Duru: ' Utata wa Utatu', Katiba, Muungano na Kura ya Maoni

Kweli Kuna tatizo Mahali!!! Elimu uliyoitoa hapa. Inatakiwa iwafikie wengi ili tuwe kwenye ukurasa mmoja wakati wa mjadala.
Matatizo ni makubwa ngawa Wazanzibar wanadai Muungano umewaumiza, Watanganyika wameumizwa zaidi.

Nimeuliza, mwananchi wa Tunduru, Tarime au Kigoma anaathirika vipi nje ya Muungano?

Kwanini Mwananchi wa Njombe, Simiyu na Geita mikoa michanga wabebe mzigo wa kuendesha Zanzibar kwa koti la Muungano? Kwanin kodi za Mkoa mpya wa Njomba au Simiyu zilipe bili za umeme Zanzibar

Kwanini Mwananchi wa Tunduru alipe kodi halafu iende kwenye ruzuku ya bajeti ya Zanzibar?

Ni kweli naunga Mkono Muungano uendelee kwa mazingira Yale niliyoeleza. Nchi moja, serikali moja kwa maana hiyo, tutakuwa na uraia wa aina moja hakutakuwa urai wa ukaazi bali raia wa Tanzania.
Nchi moja haiwezekani, Wazanzibar na Uzanzibar ni '' BORA'' Utanzania.

Kpindi cha SSH utadhani ni nchi mbili isipokuwa ambapo Zanzibar inataka masilahi ya Tanganyika.

Kwa mfano
Juzi kwenye mkataba wa Bandari kwanini Rais wa SMZ na Spika wa BLW walikuwepo wakati wamesaini mkataba Zanzibar bila kuwepo Mtanganyika! Hakukuwepo sababu yoyote ya viongozi hawa kuwepo

Hapa ni mazingira ya kwamba Bandari za Tanganyika ni za Tanzania na Zanzibar ipo

Pili, Wazanzibar wameondoa Bandari lakini hutawasikia wakitaka Elimu ya Juu iondolewe kwasababu pesa za HESLB ambazo ni hazina ya Tanganyika zinagawanywa kwa Zanzibar.

Kuna nafasi zaidi ya 1,000 za mikopo kwa Wazanzibar tu licha ya kwamba wana bodi yao ZHSLB.
Ni Formula gani na kwa vigezo gani kwamba kuna nafasi maalumu za Wazanzibar tena wasiorudisha mikopo

Mwaka huu Zanzibar wamesaini MoU na Tanzania kuhusu madini.
Rais SSH ameridhia kwamba kuna Tanzania halafu kuna Zanzibar na kalazimisha kuwe na MoU ya madini.

Kwa maana kwamba Rais SSH anakuwa wa Tanganyika kwa jina la Tanzania na Waziri wake wa Madini anasaini mkataba na Waziri wa madini wa nchi ya Zanzibar. Rais SSH '' anajivua'' Urais wa JMT ili ku-promote Uzanzibar. Endapo Tanzania a.k.a Tanganyika inaweza kuwa na MoU na Zanzibar , kwanini Tanganyika isiwe na serikali yake !

MoU aliyolazimisha Rais SSH ina maana moja, kwamba kuwepo na kubadilishana utaalamu wa katika sekta ya madini ambayo si ya Muungano. Zanzibar haina madini inakuwaje kuwe na MoU na Tanganyika?

Jibu ni moja MoU imelenga kuleta Wazanzibar Wiazara na idara za madini Tanganyika kama sehemu ya kuwatafutia ajira. Haya ndiyo ambayo Watanganyika wa kawaida wanayaona si walevi wa Dodoma

Huu ni ujanja wa kuingiza mambo ya Tanganyika katika JMT kijanja kwa lengo moja, kuinufaisha Zanzibar

Ikumbukwe Zanzibar inapata mgao wa madini kupitia 4.5% ya BoT .

Kwamba kila shilingi ya Tanganyika itoke eneo lolote ina mgao wa 4.5% kwenda Zanzibar.

Kwa maneno mengine, Wazanzibar wanahitaji DUA tu kwamba TRA ikusanye mapato zaidi kutoka madini, Kilimo, mifugo, utalii na kodi za Watanganyika ili kupitia 4.5% Zanzibar wajikusanyie.

Tusichokiona ndani ya Muungano ni eneo ambalo Zanzibar wanawajibika! Hakuna ! Hakuna
.
Hutasikia per cent ya kuchangia Muungano au kulipa madeni au kusaidia hata kidogo walicho nacho

Hapa ndipo naku challenge TUJITEGEMEE

-Mchango wa Zanzibar katika kuendesha Taasisi za Muunganoni upi? Mbona hatuoni per cent?

