Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

gfsonwin

Suala la kwenda mahakamani linawezekana, lakini pia uangalie mfumo uliopo unatoa nafasi?

Jitihada za kuzima sauti si suala la bahati mbaya, ni suala lenye mkakati mkubwa kimfumo

Kama utakumbuka, bunge lilizuiliwa kuoneyshwa na Nape Nnauye kwa maagizo ya serikali ambayo leo anaweza kutazama nyuma na kubaini alichofanya kilikuwa na athari kiasi gani katika jamii

Wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi katika chombo huru wanakamatwa katika mazingira ya kusikitisha, wanaandamwa waliko ilimradi tu kuhakikisha kuna kuogofya

Hata dhamana , jambo la kawaida kisheria limechukua mwelekeo wa kisiasa. Mahakama!

Ikaja kwa wanasheria wakiambiwa uwakili unafanywa kwa 'baadhi' mengine ni tatizo
Tukasikia hoja kuhusu mambo ya sheria zilizoleta utata sana

Ukabakia mhimili usio rasmi wa medium. Huu umeonekana ni mwiba kwa kusema yasiyotakiwa

Ikatukumbusha zama hizo ukifungua Kenya (KBC) habari ni za mtukufu Rais Moi
Na zama za RTD, Uhuru na Mzalendo. Kwamba, habari ni mambo mazuri tuu kila kitu sawia

Tukakwenda mbali kidogo kwa kuingia vituo vya matangazo kushinikiza habari tunazotaka

Hilo linaonekana ''kukubalik'' Waziri alipochukua hatua hakuchukua muda akaondolewa

Waziri aliyeingia anasema hana habari kuhusu tukio, na hawezi kuliongelea

Tumemsikia akiongelea video ya Ney wa Mitego na kwamba kauli imetoka aachiwe
BASATA wenye jukumu walipiga marufuku, Polisi walimkamata kwa kutenda kosa

Unaweza ona, kwamba, waziri anaweza kushughulikia Ney na hana 'habari' kamili za Clouds

Habari za clouds ni nzito, ni tukio la kwanza , hatukuzoea na lilitisha tasnia ya habari

Medium zimeonywa ziandike habari za maendeleo, hatujui hili la Ney ni sehemu yake au la

Ukitazama kwa undani, mfumo mzima hautoi nafasi kwa taasisi kufanya kazi.

Unategemea maelezo.Unaposema watu waende mahakamani factors zingine unaziangaliaje?

Bila kubadili mfumo wa sasa unaotoa nguvu zaidi ya kipimo, popote panapofikiriwa, nguvu ina nguvu

Tusemezane
 
KUNA TZ YA VIWANDA NA ''Vi-WONDER''

YANAYOENDELEA, NI KUKOSA MKAKATI AU KUCHANGANYIKIWA?

Kuna vijana wa JF wanatumia neno Tz ya vi-wonder.
Tulidhani wanatumia neno wakitafsiri kiswahili kwa kiingereza katika utani.

Pengine hatukuwaelewa vijana hao. Kuna Tanzania tunayotaka ya viwanda na Tanzania ya 'vi-wonder' kwa maana ya miujiza, mshangao n.k. tunawaelewa vijana wale leo, kuna tz mbili

Tunaambiwa ni muda wa kuongelea maendeleo. Kabla ya mjadala kunatokea vi-wonder
Tunaishia kuzungumzia vi-wonder kila siku kwasababu hatuna hadithi za viwanda

Kuna walimu walimpiga mwanafunzi Mbeya, Waziri wa elimu akaingilia kati
Waziri aliingilia kati suala la vyeti, kwasasa limesimama, TZ ya vi-wonder

Tarime, wababe wakamcharanga viboko mwana dada. Waziri husika akaingilia kati
Orodha ya matukio yanayoshughulikiwa na ngazi za serikali ni ndefu na inaendelea

Kwa mshangao, suala la Nay wa Mitego(NY) limepewa umuhimu wa pekee, waziri akiita wanahabari kueleza kuachiwa kwa NY, na mara kuna habari kaalikwa kwenda kuonana

Waziri aliyeshindwa kueleza la clouds aliweza kueleza la Nay. Kama si vi-wonder ni nini?

Kuna maswali ya kujiuliza, hivi nani alihisi Ney ana makosa?
Ukisikiliza nyimbo hakuna kigeni.Ney kasema kuna wanawake wanasagana, vidume vinalelewa.
Je, hayo ndiyo yameamasha hamaki? kasema kuna Bashite wa kolomije,ndilo liliamsha hisia?

Kasema alikuwepo Jakaya wakaja wengine, je hilo ndilo kukosa maadili?

Kwa hali yoyote Nay asingeshtakiwa na ingetokea hivyo angeshinda kesi bila wakili
Kwa hali ya vi-wonder suala limepewa uzito kuuondoa umma kwenye hoja halisi

Limepewa umuhimu kuliko madini , elimu na afya. Kama si tz ya vi-wonder ni nini?

Je, la Nay na clouds na silaha tunaweza kuyaweka katika mizani?
Kwanini hatukuona suluhu kama zinazotokea kwa Nay? Kuna nini katika hilo?

Sakata la clouds limegusa'mhimili wa habari' si clouds tu
Limepeleka shock wave katika media industry.
Hakuna anaehisi yu salama,uhuru wa kujieleza ni fadhila si haki

Kuna mawili yanayojitokeza. Kwanza, medium zitahisi tukio si la bahati mbaya au mtu.
Pili, tukio litahama kutoka kwa mtu na kubebwa na serikali,tutaongelea maendeleo yapi?

Timbwili la Ney haliwezi kuwa mbadala wa matatizo mengine.
Hatuwezi kusafisha uchafu kwa kuufunika chini ya kapeti,hiyo ni kwa tz ya vi-wonder tu.

Wanaoandaa mkakati wa kuhamisha mjadala, wanafunika uchafu chini ya kapeti

Watu wanaweka la Nay na Clouds katika mizani.Hawana jibu! wanashangaa, vi-wonder!

Tunadhani wapo watu wanaoandaa mikakati, hawaoni tatizo
Huwezi kutibu kidonda kwa kukifunga na kitambaa, kitaoza kikifumuka ni kuchanganyikiwa

Tumepoteza uelekeo au tumepoteza mashine ya kuonyesha dira?

Tutaendele hivi hadi lini? Lini tutaongelea Tanzania ya viwanda na si ya vi-wonder?

Tusemezane
 
wakuu labda nichangie haya kutokana na mabandiko mawili ya Nguruvi3.

kwanza tuanze na swala la Ney, unless kama mimi nimewaza tofauti ila kiukweli kuna baadhi ya watu walitaka kumuwekea rais maneno kinywani. yaani BASATA na polisi walikaa kwa hisia zao waka conclude kwamba rais amekashfiwa.

hivi unamtuhumu mtu pasi kuwa amekutaja jina yaani kwa hisia tuuu...................

istoshe hili halionekani kama kashfa kwa mheshimiwa ikiwa hakuna aliye ona kama kashfa mpaka hao watendaji waliposema kuwa ni kashfa kwa mheshimiwa!

kwa staili hii hili ni tatizo sana kwa watendaji wetu. na ndio maana nimehoji jamani ivi haya maamuzi yanapofikiwa huwaga mhusika anahusishwa?

utakuwa ni ujinga sana kama hatahusishwa afu watu wanakurupuka tuu kumsemea, hasa kwenye ishu zilizojaa hisia tuu bila kuwa na evidence za kuaminika.

