Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika


Mchambuzi,

Nimeona tunachokosa kuelewana ni kitu kidogo sana na NDIO MAANA UNASHINDWA KUNIELEWA NINAPOSEMA MUUNGANO WA tgk NA zNZ NI BATILI KISHARIA.

Nimebainisha mengi sana lakin ninalotaka kukupa darsa hapa ni kuwa KILA SHARIA INAYOTUNGWA BASI INAKUWA NA KAANUN NA UTARATIBU (PROCEDURE) YAKE.

Kwanza turejee katika The article of the Union between Tanganyika and Zanzibar inasema
(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar
shall remain in force in their respective territories subject to (a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

Na mimi nimebainisha wazi kuwa Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

SASA KISHARIA KWA KUVUNJE HIYO PROCEDURE YA RATIFICATION ndio tunasema wamevunja sharia nzima ya international treaty hivyo KUUFANYA MUUNGANO HUO UWE KINYUME CHA SHARIA HIVYO NI MUUNGANO HARAMU.

Sasa sijui ahali yangu nikueleze kitu gani ili uwelewe maana wewe umeshikiria maneno ya akina Shivji, Marhum Haroub na wengineo hao wote hawana nafasi katika sharia hii. MIMI NINACHOSEMA PROCEDURE HAIKUFATWA na kama unasema imefuatwa tuambie maandishi yapo wapi kama procedure inavyotaka? na ndio maana mpaka BLW wameomba huo mkataba wauridhie mpaka leo wanapigwa chenga achilia mbali kushirikishw kwa mwanasharia mkuu wa Znz katika mchakato mzima wa Muungano.

KIFUPI NASEMA MUUNGANO WENU NI WA MAGUMASHI TU. Waachwe Znz wapumue kwa raha zao kwani wao sio miongoni mwenu.

Nafikiri umenielewa hapo.

cc takashi, Foum Jnr, GHIBUU, nguruvi3, Joka kuu, Mkandara, Bobuk, Gombesugu, Ritz, The Big show,Mohamed said.


 
Kwanza turejee katika The article of the Union between Tanganyika and Zanzibar inasema
(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar
shall remain in force in their respective territories subject to (a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

Na mimi nimebainisha wazi kuwa Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.
SASA KISHARIA KWA KUVUNJE HIYO PROCEDURE YA RATIFICATION ndio tunasema wamevunja sharia nzima ya international treaty hivyo KUUFANYA MUUNGANO HUO UWE KINYUME CHA SHARIA HIVYO NI MUUNGANO HARAMU.

Sasa sijui ahali yangu nikueleze kitu gani ili uwelewe maana wewe umeshikiria maneno ya akina Shivji, Marhum Haroub na wengineo hao wote hawana nafasi katika sharia hii. MIMI NINACHOSEMA PROCEDURE HAIKUFATWA na kama unasema imefuatwa tuambie maandishi yapo wapi kama procedure inavyotaka? na ndio maana mpaka BLW wameomba huo mkataba wauridhie mpaka leo wanapigwa chenga achilia mbali kushirikishw kwa mwanasharia mkuu wa Znz katika mchakato mzima wa Muungano.

KIFUPI NASEMA MUUNGANO WENU NI WA MAGUMASHI TU. Waachwe Znz wapumue kwa raha zao kwani wao sio miongoni mwenu.

Nafikiri umenielewa hapo.

Cc; Nguruvi3, Joka kuu, Mkandara, Bobuk, Gombesugu, Ritz, The Big show,Mohamed said.


