Nguruvi3,
Hakika Huko Ndio tuendako.
Nikianza na hoja yako juu ya moto unaozidi kuchochea ndani ya CCM, kwa kweli ni Vigumu kuelewa nini itakuwa ni hatima ya cheche hizo ndani ya chama. Kwa mfano Mdogo tu, Kabla ya kufunga kikao cha bunge usiku wa jumatatu iliyopita, Samuel Sitta aliwaeleza wajumbe Kwamba kila mmoja wao atapewa Cheti kilichosainiwa na rais Kikwete kuonyesha Kwamba mjumbe huyo amefanya "kazi muhimu na ya kihistoria ya kutunga katiba".
Ni Vigumu kuelewa iwapo mpango huo ulikuwepo tangia awali/Kabla ya mchakato kuingia nyongo, au ni mpango mpya ulioletwa na Sitta kwa ajili ya kuwalaghai wajumbe Kwamba watatambuliwa na rais. Wengi tunajiuliza, kwanini then rais Kikwete alifikia makubaliano na ukawa hivi karibuni Kwamba kwa muda na mazingira yaliyopo, katiba mpya haiwezi kupatikana; Kauli ya Sitta kuja baada ya kauli ya rais Kikwete iliyokiri Kwamba katiba Mpya haiwezekani Kabla ya uchaguzi 2015 maana yake ni nini? Je Ina maana Sitta Ana mamlaka makubwa zaidi ya Mwenyekiti wake na rais wa nchi juu ya suala Zima la katiba mpya?
Tayari watanganyika wengi wameanza kuona athari za mwenendo wa Sitta kwa Tanganyika, Zanzibar na muungano kwa ujumla, lakini sijui Kama wajumbe wa BLK wanaelewa nini kinafuatia kutokana na mwenendo wa Sitta na katiba mpya. Kwa mfano - Sitta ameingiza masuala ya ardhi, maji, viwanda, uvuvi, serikali za Mitaa, uwekezaji, na takukuru Kama masuala ya muungano. Tuangalie baadhi ya mambo haya kwa undani:
Tukianza na Ardhi - Kuchukua mambo ya Tanganyika Kama vile ardhi na kuyaingiza Katika katiba ya muungano, hii ni Kinyume na rasimu ya tume. Pia kufanya hivyo ni kurekebisha katiba iliyopo, huku sio kutunga katiba mpya. Kazi hii haipaswi kufanywa na BLK Bali bunge la JMT. Kwa mfano, katiba ya JMT (1977) inataja suala la umilikaji wa ardhi Katika ibara ya 24. Kila Raia wa JMT anayo Haki ya kumiliki Mali na ulinzi wa Mali yake, ingawaje Haki hii Ipo upande mmoja tu wa muungano.
Sheria ya ardhi ya mwaka 1999 Katika sura yake ya 113, kifungu cha 3(a) kinatoa Dira na Sheria kuhusu kanuni muhimu ya sera ya taifa ya ardhi. Kanuni hii imemkabidhi rais wa JMT usimamizi wa ardhi kwa niaba ya wananchi wa JMT. Pia Sheria ya ardhi ya kijiji sura namba 414 na Sheria ya kusajili ardhi Sura ya 334, hizi Ndio uongoza usimamizi wa matumizi ya ardhi kwa Mujibu wa Sheria na sera ya ardhi. Tatizo ni hili:
Pamoja na Kwamba Sheria hii Inahusu jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni suala lililo wazi Kwamba Sheria hii haitumiki Zanzibar. Anachofanya Sitta kwa wazanzibari ni kuwaletea kitu kipya yani kuagiza Zanzibar kuruhusu ardhi Yao kutumiwa na Raia wa Tanganyika, suala ambalo wamelikataa Katika kipindi chote cha muungano, na kuliweka sasa itakuwa ni moja ya njiti za kibiriti zitazowasha moto na machafuko.
Masuala mengine Kama vile serikali za Mitaa, takukuru, vyama vya Ushirika, uwekezaji, viwanda, vijijini vya ujamaa, vitongoji, uvuvi, pembejeo, Kilimo etc, haya yote ni masuala yanayohusu Tanganyika moja kwa moja serikali ya Tanganyika. Ndio maana tume ya katiba ikayaweka haya Kando, nje ya muungano. Kama tunakumbuka vyema, haya ni sehemu ya malalamiko mengi ya wananchi Wakati wa ziara za tume ya katiba, ambapo wapo wananchi waliolalamika Kwamba haya mambo yanahusu Tanzania bara pekee (Tanganyika) lakini yanaendeshwa kwa kodi za wananchi wote wa Tanzania.
