Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema

jitegemee Ahsante sana kwa umakini wako na ulivyolitendea haki jamvi na bandiko. Ahsante

Mwanasheria Najma alikuwa anaongea na watu. Alichokisema wengine wamebeba. Kusema eti nikutane naye ni kunitaka nikutane na wote tunaojadiliana jamvini. Hilo haliwezekani katika maeneo ya vyombo vya habari vya kijamii

Pili, Najma ana nafasi ya kuja kujibu au kutoa maelezo kama ulivyonena,kama hawezi hilo halizuii jamii kzungumzia kauli zake.
Tuna watu tunaowajadili kila uchao, nashangaa hatujaambiwa waje hapa tuongee nao ili kutenda haki.

Tatu, Najma alipokuwa anaongea Camera na video zilikuwa zina roll, na alijua ananukuliwa.
Aliongea kama mwanasheria na kiongozi wa jamii. You tube wamepandisha video, Barubaru hajakemea,anakemea tunaotumia video.

Hizi ni jitihada za kutunyamazisha tuiseleze kilicho na ukweli. Miaka mingi umekuwepo uongo kuhusu znz dhidi ya Tanganyika.
Leo hakuna anayesimamia kuonewa. Wanaongea kuhusu kero. Kero ni 'naomba' au nipe kwa lugha ya kizanzibar na wala siyo madai.

Mkandara anasema wapewe haki yao. Tumemuuuliza haki gani walionyimwa, hana jibu.
Anasema mgao wa keki kwao ni mdogo. Tumemuuliza ushiriki wa znz katika kutengeneza keki ya taifa ni upi, hana jibu.
Huu ni mfano tu wa wale wanaoamini na kuficha ukweli na ndiyo chanzo cha sisi kusemwa tuna chuki.

Wakisema tunachuki wanamaanisha tusieleze udhaifu wa znz au ugoi goi wa Tanganyika.
Udhaifu wa zn ni kama ule wa kudai mambo 11 kuongezwa kinyemelA, Halafu wanadai haki katika hayo ya kinyemela.
Kwamba elimu ya juu si suala la muungano! wameligeuza kuwa haki tena kubwa kuliko ya wahusika

Mfano, znz ina watu 1.2 Milioni, nusu wakiishi Tanganyika bila kubaguliwa. Nafasi za elimu ya juu kwa wanafunzi wake ni 1024. Tanganyika ina watu milioni 42, nafasi za elimu ya juu kwa mikopo kwa kuangalia asilimia ni kidogo sana.

Lakini pia, hao 1024 baba zao na mama zao hawana mchango wowote katika kapu la hazina.
Na wala hawarudishi mikopo kama wale wa Tanganyika. Wa tanganyika familia zao zinalipa kodi, na inasikitisha wanarudisha mikopo.

Hii ina maana kodi ya Mtanganyika inakwenda kumsomesha mzanzibar buree, na Mtanganyika analipa mkopo au anakosa

Tukiuliza mkoa gani wenye nafasi za upendeleo kama znz, hakuna jibu.
Tukiuliza kwanini znz wana bodi yao siyochukua wabara, hakuna jibu.
Hiki hakitakiwi kusikika ndicho wanachoita chuki.
Ukisikia wanasema chuki, maana yake 'Nguruvi' kaa! kimya usiseme siri za watu.

Hoja ya misaada na mikopo iliyotumika kudanganya umma imekufa. Mungu ameonyesha wazi kuwa katika bajeti ya Tanzania ambayo ni Tanganyika inachangia peke yake kupitia mapato na misaada, asilimi 40 ni misaada kwa data zao, na asilimia 60 ni mapato.

Wafadhili wamezuia asilimia 60 ambayo ni mikopo na misaada. Hivyo nchi ya Tanzania inaendeshwa kwa asilimia 60 ambayo ni mapato ya jasho la Watanganyika.

Pamoja na hayo, Zanzibar inapata 4.5% kama kawaida kutoka BoT ambAzo hazina maelezo.
Mwanasheria Njama katika video amesema, kutenganisha bank kutaathiri znz kimapato.

Maana yake kukiwa na central bank moja, na bank zingine za washirika, znz haitakuwa na loophole ya kujizolea 4.5 ya pato la Mtanganyika.

Na katika hoja hiyo, kuna suala la 1.75Bilioni za watumishi wa taasisi za muungano.
Utashangaa wizara ya afya, ujenzi, nishati n.k. si za muungano, ni za Tanganyika, bado tunalipa pesa kwa znz kwa kuleta watu wake, jambo la hisani.

SMZ haikusanyi hata milioni 100 kwa mwezi, uhalali wa kupata 1.75 kama alivyosema Najma wanaupata wapi?

Wafanyakazi wa muungano wanalipwa mishara na kodi za Watanganyika.
Halafu znz wasio na mchango au gharama za ajira hizo wanazoa 1.75 Bilioni za Watanganyika.

Tukisema hayo wanasema chuki, hawakatai kwamba ni uongo. Wanachotaka tusiseme ili kuendelea na zile kelele za kizanzibar za inaonewa. Hivi inaonewaje katika hesabu za Bilioni 400 kwa mwaka na Bilioni 300 za Tanganyika ili kufidia Bilioni 700.
Wanasema hatujui uchumi, lakini hawaelezi kiuchumi uhalali wa znz kuchota 1.7 Bilioni na 4.5% unatoka wapi.

Kazi yetu ni kuwaonyesha Watanganyika ,dunia ya leo muungano ni uchumi na siasa.
Muungano wetu ambapo Tanganyika imetuhumiwa, hakuna chochote cha maana inapata ukiwepo au itakosa usipokuwepo.
Kilihchopo sas a ni ile spirit ya Pan Africanism tu lakini hakuna manufaa ya kiusalama, kiuchumi au kijamii kwa Mtanganyika.

Ndipo linakuja swali,. Kama ni hivyo kwanini znz inapewa kipaumbele kuliko wenye muungano!
Mchango wa znz katika muungano ni herufi mbili ZN. Kwanini Watanganyika wakamuliwe kodi na masialhi mengine kwenda sehemu isiyo wahusu?

Haiwagusu kwasababu ukisoma bandiko moja hapo juu, wznz wanaita Tanganyika nchi jirani.

Sasa kwanini Bilioni zaidi ya 300 na huduma za ulinzi, mambo ya ndani hadi umeme ziende kuhudumia nchi jirani ya znz?

Kwanini pesa hizo zisitolewe mikopo kwa wanafunzi waliodhulumiwa nafasi zao na wale wa znz?

Kwanini pesa hizo zisiendeleze bonde la mpunga la Ruvu, au Kilombero au Kyela?

Kwanini Watanganyika wachangishwe pesa za maabara, ili hali wznz wanchukua tu bila kuwa na impact ya aina yoyote katika maisha yao? Na kwanini Watanganyika wadhani kutenda wema ni wajibu wao, na kibaguliwana wznz ni haki yao

Hawa waliokimbiza gesi na mafuta debe mbili, watamjali Mtanganyika kwa lipi wakifanikiwa?
Hii investment wanayofanya Watanganyika return yake ukiacha matusi ni ipi hasa

Tusemezane
 
Last edited by a moderator:
Nyekundu: Hapa haujitendei haki kwa kumkingia kifua chako Waziri wako wa sheria, ili kauli zake zisijadiliwe hapa jukwaani kwa kigezo cha 'si vizuri kutumia video kujadilia'. Na sema haujitendei haki kwa sababu, kwanza kwa taratibu za jukwaa hili hakuna mahala pameelekeza kuzuia hilo. Pia kumbuka Mwanasheria wa Zanzibar ni mtu muhimu huko zanzibar na mahala pengine ambapo kuna wadau wanaoguswa na tasnia ya sheria. Kujadili kauli zake kupitia nukuu za video ni muhimu pia.

Na shangaa hotuba za wabunge, madiwani, kada wa vyama, marais, wahandisi, walimu, nakadhalika kauli zao zinajadiliwa kwa kutumia vyombo mbalimbali tofauti na vyombo ambavyo walivitumia kutoa kauli zao, na wala hakuna malalamiko kama haya ya kwako dhidi ya mwanzisha mada hii...! Mwezi disemba tumejadili hotuba ya Prof. Jakaya aliyoitoa kuhusu escrow... kwa kutumia video, magazeti n.k.(wakati yeye alitoa kauli zake kwa njia ya redio na televisheni, hatujamsikia Salva R. akilalamika); bado tunaendelea kujadili hotuba mbalimbali za Baba wa Taifa la Zanzibar Sheikh A. A. Karume (R.I.P), Baba wa taifa la Tanganyika baadaye Tanzania Mwl. J.K.Nyerere (R.I.P) walizozitoa na kunakiliwa katika video bila kukingiwa vifua...tena hao hatunao kimwili...!!!

Hivi unajua sababu za hao walioweka video hizo Youtube...!? Sababu kubwa, naweza kuhakikishia, ilikuwa watu wote wajue kilichosemwa na mwanasheria na wenzake, na wakijadili. Walijua kabisa akina Nguruvi3 na wenzake akiipata wanaweza kuijadili. Na mijadala inafanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo hii ya hapa JF. Nguruvi3 anaanzisha mada hapa jukwaani kwa lengo la kueleimisha, kuhabarisha, na kujieleimisha(3K) kupitia mijadala. Neno alitumialo (Nguruvi3) la Tusemezane kwa kiasi kikubwa linabeba dhana hiyo ya 3K.

Si vyema/vema hata kidogo kijinyima haki ya kujielemisha, kuelimisha, kuhabarisha kwa kuzuia mijadala inayotokea kutokana na kauli wanazozitoa na kunakiliwa katika vyombo mbalimbali vya mawasiliano kisa tu lazima wahusika wahusishwe kwenye mjadala. Wewe ni 'member' humu JF muhabarishe (mwanasheria wako) aje ajiunge jukwaani ili ajibu hoja zinazotolewa juu ya kauli zake alizozitoa na kunakiliwa kwenye video.

Bluu: Ushauri wako si mzuri, kama kweli unataka kujitendea haki pia kumtendea haki mwanasheria wako mshauri ajiunge JF na aanze kujibu hoja zinazomkabili hapa, kama nilivyoelekeza aya ya mwisho ya sehemu ya kwanza.

Kijani: Nafasi iko wazi hapa JF wala hajachelewa.

TUJITEGEMEE.