 
Barubaru,
Be what it may, hoja yangu ya msingi ni kwamba the legal foundation of the union remains to be the articles of the union (1964) ambazo katiba ya muda 1965 na ya kudumu ya 1977, zote zilikiuka mkataba husika. Hiyo ni moja;

Pili, uhusiano na ushirikiano baina ya watu wa zanzibari na watanganyika haukuanzishwa na mkataba wa muungano 1964 bali ulikuwepo kwa muda mrefu sana na ulilelewa na udugu wa damu, historia, ujirani na maingiliano ya kijamii na kiuchumi (biashara hasa); mwarabu, mreno, mjerumani na mwingereza, wote walijaribu sana kuutingisha lakini uhusiano na ushirikiano huu kamwe haukuvunjika. Sasa unaposema kwamba wazanzibari hawautaki tena uhusiano na ushirikiano huu, ni kwa kigezo hicho tu cha ratification kwa mujibu wa sheria unazojadili? Na wewe katika kundi hilo upo kimaslahi? Pengine mwenzetu ni mwingereza;

Na tatu, kama nilivyoeleza, suala la ratification lipo clouded with controversy lakini unasita kujadili presentation yangu nzima juu ya suala hilo katika bandiko ambalo nilimtaja haroub othman; kwa maana nyingine unakwepa to explore the possibilities za udanganyifu wa Dourado juu ya ratification kwani kufanya hivyo kunaweza ibua mengi juu ya nini kilikuwa ratified bali kufichwa chini ya utawala wa karume uliokuwa na kila aina ya ukiukwaji wa makubaliano from the get go, mfano karume kutangaza kwamba hapatokuwa na uchaguzi wa urais znz kwa miaka 50; kwa kweli the fact kwamba tuna ushahidi wa baraza la mapinduzi kujadili mkataba wa muungano, kwa kigeu geu cha dourado and selective statements za Jumbe, sitoshangaa kwamba ratification ilifanyika hata kama ilikuwa kwa kulazimishana halafu ushahidi ukafichwa kwa malengo ya wahusika katika mazingira ya hali ile ya hewa kisiasa; ni kwa mantiki hii, wanazuoni kama shivji wanasema hakuna ushahidi wa ratification lakini hoja hiii can't be conclusive, na ni hapo narejea kwenye hoja ya prof haroub;

Again, its all about exploring the possibilities given the fact kwamba hoja juu ya kutokuwepo kwa ratification upande wa znz is still inconclusive, and this is what makes the issue very stimulating to those who like to utilize intellect;

All that said and done, pengine ni wewe na wengine wachache ndio mnaukataa mkataba wa muungano vinginevyo walio wengi wanachopinga ni yaliyojiri baada ya nyerere na karume kuweka biki zao mfukoni;

Tafadhali jadili hoja zangu tatu hapo juu moja baada ya nyingine;



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
 
Mkuu wangu tazama sasa, umeanza vizuri kwa kusema utanijibu maswali yangu lakini napokusoma nakuta ni maswali uloyarudisha kwangu na hakuna JIBU hata moja. Hii ndio sababu tunazunnguka pale pale maana mimi nakujibu na ndio maana nimekuomba twende kwa hatua.

Na maajabu ya Mussa unailalamikia serikali ya CCM lakini wakati huo huo unataka tumalize hoja ya Muungano ndani ya serikali ile ile ya CCM chini ya kiongozi JK ambaye unamlaumu vile vile. Sasa CCM na JK wa leo ni tofauti na yule wa miaka 10 ilopita au 50?

Je wewe unajuaje kama CCM kuchagua serikali 2 ni mbinu wanayoitumia ili Katiba hi isipatikane ktk muda ulopangwa kutokana na wapinzani kuchagua serikali 3. Swala lilowapeleka wajumbe Dodoma ni kubadilisha mfumo wa uongozi, kuondoa vyeo walivyojipachika na mamlaka makubwa dhidi ya demokrasia, haki za binadamu zinapuuzwa, mipango ya ukusanyaji kodi na maendeleo, Miiko na maadili (Transparency na accountability) viwe chachu ya viongozi na kadhalika..

Sasa mnapotaka kuunda muungano upya kwa kuizaa Tanganyia hamuoni kama mnafanya exactly what CCM have planned? nyie mnafikiri mnawatoa jasho lakini ukweli ni kwamba inawezekana kabisa tukaipata katiba mpya yenye kukidhi mahitaji ya karne hii mbele ya muungano.

