Duru: UKAWA njia panda, CCM maji ya shingo

Duru: UKAWA njia panda, CCM maji ya shingo

Mkuu Mag3
Takribani mwezi mmoja, Jaji Warioba alisimama na kusema zoezi halitawezekana.

Alitoa sababu za kisheria, kwamba muda wa elimu ya umma na kampeni havitafuata sheria.
Hilo ni baada ya kulazimishwa kura ya maoni


Jaji Lubuva alipaswa kumsikiliza Jaji mwenzake. Hapana! Akaamua kufuata maagizo tu hata pale ukweli ulipodhihiri.

Akaacha kutumia hekma za taaluma yake, au hesabu za kawaida na kubaki kusema ‘ndiyo mzee'


Makundi ya wazee kama akina Bomani yalimuonya kwa njia mbalimbali yakisema mchakato ulishavurugwa.
Jaji Lubuva hakuwasikiliza


Mwezi uliopita, ilikuwa wazi hakuna kura ya maoni kwaababu zaidi ya 100.

Jaji alisimama mbele ya kusema ‘zoezi linakwenda vema, tumemaliza Njombe kwa mafanikio,tumejifunza.
Tunategemea vifaa Zaidi na ikifika April 30 zoezi litakamilika'

Jaji Lubuva hakufikiria mfumo huo mpya unahitaji uhakiki, alifikiri kumfurahisha ‘mfalme'

Ni jaji Lubuva aliyepanda ndege kwenda Kenyana Nigeria kuazima BVR.

Masikini Jaji hakujua BVR ni kitu na mfumo endelevu, kwamba unahitajika kila siku.

Jaji hakuweza kupata habari kuwa Nigeria walikuwa na uchaguzi na walihitaji BVR


Hilo tu linaonyesha Jaji Lubuva alivyo out of touch na duniaya leo.

Wenzake wakamchagiza kisiasa,mambo ni mazuri. Kila wakati mtoa taarifa alikuwa Rais, Jaji akipokea maagizo

Kimenuka wenzake wamemkimbia, wanamwachia zigo atangaze jinsi alivyofeli, na kweli akatangaza

Na si kufeli tu bali jinsi asivyojua kazi wala anachokifanya.

Haiwezekani wiki mbili tatu zilizopita asema ‘kwa mafanikio, kisha anakuja kusema tumefeli'
Hakuna aibu kubwa kama hiyo.

Jaji anapaswa kuangalia jinsi alivyoburuzwa, heshima ilivyopotea na kama anasababu za kuendelea kulitumikia taifa tena


Haiwezekani mtu aliyeonyesha udhaifu, ubutu na uwezo kama wa Jaji kuendelea kusimamia tume ya uchaguzi.

Hivi hata matokeo ya kuchagua kiranja mkuu wa sekondari, Jaji anaweza kutangaza watu wakamwamini tena!!
Seuse Uchaguzi mkuu Oktoba


Rai yetu kwa Jaji , wenzake wamemtosa na amebeba mzigo asiostahili . Jaji ameshindwa na taifa limefeli mikononi mwake.

Hana sababu za kuendelea na uenyekiti wa tume ya uchaguzi.

Tayari ni felia hatuwezi kusubiri felia nyingine inayoweza kulitumbukiza taifa katika hali ya hatari

Jaji Lubuva ni wakati sasa ‘pack and go' Unless una dhiki nyingine, hatuamini kama unasababu za kuendelea na kazi

Aibu na fedheha iliyokukumba inatosha, ni muda sasa ulinde heshima ya wajukuu wako watakaotumia jina lako.

Hutawatendea haki wajukuu, ikiwa jina lako litaendelea kunasibishwa na uchafu, dhalili na fedheha inayokukabili sasa.

