Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Mag3,

Labda nikwambie tu siku ya mapinduzi 1964 mimi niliku kijana mdogo na ufahamu wangu nikiwa hata madrasa nimeanza kusoma kwa maalim Bakhathiri shanghani,

Hivyo najua mengi sana ingawa sipendi kuyajadili kwa sasa.

Lakin Okelo enzi zile akijiita Masho hajapata kuwa MBM hata dakika moja pale ZNZ. Kumbuka na ukuu wa majeshi aliteuliwa YUSUF HIMID na msaidizi wake alikuwa SEIF BAKARI.

Tuyaache haya kwani yana machungu ndanimwe.

Yusuf Himid alikuja kuwa kiongozi wa kwanza wa Nyuki Brigade la jeshi ya Tanzania TPDF na sii kabla. Okello alikuwa kiongozi wao kabla ya Mapinduzi na baada ya Mapinduzi.
 
Nguruvi3,
Kwa miaka 50 hukuidai Tanganyika, na hiyo Zanzibar kama nchi ilikuwepo kwa miaka 50, ni kitu gani kilichowasukuma nyie mdai Tanganyika ilihali mnajua fika kwamba kuna ukweli mkubwa ktk madai ya Wazanzibar, moja ni kuwa Tanganyika imevaa koti la Muungano?. Na sii sababu ya jina la Tanzania bali Tanganyika kutumia Tanzania kama Taifa, tumeomba mikopo na misaada kwa Jina la JMT kwa manufaa ya bara, tena kibaya zaidi misaada hiyo viongozi wameifisadi hivyo leo tuna deni la Taifa kubwa kutokana na sisi. Kwa nini hatulizungumzii hili kwanza halafu taratibu tupande juu hadi tufike kwa kero zetu.

Unajua kuna hadithi moja (ya kweli) ambayo nitakusimulia, Kuna mama mmoja (jina lake kapuni) alirithi nyumba ya vyumba sita Kinondoni. katika maisha akafunga ndoa na mume ambaye baadaye kwa kutumia NDOA na mama huyo, alienda benki na kukopesha fedha nyingi tu na akaweka ile nyumba kama rehani. Baada ya muda mzee wa watu akashindwa kurudisha deni ikabidi benki waje kuikamata nyumba.

Siku walofika wakamkuta yule mama ambaye ndiye haswa mrithi wa nyumba. Wakamwambia kilichotokea na kinachafuata. Yule mama akasema hana taarifa yoyote kuhusu nyumba ile kuwekwa rehani na wala mume sii yake, yeye ndiye haswa mwenye nyumba. . Yamekwenda wee ikaonekana hata yule mama hakuwahi kubadilisha jina la mirathi ya nyumba, yule mzee pia sijui hati ya nyumba aliipata vipi hadi benki ikamkubali.

Yamekwenda wee, ikaonekana kuna mtu aloinunua nyumba ile kupitia Utaifishaji wa Benki na kalipa deni lilokuwa. Kesi mahakamani, imekwenda weee leo miaka sijiui 20 lakini yaonyesha wazi mama yule kisha liwa maana hana uwezo wa kushindana na benki wala huyo mnunuzi. Kifupi wameliwa wote kilichobakia ni lawama ndnai ya nyumba ndoa haishikiki tena. Kuna ile kesi ya Bakwata na maeneo ya Ardhi za waislaam na kadhalika. Ni usanii unaoendelea ambao sii kwa watu binafsi tu nimekuwa hadi Taifa tunapiga magoli ya visigino. Hii ndio hulka yetu, toka watu binafsi hadi viongozi na wapambe, tunafanya makosa lakini hatutaki kukubali makosa ila humrudishia victim kuwa yeye ndiye mwenye makosa tena tunakuwa wakali ajabu.

Hivyo basi kwanza sisi bara tunatakiwa kukubali makosa. Tukubali ni kweli sisi tumelitumia jina la Muungano kuchukua mikopo na misaada inayoiendesha mambo yasokuwa ya muungano. Mfano wa reli ya kati. Kisha baada ya kuyakubali makosa sasa ndio itafutwe njia nyepesi ya kuondoa tatizo hilo.

Hii kutokubali makosa na kuanza kunyoosheana vidole haitatufikisha popote na nina hakika hata hilo bunge la katiba watafika mahala watakwama kutokana na kwamba huko Bungeni kwenyewe Tayari kuna Utanganyika na Uzanzibar hakuna muungano hapo. Hatua hizi zinachukuliwa kutokana na jazba, hasira na karaha mlozidumisha kwa miaka 50.