Kisha Kero za muungano, nilisha sema wazi hakuna kikao chochote kinachoweza kuzitatua isipokuwa referendum kwa Wazanzibar. Aidha wakubali nafasi waliyopo kama ilivyokubaliwa toka awali ama wajikate.

Kura ya maoni ya wananchi wake ndio suluhisho pekee ama mamlaka yaloongezwa kinyemela kama kweli yapo yapitiwe upya na kufanyiwa amendment na sii swala lako wewe kusema yanamnufaisha nani ikiwa wao wameitaka OIC tumekataa pasipo faida ya upande wowote. Bandari leo mizigo mingi inakwenda Zanzibar kuliko Dar, Utalii leo Zanzibar wanaongoza, huwezi kupima maswala kwa kufikiri tu.

Utunzi wa katiba ulokadiliwa kuwa kazi ya miaka miwili mnaifanya kuwa kazi ya miaka 10 kweli akili hii. Kwa kuanza na Muungano nawahakikishia Katiba Mpya haitapatikana na CCM wataendeleo kutawala kwa mabavu na kuwanyanyasa wananchi wa pande zote mbili pasipo huruma.
 
Mkuu Mkandara,
Kuna hoja muhinu uayoijadili kuhusiana na muungano ambayo unaiwasilisha in the spirit of panafricanism; ningependa kujadili kidogo juu ya hilo;

Muungano wa Tanganyika na znz ulizaliwa katikati ya wingu la mjadala wa panafricanism na lile la cold war politics; miaka 50 baadae, ukiumgeuza geuza mtoto huyu (muungano) kujaribu tafuta birthmarks zake, utagundua kwamba mtoto huyu anabeba birth marks za cold war kuliko za panafricanism;

Kama ulivyojadili, muungano huu ni mfano pekee uliopo wa muungano wa mataifa huru baada ya ukoloni, lakini tukitilia maanani kwamba muungano huu ni "political association" kuliko kit chochote huku uchumi ukitumikia siasa za muungano kwa gharama yoyote ile;

Muungano huu unajadiliwa chini ya makundi mawili ya hoja: kwanza ni lile citing it as an examplar of panafricanist unity, na kundi la pili liajadili jinsi gani muungano huu ni mfano wa failure of panafricanist unity; wewe kwa gharama zote upo on the former group, mimi I should declare kwamba nipo on the later group;

Kuna literature nyingi sana juu ya muungano wetu lakini hadi sasa hakuna any serious studies zinazojadili muungano from a panafricanist standpoint; pamoja na mapungufu haya, bado muungano wetu unatoa many valuable lessons (both positive and negative) juu ya panafricanism na african unity kwa ujumla wake;

Mkuu mkandara, panafricanism kama unavyoelewa ilikuwa ni a continental project, lakini muhimu zaidi, ilikuwa ni "a major political vision" with almost zero economic design; ni muhimu kuwekana sawa katika hili ili baadae tuweze rejea kwenye hoja yako juu ya znz kuwa mfano pekee wa panafricanism barani africa na kuwa in a better position kufikia hitimisho on whether muungano baina ya Tanganyika na znz should be cited as a success or failure of the so called panafricanism project;

uzuri ni kwamba tunae nyerere kama mmoja wa the biggest proponents of panafricanism, yeye akiwa muumini wa incremental unity (block by block), huku nkrumah akiwa ni muumini wa radical unity (africa moja, serikali moja mara moja); tukumbuke kwamba mwanzoni miaka ya sitini, vision ya karume ilionekana ni ya maana zaidi huku ile ya nyerere ikionekana haifai, lakini haikuchukua muda mref kabla ya tables to turn na kumweka nyerere kama ndiye a greater visionary wa africa; kwa mfano, alisimamia sana hoja kwamba lazima kwanza bara lote liwe huru kabla ya kufikiria kuungana, na pia lazima muungano uanze kwa awamu kupitia blocks mbalimbali kisha hizi blocks baadae zikiwa tayari zije ungana;leo hii, haya ndio yanatekelezwa, huku ya nkrumah yakibakia tu kama inspiring words;

