WALIYOSEMA WASEMAJI WA MKUTANO-KIBANDA MAITI
https://www.youtube.com/watch?v=FlECaPDYzVQ
Katika video, wasemaji wa CCM walipangwa kupitia vifungu vya katiba ya Chenge/CCM
Kilichoonekana ni kuzungumzia masilahi ya Zanzibar.
Pale yanapotajwa ya Tanganyika, Tanganyika haisemwi bali Jamhuri ya muungano.
Hilo linaeleza ile hoja ya Tanganyika kuvaa koti la muungano bado ni tatizo.
Rais Shein aliwahi kusema'' Kwa mkataba wa 1964 hakuna mamlaka kamili''
Pengine amesahau kwa namna yoyote Tanganyika ni kubwa kwa znz kwa kila hali, hivyo kulivaa koti la muungano kupo tu midhali hakuna serikali ya Tanganyika.
Jamhuri ya muungano kwa katiba ya 1977 na pendekezwa ya CCM/Chenge Tanganyika haipo.
Kwa maana kuwa Jamhuri ndiyo Tanganyika, na hilo ni koti ambalo znz itabidi walikubali bila hiari.
Katika video hiyo saa 1.22 waziri wa fedha wa muungano amethibitisha,hakuna mapato ya znz yanayokuja muungano.
Huyu ni waziri wa fedha wa JMT ambaye pia ni mbunge kutoka znz na ni mzanzibar.
Ile hoja ya znz kunyonywa na Tanganyika kimapato inajieleza vema.
Lakini hoja ya Saada Mkuya itasaidia sana kuelewa hoja za wachangiaji wengine kadri tunavyosonga mbele.
Waziri Saada anasema, kwa mujibu wa katiba ya Chenge, znz ni huru kupata mikopo na misaada kutoka nje.
Katika muda wa saa 1.26 Makamu wa kwanza wa Rais, Seif Idd Ali anasema ''Katiba ya Chenge imeweka ndani ya katiba sharti la JMT kuidhamini znz katika mikopo''
Hapa ndipo Watanganyika wanatakiwa waone hatari inayokuja machoni mwao.
Kwa mujibu wa wznz, kukopa na misaada kutoka nje ni ruksa. Hiyo ni haki yao.
Lakini pia kwa mujibu wa wznz, kila wanapokopa basi JMT itawadhamini.
Kwa maneno mengine, mikopo na misaada ya znz italipwa na Watanganyika wasiofaidika hata senti moja.
Kibaya zaidi, SMZ inaweza kwenda kukopa maandazi na pili pili manga, na kisha kugoma kulipa.
Atakayelipa ni Mdhamini Tanganyika. Ndivyo walivyokopa michele kule Kenya na sasa ubalozi wa JMT upo katika wakati mgumu kulipa mchele uliokopwa na SMZ kwa ajili ya wazanzibar lakini bili analipa Mnyakyusa, Mpogoro, Mbondei na Mhaya.
Endapo znz wanataka kukopa na misaada kwanini wadhaminiwe na Watanganyika?
Kwanini Mtanganyika abebe mzigo wa znz usiomhusu kwa namna yoyote.
Ndipo naibu katibu mkuu CCM znz aliposema '' SMZ inadhamini wanafunzi 824 katika mwaka 2012/12, na JMT imedhamini wznz 1040'', sikiliza katika dakika ya 53 ya mkutano (video)
Kwa maana kuwa, znz isiyochangia pato katika JMT kwa mujibu wa waziri wa fedha Saada Mkuya, imepewa wanafunzi wengi kuliko SMZ inayochukua mapato yake kutoka kwa wznz.
Hapa ni kuwa wanafunzi wa walipa kodi wa Tanganyika wameachw mitaani wakihangaika, ili hali kodi za baba zao zinakwenda kudhamini wanafunzi wa znz waiochangia lolote katika JMT kwa mujibu wa saada Mkuya, na gavana wa benki kuu ya Tanganyika
Kodi za Watanganyika ndizo zimedhamini wanafunzi wengi kuliko kodi za wznz zinazobaki znz kwa mujibu wa Saada Mkuya
Tena bila aibu Vuai anasema, wazanzibar sasa ubwedo maana wana bodi mbili, ya ZHESLB na JMT ambayo ni HESLB.