Pia nafikiri watendaji wa serikal wanataka kuprove kuwa wachapa kazi ili wasifiwe wakasahau kabisa uchapa kazi hautokani na mhemko unatokana na hekima.

mtu atawaza tuu jinsi ya kumfanya mkuu aridhike naye lakini wakasahau approach yake.

so far mtu mjanja hawez kushindwa kujua kwamba Magufuli hawez kufanya kile mkitakacho bali kile akitakacho. na alishasema asiamuliwe lkn watendaji wake bado wanashindwa kumuelewa.
 
gfsonwin

Bandiko juu, tufikiri watu walimwekea maneno mh Rais kwa minajili ya mjadala huu

1. Basata: wimbo usipigwe hauna maadili.
Hawakusema mhusika ashtakiwe. Basata hawakueleza wapi maadili yalipokosekana
Ni katika kufanya kazi bila weledi, maarifa. Ndivyo zilivyo taasisi zetu

2. Polisi walimkamata kwanza bila kujua katenda kosa gani. Halafu ndipo wakatafuta kosa
Again ni taasisi zetu kama Basata!

Kama walitaka kumwekea maneno, ilitosha tu taarifa ndogo ya Ikulu kukanusha.

Kwa jinsi lilivyokuzwa, waziri kuitisha press na mbwembwe, kuna shaka na uaminifu

RC anapovamia kituo hilo ni kubwa sana linamgusa Rais. Ulisikia kauli yoyote?
RC kutuhumiwa kufoji vyeti ni kubwa sana, ulisikia kauli yoyote?

Kinyume chake waliotaka kusahihisi makosa ndio wakosaji na wameadhibiwa

Ukitazama kwa undani, hili la Ney ni katika kuficha ukweli kuhusu tuhuma nzito zinazomkabili RC
1. Kuhusu kufoji vyeti ambalo halijazungumziwa na kubaki tuhuma nzito sana
2. Kutumia madaraka na nguvu kuingia kituo cha habari kwa ugomvi binafsi

La Ney nikuondoa watu katika mjadala. Kama kweli kungekuwa na prompt action kama tunayoona kwa Ney, vipi la RC mbona tuhuma zinalundikana hakuna anayeeleza ni nini

Picha inayopataikana haraka, namna inavyobabaishwa, tuhuma zinazomkabili zinapata miguu.
Hakuna anayekanusha, hakuna anayetetea bali tunatakiwa tuondoke katika mjadala huo !

Tusemezane
 
Najiuliza sana,

Inakuwaje RC anajiamini sana pamoja na tuhuma zote zinazomkabili kuhusu elimu yake....kama ni kweli elimu yake iko kama inavyodaiwa....je yeye haoni kwamba ni bomu linalosubiri kulipuka?

Hivi Baba yake Mzazi anaitwa nani...au anatumia jina gani?
 
Mkuu Ogah swali lako linagonga vichwa vya wengi. Hakuna anayeelewa kujiamini kunatokana na kitu gani, lakini inaeleweka 'kulindwa' kwa namna fulani

Kwanza, RC kafanya mengi yasiyostahiki. Kutoa maagizo watu 'wapigwe' atajibu, ni jambo zito. Hiyo ni kauli ya serikali, aliitoa akiwa na bendera. Hakukemewa, tulisikia NGO zikilalamika

Akafika mahali anasema 'Bungeni' wanalala tu. Katika spirit ya kuheshimu mihimili, wajibu na heshima zake,akiwa amebeba bendera kama kiongozi inatia shaka

Hili la vyeti lina utata sana. Yapo mengi amefafanua na ni mwepesi wa kutumia 'media'.
Kwa hili hakuna rekodi kama amejaribu

Zoezi la kutafuta waliofoji limesimama, nani ana 'guts' kabla ya kukumbana na maswali?
La majina nalo limebaki kitendawili kama la vyeti , halina wa kutegua

Kwanini alikwenda Clouds kushahidia video itangazwe, ashindwe kuweka rekodi sawa?

Kinachoshangaza la clouds kama mengine nalo halijazungumziwa
Waliojaribu kuleta uelewano wameshughulikiwa!

Kwa sehemu kubwa, kama kiongozi anaikwaza serikali.
Kukwama kwa zoezi la kuhakiki vyeti kwa wahusika kuogopa hoja zinazomgusa RC,intisha

Upana wa hili ni pale suala la clouds linapozungumziwa kimataifa.

Mkutano wa media Kampala na taasisi ya US zimeto kauli nzito (gazeti la the citizen)
Ukisoma si jambo la RC bali serikali. Nchi inapata taswira tofauti kwasababu ya mtu

Swali la mwisho linaingia, RC anajiamini kwa nguvu gani kiasi hicho?

Kuna Rai inayoweza kumsaidia yeye, serikali na nchi kwa ujumla
Hili suala la vyeti na majina lipo katika uwezo wake, ajitokeze na kulifafanua

Kama hawezi, wahusika kama wizara ya elimu, baraza la mitihani , msajili wa uzazi na vifo wanaweza kusaidia kuweka ukweli. Kwanini kuna kusita?

Tusemezane
 
Asanteni wanajamvi kwa michango yenu yenye kuelemisha na pia kutoa maangalizo katika swala zima la uongozi wa nchi yetu.

Ningependa kutoa mchango wangu katika mambo matatu au manne ninayoyaona yanaukabili utawala/uongozi huu kwa mtazamo wangu:
Kwanza kabisa ni watendaji: Watendaji wetu (hasa wasaidizi wa Rais kama Makamu wa rais, Waziri mkuu, mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wengineo) katika utawala huu wanaonyesha uwoga ni waoga kutoa maamuzi, ni waoga kuchukua maamuzi fulani na ukiwangalia katika jicho la tatu unaona kuwa wapo wapo na hawafahamu nini cha kufanya. Na hii nafikiri inatokana na kasumba ya watanzania ya nidhamu ya uwoga, uwoga wa kumkosea bwana mkubwa, uwoga wa kutumbuliwa unamefika wakati kila mtu anafanya kazi wa kutegemea akili ya mtu mmoja. Yaani wanaangalia leo Rais anasema nini ndio wanachukua hatua. Mfano ukimuangalia yule Mwigulu wa Mh.Kikwete Mwigulu aliyekuwa anajihamini, Mwigulu aliyekuwa anaonyesha mapenzi wa nchi yake, Mwigulu aliyekuwa mstari mbele kutetea serikali yake si Mwigulu huyu aliyepooza, Mwigulu mwenye mashaka, Mwigulu ambaye hajui afanye nini wapi na kwa wakati gani.. Tukienda kwa Makamba, Makamba wa Kikwete aliyejaa ujasiri, si Makamba wa leo hii ambaye anasubiri Rais kasema nini leo. Waziri mkuu alianza kwa kasi kweli kweli alikuwa ni mtu aliyekuanajihamini lakini baada ya kushushuriwa na Makonda Waziri wetu mkuu amekosa ujasiri amekuwa yupo yupo tu bora mwisho wa mwezi ufike na achukue mshahara wake. Hivyo hivyo kwa mama yetu Samia masikini yule mama sijui yuko wapi?

Hii yote tatizo ni nini? Nafikiri tatizo hapa ni Mh. Rais kutokaa na Team yake na kuweka mikakati ya kutatua matatizo mbalimbali, kuwa karibu ya team yake, kuonyesha team yake kuwa kila mtu ni muhimu kwake anapenda na anathamini michango yake, kutopenda mawazo ya mtu mwingine kwamba yeye mawazo yake ni bora na ni lazima yafuatwe na kutokuwa na amini kwa team yake. Sote tunafahamu huwezi kufanikiwa katika jambo lolote kama team yako imesambaratika, kama huna imani na team yako, kama hutoi mwanya kwa watu wako kutoa mawazo yao na yale mawazo mazuri kufanyiwa kazi.