Kama nilivyojadili awali, muungano wetu ulikuwa ni wa kisiasa zaidi wenye panafricanism vision ambao ililenga to bring about baadae - african citizeship, not kenyan, or tanganyikan or zanzibar citizenship; muungano huu (kama ilivyokuwa vision ya panafricanism) haikuweka misingi ya kiuchumi kama nguzo kuliko ya kisiasa, hivyo hata uchumi ulipangwa kutumikia siasa; Nyerere aliwahi nukuliwa akisema kwamba:

Unity will not make us automatically rich but it can make it difficult for africa and the africa peoples to be disregarded and humiliated

Ni kwa misingi hii, tunaelewa kwanini nyerere sacrificed our resources kukomboa kusini mwa africa lakini pia kuleta serikali mbili kwa faida ya zanzibar kuliko Tanganyika;

Panafricanist pjct ilikuwa ni liberatory, anti imperialist and democratic; kwa sasa nimalizie kwa maswali kwako mkuu mkandara:

1.Katika zama hizi za utandawazi, je, panafricanism inaendeshwa na what kind of ideological drive and political practice? (Using our union as a case study);

2. Given that panafricanist pjct was liberatory anti imperialist and democratic, je muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar unaendeshwa kwa misingi hii? In other words, where is the panafricanism spirit in Tanganyika and Zanzibar?



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Swala la serikali 3 halikuibuliwa na wasomi bali jeuri ya wahaini. Jumbe alikuwa mhaini na ndio maana aliswekwa ndani na wapo walomfuata, akafuatia Maalim Seif hivyo wasomi walikuwa tu wakijadili hoja ya hawa viongozi. An issue on the table kama tunavyojadili leo kutokana na jeuri ya kina Jussa na Uamasho haimaanishi sisi tumeibua hoja ya Muungano. Tume zote zilizoundwa hazikuwa ktk kujadili swala la serikali 3 bali kero za muungano ambazo hazikupatiwa ufumbuzi kutokana na roho zetu ya kimaskini. Sikushangaa na sintoshangaa kwamba swala la kero litaendelea kuwepo kwa sababu ya Umaskini wetu kila mtu anataka upishi ktk kipande cha keki na hili lipo hata huku Canada ambako matatizo tulokuwa nayo na Zanzibar hayatofatiani na ya hapa kutokana na Quebec.

Lakini tofauti ni kwamba Canada wamejaribu sana kuwasilikiza Quebec na kuziondoa kero ambazo haziwezi kuathiri muungano wao wakipewa. kaitka hayo walifanikiwa baadhi na ikawagharimu mengineyo, msemo wa JK usipotaka kuliwa hata kidogo hutakula!
Na kwa bahati nzuri walipozidiwa na kero hizi maana zilikuwa zikiongezeka tu walifanya referendum, viongozi wa pande zote mbili ambao wanaunga mkono Muungano na wale wanaopinga Muungano wakapewa nafasi ya kueleza Faida za upande wao na hasara za upande wa pili. Wananchi wa Quebec wakaiona picha kamili ya mazuri na mabaya na wakachagua kubakia ktk Muungano. Hivyo haikuwa mwisho wa kero lakini waliweza ku solve jambo moja muhimu sana na sii kupitia katiba wala vikao.

Kama wajumbe wanavyosema wazi, wao pale Dodoma sio wawakilishi wa WANANCHI, na swala hili la muungano ni la WANANCHI kwa maana ya kwamba wenye dhamana ya NCHI ni WANANCHI na wenye dhamana ya TAIFA ni RAIA. Hivyo basi hakuna msomi wala mwanasiasa yeyote anayeweza ama kuruhusiwa kujadili swala la nchi husika ktk Muungano pasipo ridhaa ya wananchi (referendum) ama uwakilishi wao (bunge lao) na njia pekee ya kupata jibu ni referendum maana Tanganyika haina bunge wala serikali kuwawakilisha.

