawa hawana uchungu na Tanganyika mnatarajia watasimamia Tanganyika kwa lipi?

Matokeo ya mambo haya ni wznz kuamua tu ni kiasi gani wanachota kutoka Tanganyika wakiwa wameshika bendera ya Tanzania. Ndio maana tumeuliza hoja nyingi na hakuna mwenye majibu. Hakuna anayetuambia 4.5 inatoka wapi! Inatoka kwatika misaada na mikopo? Inatoka katika bajeti ya JMT? Inatoka katika pato la Tanganyika?

Waliojipangia kiwango hicho ambacho kuna habari kuwa sasa ni asilimi 7 ni waznz kupitia watumishi wao walioajiriwa kama Watanzania. Hapa ndipo Watanganyika wanatakliwa waamke, bila kuwa na Tanganyika mtaendelea kulipa bili za watu waliolala majumbani wakioana.

Hadi sasa hivi, pamoja na gharama za muungano kuzibeba wenyewe, Watanganyika mnalipa bili zisizowahusu kwa gharama za wary wenu. Tatizo si wznz, ni Watanganyika walioridhika kuwa wana haki ya kumenyeka!

Ndio msingi wa wzn kusema ''tunataka aina kadha ya muungano''
Tunataka mambo kadhaa yawe ya muungano.

Yaani haki ya kuhudumia muungano ipo mgongoni mwa Mtanganyika, haki ya kuamua muungano na nini kiwemo ipo kwa wazanzibar

Haki hizo zimetoka wapi kwa znz, ikiwa katika muungano ni ubua?

Tusemezane
 
nikifuatilia kwa makini mabandiko yako yote pamoja na ya ndugu yetu TUJITEGEMEE bila kumsahau ndugu yetu Barubaru yapo mengi sana nimejifunza.

hebu leo hii twende na katiba pendekezwa ili tuonyeshe mapungufu yake na jinsi ambavyo zbr inazidi kujivika kofia ya ukichwa cha familia japo kuwa inawatu mil 1 na ushee ndani ya tanganyika yenye watu mil 40.

hebu ninukuu sura ya 16 ............""NA KWA KUWA, azma ya kujenga Umoja wa Bara la Afrika inadhihirishwa na
Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;""

mie hapa shida iko kwenye iyo iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika . Hivi hii JT imefia wapi?? kwasababu hata msiba na kaburi lake hatujawah kuliona.

mie naona shida imekuja hapa ambapo Tanzania ilikubaliwa na hawa viongozi wetu wa CCM iue JT na ndio mana JWZ inauwezo mkubwa zaid kutumikiwa na WATANGANYIKA.

ivi ujue kwenye hii nchi kuna mtwa na kuna mtwana kuna nyapara na kuna mtumwa wa tanganyika tumekuwa watumwa mbele ya wanzbr na ndio mana watu kama akina Barubaru wanatukejeli tuu.

kwaanaye jua vizuri hii nchi hawez kushangaa znbr kudai haki manake tayari wao ni nchi inayojitosheleza ambayo pia imeungana na nchi ingine.
Nguruvi3 wtu wa kauwashangaa sio wa zbr bali ni hawa viongozi hasa kamati ya chenge ambayo imefumba macho kuona hali hii. unajua sitaki kuamini kwamba machozi ya wale akina mama bungen kudai wao wameoana na wabara itakuwaje hatma yao ndo iloleta huruma za kutoidai tanganyika yetu?? kama wao wamepewa huruma hiyo basi na walioolewa Kenya nao wadai haki ya kuungana na kenya??

Ebu jiulize ivi mtu unapoamua kuwa na biashara ya kauchangia ama kuwa na mahusiano na mtu ya kindugu je utajinyima haki yako ya binafsi ya kufanya yako??

sasa kwann watanganyika tumejinyima haki iyo?? je ni wapi ambapo siye jina la tanganyika liliuwawa likabatizwa la tanzania kwa maana ya Tanganyik?
 
Last edited by a moderator:
NA KWA KUENDELEZA DHAMIRA YETU HIYO, ni muhimu:
(a) kulinda, kuimarisha na kuudumisha Muungano wa nchi za Jamhuri ya Tanganyika na
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;
(b) kujenga Taifa huru na linalojitegemea;
(c) kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria;
(d) kukuza na kuendeleza maadili, uwajibikaji na uwazi;
(e) kujenga umoja na mshikamano utakaowezesha kutimiza malengo ya kisiasa,
kiuchumi, kijamii, kimazingira na kulinda urithi kwa ujumla;
(f) kujenga na kuendeleza ukuu wa mamlaka ya watu;
(g) kujenga na kuendeleza utii wa mamlaka ya Katiba; na
(h) kuimarisha na kudumisha uzalendo kwa Taifa miongoni mwa Watanzania;

hapo bold umeona jinsi ambavyo hata sisi watanganyika tunaongopewa?? iyo JWT IKO WAPI??

HAPO f. hivi ni ukuu gani tunaambiwa hapa wa wanzbr kutunyonya ama??

af hapo G tukafungwa mdomo kwamba tutatii katiba hata kama tunanyonywa si ndio?
 
Nguruvi3 hebu tufanye hivii, kwann kwa huu muda tunaosubiria kura ya maoni tujikite katika kupitia hii katiba manake ukweli ina mapungufu mengi sana na hapa tutaanza sura baada ya sura itatusaidia sana.

Kwa mfano nenda kasome sura ya 6, utaona mapungufu hapo.
mwanzoni tumeambiwa kuwa kuna JWT hapa kwenye hiki kifungu tunaambiwa kuna Tanzania bara...................hii je inamaana gani??
 
Last edited by a moderator:
Anachronism at the best.

Hujajibu hoja hata moja unakimbilia habari zingine.Hapa hatuongelei mikoa, tunaongelea nchi mbili kama ulivyosema,period.

Tunaongelea Tanganyika na Zanzibar. Nina video za kuonyesha jjinsi wznz wanavyoplilia utaifa wao, si Utanzania ni uzanzibar. Hakuna msingida au mwarusha anayedai hivyo, wao ni Watanzania.

Hivyo basi mifano yako kuhusu kugawa pesa ni jitihada za kukimbia hoja. Mimi siendi huko narudi katika hoja,
Wewe ni katika fungu la wale wanaosikia kumbe hawasikii wanaoona kumbe hawaoni kwa sababu wamezibwa masikio na macho yao kwa kutoamini hata wakiaminishwa!.

1. Tuambie kwanini znz ipate 4.5% kama sote ni taifa moja.
Nipe mkoa mwingine wenye kupata asilimia hizo.
Sasa kama ni taifa moja wewe ulitaka wapewe ngapi? Kama bara imebakiwa na asilimia 95.5, wewe ulitaka hizi zigawanywe vipi mikoani?

2. Tueleze 4.5% inayopata znz inatoka katika eneo gani? Bajeti ya Tanganyika, kipato cha Tanganyika au misaada na mikopo. Hapo lazima tuwe na jibu ili kupata uhalali wa 4.5. Kama hakuna jibu basi 4.5 ni zawadi kwa znz
Hizi ni fedha za maendeleo hata hata Canada federal government hutoa fungu la fedha hizi kwa miradi ya nchi washirika. Kifupi muundo uliopo mambo ya Zanzibar yanaendeshwa na serikali ya Zanzibar badala ya serikali kuu na ndio maana wanasema JMT ni Tanzania bara, huwezi kumuona waziri wa JMT akishughulikia mambo ya muungano Zanzibar. nchi nyinginezo mambo ya muungano hushughulikiwa na serikali ya muungano kwetu tofauti kwa sababu serikali ya JMT haina mfuko wa pamoja badala yake tunagawa na ndio chimbuko la tafran iliyopo. jibu lake ni kwamba tunatakiwa kuwa na mfuko wa pamoja na serikali kuu ishughulikie mambo ya muungano kwa pande zote.

3. Tueleze, katika muungano huu unaosema ni wa nchi mbili, znz inachangia nini? Kama hakuna mfuko wa kuchangia tueleze mfuko wa kuchota 1.76Bilioni, 4.5%, gharama za JMT ikiwa ni pamoja na malazi ya wabunge wanaokuja kusikiliza bunge analipia nani.
Zanzibar haichangii wala Bara haichangii kwa sababu hatuna mfuko wa pamoja. Kila mmoja anakusanya zake na pale tunapohitaji fedha za ziada toka nje ndipo tunapogawa kwa nchi mbili.
4. Kama 4.5% ni kutokana na misaada na mikopo, je baada ya wahisani kusitisha znz imepata pingufu ya 4.5%
Sio wahisani wote wamesitisha, mikopo haitokani na nchi zilizotajwa tu, China wametupa mikopo na kuna miradi inayojengwa kutokana na nchi tofauti na sii ajabu ipo kutoka hata Algeria! swala ni kwamba tunapohitaji fedha zaidi kwa ajili ya mfuko wa maendeleo tunagawanya na kwa hesabu gani? hakuna anayejua. Hili ndio chimbuko la malalamiko!

5. Hapo nyuma umesema hakuna mfuko wa muungano na hivyo ni ngumu kugawanya mapato ya Tanganyika na znz.

Kama sisi ni taifa moja kama ulivyosema, vipi serikali ya mkoa wa Dar es Salaam isipewe kipaumbele tukizingatia kuwa uchumi wake na kila kitu ni zaidi ya znz?
Hakuna mahala nimesema mkoa wa Dar es Salaam upewe chini ya Zanzibar isipokuwa nimekwambia kwa nini usijiulize kwa nini mijini iwe na kipaumbele zaidi ya vijijini ambako kuna watu wengi? based on your claims. Kama bara inabakiwa na asilimia 95.5, wewe ulitaka bara wabakiwe na kiasi gani ili mkoa wa Dar wapewe zaidi ya wanazopewa?

6. Unaposema znz wanadai haki yao, ni haki gani waliodhulimiwa ukilinganisha na mkoa wa Tanga kwa mantiki ya hoja zako?
Kwao wanatambua kwamba hapa tuna nchi 2 zilizoungana lazima kuwepo mfuko wa pamoja na kama haupo inaonyesha tunafanya ujanja ujanja kushikilia fedha zote kwa matumizi ya bara. Labda nikuulize wewe Je, ni hesabu gani zinatumika kwao wapewe asilimia 4.5? sidhani kaa unajua maana unalalamikia 4.5 wakati huna mfumo unaokubalika.

7. Kama tunaweza kupata mchango wa kila mkoa kwa pato la taifa, inapotokea znz inachangia sifuri hilo linaeleza nini kwa walipa kodi wa nchi hii? Na uhalali wa kudai upo wapi? Wajibu wa znz katika muungano ni nini? Nini faida yake kama mshirika wa muungano
Kodi zinazochangiwa na mikoa yetu ni kwa matumizi ya serikali yetu na hazitoshi sasa ulitaka Zanzibar wachangie ili kutuwezesha bara kukabiri matumizi yetu? maana elewa serikali kuu kwa sasa inashughulika na mambo ya bara tofauti na wakati wa mwalimu.

8. Kama waziri mmoja anashugulikia wizara ya muungano na Tanganyika,ikiwa waziri mkuu hatambuliwi znz, huyo waziri unayesema anatambuliwa na nani?
Waziri mkuu na mawaziri wa muungano hawafanyi shughuli za maendeleo ya Muungano as such, lini ulimsikia Sumaye, Malecela, Lowassa, Pinda kenda Zanzibar ama akizungumzia maswala ya maendeleo ya Zanzibar zaidi ya ahadi za marais kwao? Huu ndio mfumo wa serikali 2 na ndio maana unakuchanganya lakini kama tungekuwa na serikali 3 mamlaka ya serikali ya JMT ndiyo ingeshughulikia mambo ya muungano kwa bara na visiwani badala yake muundo huu wa serikali 2 unaipa mamlaka JMT kushughulikia mambo ya Muungano na bara. Ukielewa hapo tu nadhani swali lako limejibiwa vema.