Hapa wznz wana haki kwasababu wao ni Tanzanznia na wznz, wewe Mtanganyika ni Mtanganyika tu, huna haki ya kupata huo mkopo wa ZHESB pengine ni kwa kuosa ustaarabu kama alivyosema katibu wa baraza la mapinduzi mzee Maulid
Makamu wa Rais Seif Idd anasema kwa mujibu wa Chenge, znz imepewa haki ya kukopa.
Hapa anajaribu kueleza kuwa znz ikikopa kwa udhamini wa kodi za Mtanganyika, pesa hizo zitatumika katika mambo kama elimu ambayo Mtanganyika hahusiki kwasababu ni Mtanganyika.
Tanzania ikikopa, mkopo huo itabidi uende znz kwasababu znz ni sehemu ya JMT na hivyo ina haki.
Waziri wa Muungano Samia Suluhu anasema, kodi za wafanyakazi wa muungano sasa hivi zinakwenda znz
Kaungwa mkono na waziri Saada Mkuya aliyesema sh 1.2B kila mwezi zinakwenda SMZ kama kodi ya wafanyakazi wa muungano.
Watanganyika, hii maana yake ni kuwa ninyi mnalipa gharama za kuendesha muungano ikiwa ni pamoja na misharaha ya wafanyakazi wa muungano.
Halafu mnawazadia wznz Bilioni 1.2 kila mwezi kwa ajili ya kupunguza tatizo la ajira znz.
Wafanyakazi wa SMZ ni chini ya 10,000. Wznz wanaofanya kazi katika muungano ni 20,000.
Katika akili nzuri, wznz walitakiwa si kuchangia muungano bali pia kulipa kwa kuondoa tatizo la ajira znz.
Kinyume chake, ninyi walipa kodi wa Tanganyika, mnaendesha muungano wenyewe, mnalipa wznz mishahara na kisha mnawalipa zaidi kwa ajili ya kuwasaidia. Hapa ndipo wabunge wa CCM kutoka Tanganyika walipowafikisha.
Waziri Samia anasema formula ya kugawana idadi ya wafanyakazi kama BoT na TPDC imepatikana.
Kumbukeni wznz wameondoa mafuta na gesi hivyo TPDC haiwahusu. Swali, wafanyakazi wa znz ndani ya TPDC inawahusu nini?
Ukitazama maelezo yote, ni wznz wznz wanashangilia kupata tu.
Hakuna yoyote kuanzia Rais wa znz Shein, Makamu wa Rais Idd au mawaziri aliyesimama na kusema muungano unachangiwa vipi na wazanzibar. Hakuna aliyethUbutu kusema hilo.
Si kwamba hawajui, bali ni ile roho ya umimi na dharau kuwa wznz ni bora na wanapaswa kupewa na si kutafuta.
Lakini pia wameongelea sana mafuta na gesi, ajira mikopo na misaada.
Hakuna hata mmoja, si Rais wa znz, makamu au waziri aliyezungumzia usalama na ulinzi wa nje na ndani.
Mbona hatuwasikii wakiongelea wizara ya ulinzi, au mambo ya ndani?
Si kwamba hawajui, wanajua, lakini ni dharau tu kuwa hilo ni zigo la Mtanganyika na anapaswa kulibeba.
Hiyo ndiyo taswira nzima ya wenzetu ambao, kwao katiba ya Chenge inawafaa na Wtaanganyika ni wa siku hizi si wastaarabu pengine akisitiri kinyume cha kauli hiyo
Ni kwa mtazamo huo, na kwa kujua Watanganyika hawahoji, katibu mkuu wa kwanza wa baraza la mapinduzi, amenena katika video ya 1/5 kuwa 'Watanganyika wa siku hizi si wastaarabu''
Kwa lugha za pwani, kama mtu si mstaarabu huyo ni mshenzi.
Watanganyika mnapoona mambo kama hayo na kukaa kimya, kwanini akina Mzee Maulidi wasiwaite Washenzi!
Tusemezane