Ahali yangu nakushukuru sana kwa mawazo yako na nimeyahishimu sana kwani huo ni mtazamo wako ambao mimi sikubaliani nao japo nimeuhishimu.

Kumbuka kuwa msema pekee kila siku anashinda na katika lugha a sirka za uandishi ni laazima habari yoyote i-balance katika mizania yake. Kwa maana ya kutenda haki kwa pande zote ndio maana nikashauri hivyo.

Vile vile nilihishimu sana maneno aliyosema Mwanasharia Najma kwani hayo ni mawazo yake kama yyeye na wala SI YA WAZNZ wote . Kwa hiyo unapomjadili basi watendee haki wa Znz kwa ujumla wao kwani Najma ni mtu mmoja tu kati ya waZnz 1.5 Million waliopo Znz na hawezi kuwakilisha mawazo ya waZnz wote.

Ndio maana katika mujadala huu wa Katiba pendekezwa kutakuwa na makundi maiwli (KUNDI LA KUIKUBALI NA KUITETEA na KUNDI LA KUIPINGA NA KUIKATAA) na katika kila kundi linakuwa na ushawishi wao katika jamii na NDIO MAANA MWISHO WA SIKU ZITAPIGWA KURA KUAMUA NANI MSHINDI.

Na ndio maana ninasema kuchukua maneno ya mtu mmoja na kuyanasibisha na jamii nzima ni kutowatendea haki jamii ile.  Mathalan jana usiku nilibahatika kukaa katika maskani moja hapa unguja na watu wa CCM akiwemo kiongozi mkubwa sana wa chama naye alijikita kusema kuwa Znz mnanufaika sana na Katiba pendekezwa nami nilimuuliza je wananufaikaje katika nyanja ya uchumi, na aliweza kujieleza kwa kile alichoojaaliwa kusema japo kilikuwa na mushkira kibao.

Siku zote NASHAURI USIONGEE JAMBO USILIKUWA NA UJUZI NALO. nitakupa mfano mdogo hapo. Nguruvi3 anadai Tanganyika inalipa mishahara kwa staff wa SUK Znz.
Sasa kwa wasomi tunajiuliza je hii JMTz itawezaje kulipa mishahara kwa watu wa SMZ ikiwa bajeti yake ya 2014/15 imeonyesha inahitaji iwe na 19.2 Trillion. katika hizo matumizi ya kawaida ya Serikali ya JMTz ambayo ni kulipana mishahara ,posho,semina na uendeshaji wa ofisi zake ni 13.6 Trillion.  Na ukiangalia makusanyo yake yooote kwa mwaka ni 12.4 Trillion. hivyyo ina upungufu wa zaidi ya trillion moja.  sasa najiuliza itawezaje kulipa watu wa SMZ wakti wenyewe wameshindwa kujikimu?

Utaona wazi kuna mushkira hapo kwa mwandishi kama si kutaka tu kufurahisha barza BILA KUJUA KUWA UCHUMI NI DATA.

Hakuna kitu kibaya katika uandishi KAMA USHABIKI na kuzua mambo yasokweli kuyatakasa katika jamii yaonekane ni kweli.

Pole sana
 
HOJA YA MISAADA NA MIKOPO IMEKUFA

Hoja ya misaada na mikopo imetumiwa sana kukingia kifua Zanzibar.
Kwamba, ile asilimia 4.5 inayopewa znz ni kutokana na hayo mawili.

Wapo wanaosema 4.5% inatokana na hisa zaznz katika BoT.
Alhasir hakuna mwenye jibu la kueleza 4.5% inapatikanaje.
Nawala haielezwi, 4.5% ni makadirio ya bajeti au ni ya pato la Tanganyika. Na pia haijuikani 4.5% ilizingatia vigezo gani.

Kinachoeleweka leo ni kuwa wahisani wamesitisha takribani Trilioni 1 kama misaada.
Swali la kujiuliza, je 4.5 yawazanzibar kutoka BoT nayo imepungua?

Na kama jibu ni hapana, Kuna uhalali gani wa kusema 4.5% ni misaada na mikopo ikiwa Tanzania yenye znz imenyimwa na wafadhili!

Endapo 4.5% ni pato la Tanganyika, je,ni kigezo gani kimetumika ili kufikia kiwango hicho?
Ikumbukwe unapoweka asilimia, nayo hupanda na kushuka kutegemeana na namba inayozungumziwa.
Je, iliwahi kutokea znz ikapata chini 4.5% kwasababu mapato ya Tanganyika yalipungua?

Hoja ya pili, kwasasa znz inapata 1.75Bilioni kama kodi ya wafanyakazi wa muungano.
Swali linakuja, ni idadi gani yawafanyakazi wa znz iliokikotolewa hadi kupatikana 1.75 Bilioni kama alivyosema mwanasheria Najma na waziri Samia Suluhu

Hii ina maana kuwa znz ikiwa na wafanyakazi 10 itapewa kiasi hicho, wakiwa 100 au 20,000 ni kiasi hicho hicho.
Kiwango hicho fixed kinatia shaka. Je, serikaliikipunguza au kuongeza watumishi wa muungano, upo uwezekano wa znz kupata Zaidi au pungufu ya 1.75Bilioni kwa mwezi.

Hoja ya tatu, hao wafanyakazi wa muungano wanayoipatia znz 1.75Bilioni, mishahara na mafao yao yanalipwa nanani?
Ni mchango gani wa znz inayopokea 1.75B katika kuhakikisha kabla ya kupata mgao, wznz wanawajibika kuhudumia watumishi hao
?

Hoja hizoni muhimu kwa kuzingatiaukweli kuwa, gavana wa BoT akiwa na waziri wa fedha wa znz ndani ya bunge walisema znz haina mchango katika muungano kwa Zaidi ya miaka 30.

Waziri wafedha wa znz alikuwepo na hakukanusha. Hivyo hakuna shaka znz haina mchango.
4.5 tunazoelewa si misaada au mikopo, 1.75 Bilioni za kodi za watumishi wa muungano zinatoka katika mfuko gani?

HOJA YA MFUKO

Ipo hija dhaifu kuwa hakuna mfuko wapamoja wa znz kuchangia. Kama ni hivyo, mfuko gani wa pamoja unaoruhusu znz kuchukua 4.5% na Bilioni 1.75 achilia mbali huduma za bure kama ulinzi nausalama, mambo ya ndani n.k.

Waziri wa fedha wa znz, na mbunge wa CUFJusa kwa nyakati tofauti wamekiri kuwepo kwa fedha za muungano kusaidia bajeti ya znz. Kama fedha hizo zinatoka Tanzania ambayo znz imo, je znz inachangia nini kwa Tanzania hiyo hiyo?

Iweje kuchota kusiwe na kikapu, lakini kuweka watu wanauliza kikapu kiko wapi!
Haa!
ala

Hapa ndipo Watanganyika wanatakiwa wafungue macho na kuhisi maumivu ya zigo waliobeba
Haiwezekani kodi za Watanganyika zitumike nchi jirani kama wanavyotuita Wazanzibar, kwa gharama ya wananchi wetu.

Nguruvi3,

Hoja ya 4.5% si ngeni ni ipo wazi sana na inaeleweka LABDA KWA WALE WASIOTAKA KUFATILIA MAS'ALA YA UCHUMI WENU. Mimi nakushauri waulize wataalamu wa uchumi wa Tanzania wanaounda JOINT FINANCE COOMMISSION jfc (TUME YA PAMOJA YA FEDHWA NA UCHUMI WA NCHI HIZO MBILI katika utafiti wamebainisha mchana kweupee. NAKUSAIDIA TENA PITIA AFISI ZAO ZILIZOPO SUKARI HOUSE POSTA DAR Kwa ufafanuzi na darsa zaidi au hata website yao Joint Finance Commission.

Nafikiri utapata darsa kubwa na kukidhi haja yako insh'Allah.

Nilipo RED.

Siku zote pesa za Serikali yoyote iwe ya Znz au JMTz zinapotolewa au kupokelewa kwa mujibu wa kaanun za Fedhwa laazima ziwe documented na docs hizo laazima zionekane kwenye vitabu vya mapato na matumizi. Kwa suala la nchi mambo haya ya fedhwa yanaonyeshwa katika RIPOTI YA CAG au KATIKA UTEKELEZAJI WA BAJETI WA MWAKA ULIOPITA AU BAJETI YA MWAKA ULIOPO WA FEDHWA.

Maneno ya WAZIRI au mwanasiasa yoyote katika mfumo wa fedhwa bila kuonekana katika vitabu vya fedhwa HAYANA NAFASI.

Sasa hebu tudadavulie hayo aliosema waziri ay Jussa je yapo katika ripoti ya CAG ya mwaka gani? au Utekelezaji wa bajeti ya mwaka gani? na kama yaliwekwa katika bajeti basi tueleze katika bajeti ya mwaka gani na kifungu kipi?
KUMBUKA UCHUMI SI BLAA BLA NA POROJO BALI NI DATA ZILIZO WAZI NA MCHANA KWEUPEE.

Mimi nakurudisha tena katika bajeti ya JMTz ya mwaka 2014/2015 inaonyesha wazi kuwa Jumla ya bajeti kuu ya mwaka 2014/2015 ni T Sh 19.2 Trillion.
Matumizi ya kawaida ni Tsh 13.6 Trillion
Pesa zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ni Tsh 5.6 Trilion.
Makusanyo yoote ya nchi kwa mwaka mzima ni Tsh 12.4 Trillion.

Kwa msingi huo utaona wazi bajeti ya JMTz ina mapungufu ya zaidi 1 Trillion katika pesa zake za kulipana mishahara na mambo mengine ya uendeshaji wa serikali.
Vile vile JMTz haiwezi kuwa na maendeleo kutokana na kukosa pesa za ndani za bajeti kwa ajili ya maendeleo.

Kiuchumi tunasema bajeti ya JMTZ ni tegemezi kwa maana inategemea zaidi ya 15% ya matumizi yake ya kawaida KUTOKA KWA WAHISANI NA MIKOPO. LAKIN VILE VILE INATEGEMEA KWA ZAIDI YA 86% PESA ZA WAHISANI NA MIKOPO KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA MAENDELEO.

Sasa huo ni uchambuzi kutoka katika Kitabu cha BAJETI YA JMTz 2014/2015. sasa hebu jipime na hicho unacholalama na kunung'unika pasi na kuwa na REF.