. Kama hoja ya gesi na mafuta niliyosema ni upuuzi, tunauliza kwanini gesi ya Tanganyika itumike kumhudumia mzanzibar na gesi ya znz iwe ya znz?
Hili ni swali la kijinga kweli maana sijasikia kitu kama hiki. Sisi tunauza gas hivyo hata Kenya au Uganda wakitaka tutawahudumia na kukusanya mapato sio lazima wao watuhudumie tena sisi kwa gas yao ama iwe swali la kwa nini?. Na hakuna mahala imesemwa hivyo isipokuwa Wazanzibar wanadai kwamba kama gas ikipatikana wanataka gas na mafuta isiwe jambo la muungano kwa maana kwamba wao wenyewe wawe na maamuzi juu ya uwekezaji, gharama zake na hata mapato yake lakini haina maana hawatachangia mfuko wa Taifa kama utakuwepo. Wanachotaka wao kama serikali ni mamlaka ya kusimamia kama tunavyosimamia sisi mamlaka ya gas ya Mtwara na Lindi japo inasomeka kama ni ya muungano.

Kifupi hata vyama vya upinzani tuseme Chadema CUF na hata bunge hawana mamlaka juu ya uwekezaji wa gas na mafuta na ndio maana Zitto na wajumbe wake walipigania hili hadi baadhi ya sheria zimebadilishwa. Hii ni mikataba ya serikali ambayo wao wanaona wana sheria ya kimamlaka kufanya makubaliano na ndio maana leo tunaambulia ruzuku!

Hapa mpuuzi ni nani, yule anayeiba au yule anayeibiwa? Na unataka kuwaambia nini Watanganyika , kwamba ni wapuuzi kwa kuachia rasilimali zao zielekezwe nchi jirani ya znz
Mpuuzi ni yule asiyeelewa maana hata kama mitume watarudi na maajabu yao bado atakuwa mbishi!

10. Znz inakosa kitu gani kuwa dola kamili kwa sasa, na uhalali wa znz kudai mafao ya muungano unatoka wapi.
(Kumbuka hawa hawana msaada wa aina yoyote katika muungano bali mzigo mzito)
Swala sio uwepo wa Dola wanaolilia dola ni kina Jussa mnaowa support kwa kila hali

11. Kama tuna serikali 2 kwa mujibu wako, kwanini serikali ya Tanganyika itoe bilioni 1.75 kwenda znz kama kodi ya wafanyakazi wa muungano ikiwa tuna wizara takribani 5-6 za muungano?
Hakuna kodi ya Mtanganyika inakwenda Zanzibar ikiwa bara kwenyewe jumla ya makusanyo ya kodi zake haitoshi kukimu matumizi ya kawaida.. uambiwe lipi mkuu!

Nimalizie kwa kusema, aliyeleta hoja za mgao kwa znz kwa kutumia population ni ahali wako uliyemsifia, sasa hoja zimekuwa nzito unamruka na kusema ni upuuzi. Sisi hatukusema, tuliuliza formula inayotumika kupata 4.5% ambayo bado tunakuuliza ni ipi?
Sawa na ndio madai ya Wazanzibar wengi mimi sikubaliani nao wanapotumia population kwa sababu unapojenga uchumi wa nchi hutazami watu bali unatazama maliasili na rasilimali zilizopo utawekeza vipi. Kama ni swala la huduma za Afya na Elimu nitakubaliana na uwekezaji ktk shule na walimu kulingana na hesabu lakini miradi ya maendeleo mara zote hutazamwa location ya maliasili na rasilimali zilizopo zitakuza vipi uchumi wa nchi na hivyo serikali kuwekeza miundombinu yake.

Ni formula gani imetumika kupata 21% ya ajira za watanganyika zisizowahusu wazanzibar?
Waulize waloweka asilimia hizo ndio mfumo wa kiutawala wa CCM na sii Wazanzibar..

Hizi ndioz hoja zinazokupandisha munkari hadi kuporomosha mitusi.

Tulia, haya mambo ukiyaelewa na kutoyaonea haya hayana hasira.

Kwa mfano, wzn wanakubali kuwa hawana mchango katika muungano.
Wanakubali kwasababuhakuna hata mmoja anyeeleza znz inamsaidiaje Mtanganyika inachangia nini.

Jibu hoja mkuu,nina hakika watanganyika wanatuelewa sana jata kama unatutukana. Watanganyika wanaelewa na wameamka

Ni suala la muda watatoa yao ya moyoni, hapo ndipo utatambua kuwa dawa ya hoja ni hoja si matusi.

Mkuu usikimbie na kuruka huku na kule, kabiliana na hoja kwa mantiki, utulivu na uzito wake. Tuliza mawazo, kipigo cha hoja kinauma lakini ni dawa inayosadia!

Coming up, video za Baraza la wawakilishi. Jinsi hoja zinavyojengwa! usikose
Mkuu huwezi kunipandisha munkar ila wanishangaza kiasi kwamba naijuliza wee mzima kweli ama una matatizo ya kuelewa! Na nimeshagundua kwamba huelewi muundo wa serikali 2 na ndilo hasa lingekuwa swali lako lakini maadam limepitia kwa Uzanzibar basi ule munkar wako dhidi ya Wazanzibar ndio unaumalia hapa wakati unaungana nao ktk swala la serikali 3. Hujijui umesimama wapi ktk swala hili.
 
Nguruvi3 hebu tufanye hivii, kwann kwa huu muda tunaosubiria kura ya maoni tujikite katika kupitia hii katiba manake ukweli ina mapungufu mengi sana na hapa tutaanza sura baada ya sura itatusaidia sana.

Kwa mfano nenda kasome sura ya 6, utaona mapungufu hapo.
mwanzoni tumeambiwa kuwa kuna JWT hapa kwenye hiki kifungu tunaambiwa kuna Tanzania bara...................hii je inamaana gani??
Katiba ya Chenge/CCM ni ile ya 1977 iliyopigwa photocopy.

Kilichobadilika ni kuongeza mzigo kwa Watanganyika. Kuna kifungu kimeshinikizwa na wazanzibar '' Znz ina uhuru wa kwenda kukopa na misaada kutoka nje..'' Na ili kufanikisha azma hiyo, pale itakapohitajika, serikali ya muungano(a.k.a Tanganyika) itatoa udhamini.

Maana yake ni kuwa znz wanaweza kukopa nje michele, maandaazi na mbatata na kisha kugoma kulipa deni. Ndivyo waivyogomea kuchangia muungano miaka zaidi ya 40, kupitisha deni la ndani, na hata vitu kama umeme wamegoma! ni wajibu wa Mtanganyika

Atayelipa deni hilo ni mdhamini.Tanganyika tutalazimika kulipa kodi kufidia mchele na makaimati waliokula wananchi wa nchi jirani ya znz kama wanavyotuita sisi.

Hili si nadharia, limetokea na hadi sasa lina mgogoro. Zanzibar walikwenda Kenya kukopa mchele na kisha waligoma kulipa.
Mkopeshaji alikwenda mhakamani ili ubalozi wa Tanzania unyanganywe kiwanja kama fidia ya mchele wa wazanzibar kupitia SMZ

Walikaa, wakaamua wakope mchele. Deni la mchele anakabidhiwa Mtanganyika ambaye si kuwa hakula, bali mchele haukuwahi kufika katika ardhi ya Tanganyika.

Kwa mwendo wa katiba ya Chenge, hilo ndilo balaa linalosubiri kutokea.
Kwamba, tutawajibika kwa madeni yaliyotokana na mkataba baina ya SMZ na watu wengine.

Tunawajibika kwasababu litakuwa kikatiba,ni Tanzania. Endapo tungekuwa Tanganyika, tungeweza kumwambia kiongozi wetu, mchele wa zanzibar au Burundi unatuhusu nini?

Lakini kwavile sisi ni Tanzania, huo ni mlango wa uani wa wazanzibar kukidhi dhiki na haja zao.

Hapa ndipo tunasema, tatizo si wazanzibar. Wao wanatumia mwanya huo kutenda wanalotaka.
Tatizo ni viongozi wa Tanganyika walioamua kuuza uhuru na nguvu za wananchi wao kwa nchi jirani.

Kujadili katiba ya Chenge hakuna tofauti na kujadili ya 1977. Ni vema tukajadili ya 1977.
Hii ya Chenge hakuna anayejua imetokana na nini. Walisema Warioba ameleta takwimu mbovu.
Tunawauliza takwimu zilizotengeneza katiba ya Chenge ziko wapi? Hakuna! Maana yake wamekaa katika vikao na kuamua tu.

Kibaya,waliofanya hivyo ni mafisadi katika harakati za kuua issue ya escrow.
Ndiyo maana Chenge/Ngeleja/Mhongo/Tibaijuka walijitoa ili kuhakikisha akili zetu zinaelekea katika katiba waliyotengeneza si escrow.

Ni katiba iliyoandikwa na mafisadi, na si busara kuizungumzia kwasababu hatujui imetoka wapi na chanzo chake ni kipi.

Tunajua imeandikwa na genge la mafisadi, ikasimamiwa na wahuni walioiba kura hata walipobaki wenyewe halafu wanatuletea tujadili. Kama hatukushirikishwa hakuna uhalali wa kuijadili.

Pengine ni muhimu tukaendelea kuwaonyesha Watanganyika wapi wameumia.

Tunajaribu kupitia kila mahali kubaini uhuni na kuwaeleza Watanganyika muda umekwisha, ni wakati wa kcuhukua hatua.

Hatua si katiba tu, bali kukataa uhuni unaofanywa kwa jina la Tanzania. Njia mojawapo ni kuhakikisha kuwa tunakuwa na Tanganyika ili tujadili mafisadi, wezi na umasikini wa watu wetu, kuliko ilivyo sasa tunapojadili namna ya kukaa na wazanzibar.

Hilo si tatizo letu kwasababu hata bila ya znz hakuna kitakachopotea zaidi ya kupatikana.

Ni kwa kutambua kuwa Watanganyika hawapo imara au Tanganyika haipo kama mshirika mwenza, wznz wanachukua nafasi ya kujivika ukuu wa muungano. Utawasikia wakisema hili liwe la muungano, lile lisiwe la muungano. Tunataka muungano wa aina ABCD.

Kwa matu asiyejua, ni rahisi kudhani znz ni muhimu katika huu muungano.
Umuhimu wa znz ulikwisha baada ya mabadilliko ya dunia. Kwasasa anayefikri znz ni muhimu basi atakuwa na mapungufu.

Mbali ya umuhimu wao, znz ni mzigo. Tumeonyesha jinsi muungano ulivyobebwa na Watanganyika kwa asilimia 100.
Bado pamoja na ufadhili huo kwa wznz, wao ndio vinara wa kuamua nini wapate na wala si nini wachangie.

Tumefika mahali tunaumiza watu wetu bila sababu. Kipato cha mkazi wa Singida ni kidogo kuliko Mzanzibar.
Yet, mtu wa singida analazimika kulipa kodi ya kuendesha SMZ isiyomhusu.

