nasema kulumbana na wewe ni sawa na kumfukuza kichaa nikiwa uchi kwa sababu hata ukioa leo lengo la ndoa ni upendo na kuwa na familia yako ikitokea maswala ya mkeo kudai fedha au mali haina maana ndoa yenu ilitokana na malengo ya kifedha na mali. Unashindwa vipi kuelewa kwamba haya ya siasa na uchumi yamekuja baada ya muungano. Hata Mchambuzi kasema muungano wetu ulikuwa wa kisiasa na sio kiuchumi wewe umekazania tu uchumi. Mimi nimewakosoa nyote na kuwambai muungano wetu ulikuwa wa WATU yaani jamii yetu kuwa moja, haya madai mengine yapo na yataendelea kuwepo na ndio maana Wazanzibar hawaelewi wanapoambiwa Zanzibar sio nchi ni kutokana na fikra za kisiasa na kiuchumi baada yaa.Mkuu kinachoongelewa hapa ni hoja. Tumekujibu hoja zako na pengine ungettuelewesha kama hatuelewi.
Hatuwezi kukaa kimya hata pale tunapoona unapotosha. Unaposema mfano wa Canada na Tanzania ni sawa, tutasema hapana! Unaposema issue siyo uchumi, wakati madai ya wznz ni kuhusu kuonewa kiuchumi nawe ukiwasadidia katika mikopo na misaada, tuakwambia no, uchumi ndilo tatizo.
Ukitaka tuamini kuwa znz inaonewa, tutakuonyesha haionewei.
Ukisema S2 ni nafuu kuliko 3, tutakuuliza, tuonyeshe unafuu ulipo.
Nashangaa kukuuliza utuonyeshe unafuu wa S2 unakuwa mbogo. Ni hoja mkuu, matusi na kashfa hazina nafasi.
Unataka kubabaisha umma kuwa unaishi Canada, wakati mfumo wenyewe huelewi. Hakuna wabunge wa majimbo wanaoingia federal gov na hakuna wa fed wanoingia majimboni. Tanzania si Canada, mfumo upo tofauti na hakuna mwingine kama huu duniani.
Ulipokuja na hoja ya bima ya afya, tuliweka sawa hata pale usipopajua ingawa unatumia bima hiyo.Tunausaidia umma dhidi ya wapotoshaji na wababaishaji.
Tunakwenda kwa hoja. 'If you can't take the heat get out of the kitchen'
Sasa wewe unakuja namaswala ya Ethiopia na Eretria ambao waliungana lakini Ukabila ukawatenganisha, sijui Syria na Egypt sielewi unazihusishaje. Somalia na Ogaden wakati Ogaden ipo Ethiopia ilhali wakazi wake ni Wasomali bado huelewi kwamba muungano wa WATU huondosha ukabila na unaposhindwa kuondoa hilo lolote linaweza tokea. Maswala ya kiuchumi yapo EU kweli na unaweza kusoma mkataba (TREATY) Waloandaa toka mwaka 1958 kuundwa kwa jumuhiya hiyo na wakaja unda mwaka 1992. EU was Originally signed in Rome as the Treaty establishing the European Economic Community.Na ukija soma Artical of Union yetu hakuna mahala popote siasa wala Uchumi umehusishwa hata ktk functions zake (mambo 11) siasa na uchumi havikuwemo lakini wewe bado unalazimisha vilikuwemo, kuna haja gani mimi kuendelea kumfukuza kichaa!