Labda tuweke wazi hilo kapu wanalochangia TGK lipo wapi ili na waznz wachangie?. nani msimamizi wa mapato na matumizi wa kapu hilo?

Pole sana ahali yangu tumezowea kunung'unika kwako LAKIN TU INATUUMA UNAPOTWISHA ZIGO HILO KWA ZNZ NA WAZNZ wakti EPA, Tegeta Escrow mmekula wenyewe lakin we unawashupalia Znz.

Utakufa na kijiba chako cha Roho na Znz huru ileeeeeeeee.

Pole SANA TUSEMEZANE KATIKA UKWELI NA SI KUONGOPEANA BILA KUWA NA ref.

Na mimi nilikuwa naswali kwako mh nguruvi03 hasa hapo unaposema Jusa amesema bajeti ya serikali ya znz inachangiwa na pesa toka serikali ya JMT(TGK&ZNZ), sasa utatumiaje maneno ya mwanasiasa kujustfy hoja yako nzito ambayo inaitaji ushahidi wa number? Kama kataja ni kiasi gani kakitaja twaombea utusaidie wasomaji. Nadhani ukija kumjibu Barubaru hutolisahau hili.
 
Kuna kitu kimoja ninachokiona. Kwanza, nliposema waziri wa fedha na Jusa, na sasa naongezea Tundu Lissu ninajaribu kuonyesha kuwa suala hili halikuwa lakisiasa bali la namba.
Ipo video nitaitafuta ikionyesha jinsi senti za bajeti ya znz zinavyopataikana kutoka katika Muungano ambao basically ni Tanganyika tukijua kuwa znz haina mchango, na hapa nasema tena, kwa mujibu wa gavana wa BoT na Waziri wa fedha wa SMZ.

Mwaka 2013/14 Zanzibar ilipewa Bilioni 32 kupitia ofisi ya makamu wa Rais wa JMT.
Pesa hizo hazipo katika mfumo mnaoujua ninyi. Hili tumelijadili sana na JokaKuu Mchambuzi na wengine na hakuna ubishi.
Maelezo yaliyotolewa ni kuwa pesa hizo ni kwa ajili ya mazingira. Katika taarifa zote za umma hakuna mahali imeonyeshwa.

Pili, Znz ina mapato ya Bilioni 400. Bajeti yake inatarajiwa kuwa na Bilioni 700.
Znz kwasasa hairuhusiwi kukopa nje. Katika bajeti ya mwaka 2014 hakuna mahali ime justify mapato ya nakisi tajwa.

Tatu, Ni wapi kuna sheria ya umma inayoeleza znz ipate 1.7Bilioni? Lakini zinakwenda kule kila mwezi.
Ni formula gani imetumika kupata 1.75, sijui kama unaweza kunipa. Lakini je, si kweli kuwa znz inapata kiasi hicho?

Nne, 4.5% inayopata inaonekana wapi katika bajeti ya Tanzania ya mwaka 2014. Je, si kweli kuwa znz inapata 4.5% ya pato la Mtanganyika? 4.5% inaonekana wapi katika bajeti ya znz ya 2014. Je si kweli znz inapata kiasi hicho.

Tano, nenda katika bajeti ya znz ya mwaka huu, nionyeshe wapi znz imeonyesha kulipa deni la ndani na nje.
Ukishatambua haya nadhani utapata jibu. Kwa namba znz haonyeshi madeni yake yanalipwaje. Umenielewa?

Hivyo, ningeomba uninukuu kikamilifu, kisha uelewe mantiki ya hoja bila kutafuta neno moja ili kujenga hoja.

Kuhusu Baru baru, nadhani umesoma bandiko langu, nilishampuuza.
Lengo lake ni kuteremesha hadhi ya mjadala na kuufanya uwe wa maskani na kitoto.

Tofauti yangu na yeye ni kuwa mimi naongelea hoja, yeye ananiongelea mimi(personality).
Ana haki ya kuiongelea personality yangu hadi Serana Hotel, sijibu hoja zake, si lengo la bandiko kuzungumzia matusi na personality.

Ndio mana unaona hata akiwa na hoja za maana tunampuuza, na huko kwingine jamvini alishapuuzwa
 
MASWALI YASIYO NA MJAIBU YANAONGEZEKA

Tumeuliza,ni hesabu gani na vigezo gani vimetumika kupata 4.5% kutoka Tananyika?
Ipo hoja kutoka kwa wznz na baadhi ya mashabiki kuwa 4.5 ni mgao wa hisa za BoT
Pili, ipo hoja 4.5 ni misaada na mikopo

Kwa hoja ya pili, kama ni misaada na mikopo, je wahisani walipositisha kiwango cha 4.5% kimepungua kwenda znz.
Na pia tunafahamu, kiasi walichositishani takribani Trilioni 1. Kwa kiwango cha 4.5, znz isingeweza kupata Zaidi yabilioni 50.

Je, baada ya misaada kusitishwa, znz imeendelea na 4.5% au hali ipoje na kwa kiasi gani?

Endapo hoja ni gawio la BoT, ni utaratibu gani unatumika kugawana bilaku-support mtaji huo wa znz kwa miaka Zaidi ya 30 kwa mujibu wa gavana wa BoT na waziri wa fedha wa znz?(znz haijachangia muungao)

Kinachoonekana hapa ni kitu kimoja, hakuna justification yoyote au maelezo ya maana ni vipi asilimia 4.5 ilifikiwa.
Na hakuna sababu za kwanini znz ipate 4.5.

Sababu zilizopo zinabadilika kila asubuhi ikiwa ni ushahidi kuwa4.5 ni kundi la watu wameamua bila hesabu za kutueleza. Vinginevyo atokee mtu atuelimishe, 4.5% imepatikanaje

HOJA YA PESA ZA WATUMISHI WA MUUNGANO

ZNZ inapata 1.75 Bilioni kwa mwezi kama kodi ya watumishi wa muungano
.Bado tunauliza, ni watumishi wa maeneo gani ili hali kuna maeneo si yamuungano? K

wa mfano wznz wanaofanya kazi wizara ya maliasili, afya, kilimo,nishati au uvuvi, wana sababu gani za kulipiwa kodi kule znz ikiwa wizara hizo si za muungano?

Hapa napo kuna hoja inajirudia sana, ni kigezo gani kimetumika kupata kiwango hicho cha kodi kwenda znz.
Je, SMZ inapata kodi ya bilioni 1.75 kutokakwa watumishi wake?

Hoja hizi zitajirudia sana, dhumuni kubwa ni kuwaonyesha Watanganyika jinsi ambavyo muungano huu walivyo ubeba kwa gharama kubwa. Kwamba, kuna vitu havina formula bali hisia tu na Watanganyika wanalazimika kulipia.

Tume ya Warioba ilipotenga nchi hizi kwa uwazi, lengo lilikuwa kuondoa manung'uniko yanayojitokeza hasa baada ya Watanganyika kutambua uzito walioubeba begani.

Hoja kubwa ya tume ilikuwa kushirikiana kwa uhalali na kwa njia za wazi.
Kinyume na maoni ya tume, muungano huu upo hatarini kuvunjika kabisa.
Utavunjika kwasababu
Watanganyika wameng'amua mengi mazito kuliko madai ya wznz.

Kama wznz wanahoja ya muungano wa nchi mbili sawa zilizo huru na hivyo uwepo usawa, basi pia wanawajibu wa kutuonyesha ni kwa vipi wanawajibika katikamuugano huo wanaoudai katika usawa.

Ndipo swali la leo lilipo, ni nani anaweza kutonyesha kuwajibika kwa znz katika kuendesha na kuendeleza muungano?

Tusemezane
 
UTATA ZAIDI KATIKA HUU MFUMO WA MUUNGANO
NANI ANAZUNGUMZA KWA NIABA YA TANGANYIKA?

Tumeshaona utata kuhusu pesa za BoT za malipo ya 4.5%Tumeangalia kodi za watumishi wa muungano
Huko nyuma tumeangalia kuhusu gharama za bunge na wabunge

Turudi kwenye bunge na wabunge wa JMT. Wote ni wa wabunge wa JMT. Wakati wa kuamua masuala ya muungano, znz wanapewa 2/3
Hatujui Watanganyika wanapewa kiasi gani kwasababu hakuna Wabunge wa Tanganyika
Tunachojua ni 2/3 ya wabunge wa Bara ambao ni wa JMT kama wale wa znz

Ni haki kusema, kura zinakuwa baina ya Tanzania na visiwani. Mtanganyika hana kura, ni Mtanzania. Mzn anabaki kuwa mzanzibar

Inakuwaje gharama za wabunge wa znz zilipwe na JMT ikiwa wamekuja kwa ajili ya kutetea maslahi ya znz?
Kwanini wasigharamiwe na nchi wanayowakilisha.

Kwanini mzigo wa wznz aubebe Mtanganyika kwa jina la Tanzania, ili hali mznz yupo kwa maslahi ya znz?

Utata mwingine ni pale wabunge wa znz wanapolipiwa gharama ndani ya kamati za bunge. Ni haki kuwa miongoni mwa wanakamati kwa zile sughuli zinazohusu muungano.
Inakuwaje mbunge wa znz anakwenda kuhoji masuala ya TBS ikiwa wana ZBS isiyo na uhusiano na Tanzania?

Ni kwanini mbunge wa znz aende kukagua na kuhoji shughuli za madini, kwa mfano suala la gesi na mafuta, ili hali si jambo la muungano?
Ni kwanini mbunge znz ahoji huduma za elimu na afya tukijua si mambo ya muungano?

Inakuwaje mbunge wa znz kuzungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa, kukagua shughuli za serikali za mitaa na kuhoji ofisi ya waziri mkuu ikiwa, kwanza, serikali za mitaa si jambo la muungano na pili waziri mkuu hatambuliki znz.

Hivi,kuna uwezekano Mtanganyika akawa waziri wa afya wa znz, kama ambavyo mznz ni waziri wa afya Tanganyika?
Kwa znz hilo haliwezekani kwasababu ya ubaguzi na kutetea masialhi yao.

Waziri wa afya mznz anatetea masilahi gani ya wznz katika wizara isiyomhusu,anakuwaje mzalendo kwa wizara ya nchi jirani kama wanavyotuita?

Kizungu zungu chote ni kwasababu ninyi Watanganyika ni Watanzania tu, lakini wazanzibar ni wznz na ni Watanzania wanapowahitaji.