Na kwavile kuna pesa zisizo na utaratibu wa kutafuta, wznz wameamua kuzitumia kwa jinsi wanavyojua.
Ka nchi ka watu milioni 1.2 wachache kuliko wananchi wa majimbo ya uchaguzi wa Tanganyika kana makamu wawili wa Rais!!!

Tunafikia mahali pa kulipa kodi znz kwa hisani zetu. Kwa mfano, sasa hivi wanapata 1.75Bilioni kutoka hazina Dar kama kodi za Watanganyika.

Hilo linasemwa ni kodi za wafanyakazi wa muungano. Znz hao hao wanasema hawataki mambo ya muungano yaongezwe.
Sasa iweje tuchukue kodi za halmashauri zetu zilizoajiri wazanzibar na kisha wznz watuadhibu kwa kuajiri watu kwa kuwalipa kodi?

Hivyo suala zima si znz, ni Tanganyika na hapo ndipo pa kuanzia. Ni wakati wajitambue kuwa katika muungano wao peke yao ndio Watanzania. Lakini pia watambue katika Utanzania huo, wapo Watanzania wa msimu.

Hawa ni wzn, na msimu wa madai unapofika ndio wapiga kelele wakubwa. Wakati wa kutafuta wao ni wznz.

Ni kwa return gani tunadhani investment hii itasaidia kizazi cha sasa na kijacho?
 
Mkandara;11769590]Wewe ni katika fungu la wale wanaosikia kumbe hawasikii wanaoona kumbe hawaoni kwa sababu wamezibwa masikio na macho yao kwa kutoamini hata wakiaminishwa!.
Well, ninaamini nikielezwa ukweli.Laiti ningalikuwa sielewi basi hoja zangu zingejibiwa. Midhali zinakimbiwa bado naamini naelewa.
Sasa kama ni taifa moja wewe ulitaka wapewe ngapi? Kama bara imebakiwa na asilimia 95.5, wewe ulitaka hizi zigawanywe vipi mikoani?
Taifa moja! sasa kwanini kuwe na sehemu ina mgao tofauti na sehemu nyingine. Nadhani waulize wazanzibar kama ni watu wa taifa la Tanzania. Usiwashushe hadhi, wao ni wazanzibar
Hizi ni fedha za maendeleo hata hata Canada federal government hutoa fungu la fedha hizi kwa miradi ya nchi washirika. Kifupi muundo uliopo mambo ya Zanzibar yanaendeshwa na serikali ya Zanzibar badala ya serikali kuu na ndio maana wanasema JMT ni Tanzania bara, huwezi kumuona waziri wa JMT akishughulikia mambo ya muungano Zanzibar. nchi nyinginezo mambo ya muungano hushughulikiwa na serikali ya muungano kwetu tofauti kwa sababu serikali ya JMT haina mfuko wa pamoja badala yake tunagawa na ndio chimbuko la tafran iliyopo. jibu lake ni kwamba tunatakiwa kuwa na mfuko wa pamoja na serikali kuu ishughulikie mambo ya muungano kwa pande zote.
Swali halikuuliza 4.5% ni ya maendeleo, madeni ya kitu gani.

Swali na hoja ilikuwa ni hivi: 1. 4.5% wanayopata wazanzibar inatoka eneo gani kati ya haya
a) Bajeti ya Tanzania ambayo ni trilioni 19(b)Mapato ya Tanganyika ambayo ni Trilioni 12 kwa mujibu wenu(c)Misaada na mikopo ambayo ni deficit ya trilioni 1 kwa mujibu wenu piaMaelezo yako hayajajibu swali na wala hayana uelekeo kama yalilenga kujibu hoja.

Pili, kama hatuna mfuko wa pamoja wa kuweka li tugawane, mfuko wa pamoja unaoruhusu zanzibar kuchota ni upi?
4.5% inatoka mfuko gani? Zile pesa wanazolipwa wale watalii Dodoma zinatoka mfuko gani.
Imakuwaje wakati wa kugawana mfuko upo, wakati wa kutunisha mfuko hakuna mahali. Huoni something is wrong
Zanzibar haichangii wala Bara haichangii kwa sababu hatuna mfuko wa pamoja.
Kila mmoja anakusanya zake na pale tunapohitaji fedha za ziada toka nje ndipo tunapogawa kwa nchi mbi
Alaa, hapo nyuma umesema ni taifa moja, sasa unasema tugawe kwa nchi mbili. Wakati tukisema formula gani imetumika unasema ni taifa moja. Tukipata unasema ni nchi mbili. Haya ndiyo mazonge zonge tusiyotaka.
Halafu unasema pesa za ziada zinatoka nje. Huduma za huu muungano zinaendeshwaje kwa sasa?Wahisani wamegoma kutoa, na hapo je,muungano umekufa

Na muhimu sana, unaposema hizi ni nchi mbili kwa mtu mwenye weledi ni Tanzania na Zanzibar.
Sijui Tanzania inakuwaje nchi ikiwa znz imo ndani. Kama una maana Tanganyika, fungu la Tanganyika linakwenda serikali gani. Ukiliweka katika ''nchi ya pili Tanzania' hizo si za Tanganyika ni za Tanzania. Mkuu huoni hata logic inakusuta!

Na pia kama hakuna mfuko, hizo za ziada zinawekwa wapi? Kama tunagawana kama njugu, kuna ugumu gani kuchangia kama karanga? Huoni logic inavyokusimamisha usiendelee na hoja!

Mkuu kuelewa swali ni sehemu ya ufaulu wa mtihani!
Sio wahisani wote wamesitisha, mikopo haitokani na nchi zilizotajwa tu, China wametupa mikopo na kuna miradi inayojengwa kutokana na nchi tofauti na sii ajabu ipo kutoka hata Algeria! swala ni kwamba tunapohitaji fedha zaidi kwa ajili ya mfuko wa maendeleo tunagawanya na kwa hesabu gani? hakuna anayejua. Hili ndio chimbuko la malalamiko!
Ndio maana nimeuliza, kama wahisani (mfano 10) wamekataa na mhisani mmoja anaendelea, je znz bado inachukua 4.5%? na kama itakuwa ni percentage iweje 4.5% ikaribie pato la bilioni 400 la znz.
Hapa mkuu ni hesabu tu
Hakuna mahala nimesema mkoa wa Dar es Salaam upewe chini ya Zanzibar isipokuwa nimekwambia kwa nini usijiulize kwa nini mijini iwe na kipaumbele zaidi ya vijijini ambako kuna watu wengi? based on your claims. Kama bara inabakiwa na asilimia 95.5, wewe ulitaka bara wabakiwe na kiasi gani ili mkoa wa Dar wapewe zaidi ya wanazopewa
Bara inabaki na asilimia 95.5 ya kitu gani? Pato lake, bajeti au misaada na mikopo
Huwezi kusema 95.5 bila kusema ya kitu gani. Hebu tueleze 95.5 ya nini. Na hapa panakuwia pagumu kwasababu hujaweza ku-define 4.5% kutoka wapi. Unaona hoja zetu za kiuuzi zilivyo na mantiki! Tukiuliza tuna maana hatuandiki tu
Kwao wanatambua kwamba hapa tuna nchi 2 zilizoungana lazima kuwepo mfuko wa pamoja na kama haupo inaonyesha tunafanya ujanja ujanja kushikilia fedha zote kwa matumizi ya bara. Labda nikuulize wewe Je, ni hesabu gani zinatumika kwao wapewe asilimia 4.5? sidhani kaa unajua maana unalalamikia 4.5 wakati huna mfumo unaokubalika.
Ndio maana tunasema tunataka Tanganyika ili tuwakomboe. Tunataka znz waende kukopa wenyewe na misaada wenyewe, walipe madeni yao wenyewe, na wajidhamini wenyewe. Tanganyika haihitaji herufi ZN kupata inachokitaka. Mkuu tunauliza kila siku, kinachowazuia kuondoka ni nini? Kwanini kila siku wanasema 'mkataba'mashirikiano hawasemi sasa basi tuvunje jahazi tugawane mbao.
Hivi unaamini Tanganyika inafaidika kwa uwepo wa znz. Nikuulize wangapi wanaijua znz huko nje tofauti na mafia au Ukerewe. Kwa taarifa yako, hatuwahitaji na kama wanaamua kuondoka hata leo, hewala. Kitu gani kinawafanya wang'ang'anie mfumo ule ule unaowaumiza?
Kodi zinazochangiwa na mikoa yetu ni kwa matumizi ya serikali yetu na hazitoshi sasa ulitaka Zanzibar wachangie ili kutuwezesha bara kukabiri matumizi yetu? maana elewa serikali kuu kwa sasa inashughulika na mambo ya bara tofauti na wakati wa mwalimu.
Ni kweli kabisa hazitoshi, na hapo ndipo tunasema hatuna sababu za kupeleka znz.
Kama hazitoshi wznz wanadai nini kutoka katika kitu kisichojitosheleza.
Ulinzi na usalama hawana bajeti, inatoka TanganyikaMambo ya ndani hawana bajrti inatoka Tanganyika
Lini umesikia wazanzibar wakisema mambo hayo si ya muungano! thubutu!

Mishahara wanachuku hazina, sasa huoni ni uonevu kuchukua kule kwenye upungufu
Waziri mkuu na mawaziri wa muungano hawafanyi shughuli za maendeleo ya Muungano as such, lini ulimsikia Sumaye, Malecela, Lowassa, Pinda kenda Zanzibar ama akizungumzia maswala ya maendeleo ya Zanzibar zaidi ya ahadi za marais kwao? Huu ndio mfumo wa serikali 2 na ndio maana unakuchanganya lakini kama tungekuwa na serikali 3 mamlaka ya serikali ya JMT ndiyo ingeshughulikia mambo ya muungano kwa bara na visiwani badala yake muundo huu wa serikali 2 unaipa mamlaka JMT kushughulikia mambo ya Muungano na bara. Ukielewa hapo tu nadhani swali lako limejibiwa vema
Sasa kuna tatizo gani hao wakiwa na serikali yao ya Tanganyika? Huoni kuwafanya kama viongozi wa muungano ni ku-fool akili zetu. Hapa tena unaunga mkono Tanganyika vema sana. Tunataka wafanye shughuli za Tanganyika.

