Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Nadhani unajua kuna tofauti kubwa Kati ya tanu na CCM.

CCM ilizaliwa miaka 13 baada ya muungano (1977), kabla ya hapo, kulikuwa na TANU kwa upande wa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar. Hata katiba ya muda ya JMT kwa miaka 13 (kipindi cha 1965-77) ilitamka wazi kwamba - hadi pale tanu itakapoungana na asp, chama pekee cha kisiasa katika jamhuri ya muungano kitakuwa ni TANU.

Hivyo basi ujenzi wa huo utaifa wa Tanzania unaoujadili, ujenzi huu ulikuwa ukiendeshwa na chama cha Tanganyika (Tanu), sio CCM (chama cha muungano). Kwa maana nyingine, haupo sahihi kusema Kwamba ccm ndiyo taasisi iliyotumika kujenga utaifa wa Tanzania, unless hoja ibadilike kuwa kwamba ujenzi wa utaifa wa Tanzania ulianza mwaka 1977, na sio 1964.

Tanu ilizaliwa miaka kumi kabla ya muungano, miaka saba kabla ya uhuru. Na kama umesoma vizuri historia ya nchi yetu, Tanu iliundwa kwa madhumuni ya kuwaunganisha waafrika ndani ya Tanganyika dhidi ya mkoloni, kwa hiyo hii ilikuwa ni hatua ya mwanzo ya ujenzi wa utaifa wa Tanganyika. Tanu ilifanikiwa kujenga utaifa wa Tanganyika over and beyond udini na ukabila, na umoja na utaifa huo ndio uliofanikisha harakati za uhuru chini ya Tanu. MaSwali kwako kufuatia mafanikio ya tanu:

1. Je utaifa wa Tanganyika ulikuwa na mapungufu gani?

2. Utaifa wa tanzania ulilenga watanganyika au watu gani? Kwa maana nyingine, je, mradi wa utaifa wa tanzania ulilenga kuimarisha mapungufu ya utaifa wa tanganyika au kitu kingine?

3. Kwanini leo wale wanaohusishwa na utaifa wa tanzania ni wale wale waliohusishwa na utaifa wa tanganyika?

4. Kati ya mzanzibari na mtanganyika, ni yupi anayefupisha ndoto ya utaifa wa Tanzania ndani ya muungano?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu wangu mbona mnatafuta visa humu kwa kutoa miaka ilihali hakuna mahala nimeitaja hiyo miaka?. Sasa utajenga vipi Utaifa wa Taifa la Tanzania ikiwa hili neno lenyewe Tanzania halikuwepo toka siku ya Muungano wala hiyo Katiba ya nchi (mwongozo) haikutungwa siku ya Muungano? sasa kwa ufahamu wako ndio tuseme hatukuwa na Taifa hadi mwaka 1977? Jamani jaribuni kuelewa mtu anazungumza nini badala ya kutafuta makosa ambayo hayana msingi. Hivi wewe Ukizaliwa mwaka 1972 lakini ukabatizwa mwaka 1980 ina maana hukulelewa ktk mazingira ya Kikristu kwa sababu ulizaliwa kama Mchambuzi na baada ya kubatizwa ukaitwa Joseph? Hii miaka ya nini mkuu wangu ikiwa tunachoongelea hapa ni Utaifa wa nchi hii iitwayo Tanzania.

Utaifa wetu huu umejengwa baada ya mwaka 1967 baada ya katiba ya TANU kutolewa, na haikuwa na msisitizo kiutendaji hadi mwaka 1971 baada ya kupitiswa mwongozo mpya wa TANU ambao ulikuja fuatiwa na Azimio la Arusha mwaka 1977, hivyo hatua kwa hatua ama awamu kwa awamu mikakati ilibuniwa kutokana na hali halisi iwe kwa wananchi wake ama Utaifa wetu. Nia ianweza kuwepo toka mwaka 1961 lakini ujenzi halisi wa Utaifa wetu ulianza haswa baada ya Katiba ya mwaka 1977 ambayo hadi leo ndio tunatoitumia na ndivyo mataifa wanavyotutazama kutokana na malezi ya Katiba hiyo. Yapo marekebisho mengi yamefanyika lakini maadam Mwongozo uliopo leo unatokana na katiba ya mwaka 1977 basi huu ndio UTAIFA tuloujenga hadi leo na kama tuna mapungufu yoyote ya Utaifa wetu basi unatokana na katiba hiyo!

Mimi binafsi nina hakika Nyerere anygeweza kuujenga Utaifa wa Tangantyika tofauti kabisa kama sio muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu naamini Kwa dhati Abdulrahman Babu alikuwa sababu kubwa ya siasa ya Ujamaa (1964 -1976) japo wengi wanaamini kwamba Nyerere alikuwa mjamaa hata kabla ya Uhuru. Tafadhali usianzishe ubishi mwingine maana hii ni imani yangu mimi sii lazima uikubali.