Ndio maana ni rahisi wznz kuleta bili zao ili mshughulikie kama Watanzania. Lini wamekuja na hoja inayotetea maslahi ya Watanzania

Wznz wanalani dubwana muungano(rejea maongezi ya video za nyuma) hawataki muungano unaowanyonya.
Wanataka kitambulisho cha Tanzania waje kubabana na Watanganyika.

Swali, ninyi Watanganyika mnakitambulisho cha uzanzibar ukaazi? Mnaweza kukipata hata kwa bahati mbaya?

Wapi kitambulisho cha Mkigoma mkaazi, au Mlindi mkaazi au Msingida mkaazi?

Tusemezane
 
Nguruvi3 heri ya mwaka mpya.
napenda kumshukuru sana ndugu yangu TUJITEGEMEE kwa bandiko lake zuri lenye utash wa hali ya juu.
haya hapa naomba nikwambie jambo moja sana tutakaa miaka 800 bila kuona mchango wa Z'bar kwenye keki ya taifa.
Wazanzibar acha wale urojo na tende tunawawajibikia sana, kimsingi wao kila wanachokifanya ni chao, na bado na siye tuwafanyie tugawane.

Muungano unamapungufu mengi sana tena ambayo yanatakiwa kurekebishw maapema lkn viongozi wetu wako kimya na tukitaka kusema lolote tunanyamazishwa.

am praying ifike mahali uvunjike tu
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin

Wengine tumekubali kuvaa ubaya, tukiitwa tuna chuki, bongo lala, wambeya n.k.
Tumekubali ili kuondokana na utamaduni wa ‘mambo tambarare' ilihali si nzuri

Tunaitwa wenye chuki kwakusema siri zisizotakiwa kusemwa.
Tulichopaswa kufanya ni kuendelea na wimbo wa Zanzibar inaonewa, inapunjwa n.k.

Tumefanikiwa kumaliza hadithi za uonevu. Hakuna anayesimama kutuonyesha uonevu upo wapi.
Sisi tunasimama kuonyesha Watanganyika wanavyomenyeka na mzigo huu.

Kwasasa lugha inayotumika ni kero. Kero ni pale waznz wanapodai haki wasiokuwa nayo.
Tumeonyesha mfano wa kero, wanasema, kero ni kuruhusiwa kuingiza bidhaa Tanganyika bila kodi

Kero nyingine ni kodi za watumishi wa muungano ambao znz haijui wanalipwa na nani lakini wanapewa.
Kwao kodi ni kero, haijalishi nani analipa hao wafanyakazi

Kero nyingine ni asilimia 21 ya watumishi na haijulikani inapatikanje
Hata pale SMZ inapoajiri chini ya 10,000, bado wanataka muungano uwape zaidi ya kile wanachoweza tena wakidai kama haki.
Mfanyakazi wa wizara ya uvuvi Tanganyika anawahusu nini hadi alipe kodi kwao?

Kero nyingine ni kudai 7% badala ya 4.5% bila kujua wanadai kutoka mfuko wa nani

Tunawaeleza Watanganyika jinsi walivyobeba mzigo tena wakiitwa nchi jirani(nukuu ipo katika maandishi katika mabandiko ya nyuma).

Tunawaonyesha Watanganyika hesabu zisizo na formula zinavyotumika kuwaumiza

Tunawaonyesha Watanganyika mengi waliyokuwa hawajui kutokana na wingi wa kelele za znz inaonewa.

Na sasa Watanganyika wanajitambua kuliko wakati mwingine.Kujitambua huko ndilo bomu linalosubiri muda.

Profesa Palamagamba kasema, Watanganyika wana yao vifuani. Siku wakiyatoa hapakalika tena.
Na hapa tulipo sasa si kifuani, bali yapo kwenye koo.
Ni suala la muda tu yatatoka.

Tatizo ni kuwa yakitoka hakutakuwa na muda wa majadiliano. Hatari hiyo haionekani lakini ipo and is for real.

Kibaya zaidi badala ya kuwasikiliza, wanabezwa na kutukanwa.

Mfano, rasimu ya Chenge/Sitta/CCM imekubali madai ya wznz kuwa udhamini wao katika mikopo ya nje uwe kikatiba.

Hii maana yake ni kuwa wznz watakopa watakacho, na deni atatupiwa Mtanganyika.

Ndio hasa msingi wan chi yenye wakazi 500 kwa wakati mmoja kuwa na makamu wawili wa rais.
Hawajui uzito na gharama,wanapata mgao usio na hesabu kutoka Tanganyika.

Hapa ndipo Watanganyika wajiulize, je wanataka kumaliza tatizo au kurithisha tatizo kubwa tena ndani ya katiba kwa vizazi vyao?

Na wznz wajiulize, siku ya Watanganyika yakitoka vifuani watajificha wapi?

Je, si kweli kuwa heri nusu ya shari kuliko shari kamili!! Warioba alitaka kuwasaidia, hawataki.

Je, mbele kuna future ikizingatiwa mwamko wa Watanganyika katika suala hili?
 
Kuna kitu kimoja ninachokiona. Kwanza, nliposema waziri wa fedha na Jusa, na sasa naongezea Tundu Lissu ninajaribu kuonyesha kuwa suala hili halikuwa lakisiasa bali la namba.
Ipo video nitaitafuta ikionyesha jinsi senti za bajeti ya znz zinavyopataikana kutoka katika Muungano ambao basically ni Tanganyika tukijua kuwa znz haina mchango, na hapa nasema tena, kwa mujibu wa gavana wa BoT na Waziri wa fedha wa SMZ.

Mwaka 2013/14 Zanzibar ilipewa Bilioni 32 kupitia ofisi ya makamu wa Rais wa JMT.
Pesa hizo hazipo katika mfumo mnaoujua ninyi. Hili tumelijadili sana na
JokaKuu Mchambuzi na wengine na hakuna ubishi.
Maelezo yaliyotolewa ni kuwa pesa hizo ni kwa ajili ya mazingira. Katika taarifa zote za umma hakuna mahali imeonyeshwa.

Pili, Znz ina mapato ya Bilioni 400. Bajeti yake inatarajiwa kuwa na Bilioni 700.
Znz kwasasa hairuhusiwi kukopa nje. Katika bajeti ya mwaka 2014 hakuna mahali ime justify mapato ya nakisi tajwa.

Tatu, Ni wapi kuna sheria ya umma inayoeleza znz ipate 1.7Bilioni? Lakini zinakwenda kule kila mwezi.
Ni formula gani imetumika kupata 1.75, sijui kama unaweza kunipa. Lakini je, si kweli kuwa znz inapata kiasi hicho?

Nne, 4.5% inayopata inaonekana wapi katika bajeti ya Tanzania ya mwaka 2014. Je, si kweli kuwa znz inapata 4.5% ya pato la Mtanganyika? 4.5% inaonekana wapi katika bajeti ya znz ya 2014. Je si kweli znz inapata kiasi hicho.

Tano, nenda katika bajeti ya znz ya mwaka huu, nionyeshe wapi znz imeonyesha kulipa deni la ndani na nje.
Ukishatambua haya nadhani utapata jibu. Kwa namba znz haonyeshi madeni yake yanalipwaje. Umenielewa?

Hivyo, ningeomba uninukuu kikamilifu, kisha uelewe mantiki ya hoja bila kutafuta neno moja ili kujenga hoja.

Kuhusu Baru baru, nadhani umesoma bandiko langu, nilishampuuza.
Lengo lake ni kuteremesha hadhi ya mjadala na kuufanya uwe wa maskani na kitoto.

Tofauti yangu na yeye ni kuwa mimi naongelea hoja, yeye ananiongelea mimi(personality).
Ana haki ya kuiongelea personality yangu hadi Serana Hotel, sijibu hoja zake, si lengo la bandiko kuzungumzia matusi na personality.

Ndio mana unaona hata akiwa na hoja za maana tunampuuza, na huko kwingine jamvini alishapuuzwa

Nguruvi3,

Ndio maana kila wakti nasema unaongea MAMBO USOKUWA NA UJUZI NAYO.

Nilipo RED

Mosi, Je itawezekana vipi pesa ya Serikali ikatoka nje ya mfumo uliowekwa na kutungiwa sharia na Bunge? Tujaaalie basi Znz walipewa hizo 32 Bil na jirani zao wa JMTz (ingawa mimi kitaaluma haiingii akilini) je tujaribu kupitia ripoti ya CAG kuhusu pesa hizo tuangalie je kulikuwa na Q hapo?

Mimi ninavyojua na ndivyo ilivyo kila pesa inayotoka wizara ya fedhwa ya JMTz ni laazima iwe doc na kule inakopokelewa laazima iwe doc pia na CAG ana mamlaka ya kukagua kila pesa iliyotoka na ilivyotumika. Na kama ilipelekwa Znz basi afisi ya CAG JMTz atawasiliana na mwenzake wa Znz (CAG Znz) katika ufatiliaji huo na taarifa zao zinawekwa hadhwarani.

Sasa nashindwa kukuelewa unapojaribu kusema uongo ambao kwa mwanataaruma yoyote wa uchumi au mambo ya fehdwa anakuona unakurupuka.

Pili.
bajeti kuu ya Znz 2014/15 ni Tsh 700 Milion.
Fedhwa zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ni Tsh 450 Milion
Fedhwa zilizotengwa kwa maendeleo ni 250 Milion.
Makusanyo yake ya ndani ni Tsh 380 Milion
Huu ndio usahihi wa bajeti ya Znz ya 2014/2015.

Kumbuka kuwa Znz kama ilivyo kwa JMTz bajeti zao zooote ni tegemezi.Na bajeti zao zinategemea MISAADA YA MIKOPO YA NDANI NA NJE YA NCHI.
NAPENDA NIKUPE TAARIFA kuwa kuna % iliyokubalika na Tume ya wataalamu wa fedhwa na uchumi wa nchi hizo mbili yaani Joint finance Commission (JFC)ya misaada na mikopo ambayo inapelekwa Znz katika utekelezaji wa BAJETI yao. SI KILA MKOPO AU MSAADA NI WA TGK TU NA ZNZ WAMO HUMO
.

Tano
Kama umepitia Bajeti ya Znz ya mwaka 2014/2015 pitia katika wizara ya ilmu, mafunzo ya amali utaona pale Znz imetenga pesa maalum kulipa malimbikizo ya uhamisho na masurufu na mishahara ya waalim.