Huko nyuma (ulivyo mahiri wa kuandika na kusahau) umesema mawaziri wa muungano ni katika kupunguza gharama ili wafanye kazi zote za Tanganyika na muungano. Just bandiko moja au mawili yaliyopita. Hapa unakuja na single nyingine kuwa hawana kazi. Hee mkuu wapi unasimama katika hoja. Mara wanafanya kazi mara hawana faida, position yako ni ipi hasa maana upo kila mahali. Tulia na tuliza akili, haya mambo hayahitahi jazaba wala hasira. Ukweli tu unaongoza.
Hili ni swali la kijinga kweli maana sijasikia kitu kama hiki. Sisi tunauza gas hivyo hata Kenya au Uganda wakitaka tutawahudumia na kukusanya mapato sio lazima wao watuhudumie tena sisi kwa gas yao ama iwe swali la kwa nini?. Na hakuna mahala imesemwa hivyo isipokuwa Wazanzibar wanadai kwamba kama gas ikipatikana wanataka gas na mafuta isiwe jambo la muungano kwa maana kwamba wao wenyewe wawe na maamuzi juu ya uwekezaji, gharama zake na hata mapato yake lakini haina maana hawatachangia mfuko wa Taifa kama utakuwepo. Wanachotaka wao kama serikali ni mamlaka ya kusimamia kama tunavyosimamia sisi mamlaka ya gas ya Mtwara na Lindi japo inasomeka kama ni ya muungano
Wakishaliondoa jambo katika katiba, nini kitawalazimisha wachangie muungano.
Halafu unasema gesi na mafuta ni kwa matumizi yao, well, hii ya Tanganyika ni kwa matumizi ya nani?
Kwanini ya Tanganyika iwe ya JMT na yao iwe yao. Huoni kuna tatizo hapo na ndilo litavunja muungano
Siku watanganyika wakifunga mabomba, nini kitatokea?
Mpuuzi ni yule asiyeelewa maana hata kama mitume watarudi na maajabu yao bado atakuwa mbishi!
Hewala , tuendelee mkuu tuwape wasomaji kitu cha kufikiria. Matusi yapo mitaani hatuna sababu ya kuandika.
Swala sio uwepo wa Dola wanaolilia dola ni kina Jussa mnaowa support kwa kila hali
Kwani hao si wazanzibar?
Hakuna kodi ya Mtanganyika inakwenda Zanzibar ikiwa bara kwenyewe jumla ya makusanyo ya kodi zake haitoshi kukimu matumizi ya kawaida.. uambiwe lipi mkuu!
Hee, hata hili la kodi zawafanyakazi wa muungano hulijui. Muulize Rais Shein, Waziri Samia Suluhu,Mwanasheria nguli Najma watakueleza.
Mimi nilijua ni 1.2Bilioni, wao wakanifungua macho ni Bilioni 1.75
Sawa na ndio madai ya Wazanzibar wengi mimi sikubaliani nao wanapotumia population kwa sababu unapojenga uchumi wa nchi hutazami watu bali unatazama maliasili na rasilimali zilizopo utawekeza vipi. Kama ni swala la huduma za Afya na Elimu nitakubaliana na uwekezaji ktk shule na walimu kulingana na hesabu lakini miradi ya maendeleo mara zote hutazamwa location ya maliasili na rasilimali zilizopo zitakuza vipi uchumi wa nchi na hivyo serikali kuwekeza miundombinu yake.
Wanatumia population hata ahali yako katumia na ukasema ameongea la maana, vipi unamruka kimanga mkuu.
Waulize waloweka asilimia hizo ndio mfumo wa kiutawala wa CCM na sii Wazanzibar..
Wanaodai kila siku ni wazanzibar. Kama mfumo wa asilimia ni wa CCM, unakubaliana nasi kuwa hakuna fairness, sijui unabisha nini tena mkuu. Wewe hujui, lakini unawazungumzia wazaznibar wanaodai! wapi na wapi mheshimiwa, mbona unajikanganya namna hiyo?
 
nikifuatilia kwa makini mabandiko yako yote pamoja na ya ndugu yetu TUJITEGEMEE bila kumsahau ndugu yetu Barubaru yapo mengi sana nimejifunza.

hebu leo hii twende na katiba pendekezwa ili tuonyeshe mapungufu yake na jinsi ambavyo zbr inazidi kujivika kofia ya ukichwa cha familia japo kuwa inawatu mil 1 na ushee ndani ya tanganyika yenye watu mil 40.

hebu ninukuu sura ya 16 ............""NA KWA KUWA, azma ya kujenga Umoja wa Bara la Afrika inadhihirishwa na
Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar;""

mie hapa shida iko kwenye iyo iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika . Hivi hii JT imefia wapi?? kwasababu hata msiba na kaburi lake hatujawah kuliona.

mie naona shida imekuja hapa ambapo Tanzania ilikubaliwa na hawa viongozi wetu wa CCM iue JT na ndio mana JWZ inauwezo mkubwa zaid kutumikiwa na WATANGANYIKA.

ivi ujue kwenye hii nchi kuna mtwa na kuna mtwana kuna nyapara na kuna mtumwa wa tanganyika tumekuwa watumwa mbele ya wanzbr na ndio mana watu kama akina Barubaru wanatukejeli tuu.

kwaanaye jua vizuri hii nchi hawez kushangaa znbr kudai haki manake tayari wao ni nchi inayojitosheleza ambayo pia imeungana na nchi ingine.
Nguruvi3 wtu wa kauwashangaa sio wa zbr bali ni hawa viongozi hasa kamati ya chenge ambayo imefumba macho kuona hali hii. unajua sitaki kuamini kwamba machozi ya wale akina mama bungen kudai wao wameoana na wabara itakuwaje hatma yao ndo iloleta huruma za kutoidai tanganyika yetu?? kama wao wamepewa huruma hiyo basi na walioolewa Kenya nao wadai haki ya kuungana na kenya??

Ebu jiulize ivi mtu unapoamua kuwa na biashara ya kauchangia ama kuwa na mahusiano na mtu ya kindugu je utajinyima haki yako ya binafsi ya kufanya yako??

sasa kwann watanganyika tumejinyima haki iyo?? je ni wapi ambapo siye jina la tanganyika liliuwawa likabatizwa la tanzania kwa maana ya Tanganyik?

gfsonwin,

Nimengi umeongea LAKIN napenda kukufahamisha hakuna mtu wa kuwakejeli wala kuwadhihaki katika hili la Tanganyika.

Barubaru ni mchambuzi tu wa mas'ala ya kiuchumi na hana lake zaidi ya kukuonyesha na kupitia tafiti , makongamano na Data mbali mbali katika uchambuzi wake.

Ushauri kwako NI KUPEANA KWA WINGI SANA ILMU YA URAIA NA UTAMBUZI WA UTAIFA WENU kwa wananchi woote kama ilivyofanyika Znz na kujenga uzalendo na mapenzi ya nchi yenu.

Siku zote mbaya wenu ni viongozi wenu na wananchi wenu wasiojua umuhimu wa utaifa wenu na maslah ya nchi yenu.

Kuwachukia waZnz na kuwalaumu wa Znz kwa kudai haki zao ni kujipotezea muda kwani uhuru wenu upo mikononi mwenu na sio kwa Znz.

Elekezeni nguvu nyingi katika ilmu ya uraia na insh'Allah mtafanikiwa.

Karibu sana

Well, ninaamini nikielezwa ukweli.Laiti ningalikuwa sielewi basi hoja zangu zingejibiwa. Midhali zinakimbiwa bado naamini naelewa.Taifa moja! sasa kwanini kuwe na sehemu ina mgao tofauti na sehemu nyingine. Nadhani waulize wazanzibar kama ni watu wa taifa la Tanzania. Usiwashushe hadhi, wao ni wazanzibar Swali halikuuliza 4.5% ni ya maendeleo, madeni ya kitu gani.

Swali na hoja ilikuwa ni hivi: 1. 4.5% wanayopata wazanzibar inatoka eneo gani kati ya haya
a) Bajeti ya Tanzania ambayo ni trilioni 19(b)Mapato ya Tanganyika ambayo ni Trilioni 12 kwa mujibu wenu(c)Misaada na mikopo ambayo ni deficit ya trilioni 1 kwa mujibu wenu piaMaelezo yako hayajajibu swali na wala hayana uelekeo kama yalilenga kujibu hoja.

Nguruvi3,

Nilitaka nikujibu kidigo kuhusu hilo la 4.5% wanayopata waZnz ili nikukidhi na kukukonga roho yako kama hu mwenye kuridhika na kukinai.

4.5% wanayopewa waZnz inatoka katika MISAASA NA MIKOPO
na wala si katika matumizi ya kawaida ya Serikali ya JMTz.

Ngoja tujaribu kuangalia Utekelezaji wa bajeti 2014/15. Hususan kwa kuangalia vyanzo vya mapato vya JMTz kwa mujibu wa utekelezaji wa bajeti 2014/15

[TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD]Tsh (Trillion)
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 1 MAPATO YA NDANI[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]i.[/TD]
[TD]Mapato ya kodi TRA[/TD]
[TD]11,318,222/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]ii[/TD]
[TD]Mapato yasiyo ya kodi[/TD]
[TD]859,812/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]Jumla ya mapato ya ndani[/TD]
[TD]12,178,034[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]iii[/TD]
[TD]Mapato ya halmashauri
[/TD]
[TD]458,471/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]iv[/TD]
[TD]Mapato ya misaada ya nje
[/TD]
[TD]2,941,599/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]v[/TD]
[TD]Mikopo ya ndani
[/TD]
[TD]2,955,227/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]vi
[/TD]
[TD]Mikopo ya masharti ya kibiashara[/TD]
[TD]1,320,000/=

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Sasa 4.5% ya hiyo misaada na mikopo ya nje ni laazima ielekezwe Znz. Sasa ima imepungua au imezidi kinachokatwa ni hicho hicho 4.5%. Na kama hakuna basi hakuna wanachopata.

Katika skuli ya kawaida inatufunza kuwa mtu akikwambia umpe 4.5% ya kile unachopata basi utampa na kikipungua basi utampa hiyo hiyo % na kama hukupata kabisa basi humpi kitu.

Lakin chochote kikiingia laazima apewe % yake kwa mujibu wa makubaliano.

NB.
Juzi nafikiri umemsikia waziri wa Miundombinu huko JMTz Mh Magufuli akisema kuwa Wizara yake imetafuta mkopo wa TSh Trilion Moja ili kujenga flyovers na barabara za michepuko na kuongeza ukubwa wa barabara kuu za Dar ili kuondosha foleni.

Kumbuka fedhwa hizo Trilion moja zitakopwa kwa jina la JMTz ambapo na Znz wamo humo. Hivyo 4.5% yao nao wataichukua ili kujenga barabara zao au hata kufanyia jambo lingine la kipaumbele kwao.

Pole sana

Katiba ya Chenge/CCM ni ile ya 1977 iliyopigwa photocopy.

Kilichobadilika ni kuongeza mzigo kwa Watanganyika. Kuna kifungu kimeshinikizwa na wazanzibar '' Znz ina uhuru wa kwenda kukopa na misaada kutoka nje..'' Na ili kufanikisha azma hiyo, pale itakapohitajika, serikali ya muungano(a.k.a Tanganyika) itatoa udhamini.

Maana yake ni kuwa znz wanaweza kukopa nje michele, maandaazi na mbatata na kisha kugoma kulipa deni. Ndivyo waivyogomea kuchangia muungano miaka zaidi ya 40, kupitisha deni la ndani, na hata vitu kama umeme wamegoma! ni wajibu wa Mtanganyika

Atayelipa deni hilo ni mdhamini.Tanganyika tutalazimika kulipa kodi kufidia mchele na makaimati waliokula wananchi wa nchi jirani ya znz kama wanavyotuita sisi.

Hili si nadharia, limetokea na hadi sasa lina mgogoro. Zanzibar walikwenda Kenya kukopa mchele na kisha waligoma kulipa.
Mkopeshaji alikwenda mhakamani ili ubalozi wa Tanzania unyanganywe kiwanja kama fidia ya mchele wa wazanzibar kupitia SMZ

Walikaa, wakaamua wakope mchele. Deni la mchele anakabidhiwa Mtanganyika ambaye si kuwa hakula, bali mchele haukuwahi kufika katika ardhi ya Tanganyika.

Kwa mwendo wa katiba ya Chenge, hilo ndilo balaa linalosubiri kutokea.
Kwamba, tutawajibika kwa madeni yaliyotokana na mkataba baina ya SMZ na watu wengine.

Tunawajibika kwasababu litakuwa kikatiba,ni Tanzania. Endapo tungekuwa Tanganyika, tungeweza kumwambia kiongozi wetu, mchele wa zanzibar au Burundi unatuhusu nini?

Lakini kwavile sisi ni Tanzania, huo ni mlango wa uani wa wazanzibar kukidhi dhiki na haja zao.