Nikija kwa Mh. Rais nafikiri ukimwagalia Mh. Rais ni mtu aliyekulia katika malezi ya mfumo dume, kwamba baba akisema basi yote mfuate, mwenye chuki na visasi hasa kwa watu ambao wako kinyume na mtazamo wake, hafahamu maana ya kusiliza mawazo ya mtu mwingine hata kama ni mtoto mdogo msililize unaweza kujifunza kitu fulani kwake, Hapendi kuambiwa ukweli maana kwake akifanya kitu alichoambiwa anajiona si mkubwa tena (kumbuka mfumo dume aliyokulia baba ndio mwenye uamuzi wa mwisho) ni mtu ambaye anapenda sana kusifiwa, anayependa majungu/kusikia habari za fulani/uongo,nafikiri anahisi kuwa na akili kuliko watanzania wote, ni mtu hasiye na imani kwa mtu yeyote yaani kwake kila mtu ni mwizi na jambo likifanywa na mtu mwingine basi anahisi lazima kuna cha juu, nafikiri pia anainfo za kila kiongozi kupitia TISS na hii inamvuja moyo na inamfanya hakose uaminifu kwa watu wake. (maana viongozi karibia wote wa siasa wawe ni wapinzani au CCM ni mafisadi/wezi.

Mh. Rais ni mtu anayependa nchi yake, anayependa watu wake, mwenye uchungu na masikini wa nchi yake, anayependa kuona Tanzania inapiga hatua ya kwenda mbele lakini tatizo hafahamu la kufanya matokeo yake ameanza kukimbizana na wapinzani na wapinzani wameisha msoma (hasa Lissu) anamchokonoa naye anaigia kingi.

Kutokana na kuwa na mawazo yake peke yake unakuta vitu vingi ni nguvu ya soda baada ya muda mfupi tunarudi pale pale kama Mwanzo rejea swala la Muhimbili. au vitu vingine ni maamuzi ambayo katika hali ya kawaida ni vigumu kuyaelewa Mfn swala vyeti feki, kuna watu walitumia majina ya watu wengine kwa ajiri ya kurudia madarasa (kitu ambacho miaka ya 1990 kama mtu alifeli Darasa la saba ulikuwa hurusiwi kurudia Darasa) tena kwa nia njema mf. Mwigulu wamesoma wamefanya kazi vizuri tu unakuta mtu kafanya kazi yake miaka 40 kabakisha miaka 2 kustaafu unamfukuza kazi, huyu mtu akifukuzwa kazi hata hela yake ya kustaafu halipwi, Jamani kama Taifa tulishindwa kuangalia ni watu gani wenye vyeti feki na walivipata kwa njia gani? hebu niambie mtu aliyerudia darasa kwa jina la mtu mwingine utasemaje ana cheti feki? Tukitafsiri vyeti feki basi Makonda ndo mfano wa mtu mwenye cheti feki maana alifeli na akaendelea na masoma ya juu huku akifahamu kuwa hana sifa za kuendelea na masomo hayo.. Lakini si kwa mtu aliyechukua jina la mtu akarudia darasa akafanya mtiani na kufaulu hivyo kuwa na sifa ya kuendelea na masomo ya juu..

Sasa basi swala linapofika kwa mteule wake akawa na kigugumizi/hasira vitisho, jeuri hali anafahamu alitumia vigezo, hiyo hivyo kuwafukuza watu wengine waliotumikia taifa ili kwa maisha yao yote wakiwa na feki ambavyo si feki, ila majina ndo sio yao, hapo ndo tunajiuliza hivi kulikuwa na ulazima gani wa kukurupuka na vyeti feki hali ungekaa na team yako ukasikiliza mawazo yao na hapo wangetoko na mawazo ambayo yangeangalia pande zote na kuja na suruhisho ambalo la kwajibisha wale ambao wanatumia vyeti vya watu wengine kama Makonda na wale waliorudia kwa kutumia majina ya watu wengine kwa namna moja au nyingie basi na wao wangetafutiwa ufumbuzi mwingine(rejea miaka ya 1990)

Ukiangalia yote hayo unaona kuwa maamuzi ya haraka, maamuzi ya mtu mmoja na maamuzi ambayo yanamuacha na kigugumizi.
 
Sote tunafahamu huwezi kufanikiwa katika jambo lolote kama team imesambaratika,huna imani na team, hutoi mwanya kwa watu na mawazo yao na yale mawazo mazuri kufanyiwa kazi..
Alinda ahsante , bandiko lako linahoja nyingi na nzito

Naomba nizipitie moja baada ya nyingine kwa kadri ya muda

Hayo niliyonukuu ni miongoni mwa mifano hai. Tuanze na suala la kusambaratika

Tunakumbuka sakata la Dangote, kila waziri alikuwa na lake la kunena.
Mwisho ikaonekana hakuna aliyefahamu nini hasa tatizo.
Kulikuwa na ukweli wa kutokuwa na 'team work'
Haiwezekani jambo moja lijadiliwe na watu wale wale wa team, kisha wakaeleza tofauti

Kukosa imani:
Tulisikia Waziri mkubwa akiaambiwa pengine hajui kama ni mwenyekiti wa kamati ya Taifa..
Hili maana yake ni kukosa imani na wasaidizi wake. Orodha ya kukosa imani ni ndefu

Kutoa mwanya: Hapa kuna mifano mingi hai.
Kwanza, tunasikia mawaziri na makatibu wakuu wakifanyia kazi maagizo.
Hiyo maana yake hawana nafasi ya kutoa mawazo yao.

Mwisho wa siku kuna kuboronga kwasababu wamebeba dhamana wasio na ufahamu nayo au wasioshirikishwa katika kuiratibu

Mawazo mazuri:
Waziri wa sheria alisema ndoa lazima iambatane na cheti cha kuzaliwa.Hili jambo jema na sahihi Duniani ndivyo wanavyofanya ili ku consolidate information za watu na kuweza kujua wananchi.

Ni wazo lililolenga kusaidia kizazi kipya kuondokana na matatizo tunayoyaona leo ya ID

Kwa wenzetu huko duniani, mtoto haandikishwi shule hadi awe na cheti cha kazualiwa
Cheti kitakuwa reference popote katika maisha kikipatikana kwa urahisi alikoanzia shule

Mtoto huyo akijitambulisha kama Bushiri wakati cheti cha shule ya awali ni Bashile lipo jambo.
Atahitajika kuthibitisha lini alibadilika kutoka Bushiri hadi Bashile na kwa ushahidi gani

Mabadiliko mengine yataambatana na taarifa za cheti. Hivyo, unaweza kutaja shule ya chekechea uliyoanza nayo, watu wakapata information kuhusu wewe ni nani hadi wakati wanatafuta habari

Cheti cha kuzaliwa hakiepukiki duniani. Tunajua kwa 'ujima' wa nchi yetu si kila mtu anacho
Hata hivyo dunia ya Tanzania inabadilika, wazazi wanaelewe umuhimu leo hii

Hili halina maana waliokosa vyeti visingeoa, kungelikuwa na mbadala wakati kiazai kinabadilika
Hata baada ya uhuru 1961, vyeti vya wakoloni vya maliwali na matarishi vilikubaliwa

Serikali ilitambua baada ya muda vyeti vitafutika kutokana na kizazi kufutika
Hakuna aliyesema cheti cha mkoloni ni haramu, wala aliyezuiliwa kuoa wakati huo!