2. Utaifa wa Tanganyika haukuwa na tatizo lolote zaidi ya kwamba kila penye nia kuna malengo. Uhuru wa Tanganyika haukuwa na malengo ya wananchi wa Tanganyika tu, bali ni hatua moja ya UHURU wa nchi zote za Kiafrika kwa lengo la kuunda TAIFA wao. Hivyo unachoweza kusema leo pengine ni kwamba fikra hizo zimepitwa na wakati ama azma hiyo isingewezekana. baada ya kujua kwamba MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO. Lakini huwezi kufikiria ya leo kuyaweka mwaka 1964 ama 1977 wkaati wao waasisi wetu waliweka nia ya kuwa na TAIFA moja wakianza kwa hatua ya nchi jirani (wazo la Nyerere).

Kama lisingekuwepo wazo la kuunda Umoja wa nchi huru za Kiafrika kama jumuiya ya Utaifa wa nchi hizo pengine Tanganyika ingekuwa tofauti lakini haikuwa na hawezi kuwa maaa tayari leo tyuna nchi inayoitwa Tanzania. Kuna hata habari ya kwamba TaNGANYIKA TULIKUWA TAYUARI KUAHIRISHA uHURU WETU IILI SISI NA kENYA NA uGANDA tupate Uhuru siku moja na pengine kuunda TAIFA moja lakni haikuwezekana hivyo mimi na wewe hatuwezi kubashiri Tanganyika huru wlala Utanganyika kwa leo.

3. Hao wanaohusishwa na Utanzania ndio wale wale wa Utanganyika ni kina nani hao maana wauliza swali wakati jibu lake unalo wewe. Hawa watu wanahusishwa kivipi?

4. Anayefupisha ni yule asiyependa kusikia akilaumiwa naye ni sisi Watanganyika. Ni kweli tulimelivaa koti la Muungano, na maneno haya yanatuuma sana japo ni kweli tupu. Waswahili wanasema Ukweli unauma, hivyo badala yetu kukana kulivaa koti ebu turudi nyuma na tufikiri tena wakati huu bunge likiendelea na kukubali kwamba kweli tumelivaa koti la Muungano.

Wee siikiliza kwa makini bunge liitwalo la Muunano, utakuta karibu mambo yote yanayojadiliwa humo ni mambo ya Tanganyika na Mzanzibar akiinuka tu na kuhoji basi atashambuliwa kana kwamba hana mamlaka ya kuzungumza pale. Sasa tujiuklize hao wabunge wa Zanzibar wnaafanya nini pale Bongeni Dodoma ikiwa asilimia 90 kama sio 95 ya mambo yote yanayojadiliwa mule ni ya Tanganyika! Hata vyama vya wapinzani nao vile vile kama hawatakiwi utadhani bunge hilo ni kikao cha wanaCCM na sii bunge la Muungano. Hivyo ni kama tuna serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar, mnachotakiwa kuomba ni serikali ya Muungano ambayo kiuhalisia HAIPO.

Halafu wakiona wameonewa ktk hilo wakaitaka Zanzibar yao tunaanza kusema wao ndio wanataka kuvunja Muungano! haya sii ndio yale ya ndoa ambayo mwanamke ashirikishwe tu kwa mambo ya Jikoni? Bibie akiuliza tu maswala ya kazi au biashara anaambiwa wewe unataka nini, Unalishwa bure, unalala bure kazi yako iko jikoni na kitandani kaa kimyaa!. Kisha huyo mke akiomba talaka basi yeye ndio anayetaka kuivunja ndoa, hii mkuu tumeitoa wapi?

Kwa nini tunaendekeza mila chafu kama hizi ambazo leo hii wap[o baikna yetu wanaopinga kabisa Mwananke kudai haki zake kama mzazi! tena mkitumika lugha nya kwamba Nyerere aliilazimisha ndoa hii pasipo kushauriana na wengine jambo ambalo ni Uongo mkubwa ulotungwa na wale waliokuwa upande wa pili (Hizbu).

Zanzibar wamedai nchi yao kutokana na sisi tunavyo wa abuse, na huwezi kushindana na mwanamke kwa matusi ndio maana tunazidi kuchukia. Wazanzibar mdomo wanao na wanajua sana jinsi ya kutuchokonoa haswa pale panapo
wauma na sasa mnafikia kutaka kuandika hiyo talaka pasipo kujua kwamba tumezaa watoto wengi na ile child support itakula kwetu na sii kwa Zanzibar. Kuna Wzanzibara wengi bara kuliko population yao huko makwao na karibu kila familia Zanzibar ina ndugu zake bara hivyo wao wanaweza kuishi bara lakini sisi hatutaweza..
 