Hapa ndipo tunasema, tatizo si wazanzibar. Wao wanatumia mwanya huo kutenda wanalotaka.
Tatizo ni viongozi wa Tanganyika walioamua kuuza uhuru na nguvu za wananchi wao kwa nchi jirani.

Kujadili katiba ya Chenge hakuna tofauti na kujadili ya 1977. Ni vema tukajadili ya 1977.
Hii ya Chenge hakuna anayejua imetokana na nini. Walisema Warioba ameleta takwimu mbovu.
Tunawauliza takwimu zilizotengeneza katiba ya Chenge ziko wapi? Hakuna! Maana yake wamekaa katika vikao na kuamua tu.

Kibaya,waliofanya hivyo ni mafisadi katika harakati za kuua issue ya escrow.
Ndiyo maana Chenge/Ngeleja/Mhongo/Tibaijuka walijitoa ili kuhakikisha akili zetu zinaelekea katika katiba waliyotengeneza si escrow.

Ni katiba iliyoandikwa na mafisadi, na si busara kuizungumzia kwasababu hatujui imetoka wapi na chanzo chake ni kipi.

Tunajua imeandikwa na genge la mafisadi, ikasimamiwa na wahuni walioiba kura hata walipobaki wenyewe halafu wanatuletea tujadili. Kama hatukushirikishwa hakuna uhalali wa kuijadili.

Pengine ni muhimu tukaendelea kuwaonyesha Watanganyika wapi wameumia.

Tunajaribu kupitia kila mahali kubaini uhuni na kuwaeleza Watanganyika muda umekwisha, ni wakati wa kcuhukua hatua.

Hatua si katiba tu, bali kukataa uhuni unaofanywa kwa jina la Tanzania. Njia mojawapo ni kuhakikisha kuwa tunakuwa na Tanganyika ili tujadili mafisadi, wezi na umasikini wa watu wetu, kuliko ilivyo sasa tunapojadili namna ya kukaa na wazanzibar.

Hilo si tatizo letu kwasababu hata bila ya znz hakuna kitakachopotea zaidi ya kupatikana.

Ni kwa kutambua kuwa Watanganyika hawapo imara au Tanganyika haipo kama mshirika mwenza, wznz wanachukua nafasi ya kujivika ukuu wa muungano. Utawasikia wakisema hili liwe la muungano, lile lisiwe la muungano. Tunataka muungano wa aina ABCD.

Kwa matu asiyejua, ni rahisi kudhani znz ni muhimu katika huu muungano.
Umuhimu wa znz ulikwisha baada ya mabadilliko ya dunia. Kwasasa anayefikri znz ni muhimu basi atakuwa na mapungufu.

Mbali ya umuhimu wao, znz ni mzigo. Tumeonyesha jinsi muungano ulivyobebwa na Watanganyika kwa asilimia 100.
Bado pamoja na ufadhili huo kwa wznz, wao ndio vinara wa kuamua nini wapate na wala si nini wachangie.

Tumefika mahali tunaumiza watu wetu bila sababu. Kipato cha mkazi wa Singida ni kidogo kuliko Mzanzibar.
Yet, mtu wa singida analazimika kulipa kodi ya kuendesha SMZ isiyomhusu.

Na kwavile kuna pesa zisizo na utaratibu wa kutafuta, wznz wameamua kuzitumia kwa jinsi wanavyojua.
Ka nchi ka watu milioni 1.2 wachache kuliko wananchi wa majimbo ya uchaguzi wa Tanganyika kana makamu wawili wa Rais!!!

Tunafikia mahali pa kulipa kodi znz kwa hisani zetu. Kwa mfano, sasa hivi wanapata 1.75Bilioni kutoka hazina Dar kama kodi za Watanganyika.

Hilo linasemwa ni kodi za wafanyakazi wa muungano. Znz hao hao wanasema hawataki mambo ya muungano yaongezwe.
Sasa iweje tuchukue kodi za halmashauri zetu zilizoajiri wazanzibar na kisha wznz watuadhibu kwa kuajiri watu kwa kuwalipa kodi?

Hivyo suala zima si znz, ni Tanganyika na hapo ndipo pa kuanzia. Ni wakati wajitambue kuwa katika muungano wao peke yao ndio Watanzania. Lakini pia watambue katika Utanzania huo, wapo Watanzania wa msimu.

Hawa ni wzn, na msimu wa madai unapofika ndio wapiga kelele wakubwa. Wakati wa kutafuta wao ni wznz.

Ni kwa return gani tunadhani investment hii itasaidia kizazi cha sasa na kijacho?
Nguruvi3, sasa hapo uliposema shida ni kwa watgnyk kujitambua mie nakubaliana na wewe kwa 100%
unajua ukimsoma Barubaru utaelewa kwamba japo yapo makosa lkin yeye hayaoni kama ni makosa ya znbrbali ni makosa ya tgnyk simply kwasabb watgnyk tumeukataa utanganyika wetu.

tatizo lipo kwa hawa viongozi wetu kama akina chenge ambao kwasababu wanapata pa kuchumia tumbo basi wengine wanao kufa kwa kukosa dawa na matibabu sio watanzania na wala haiwahusu.

mie nafkiri sasa lile alilolisema Dr Kabudi liko karibuni sana kutokea na mie ni miongoni mwa wanaosema huu Muungano ni ama uwe wa serikali moja so zbr iwe mkoa ama wa S3.

tumesha wapigia magoti sana, tumesha kwua humble in the name of amani for the past 50yrs lkn sasa tunataka tuseme tuone kama kudai haki yetu ya msingi ni uvunjifu wa amani ama la.

leo hii ukuniambia kwann siye tumetumika kutengeneza katiba ta JMT sielewi kabisa manake kama tunayo JMT basi ni wazi kwamba tunapaswa kuwa na JWT, JWZ na SJMT.

umehoji sana juu ya 4.5% je umesha jiuliza mkopo wa smart city ambao zbr imeupokea unaliapwa na nani?? je huu nao ni mzigo mwingine kwa wa tgnyk kama ulivyokuwa wa mchele na tende toka mombasa??
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Nilitaka nikujibu kidigo kuhusu hilo la 4.5% wanayopata waZnz ili nikukidhi na kukukonga roho yako kama hu mwenye kuridhika na kukinai.

4.5% wanayopewa waZnz inatoka katika MISAASA NA MIKOPO
na wala si katika matumizi ya kawaida ya Serikali ya JMTz.

Ngoja tujaribu kuangalia Utekelezaji wa bajeti 2014/15. Hususan kwa kuangalia vyanzo vya mapato vya JMTz kwa mujibu wa utekelezaji wa bajeti 2014/15

[TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD]Tsh (Trillion)
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 1 MAPATO YA NDANI[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]i.[/TD]
[TD]Mapato ya kodi TRA[/TD]
[TD]11,318,222/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]ii[/TD]
[TD]Mapato yasiyo ya kodi[/TD]
[TD]859,812/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]Jumla ya mapato ya ndani[/TD]
[TD]12,178,034[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]iii[/TD]
[TD]Mapato ya halmashauri
[/TD]
[TD]458,471/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]iv[/TD]
[TD]Mapato ya misaada ya nje
[/TD]
[TD]2,941,599/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]v[/TD]
[TD]Mikopo ya ndani
[/TD]
[TD]2,955,227/=[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]vi[/TD]
[TD]Mikopo ya masharti ya kibiashara[/TD]
[TD]1,320,000/=

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Sasa 4.5% ya hiyo misaada na mikopo ya nje ni laazima ielekezwe Znz. Sasa ima imepungua au imezidi kinachokatwa ni hicho hicho 4.5%. Na kama hakuna basi hakuna wanachopata.

Katika skuli ya kawaida inatufunza kuwa mtu akikwambia umpe 4.5% ya kile unachopata basi utampa na kikipungua basi utampa hiyo hiyo % na kama hukupata kabisa basi humpi kitu.

Lakin chochote kikiingia laazima apewe % yake kwa mujibu wa makubaliano.

NB.
Juzi nafikiri umemsikia waziri wa Miundombinu huko JMTz Mh Magufuli akisema kuwa Wizara yake imetafuta mkopo wa TSh Trilion Moja ili kujenga flyovers na barabara za michepuko na kuongeza ukubwa wa barabara kuu za Dar ili kuondosha foleni.

Kumbuka fedhwa hizo Trilion moja zitakopwa kwa jina la JMTz ambapo na Znz wamo humo. Hivyo 4.5% yao nao wataichukua ili kujenga barabara zao au hata kufanyia jambo lingine la kipaumbele kwao.

Pole sana

nakubaliana na wewe kwamba katika kile kinachoitwa muungano iwapo tutapata msaada basi lazima tugawane.
lakini nina swali hapa je ni kweli kwamba zbr imekuwa na desturi ya kukopa yenyewe kama yenyewe na mzigo huo kuwaangushia JMT?

na je kuna misaada ya kirafiki ambayo zbr hupata kwa marafiki zake ambayo huwa ni yao tu na kwenye JMT haifiki wala haisemewi??

mie nimeona marafiki wa JMT wakitoa misaada na misaada iyo ikipelekwa hadi zbr mfano ni mradi wa STHEP ambao si tu ulikuwa ka tanganyika bali hata kwa zbr. lakin na penyewe hapo nikawa na swala la kujiuliza hivi kwani ELIMU YA JUU ni maswala ya muungano??

naomba unijibu hapo na ukweli nakiri sielewi kama E/JUU ni swla la muungano.
 
Katika katiba hii mpya ndio wamepitisha pendekezo la kuwapa Zanzibar mamlaka ya kukopa wenyewe! katiba ikipita ndio itakuwa hivyo.

Unajua kinachowachanganya ni hii serikali 2 wala sio Zanzibar maana mnaitafuta Tanganyika iko wapi lakini sii kwenye mapato wala matumizi kwa sababu tunakopa fedha za misaada kwa jina la JMT, na hivyo misaada hiyo hupitia wizara ya fedha na benki kuu na tuseme bara ndio tunashika mpini. Serikali ya JMT ndio wenye dhamana ya kulipa deni na sio Tanganyika kutokana na mapato ya mauzo yetu nchi za nje iwe vinyago, korosho, Karafuu, Utalii ama makubaliano yalopitishwa baina ya wafadhili na sisi. Tunapewa mikopo sii kwa Tsh wala dola iliyopo mfukoni bali mali kwa mali! mfumo wa kibepari usemao Usipokubali kuliwa kidogo hutakula!

Kama tungekuwa na serikali 3, Serikali ya JMT ingekamata misaada hiyo na kisha kuzigawa vile vile 4.5 kwa Zanzibar na 95.5 kwa Tanganyika na siii kazi ya seirkali za nchi kulipa deni hilo isipokuwa ni jukumu la serikali ya JMT ambayo inakula kodi pia kwa kila exports zetu nchi za nje na ndio wenye dhamana ya kuweka mikataba ya misaada hiyo. Nasema hivi kwa sababu swala sio muundo isipokuwa tatizo lipo kwenye mfuko huu wa kugawana kwa asilimia. Kilichotakiwa kufanyika ni serikali ya JMT kutazama miradi ya uwekezaji nchini na kuwekeza huko, sasa kama Zanzibar hawaiamini serikali hiyo hapo ndio maswala la muungano yanapoingizwa na wao kudai kujitenga.