Lakini ukiingia ndani zaidi utagundua kwamba hizo serikali 3 zinazoombwa mfumo wake ni wa ajabu kabisa. Haiwezekani serikali za nchi ziwe juu ya serikali kuu, ama rais wa Muungano awe ni ceremonial sasa unafikiri kuna muungano hapo kweli. Hakuna Taifa hata moja lenye muungano wake halafu serikali za nchi zipo juu ya serikali kuu. na ndio maana JK akasema mnalikaribisha jeshi kuchukua nchi akijua makosa yalofanyika ktk mapendekezo yenu. Pande mbili zisipokubaliana na kuingia uhasama hili Jeshi litakuwa upande gani? JK ametishia tu kutokana na makosa mnayoyafanya kupendekeza serikali 3 wakati hamjui mamlaka yapi hutengeneza muungano wa nchi

Tukubali kwanza makosa walotupa, tuyatazame na kukubali sii swala la Zanzibar inatutegemea sisi zaidi ya sisi kuwateemea wao. Muungano wetu haukuwa wa kutegemeana ama nani anamtegemea mwenzake. Hii kunyoosheana vidole kusema kweli mimi Kwanzasiiafiki. NI mwanzo wa kiburi cha kutokubali makosa yalokwisha fanyika.

Mkuu Mkandara.

Nadhani niseme kwamba wewe umeweka moja na moja sawa sawa asiye na macho hawezi tazama. Ndio maana wengine tunasema huu muungano ulikosewa tangu mwanzo.
 
Naona hapo ahali yangu na hiyo source yako imewapuruchuka, MBM wa kwanza kabisa baada mapinduza walikuwa kumi tu na wote wamefariki.

Hao ulio ongeza walikuwa wanaongezeka mpaka leo .lakin wale 10 wa kwanza ninaowajua mimi wakti ule wa mapinduzi walikuwa hawa.

Karume
Edington Kisassi
Hasnu makame
Abdulah aziz twala
Salehe Saadalla
Yusuf Himid
Seif bakari
Said idi bavuai
Said wa shoto
Khamis darwesh.

Tukumbuke historia ya Znz imepotoshwa sana kama yalivyopotoshwa ya Tgk.

Hata wewe umekosea walokuwa 10, nimewataja hapo juu, sasa wewe nambie kati yao nani hakushiriki?
 
Mkandara,

Kwa bahati mbaya nilikujibu swali lako juu ya full source ya shivji kwenye uzi ambao haukuwa sahihi, uzi wenyewe ni ule wa mtazamo kuhusu hotuba ya JK, bandiko #85 ;niwie radhi, nilipo natumia simu, mambo huwa yanachanganya kidogo;

Nilisema hivi:

Mkandara,

Orodha ya wajumbe 30 wa BLM ni kwa mujibu wa kitabu latest cha issa shivji titled: Panafricanism or Pragmatism: Lessons from the union of Tanganyika and Zanzibar. John Okello sio tu anatajwa kama mjumbe wa BLW as of January 1st 1964, lakini pia mjumbe wa kamati ya watu kumi na nne (the infamous committee of 14); Katika kitabu hiki, shivji alifanya mahojiano ya miaka mingi na wajumbe wa BLW, wanasiasa mbalimbali wa zanzibar na pia anaonyesha nyaraka muhimu sana ambazo hazipo in public.

Cc Mag3

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

samahani umenipoteza hapa kidogo. Unasema Okello anatajwa kama mjumbe wa BLM au BLW.... maana tukumbuke tu ya kwamba Baraza la Mapinduzi la tarehe 13 January 1964 sio baraza lile lile la Mapinduzi baada ya Muungano, kama alivyosema Barubaru kuna watu waliongezwa lakini nachosema miye ni siku ile ya kuweka mkataba wa Artical of Union kina nani walikuwa baraza hilo na ndio walokuwa na dhamana ya kusimama na kusema Ndio ama Hapana.

Na ikumbukwe pia kwamba Okello baada tu ya Mapinduzi alitangaza serikali yake na bendera yake ambayo kama sikosei ilikuwa na njano lakini alipoondolewa bendera ya Zanzibar ikabadilishwa tena na kuwa hii waliyokuwa nayo leo. Hivyo kuna utata kidogo ktk watu kutuhabarisha vizuri ya wakati ule zaidi ya kila mtu anakuja na yake. Na kama ulivyoona Wazanzibar wenyewe hawajui ni kina nani walokuwa BLM kabla ya siku hiyo yaani toka January 13, 1964 hadi April 26, 1964.
 
Nashindwa kuelewa. Mods, nifahamisheni.
Kila nachoandika sasa hivi kinakwenda kurasa za nyuma kumetokea nini?
 