Nimesema na nitarudia kusema kwamba maadam kuna serikali kuu ile ya 3, swala la OIC haliwezi kupata ufumbuzi ikiwa limeshindikana krk serikali 2 maana zanzibar waliitaka OIC kwa ajili yao yaani mambo yasiyokuwa ktk Muungano. Ushirika huo ukaleta mgawanyiko mkubwa japo Tanzania ni member wa Red Cross, YMCA, Aghakhan na kadhalika. Hivyo kama tumekataa leo OIC kwa WaZanzibar itawezekana vipi kesho tukubali(serikali kuu ya CCM) ikiwa viongozi ni wale wale walokataa mwanzo. Hivyo kero hiyo itakuwepo hata tukiwa na serikali 3, hatukutazama kero zao ila sasa tunatazama kero ya Wadanganyika na kuitaka Tanganyika.

Kifupi utaona jinsi bara tunavyotawala mijadala, kero za Wazanzibar hazikuwahi kufikia hatua hii lakini toka wao kuandika katiba mpya kinyume cha sheria tumechukua hatua kubwa zaidi na haraka zaidi kuuvunja muungano maana ujio wa Tanganyika ni kinyume cha sheria vile vile. Na sisi wengine hatutaki wala sipendi kuitwa Mtanganyika bali Mtanzania na naipenda Tanzania yangu. Utanganyika kaeni nao nyie, kesho mtafikia Uchagga na Usukuma kwa sababu tu ya kugawana umaskini.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

Naingia hatua ya pili kuhusu Pan africanism. Ikumbukwe tu kwamba hao viongozi wetu walikuwa visionary walitazama nguvu ya nchi za Kiafrika kwa jicho la KIUCHUMI hii habari ya ukombozi na kuunganisha tu bara ni hadithi za wanasiasa. Uhuru wa nchi zote za Kiafrika kasoro South Afrika ilikuwa kujikomboa ktk kutawaliwa kiuchumi. Nakumbuka vizur sana hotuba za mwalimu akizungumzia jinsi tunavyoibiwa na kufanywa manamba wakati malighafi zetu ziliibiwa na kuzijenga nchi zao.

Hivyo swala la umoja wa nchi za kiafrika haikuwa kupata umoja wenye nguvu nje ya Kiuchumi kwa sababu Uchumi ndio unatawala ndoto nzima ya Ukoloni na kukoloniwa. kama Tanzania ingekuwa jangwa isokuwa na malighafi mzungu asingepoteza muda wake kuitawala labda ingekuwa tu kambi ya jeshi. Zanzibar kwa kuwa kitovu cha biashara zote mashariki ya Afrika ilitupiwa macho na Mreno, Mwarabu, Mjarumani na Muingereza kwa mida tofauti japo waliwekeana mikataba. Na baadaye ikawa swala la west against East kutawala chumi za nchi za kiafrika na sio ardhi ama watu.

Hivyo hii dhana mpya ilotokana na viongozi wa leo ambao wanataka kutuaminisha kwamba UHuru wetu ilikuwa kumuondoa Mkoloni mtawala ngozi nyeupe na kumweka mtu mweusi mwenye fikra za tabia sawa na mkoloni ni kuipoteza kabisa maana ya UHURU wa mwafrika. Ni hawa hawa walompiga vita Ghadaff aliposema ni wakati muafaka wa kuunganisha Afrika kwa sababu ndiye pekee alobakia toka kundi lile la kina mwalimu maana hawa waloingia wote ni wakoloni weusi. Sikiliza hotuba za Ghadafi utajua kwamba UCHUMI na kupiga vita ukoloni mamboleo ulikuwa swala la juu ya mambo yote ktk Pan Africanism.

Ni Mandela tu aloitakia South Afrika UHURU wa haki za kibinadamu na amepewa sifa za ajabu kuliko kiongozi yeyote Afrika kwa sababu MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO na leo tunawachukia viongozi wote wanaotaka nchi za kiafrika zijitegemee kiuchumi kwa sababu tumerithi athari za Utumwa kutoumiza bongo zetu ila kumtumikia bwana. Hivyo basi sii kweli Pan Africanism haikulenga kujitawala kiuchumi maana kila nchi ilitaifisha mali za wakoloni ama kuwapa uraia wale waliokubali kubakia ili kuziendeleza nchi zao. Kulikuwa na plan ya kujenga reli toka kusini hadi kaskazini ndoto ile imekufa kifo cha nyani kwa sababu ya hawa viongozi wachumia tumbo.
 