Haja ya wakati tunapoelekea katika national ID, cheti cha kuzaliwa ni sehemu muhimu
Wazo la cheti lilikuwa zuri sana na bado ni zuri sana kwa wana ndoa

Kama Taifa tulilozungukwa na nchi 8 tunawezaje kuwa na information za kutosha za wananchi wetu endapo hatufanyi jitihada za 'ku conslidate' information za mtu au familia?

Tunawezaje kupanga mipango ya maendeleo ikiwa hatujui status za watu kwa wakati?
Tunawezaje kudhibiti uhamiaji haramu na vyeti feki kama hatuna information za kutosha?

Kilichotokea, asubuhi i mheshimiwa Rais akakanusha tangazo la waziri wake. Hapa kuna haya
1. Alikosa imani kwamba anaweza kusimamia zoezi hilo vema
2. Kulikuwa na kusambaratika kwa maana wazo halikujadilikwa
3. Mh Rais hakutoa nafasi ya mawazo mapya na hapo hapo kujenga hofu miongoni mwa wasaidizi

Inaendelea
 
Mh. Rais ni mtu anayependa nchi yake, anayependa watu wake, mwenye uchungu na masikini wa nchi yake, anayependa kuona Tanzania inapiga hatua ya kwenda mbele lakini tatizo hafahamu la kufanya matokeo yake ameanza kukimbizana na wapinzani na wapinzani wameisha msoma
Tangu mwanzo kulikuwa na dalili zikishiaria matatizo

Kuzuia bunge ni hatua ya kwanza ya kuminya uhuru wa habari na kudhibiti wapinzani
Hili ni kosa, suala si kudhibiti wapinzani bali kujiuliza kwanini wa chama tawala hawavumi?
Ni kosa, bila kusikiliza upande wa pili, utapataje ukweli na utapata wapi maarifa na njia?

CCM inayosema inajisafisha kwa hakika imejifunza mengi kutoka upinzani.
Vita ya rushwa na ufisadi, kupotea nidhamu ni agenda za wapinzani kwa miaka nenda
Rais alipopata fursa aliitumia vema na kumjengea umaarufu, kwanini sasa inakuwa mwiba?

CCM kutimua wanachama ni template ya wapinzani. Kila walipojisafisha CCM walisema wana mfumo imara hakuna kutimuana. Je, mfumo imara umetowekea wapi?

Kosa la kuzuia mikutano ya siasa ilikuwa kuziba sauti za wapinzani.
Ikiwa CCM hawana sauti, wapinzani wakipigwa marufuku, inasaidiaje CCM na Taifa?

Imekwenda ambapo serikali inakimbizana si wapinzani kama kundi bali wapinzani kama watu

Kesi ya dhamana ya mbunge imepoteza muda mrefu na rasilimali nyingi bila maana yoyote
Imejenga sympathy kwa wapinzani bila gharama na imeonyesha chuki bila sababu

Rais anapochaguliwa ni kiongozi wa wote, anawajibika kusikiliza awapendao na asiowapenda kwani wapo ndani ya tenga moja la Taifa. Hakuna mafanikio kama Taifa linagawanyika

Mafanikio yanapatikana penye kuungwa mkono, hilo kwa sasa halionekani kama lipo

Ukitazama kwa mboni, umaarufu wa wapinzani unaongezeka bila mikutano ya bunge
Si kwamba wana sera, in fact wamepwaya.Kinachowapa umaarufu ni mbadala.
Mbadala wa chuki ni upendo, na hilo ndilo wananchi wanaliona

Bila kujali tunaipenda nchi kiasi gani, taifa kiasi gani, maendeleo kiasi gani au tunachukia umasikini kiasi gani kuna jambo moja tunalopaswa kulipenda kwanza, Utaifa.

Utaifa haujengwi na mkusanyiko wa watu, bali vile vinavyowaunganisha yaani values
Thamani zetu ni upendo, kuheshimiana, kuheshimu taratibu, kupingana bila kupigana, kujadiliana , kukubali, au kukubaliana kutokubaliana, utawala wa haki na sheria na upendo

Taifa lililogawanyika, lenye manung'uniko, na hata watu kuaswa kutosalimina, hatuwezi kufanikiwa hata kama tuna sera nzuri gani, tumejitoa kiasi gani na tunajituma kiasi gani

Mafanikio ya Mwalimu Nyererer hayakuwa eneo jingine isipokuwa moja, kujenga Utaifa
Utaifa na upendo umetusaidia kuvuka mitihani tukiwa Taifa changa na siku za karibuni

Swali la kujiliza, hivi kweli tunaenzi thamani zetu kama tulivyoachiwa na Watangulizi?

Hivi kweli tunapenda maendeleo, tunakataa umasikini ikiwa tumekubali kugawanya na chuki?

Tusemezane
 
Mh WAZIRI Mwakyembe(mb)

muombe radhi Nape Nnauye, Waombe radhi Watanzania
Itendee haki taaluma yako, Watendee haki wasomi wenzako

Bandiko 318 nyuma, tulisema kuna namna mawaziri wanafanya mambo walikujua Watz ni Majuha

Kinachosikitisha ni kusema wakijua si kweli bila hofu na kwa kujiamini mbele ya camera

Ni kana kwamba, kuongopa , kudanganya au kulaghai ni jambo la kawaida,ni utamaduni

Tulisema, waziri wa mambo ya ndani anapotaka aliyetoa bastola atafutwe ilifikirisha sana
Waziri alionekana kutuaminisha yule ni 'jambazi' aliyetaka Nape arudi kwenye gari tu

Siku chache baadaye, waziri akaja na kusema ni mtu wa 'taasisi zisizotangazwa'!!!
Bandiko 327 Alinda alihoji kulikoni watu kama waziri Nchemba kupoteza credibility kihivyo?

Bandiko 318 tulihojia mh waziri kushughulikia la Ney wa Mitego kuliko sakata la clouds

Waziri aliulizwa kabla ya hapo, jibu lake likawa rahisi 'hana habari kamili za tukio la cloud'

Leo amejitokeza na kukutana na maswali yale yale ikionyesha uzito wa suala la Ney

1. Waziri akajibu, taarifa ilikuwa ya upande mmoja hawezi kuifikisha kwa bosi
2. Na hana haja ya kuunda kamati kwasababu yeye na wenzake watashughulikia
3. Na mwisho akasema atatafuta habari za upande wa pili ambao haukuhojiwa

Mh Waziri anasema ni mwanasheria,taaluma haimruhusu kushughulikia ripoti ya tume ya Nape

Hebu tuangalie mantiki za hoja za Mh waziri

Inaendelea....
 
Shemu ya II

Mh Nape aliunda tume kuchunguza tukio la Clouds. Kabla ya hapo, alilaani tukio jinsi lilivyotokea

Haja ya tume ni kujiridhisha na ukweli wa pande zote ili kupata haki na ukweli 'natural justice'

Nape alisema wazi, wamesikia hoja za Clouds ilikuwa zamu ya RC kupewa fursa ya kujieleza

Hivyo jukumu la tume lilikuwa kukutana na pande zote mbili kubaini ukweli wa tukio

Tume ilikuwa na wajumbe kutoka idara ya habari maelezo, TCRC na vyombo vya habari binafsi
Ni wazi Nape akiwa serikali aliangalia umuhimu wa pande muhimu kushiriki

Tume iliundwa na waziri,hadi inatoa taarifa hakuna kiongozi aliyeonyesha kutokubaliana

Taarifa ya tume ilieleza kwa kina jinsi ambavyo mkuu wa mkoa aliwakimbia wajumbe

Haiingi akilini kuwa RC hakukanusha taarifa hizo halafu isemewe hakusikiliza ,
Kwamba hakujua anatafutwa na tume, ukweli wa kimazingira hakutaka kuonana na tume

1. Waziri anaposema tume haikusikiliza upande wa pili,anabadilisha taarifa ya RC kawakimbia.

Pili, anaposema tume ilikiri kutomsikiliza RC, ni kupotosha.
Tume ilikiri kutopata taarifa za RC kwa kutopatikana, siyo kutosikiliza upande wa pili

Mh Waziri amebadili kauli za tume ku fit haja yake na si ukweli wa hoja za tume.

