gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,692
Kuna suala la msingi sana umelibainisha katika manung'uniko yako NALO NI HILI LA MFUKO WA JIMBO KWA WABUNGE WA ZNZ.
Hakika suala hili niliwahi kutanabaisha wakti tunajadili kupitishwa kwa SHARIA YA KUANZISHWA KWA MFUKO WA JIMBO hapa barzani. Nakumbuka niliwahi kuhoji kuwa fedhwa hizi zinatoka katika mfuko mkuu wa Hazina. Na CAG wa JMtz ndio atakae kuwa mdhibiti wa matumizi ya fedhwa hizi yaani yeye ndie atakae kagua pesa matumizi ya fedhwa hizi.
Nakumbuka niliuliza JE KWA WALE WABUNGE WA ZNZ WALIOPEWA FEDHWA HIZI ZA JIMBO WATAKAGULIWA NA NANI? Wakti CAG wa JMTz hana mamlaka hayo ya kufanya ukaguzi Znz? nakumbuka nilipewa jibu kuwa CAG JMTz atamkaimisha madaraka hayo kwa CAG Znz aweze kufanya kazi hiyo na kumletea ripoti.
Niliguna sana kwani kwa lugha ya kiuhasibu kupokea nyaraka bila kuzithibitisha kwa macho kwa utekelezaji wa jambo hilo ni mtihani mzito sana.
Ok all in all Bunge la JMTz lilipitisha kwa kauli moja NA SASA WABUNGE WA ZNZ WANAJINOMA.
Hakika cha mjinga uliwa na mwerevu!!!.
Laiti kama wabunge wa Tanganyika na wawakilishi kutoka TGK wangesimama kidete katika Bunge la Katiba kuitetea RASIMU ya WARIOBA kama walivyofanya wawakilishi na wabunge na wajumbe kutoka Znz basi hayo MANUNG'UNIKO yangefika ukingoni.
Binafsi nawapa pole waTgk kupoteza bakhati adhwiim.
kwanza nakuomba usijibu tena hoja yangu kwenye bandiko #320 , hapo juu.
hakika hiki ndicho nilichokuwa nakitetea toka tuanze hii mada kwamba Chenge na wenzie wametuingiza mkenge ili wapate mwanya wa kutunyonya vizuri.
nionavyo mimi huu ni mpango mwingine wa hawa wenye meno yasochoka kutafuna kuendelea kuchota fedha ilihali siye wengine tunaambiwa zimepelekwa kwenye mfuko wa jimbo.
sasa najua kwann inawezekana mambo kama sherehe kubwaaa za uhuru na muungano zinazogharimu serikali hela nyingi zinawezekana ilihali tukiambiwa kwamba serikali haina hela hata ya dawa hosp.
ofc nyingine utakuwa hata OC hazijaja kwa karibu nusu mwaka sasa, lkn mambo yasiyokuwa ya umuhimu yanafanyika unajiuliza kwan fedha zilizopatikana kwenye hili zimetoka wapi??
apa sasa ndo napata jibu kwamba kuna mwanya ulioachwa wazi ambao pia hakuna anayeweza kuuhoji ndiko zinavujishiwa hizi hela. No wonder kila mbunge wa zbr anapitishiwa bakuli kuchangia yajapo masherehe, ama safari za ambazo hazikuwa kwenye ratiba.
sitashangaa siku kusikia kwamba hata fedha hizo za mfuko wa jimbo wabunge hao wa zbr hawazitumii manake zinawekwa kama amana tu ambapo siku mwenyewe anapoitaka basi huenda kuichukua. sitashangaa hata kidogo