Jaji ondoka, umelitia taifa aibu ya BVR na sasa aibu nyingine! Tulindie heshima ya taifa letu. Umefeli kikamlifu



 
MAAZIMIO YA KMATI KUU YA CHADEMA

MAPUNGUFU YA TAMKO LAO NA HATARI INAYOWAKABILI

sehemu ya I

Jana kamati kuu ya Chadema imetoa tamko baada ya kkao chao. Pamoja na mambo mengine, kamati kuu imeongelea suala la katiba inayopendekezwa kuahirishwa hadi baada ya uchaguzi.

Kauli hiyo ima haikuandaliwa kifundi au imetolewa kama sehemu ya kuwa njia panda kama bandiko linavyosema.
Turejee tamko hilo kwanza
Tumaini Makene;12649755]

C/HQ/ADM/KK/08 05/05/201


MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHADEMA ILIYOKUTANA DAR ES SALAAM, MEI 3-4, 2015.

Ndugu waandishi wa habari

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imekutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama kuanzia tarehe 03-04/05/2015 pamoja na masuala mengine imejadili na kufanyia maazimio mambo yafuatayo;


  • Uteuzi wa wagombea ndani ya chama
Kamati Kuu imeazimia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu kwa ajili ya uteuzi wa ndani ya chama uanze ili watia nia katika maeneo mbalimbali wachukue fomu za udiwani, uwakilishi na ubunge na imetoa ratiba rasmi ya kuanza kwa zoezi hilo (Ratiba imeambatanishwa).


  • UKAWA
Kamati Kuu imepokea na kujadili mwenendo wa majadiliano na makubaliano ambayo hadi sasa yameshafikiwa na vyama vinavyounda UKAWA (NLD, NCCR- Mageuzi, CUF na CHADEMA), ambapo imewapongeza viongozi wakuu wa vyama vyote kwa hatua ambayo wameshafikia na imewataka wamalize masuala machache yaliyobakia ndani ya wakati ili waweze kuwatangazia Watanzania wanaoendelea kuunga mkono umoja huo wa dhati.


  • B.V.R, Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu
Kamati Kuu imepokea taarifa ya kina kuhusu mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR unaonedelea katika maeneo mbalimbali ambapo baada ya mjadala, imejiridhisha kuwa hadi sasa hakuna dhamira ya dhati ya kisiasa wala maandalizi ya kutosha yakiwemo matakwa ya kisheria, kitaalam na kibajeti ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa Katiba ..

Kutokana na taarifa hizo, Kamati Kuu imeridhika kuwa iwapo Watanzania hawatahamasishwa na kuamuka kudai haki yao ya kikatiba ya kuandikishwa na kupiga kura, zipo dalili za wazi kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chini ya Jaji Damian Lubuva inaweza kusababisha majanga makubwa kama ambavyo Tume ya Uchaguzi ya Kenya chini ya Bwana Kivuitu ilisababisha nchini humo mwaka 2008, Jaji Lubuva anajiandalia mazingira ya kuwa ‘Kivuitu wa Tanzania'.

Mbali na kukubaliana na hatua ambazo zimeshachukuliwa na UKAWA katika jambo hili hadi sasa, katika hali inayoendelea kwenye mikoa ambako sasa uandikishaji unafanyika baada ya Mkoa wa Njombe, imeazimia ifuatavyo;

Watanzania wote wenye sifa ya kuwa wapiga kura wanaandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi.

1.3 Kuhusu Kura ya Maoni

Kamati Kuu pia imejadili kwa kina namna ambavyo mazingira ya kisheria na uhalisia wa mwenendo wa kisiasa na kiuchumi nchini kwa sasa hauruhusu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, isipokuwa hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwezi Octoba 2015 kwa mujibu wa Katiba.

Hivyo kikao kimeazimia kuwa chama kiendelee kusimamia msimamo wa UKAWA uliotolewa hivi karibuni kuwa Kura ya Maoni isifanyike pamoja na Uchaguzi Mkuu lakini pia kwa vyovyote vile kura ya maoni iwe mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Octoba 2015.

