KUNDI LA VIONGOZI WA DINI
Sehemu ya I
Hapo bandiko 21 tueongelea makundi 3 yatakayopewa kazi yapromotion ya rasimu ya CCM.
Waandishi wa habari, kutisha viongozi na viongoziwa dini.
King Suleiman kaeleza vizuri sana. Uwepo wa viongozi wa diniulikuwa na sababu kuu zifuatazo;
Kuhakikisha KUNDI LA VIONGOZI WA DINI
Sehemu ya I
Hapo bandiko 21 tueongelea makundi 3 yatakayopewa kazi yapromotion ya rasimu ya CCM.
Waandishi wa habari, kutisha viongozi na viongoziwa dini.
King Suleiman kaeleza vizuri sana. Uwepo wa viongozi wa diniulikuwa na sababu kuu zifuatazo; (1)Kuhakikisha kuwa wao kama sehemu ya taasisina jamii yenye wafuasi wengine inashiriki katika mchakato
(2)Kuhakikisha masilahi ya waumini katika yanalindwa ili katibaisiingilie au kuacha wazi uhuru wa kuabudu
(3) Kuwa wapatinishi kati yawabunge wenyewe au bunge na wananchi
(4) Kuwasikio la wananchi katika kuona haki inatendeka kwa dhamana ya kiroho waliyonayo
Viongozi wa dini wamekuwa wahanga wa wanasiasa. Kilawanapomaliza kutumika, wanasiasa huwasimanga hata kuwatia matatani. Juzi turais alisikika akikemea kuchanganya siasa na dini na dini na siasa.
Huwezi kutenganisha siasa na dini. Chimbuko la siasa niuwepo wa dini na maadili ya kiroho hayatengi jambo la siasa au nje ya siasa.
Hivyo kuwaambia wasichanganye dini na siasa kuna maana pale tu siasaitakapoachwa kuchanganywa na dini.
Inashangaza Rais aliyesema wasichanganye dini na siasa,hakukemea viongozi wa siasa kama waziri wake Lukuvi aliyepeleka siasa ya katibakanisani.
Kwa maneno mengine Rais anaruhusu siasa kuchanganywa na dini na sikinyume chake.
Inashangaza wakati wa maadhimisho ya kidini, viongozi wa kisiasa tunawaona wakihudhuria, iwe Krismas au baraza la Idd. Wakitoka hapo wanakemea kuchanganya dini na siasa.
Yanapotokea matatizo yaliyosababishwa na wanasiasa,utawasikia viongozi wa siasa wakiwaomba viongozi wa dini waombee taifa.
Inakuwaje wanasiasa wanaruhusiwa kushiriki shughuli za dini wakiwa na majoho yao ya kisiasa lakini ni marufuku viongozi wa dini kushiriki siasa?
Viongozi wa dini nao wanasehemu yao ya kulaumiwa. Hivi wanasiasa wanaingiaje katika shughuli za maadhinmisho yanayohusu Imani. Kwanini wanawakaribisha.
Hata wziri Lukuvi naye alikaribishwa kuongea kanisani.
Kwaniniviongozi wa dini wasialike viongozi wenzao kama wanataka mbadala katikashughuli zao?
Kwanini, kwa mfano tu, mwadhama Pengo asimwalike kadinalimwingine kutoka nje katika sherehe za Wakristo?
Kwanini shehe mkuu asimwalike mufti wa taifa jingine katika shughuli za waislam?
Maana hao wageni wana lakusema kuhusu Imani, ukimwalika Sitta atakwambia namna wananvyojipanga kwa kura za facebook, Tango na Whatsup na ataomba umuombee mipango yake inyoke.
Kiongozi wa dini utakataa vipi ili hali umwemwalika katika nyumba yako na unajua hajui wala hana mamlaka ya kiroho (moral authority) kuzinyoosha roho zawaumini akiwayeye I muovu namba moja?
Unamkaribisha tumbili shambani utegemee nini kama si kuvuna mabua?
Hebu turudi katika mchakato tuone ushiriki wao
Inaendelea…. (1)Kuhakikisha kuwa wao kama sehemu ya taasisina jamii yenye wafuasi wengine inashiriki katika mchakato

Inaendelea….
VIONGOZI WA DINI NA MISIMAMO YAO YENYE UTATA
JAMII INAWAANGALIA KWA JICHO LA HADHARI NA MASHAKA
WANATUMIKA, HAWAJIELEWI.
Bandiko hapo juu tumejaribu kuonyesha ni kwanini viongozi wa dini walihitajika katika mchakato.
1.Kuhakikisha wanakuwa sehemu ya mchakato.Hakika wamekuwemo ndani ya bunge la katiba kama ilivyotarajiwa
2.Wanalinda masilahi ya waumi wao. Hilo limejitokeza dhahiri3.Wapatanishi, hilo limetokea wakiwa wamegemea upande bila kuangalia haki
4.Kuwa sikio la wananchi. Hapa wame feli kiasi cha kusikitisha
Kwanini wamefeli katika hoja namba 3 na 4
Kwanza, walichotakiwa ni kuzungumza na pande mbili, CCM na UKAWA kwa kuangalia haki sio za wingi bali haki za kila mmoja.
Tofauti ya idadi haitoi au kupunguza haki kwa kundi husika.
Viongozi hao walitafuta suluhu wakielewa kuwa haki haitatendeka.