Yusuf Himid alikuja kuwa kiongozi wa kwanza wa Nyuki Brigade la jeshi ya Tanzania TPDF na sii kabla. Okello alikuwa kiongozi wao kabla ya Mapinduzi na baada ya Mapinduzi.
Wakuu Mkandara na Mchambuzi, binafsi naelewa sana kwa nini Barubaru hapendi kabisa kulisikia jina hilo, Okelo, na kwa kweli vitendo vya kikatili vya Okelo kwa Waarabu na Waasia huko visiwani, viliwaacha wengi midomo wazi. Mathalan, siku ya tarehe Januari 23, 1964 alipotua kisiwani Pemba akitokea Unguja baada ya Mapinduzi, mbona Waarabu walikiona! Ni siku hiyo yaliyotendeka kisiwani Pemba hayawezi kusahauliwa na watu kama Barubaru kwa sababu, kama watoto, walishuhudia unyama uso mfano wakifanyiwa wazazi wao. Huyo ndiye alikuwa Okelo lakini mtu apende asipende, Okelo aliongoza mashambulizi kuwanusuru the down trodden wa visiwa hivi, na kweli chini ya Usultani yalifanyika pia makubwa! Hata hivyo wanachosahau hawa ndugu zetu ni mchango wa Mwalimu (wanayemlaani) katika kuwaondolea Field Marshal John Okelo Zanzibar na hivyo kumwezesha Karume kupumua! Hii ni hadithi nyingine kabisaaa!
 
Mkuu Mkandara kwa miaka 50 tumekuwa na imani ipo siku tutakuwa taifa moja.
Kwa yanayotokea haiwezekani tena. Nina maana serikli moja haipo, mbili zimeshindwa kutatua matatizo.Tunadai Tanganyika ili kuleta usawa wakujificha katika koti la muungano.

Nimekuuliza mara zaidi ya 20, tunawezaje kutenga mambo ya muungano na yasiyo ya muungano tukiwa na serikali 2?

Hadi leo huna jibu, na sitarajii jibu kwasababu hakuna jibu hata kama mtu ataamua kujitoa fahamu.

Mkuu, kuhusu misaada hiyo hoja imetumika sana na wznz wa mitaani nashangaa nawe pia unaitumia mkuu wangu.

Nani amekueleza kuwa znz haipati misaada? Mathalan, msaada na mkopo wa kupitisha nyaya za umeme kwenda unguja na hivi karibuni Pemba nani amelipa? Na deni la znz nje ni kiasi gani?

Ile asilimia 4 wanayopata ya pato la taifa ni kiasi gani kiasia kwamba wangeweza kupata misaada zaidi ya hapo?

Bajeti ya znz ni bilioni 700, mapato ni bilioni 240, tofauti inapatikana wapi? I mean bilioni 460.

Mkuu Mknadara, gharama za ulinzi na usalama ni kiasi gani znz inachangia?
Bajeti ya mwaka huu ulinzi na usalama ni trilioni moja.

Kwa mapato ya bilioni 240 ambayo si robo ya bajeti hiyo znz imeachangia kiasi gani?
Lini ulisikia znz wanasema ulinzi na usalama si suala la muungano na unadhani ni sababu gani hasa.

Nikakuuliza wale wabunge wa znz wanaokuja kutalii Dodoma wanalipwa na nani?
ZNZ inachangia nini katika gharama zao? kama ni sehemu ya Tanzania, iweje udhani misaada inapaswa kuwa tofauti na matumizi?

Nikakuambia, wanafunzi wa znz wanaposoma bure bila mikopo kwasababu ya uzanzibar nani analipia gharama hizo?

Kama nao ni sehemu ya Tanzania iweje wao wapewe bure na wa Tanganyika baba yake alipe kodi? Kuna tofauti gani ya misaada na matumizi?
Kwanini udhani wanapaswa kupata misaada na huulizi wanachangia nini au wanapata nini.

Mwaka jana wakapewa bilioni 32 bila kuchangia, hivi hiyo unaiyeweka katika kundi gani.
Orodha ni ndefu

Muhimu ni kuwa ili Tanganyika isivae koti la Tanzania lazima kuwe na mechanism ya kutenganisha mambo ya muungano na yasiyo ya muungano.

Ninakuomba utueleze namna ambavyo serikali 2 unazofikiria ni muafaka zinaweza kufanya hayo.

Narudia tena Mkandara tuonyeshe namna serikali 2 zinaweza kutenga mambo ya muungano na yasiyo ya muungano.

Na mwisho, kama unadhani znz wanaonewa kwanini wanag'ang'ani muungano, mkataba na ujuha mwingine kama huoNini kinawashinda kuondoka Dodoma na znz huru.

Ahsante na nakusikiliza

Last edited by a moderator:
Mkandara,
Wajumbe naojadili ni wa baraza la mapinduzi zanzibar, sio baraza la wawakilishi, na Okello anatajwa na vyanzo vinavyotumika na Shivji; kuna nyaraka ya Shivji inasema hivi:

Legislative Powers Law-The Zanziba Gazette (Gazeti Kuu La Serikali), Vol LXXIII, No.43371,
Registered at G.P.O as a newspaper, 6th February, 1964. General Notice No.111.

LEGAL SUPPLEMENT

The under mentioned legal notice is published in the Legal supplement to his number of the Zanzibar Gazette Extraordinary:-

The Legislative Powers Law, 1964, 3rd February 1964, W. Dourado, Acting Attorney General.

THE LEGISLATIVE POWERS LAW, 1964.

In Exercise of its supreme authority in the people's republic of zanzibar, the revolutionary council in conjunction withe the cabinet of ministries hereby makes the following Laws:-

1. This law may be cited as the legislative powers law, 1964.

2. The power to make law for the government of the people's republic of zanzibar is hereby vested in the president of the republic acting by and with the advice and consent of the revolutionary council.

Signed by the members of the revolutionary council, this 31st Day of January, 1964.

Then inafuatia orodha ya wajumbe wa BLM, na jina la Okello ni la kumi na moja kati ya majina 30, likiandikwa: Field Marshall John Okello.

Nikipata muda nina scan hii document and share it accordingly.
Mag3,
Unachojadili kuhusu okello kimeandikwa na shivji kama ifuatavyo:

"While the government was violently toppled in Unguja, Pemba was calm, utterly unruffled. Jumbe says that he personally knew the government administrators in Pemba. On Sunday evening he rang them and advised them to raise the ASP flag the next day if they wanted to avoid blood shed. ("I was threatening them!", he said). It was only next week that a number of people including Jumbe and Okello went to Pemba. Okello arrested some Arabs and terrorised and humiliated the asians and arab population as a warning. Otherwise Pemba did not participate in the insurrection in any form. At best, the population there was either indifferent or leaderless and lost. Ali Sultan Issa, a Pemban Arab and a Cuban trained Umma cadre was installed as the administrator of pemba.

Kama nilivyowasilisha awali, a CIA memo ya mwaka 1964 assessing the 4 years of the union inaeleza kwamba waliopitisha muungano ilikuwa ni only one third of the 30 members of the revolutionary council, which means wajumbe kumi. Swali kwamba ni kina nani, Shivji anatupatia indication ni kina nani wakiongozwa na Karume na Shamte. Kwa maana hii, ratification ya articles ilifanywa kwa idadi ya kura theluthi moja; swali linalofuata ni je, kanuni ya theluthi mbili anayojadili Barubaru ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria zipi za zanzibar? Kama ni kwa kanuni za kimataifa anazojadili barubaru, ni sheria zipi wakati mkataba wa muungano ndio ilikuwa ni nyaraka ya kwanza kwa serikali ya zanzibar kutia saini katika kiwango cha kimataifa? These are just mind boggling questions;

Pamoja na umuhimu wa masuala haya for our records, hayana umuhimu sana kuliko kazi iliyo mbele yetu ya kuizindua Tanganyika kwani hivyo ndivyo zanzibar pia itapata mamlaka yake ya kweli.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Kama nilivyowasilisha awali, a CIA memo ya mwaka 1964 assessing the 4 years of the union inaeleza kwamba waliopitisha muungano ilikuwa ni only one third of the 30 members of the revolutionary council, which means wajumbe kumi. Swali kwamba ni kina nani, Shivji anatupatia indication ni kina nani wakiongozwa na Karume na Shamte. Kwa maana hii, ratification ya articles ilifanywa kwa idadi ya kura theluthi moja;

swali linalofuata ni je, kanuni ya theluthi mbili anayojadili Barubaru ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria zipi za zanzibar?
Kama ni kwa kanuni za kimataifa anazojadili barubaru, ni sheria zipi wakati mkataba wa muungano ndio ilikuwa ni nyaraka ya kwanza kwa serikali ya zanzibar kutia saini katika kiwango cha kimataifa? These are just mind boggling questions;

Pamoja na umuhimu wa masuala haya for our records, hayana umuhimu sana kuliko kazi iliyo mbele yetu ya kuizindua Tanganyika kwani hivyo ndivyo zanzibar pia itapata mamlaka yake ya kweli.
Hapa ni patamu sana,tena ukizingatia kuwa baraza la mapinduzi halikuwa na nyaraka yoyote. Zanzibar imeandika katiba miaka 20 baadaye.

Suala la theluthi mbili sijui linatoka wapi. Kuna watu wanatumia 51%, kuna sehemu ni simple majority na kwingine ni two third. Nadhani tunapaswa tuonyeshwe nyaraka iliyokuwa na taratibu za upigaji kura.
 
Ndiyo maana nimemuuliza atupe maandishi ya kuonyesha jinsi Nyerere alivyomzuia Jumbe kuhoji muungano katika mahakama maalumu ya katiba.
Kama hana, anapata wapi ushujaa wa kuomba maandishi kwa wenzake?

Nguruvi3,

Inawezekana kipindi hicho 1983/84 Aboud Jumbe kuondolewa madarakani ulikuwa bado mdogo. Lakin kwa kuwa moja ya dhumuni kuu ya JF ni kuilimishana basi nami nitakupa kisa hicho cha Jumbe kuondolewa madarakani kwa faida ya wasomaji wengine wasiolijua hilo.

ilikuwa katika Mdahalo wa mwanzo kabisa juu ya mfumo na muundo wa Muungano ulianza kwa njia ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1983/84. Hapo, kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais Aboud Jumbe, na wale wa Serikali ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Nyerere, walikuwa na mitazamo tofauti inayokinzana juu ya Muungano.

Jumbe na timu yake walitaka Muungano uwe na Serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar (iliyopo sasa) na Serikali ya Muungano yenye kushughulikia mambo ya Muungano tu, ambayo yameainishwa katika Ibara ya 6(a) ya Katiba ya Muungano (Articles of Union) na kifungu cha 8 cha Sheria ya Muungano (Acts of Union) Namba 22 ya 1964, na hatimaye ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.

Jumbe alikwenda mbali zaidi kwa kuandaa Hati ya Maombi ya kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba juu ya muundo sahihi wa Muungano kwa kutumia ibara ya 125 ya Katiba.

Tofauti hizi kati yake na Mwalimu hazikwisha salama kwa Jumbe kuthubutu kukanyaga mahali “patakatifu” bila kuvua viatu. Jumbe alilazimishwa kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi kuanzia Urais wa Zanzibar, Umakamu wa Rais wa Muungano, na nafasi zote za kichama Januari, 1984.

Yusuf Himid alikuja kuwa kiongozi wa kwanza wa Nyuki Brigade la jeshi ya Tanzania TPDF na sii kabla. Okello alikuwa kiongozi wao kabla ya Mapinduzi na baada ya Mapinduzi.

Angalizo ahali yangu.

Usije sahau kuwa MUUNGANO ULIFANYIKA BAADA YA MAPINDUZI sio kabla mapinduzi. Na Nyuki Brigade iliundwa mara tu baada ya Muungano na baadae ikaja pandishwa darja na kuwa DIVISION YA KUMI (10 Div).
 
Na ndivyo nilivyosema.
Kabla ya Mapinduzi kiongozi wao alikuwa Okello na sii Himid na hata baada ya Mapinduzi kabla ya Muungano. Okello ndiye aliyeunda serikali yake akidai yeye ndiye kiongozi na akasimamisha bendera yake hadi pale alipofukuzwa nchini. Yusuph Himid alikuja kuwa kiongozi baada ya Mapinduzi na Muungano na sii kabla.
 
Naona sasa umeshachanganya madawa na umeanza kuweweseka.

Kumbuka Mada iliyopo mbele yetu JE OKELO ALIWAHI KUWA MBM?
Lakin ulichoandika ni sawia kabisa alitakiwa Mchambuzi ajue hilo.

kwa kukusaidi zaidi HIMID alikuwa mkuu wa majeshi MARA TU BAADA MUUNGANO na sio baada muungano.

Tuyaache hayo.

Pole sana
 
Tuyaache hayo.Pole sana
Swali, hivi Okello alishawahi kuwa kiongozi Zanzibar na katika wadhifa gani Hebu tuendelee ha hapo kwanza
 
KIWEWE CHA KUZINDUKA TANGANYIKA KINAITIA WAZIMU CCM
JITIHADA ZA KIKWETE NA AKINA SHIVJI ZINAKWA
ZWA NA KIKWETE MWENYEWE

Wana duru, kile kiwewe cha kuzinduka Tanganyika kilionekana kama hadithi ya kuoendeza. Ukidhani hivyo utakuwa umekosea. Baada ya mbinu za Rais na Samwel Sitta kudhalilisha tume na kura ya siri kufanikiwa, hatua ya mwisho ilikuwa kuunda kamati za CCM katika bunge la katiba ili kukamilisha ngwe.

Jitihada za kuzuia Tanganyika zimetumiwa na wasomi kama Shivji. Shivji amewaambia wznz kuhusu kutekwa kwa utaifa wao. Amezungumzia katiba iliyopo kukosa uhalali na ni muumini wa serikali 3 kwavile ile ya muungano ni Tanganyika imevaa koti la Tanzania.

Ghafla akiwa na makada wa chama Shivji kakana hotuba zake na maandishi yake kwa kutaka serikali 3. Hoja yake iklenga kuwatisha Watanganyika kuwa hawakua na taifa isipokuwa baada ya uhuru. Shivji hakuzungumzia kuhusu Jamhuri ya Pemba na Okello.

Shivji anadai kuwa uwepo wa Tanganyika utachochea hisia. Amesahau kuwa muda mwingi alikuwa znz katika mabaraza akichochea uzanzibar. Hofu yake ni kuwa tayari joto wanalopata wznz kuhusu muungano siku za baadaye watambebesha lawama. Anajaribu kuzuia madhara ya uchochezi wake kwa kuikana Tanganyika. Tanganyika ile ile aliyosema imejificha katika koti la Tanzania kuinyonya Znz.

Shivji ametetea kuvunjwa kwa katiba ya JMT na ile ya znz ya 2010. Ni shivji huyo huyo aliyeandika jinsi katiba iliyopo ilivyokiuka misingi ya uandikaji wa katiba. Usiku mmoja akageuka na kuitetea kuwa ndiyo imewapa wznz uwezo wa kuandika katiba na kuvunja katiba ile ile haramu anayosema

Alichokitetea ni znz na utaifa wake kwa kufumbia macho uvunjwaji wa katiba ya JMT. Amefikai mahali anakwepa ukweli na kusema BLW linasikiliza tu mambo yaliyoamuliwa na JMT.

Tumejaribu kumwelezea Shivji kwasababu tatizo lililopo Dodoma msingi wake upo katika maandishi yake siku nyingi ambalo ni kukiukwa misingi ya mkataba ya 1964 (Legal foundation).

Shivji anasema huo si msingi wa mkataba, msingi ni kugawana madaraka.
Utaona Shivji alivyopoteza uelekeo. Ninamuheshimu ana, kwa hili sikubaliani.
Nina swali moja kwake, je ni bei gani?

Sitta amechomeka rasimu ya CCM ndani ya kamati ili kuvunja nguvu za tume. Kuna taarifa ndani ya kamati 12 kuna kutoafikiana . Ni kamati mbili zenye utata, ile inayoangalia kifungu cha kwanza na Sita kuhusu muundo wa muungano. Kamati hizi ni za CCM chini ya Sitta zikiitwa za bunge maalumu.

Tatizo kubwa linalosababisha CCM washindwe kuafikiana ni kuhusu muundo. Ndani ya kamati kuna uwakilishi wa makundi ya CCM
1. Kuna mapinduzi Daima la znz ambalo halitaki kusikia lolote isipokuwa serikali 2
2. Wapo znz kwanza na huru ambao ni CCM lakini sympathizer wa CUF kiaina

Kimbembe kilichopo ndani ya CCM yenyewe
Inaendelea....

3. Kuna la Wabara ambao limetumwa kutetea serikali 2, nalo limegawanyika
i) Nidhamu ya woga (Hawafikiri ila ndiyo mzee)
ii) CCM masilahi (Wanataka serikali 2 kwa masilahi yao, ndio wenye rasimu)
iii) CCM Asili (Ndio wanaosympathize na Warioba na wanataka wananchi wasikilizwe_

Kimbembe kilichopo sasa hivi

Inaendelea...
 
KIWEWE CHA KUZINDUKA TANGANYIKA KINAITIA WAZIMU CCM
JITIHADA ZA KIKWETE NA AKINA SHIVJI ZINAKWA
ZWA NA KIKWETE MWENYEWE

Wana duru, kile kiwewe cha kuzinduka Tanganyika kilionekana kama hadithi ya kuoendeza. Ukidhani hivyo utakuwa umekosea.

Baada ya mbinu za Rais na Samwel Sitta kudhalilisha tume na kura ya siri kufanikiwa, hatua ya mwisho ilikuwa kuunda kamati za CCM katika bunge la katiba ili kukamilisha ngwe.