1.4 Kuhusu hatma ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015

Kamati Kuu ilipokea taarifa ya kina namna ambavyo hadi sasa maandalizi ya msingi yanayotakiwa kisheria kwa ajili ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu hayajafanyika kama vile maandalizi ya vifaa, fedha , kutangaza Majimbo na Kata Mpya , kutangaza vituo na kusuasua kwa zoezi la Uandikishaji wapiga kura .

Katika jambo hili Kamati Kuu imeazimia kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu LAZIMA ufanyike mwezi Octoba kwa Mujibu wa Katiba na Serikali ya CCM isijiandae kutumia kisingizio chochote kuahirisha kwa sababu uchaguzi sio jambo la dharura, bali lilijulikana miaka 5 iliyopita.

Aidha imeitaka Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete kuacha hila zozote za kutaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani, ikiwemo kutaka kupeleka ‘Muswada wa Marekebisho ya Katiba Bungeni' ili kujihalalishia kuongeza uhai wa Serikali ya Kikwete.

  • Kamati Kuu imeitaka serikali kuchukua hatua za dharura kunusuru shilingi kwani athari zake ni kubwa sana kiuchumi na kijamii na zitasababisha mfumko wa bei .

  • Kamati Kuu imeazimia na kulaani tabia ya Rais wa nchi kusafiri ovyo nje ya nchi wakati ipo katika kipindi kigumu ikiwa na matatizo makubwa ambayo yanahitaji uongozi thabiti wa Mkuu wa nchi.

  • Sekta ya usafirishaji Nchini
Kamati kuu ilipokea ,kujadili na kutafakari hali halisi ya sekta ya usafirishaji nchini na kubaini udhaifu mkubwa ambao upo ndani ya sekta hiyo kutokana na usimamizi dhaifu wa watu ambao walipewa dhamana ya kusimamia sekta hiyo kuanzia waziri wa uchukuzi ambaye ameshindwa kabisa kuisimamia sekta hiyo , hali hiyo imepelekea sekta hiyo kukosa mwelekeo na kusababisha madhara mengi kwa wananchi kutokana na ajali za kila siku kuanzia vyombo vya Majini na Barabarani.

Kamati kuu imebaini athari ambazo zimewakumba watanzania kutokana na Mgomo wa Madereva kama vile wagonjwa kushindwa kufika hospitalini, maiti kushindwa kusafirishwa na kuzikwa , wanafunzi ambao wanafanya mitihani ya kidato cha sita kushindwa kufika kwenye vituo vyao hali iliyopelekea kushindwa kufanya mitihani yao , kuathirika kwa uchumi na wananchi kuathirika kisaikolojia.

Baada ya tafakuri ya kina, Kamati Kuu imeazimia kuunga Mkono madai ya Madereva kwani ni halali na hivyo ni lazima serikali iyatekeleze madai yao yote ya muda mrefu , kuendelea kuyapuuza madai hayo ni kukubali kuendelea kuhatarisha maisha ya Abiria ambao wanasafiri kutokana na ajali za kila mara, hivyo ili kuokoa maisha ya wasafiri, Madereva wasikilizwe na wapatiwe ufumbuzi wa madai yao yote kuanzia mikataba ya ajira, maslahi yao na kulipwa ujira unaolingana na kazi zao.

Imetolewa leo

Freeman Mbowe


……………………………

Mwenyekiti wa CHADEMA (T)





CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDEKELEO

(CHADEMA)



KWANINI TUNAONA TATIZO KATIKA TAMKO HILI?

Inaendelea sehemu ya II

 
Sehemu ya II

Kama inavyumbukwa, UKAWA wakiwemo Chadema walitoka nje ya bunge maalumu la katiba kama hatua ya kupinga na kutoshiriki mchakato uliovurugwa na CCM.