Nilikuwa napitia kwa haraka haraka wizara ya afya Znz walikuwa wakilipa wametenga pesa za kulipa malimbikizo ya overtime na uhamisho wa wafanyakazi wa wizara hiyo kwa 86%.

Sasa unaposema bajeti ya Znz haionyeshi kulipa madeni sijui wasomaji wakuelewe vipi Nguruvi3.

Tatizo lako ni uchache wa Ilmu hususan ya mambo ya uchumi na fedhwa kwani unapenda kuongea saaaana uchumi bila kuwa na REF. na Kubwa lililokukumba ni Chuki dhidi ya Znz na wa Znz jambo ambalo halikusaidii.

Lakin si kweli kuwa mimi sijadili hoja bali nakujadili wewe. Naomba kama kuna sehemu nimekuwa nakujadili wewe na si hoja zako basi paweke hadhwarani ili niwajibike kwalo ikiwa na kukuomba radhwi.

USHAURI wangu katika maandiko yako ni kuwa JIKITE KUWA SEHEMU LA SULUHISHO LA MATATIZO YA NCHI YAKO NA SIO KUWA KINARA WA KUNUNG'UNIKA na kulalamika bila kutoa suluhisho.

Mara nyingi sana
0
 
Nguruvi3,

Hoja ya 4.5% si ngeni ni ipo wazi sana na inaeleweka LABDA KWA WALE WASIOTAKA KUFATILIA MAS'ALA YA UCHUMI WENU. Mimi nakushauri waulize wataalamu wa uchumi wa Tanzania wanaounda JOINT FINANCE COOMMISSION jfc (TUME YA PAMOJA YA FEDHWA NA UCHUMI WA NCHI HIZO MBILI katika utafiti wamebainisha mchana kweupee. NAKUSAIDIA TENA PITIA AFISI ZAO ZILIZOPO SUKARI HOUSE POSTA DAR Kwa ufafanuzi na darsa zaidi au hata website yao Joint Finance Commission.

.......

Nimepitia kwa haraka machapisho mawili ya JFC yaliopo kwenye mtandao wao. >>> Joint Finance Commission - Publications

Wameonyesha vyanzo vya mapato ya Muungano kuwa ni == -a)Kodi ya Mapato kwa watu binafsi na mashirika.b) Ushuru wa Forodha.c)Ushuru wa Bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha . Wakaeleza pia kuwa chanzo kikuu cha mapato ni Kodi ya mapato (a). Kwa jedwali liloonyeshwa ni kuwa ZRB (ZRB ni TRA ya Zanzibar) ilikusanya jumla ya mapato chini ya karibu asilimia mmoja kulinganisha na yale ya Tanganyika/TRA mpaka kufika mwaka 2009/2010.

Ukisoma pia mapendekezo ya JFC kwenye chapisho la kwanza ukurasa wa 11 kuna maelezo haya,
4.0 Mapendekezo ya Stadi:
Stadi hii imetoa mapendekezo mbalimbali ya kuboresha Vyanzo vya Mapato ya Muungano vilivyopo, na kupanua wigo wa kodi kwa lengo la kuongeza Mapato ya Muungano. Mapendekezo hayo ni pamoja na yafuatayo:-i) Kuweka utaratibu utakaowesha kutenganisha mapato ya Muungano na yasiyo ya Muungano, kwa Asasi ambazo hazina utaratibu.

Ukisoma sheria iliyoanzisha ZRB ya mwaka 1996>>> Zanzibar Revenue Board - Laws & Regulations - Laws and Regulation ambayo imefanyiwa marekebisho toka ilipoanzishwa mpaka 2012, bado inasisitiza kuwa makusanyo yote yanayotokana na usimamizi wa ZRB yatakuwa kwa ajili ya matumizi ya serikali ya Zanzibar. ESTABLISHMENT, FUNCTIONS, AND POWERS OF THE BOARD(ZRB): Establishment of the Board ==There is established a Board to be known as the Zanzibar Revenue Board which shall consist of all Board departments, sections establishments concerned with collection of revenue for the Government of Zanzibar.

Ukisoma sehemu ya Madhumuni ya Stadi kwenye Chapisho la pili, JFC wanasema katiba ya Sasa ya JMT inaelelekeza kuanzishwa kwa Akaunti ya Pamoja. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 133 na 134 zimetoa maelekezo kuhusu masuala ya kugharamia Muungano na upatikanaji wa Mapato ya kuchangia Gharama hizo na matumizi yake.

Ukisoma pia mapendekezo ya JFC kwenye chapisho la pili ukurasa wa 6 utakauta maelezo haya.
5.
Yaliyojitokeza katika Stadi Katika uchambuzi huu, mambo yaliyojitokeza ni kama ifuatavyo:-
.........
(b)Kutokuanzishwa kwa Akaunti ya Fedha ya Pamoja,ambamo kungewekwa fedha inayochangwa na (SMT na SMZ) kwa ajili ya kugharamia Mambo yaMuungano; Kukosekana kwa ufafanuzi wa utekelezaji wa Mambo ya Muungano yaliyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania;
..............

======================================================================================
NILIYOYAGUDUA

1. Ni kweli kabisa na huko sahihi Mkuu Barubaru hakuna kapu la kuweka michango ya nchi washirika (Bara & Visiwani) kwa ajili ya masuala ya Muungano, maana akaunti ya pamoja haijafunguliwa/anzishwa. Lakini suala la kukosekana kwa kapu (Akaunti ya pamoja) ni kisingizio tu, kwani kama Zanzibar ingekuwa na nia ya kuchangia kwenye masuala ya gharama za Muungano ingeainisha hilo kwenye sheria yake ya kuanzisha ZRB.Sheria iliyoanzisha ZRB haielekezi kupeleka kiasi cha mapato huko kwenye serikali ya Muungano. Na hili linaweza kuimarisha uhai wa hoja ya Nguruvi3 kuwa Zanzibar ina nia ya dhati kuendelea kuinyonya Tanganyika.

2.Kwa takwimu walizotoa JFC (rejea link hapo juu), Zanzibar makusanyo yake ya kodi ya mapato ni chini ya asilimia 1 % ya yale ya Tanganyika/TRA. Hivyo Zanzibar kuendelea kupata 4.5% ya mapato ya Tanganyika( Yanayotokana na kazi ya TRA) ni 'uporaji' wa haki ya watokwa jasho wa Tanganyika/Tanzania Bara huku wakijua (Zanzibar) kabisa hawachangii chochote(ZRB ....Act, 1996 imeeleza makusanyo yake ni kwa ajiri ya Zanzibar tu).

3. Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha JFC ya mwaka 1996>>> http://www.jfc.go.tz/downloads/Joint_Finance_Act_No_14_of_1996.pdf na kufanyiwa marekebisho mwaka 2004 >>> http://www.jfc.go.tz/downloads/Act_No_19_of_2004.pdf ; majukumu ya JFC ni kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na, au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Muungano, na kutoa mapendekezo kwa Serikali mbili kuhusu mchango na mgao wa kila mojawapo ya Serikali hizo. Ili majukumu haya ya JFC yaweze kutekelezeka ni lazima Kuweka utaratibu utakaowesha kutenganisha mapato ya Muungano na yasiyo ya Muungano na pia kuanzishwa kwa Akaunti ya Pamoja.

Kukosekana kwa mambo haya mawili muhimu kwa ajili ya tume kutekeleza majukumu yake, binafsi, ninaona Tume hii (JFC) haina uhalali wa kuendelea kuwepo, hivyo inatakiwa ivunjwe; iundwe tena pale tu serikali zote mbili zitakapokuwa Tayari kufanya mambo tajwa hapo juu. Kuendelea kuwepo kwa Tume hii wakati inashidwa kutekeleza majukumu yake ni ufujaji wa pesa na mali za Watanganyika. Ni mali za watanganyika maana katika sheria iliyoanzisha JFC inaelekeza chanzo cha mapato kitakuwa ni kwa mujibu wa bunge la JMT na vyanzo vingine(haikutajwa Zanzibar). Lakini sheria hiyo inaelekeza JFC kufanya kazi Bara na Visiwani.

Na sisitiza tume hii ivunjwe mpaka hapo mambo mawili niliyotaja(red kwenye sehemu hii) yatakapotekelezwa. Vinginenvyo iletwe hoja ya kuhalalisha kuendelea kuwepo kwake bila kunyonya jasho la Watanganyika.
 
Mkuu nikushukuru tena.
Hoja hii tumeizungumza sana, na nakumbuka JokaKuu aliweka bayana kama ulivyoweka, na tumeenda kuchambua JFC ambayo si tu inawatetea Watanganyika bali pia inaonyesha unyonyaji.

Hiyo JFC inaendeshwa na fedha za Tanganyika, hilo tu mtu mwenye kutumia weledi anaweza kuliona.

Pia tukauliza,gharama za kuendesha JF ni kubwa kuliko mchango wa znz na ingekuwa bora isiwepo.

Njia rahisi ilikuwa kutenga Tanganyika na wao kama wanahitaji wajiunge na Tanganyika.
Tunasema hivyo kwasababu hakuna muungano hadi sasa. Kilichopo ni wao kuwa ndani ya mbeleko, na Tanganyika kwa jinsi ilivyo haiwahitaji. Tunasema hivyo kwasababu znz iwepo isiwepo hakuna kinachobadilika kwa Mtanganyika. Tena uwepo wake ni hasi kwasababu ni tegemezi tu na anayebeba mzigo wa znz ni Tanganyika

Ukisoma hoja za mwenzetu utacheka sana. Anasema hakuna mfuko wa pamoja wa kuchangia. Wakati huo huo anadai ni haki ya znz kupata 4.5 na pesa zizso na sababu kama kodi za watumishi wa muungano. Yaani kuweka hakuna kikapu, kuchukua kipo, sasa haelezi kikapu gani kinachoruhusu kutoa tu na si kuweka.

Kuhusu formula ya 4.5 huu ni mwaka wa 3, mwenzetu haweki wazi kwa wana jamvi hiyo formaula ni ipi na imepatikanaje. Anachosema na naomba upitie mabandiko yake, watu waende kusoma. Hiyo ndiyo mantra yake. Hapo ndipo tunasema kama hawezi kulisaidia jamvi,akae kimya.