Last edited by a moderator:
Barubaru,
Be what it may, hoja yangu ya msingi ni kwamba the legal foundation of the union remains to be the articles of the union (1964) ambazo katiba ya muda 1965 na ya kudumu ya 1977, zote zilikiuka mkataba husika. Hiyo ni moja;

Hapa naona tupo sawa na kwa kukiuka hizo PROCEDURE ZA INTERNATIONAL TREATY ndiko kunakopelekea kuonekana mfumo mzima wa MUUNGANO WENU KUWA BATILI NA KINYUME CHA SHARIA.


Hapa naomba niongeze nyama kidogo.
Znz ilikuwa na mahisiano na wengi sana kuanzia Mombasa, lamu, pate kilwa mpaka sofala n.k
Na vile vile TGK iikuwa na mahusiano ya kidugu na Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi, Zambia,Zaire, Malawi na kwingineko kama yalivyo kwa Znz. SUALA LANGU HAPA KWANINI NYERERE ALIACHA NCHI ZOTE HIZO NA KWENDA KUJIUNGA NA ZNZ? TENA KWA YEYE KWENDA KUOMBA MUUNGANO? Kumbuka Znz na TGK zipo mbali kimpaka ukilinganisha na Rwanda,
Burundi, kenya au Uganda.

Lakin kubwa sijasema kuwa waZnz hawataki uhusiano wa kidugu na wenzao wa TGK. Kwani
kudai MAMLAKA KAMILI HAKUVUNJI MAHUSIANO BALI KUNAIMARISHA UCHUMI, SIASA NA KUONDOA ILE DHANA YA KUTOAMINIANA NA KUOGOPANA. Na italeta kuhishimiana miongoni mwa raia wa nchi hizo kama ilivyo kwa wakenya, waganda n.k

Mimi nipo katika la kutaka haki itendeke kwa pande zote na kuondoa

malalamiko kwa raia wote wa nchi hizo



Hapa naomba nikupe darsa tena.
Mimi katika huu NIMEARJADILI SHARIA ZA MAHUSIANO YA KIMATAIFA NA NIMEBAINISHA WAZI UKWELI NA BAYANA ZAKE NA NIKAKUONYESHA MAPUNGUFU YAPO WAPI. SIJAMJADILI MTU YOYOTE.

Sasa unapoleta habari za Prof Haroub na wengine nashindwa kukuelewa.KUMBUKA KUWA PROF HAROUB NA SHIVJI sio sheria hao ni wanazuoni tu hawana mamlaka ya kubadilisha sharia zilizotungwa na mamlaka husika.e

Rejea katika The article of the Union between Tanganyika and Zanzibar inasema
(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar
shall remain in force in their respective territories subject to
(a) to any provision made hereafter by a competent legislature;

sasa hata ansard zimefutwa au kuibiwa. Kumbuka mpaka leo BLW wanataka huo mkataba lakin hawajapewa. TUJIULIZE
KUNANI?
je inaingia akilini kweli hiyo?
Tuache ushabiki katika hili kwani huwezi kuficha ulaghai hata siku moja.

Pole sana
NAFIKIRI NIMEKUJIBU. JE UNA ZIADA?
 
Mkuu samahani kidogo naomba unifunue macho. Artucal inasema sheria za Zanzibar na Bara zitaendelea kuwepo ktk maeneo yake Je, ina maana zimekiukwa na kivipi? maana nijuavyo Zanzibar wana (judicial system) mahakama yao na ile ya JMT inawakilisha Watanzania bara. Kumbuka tu ya kwamba Mambo yasiyokuwa ya Muungano yanaihusu Zanzibar pekee huku Bara tumeendelea na sharia ile ile ilokuwepo japo yameongezwa mengi kutokana na haki za binadamu na kadhalika.