-Wapi Zanzibar inalipa mishahara ya 21% ya Wafanyakazi wa Muungano!

-Kwanini Zanzibar imeondoa banadari na Bandari za Tanganyika zinasimamiwa na Wazanzibar

-Ajira za Muungano zinahusu mambo mangapi na mambo gani.

-Tuonyeshwe Formula ya kulipa mikopo ya nje ambayo hugawanywa Zanzibar kwa Formula

-Kwanini Wabunge wa Zanzibar walipwe mishahara na marupu rupu na kodi za Tanganyika si SMZ?

-Kwanini Wabunge wa Zanzibar wanaamua mambo yasiyo ya muungano AN kamati zsisizohusu Muungano

-Kwanini Mbunge wa watu 4000 Zanzibar apewe MFUKO wa Jimbo sawa na Mbunge wa Ilala watu 100,000+

-Kwanini kodi kutoka Hazina Tanganyika ziende kuhudumia majimbo ya Zanzibar

-Kwanini TCRA ikusanye pesa za simu za Tanganyika halafu itoe mgao kwa Zanzibar !

-Kwanini mwanafunzi wa Tanganyika arudhishe mkopo wa HESLB yule wa Zanzibar apewe grant

-Kwanini Mzanzibar aajiriwe eneo lisilo la Muungano lakini Mtanganyika hana nafasi kule Zanzibar

-Ikiwa tuna national ID, Kitambulisho cha Z'bar ukaazi kina kazi gani zaidi ya ubaguzi dhidi ya Watanganyika

-Kwanini ardhi liwe suala la Muungano kwa Tanganyika lakini kwa Zanzibar ni marufuku kwa Mtanganyika

-Kwanini kodi za TRA kutoka Zanzibar zibaki Zanzibar na kodi za TRA za Tanganyika zihudumie Muungano

-Kwanini kuwe na Taasisi za Muungano ambazo Wazanzibar wapo halafu kuna mbadala wa Taasisi hizo Z'bar

-Katika Muungano ni kiongozi gani ampewa jukumu la kusimamia masilahi ya Tanganyika
Kwa mfano, Wazanzibar wameondoa Bandari katika Muungano.
Wanosimamia mikataba ya Bandari za Tanganyika ni Rais (Mzanzibar), Waziri (Mzanzibar) Katibu mkuu (Mzanzibar).

Wazanzibar wapewe nafasi ya kuamua kama wanataka Muungano au la. Kama hawataki waachwe waondoke

Kama wanataka Muungano lazima lazima ushiriki wao uwe wa kuwajibika si wao washiriki migao
 
MSWADA WA 'TUME HURU YA UCHAGUZI NA SHERIA YA MSAJILI WA VYAMA''

USALITI NA MASILAHI BINAFSI NI HATARI SANA KULIKO KATIBA YA 1977


Hata kabla ya kuuona na kuusoma mswada wa mabadiliiko ya Tume ya Uchaguzi na sheria ya msajili wa vyama, tumeandika mara nyingi, kinachotokea ni ' Ujinga na Ujuha wa vyama vya Upinzani''

ACT Wazalendo
Kauli mbiu ya ACT ni Zanzibar yenye mamlaka kamili. ACT wanadai mkataba wa Muungano ni mbovu kuliko mikataba mingine. ACT wanadai uwepo wa Serikali 3 ili ya Tanganyika na Zanzibar ziwepo.

ACT kinasema Wazanzibar hawataki Muungano., madai ya kila siku .

Kiongozi wa ACT Bw Zitto Zuberi, mshiriki mkubwa wa Tume ya Mkandara alifurahishwa na mswada akisema ni hatua ya kupongezwa kwasababu msimamo wa ACT ni kuwa na Tume huru ya uchaguzi.

Zanzibar iliwahi kuwa na Tume huru ya uchaguzi wakati wa Maalim Seif na CUF.
Hadi Maalim anafariki hakuwa Rais kwasababu tume aliyodhani ni huru haikuwa huru, ilikuwa ni ghiliba tupu

ACT Wazalendo ( CUF ya Zamani ) wanaposhangilia uwasilishwaji wa mswada ni uzetete na uhayawani

Ni uzezeta kwasababu hawakujifunza kutokana na Tume huru ya Zanzibar au Uchaguzi wa 2020.
ACT wanaamini kwa kutumia katiba ya 1977 wanaweza kupata tume huru ya uchaguzi na sheria nzuri ya msajili

ACT wanatambua CCM ndio wenye Bunge na sheria yoyote itatungwa kukidhi matakwa yao

ACT hawakuona uhuni wa mkataba wa Bandari ulivyofanyika Dodoma, wanaamini miujiza, siyo fikra na sayansi

ACT wanaamini sheria zinaweza kupingana na sheria ya kuu ya Katiba kwa matakwa au hisani za CCM

Hakuna mwenye akili timamu anayesimama na kusema mswada huo ni jambo jema.
Ni ima awaye hajui nini cha kufanya au anatumika.! wenye shaka na usaliti wa ACT wana sababu..

ACT walishiriki tume ya Mkandara ambayo lengo lake ni kupiga teke maoni ya Tume ya Warioba
Ikiwa CCM walikuwa na nia njema kwanini Tume ya Warioba na maoni yake yalitupiliwa mbali?

Zitto alikuwa mjumbe wa Bunge la Katiba, leo anaaminisha watu kwamba Kamati ya Mkandara ambayo yeye ni mjumbe ilifanya kazi nzuri kuliko ya Warioba. Huu ni uzumbukuku kama siyo usaliti.

Zitto aeleze umma, Kamati ya Mkandara ilihoji watu wangapi dhidi ya ile ya Mzee Warioba?

Pamoja na ukweli ACT wanashiriki serikali ya nusu mkate Zanzibar (GNU) kuna kila sababu ya kuamini Usaliti

Ukisilikiza kauli za ACT kule Zanzibar halafu ukafuatilia matendo yao utabaini unafiki na Usaliti.

CHADEMA
Msimamo wao ni katiba mpya, karibuni wamekuwa na msimamo wa marekebisho ya katiba ya 1977.

Msimamo wa marekebisho umeletwa na Mwenyekiti baada ya kukutana na Rais Samia akitokea magereza

Mbowe amebadili misimamo ya CHADEMA kwa kile alichokiita Maridhiano.
Mbowe aliambiwa CCM hawana ni njema lakini alisisitiza Mama ana nia njema
Mbowe ameshiriki vema kudhoofisha kabisa harakati za kudai katiba mpya kwa kujua au kutojua

Mwisho wa siku CCM wamemchezea akilia kama Mbowe alivyofanywa na Magufuli pale Mwanza.

Mbowe hufanya jambo lile lile kwa namna ile ile akitaraji matokeo tofauti. Ni kieleleza kizuri cha Insanity

Marekebisho ya katiba ya 1977 ni Ujinga na ujuha tu. Hivi unawezaje kuweka kiraka juu ya kiraka?

Katiba ya 1977 ni mbovu, haiwezi kujitetea kwa ushahidi. Kila Rais amekiuka katiba bila hofu.
Kutegemea marekebisho ni ujinga , uzwazwa na ujuha wa siasa.

Wanaharakati wanaondelea kudai katiba mpya wapo sahihi, ni wakati wa kuwapuuza akina Mbowe na Zitto,
Ni wakati wa kuwaambia Wanafiki kule visiwani waache matarumbeta na kuwageuza Wazanzibar majuha

OMO , Jussa na Duni waulizwe, wanawezaje kupata mamlaka kamili kwa katiba ya 1977! huu ni ujinga upuuzwe, hauna uhalisia ni upuuzi kama mwingine. Inaonekana hawajui wanataka nini au wanajua lakini ni wasaliti.

Hawa wakae pembeni waache wana harakati waendelee na jitihada.
 

Kwa hisani ya gazeti la The citizen

Kuna ushahidi wa kutosha kwamba Zanzibar inapewa 9% ya Bajeti ya Muungano, yaani mara mbili ya kile kiwango cha 4.5%. Anayesema hayo ni MNEC Zanzibar akimshukuru Rais Samia

Swali, ni kiasi gani Zanzibar inachangia Bajeti ya Muungano kiasi cha kupewa 9%

Tuendelee na mjadala kutoka uzi wa Yoga na mengine hapa

Pascal Mayalla STALIN J V ngaboru ruaharuaha raraa reree TUJITEGEMEE
Tafadhali mkaribishe yoyote
 


Kuna mamlaka ya anga ya Tanzania ambayo ni ya Tanganyika (TCAA) halafu kuna mamlaka ya anga Zanzibar (ZCAA). Ukisoma habari hiyo kwa hisani ya gazeti la the citizen utaona Tanganyika imetumia Bilioni 30 kununua vifaa vya anga ambavyo pia vimegawanywa kwa viwanja vya ndege vya Zanzbar kwa jina la Muungano.

Inapofika wakati wa kugawa mafao Wazanzibar ni Watanzania. Swali la Kujiuliza, iwapo tuna TCAA kwanini kuwe na ZCAA. Ikiwa hizi ni taasisi mbili tofauti kwanini fedha za TCAA ziende Zanzibar badala ya kuendeleza viwanja vya walipa deni au kodi wa Tanganyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…