2. Mh Waziri anapokataa taarifa ya tume, kwa kauli nyingine amekataa taarifa ya serikali
Kwa hili ana wananga Waziri, mkuu wa habari maelezo na TCRC !!

3. Mh anasema hataunda tume,yeye na wenzake watautafuta upande wa RC
Kwa maana wa clouds umesikilizwa, amekubali taarifa anayosema si balanced

Halafu anatumia ''unbalanced'' story ku balance na yake kutoka kwa RC
Waziri hakubali taarifa, halafu anatumia taarifa hiyo ku balance na upande wa pili!

Tuhuma dhidi ya RC zinapochunguzwa na Waziri ni mbaya zaidi ya tume ya Nape

Waziri Mwakyembe hawezi kuchunguza RC Vs clouds, kama mchunguzi, kisha aendeshe mashtaka na mwisho awe hakimu.

Mh hapo hakuna natural justice kama taaluma yako isemavyo, itendee haki

Ukiwa mteule wa Rais, halafu unamchunguza mteule wa Rais!!! Itendee haki taaluma yako

Kwa mantiki tu, waziri amuombe radhi Nape kwa kuonyesha kazi yake haikuwa na weledi ingawa anaitumia ku balance na taarifa za upande wa pili uliokataa kuhojiwa na si kutofikiwa

Waziri awaombe radhi wasomi, kauli yake inajichanganya, imepotosha na haieleweki
Na mwisho awaombe radhi Watanzania wanaoelewa nini kinaendelea kwa kuwafanya 'majuha'

Safari yetu kutoka Tz ya 'vi-wonder' kwenda ya Viwanda ina mashaka na haisadikiki

Tusemezane
 
BUNGE LA ''EALA''

Uchaguzi wa wabunge wa EALA unaendelea huko Dodoma
Hawa ni wabunge wa nchi wanaokwenda kwa masilahi ya Tanzania

Hawaendi EALA kama wabunge wa CCM au upinzani bali wabunge wa nchi

Uchaguzi unagubikwa na mambo yanayoonyesha Taifa ''lilivyooza'' kwa itikadi

Wagombea wanaangalia kwa jicho la uchama si nchi, kukiwa na mizengwe chama fulani kiwe na wabunge wengi kana kwamba wanawakilisha masilahi ya chama si Taifa

Tunapochagua watu wasio na ufahamu, weledi, wasioweza kujenga hoja , kusimamia au kuzitetea kwa mantiki, tunafeli kama Taifa si chama tawala au upinzani

Utamadumi wa kijinga wa uchama unaliumiza Taifa katika mambo ya msingi

Lini tutaacha uchama na kuweka Taifa mbele? Lini mgawanyiko utaisha nchini?

Ifike mahali tulaani migawanyiko, viongozi waongoze kuunganisha na si kuligawa Taifa.
Hali ilivyo sasa ni mbaya ingawa wapo wanaoamini ina imarika

Wanaoamini ni kwa mpinzani kuchaguliwa nafasi ya utendaji ya serikali.
Hili halitoshi kuunganisha Taifa.

Wapinzani kusakamwa kila uchao si ushahidi wa kuliunganisha Taifa
Bunge kuendeshwa kama mkutano wa chama , si kuliunganisha Taifa

Kama tungetaka kuunganisha Taifa tungeanza na mambo muhimu ya taasisi zetu
Tungeangalia teuzi zetu, tungejadiliana hata kama hatukubaliani

Tungekuwa na lugha ya stara hata tunapohitilifiana.
Tungeacha lugha za ubabe na kukumbatia za suluhu. Huko ndiko kuliunganisha Taifa

Leo uteuzi wa mtu mmoja unadhaniwa ni mwanzo wa kuliunganisha Taifa

Kwanini tusikae kitako na kuangalia miongozo yetu kama katiba tukiwa kama Taifa?

Tutaukataa ukweli, lakini ukweli unatabia moja , hujidhihiri.

Hapa tulipo tumegawanyika vibaya kuliko wakati mwingine wa uhai wa Taifa hili.

Tukiri hilo, halafu tuangalie tunashonaje palipoharibika.

Uchaguzi wa EALA ni kielelezo kizuri cha kuoza na kugawanyika kwa Taifa

Tusemezane
 
@guruvi3, unless HAUTAKI KUTUMIA LUGHA SAHIHI

hii nchi watu ni wabaguzi sana. Huwez kuamini kile alichokisema Nyerere miaka ya nyuma ndo leo tunakiona kuhusu dhambi ya ubaguzi. Hii tunaiona ikitutafuna si tu kwa uchama bali kwenye udini, ukabila na hata jinsia.

kuna mengi sana nimejifunza upinzani hauna maslahi kwasababu ya ubaguzi, hata uchama hauna maslahi kama wewe sio wa kanda fulani na hata ukanda ukanda hauna maslahi kama wewe sio wa mkoa fulani, na hata mkoa hauna maslah kama wewe sio dini fulani, hata hiyo dini haina maslahi kama wewe sio wa dhahabu fulani.

naona wewe unatumia lugha nyepesi sana sana kulielezea hili kwa kuliita "kuliunganisha taifa" mimi naomba nitumie lugha yake halisi kwamba ni "UBAGUZI"
 
EALA

TUTAKUWA WASINDIKIZAJI KILA UCHAO

HATUJIEWELI, TUMELEWA UVYAMA, UTAIFA BAADAYE

Kwa kumbukumbu,miaka michache iliyopita EA ilitaka kuharakisha suala la soko huria
Hii ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha ardhi inakuwa sehemu ya makubaliano

Nchi wanachama walishinikiza Ardhi iwe sehemu ya soko la pamoja
Zilifanya hivyo kwa kujua Tanzania itaathirika na zitafaidika

Nchi zote wanachama zilikuwa pamoja isipokuwa Tanzania peke yake

Rais JK alitumia mabingwa wa hoja akiwemo Prof Kabudi dhidi ya wenzetu
Hatimaye hoja za Tanzania zikasimama wima na suala kufikia ukomo

Lau kama si Wataalam hao wabobezi kujenga hoja, hali ingelikuwa tofauti

Ndani ya EALA wanaoingia wamebobea katika ufaham wa mambo ya dunia
Wamezama katika kuangalia kesho,wameishi jana na wanaijua leo

Uchaguzi wa wabunge kwenda EALA si suala la masihara au utani. Ni jambo serious

Kama tulivyosema hapo nyuma, fikra za uvyama zilitawala badala ya fikra za Utaifa

Kuna mmoja wa wabunge umri unaonyesha hakuwepo 1977 EAC ikivunjika.
Yaani miaka takribani 40 kwake ni mingi, na hili ni jambo la juzi tu

Elimu ya mbunge huyo na wengine zinatia shaka, na wala hawana historia ya kusimama katika kujenga hoja, kutetea au hata ufahamu wa Taifa letu achilia mbali taratibu

Namuangalia mgombea mwingine.
Huyu simwangalii kama mpinzani bali mwananchi aliyewahi kuwa mbunge na waziri.