Kwa maana hiyo JMT inaweza kuruhusu Ushoga lakini bunge na mahakama na serikali ya Zanzibar wakapinga na ikaendelea kuwa haramu visiwani. Nijuavyo mimi kila linalokubaliwa ktk serikali ya JMT kisheria, sio lazima liwahusu Zanzibar pia. Kama nimekosea nikoshe macho!
 
Barubaru,

Awali nilisema kwamba:

1. Kuna Gaps and inconsistencies katika narratives za Jumbe na Dourado juu ya ratification ya BLM Zanzibar.

2. Kuna uwezekano mkubwa kwamba Dourado alidanganya in his seminal paper kwama Tanganyika Legal society 1983 kwamba znz BLM halikufanya ratification, lakini miaka kumi baadae akiwa mjumbe wa tume ya nyalali akaunga mkono hoja ya tume kwamba ratification ilifanyika.nilikuwekea nukuu ya haroub othman juu ya hilo lakini katika spinning strategies zako, ukaanza kumfananisha dourado na othman wakati suala la msingi hapa ni ushahidi kwamba dourado aligeuza maneno yake ya 1983 mwaka 1992. Hata kama ni mwanafunzi wa darasa la saba ndio kaleta ushahidi huu badala ya haroub othman, hoja inasimama pale pale.

3. Pia nilijadili hoja ya shivji kwamba ushahidi wa kutofanyika ratification znz bado ni inconclusive.

Hadi sasa haujajibu hoja zangu hapo juu kikamilifu, sana sana umekazia kwenye ushahidi wa ratification ya BLM znz. Sasa nimepata CIA intelligence memorandum assessing muungano miaka minne baadae (dated 2nd December 1968) ambayo inaunga mkono hoja zangu za awali ambazo nime summarize hapo juu.

The CIA memorandum inaitwa "The current disarray in zanzibar, 1968 na inasema:

Huu ni ushahidi mwingine kwamba ratification kumbe ilifanyika lakini kwa vile haikufikia 2/3, pengine ndio maana ilifichwa. Kwahiyo mjadala wa ratification tumeumaliza, sana sana labda uje kwenye mjadala wa kura kutotosha, hoja ambayo awali kwako haikuwa na umuhimu kwani ulichosimamia ni kwamba kwanza mkataba haukuwa debated kwenye BLM na pili haukuwa ratified. Nimekupa ushahidi hapa na awali kwamba mkataba ulijadiliwa na pia ratification ilifanyika.

Awali nilijadili kwamba given inconclusive evidence kwamba ratification haikufanywa na BLM, kuna uwezekano ratification happened lakini ikafichwa kwa sababu tusizojua. Kumbe tunaona kupitia CIA kwamba kura hazikutosha hivyo karume akaamua kwa nguvu kwamba 1/3 zinatosha, huku nikizidi sisitiza kwamba hapakuwa na mkono wa Tanganyika katika hili.

Cc JokaKuu, Ritz , Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Pasco


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Mchambuzi, umeelezea vizuri sana labda kuna kitu kimoja kwa watu wengi wenye kudai "ratification haikufanyika" wanashindwa kukikubali au kukielewa. Ratification haikufanywa na Baraza la Wawakilishi kama wengi wanavyotaka. Isingewezekana kufanywa na BLW kwa sababu moja kubwa tu; halikuwepo.

Chombo kilichofanya ratification ni Baraza la Mapinduzi la Zanzibar. Sasa, watu wengi kwa makosa tu wanafikiria kuwa Baraza la Mapinduzi (Revolutionary Council) ni kama Bunge au Baraza la Wawakilishi. Watu wengi hawajui kuwa pamoja na mabadiliko mbalimbali Baraza la Mapinduzi (BLM) na BLW si kitu kile kile.