Tukichukulia mfano wa uwekezaji, kwanini TIC iwe ni ya muungano, huku taasisi hii kwa upande wa Zanzibar ibakie nje ya muungano? Wazanzibari ni mabingwa wa kusamehe kodi, kwa vile mjomba Tanganyika yupo kutoa fedha. Kitendo cha TIC kuwa Chombo cha muungano kitakuwa Kama uwepo wa TRA na ZRA Zanzibar, mzigo kwa Tanganyika.
Tukija kwenye suala la viwanda, sekta hii Ndio inayobeba matumaini ya Ajira kwa vijana wetu. Kufanya viwanda kuwa sehemu ya muungano, Wakati viwanda karibia vyote vitakuwa bara ni kujenga mazingira Kama yake ya 21% ya Ajira kwa wazanzibari; wazanzibari watadai vijana wao waajiriwe kwa quota Fulani Katika viwanda ambavyo haviwahusu, huku mtanganyika akiumia. Na kwa viwanda ambavyo vitashamiri znZ iwapo itatokea hivyo, watanganyika hawatopewa fursa kule.
Tukichukulia mfano TAKUKURU, Sitta na Kundi lake wanaigeuza kuwa ni ya muungano Wakati Chombo Hiki hakiruhusiwi kufanya kazi nchi Jirani ya Zanzibar. Nchi hii Jirani haitambui takukuru ni kiumbe gani, na Wala haimo Katika Orodha ya mambo ya muungano kwa Mujibu wa mkataba wa muungano (1964). Unga'ng'anizi huu wa Sitta na wenzake ni kuua muungano, sio kuboresha muungano.
Zanzibar wana Chombo kinachofanana na takukuru, kinaitwa - kamishen ya rushwa na uhujumu uchumi. Kitendo cha Sitta kuifanya takukuru kuwa ni suala la muungano ni kuzidi kuiminya Zanzibar, lakini pia kuongeza matumizi ya fedha za walipa kodi wa Tanganyika kwa nchi Jirani bila ya faida kwani gharama za kuendesha Chombo Hiki chini ya serikali Mbili, wazanzibari watasema Hilo ni la muungano (Tanganyika).
Nchi Mbili zinapoungana, hubadilika huwa nchi moja yenye mamlaka moja ya Kidola. Tofauti na hili, kupitia katiba yake ya 2010, chini ya uongozi wa Sitta na wenzake, Zanzibar imekuwa ni nchi huru. Ina bendera yake, Wimbo wake wa taifa, Ina serikali yake kamili inayoambatana na political autonomy, na Ina fiscal and policy autonomy.
Katiba yake inatambua Kwamba Zanzibar ni nchi, na Sitta na wenzake wanatambua Kwamba nchi hii Ipo ndani ya nchi nyingine ya Tanzania, lakini wanadhania Kwamba hatari hii watanganyika watapuuzia na suala hili litapita tu Kama upepo. Katiba ya Zanzibar imeruhusu nchi hii ya Jirani kuanzisha majeshi yake, ambayo yapo chini ya amiri jeshi mkuu wa nchi hiyo Jirani. Tuna uhakika gani Kwamba hatutaanza kutuniana misuli Kama Korea kusini na kaskazini kwa masuala ya rasilimali? Kitendo cha kuruhusu znZ kuwa ni nchi kamili, nchi hii itakuwa na Haki ya kutetea Kile inachoamini ni chake na hata Jumuiya ya kimataifa itaelewa hivyo.
Kitendo cha wajumbe wa BLK pale Dodoma kushabikia juhudi za Sitta kuzima serikali Tatu kitasababisha muungano kuingia Katika machafuko makubwa sana ndani ya kipindi kifupi. Kutaibua migogoro mipya ndani ya muungano, hasa baada ya watanganyika Kuamka na kujua nini kinaendelea. Hali hiyo itavunja muungano. The question that follows ni je, Nani atakuwa loser zaidi Kati ya Tanganyika na Zanzibar? Jibu ni dhahiri - ZANZIBAR.
Sent from my iPhone using JamiiForums