Mwananchi aliyewahi kuingia baraza la mawaziri na aliyewahi kufanya maamuzi ya nchi
Mwananchi msomi na ana exposure ya kutosha ya masuala ya dunia ya leo

Mgombea huyo anapowekwa katika mizani na baadhi ni dhahiri tuna tatizo kubwa sana
Amepigiwa kura ya hapana kwasababu tu ya kuwa upinzani, si maarifa au weledi wake

Yaani tunapeleka watu kujaza viti na si kusimamia masilahi ya nchi kwa uvyama

Tumefika hapa kwasababu hakuna 'wazee' wa kusem, viongozi wanaosimama kuhesabiwa

Hatuna viongozi wanaoangalia leo na kesho

Tuna makundi ya watu yasiyoangalia nchi bali kuendeleza vinyongo, visasi na hasira

Tunachukua chuki na visasi kwa kuliumiza Taifa. Kesho tunajiuliza ilikuwaje

Hili la EALA ni dalili nzuri ya uelekeo wa nchi. Hatupo sawa, kuna tatizo kubwa sana

Tusemezane
 
SPIKA WA BUNGE LETU!
MATUSI SI HOJA, HOJA NI KUYUMBA KWA BUNGE

Katika uchaguzi wa wabunge wa EALA, tumeshuhudia 'madudu' makubwa ndani ya chombo kinachotunga sheria. Madudu yaliyoambata na udhaifu wa Bunge la leo

Bunge ni mhimili , kiini na mfano wa demokrasia, taratibu na sheria

Yapo malalamiko ya uendeshwaji mbunge wa kuteuliwa na N/Spika anapoongoza

Hali haionekani kutengemaa hata anapokali Spika mwenyewe.

Ukifuatilia mchakato wa EALA hutahitaji kubaini Bunge limepotea njia

Mhimili huu unatakiwa uwe tofauti kwa namna nyingi.

Ndio wenye uwakilishi wa wananchi ukisimamia serikali, ukitunga sheria na ukipitisha mipango inayogusa maisha ya wananchi kwa mamilioni

Mhimili umejiingiza katika kazi za kiutendaji ambazo kimsingi zingefanywa serikalini.
Mchanga wa makontena ni hoja ndani ya Bunge, si suala la Spika kufuatilia bandarini

Mhimili umegubikwa na uchama , hakuna anayesimama kwa masilhi ya Taifa kuanzia wabunge hadi Uongozi unaoelekea ''kuliangausha'' Taifa kimafanikio

Ni kwa utaratibu huo wa kushangaza, bunge limepoteza nguvu na kuwa tawi tu

Hatuoni kwanini Spika alitumia nguvu katika masuala ya kujibizana kisheria, kutoa ufafanuzi na kuongea kiustarabu

Hivi barua inafutwaje kwa kauli?kwanini asitolee ufafanuzi? Kulikuwa na sababu zipi za kumzuia mbunge asisome barua? Je, taratibu zilifuatwa kufuatilia malalamiko husika?

Maswali ni mengi inatosha kusema Bunge limeondoa matumaini ya nchi, Uongozi umefeli

Kwa hali ilivyo, nchi imegawanyika na Bungeni ndipo wananchi hukutana, hali ni mbaya

Bunge limepoteza nguvu za asili, hatuna uhakika na kiwango cha heshima iliyonayo

Katika hali ya kushangaza, matusi yalitamalaki na wahusika watahojiwa.

Yaani kuhoji matusi ni muhimu kuliko matatizo yaliyotokea katika uchaguzi?

Kamati inajadili matusi ambayo ni maneno, si hoja nzito zinazohusu EALA na nchi!

Kamati kwa haki, mujibu na mamlaka iliyo nayo ina uwezo wa kufanya hivyo
Lakini kama Taifa lazima tuwe na busara za kupanga, kuchagua na kutenda

Hatudhani matusi ni tatizo la kitaifa, tatizo la kitaifa ni kushindwa kwa uongozi wa Bunge, na chombo kupoteza ''thamani' zake mbele ya nchi na uso wa dunia

Argubly matusi ni sehemu ya kupoteza thamani na heshima, hata hivyo tujiulize inafikaje mahali wabunge wanakosa uvumilivu? Hapo ndipo pa kuanzia.

Katika majadiliano hatudhani mtu anaweza kupoteza ufahamu na kutoa mitusi tu.
Matusi mara nyingi ni 'silaha' ya mwisho anayoweza kuitumia mtu anapohisi uoenevu

Matusi si busara na hilo halina masamaha, tatizo ni kuelekeza nguvu katika matusi bila kuangalia chanzo kinachoplekea yatokea.

Ukitaza bunge utakubaliana nasi kuwa matusi hayakuwa tatizo, tatizo lilikuwa uongozi.

Uongozi ulishindwa kujibu hoja, haukuweza kusimamia uendeshaji n.k.

Yes watajadili matusi na kutoa adhabu, tatizo halitakwisha
Ni wakati ''wenye busara'' wajadili uongozi wa bunge kama unakidhi haja za nchi

Kwa mwendo huu, tutabaki kulalama tu wenzetu wakipiga hatua.

Wapo tayari ku sacrifice thamani za nchi kutetea masilahi binafsi au vyama vyao
Nchi imefika mahali watu wanaangalia 'matumbo' kwanza Taifa baadaye

Rai yetu ni kwa Mh Spika , ajitazame ajitathmini kama ana uwezo wa
kusimamia Bunge na masilahi ya umma kwa ujumla kwa hali inavyoonekana

Insikitisha sana

Tusemezane
 
SPIKA 'OMBA RADHI KWA KUCHOCHEA MGAWANYIKO'

KAULI ZINATISHA , ZINATISHIA UMOJA WA KITAIFA

Spika Ndugai: CHADEMA wakiendelea kuchezea nafasi za Ubunge EA tutawapa nafasi vyama vingine

Katika hali isiyo ya kawaida tumesikia kauli nzito za kutisha, kusikitisha na zenye lengo la kupanda mbegu za ukabila, udini na kuligawa Taifa vipande vipande

Bandiko la awali tumezungumzia uongozi wa Bunge na jinsi unavyolegalega
Kulega lega si jambo la kutisha kuliko kauli za kuligawa Taifa na kuchochea hisia

Spika anahoji kwanini wagombea wa EALA-Chadema wanatoka mkoa mmoja.
Hee! sheria gani ya nchi inayozuia ugombeaji kwa maeneo ya nchi?

Spika anahoji kwanini hakuna Wanawake. Hee! katika watu 2 unawezaje kupata 1/3?

Spika anahoji, kwanini hakuna watu kutoka znz? Sheria inasemaje?kukiwa na 2?

Kubwa la hatari ni aliposema kwasababu gani wagombea wawe wakristo.

Kwanza, hatujui kigezo gani Spika anatumia kubaini ni Wakristo

Pili, sheria gani ya nchi inasema kuwepo na uwiano wa Wakristo na dini zingine?
Je, kuna mabohara waliochaguliwa na CCM? Kuna Ismailia? Kuna Walokole? Kuna wasioamini? Kuna wapagani? Kuna wanaoamini mizimu?

Spika aonyeshe ni dini zipi na uwiano upi umezingatiwa.
Akisema Waislam, tayari atakuwa amekiuka haki za dini na wananchi wengine

Lini dini zikawa Waislam na Wakristo peke yao?