Kifupi ukweli ulojificha ni kwamba HATUAMINIANI.. hii habari ya serikali 2 au 3 ni mchezo tu wa kisiasa ukweli utasimama kuwa sisi hatuaminiani iwe bara na Zanzibar au bara na viongozi wake kama hao kina Chenge na CCM hawaaminiki na ndio maana watetezi wa Tanganyika hawakubaliani na serikali 2 zao la CCM. Na Wazanzibar nao wanaamini CCM ndio Tanganyika na ushahidi upo mkubwa tu ktk kura za maoni ya kupitisha katiba pendekezwa 2!

Nawaomba tu mfahamu ya kwamba mara nyingi kodi yako wewe na mimi hutumika kwa matumizi ya kawaida yaani kulipa mishahara ya viongozi, posho na kulipia gharama zote za uendeshaji huduma na miradi ya serikali hizi. Hata serikali za mitaa wanayo miradi yao wenyewe ambayo haigharamiwi na serikali ya JMT isipokuwa wao wenyewe hujipanga kutokana na mapato walokusanya na majuzi tu ndio madiwani wameingizwa ktk kulipwa mishahara. Hii hufanyika kote dunani hata kwenye serikali 3 gharama za uendeshaji serikali moja hutokana na kodi za wananchi wake lakini ukopaji nje ni swala la serikali ya Muungano ambayo huwa na mfuko wake.

Kwa hiyo nachoweza kusema mimi ni kwamba sielewi huu mpango wa kugawa kwa asilimia umetoka wapi badala ya serikali zote kutazama mahitaji ya wananchi ktk huduma na kijamii na kiuchumi. Ni wapi tuwekeze nini na kwa gharama gani na return yake itakimu mahitaji na kwa kiwango gani. Swala linalowahusu serikali kuu, pia hizi serikali ndogo huomba msaada (grant) toka serikali kuu kukamilisha mipango yao ya maendeleo yalokuwa juu yao na hutazamwa wakaahidiwa ama wakaambiwa fedha hiyo hakuna.

Elimu ya juu ni swala la Muungano ni kutokana na ukweli kwamba asilimia 80 kama sio 90 ya bajeti ya elimu nchini inatokana na misaada. Kama unakumbuka serikali yetu ya JMT imeingia muafaka wa MoU na shirikisho la kikristu na wanapata misaada ya mikopo kutoka Ujarumani na wao kuwa sehemu ya wasimamizi wa shughuli za Elimu na Afya nchini kupitia chombo walichokiunda hapa nchini CSSC mwaka 1992. Na katika makubaliano hayo serikali ilirudisha shule na Hospitali zao zote zilizokuwa zimetaifishwa na mwalimu. Hii ndio nipe nikupe!

Kwa hiyo unaona hapa kwamba fedha za maendeleo hupitia mikataba kama hii ambayo aidha upande wowote wanaweza kulalamika. Na kama unakumbuka Waislaam wamelipigia kelele sana swala hili lakini jibu lake limekuwa kwamba hata wao wanafaidika na elimu inayotolewa pasipo kubaguliwa. Leo inakuwaje unaanza kuwabagua hata Wazanzibar? Je, katiba yetu ya JMT imeruhusu serikali kuinga mikataba na mashirikisho ya kidini? Sasa hapa pia unaweza jikuta ukasimama upande wowote kutetea japo ukweli upo wazi!..
 
nakubaliana na wewe kwamba katika kile kinachoitwa muungano iwapo tutapata msaada basi lazima tugawane.

lakini nina swali hapa je ni kweli kwamba zbr imekuwa na desturi ya kukopa yenyewe kama yenyewe na mzigo huo kuwaangushia JMT?

na je kuna misaada ya kirafiki ambayo zbr hupata kwa marafiki zake ambayo huwa ni yao tu na kwenye JMT haifiki wala haisemewi??

mie nimeona marafiki wa JMT wakitoa misaada na misaada iyo ikipelekwa hadi zbr mfano ni mradi wa STHEP ambao si tu ulikuwa ka tanganyika bali hata kwa zbr. lakin na penyewe hapo nikawa na swala la kujiuliza hivi kwani ELIMU YA JUU ni maswala ya muungano??

naomba unijibu hapo na ukweli nakiri sielewi kama E/JUU ni swla la muungano.
Hili suala la misaada na mikopo, huwa naliangalia kama la dhalili kiasi fulani.

Kwanini tuamini kuwa sisi ni taifa linaloishi kwa matumaini hayo na wala si kujijengea uwezo.
Hata hivyo, suala huchukuliwa kama 'advantage' ya malalamiko ya wznz bila justifications. Tumeonyesha mara nyingi utata uliopo

Ukitaka kufahamu jinsi linavyotumika vibaya, ipo asilimia inayozungumziwa ya misaada ambayo ni 4.5.

Wengine wanasema ni kutoka katika misaada, wengine hawajui inatoka wapi ilimradi kujenga hoja kwa kutumia njia za kubuni buni.

Kwa mfano, kama misaada na mikopo itakuwa ni Trilioni 1, 4.5% yake ni Bilioni 45.

Tujiulize, pesa zinazokwenda znz kutoka JMT ni 45 Bilioni peke yake?
Utaona ni zaidi ya bilioni 200. Kama ni hivyo, tofauti ya kiasi hicho inatoka wapi?

Pili, tujiulize kama 4.5% ni misaada, na znz haina bajeti ya elimu ya juu, wizara ya ulinzi, mambo ya ndani na nje, na taasisi za muungano, je vyombo hivyo vinahudumiwa na bajeti ipi?

Kwa minajili ya mjadala, tufanye zinatoka katika fungu la muungano.
Sasa inakuwaje Tanganyika iliyobaki na 95.5 itoe tena kwa ajili ya muungano na znz ichukue tu. Unaona utata uliopo.

Hapa maana yake ni kuwa 4.5% ya znz ni yao, 95.5 ni ya znz na Tanganyika kupitia wizi wa jina Tanzania.

Hoja yako ya pili, upo ushahidi kuwa znz inakopa na mzigo kutupiwa JMT. Mchele waliokopa Kenya aanyebanwa ni wewe na mimi. Swali ni kuwa mchele huo ulikanyaga ardhi ya Tanganyika?Kama ni hapana kwanini JMT ihusike katika mchele uliokopwa na SMZ!

Kuhusu misaada, ni kweli kuwa ile inayopatikana nje ya JMT ni ya znz peke yao.
Hapa ndipo tunahoji uhalali wa jambo hili.

Je, wapi ambapo Tanganyika inapata bila kuwa na 'tag' ya Tanzania.

Unaposema Tanzania ndipo wznz wanaingia kwa malalamiko kwasababu nao ni sehemu ya.

Katika katiba ya Chenge, imeandikwa kuwa znz wakikopa, mdhamini ni JMT.
Hilo Mkandara amekwepa kulisema.

Maana ya hili ni kuwa wataenda kukopa na mwisho wa siku mzigo unaweza kutua mabegani kwa Matanganyika.
Lakini basi tuelezwe, huyu Mtanganyika fursa yake ya kujiamulia mambo kama kukopa iko wapi?

Ukisoma Rasimu ya Warioba, jambo hili liliwekwa wazi na katika mizani sawa. Kwamba washirika, Tanganyika na znz kila mmoja akope na serikali kuu itakuwa mdhamini.

Na mwisho,utasikia hoja za kukopa na misaada tena wakisema asilimia 4.5 ni ya znz.
Mkandara kasema pesa hizo zinapitia Bank kuu na serikali ya muungano.

Sasa ukitaka kujua lipo tatizo waulize, kwanini znz hiana mchango kwatika muungano.
Jibu la haraka watakalokupa ni kuwa hakuna mfuko wa pamoja.
Je, kwanini wasitumie utaratibu ule ule unaotumika kuchukua?

Katika kodi za JMT anazosema Mkandara, hakuna inyovuka bahari. Hivyo kodi zinazoongelewa na anazoongela za kuendesha muungano ni za Watanganyika, hilo linafichwa.

Hebu tujiulize, je tunaweza kuendesha muungano kwa mikopo na misaada peke yake? Na kama jibu ni ndiyo basi hakuna muungano. Si wahisani wa mikopo na misaada wamesitisha, sasa muungano unaendeshwaje
 
Nguruvi3, sasa hapo uliposema shida ni kwa watgnyk kujitambua mie nakubaliana na wewe kwa 100%

tatizo lipo kwa hawa viongozi wetu kama akina chenge ambao kwasababu wanapata pa kuchumia tumbo basi wengine wanao kufa kwa kukosa dawa na matibabu sio watanzania na wala haiwahusu.

Alilolisema Dr Kabudi liko karibuni kutokea na mie ni miongoni mwa wanaosema huu Muungano ni ama uwe wa serikali moja so zbr iwe mkoa ama wa S3.

tumesha wapigia magoti sana, tumesha kwua humble in the name of amani for the past 50yrs lkn sasa tunataka tuseme tuone kama kudai haki yetu ya msingi ni uvunjifu wa amani ama la.

leo hii ukuniambia kwann siye tumetumika kutengeneza katiba ta JMT sielewi kabisa manake kama tunayo JMT basi ni wazi kwamba tunapaswa kuwa na JWT, JWZ na SJMT.

umehoji sana juu ya 4.5% je umesha jiuliza mkopo wa smart city ambao zbr imeupokea unaliapwa na nani??
je huu nao ni mzigo mwingine kwa wa tgnyk kama ulivyokuwa wa mchele na tende toka mombasa??
gf kuna mengi sana tumehoji.Hili la 4.5% linawatatiza hata wale wanaojaribu kulitumia.

Mfano, bajeti ya znz 2015 haina wizara ya ulinzi. Kama tutasema 4.5 ni kitokana na mikopo, na kwa mfano wa deficit ya JMT ya Trilioni 1 kwa mujibu wa watetezi, znz inapaswa kupata bilioni 45.

Na endapo itakuwa na brigedi moja tu ya jeshi gharama zake si chini ya bilioni 45. Hii maana yake, znz imeokoa kiasi hicho kwa kumega kutoka kile wanachosema ni cha Watanganyika. Hapo hakuna taasisi za muungano na wizara nyingine bado!!!

Jambo la kujiuliza, mbona watetezi wa 4.5 hawatuelezi hizo taasisi nyingine zinalipiwaje?
Tumeambiwa ni misaada na mikopo, sasa yote yamekwama, je muungano umekufa?

Alichosema Prof Kabudi ni kitu cha muhimu sana. Kwa jinsi watu wanavyobabaika na utetezi hafifu wa madai ya wazanzibar ndivyo Watanganyika wanavyoona yale waliyokuwa hawayajui.

Mfano, kwa mwezi tu znz inapata 1.75Bilioni za wafanyakazi wa muungano.
Hiyo ni sawa na Bilioni 21 kwa mwaka. SMZ haikusanyi kiasi hicho.

Hivyo kodi inayosemwa inatokana na fadhila za Watanganyika kutoa nafasi za ajira kwa wznz na kisha kuadhibiwa kwa kuambiwa walipe kodi, Kuna akili hapa Watanganyika? Kana kwamba wznz wanaofanya kazi muungano si kwa ajili ya JMT inayowahudumia kwa gharama, bali ni ma-TX waliokuja kutoa ujuzi

Chukua pato la mtu wa Singida kwa mwaka, ni dogo ukilinganisha na la mzanzibar.

Kodi ya mtu wa Singida ilotumika Kigoma au Mtwara kwa shughuli za maendeleo ni halali.
Ni halali kwasababu Msingida ana uwezo wa kuhamia popote akafaidika na fursa zile zile anazopata mkaazi wa eneo.

Watu wa kaskazini wanahamia Mkuranga na Handeni. Kodi walizolipa huko nyuma ndizo zimetengeneza huduma wanazizozikuta kule wanakohamia.