Pili, hajatueleza hizo Bilioni 1.75 za watumishi wa muungano zimepatikana vipi. Hilo nalo atasema nenda kasome website ya sujkati house. Ni kwa msingi huo wengine tunampuuza maana hana msaada jamvini zaidi ya kumjadili Nguruvi3.
Mkuu, soma mabandiko yake uone kama kuna mahali kuna point ya aina yoyote zaidi ya matusi. Na huyu ana PhD usisahau

Mtu anayesema uchumi wa znz ni sawa na Watanganyika, utamweleza nini akuelewe?

Ameonyesha kuwa znz katika bajeti ina mikopo na misaada.
Hadi sasa hivi znz hairuhusiwi kukopa, sasa sijui hiyo mikopo na misaada imepatikana wapi.

Ukitaka kuona bajeti ya znz ilivyo kiini macho, hakuna mahali wanaonyesha jinsi gani wanalipa deni la ndani na nje kama lipo.

Huyu mwenzetu anashangilia bajeti isiyo na ulinzi na usalama waala mambo ya ndani.
I mean, hayo hasemi ukimuuuliza atakwambia nenda website ya JKU utapata detail. Phwee! Akina Najma na Najmu ni wengi
 
TUJITEGEMEE,

Hakika nimefurahi sana kupitia chambuzi na papers zilizoainishwa na wataalamu na kuzisoma na kuweza kugundua mengi sana. nakupongeza sana kwani siku zote wasomi tunazungumza baada ya kusoma na kuelewa pepers au tafiti zilizofanywa na kama kunakuwa na suala basi tunakaa kulijadili tukiongozwa na REf mbalimbali zilizopo. Hakika mnakasha wetu utakuwa mzuri kama utapenda kujifunza na kutafuta ukweli kutoka sehemu sahihi na kujadili hayo tu. NAKUPONGEZA SANA.

Nikirejea kwa yale uliyogundua sehemu ya kwanza.

Nafikiri hapa umejichanganya kidogo kwani umenikubaliana na mimi kuwa hakuna kapu la pamoja la kila nchi kuchangia katika muungano lakin unajichanganya unaposema hauoni umuhimu wa JFC (tume ya pamoja ya fedhwa na uchumi)

Hapa napenda nikusaidie mambo makuu yafuatayo.
1. Kwa mujibu wa katiba zote mbili ya JMTz na ile ya ZNZ utaona kuwa BLW halina mamlaka ya kujadili mambo ya muungano. Mambo yoye ya muungano yanajadiliwa na kupitishwa na Bunge la JMTz.

2. Sharia ya kuanzisha kwa Tume ya Pamoja na Uchumi na Fedhwa (JFC ) imepitishwa na Bunge la JMTz pale dodoma.

3. Kimantiki JFC imependekeza na kuelekeza Kuweka utaratibu utakaowesha kutenganisha mapato ya Muungano na yasiyo ya Muungano na pia kuanzishwa kwa Akaunti ya Pamoja. kwani hii itasaidia kuonyesha
a. Kila nchi inatakiwa kuchangia kiasi gani katika muungano.
b. Kuonyesha katika ripoti yake ya kila mwaka kuwa kila nchi ilichangia kiasi gani na kuondoa manung'uniko kwa nchi hizi mbili kutuhumiana.
c. Matumizi ya mapato hayo ya muungano yangetumika kwa yale yaliokubalika na nchi hizo mbili tu na kwa uthibiti sahihi kabisa wa nchi hizo mbili.

Ninaposema mapato ya nchi hizo mbili hii inajumuisha
1. Michango yao katika JFC
2. Misaada na ufadhwili
3. Mikopo.

Labda suala la kujiuliza hivi kwanini SERIKALI YA JMTz inapata kigugumizi kutekeleza sharia ya uanzishwaji wa hii JFC?

Kwanini wana wasiwasi nayo wakt hii ndio itakuwa suluhisho la manunguniko ya pande zote mbili? kwanini wakhofie kama wanavyokhofia kuanzishwa kwa serikali ya TGK?

Suala la mgawo wa 4.5% hili ni pana sana nakushauri usome kuanzishwa kwa BOT na michango ya nchi zote mbili katika uanzishwaji wake kisha tutakaa na kujadili kwa kina.

Kuhusu TRA Znz kukusanya mapato chini ya 1%. Hili linapaswa kujadiliwa kwa kina sana. Kumbuka kuwa kuna mashirika kama VODA, TIGO, CELTEL na mengine kama TCRA , Bandari kwa mizigo ya Znz etc ambayo yanafanyakazi mpaka Znz lakin malipo yao wanalipia TGK na hivyo ripoti hiyo kutoonyesha kuwa kuna kodi za waZnz hapo.

Na nilishawahi dadavua huko juu kuwa bajeti ya JMTz ya mwaka 2014/2015 inaonyesha wazi kuwa Jumla ya bajeti kuu ya mwaka 2014/2015 ni T Sh 19.2 Trillion.
Matumizi ya kawaida ni Tsh 13.6 Trillion
Pesa zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ni Tsh 5.6 Trilion.
Makusanyo yoote ya nchi kwa mwaka mzima ni Tsh 12.4 Trillion.

Kwa msingi huo utaona wazi bajeti ya JMTz ina mapungufu ya zaidi 1 Trillion katika pesa zake za kulipana mishahara na mambo mengine ya uendeshaji wa serikali.
Vile vile JMTz haiwezi kuwa na maendeleo kutokana na kukosa pesa za ndani za bajeti kwa ajili ya maendeleo.

Kiuchumi tunasema bajeti ya JMTZ ni tegemezi kwa maana inategemea zaidi ya 15% ya matumizi yake ya kawaida KUTOKA KWA WAHISANI NA MIKOPO. LAKIN VILE VILE INATEGEMEA KWA ZAIDI YA 86% PESA ZA WAHISANI NA MIKOPO KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA MAENDELEO.

Sasa huo ni uchambuzi kutoka katika Kitabu cha BAJETI YA JMTz 2014/2015.

Lakin pia ni laazima ujue kuwa Znz ni nchi yenye idadi ya watu wasiozidi 1.5 Milioni na Area isiyozidi 2000 sq Km ikiwa pamoja geographical position yake. DHIDI YA TGK YENYE WATU ZAIDI 45 mILION NA UKUBWA WA 264,888 Sq Km.

Kuna mengi ya kuangalia lakin ALL IN ALL ILI KUONDOSHA MANUNG'UNIKO YA WANANCHI WA nchi hizo mbili JFC ndio ilikuwa suluhisho la yoooote manung'uniko w\ya wananchi na wasomi wa nchi hizo mbili hususan katika mambo ya uchumi na ustawi wa nchi hizo mbili.

Labda unidadavulie khofu yako na JMTz ya kuanzishwa kwa JFC ni nini?
 
Mkuu nikushukuru tena.
Hoja hii tumeizungumza sana, na nakumbuka JokaKuu aliweka bayana kama ulivyoweka, na tumeenda kuchambua JFC ambayo si tu inawatetea Watanganyika bali pia inaonyesha unyonyaji.

Hiyo JFC inaendeshwa na fedha za Tanganyika, hilo tu mtu mwenye kutumia weledi anaweza kuliona.

Pia tukauliza,gharama za kuendesha JF ni kubwa kuliko mchango wa znz na ingekuwa bora isiwepo.

Njia rahisi ilikuwa kutenga Tanganyika na wao kama wanahitaji wajiunge na Tanganyika.
Tunasema hivyo kwasababu hakuna muungano hadi sasa. Kilichopo ni wao kuwa ndani ya mbeleko, na Tanganyika kwa jinsi ilivyo haiwahitaji. Tunasema hivyo kwasababu znz iwepo isiwepo hakuna kinachobadilika kwa Mtanganyika. Tena uwepo wake ni hasi kwasababu ni tegemezi tu na anayebeba mzigo wa znz ni Tanganyika

Ukisoma hoja za mwenzetu utacheka sana. Anasema hakuna mfuko wa pamoja wa kuchangia. Wakati huo huo anadai ni haki ya znz kupata 4.5 na pesa zizso na sababu kama kodi za watumishi wa muungano. Yaani kuweka hakuna kikapu, kuchukua kipo, sasa haelezi kikapu gani kinachoruhusu kutoa tu na si kuweka.

Kuhusu formula ya 4.5 huu ni mwaka wa 3, mwenzetu haweki wazi kwa wana jamvi hiyo formaula ni ipi na imepatikanaje. Anachosema na naomba upitie mabandiko yake, watu waende kusoma. Hiyo ndiyo mantra yake. Hapo ndipo tunasema kama hawezi kulisaidia jamvi,akae kimya.

Pili, hajatueleza hizo Bilioni 1.75 za watumishi wa muungano zimepatikana vipi. Hilo nalo atasema nenda kasome website ya sujkati house. Ni kwa msingi huo wengine tunampuuza maana hana msaada jamvini zaidi ya kumjadili Nguruvi3.
Mkuu, soma mabandiko yake uone kama kuna mahali kuna point ya aina yoyote zaidi ya matusi. Na huyu ana PhD usisahau

Mtu anayesema uchumi wa znz ni sawa na Watanganyika, utamweleza nini akuelewe?

Ameonyesha kuwa znz katika bajeti ina mikopo na misaada.
Hadi sasa hivi znz hairuhusiwi kukopa, sasa sijui hiyo mikopo na misaada imepatikana wapi.

Ukitaka kuona bajeti ya znz ilivyo kiini macho, hakuna mahali wanaonyesha jinsi gani wanalipa deni la ndani na nje kama lipo.

Huyu mwenzetu anashangilia bajeti isiyo na ulinzi na usalama waala mambo ya ndani.
I mean, hayo hasemi ukimuuuliza atakwambia nenda website ya JKU utapata detail. Phwee! Akina Najma na Najmu ni wengi

Nguruvi3,

Nafikiri kuna jambo umejifunza kutoka kwa TUJITEGEMEE kuwa ninapokwambia soma jambo fulani ni vizuri usome kisha upate uelewa isha tukijadili basi tunajadili katika same level.

Kwani kutaka mtu akutafunie na kukumezea kabisa hiyo ni khasara kubwa.

nakuomba utulie uone mnakasha utakavyokuwa unakwenda kwani MARA ZOTE NINAPOKWAMBIA SOMA JAMBO FULANI NA KUKUPA LINK NINA MAANA UJUE KISHA MIMI KAZI YANGU IWE KUKUFAFANULIE NA SIO KUKUFUNDISHA.

Kumbuka kuwa nia ya JF ni kuilimishana, kupashana habari na kuburudishana. SIO Kufundishana.