Hiyo ililazimisha katiba ya CCM kususiwa na wananchi, uandikishaji kusuasa sua na mwisho kuahirishwa

Hoja kubwa ya wapinzani ni kudharauliwa kwa maoni ya wananchi, na kuingizwa katiba ya CCM.
Pia, ni kushinikiza CCM warudi katika ramani 'map' iliyokusudia katiba ya wananchi na si kikundi cha watu

Tume ya Warioba na wananchi wamesimama kidete katika rasimu, kutetea msimamo wa kurudi kwenye rasimu

Tunakumbuka pia, UKAWA walihamasisha ususiaji wa katiba pendekezwa ya CCM, wito uliotikiwa na wananchi

Hadi sasa katiba pendekezwa imekosa hamasa, msisimko na kupoteza maana nzima ya uandikaji wa katiba

Hayo yamewezekana kwasababu wananchi wapo nyuma ya UKAWA wakiamini kwa dhati, katiba inayopendekezwa si yao ni ya wana CCM na kwamba mchakato mzima ulivurugwa.

Tunakumbuka sheria ya mchakato imeeleza hatua na muda wa shughuli za zoezi ikiwemo elimu kwa umma, uandikishaji na upigaji kura. Pamoja na kuvurugwa kuna sababu za kisheria zinazozuia mchakato haramu usiendelee

Kwa maana nyingine 'haramu' imezidi kuwa haramu kwasababu kisheria hakuna jambo linaloweza kufanyika bila kubadili sheria. Muda wa rais kutangaza kura ya maoni iumepita, elimu ya umma na uandikishaji umepita. Hii maana yake ni kuwa haramu imezidi kuwa 'haramu'

Hakuna uwezekano wa 'haramu' ya katiba kuendelea kwasababu kisheria haikubaliki.


TATIZO LA KAULI YA KAMATI KUU YA CHADEMA

Zipo njia za kuifanya 'haramu' iwe 'haramu' kidogo

1. Kurudi katika bunge la JMT na kurekebisha sheria ili muda wa kura ya maoni utangazwe,uandikishaji umalizwe,muda wa elimu ya umma utangazwe.

Hapo ni kurudi katika ubao kuanza upya hata kama haramu itapendekezwa kwa nguvu.

2. Kufuta kabisa katiba pendekezwa na kurudi kwenye rasimu

3. Kufuta zoezi zima na kuliandaa upya

Katika hayo matatu, hakuna hata moja linalotambua katiba pendekezwa.

Inaendelea.....
 
Sehemu ya II


KATIBA PENDEKEZWA NI 'OFF THE TABLE ab initio''

Tunaweza kusema kwa dhati kuwa nia ya UKAWA NA CDM wakwemo ilikuwa
1. Kususia mchakato mbovu
2. Kutotambua katiba pendekezwa
3. Kususia zoezi zima litalozaa katiba mbovu, isiyo ya wananchi na iliyoandaliwa na CCM

Kwa mantiki hiyo suala la katiba pendekezwa ni kando ya meza ya agenda (off the tabel) kwa kuanza hapo tu

KAMATI KUU CHADEMA

Ukisoma tamko la kamati kuu ya Chadema hapo juu, linasema katika vipengele kama ifuatavyo
1. Kichwa cha habari 'Kuhusu kura ya maoni''

Inashangaza kuwa suala la katiba pendekezwa limeweza kuwa katika agenda ya kikao cha kamati kuu yao

Kwa kuanzia , hiyo haikuwa agenda yao kuanzia walipotoka katika BMLK, waliohamasisha wananchi kususia na walipokuwa na msimamo na UKAWA kwa pamoja.

Ni makosa makubwa kwamba suala la katiba pendekezwa lilipewa hata nafasi na suala la kura ya maoni lilijadiliwa. Kura ipi ya maoni?