Kodi ya Msingida kwenda znz ni uonevu. Hakuna msingida atakayekwenda znz na kufaidika na fursa kama mzanzibar.
Huko znz, Msingida atahitaji kitambulisho cha ukaazi ambacho hutolewa si kwa Mtanzania bali mzanzibar.
Kitambulisho hicho kitamnyima fursa za huduma za jamii, ajira, ardhi n.k. Amepigwa pini.

Siku watu wa Tanganyika watakapobaini huu uhuni wa kutumia jina la Tanzania, watachachamaa.

Hakutakuwa na nafasi ya majadiliano bali kila mtu abebe mbao zao.
Na ndio msingi wa mada kama unavyosomeka katika kichwa cha habari.

Fikiria hivi, watu wawili wanatofautiana kwa msimamo wa 4.5% . Hawa wana exposure ya kutosha sana.

Tumeuliza, 4.5% inatoka wapi, bajeti ya JMT, Pato la Tanganyika au misaada na mikopo

Barubaru anasema ni misaada na mikopo. Tukamuuliza kwa kigezo gani, jibu ni population

Mkandara anasema ni fedha zinazopitia bank kuu na serikali, na kigezo cha population si kweli
Think about this, hawa ni watu ambao ni juu ya average Tanzanian halafu wanababaika kiasi hicho.

Tumeuliza zaidi, 4.5 inayosemwa kama ni ya misaada hebu watupe namba za pesa za misaada na mikopo, halafu watupe namba ambazo znz inapata kutoka JMT tuone kama kuna uwiano, wamekimbia.

Tumeuliza tena,vipi gharama za muungano, serikali na taasisi zake kwanini zitoke kwenye 95.5% ya JMT ambayo znz ipo, wakati huo huo znz ipewe cha juu cha 4.5% , wamekimbia.

Tumeuliza tuonyeshwe bajeti ya znz na wizara za ulinzi, mambo ya ndani, nje na taasisi na jinsi znz inavyochangia.
Wanasema hakuna mfuko wa pamoja. Lakini wanataka 4.5% na Bilioni 1.75 kila mwezi kutoka katika mfuko wasiousema ni upi.

Hadi hapo unaona jinsi tunavyotengeneza mazingira mazuri ya kuvunjika kwa muungano.

Kama wznz wanataka muungano, basi wakatae katiba ya Chenge, warudi kwa Warioba

Wakiendelea na hii ya Chenge, Watanganyika watatoa yao ya moyoni. mwisho na hapo ni kupoteza meli na mzigo
 
TANGANYIKA INAPOADHIBIWA KWA FADHILA

BILIONI 1.75/MWEZI KWENDA ZANZIBAR

Ili kutuondoa katika hoja na maswali yasiyo na majibu, hoja ya mikopo na misaada inaonekana kutumiwa sana. Swali linakuja, kuna utaratibu gani wa kulipa madeni yanayoyokana na mikopo hiyo?
Kama tuna utaratibu wa kugawana kwa asilimia na population, upi unaotumika kulipa deni.

Kisichozungumzwa ni pesa za ndani zinazotokana na mapato ya ndani.
Kuna suala la znz kupewa Bilioni 1.75 kama pesa za kodi za wafanyakazi wa muungano.

Tunaelewa wizara husika ni ya ulinzi na usalama, mambo ya ndani, nje, na taasisi za muungano kama BoT.

Zanzibar imepewa asilimia 21 ya ajira. Haielezwi ni za wizara husika au ni za ajira za Tanganyika.
Hata hivyo upo ushahidi kuwa wznz wameajiriwa katika maeneo wasiyostahili ambayo si sehemu ya muungano.

Kutokana na asilimia 21, zanz inapata 1.75Bilioni/mwezi sawa na Bilioni 21 kwa mwaka kama kodi ya wafanyakazi.
Hakuna anayeeleza ni kigezo gani kimetumika kupata namba husika.

Mtiririko wa wznz kuajiriwa ni mpana. Kwanza, katika elimu wao wanapata mgao maalum.
Hakuna mkoa unaopata mgao bali nafasi ni za taifa na ushindani ndio unaamua kwa upande wa Tanganyika.

Pili, wznz hawarudishi mikopo kama wenzao wa Tanganyika. Ingawa kule kwao wanarudisha katika bodi yao, wanapovuka bahari kwao ni sadaka.

Utaratibu huo si kama wa Tanganyika ambapo mhitimu anaanza kudaiwa wakati ukifika.

Endapo pesa za elimu ya juu ni za JMT kama anavyodai Mkandara, iweje basi kundi moja lirudishe na lingine lisamehewe? Na iweje basi kuwe na bodi mbili, ya JMT kwa wote nay a znz kwa wazanzibar tu?

Wahitimu wa mikopo ya bure, wanapewa nafasi ya 21% katika soko la ajira katika taasisi zisizo za muungano.

Kituko ni pale, pamoja na wznz kupewa mgao maalumu wa nafasi za elimu, mikopo wasiorudisha, asilimia 21 za ajira zisizowahusu, bado Mtanganyika aliyesoma kwa mkopo, ushindani, kurudisha mkopo, na kukosa nafasi za soko la ajira, pindi anapopata nafasi ANAADHIBIWA kwa kulipa kodi ili ifidie 1.75 Bilioni kwenda znz.

Kwa maneno mengine, ufadhili wote waliopata wnz bado wanadai kutunukiwa kodi kwa fadhila walizopewa.

Hapa ndipo Watanganyika wafungue macho. Kinyume chake, huo utakuwa mzigo mzito kwa vizazi vijavyo. Rasimu ya Warioba iliweka utaratibu mzuri sana ambao Watanganyika wanapaswa kuuangalia tena.

Tusemezane
 
nakubaliana na wewe kwamba katika kile kinachoitwa muungano iwapo tutapata msaada basi lazima tugawane.
lakini nina swali hapa je ni kweli kwamba zbr imekuwa na desturi ya kukopa yenyewe kama yenyewe na mzigo huo kuwaangushia JMT?

na je kuna misaada ya kirafiki ambayo zbr hupata kwa marafiki zake ambayo huwa ni yao tu na kwenye JMT haifiki wala haisemewi??

mie nimeona marafiki wa JMT wakitoa misaada na misaada iyo ikipelekwa hadi zbr mfano ni mradi wa STHEP ambao si tu ulikuwa ka tanganyika bali hata kwa zbr. lakin na penyewe hapo nikawa na swala la kujiuliza hivi kwani ELIMU YA JUU ni maswala ya muungano??

naomba unijibu hapo na ukweli nakiri sielewi kama E/JUU ni swla la muungano.

gfsonwin,

Kwa mujibu wa MAKUBALIANO YA MUUNGANO WA TGK na ZNZ ni kuwa mambo ya nje ni suala la muungano. Hivyo Znz kama Znz pekee haina mamlaka ya kuweza kukopa au hata kupokea mikopo na misaada ya nje bila kupitia JMTz.

Hivyo hakuna chance ya Znz kuweza kukopa kinyemela au hata kupokea misaada kutoka nje bila mkono wa JMTz na misaada hiyo na mikopo hiyo inakuja kwa jina la JMTz. HIVYO HAKUNA CHANCE ZNZ KUKOPA NA DENI NJE.

Kumbuka kuwa hiyo 4.5% ambayo Znz inapokea kama Misaada na Mikopo ni jambo ambalo Znz inatakiwa ilipe vile vile katika DENI Hilo. Tujaalie mvungano wenu umevunjika na Deni la JMTz ni 38 Tril. Znz atatakiwa kulipa 4.5% ya deni hilo na TGK atalipa the rest 95.5%. Kwa hiyo usifurahie tu kukopa lakin na kulipa imo.

Znz ana mamlaka kamili ya kukopa katika taasisi na ma bank ya ndani kama DENI la NDANI tu bila kuijulisha JMTz.

Misaada ya Siri hili sina ujuzi nalo japo ukiliangania kisharia na kwa mujibu wa mkataba wa muungano WA NCHI HIZO MBILI hilo HALIWEZEKANI.

Labda unidadavulie marafiki wa JMTz ni akina nani hao ambao Znz wanakuwa hawaitambui?
Kwa ninavyoelewa mimi na ndivyo ilivyo misaada yote ya nje ikiwemo na mikopo laazima znz wapate 4.5%. hivyo wafadhwili kama Global Fund, MDH, USAID, EU na wengine wote zikiwemo taasisi za fedhwa kama IMF, Badea nk zinaitambua Znz.

Labda nikupe kiduchu kuwa BAJETI KUU YA ZNZ ya 2014/15 ni 700 Bil. Matumizi ya kawaida ya Serikali (SUK) Znz ni 400 Bil. Na Bajeti yake ya Maendeleo ni 300 Bil ambazo hizo wanategemea mikopo na misaada ya nje.

Sasa tukiitazama JMTz mwaka wa fedhwa 2013/14 walipata mikopo iliyozidi 3.8 Tril. hivyo Znz walihitaji 4.5% ya fedhwa hizo nao kukamilisha na kutimiza bajeti yao.

Sio kama kila mkopo JMTz wanaokopa basi pesa hizo laazima Znz wakate 4.5% japo hawana kipaumbele na suala hilo. (Mathala JMTz inakopa 1 Tril kuboresha na kujenga miundombinu ya barabara Dar ili kuondosha foleni ) sasa inawezekana Znz walishamaliza suala la barabara na sasa kipaumbele chao ni uvuvi.

Kinachofanyika ni kupata jumla ya mikopo inayokopwa kwa mujibu wa vipaumbele vya nchi husika na kuviombea mkopo LAKIN MWISHO WA SIKU ZNZ HARUHUSIWI KUKOPA ZAIDI YA 4.5% YA DENI LA TGK kwa mwaka.

Kwa mujibu wa mkataba wa muungano na mambo yaliyoongezwa suala la ILMU YA JUU NI SUALA LA MUUNGANO.

Ahsantum

gf kuna mengi sana tumehoji.Hili la 4.5% linawatatiza hata wale wanaojaribu kulitumia.

Mfano, bajeti ya znz 2015 haina wizara ya ulinzi. Kama tutasema 4.5 ni kitokana na mikopo, na kwa mfano wa deficit ya JMT ya Trilioni 1 kwa mujibu wa watetezi, znz inapaswa kupata bilioni 45.

Nguruvi3,

Naona hapa imekupuruchuka.
Je 4.5% ya Trillion moja ni 45 Bilion?

MFUKO WA JIMBO, WABUNGE WA ZNZ
MZIGO ALIOBEBA MTANGANYIKA BILA SABABU ZA MAANA

Hoja ya misaada na mikopo, ambayo wengine tunaiona ni dhalili inazidi kukosa mashiko
Mkandara kasema, elimu ni suala la muungano na hutegemea asilimia 80-90 ya misaada.
Tunarudi pale pale, je, wahisani waliogoma kutoa misaada, vyuo vimefungwa?

Twende mbele zaidi, suala la wabunge wa znz kupewa pesa za mfuko wa jimbo.
Hizi kwa kuanzia ni rushwa, hata hivyo tujadiliane tu uhalali wake kule zinakoelekea.

Hivi kwanini mbunge wa znz anayekuja Dodoma kuwakilisha znz katika ulinzi na usalama, mambo ya ndani na nje,na taasisi za muungano naye apewe mfuko wa jimbo ambazo ni mamilioni ya sh?

