Yusuf Himid alikuja kuwa kiongozi wa kwanza wa Nyuki Brigade la jeshi ya Tanzania TPDF na sii kabla. Okello alikuwa kiongozi wao kabla ya Mapinduzi na baada ya Mapinduzi.Mag3,
Labda nikwambie tu siku ya mapinduzi 1964 mimi niliku kijana mdogo na ufahamu wangu nikiwa hata madrasa nimeanza kusoma kwa maalim Bakhathiri shanghani,
Hivyo najua mengi sana ingawa sipendi kuyajadili kwa sasa.
Lakin Okelo enzi zile akijiita Masho hajapata kuwa MBM hata dakika moja pale ZNZ. Kumbuka na ukuu wa majeshi aliteuliwa YUSUF HIMID na msaidizi wake alikuwa SEIF BAKARI.
Tuyaache haya kwani yana machungu ndanimwe.
Nguruvi3,
Kwa miaka 50 hukuidai Tanganyika, na hiyo Zanzibar kama nchi ilikuwepo kwa miaka 50, ni kitu gani kilichowasukuma nyie mdai Tanganyika ilihali mnajua fika kwamba kuna ukweli mkubwa ktk madai ya Wazanzibar, moja ni kuwa Tanganyika imevaa koti la Muungano?. Na sii sababu ya jina la Tanzania bali Tanganyika kutumia Tanzania kama Taifa, tumeomba mikopo na misaada kwa Jina la JMT kwa manufaa ya bara, tena kibaya zaidi misaada hiyo viongozi wameifisadi hivyo leo tuna deni la Taifa kubwa kutokana na sisi. Kwa nini hatulizungumzii hili kwanza halafu taratibu tupande juu hadi tufike kwa kero zetu.
Unajua kuna hadithi moja (ya kweli) ambayo nitakusimulia, Kuna mama mmoja (jina lake kapuni) alirithi nyumba ya vyumba sita Kinondoni. katika maisha akafunga ndoa na mume ambaye baadaye kwa kutumia NDOA na mama huyo, alienda benki na kukopesha fedha nyingi tu na akaweka ile nyumba kama rehani. Baada ya muda mzee wa watu akashindwa kurudisha deni ikabidi benki waje kuikamata nyumba.
Siku walofika wakamkuta yule mama ambaye ndiye haswa mrithi wa nyumba. Wakamwambia kilichotokea na kinachafuata. Yule mama akasema hana taarifa yoyote kuhusu nyumba ile kuwekwa rehani na wala mume sii yake, yeye ndiye haswa mwenye nyumba. . Yamekwenda wee ikaonekana hata yule mama hakuwahi kubadilisha jina la mirathi ya nyumba, yule mzee pia sijui hati ya nyumba aliipata vipi hadi benki ikamkubali.
Yamekwenda wee, ikaonekana kuna mtu aloinunua nyumba ile kupitia Utaifishaji wa Benki na kalipa deni lilokuwa. Kesi mahakamani, imekwenda weee leo miaka sijiui 20 lakini yaonyesha wazi mama yule kisha liwa maana hana uwezo wa kushindana na benki wala huyo mnunuzi. Kifupi wameliwa wote kilichobakia ni lawama ndnai ya nyumba ndoa haishikiki tena. Kuna ile kesi ya Bakwata na maeneo ya Ardhi za waislaam na kadhalika. Ni usanii unaoendelea ambao sii kwa watu binafsi tu nimekuwa hadi Taifa tunapiga magoli ya visigino. Hii ndio hulka yetu, toka watu binafsi hadi viongozi na wapambe, tunafanya makosa lakini hatutaki kukubali makosa ila humrudishia victim kuwa yeye ndiye mwenye makosa tena tunakuwa wakali ajabu.
Hivyo basi kwanza sisi bara tunatakiwa kukubali makosa. Tukubali ni kweli sisi tumelitumia jina la Muungano kuchukua mikopo na misaada inayoiendesha mambo yasokuwa ya muungano. Mfano wa reli ya kati. Kisha baada ya kuyakubali makosa sasa ndio itafutwe njia nyepesi ya kuondoa tatizo hilo.
Hii kutokubali makosa na kuanza kunyoosheana vidole haitatufikisha popote na nina hakika hata hilo bunge la katiba watafika mahala watakwama kutokana na kwamba huko Bungeni kwenyewe Tayari kuna Utanganyika na Uzanzibar hakuna muungano hapo. Hatua hizi zinachukuliwa kutokana na jazba, hasira na karaha mlozidumisha kwa miaka 50.
Lakini ukiingia ndani zaidi utagundua kwamba hizo serikali 3 zinazoombwa mfumo wake ni wa ajabu kabisa. Haiwezekani serikali za nchi ziwe juu ya serikali kuu, ama rais wa Muungano awe ni ceremonial sasa unafikiri kuna muungano hapo kweli. Hakuna Taifa hata moja lenye muungano wake halafu serikali za nchi zipo juu ya serikali kuu. na ndio maana JK akasema mnalikaribisha jeshi kuchukua nchi akijua makosa yalofanyika ktk mapendekezo yenu. Pande mbili zisipokubaliana na kuingia uhasama hili Jeshi litakuwa upande gani? JK ametishia tu kutokana na makosa mnayoyafanya kupendekeza serikali 3 wakati hamjui mamlaka yapi hutengeneza muungano wa nchi
Tukubali kwanza makosa walotupa, tuyatazame na kukubali sii swala la Zanzibar inatutegemea sisi zaidi ya sisi kuwateemea wao. Muungano wetu haukuwa wa kutegemeana ama nani anamtegemea mwenzake. Hii kunyoosheana vidole kusema kweli mimi Kwanzasiiafiki. NI mwanzo wa kiburi cha kutokubali makosa yalokwisha fanyika.
Hata wewe umekosea walokuwa 10, nimewataja hapo juu, sasa wewe nambie kati yao nani hakushiriki?Naona hapo ahali yangu na hiyo source yako imewapuruchuka, MBM wa kwanza kabisa baada mapinduza walikuwa kumi tu na wote wamefariki.
Hao ulio ongeza walikuwa wanaongezeka mpaka leo .lakin wale 10 wa kwanza ninaowajua mimi wakti ule wa mapinduzi walikuwa hawa.
Karume
Edington Kisassi
Hasnu makame
Abdulah aziz twala
Salehe Saadalla
Yusuf Himid
Seif bakari
Said idi bavuai
Said wa shoto
Khamis darwesh.
Tukumbuke historia ya Znz imepotoshwa sana kama yalivyopotoshwa ya Tgk.
samahani umenipoteza hapa kidogo. Unasema Okello anatajwa kama mjumbe wa BLM au BLW.... maana tukumbuke tu ya kwamba Baraza la Mapinduzi la tarehe 13 January 1964 sio baraza lile lile la Mapinduzi baada ya Muungano, kama alivyosema Barubaru kuna watu waliongezwa lakini nachosema miye ni siku ile ya kuweka mkataba wa Artical of Union kina nani walikuwa baraza hilo na ndio walokuwa na dhamana ya kusimama na kusema Ndio ama Hapana.Mkandara,
Kwa bahati mbaya nilikujibu swali lako juu ya full source ya shivji kwenye uzi ambao haukuwa sahihi, uzi wenyewe ni ule wa mtazamo kuhusu hotuba ya JK, bandiko #85 ;niwie radhi, nilipo natumia simu, mambo huwa yanachanganya kidogo;
Nilisema hivi:
Mkandara,
Orodha ya wajumbe 30 wa BLM ni kwa mujibu wa kitabu latest cha issa shivji titled: Panafricanism or Pragmatism: Lessons from the union of Tanganyika and Zanzibar. John Okello sio tu anatajwa kama mjumbe wa BLW as of January 1st 1964, lakini pia mjumbe wa kamati ya watu kumi na nne (the infamous committee of 14); Katika kitabu hiki, shivji alifanya mahojiano ya miaka mingi na wajumbe wa BLW, wanasiasa mbalimbali wa zanzibar na pia anaonyesha nyaraka muhimu sana ambazo hazipo in public.
Cc Mag3
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Wakuu Mkandara na Mchambuzi, binafsi naelewa sana kwa nini Barubaru hapendi kabisa kulisikia jina hilo, Okelo, na kwa kweli vitendo vya kikatili vya Okelo kwa Waarabu na Waasia huko visiwani, viliwaacha wengi midomo wazi. Mathalan, siku ya tarehe Januari 23, 1964 alipotua kisiwani Pemba akitokea Unguja baada ya Mapinduzi, mbona Waarabu walikiona! Ni siku hiyo yaliyotendeka kisiwani Pemba hayawezi kusahauliwa na watu kama Barubaru kwa sababu, kama watoto, walishuhudia unyama uso mfano wakifanyiwa wazazi wao. Huyo ndiye alikuwa Okelo lakini mtu apende asipende, Okelo aliongoza mashambulizi kuwanusuru the down trodden wa visiwa hivi, na kweli chini ya Usultani yalifanyika pia makubwa! Hata hivyo wanachosahau hawa ndugu zetu ni mchango wa Mwalimu (wanayemlaani) katika kuwaondolea Field Marshal John Okelo Zanzibar na hivyo kumwezesha Karume kupumua! Hii ni hadithi nyingine kabisaaa!Yusuf Himid alikuja kuwa kiongozi wa kwanza wa Nyuki Brigade la jeshi ya Tanzania TPDF na sii kabla. Okello alikuwa kiongozi wao kabla ya Mapinduzi na baada ya Mapinduzi.
Hapa ni patamu sana,tena ukizingatia kuwa baraza la mapinduzi halikuwa na nyaraka yoyote. Zanzibar imeandika katiba miaka 20 baadaye.Kama nilivyowasilisha awali, a CIA memo ya mwaka 1964 assessing the 4 years of the union inaeleza kwamba waliopitisha muungano ilikuwa ni only one third of the 30 members of the revolutionary council, which means wajumbe kumi. Swali kwamba ni kina nani, Shivji anatupatia indication ni kina nani wakiongozwa na Karume na Shamte. Kwa maana hii, ratification ya articles ilifanywa kwa idadi ya kura theluthi moja;
swali linalofuata ni je, kanuni ya theluthi mbili anayojadili Barubaru ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria zipi za zanzibar?
Kama ni kwa kanuni za kimataifa anazojadili barubaru, ni sheria zipi wakati mkataba wa muungano ndio ilikuwa ni nyaraka ya kwanza kwa serikali ya zanzibar kutia saini katika kiwango cha kimataifa? These are just mind boggling questions;
Pamoja na umuhimu wa masuala haya for our records, hayana umuhimu sana kuliko kazi iliyo mbele yetu ya kuizindua Tanganyika kwani hivyo ndivyo zanzibar pia itapata mamlaka yake ya kweli.
Ndiyo maana nimemuuliza atupe maandishi ya kuonyesha jinsi Nyerere alivyomzuia Jumbe kuhoji muungano katika mahakama maalumu ya katiba.
Kama hana, anapata wapi ushujaa wa kuomba maandishi kwa wenzake?
Yusuf Himid alikuja kuwa kiongozi wa kwanza wa Nyuki Brigade la jeshi ya Tanzania TPDF na sii kabla. Okello alikuwa kiongozi wao kabla ya Mapinduzi na baada ya Mapinduzi.
Na ndivyo nilivyosema.Angalizo ahali yangu.
Usije sahau kuwa MUUNGANO ULIFANYIKA BAADA YA MAPINDUZI sio kabla mapinduzi. Na Nyuki Brigade iliundwa mara tu baada ya Muungano na baadae ikaja pandishwa darja na kuwa DIVISION YA KUMI (10 Div).
Na ndivyo nilivyosema.
Kabla ya Mapinduzi kiongozi wao alikuwa Okello na sii Himid na hata baada ya Mapinduzi kabla ya Muungano. Okello ndiye aliyeunda serikali yake akidai yeye ndiye kiongozi na akasimamisha bendera yake hadi pale alipofukuzwa nchini. Yusuph Himid alikuja kuwa kiongozi baada ya Mapinduzi na Muungano na sii kabla.
Swali, hivi Okello alishawahi kuwa kiongozi Zanzibar na katika wadhifa gani Hebu tuendelee ha hapo kwanzaNaona sasa umeshachanganya madawa na umeanza kuweweseka.
Kumbuka Mada iliyopo mbele yetu JE OKELO ALIWAHI KUWA MBM?
Lakin ulichoandika ni sawia kabisa alitakiwa Mchambuzi ajue hilo.
kwa kukusaidi zaidi HIMID alikuwa mkuu wa majeshi MARA TU BAADA MUUNGANO na sio baada muungano.
Tuyaache hayo.Pole sana
KUAHIRISHWA KWA BUNGE
Kwa mantiki rahisi, zimetumika siku 30 kukamilisha taratibu za bunge. Kutokana na mijadala mizito ndani ya kamati za CCM, uwezekano wa kuwa na mjadala usio na kikomo kama wa kanuni ni mkubwa.
Ushahidi uliopo ni kamati za CCM(dugu moja) hazielewani, seuse suala likiingia katika pool, hali itakuwaje.
Siku 50 hazitosha, uwezekano wa kuchakachua haraka haraka unaonekana kuwa tatizo ndani ya CCM .
Na uwezekano wa bunge kuvunjika tu kwa wapinzani na wajumbe wengine kuondoka upo mezani pia.
Hayo yatakapotokea zigo atabeba Kikwete na Samwel Sitta.
Ili kuepusha zimetafutwa mbinu za kisingizio cha bunge la bajeti. Huu ni uongo kwasababu taratibu za zilijulikana miaka 2 iliyopita, hakukuwa na tatizo la rasimali . Kisingizio ni kutafuta malango wa kutokea.
Kwanini ni muhimu kwa CCM kuahirisha bunge
1. Ili kupata nafasi ya kutisha wajumbe na kununua baadhi yao.
Wameanza na wasomi , muda wa miezi 3 unatosha kukamilisha kazi ya ununuzi na kutishiana.
2. Kutafuta namna mbadala ya kuondoa vikwazo.
Pandu atatumwa kwenda kufanyia katiba ya znz ya 2010 marekebisho ili kujenga hoja utata umeondoka.
3. Kuepusha balaa la kupatikana kwa hati halisi za mkataba wa muungano.
MAKOSA YA KIKWETE
JK Kujitetea alikuwa na haki ya kumsumanga Warioba kwa maoni yake kumechochea hisia katika jamii.
JK alikuwa na fursa ya kutoa maoni, kwanini hakutoa siku za nyuma?
Na je yeye alikuwa mjumbe wa BMLK hadi ajadili mada za bunge hilo.
JK na Ikulu kuwashambuliwa akina Butiku, Augustino Ramadhani, Warioba na maprofesa kumejenga udadisi 'curiosity' ambao unajenga awareness ya alichosema Warioba. Hadi ya Warioba inaongezeka sana
Kudhani kuwa kukiuka mkataba wa 1964, kura ya maoni n.k. ni kuepusha tatizo, ukweli ni kukaribisha matatizo. JK kakaribisha matatizo makubwa katika jamii kwa kuizuia isiamue utangamano.
Mahusiano ya wznz na Watanganyika ni ya chuki kwasasa,lipo na li wazi
Na mwisho kitendo cha kuteka mjadala wa wananchi na kuwadharau kwa kutumia CCM ni hatari sana na kitaligawa taifa katika mapande mapande JK akishuhudia.
JK afanye nini kuhusu mustakabali wa taifa?
Lazima aheshimu maoni ya wananchi, nayo ni kurjea kwa Tanganyika kwanza halafu muungano ujadiliwe. Kuwatumia watu kudanganya ni sawa na dawa ya maumivu, baada ya muda maumivu hurudi pale pale.
Samwel Sitta anayetumika kama mpini na yeye akiwa ni kipande cha mti ana machaguo mawili
1. Kuahirisha bunge kwa visingizio vya kitoto(bajeti ya serikali)
2. Kusubiri bunge livunjike kwa wapinzani kuwaacha CCM wenyewe
Katika wiki mbili zijazo moja ya mambo hayo yatatokea.
Tusemezane
Tusemezane