Kauli za Spika zinaelekeza umma kutafuta 'ukweli' kwa mujibu wa kauli zake

Umma utahoji

1. Ndani ya Bunge kuna uwiano wa mikoa? Kilimanjaro ina wabunge sawa na Simiyu?

2. Ndani ya kamati za Bunge kuna uwiano wa kanda au mikoa na jinsia?

3. Ndani ya mawaziri walioko bungeni, kuna uwiano wa kanda, jinsia, au dini?

4. Katika wakuu wa mikoa, kuna uwiano wa mikoa , makabila au dini?

5. Katika wakuu wa Wilaya na wakurugenzi, kuna uwiano wa kabila, kanda na dini?

Orodha ni ndefu inaendelea

Katika nchi yetu, utamaduni ni kupata viongozi au watumishi kwa uwezo wao bila kuangalia kanda wanazotoka, makabila, au dini zao.

Utamaduni huo upo katika taasisi za umma na binafsi, mashirika na serikali.

Alichokifanya Spika ni ''kuwaelekeza'' wananchi kuanza kuangalia kila jambo kwa jicho la ukabila, ukanda na udini.

Hili ni jambo hatari sana katika jamii yetu, itashangaza kama litaonekana ni la kawaida

Katika hatari kubwa ya kuligawa taifa, Spika ana mawili ya kufanya kunusuru Taifa

1. Ajitokeze na kuomba radhi kwa matamshi yanayohatarishi umoja wa Taifa
2. Ajiuzulu kwa matamshi hayo yanayoshadidia udhaifu wa uongozi wa Bunge

Kwa kila mpenda amani, anayeipenda Tanzania hili si la kukalia kimya

Ni hatari kubwa sana na mbegu mbaya sana inayopandwa , tusiache ichanue

Tusemezane
 
Huyo ni Spika wa Bunge letu, tuliitalo Tukufu, mwanasiasa mwenye uzoefu na msomi mzuri, NA HIVYO NDIVYO ANAVYOTUMIA UHURU WAKE WA KUONGEA,(tena ina jina zuri HAKI YAKE KIKATIBA) Aje wale wenzangu na mimi mtaani tutaongea nini?

Hiyo ni MIHEMKO, ni wachache wenye uwezo wa kutafakari kauli zao kabla ya kuzitoa. Hisia zetu ambazo zimefungwa na chuki binafsi, udini, ukabila, uchama, ukanda, usomi, utajiri, na upuuzi mwingine kama huo, ndizo zinazotawala matendo na matamko yetu, HATUTOFIKA MILELE.

Anaita sasa.
 
Huyo ni Spika wa Bunge letu, tuliitalo Tukufu, mwanasiasa mwenye uzoefu na msomi mzuri, NA HIVYO NDIVYO ANAVYOTUMIA UHURU WAKE WA KUONGEA,(tena ina jina zuri HAKI YAKE KIKATIBA) Aje wale wenzangu na mimi mtaani tutaongea nini?

Hiyo ni MIHEMKO, ni wachache wenye uwezo wa kutafakari kauli zao kabla ya kuzitoa. Hisia zetu ambazo zimefungwa na chuki binafsi, udini, ukabila, uchama, ukanda, usomi, utajiri, na upuuzi mwingine kama huo, ndizo zinazotawala matendo na matamko yetu, HATUTOFIKA MILELE.
Tunapoeleza tatizo wengine hudhani ni jambo rahisi

Hili la Mh Spika kupenyeza 'kauli' zenye mwelekeo wa kuligawa Taifa lina madhara

Nimesoma maoni sehemu fulani nikaanza kutishika.
Katika uzi huu Rais Magufuli aunda kamati ya pili kuchunguza madini yaliyopo kwenye mchanga, kuapishwa kesho kuna majina ya walioteuliwa

Rais ana haki ya kikatiba na kimazingira kuteua watu watakaofanya kazi ya Taifa bila kujali sifa nyingine nje ya zile zenye tija. Ndivyo Mh Rais amefanya

Kauli ya Spika kuwataka Chadema izingatie uwiano akishadidia Ukanda na Udini inaleta maswali kama nilivyoona

Katika uzi huo wa uteuzi, Mh Spika anaweza kumweleza huyo aliyeuliza uwiano ni jinsi gani uwiano wa kanda, dini , na jinsia ulivyokuwa?

Tunasema hayo kwasababu yeye ndiye ameanzisha utaratibu wa kuangalia mambo kwa jicho hilo akiwashauri Chadema kuzingatia ukanda, udini , jinsia na pande za muungano

Mh Spika amepanda mbegu ya hatari, bado ana nafasi ya kulinusuru Taifa

Aombe radhi kuzuia hoja kutumiwa vibaya hata pale masilahi ya Taifa yanapozingitiwa

Siku kauli za Spika zitakapokamata kasi hatakuwa na nafasi ya kuzuia uharibifu utakaotokea na hapo atakuwa katikati ya historia pengine isiyo nzuri.

Kauli za Spika za kuligawa Taifa si njema kwa umoja wa kitaifa

Tunasisitiza, Mh Spika omba radhi ili kufuta kauli zako. Kukaa kimya kutaendeleza kauli zako za kuangalia chaguzi, teuzi n.k. katika jicho lako yaani la ukanda, udini na jinsia

Tunahitaji watu wa kulisaidia Taifa bila kujali wapi wanatoka, wana imani gani n.k.
Tanzania tuoijua ni yetu na hilo tusimame kulilinda kwa pamoja
 
''KUSHAMIRI'' KWA VYUO VIKUU

Katika kipindi cha miaka 10 Taifa limekuwa na vyuo kuliko awamu tatu kwa mfululizo

Katika kipindi hicho idadi ilifikia 50 kwa vile vya umma na binafsi

Kama tulivyoeleza awali, mfumo wa soko huria ulichukuliwa huria katika maeneo nyeti

Awamu ya pili iliyofungua soko huria ilikuwa makini, kama ilivyokuwa awamu ya tatu

Vyuo holela vilishamiri awamu ya 4, na kushindwa kutofauti high school na University

Ubora wa baadhi ya vyuo hasa binafsi ni wa kutilia shaka kila eneo

Tatizo lilianzia wapi?

1. Serikali:
Haikuwa na mipango madhubuti ya elimu kuanzia ngazi za chini.
Kukawa na ongezeko la wanafunzi wanaohitaji elimu ya juu kwavile hakukuwa na maandalizi ya muda mfupi na mrefu. Kilichotokea ni mambo ya zimamoto

Tatizo hii lilitengenezwa na siasa kutawala utaalam.
Kwamba, wanasiasa walichotaka ni idadi ya vyuo na wanafunzi ili kujenga hoja ya maendeleo bila kujali ubora wa elimu na wahitimu wake

2. TCU:
Tume ya vyuo yenye jukumu la kutathmini/kusimamia ubora wa elimu ikawa njia panda

Kwanza, inaongozwa na maamuzi ya wanasiasa, utaalam haukuwa sifa au muhimu tena

Pili, wahadhari wa vyuo vikongwe wakaona huo ni mradi wa kupata part time
Wakasimama kidete dhidi ya tume na serikali ili mradi wao wa 'pembeni' uwe endelevu

Kwa pamoja, wanasiasa na wahadhiri wakapoka nguvu za TCU kusimamia uanzishwaji na ubora wa elimu inayotolewa.

Tukafika mahali ambapo mwanafunzi aliyemaliza chuko kikuu ni mhadhiri katika majengo yaliyopakwa rangi na maua na mti wa bendera nje. Ni chuo kikuu!