Sasa, swali linaweza kuulizwa: Je Baraza la Mapinduzi lilikuwa na nguvu ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi wa Zanzibari? Jibu ni lazima useme "ndiyo" kwani ukisema "hapana" utajikuta kuwa maamuzi mengi yaliyofanywa baada ya Mapinduzi na yanakubaliwa na kusherehekewa na WAzanzibari wengi leo hii yalifanywa na BLM na si BLW.

Kitu ambacho wasomi wetu wengi hawajakifanyia kazi ya kutosha ni hili la BLM na nafasi yake katika utawala wa Zanzibar kabla ya mabadiliko ya 1984 na baadaye.
 
Mkuu Barubaru,
Hebu pitia mchango wako huo, na mchango wangu hapa chini nilioutoa kwenye thread ya Mzee Mwanakijiji,Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi ...


Hakuna ubaya ku copy na ku paste mawazo ya memba yoyote, tatizo ni pale mtu unapochukua mawazo ya mtu mwingine, pari materiale (word for word) na kuyaita yako, bila hata attribution or just mention mawazo hayo ni ya nani au just to mention the source kuwa ni thread ya Mzee Mwanakijiji, Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi ...

Japo hili sio lile kosa la jinai la plagiarism, ila hata michango ya jf, ni literacy job, itendee haki jf, watendee haki wana jf!.
Pamoja na concern yangu hapa, hii pia ni such an honour kwangu na kwa jf, kumbe hata michango ya wana jf, inaweza kutumiwa kama "citation" na "authority" kwa wasomi wa vyuo vikuu vya Bara Arab!.

NB. Natanguliza sorry kama just incase mule nyuma ili mention kabla, hii thread nimeikutia page 10!.

Pasco
 
Mkandara,

Ulichoongea ni sawia kabisa ila NILICHOTAKA UJUE KUWA HATA ULE MKATABA WA MUUNGANO ILIBIDI URIDHIWE NA BLM WAKTI ULE ILI UWE SHARIA KULE ZNZ. Sasa kwa vile mpaka leo haujaridhiwa hivyo ni batili kisharia kutumika Znz.

Hivyo Znz wana haki kamili kufanya chochote kile bila kuogopa muungano. na hawapaswi kulipia muungano kwani wao SI MIONGONI MWENU. vile vile

Lakin kumbuka mahakama ya rufaa ni sehemu ya mvungano wenu.








 
Pasco,

Moja ya dhumini la JF ni KUELIMISHANA, KUPASHANA HABARI NA KUBURUDISHANA.

Hivyo nami point hiyo yako ilinielimisha sana kiasi cha kuitumia kama reference katika kadhia hii.

Nikija katika sharia YA HATI MILIKI. KWA MAANDIKO YOTE HUMU MIMI nijuavyo yapo chini ya JF, HIVYO SIKUONA ULAZIMA WA KUMTAJA MTU KWA KUWA NIMETUMIA NDANI YA JF. Ila kama ningetumia nje ya JF labda Zanzinet au kwingine ingekuwa mushkira.

Samahani sana kama nitakuwa
nimekukwaza .

Ijumaa njema .






 

Naona unajichanganya. Suala hapo sio BLM au BLW , SUALA NI MAANDISHI YAPO WAPI? watu wanataka ansard ya kikao hicho na si vinginevyo.

Pole sana

 

Mchambuzi,

naona sasa umeamua kuogelea katika bahari ya tope.

Nani aliyesema kuna mkono wa TANGANYIKA hapo, suala ni UTARATIBU WA ratification haukufatwa hivyo kuvunja

sharia nzima NA KUUFANYA MUUNGANO KUWA BATILI.

Kumbuka kuwa hakuna sharia NUSU.




 
Zpo tetesi kuwa CCM imewaweka kiti moto wawakilishi wake kwenye tume ya katiba, na kuwataka wajitokeze hadharani kukana uhalali wa rasimu, walisema kuwa Warioba alichakachua waliyokusanya kutoka kwa wananchi!
 
nashukuruni wakuu kwa mjadala ulioenda shule, wengine tunapata elimu kubwa sana hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…