Pesa za mfuko tunaamini si misaada na mikopo,, hutoka hazina Dar. Hapa kuna la kujiuliza, wabunge wa znz wapo kwa ajili ya kutetea znz na si majimbo yao. Wale wa BLW ndio wanaotetea masilahi ya majimbo.
Hawa wa Bunge la muungano wapo kwa ajili ya masilahi ya znz na si majimbo ya znz

Hakuna kiongozi wa Tanganyika anayeweza kwenda kuangalia hiyo miradi kama ikitokea!!!
Pesa zinatoka hazina ambayo Gavana kasema, wenzetu kwa miaka mingi tu hawana mchango, mbele ya waziri wa fedha wa znz.

Hata kwa manitiki haiingii akilini. Kama znz wameshapata 4.5 ya misaada na mikopo(dhalili kusema) kwanini wapate pesa za mfuko wa jimbo kutoka 95.5 ya zile za Tanganyika ikiwa tutafanya assumption kuwa ni pesa za misaada?

Kwanini wanapewa mfuko wa jimbo, jibu ni rahisi ni wabunge wa bunge la JMT.

Kiuhalisia wale ni wabunge wa znz katika bunge wenye 2/3 ya maamuzi kwa niaba ya znz.
Kupewa za miradi ya maendeleo ni kuwanyima Watanganyika.

Hawa wanakuja kusikiliza mambo ya ulinzi na usalama, mambo ya ndani na nje na taasisi za muungano kama BoT.
Hatuoni mantiki ya wao kupewa mfuko wa jimbo kutoka pesa za Tanganyika.

Ni za Tanganyika kwasababu wana bajeti yao, hawachangii na wameshachukua 4.5% na kodi 1.75 Bilioni kila mwezi kwa ajili ya znz. Wana kura yenye nguvu kwa ajili ya znz. Hawapaswi kupewa mfuko wa jimbo, hauwahusu.

Lakini pia tuangalie jambo moja. Ikiwa uwepo wao ni kwa ajili ya znz, na kura yao ya 2/3 ni kwa ajili ya znz, kwanini walipiwe gharama na JMT?

Ikumbukwe, JMT inayosemwa ni Tanganyika. Inakuwa JMT pale penye mafao, penye madeni inakuwa bara na Zanzibar.

Ndio maana tunauliza, huu mfuko wa pamoja wa kupata pesa za jimbo, mishahara ya wabunge wa znz uko wapi?
Na kwanini utaratibu wa kuwapatia mafao usiende samba mba na utaratibu wa kuchangia kwa mfumo huo huo wa kuchota?

Tunadhani, wabunge wa znz, wahudumiwe na SMZ kwa kila jambo .
Kama wapo Dodoma basi waje siku za kujadili mambo ya muungano katika wizara zisizozidi 5.

Kitendo cha wao kukaa Dodoma miezi wakijadili mambo yasiyo ya muungano ni kuingilia uhuru wa Watanganyika na kuwabebesha gharama wasizostahili kwa jina la Tanzania

Kwanini mbunge wa znz apewe fungu la kukagua shughuli za kilimo, afya, au serikali za mitaa!
Hayo ni mambo yasiyomhusu kwasababu ana kura ya 2/3 ya mambo ya muungano yanayohusu znz tu

Wapo wabunge 5 kutoka BLW. Nao wanalipwa na JMT na si SMZ au BLW.

Hawa wanakuja kusikiliza habari ambazo hakuna anyejua nguvu zake. Kwa mujibu wa katiba ya znz ya 2010, wabunge wa BLW ni wasindikizaji, hawana mchango kwa bunge la JMT wala BLW. Gharama hizi za wabunge wa znz kwanini azibebe Mtanganyika?

Haya ni mambo ambayo watetezi wa misaada na mikopo hawataki yazungumzwe.
Hata hivyo, wznz wamefungua pandora box, tutahoji kila jambo kwa utimilifu wake ili tubaini wapi wanaonewa na wapi wanaoenea.

Ni mambo ambayo Watanganyika lazima wayaangalie kwa jicho pana.

Ni gharama zisizo za lazima kwa Mtanganyika.

Bila Tanganyika, hakika Watanganyika watavaa koti la muungano likiwabana kulia kushoto. Hawana uwezo wa kulivua.

Ipo siku watatoa ya moyoni!

Tusumezane
 
Kuna suala la msingi sana umelibainisha katika manung'uniko yako NALO NI HILI LA MFUKO WA JIMBO KWA WABUNGE WA ZNZ.

Hakika suala hili niliwahi kutanabaisha wakti tunajadili kupitishwa kwa SHARIA YA KUANZISHWA KWA MFUKO WA JIMBO hapa barzani. Nakumbuka niliwahi kuhoji kuwa fedhwa hizi zinatoka katika mfuko mkuu wa Hazina. Na CAG wa JMtz ndio atakae kuwa mdhibiti wa matumizi ya fedhwa hizi yaani yeye ndie atakae kagua pesa matumizi ya fedhwa hizi.

Nakumbuka niliuliza JE KWA WALE WABUNGE WA ZNZ WALIOPEWA FEDHWA HIZI ZA JIMBO WATAKAGULIWA NA NANI? Wakti CAG wa JMTz hana mamlaka hayo ya kufanya ukaguzi Znz? nakumbuka nilipewa jibu kuwa CAG JMTz atamkaimisha madaraka hayo kwa CAG Znz aweze kufanya kazi hiyo na kumletea ripoti.

Niliguna sana kwani kwa lugha ya kiuhasibu kupokea nyaraka bila kuzithibitisha kwa macho kwa utekelezaji wa jambo hilo ni mtihani mzito sana.

Ok all in all Bunge la JMTz lilipitisha kwa kauli moja NA SASA WABUNGE WA ZNZ WANAJINOMA.

Hakika cha mjinga uliwa na mwerevu!!!.

Laiti kama wabunge wa Tanganyika na wawakilishi kutoka TGK wangesimama kidete katika Bunge la Katiba kuitetea RASIMU ya WARIOBA kama walivyofanya wawakilishi na wabunge na wajumbe kutoka Znz basi hayo MANUNG'UNIKO yangefika ukingoni.

Binafsi nawapa pole waTgk kupoteza bakhati adhwiim.

MFUKO WA JIMBO, WABUNGE WA ZNZ
MZIGO ALIOBEBA MTANGANYIKA BILA SABABU ZA MAANA

Hoja ya misaada na mikopo, ambayo wengine tunaiona ni dhalili inazidi kukosa mashiko
Mkandara kasema, elimu ni suala la muungano na hutegemea asilimia 80-90 ya misaada.
Tunarudi pale pale, je, wahisani waliogoma kutoa misaada, vyuo vimefungwa?

Twende mbele zaidi, suala la wabunge wa znz kupewa pesa za mfuko wa jimbo.
Hizi kwa kuanzia ni rushwa, hata hivyo tujadiliane tu uhalali wake kule zinakoelekea.

Hivi kwanini mbunge wa znz anayekuja Dodoma kuwakilisha znz katika ulinzi na usalama, mambo ya ndani na nje,na taasisi za muungano naye apewe mfuko wa jimbo ambazo ni mamilioni ya sh?

Pesa za mfuko tunaamini si misaada na mikopo,, hutoka hazina Dar. Hapa kuna la kujiuliza, wabunge wa znz wapo kwa ajili ya kutetea znz na si majimbo yao. Wale wa BLW ndio wanaotetea masilahi ya majimbo.
Hawa wa Bunge la muungano wapo kwa ajili ya masilahi ya znz na si majimbo ya znz

Hakuna kiongozi wa Tanganyika anayeweza kwenda kuangalia hiyo miradi kama ikitokea!!!
Pesa zinatoka hazina ambayo Gavana kasema, wenzetu kwa miaka mingi tu hawana mchango, mbele ya waziri wa fedha wa znz.

Hata kwa manitiki haiingii akilini. Kama znz wameshapata 4.5 ya misaada na mikopo(dhalili kusema) kwanini wapate pesa za mfuko wa jimbo kutoka 95.5 ya zile za Tanganyika ikiwa tutafanya assumption kuwa ni pesa za misaada?

Kwanini wanapewa mfuko wa jimbo, jibu ni rahisi ni wabunge wa bunge la JMT.

Kiuhalisia wale ni wabunge wa znz katika bunge wenye 2/3 ya maamuzi kwa niaba ya znz.
Kupewa za miradi ya maendeleo ni kuwanyima Watanganyika.

Hawa wanakuja kusikiliza mambo ya ulinzi na usalama, mambo ya ndani na nje na taasisi za muungano kama BoT.
Hatuoni mantiki ya wao kupewa mfuko wa jimbo kutoka pesa za Tanganyika.

Ni za Tanganyika kwasababu wana bajeti yao, hawachangii na wameshachukua 4.5% na kodi 1.75 Bilioni kila mwezi kwa ajili ya znz. Wana kura yenye nguvu kwa ajili ya znz. Hawapaswi kupewa mfuko wa jimbo, hauwahusu.

Lakini pia tuangalie jambo moja. Ikiwa uwepo wao ni kwa ajili ya znz, na kura yao ya 2/3 ni kwa ajili ya znz, kwanini walipiwe gharama na JMT?

Ikumbukwe, JMT inayosemwa ni Tanganyika. Inakuwa JMT pale penye mafao, penye madeni inakuwa bara na Zanzibar.

Ndio maana tunauliza, huu mfuko wa pamoja wa kupata pesa za jimbo, mishahara ya wabunge wa znz uko wapi?
Na kwanini utaratibu wa kuwapatia mafao usiende samba mba na utaratibu wa kuchangia kwa mfumo huo huo wa kuchota?

Tunadhani, wabunge wa znz, wahudumiwe na SMZ kwa kila jambo .
Kama wapo Dodoma basi waje siku za kujadili mambo ya muungano katika wizara zisizozidi 5.

Kitendo cha wao kukaa Dodoma miezi wakijadili mambo yasiyo ya muungano ni kuingilia uhuru wa Watanganyika na kuwabebesha gharama wasizostahili kwa jina la Tanzania

Kwanini mbunge wa znz apewe fungu la kukagua shughuli za kilimo, afya, au serikali za mitaa!
Hayo ni mambo yasiyomhusu kwasababu ana kura ya 2/3 ya mambo ya muungano yanayohusu znz tu

Wapo wabunge 5 kutoka BLW. Nao wanalipwa na JMT na si SMZ au BLW.

Hawa wanakuja kusikiliza habari ambazo hakuna anyejua nguvu zake. Kwa mujibu wa katiba ya znz ya 2010, wabunge wa BLW ni wasindikizaji, hawana mchango kwa bunge la JMT wala BLW. Gharama hizi za wabunge wa znz kwanini azibebe Mtanganyika?

Haya ni mambo ambayo watetezi wa misaada na mikopo hawataki yazungumzwe.
Hata hivyo, wznz wamefungua pandora box, tutahoji kila jambo kwa utimilifu wake ili tubaini wapi wanaonewa na wapi wanaoenea.

Ni mambo ambayo Watanganyika lazima wayaangalie kwa jicho pana.

Ni gharama zisizo za lazima kwa Mtanganyika.

Bila Tanganyika, hakika Watanganyika watavaa koti la muungano likiwabana kulia kushoto. Hawana uwezo wa kulivua.

Ipo siku watatoa ya moyoni!

Tusumezane
hapa naomba kwamba tuanze kwa kuulizana maswali na ninaomba Mkandara na Barubaru waanijibu.

Je wabunge wanaotoka zanzibar kuingia kwenye BLMT wanapatikana akwa vigezo gani?
Je wabunge hao wakiingia kwenye BLMT wanaingia kama wawakilishi wa majibo yao ama kama wawakilishi wa zbr?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom