Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #41
Matatizo ni makubwa ngawa Wazanzibar wanadai Muungano umewaumiza, Watanganyika wameumizwa zaidi.Kweli Kuna tatizo Mahali!!! Elimu uliyoitoa hapa. Inatakiwa iwafikie wengi ili tuwe kwenye ukurasa mmoja wakati wa mjadala.
Nimeuliza, mwananchi wa Tunduru, Tarime au Kigoma anaathirika vipi nje ya Muungano?
Kwanini Mwananchi wa Njombe, Simiyu na Geita mikoa michanga wabebe mzigo wa kuendesha Zanzibar kwa koti la Muungano? Kwanin kodi za Mkoa mpya wa Njomba au Simiyu zilipe bili za umeme Zanzibar
Kwanini Mwananchi wa Tunduru alipe kodi halafu iende kwenye ruzuku ya bajeti ya Zanzibar?
Nchi moja haiwezekani, Wazanzibar na Uzanzibar ni '' BORA'' Utanzania.Ni kweli naunga Mkono Muungano uendelee kwa mazingira Yale niliyoeleza. Nchi moja, serikali moja kwa maana hiyo, tutakuwa na uraia wa aina moja hakutakuwa urai wa ukaazi bali raia wa Tanzania.
Kpindi cha SSH utadhani ni nchi mbili isipokuwa ambapo Zanzibar inataka masilahi ya Tanganyika.
Kwa mfano
Juzi kwenye mkataba wa Bandari kwanini Rais wa SMZ na Spika wa BLW walikuwepo wakati wamesaini mkataba Zanzibar bila kuwepo Mtanganyika! Hakukuwepo sababu yoyote ya viongozi hawa kuwepo
Hapa ni mazingira ya kwamba Bandari za Tanganyika ni za Tanzania na Zanzibar ipo
Pili, Wazanzibar wameondoa Bandari lakini hutawasikia wakitaka Elimu ya Juu iondolewe kwasababu pesa za HESLB ambazo ni hazina ya Tanganyika zinagawanywa kwa Zanzibar.
Kuna nafasi zaidi ya 1,000 za mikopo kwa Wazanzibar tu licha ya kwamba wana bodi yao ZHSLB.
Ni Formula gani na kwa vigezo gani kwamba kuna nafasi maalumu za Wazanzibar tena wasiorudisha mikopo
Mwaka huu Zanzibar wamesaini MoU na Tanzania kuhusu madini.
Rais SSH ameridhia kwamba kuna Tanzania halafu kuna Zanzibar na kalazimisha kuwe na MoU ya madini.
Kwa maana kwamba Rais SSH anakuwa wa Tanganyika kwa jina la Tanzania na Waziri wake wa Madini anasaini mkataba na Waziri wa madini wa nchi ya Zanzibar. Rais SSH '' anajivua'' Urais wa JMT ili ku-promote Uzanzibar. Endapo Tanzania a.k.a Tanganyika inaweza kuwa na MoU na Zanzibar , kwanini Tanganyika isiwe na serikali yake !
MoU aliyolazimisha Rais SSH ina maana moja, kwamba kuwepo na kubadilishana utaalamu wa katika sekta ya madini ambayo si ya Muungano. Zanzibar haina madini inakuwaje kuwe na MoU na Tanganyika?
Jibu ni moja MoU imelenga kuleta Wazanzibar Wiazara na idara za madini Tanganyika kama sehemu ya kuwatafutia ajira. Haya ndiyo ambayo Watanganyika wa kawaida wanayaona si walevi wa Dodoma
Huu ni ujanja wa kuingiza mambo ya Tanganyika katika JMT kijanja kwa lengo moja, kuinufaisha Zanzibar
Ikumbukwe Zanzibar inapata mgao wa madini kupitia 4.5% ya BoT .
Kwamba kila shilingi ya Tanganyika itoke eneo lolote ina mgao wa 4.5% kwenda Zanzibar.
Kwa maneno mengine, Wazanzibar wanahitaji DUA tu kwamba TRA ikusanye mapato zaidi kutoka madini, Kilimo, mifugo, utalii na kodi za Watanganyika ili kupitia 4.5% Zanzibar wajikusanyie.
Tusichokiona ndani ya Muungano ni eneo ambalo Zanzibar wanawajibika! Hakuna ! Hakuna
.
Hutasikia per cent ya kuchangia Muungano au kulipa madeni au kusaidia hata kidogo walicho nacho
Hapa ndipo naku challenge TUJITEGEMEE
-Mchango wa Zanzibar katika kuendesha Taasisi za Muunganoni upi? Mbona hatuoni per cent?
-Wapi Zanzibar inalipa mishahara ya 21% ya Wafanyakazi wa Muungano!
-Kwanini Zanzibar imeondoa banadari na Bandari za Tanganyika zinasimamiwa na Wazanzibar
-Ajira za Muungano zinahusu mambo mangapi na mambo gani.
-Tuonyeshwe Formula ya kulipa mikopo ya nje ambayo hugawanywa Zanzibar kwa Formula
-Kwanini Wabunge wa Zanzibar walipwe mishahara na marupu rupu na kodi za Tanganyika si SMZ?
-Kwanini Wabunge wa Zanzibar wanaamua mambo yasiyo ya muungano AN kamati zsisizohusu Muungano
-Kwanini Mbunge wa watu 4000 Zanzibar apewe MFUKO wa Jimbo sawa na Mbunge wa Ilala watu 100,000+
-Kwanini kodi kutoka Hazina Tanganyika ziende kuhudumia majimbo ya Zanzibar
-Kwanini TCRA ikusanye pesa za simu za Tanganyika halafu itoe mgao kwa Zanzibar !
-Kwanini mwanafunzi wa Tanganyika arudhishe mkopo wa HESLB yule wa Zanzibar apewe grant
-Kwanini Mzanzibar aajiriwe eneo lisilo la Muungano lakini Mtanganyika hana nafasi kule Zanzibar
-Ikiwa tuna national ID, Kitambulisho cha Z'bar ukaazi kina kazi gani zaidi ya ubaguzi dhidi ya Watanganyika
-Kwanini ardhi liwe suala la Muungano kwa Tanganyika lakini kwa Zanzibar ni marufuku kwa Mtanganyika
-Kwanini kodi za TRA kutoka Zanzibar zibaki Zanzibar na kodi za TRA za Tanganyika zihudumie Muungano
-Kwanini kuwe na Taasisi za Muungano ambazo Wazanzibar wapo halafu kuna mbadala wa Taasisi hizo Z'bar
-Katika Muungano ni kiongozi gani ampewa jukumu la kusimamia masilahi ya Tanganyika
Kwa mfano, Wazanzibar wameondoa Bandari katika Muungano.
Wanosimamia mikataba ya Bandari za Tanganyika ni Rais (Mzanzibar), Waziri (Mzanzibar) Katibu mkuu (Mzanzibar).
Wazanzibar wapewe nafasi ya kuamua kama wanataka Muungano au la. Kama hawataki waachwe waondoke
Kama wanataka Muungano lazima lazima ushiriki wao uwe wa kuwajibika si wao washiriki migao