Jitihada za kuzuia Tanganyika zimetumiwa na wasomi kama Shivji.
Shivji amewaambia wznz kutekwa kwa utaifa wao. Amezungumzia katiba iliyopo kukosa uhalali na ni muumini wa serikali 3 kwavile ile ya muungano ni Tanganyika imevaa koti la Tanzania.

Ghafla akiwa na makada wa CCM, Shivji kakana hotuba zake na maandishi yake .
Hoja yake ikilenga kuwatisha Watanganyika, hawakua na taifa isipokuwa baada ya uhuru. Shivji hakuzungumzia kuhusu Jamhuri ya Pemba na Okello.

Shivji ametetea kuvunjwa kwa katiba ya JMT na ile ya znz ya 2010. Ni shivji huyo huyo aliyeandika jinsi katiba iliyopo ilivyokiuka misingi ya uandikaji wa katiba. Usiku mmoja akageuka na kuitetea kuwa ndiyo imewapa wznz uwezo wa kuandika katiba na kuvunja katiba ile ile haramu anayosema

Alichokitetea ni znz na utaifa wake kwa kufumbia macho uvunjwaji wa katiba ya JMT. Amefikai mahali anakwepa ukweli na kusema BLW linasikiliza tu mambo yaliyoamuliwa na JMT.

Tumejaribu kumweleza Shivji kwasababu tatizo lililopo Dodoma msingi wake upo katika maandishi ya siku nyingi ambalo ni kukiukwa misingi ya mkataba ya 1964 (Legal foundation).

Shivji anasema huo si msingi wa mkataba, msingi ni kugawana madaraka. Hadi hapo utaona Shivji alivyopoteza uelekeo. Ninamuheshimu sana prof, kwa hili sikubaliani naye. Nina swali moja kwake, ni bei gani?

Sitta amechomeka rasimu ya CCM ndani ya kamati za CCM Dodoma ili kuvunja nguvu za tume ya Warioba. Kuna taarifa ndani ya kamati 12 za CCM za BMLK kuna kutoafikiana . Ni kamati mbili zenye utata, ile inayoangalia kifungu cha kwanza na Sita kuhusu muundo wa muungano.

Tatizo kubwa linalosababisha CCM washindwe kuafikiana ni kuhusu muundo. Ndani ya kamati kuna uwakilishi wa makundi ya CCM
1. Kuna mapinduzi Daima la znz ambalo halitaki kusikia lolote isipokuwa serikali 2
2. Wapo znz kwanza na huru ambao ni CCM lakini sympathizer wa CUF kiaina

Kimbembe kilichopo ndani ya CCM yenyewe
Inaendelea....

3. Kuna la Wabara ambao limetumwa kutetea serikali 2, nalo limegawanyika
i) Nidhamu ya woga (Hawafikiri ila ndiyo mzee)
ii) CCM masilahi (Wanataka serikali 2 kwa masilahi yao, ndio wenye rasimu)
iii) CCM Asili (Ndio wanaosympathize na Warioba na wanataka wananchi wasikilizwe

Makundi yote hayo ni ya CCM angalia mtifuanio uliopo. Hakuna sababu nyingine kubwa isipokuwa makosa matatu makubwa ya Kikwete
1. kuachia katiba ya 2010 ivunjwe
2. Kutoruhusu mjadala wa kitaifa ili kujua tunataka kujenga taifa la namna gani kwanza.
3. Kura ya maoni kuhusu muungano.

Ndani ya kamati za CCM za bunge la taifa kuna tatizo, likifika nje ya bunge litakuwa kubwa pengine kuvuruga kabisa mkakati wa kuziba midomo watu kwa kura ya siri. Mbaya zaidi, hilo litachochea hisia kule znz na Tanzania bara wanaoitaka serikali yao ya Tanganyika.

Mikakati yote iliyotumiwa na Kikwete, CCM na Samwel Sitta huenda ikakwama. Kinachosumbua ni suala la katiba ya 2010, znz ni nchi au si nchi. Pili, uwepo wa Tanganyika kutetea masilahi yake.
Kushindwa kwa mikakati kunaweza kupeleka vurugu kubwa nchini, na mungu pishilia mbali hata watu kupoteza nafsi zao. Hilo hatuwezi kuliondoa mezani.

Ili kuzuia matatizo yanayoonekana wazi, CCM kupitia Sitta inaa andaa mkakati mwingine.
Kuna taarifa ziszo rasmi za kuahirishwa kwa bunge. Lakini kwa mantiki bila taarifa yoyote, bunge ni lazima liahirishwe.

Kwanini bunge liahirishwe?

Endelea hapa chini......