2. ''Mwendendo wa kisiasa na kiuchumi hauruhusu kura ya maoni ya katiba inayopenekezwa''

Maana yake ni kuwa kama hali ingekuwa nzuri kidogo kisiasa na kicuhumi, Chadema wangefikiria kura ya maoni ya katiba pendekezwa, kura ya kile walichosema ni haramu!

Kura ya maoni ya katiba ipi penekezwa CDM walioshiriki?

3. ''...Isipokuwa hadi baada ya uchaguzi mkuu wa Oktober 2015 kwa mujibu wa katiba''
Yaani wanapendekeza katiba ya Cheng' ifikiriwe baada ya uchaguzi mkuu.
Kwamba, sasa wanaanza kufikiria katiba ya CCM kwa kuipa uhalali taratibu.

Ni makosa makubwa sana
Hivi uchaguzi ukiisha na CCM wakaja na katiba yao kama watakuwa madarakani, wakisema wanafuata mapendekezo ya kamati kuu ya CDM, Kamati kuu ya CDM na CDM watajibu nini

4, Kamati kuu imeazimia kwenda na msimamo wa UKAWA kuwa kura ya maoni isifanyike na uchaguzi mkuu

Ni makosa kutaja kura ya maoni, na ni makosa makubwa kufikiria kuwa pamoja na uchaguzi mkuu.

Pengine wangesema kura ya maoni haipo, uchaguzi mkuu ufanyike wenyewe.
Kwamba hawakubali kura ya maoni kwanza, na hivyo isiunganishwa na uchaguzi mkuu.

5. ''Lakini kwa vyovyote vile kura ya maoni iwe baada ya uchaguzi mkuu''

Hapa ina maana tayari wameshaanza kuikubali katibapendekezwa, tatizo lao ni muda tu.


Inaendelea....
 
Sehemu ya IV

Hoja:

Tamko la kamati kuu ya CDM linatia shaka. Haieweki kwanini suala la kura ya maoni na katiba pendekezwa, waliosusia wakiwa ndani ya UKAWA liwe agenda ya kikao cha kamati kuu

Agenda ingekuwa rahisi, hawaitambui katiba pendekezwa na hawatambui hatua zote zinazofuata za kuhalalisha katiba hiyo.

Katika kipengele hicho, CDM hawaonekani kuwa makini

Kitendo cha kutosimama eneo moja, kinatoa fursa kwa CCM kuendelea na katiba ikiwa tayari walishakubali kuwa zoezi hilo limekosa uhalali wa kisiasa kwa kigezo chochote kile

Bandiko hili tulisema CCM maji ya Shingo, na sote tumeona maji yalivyokuwa marefu hadi kukubali kuacha zoezi lililolazimishwa na mzee wa Urambo na wenzake kwa rushwa, na kila aina ya uhalifu

Tulisema wapinzani wapo njia panda. Kwamba hawaoni mitego wanayotegewa.
Hili la tamko la CDM ni moja ya njia panda tulizoeleza

Katika mazingira haya, Chadema watoke mbele na kufafanua kuhusu tamko lao katika kipengele cha kura ya maoni.

Hilo litawasaidia na kusaidia upinzani kwa ujumla kujua wanasimama wapi na wanaelekea wapi

Kinyume chake, tutashuhudia Rais Mwingine akija na kuwaita kunywa juice ya maembe na baada ya hapo watatoka na msimamo wa Rais huyo kama atakuwa si wa upande wao.

Kamati kuu ya Chadema, kauli yenu ni tata tokeni mbele mueleze umma nini mlifikiria
Tamko lina mapungufu mengi na mazito

Tusemezane
 
Ndiomana Tunasema CDM ni walaghai tu,mfano wao walisema wamesusia kura ya maoni,sababu mchakato haramu,lakini wamekuwa wanajadili Tarehe ya kura ya Maoni,mfano Hotuba ya Mbowe katika bunge la bajeti tarehe 12 May 2015
 
Back
Top Bottom