Pole sana mkuu.

Kufundishana sijui kama unajua maana yake. Unapohabarisha unaelimisha, unapasha na unaburdisha.
Vyote vipo katika kapu moja ambalo la knowledge.

Tunajadiliana si kama watu binafsi bali forum.
Hiyo JFC tumeiongelea miaka nenda rudi. Web yao ipo na source nyingine tumezitembelea.

Tunapojadili jambo, unapaswa kueleza ima kukubaliana au kukataa kwa hoja.
Narudia, JokaKuu na wengine walishaweka wazi na tulijadili sana, wala hakuna ugumu wa kupitia web

Tumeeleza kuwa 4.5% na 21% ya ajira za muungano hazina justifications kwa namna yoyote.

Tunakuuliza, ni wapi gharama za ulinzi na usalama, mambo ya ndani, deni la ndani na la nje la znz yameonyeshwa katika bajeti ya SMZ iliyo wazi kwa kila mtu?

Tumekuuliza, ni kiasi gani znz ina mchango katika muungano ikiwa Gavana wa BoT na waziri wa fedha wa znz wamesema bungeni, hakuna mchango kwa miaka zaidi ya 30.
Tuthibitishie kuwa ni waongo

Inashangaza unaposema bajeti ya znz ina mikopo na misaada, wakati hilo ni dai lao na wala halijatekelezwa. Sasa onyesha misaada na mikopo wanayopata sasa inatoka wapi, na kama ipo hoja ya znz kupata nafasi ya misaada na mikopo
inayoendelea inahusu nini. Kwa mujibu wako, kwasasa wana mikopo na misaada, sasa wanadai nini tena?

Tuonyeshe wapi kodi za TRA znz zinaingia katika mfuko wa muungano.

Kubwa zaidi, kama hakuna mfuko wa pamoja wa JFC, na hilo linawazuia zn kuchangia, iweje ;
1Useme upo utaratibu wa znz kuchangia kupitia JFC ambayo ni functionless kwa mujibu wako

2.Znz inapata bilioni 1.75 za watumishi wa muungano kutoka mfuko gani ambao wanaweza kuchukua lakini hawawezi kuweka

3.4.5% ya znz inatoka mfuko gani, ikiwa unadai Tanganyika haipo na haichangii

4.Ile hoja ya Tanganyika kuvaa koti la muungano imefia wapi?

Sitegemei majibu ya maana, nilichotaka kukuambia acha kuvuruga mada.
Unachoweza ni kujadili personality na matusi, na hapa si mahala pake. Tuna ku-ignore
 
NCHI MBILI HURU ZILIZOUNGANA !!!

Ipo hoja ya wazanzibar inayodai hizi ni nchi huru zilizoungana , mgawanyo wa uwe sawa.

Ni kweli ni nchi mbili, tatizo ni pale wanaposema mgawanyo hasa wa madaraka

Ingalikuwa vema wangesema mgawanyo wa rasilimali, mali, madaraka na madeni uwe sawa kwa nchi mbili.

Hilo halisemwi isipokuwa pale tu penye mgawanyo wa madaraka.

Madai yao ni kuwa katika taasisi inapotokea mkuu akawa wa upande mmoja, basi makamu wake awe wa upande wa pili.

Ndivyo walivyopewa nafasi ya umakamu wa Rais na bado hawajaridhika ,wanataka Rais wa znz awe makamu pia.

Madaraka ya watumishi ni suala la gharama. Kuna gharama ya kuhudumia wafanyakazi .

Lakini pia, kuna sababu za kujiuliza, ni kwanini awepo mzanzibar katika taasisi isiyomhusu na bado adai madaraka.

Kwa mfano,baraza la mitihani, Bandari, TBS, Maritime n.k. kunahusu nini kuwe na mgawanyo wa madaraka ikiwa vyombo hivyo hawavitabui?

Sumatra, mzanzibar anahusika vipi ikiwa wana mamlaka zao katika eneo zima la bandari.

Na huko wanakohusika, kuna swali la kujiuliza.

Kwavile Gavana na waziri wa fedha wa znz wamethibitisha znz kutokuwa na mchango wa aina yoyote katika muungano, hao wanaotakiwa kupewa madaraka kwa uzanzibar wao wanahudumiwa kwa gharama za nani na kwanini.

Kwa mfano, unapokuwa na katibu mkuu, waziri au mkurugenzi mzinzibar, kwanini apewe nafasi hiyo kwa gharama za Mtanganyika yeye akiweka mezani uzanzibar kama CV?

Na hili la makamu wa Rais kuwa mznz linatisha. Rais wa znz anachaguliwa na watu laki 5, iweje leo aje kutawala watu milioni 45 kwasababu tu ya uzanzibar na si taratibu nyingine.

Endapo wazazn hawamtambui waziri mkuu wa Tanzania, mtima wa kutaka kuleta Rais wa znz kutawala Tanzania ambayo ni Tanganyika in reality, wanaupata wapi?

Hoja kubwa hapa ni kuwa, huu muungano haupo kwasababu ya kuwatafutia wzn ajira, kuwapa mafao au kuwatumikia.

Ni muungano uliolenga kuleta manufaa kwa pande mbili.
Upande mmoja unapobonyea kwa kelele za upande mwingine ni uonevu.

Hii hali ya kuwapa wznz kila wanachotaka kama jamii fulani, mwishowe itajenga matabaka nchini.
Ipo siku sehemu nyingine nazo zitaomba kipaumbele kama znz. Tena zikiwa na uhalali zaidi ya znz.

Kwanini mtu wa singida anayelipa kodi zake asipewe asilimia 21 ya ajira, 4.5 na makando kando mengine kama wazanzibar.

Nini hasa swifa ya kulelewa kama wznz, ni utanzania au ni kwavile ni wznz, na inamsaidiaje mwananchi wa Ruvuma.

Ni wapi znz inawajibika kulea muungano zaidi ya kudai madarka na vyeo? Na hayo ni kwanini yawe kwa gharama za Mtanganyika?
Ni wapi usawa wa nchi mbili ulipo, ni wakati wa kuhudumia muungano au kugawana madaraka?
Na kwanini wznz hawaongelei wajibu wao ndani ya muungano, zaidi ya kudai maraka, fursa na pesa tu kila siku. Nini fikra zao juu ya muungano?

Haya ni mambo madogo madogo lakini yana athari kubwa sana kwa jamii

Ndiyo yale Palamagamba aliyosema, Watanganyika wanayo kifuani siku yakitoka itakuwa dhahma.

Upo umuhimu wa kusikiliza Watanganyika waliobeba huu muungano wana hoja gani.

Kinyume chake tunatengeneza mazingira mazuri ambayo siku moja hatutakuwa na uwezo nayo, tutabaki tunasikitika wengine wakijuta na kulia.

Tusemezane
 
Barubaru,
Kama ulivyosema hapo nyuma ni kwamba unaongea na watu wasiojua kabisa kuhusu maswala ya fedha na mifuko yake na jinsi gani fedha hizo hutumika. Ndugu yetu Nguruvi3 anachanganyikiwa na kudhani kwamba kodi yake ndiyo hutumika kwa manedeleo wakati hiyo kodi yake haitoshi hata kulipia matumizi ya kawaida ya bara.

Na mara zote kodi za wananchi zinatembea mle mle ndani kulipia vmatumizi ya idara zake na nasema hivi sii kwa kudhania kwani nilifanya kazi ya uhasibu wizara na idara za serikali kwa miaka 8. Umemuonyesha breakdown ya bajeti yetu lkn bado hakubali, sasa hiyo 4.5% kama fedha ni za misaada kutoka nje kwa JMT, yeye alitaka Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ipewe asilimia ngapi? na kwa nini anatumia neno walipewa? nani alompa nani ikiwa anaamini Znz ni ktk muungano wa JMT?.
 
Kuna hojambili unazochanganya, na mnataka kuzitumia kuwachanganya wasomaji. Hoja kamili mnakimbia kuijibu.
Twenda taratibu

Kodi haitoshi kwa maendeleo
Ni kweliyapo matumizi mabaya ya kodi
Ni kweli znz inapata pesa za kodi hiyo ikiwa ni matumizi yale yale mabaya

Pili, pesaza misaada.
Mwaka huuwadhamini wamezuia 1 Trillion

-Je znz imepata less ya 4.5%? Kama ndivyotuambiwe ni kiasi gani imepata.

Kama hakuna jibu, basi ukweli wa kwamba znzinapata 4.5% unabaki pale pale

-Zanzibar inapata 1.75 ya kodi za Tanganyika kwa wafanyakazi wa muungano. Tuonyesheni formula iliyotumika kupata kiasi hicho

-Znz ina 21% ya nafasi za ajira za muungano.Tuonyesheni formula iliyotumika kupata asilimia hizo

-Znz ina wafanyakazi katika taasisi zisizo zamuungano kwa mujibu wao wenyewe. Tuambieni ni kigezo gani kimetumika

-Gavana na waziri wa fedha wa SMZ wameliambiabunge, znz haijachangia muungano. Tuambieni ni kwanini na haki ya kupata a-dhapo juu inatoka wapi

-Hakuna mfuko wa pamoja (JFC) wa kuchangia.Tuambie znz inapata 4.5% kutoka mfuko wa pamoja, 1.75Bilioni kutoka mfuko ganiwa pamoja

-Tuonyesheni watumishi wa muungano ambao znzinapata 1.75 Bilioni , znz inachangia kiasi gani katika kuwahudumia

-Pesa za kuwasomesha vijana 1024 wa znz katikaJMT zinatoka mfuko gani na kwanini ikiwa znz inapata 4.5% tayari na ina vyombovyake ZHESL na haitambui HESLB

-Tuonyesheni bajeti ya ulinzi na usalama pamojana taasisi za muungano, zinaonekana katika jedwali gani la bajeti ya znz

-Tuonyesheni, bajeti ya znz ya mwaka huu wapi znzimeonyesha sehemu ya madeni ya ndani nay a nje.

Kwa taarifa yako, Barubaru anasema, znz inafidiabajeti yake, na wewe umemuunga mkono kwa mikopo na misaada.
Tuonyesheni bajeti ya mwaka jana na mwaka huu znzimekopa au kupata msaada gani ikiwa znz yenyewe.