3. Mashirika na wafanya biashara wakatumia udhaifu wa serikali na wanataaluma kuanzisha vyuo hata kupanga namna gani wanataka wanafunzi wafaulu biashara iwe endelevu

Hatua za Mh Waziri kufunga vyuo visivyo na sifa ni ya kuungwa mkono
Hatuhitaji lundo la wenye degree zisizo na ubora.

Tunahitaji wahitimu watakaoshindina katika soko la dunia katika mazingira yetu kwa ubora ule ule unaopatikana kwingine.

Tunahitaji vyuo kama centre for excellence na si mkusanyiko wa wanafunzi

Zoezi halifurahiwi na baadhi yakiwemo mashirika , wafanyabiashara na wahadhiri

Ni zoezi la maana kwa muskabali wa taifa letu, inasikitisha waziri akipingwa kwa hili

Je wapi waziri amekosea?

Na nini mbadala wake kwa haya tunayoona ambapo chuo kikuu cha afya hakiwezi kutunza afya za wananchi kwa kutupa 'vitu nyeti' hovyo kama tulivyoona kule Mbezi?

Kwanini chuo kama hicho kiendelee kuwepo? Chuo hicho kinatoa elimu gani?

Inaendelea
Katika mabandiko #262-265 Tumeongelea kushamiri kwa vyuo vikuu

Jana wakifungua mabweni ,Waziri wa elimu na Mh Rais wameongelea wakinyooshea mkono TCU

Kwamba kumekuwa na kulazimisha wanafunzi kujiunga na vyuo vyenye viwango duni

Katika hilo wamesema upo uwezekano wa kuwa na vyuo vikuu 4 vyenye ubora na vinavyokidhi mahitaji

Tunashukuru kwa kuona tatizo tulilolijadili.Tunaunga mkono vyuo vichache bora kuliko bora vyuo

UDSM inaweza kuwa na wanafunzi 100,000+ na vyuo vingine kama SUA na UDOM vikajaza

Hatuna tatizo na vyuo binafsi, tuna tatizo na vyuo hafifu visivyokidhi haja wala matakwa

Hata vyuo vya serikali hafifu navyo vinapaswa kufa kifo cha asili.
Mfano ni chuo kikuu cha Mzumbe ambacho kinyume na matarajio, kasi ya ukuaji inatia shaka

Haikuwepo sababu ya kuwa na chuo kikuu cha Mzumbe. Kulikuwa na sababu za kubadilisha institute hiyo kuwa college kwanza ili ijenge jina na kisha kuwa chuko kikuu kamili.

Ndivyo SUA ilivyoanza na kujitanua taratibu ikipata hadhi

Makosa hayo yamefanywa kwa kufanya Muhimbili kuwa chuo kikuu moja kwa moja.
Muhimbii ingeweza kubaki kuwa college of Health ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (MUCHS)

Kitendo cha kuanzisha MUHAS kimekuwa na athari kama ile ya Mzumbe

Hoja, kuwa wingi wa vyuo si jambo la muhimu, uchache na ubora wa vyuo ni muhimu sana
Na uchache wa vyuo hauathiri udahili kama kuna mipango, ni kupanga na kugawanya tu

Hatua za kuimarisha UDSM ni nzuri,kama chuo mama, kitaleta ushindani kwa vyuo vingine.

Hatua ya kuruhusu wanafunzi kuchagua vyuo ni nzur itaamsha walio lala na kuleta ushindani

SUA ni wakati mtafute rasilimali kama UDSM ili kuimarisha campus zenu za Olmotoni na Mweka
Tazameni maeneo kama chuo cha Mlingano katika research na kwingineko

UDOM kuna infrastructure nzuri, ubora unatia shaka. Tumieni fursa za Capital city kujiimarisha

Bila kufanya hivyo, UDSM inaelekea kuwa tishio nanyi mnaweza kujikuta katika mazingira ya Mzumbe na Muhas. UDSM itakuwa kimbilio na mtabaki nyuma.

Kwa yote, hatua za kuimarisha UDSM ni nzuri sasa ni kuangalia maeneo kama lecture theatre na kufanya eneo hilo liwe na hadhi yake hasa ubora wa wahitimu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma

Tusemezane
 
Katika mabandiko #262-265 Tumeongelea kushamiri kwa vyuo vikuu

Jana wakifungua mabweni ,Waziri wa elimu na Mh Rais wameongelea wakinyooshea mkono TCU

Kwamba kumekuwa na kulazimisha wanafunzi kujiunga na vyuo vyenye viwango duni

Katika hilo wamesema upo uwezekano wa kuwa na vyuo vikuu 4 vyenye ubora na vinavyokidhi mahitaji

Tunashukuru kwa kuona tatizo tulilolijadili.Tunaunga mkono vyuo vichache bora kuliko bora vyuo

UDSM inaweza kuwa na wanafunzi 100,000+ na vyuo vingine kama SUA na UDOM vikajaza

Hatuna tatizo na vyuo binafsi, tuna tatizo na vyuo hafifu visivyokidhi haja wala matakwa

Hata vyuo vya serikali hafifu navyo vinapaswa kufa kifo cha asili.
Mfano ni chuo kikuu cha Mzumbe ambacho kinyume na matarajio, kasi ya ukuaji inatia shaka

Haikuwepo sababu ya kuwa na chuo kikuu cha Mzumbe. Kulikuwa na sababu za kubadilisha institute hiyo kuwa college kwanza ili ijenge jina na kisha kuwa chuko kikuu kamili.

Ndivyo SUA ilivyoanza na kujitanua taratibu ikipata hadhi

Makosa hayo yamefanywa kwa kufanya Muhimbili kuwa chuo kikuu moja kwa moja.
Muhimbii ingeweza kubaki kuwa college of Health ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (MUCHS)

Kitendo cha kuanzisha MUHAS kimekuwa na athari kama ile ya Mzumbe

Hoja, kuwa wingi wa vyuo si jambo la muhimu, uchache na ubora wa vyuo ni muhimu sana
Na uchache wa vyuo hauathiri udahili kama kuna mipango, ni kupanga na kugawanya tu

Hatua za kuimarisha UDSM ni nzuri,kama chuo mama, kitaleta ushindani kwa vyuo vingine.

Hatua ya kuruhusu wanafunzi kuchagua vyuo ni nzur itaamsha walio lala na kuleta ushindani

SUA ni wakati mtafute rasilimali kama UDSM ili kuimarisha campus zenu za Olmotoni na Mweka
Tazameni maeneo kama chuo cha Mlingano katika research na kwingineko

UDOM kuna infrastructure nzuri, ubora unatia shaka. Tumieni fursa za Capital city kujiimarisha

Bila kufanya hivyo, UDSM inaelekea kuwa tishio nanyi mnaweza kujikuta katika mazingira ya Mzumbe na Muhas. UDSM itakuwa kimbilio na mtabaki nyuma.

Kwa yote, hatua za kuimarisha UDSM ni nzuri sasa ni kuangalia maeneo kama lecture theatre na kufanya eneo hilo liwe na hadhi yake hasa ubora wa wahitimu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma

Tusemezane
Mkuu Nguruvi3

Sidhani kama wingi wa vyuo maana yake ni kuwa na vyuo visivyokidhi ubora. Unaweza kuwa na vyuo vingi na vyote vikakidhi ubora au unaweza kuwa na vyuo vichache lakini bado vikawa bogus vilevile.

Kuhusisha mambo haya mawili sidhani kama ni sahihi na kwa namna moja au nyingine ni upotoshwaji.
 
Back
Top Bottom