KUAHIRISHWA KWA BUNGE

Kwa mantiki rahisi, zimetumika siku 30 kukamilisha taratibu za bunge. Kutokana na mijadala mizito ndani ya kamati za CCM, uwezekano wa kuwa na mjadala usio na kikomo kama wa kanuni ni mkubwa.
Ushahidi uliopo ni kamati za CCM(dugu moja) hazielewani, seuse suala likiingia katika pool, hali itakuwaje.

Siku 50 hazitosha, uwezekano wa kuchakachua haraka haraka unaonekana kuwa tatizo ndani ya CCM .
Na uwezekano wa bunge kuvunjika tu kwa wapinzani na wajumbe wengine kuondoka upo mezani pia.

Hayo yatakapotokea zigo atabeba Kikwete na Samwel Sitta.
Ili kuepusha zimetafutwa mbinu za kisingizio cha bunge la bajeti. Huu ni uongo kwasababu taratibu za zilijulikana miaka 2 iliyopita, hakukuwa na tatizo la rasimali . Kisingizio ni kutafuta malango wa kutokea.

Kwanini ni muhimu kwa CCM kuahirisha bunge
1. Ili kupata nafasi ya kutisha wajumbe na kununua baadhi yao.
Wameanza na wasomi , muda wa miezi 3 unatosha kukamilisha kazi ya ununuzi na kutishiana.

2. Kutafuta namna mbadala ya kuondoa vikwazo.
Pandu atatumwa kwenda kufanyia katiba ya znz ya 2010 marekebisho ili kujenga hoja utata umeondoka.

3. Kuepusha balaa la kupatikana kwa hati halisi za mkataba wa muungano.

MAKOSA YA KIKWETE

JK Kujitetea alikuwa na haki ya kumsumanga Warioba kwa maoni yake kumechochea hisia katika jamii.
JK alikuwa na fursa ya kutoa maoni, kwanini hakutoa siku za nyuma?
Na je yeye alikuwa mjumbe wa BMLK hadi ajadili mada za bunge hilo.

JK na Ikulu kuwashambuliwa akina Butiku, Augustino Ramadhani, Warioba na maprofesa kumejenga udadisi 'curiosity' ambao unajenga awareness ya alichosema Warioba. Hadi ya Warioba inaongezeka sana

Kudhani kuwa kukiuka mkataba wa 1964, kura ya maoni n.k. ni kuepusha tatizo, ukweli ni kukaribisha matatizo. JK kakaribisha matatizo makubwa katika jamii kwa kuizuia isiamue utangamano.
Mahusiano ya wznz na Watanganyika ni ya chuki kwasasa,lipo na li wazi

Na mwisho kitendo cha kuteka mjadala wa wananchi na kuwadharau kwa kutumia CCM ni hatari sana na kitaligawa taifa katika mapande mapande JK akishuhudia.

JK afanye nini kuhusu mustakabali wa taifa?
Lazima aheshimu maoni ya wananchi, nayo ni kurjea kwa Tanganyika kwanza halafu muungano ujadiliwe. Kuwatumia watu kudanganya ni sawa na dawa ya maumivu, baada ya muda maumivu hurudi pale pale.

Samwel Sitta anayetumika kama mpini na yeye akiwa ni kipande cha mti ana machaguo mawili
1. Kuahirisha bunge kwa visingizio vya kitoto(bajeti ya serikali)
2. Kusubiri bunge livunjike kwa wapinzani kuwaacha CCM wenyewe

Katika wiki mbili zijazo moja ya mambo hayo yatatokea.

Tusemezane

Mkuu samahani lakini nadhani swala la Wapinzania kususia bunge la katiba ni sawa na wao kuzima mshumaa kwenye giza totoro ambalo hawajui njia. CCM watapitisha wanachotaka wao, Wapinzania wajifunze kuchagua vita kwani kama watataka kupigana kila vita basi ni ukweli usipingika watashindwa kwa kila kitu kimawazo na kimatokeo, kama nilivyosema awali, hesabu hazipo upande wowote zaidi ya CCM. Hapa nazungumzia uhalisia na kukimbia kusadikika. Mwisho wa siku kama tungetaka katiba mpya yenye mhimili wa usawa basi tungejikita kwenye kuongeza wabunge bungeni.

Tumeona kwenye swala la kura za wazi au kificho CCM wamekuja na mchezo wao ambao wao wenyewe wanaujua. Na kelele zote zimekwisha. Week ijayo hili la muungano litazikwa na watalimaliza baada ya hapo katiba ndio imekwisha. Mwisho wa siku walipoteza ni Mimi na Wewe na Masikini Million 35. Huo ndio uhalisia wa mambo.
 
Back
Top Bottom