Tuanzie hapo, tusichanganye wizi na fadhila. Wizi upona ufisadi upo. Hilo halitoi uhalali wa sehemu moja ya nchi kuchangia sifuri nakuchukua Zaidi ya wachanganyaji. Hoja hapa si matumizi ya kodi za Tanganyika,ni kwanini znz inapata kipaumbele ikiwa haina lolote la kuchangia kuliko mkoamasikini kabisa wa Tanganyika. Rationale ni nini.

Haya maswali hayo, tuelimishane

Tusemezane
 
Kufundishana sijui kama unajua maana yake. Unapohabarisha unaelimisha, unapasha na unaburdisha.
Vyote vipo katika kapu moja ambalo la knowledge.

Tunajadiliana si kama watu binafsi bali forum.
Hiyo JFC tumeiongelea miaka nenda rudi. Web yao ipo na source nyingine tumezitembelea.

Tunapojadili jambo, unapaswa kueleza ima kukubaliana au kukataa kwa hoja.
Narudia, JokaKuu na wengine walishaweka wazi na tulijadili sana, wala hakuna ugumu wa kupitia web

Tumeeleza kuwa 4.5% na 21% ya ajira za muungano hazina justifications kwa namna yoyote.HILI NILISHAJIBU MARA NYINGI SANA LAKIN KIFUUPI HIYO NI FORMULA ILIYOWEKWA NA WATAALAMU WALIOBOBEA WA UCHUMI WA NCHI HIZO MBILI MARA BAADA YA KUANGALIA MASUALA YOTE MUHIMU YANAYOHUSU UCHUM NA UTENDAJI WA SEKTA HUSIKA. SASA KAMA UNAWEZA KUPINGANA NA HAO TENA BASI HILO TENA NI SUALA LAKO BINAFSI NAMI SINA UWEZO WA KUKUDARSISHA KWALO

Tunakuuliza, ni wapi gharama za ulinzi na usalama, mambo ya ndani, deni la ndani na la nje la znz yameonyeshwa katika bajeti ya SMZ iliyo wazi kwa kila mtu?KWA MUJIBU WA SHARIA ZA Tz MASUALA YOOOOTE YA MUUNGANO YANAJADILIWA NA BUNGE LA MUUNGANO NA BARAZA LA WAWAKILISHI KAZI YAO KUJADILI MAMBO YOOTE YASIYO YA MUUNGANO YANAYOKHUSU ZNZ. SASA UKIPITIA BAJETI YA ZNZ HAIWEZI KUONYESHA MAMBO YA ULINZI WA NCHI NA USALAMA KWANI HAKUNA WIZARA AU WAZIRI WA ULINZI NA USALAMA AU MAMBO YA NDANI YA ZNZ. HILO NI SUALA LA KIKATIBA NA MAKUBALIANO YA MUUNGANO

Tumekuuliza, ni kiasi gani znz ina mchango katika muungano ikiwa Gavana wa BoT na waziri wa fedha wa znz wamesema bungeni, hakuna mchango kwa miaka zaidi ya 30.
Tuthibitishie kuwa ni waongo. JE INAWEZEKANA GAVANA WA BoT AKAINGIA BUNGENI NA KUZUNGUMZA? INAWEZEKANA WAZIRI WA FEDHA ZNZ AKAINGIA BUNGENI DODOMA NA KUZUNGUMZA? JE ATAONGEA BUNGENI KAMA NANI? MBUNGE AU ? HILO KWA KINYWA KIPANA NAKWAMBIA NI UONGO MKUBWA SANA.
LAKIN VILE VILE MASUALA YA UCHUMI YANAKUWA KATIKA RIPOTI MBALIMBALI ZA KITAFITI AU UKAGUZI AU BAJETI NA SIO MIDOMONI MWA WANASIASA AU VIONGOZI. HEBU TUFAFANULIE IPO KATIKA RIPOTI/ TAFITI AU BAJETI GANI MAMBO HAYO?

Inashangaza unaposema bajeti ya znz ina mikopo na misaada, wakati hilo ni dai lao na wala halijatekelezwa. Sasa onyesha misaada na mikopo wanayopata sasa inatoka wapi, na kama ipo hoja ya znz kupata nafasi ya misaada na mikopo
inayoendelea inahusu nini. Kwa mujibu wako, kwasasa wana mikopo na misaada, sasa wanadai nini tena? ZNZ INAPATA MISAADA NA MIKOPO MBALIMBALI NJE NA NDANI YA TZ KAMA INAVYOPATA JMTz. MIKOPO HII NA MISAADA HII INAPITIA KATIKA JMTz LAKIN INAPELEKWA ZNZ. KUMBUKA KUWA KAMATI YA WATAALAM WA UCHUMI WA NCHI HIZI WAMEAINISHA NI % NGAPI ZA MISAADA NA MIKOPO INATAKIWA KUPELEKWA ZNZ KAMA MSHIRIKA WA MUUNGANO. NAO WANAPATA PIA. NITAFAFANUA KIDOGO HAPO CHINI KUHUSU MAS'ALA HAYA KWAKO HAPO CHINI.
WANACHODAI ZNZ NI KUTAKA KUKOPA MOJA KWA MOJA NJE BILA KUOMBA KIBALI AU RUHSA KUTOKA MUUNGANO. WAO KAMA NCHI WANATAKA WAWE HURU KABISA KUKOPA NA KUPATA MISAADA KUTOKA NJE BILA KUBANWA NA MUUNGANO

Tuonyeshe wapi kodi za TRA znz zinaingia katika mfuko wa muungano.LABDA UNISAIDIE HAPO NI MFUKO GANI HUO WA MUUNGANO AMBAO WEWE UNATAKA ZNZ WAELEKEZE PESA ZAO ZA TRA? NAOMBA JIBU

Kubwa zaidi, kama hakuna mfuko wa pamoja wa JFC, na hilo linawazuia zn kuchangia, iweje ;
1Useme upo utaratibu wa znz kuchangia kupitia JFC ambayo ni functionless kwa mujibu wako. KUMBUKA KUWA JFC IMEANZISHWA KISHERIA KABISA ZA JMTz NA IMEPITISHWA NA BUNGE LA MUUNGANO BAADA YA MJADALA MREFU.LABDA NIKUULIZE KWANINI SERIKALI YA JMTz INAKATAA KUTEKELEZA SHARIA ILIYOTUNGWA NA BUNGE YA UANZISHWAJI WA JFC NA ACCOUNT MAALUM YA MUUNGANO?

2.Znz inapata bilioni 1.75 za watumishi wa muungano kutoka mfuko gani ambao wanaweza kuchukua lakini hawawezi kuweka

3.4.5% ya znz inatoka mfuko gani, ikiwa unadai Tanganyika haipo na haichangii. LABDA UNISAIDIE JE TANGANYIKA WANACHANGIA KATIKA MFUKO GANI WA MUUNGANO? NANI MSIMAMIZI NA MDHIBITI WA MAPATO NA MATUMIZI WA MFUKO HUO? JE ZNZ INATAKIWA ICHANGIE KIASI GANI KWA MWAKA? JE TGK ILICHANGIA KIASI GANI 2012/13 NA 2013/14?

4.Ile hoja ya Tanganyika kuvaa koti la muungano imefia wapi? IPO PALE PALE NA NDIO MAANA ZNZ WANATAKA UHURU KAMILI KAMA NCHI WA KIUCHUMI.

Sitegemei majibu ya maana, nilichotaka kukuambia acha kuvuruga mada.
Unachoweza ni kujadili personality na matusi, na hapa si mahala pake. Tuna ku-ignore

Nguruvi3,

Naona umeishupalia saaaaana hiyo hoja ya 4.5% inayokwenda kwenda Znz. Nimeshabainisha tena kwa kukupa data kamili kabisa kutoka katika Bajeti ya JMTz ya 2014/15 na hata ile ya Znz.

Nimekubainishia Bajeti za nchi zote mbili zinategemea mikopo na misaada katika kukamilisha na kutekeleza bajeti zake kwa zaidi ya 60%. wahisani au wafadhwili wakigoma basi hata MSD haiwezi sambaza dawa na wananchi wanaata taabu na kufa kwa maradhwi na magonjwa.

Nitakupa mfano kidogo hapa kigezo kinachotumiwa na wachumi katika kupanga maendeleo na bajeti mbalimbali.
TGK ina ukubwa wa Eneo 885,800 Sq Km. na ina watu zaidi ya 45 milion
Znz ina ukubwa wa eneo 2,000 Sq Km na ina watu wasiozidi 1.5 milion.

Mfano: tujadili kuhusu suala la ulinzi kidogo.
labda tuweke kigezo tunataka kuajili Polisi wa nchi hizi mbili. Tuweke kigezo kuwa polisi mmoja anatakiwa kulinda raia 300. Kwa maana hiyo utaona TGK itahitaji Askari polisi 150,000 na Znz watahitajika askari polisi 4,000 tu.

Tuendelee tunataka tujenge nyumba za polisi hawa ili waweze kukaa kambini. Na tujaalie kuwa nyumba moja ya polisi mmoja Dola za Kimarekani elfu tatu. utaona tgk watahitaji Dola za kimarekani 450,000,000. na Znz watahitaji kiasi cha 12,000,000.

Kumbuka kuwa katika Bajeti ya JMTz ya 2014/15 utekelezaji wake hakuna pasa za maendeleo zilizopo hivyo itabidi waende kwa wafhadhwili kuomba msaada au kukopa.

Huo ni mtazamo mdogo sana katika nchi sasa endeleo kwa kila kitu cha muungano kwa kuangalia stahiki za kila mfanyakazi wa muungano utaweza kujua mahitaji sahihi.

Kwa kigezo hicho na vingine tena ndio wataalamu wenu wa fedhwa na uchumi kutoka nchi hizo mbili waliamua kutengeneza formula hiyo. Hiyo inakhusu mikopo na misaada kwa mambo yote ya muungano.

NOTE.
Kufikia 30 April 2014. JMTz ilikuwa inadaiwa zaidi ya 38.5 Trilion kama deni la taifa.
Na katika fedhwa hizo about 38.6% zimetumiwa na wizara za miundombinu na wizara ya uchukuzi TGK (ambazo si wizara za muungano.

12.8% zimetumiwa na wizara ya Afya Tgk (ambayo si wizara ya Muungano )

Kumbuka kuwa deni hilo ni la TZ ambayo ni muungano wa TGK na Znz. Je Znz kulipa % hizo zilizotumiwa na wizara zisizi za muungano ni khaki?

Back
Top Bottom