Kimaadili walipaswa kujua hili mapema sana.
Pili, hoja ya sikio la wananchi, hapa ndipo rangi zao halisi zilipoonekana.
Walijitokeza na kuandika tamko likizungumzia uhalali wa BMK, akidi n.k.
Mambo yote hayo walifahamu yalikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki na makubaliano.
Wakajipambanua kuwa wasemaji wa Bunge kwa maagizo.
Wakaacha msingi mkubwa wa kiimani wa kusimamia haki,badala yake wakazingatia allowance zao pengine na ziada.
Viongozi wa dini wakashuhudia uchakachuaji wa bunge la CCM kwa kukaa kimya pale facebook, TanGo, yahoo zilipotumika. Walifahamu kanuni zinabadilishwa ili kukidhi haja na si matakwa ya wananchi.
Viongozi wa dini hawakuthubutu kunyanyua midomo yao kukemea uovu uliokuwa unatendeka machoni mwao mchana kweupe. Suala zima likiwa masilahi yao na si ya taifa.
Hapa walipopoteza kile kiungo baina yao na wananchi, wameshindwa kiimani, wameshindwa kimaadili na hata kibinadamu.
SITTA AWAGEUZIA KIBAO, AWANANGA KISAWA SAWA
Mwenyekiti wa BMK-CCM aliwageuzia kibao baada ya matamko kutoka taasisi nje ya bunge.
Ilikuwa dhahiri taasisi wanazowakilisha ziliona tatizo miongoni mwa wawakilishi wao.
Zikatoa matamko ya kutoridhika na mwenendo, matamko yaliyotibua nyongo ya Sitta.
Sitta akawasema,matamako yao ni ya kipuuzi na wananchi wapuuzie.
Hili alilisema kwa kutoa mfano wa makanisani akiogopa kugusa imani nyingine ili masuala nyeti yasijeizuia uchakachuaji
Kimsingi aliwasema viongozi wote wa dini na imani zao baada ya kuwatumia.
Viongozi wakageuka kuwa karatasi za maliwato baada ya kutumika kupamba bunge la CCM.
Jambo la kushangaza, Sitta aliwahi kusimama katika mikutano akimtetea mwenzake aliyetoka India kutibiwa kwa kutumia majukwaa ya dini.Ghafla akawageuka na kuwaita wapuuzi. Hivi ndivyo wanavyotumika.
Baada ya kubaini hilo, Rais akakutana nao katika chakula cha jioni ikiwa ni jitihada za kuzima makali ya maneno ya Sitta. Nao kama kawaida wakahudhuria na kusikia walichotaka kusikia na si kile wanahokisimamia
Siku iliyofuata tukawaona wakiombea mchakato umalizike kwa amani. Ni wakati mh Rais anapokeaa rasimu ya CCM.
Jambo la kujiuliza, hivi wao wamejiridhisha vipi kuwa mchakato mzima ulizingatia uhalali wa makubaliano na sheria husika?
Hivi hawa viongozi hawakuona maajabu ya kura zilivyopatikana, kanuni zilivyopindwa kila uchao, sheria ikikiukwa kwa wingi n.k!
Viongozi hao hawakuthubutu kukemea uovu, wakabeba vitabu vitakatifu kuombea amani mchakato umalizike salama.
Mchakato uliogubikwa na uovu eti umalizike salama.
Kwamba, mwisho wa uovu ni maombezi ya salama hata kama wanajua haki ni tunu ya mwanadamu aliyopewa na mola wake. Wakasimama upande wa wanadamu wakimwacha mungu
Kwamba, uovu uliotendeka wakaupa uhalali wa dua. Hili limetokea si kwa bahati mbaya ni kutokana na ‘manunuzi' ya ghali.
Ni kwa hali hiyo, kwasasa hakuna mwenye imani na viongozi hao.
Wakati wanaambiwa wasichanganye dini na siasa, wao wametumika kuchanganya siasa na dini na mwisho wa siku wakitupwa chini''under the bus'' na wale wale wanaowatumia.
Kwasasa wananchi wamekosa sikio la haki, wamepoteza imani na viongozi wao na wengine wanahoji kama misingi ya imani imetumika kulileta taifa pamoja.
Haitatokea viongozi hao kuaminika tena katika mizani ya kisiasa.
Wamepoteza uhalali wa kimaadili kwa kile walichoagizwa kusimamia kutokana na mienendo ya dini.
Wapo wanaowaangalia kwa kutumia ‘aya za wanafiki'' wapo wanaowaangalia kama ''Yuda Iscariote''
Haya yote wameyatengeneza wao kwa kuacha msingi mkubwa wa imani wa dini zote ambao ni ukweli na haki.
Ni kwa mtazamo huo, tunazidi kuona tatizo katika kundi hili tofauti na makundi mengine tuliyoyadili.
Bei ya kundi la wasomi inaweza kukokotolewa, bei ya wana habari inaweza kupigiwa hesabu, bei ya viongozi wa dini haijulikani ingawa wapo sokoni.
Na hilo ndilo linatulazimu tuseme, kundi la viongozi wa dini ni kwa mfano wa ‘wanayama waishio mwituni, kila mmoja hula kwa nguvu zake''
Swali, je, ushiriki wao una maana yoyote katika hali tuliyoishuhudia?
Tusemezane