Mkandara;9704281 2. Utaifa wa Tanganyika haukuwa na tatizo lolote zaidi ya kwamba kila penye nia kuna malengo.
Thank you Sir, hivyo hoja ya kwamba wengi wamezaliwa wakiwa katika utaifa wa Tanzania haina mantiki. Pili, wanaodai utaifa wa Tanganyika hawana makosa.
4. Unayefupisha ni yule asiyependa kusikia akilaumiwa naye ni sisi Watanganyika.
Ni kweli tulimelivaa koti la Muungano, na maneno haya yanatuuma sana japo ni kweli.
Waswahili wanasema Ukweli unauma, hivyo badala yetu kukana kulivaa koti ebu turudi nyuma na tufikiri tena wakati huu bunge likiendelea.
Hakuna anayekana, tunasema ili kuweka mambo sawa, tulivue koti la Tanzania na kuzindua Tanganyika.

Tutakuwa na Tanganyika, Zanzibar na Tanzania. Ikifika wakati wa kulihudumia koti kila mmoja atawajibika. Tutakuwa tumevua koti salama salimini
Siikiliza kwa makijni bung la Muunano, utakuta katibu yote yanayojadiliwa humo ni mambo ya Tanganyika na Mzanzibar akiinuka tu na kuhoji basi atashambuliwa kana kwamba hana mamlaka ya kuzungumza pale. sasa tujiuklize hao wabunge wa Zanzibar wnaafanya nini pale Bongeni Dodoma ikiwa asilimia 90 kama sio 95 ya mambo yote yanayojadiliwa mule ni ya Tanganyika!
Ni kweli mzanzibar hana mamlaka ya kuzngumzia jambo la Tanganyika.
Mfano, wazanzibar wameondoa Bandari katika mambo ya muungano, hivi mzanzibar anaongelea bandari ya Tanganyika ili iweje. Ana masilahi gani , yake yapo znz na Tanganyika hatuongelei.
Tunapoongelea afya mzanzibar hana masilahi na afya na ndivyo kwa wizara na idara nyingine.

In fact hawapaswi hata kuwemo mule, hata yale ya muungano kama ulinzi na usalama, wanajadili nini wakati hawana mchango wowote?

Mkuu tunasema wazi uwepo hauna maana zaidi ya kuzua rabsha.
Sikiliza michango yao utagundua tatizo, mfano, Juzi mbunge wa znz kauliza swali kwa werema, hivi wizara ya sheria inamhusu vipi ikiwa wao wana mwanasheria wao na hawamtambui Werema au wizara husika.

Wao pale Dodoma wakusanye posho na kulalala.
Hawana haki na ni haramu kuongelea mambo yanayohusu nchi yetu.
Wana nchi yao serikali yao na utaifa wao
Halafu wakiona wameonewa ktk hilo wakaitaka Zanzibar yao tunaanza kusema wao ndio wanataka kuvunja Muungano!
Mkuu wangu, si tuliongeza mambo yakawa 22 ambayo ni sawa na 47 ili tuongelee mambo kwa pamoja.

Wznz wakasema yameongezwa kinyemela na hawataki.
Wanataka turudi katika 11. Wakaanza hata bila majadilaino kwa kuondoa.
Leo unasema wanaonewa wakati wenyewe wanataka mamlaka kamili.
Hivi hapa mkuu huoni unavyojichanganya.

Wazanzibar wanataka mamlaka kamili, huwezi kuwa na mamlaka kamili ukiwa na mambo luluki ya muungano. Tumejaribu 22 wamekataa sasa unataka warudi kujadili mambo yasiyowahusu.

Hilo halitatokea tena, kama 7 hawakubali, basi njia Nyeupee.
Hatuwezi kuishi na wznz mchango wao ukiwa ulamamishi wa kudai perememnde.

This time tutakomaa nao na ahueni yao ni mambo 7, kama hataki wajiandae kwa mambo 0 na hapo sitaki hata kufikiri nini kitatokea.
Zanzibar wamedai nchi yao kutokana na sisi tunavyo wa abuse, na huwezi kushindana na mwanamke kwa matusi ndio maana tunazidi kuchukia. Wazanzibar mdomo wanao na wanajua sana jinsi ya kutuchokonoa haswa pale panapo
wauma na sasa mnafikia kutaka kuandika hiyo talaka pasipo kujua kwamba tumezaa watoto wengi na ile child support itakula kwetu na sii kwa Zanzibar.

Kuna Wzanzibara wengi bara kuliko population yao huko makwao na karibu kila familia Zanzibar ina ndugu zake bara hivyo wao wanaweza kuishi bara lakini sisi hatutaweza..
Well, sisi hatutaki Tanganyika kwasababu ya mdomo wao, tunataka kwasababu ni muhimu kwa ustawi na maendeleo yetu.

Mdomo wao utawagharimu kwasababu hatarudi nyuma hadi Tanganyika izinduke.
Tanganyika itazinduka ima kwa sheria au kwa njia za asili.
Ninachojua ni kuwa hakuna njia ya kurudi tena miaka 50 ya kutoa peremende na zawadi hovyo.

Hakuna sababu za kupanga mambo yetu wznz waende kudhinisha.
Hatuna sababu za kutumia rasilimali zetu kuwafuta machozi kila wanapotaka peremende.
Mwisho umetimia ni suala la muda.

Kuhusu wznz watakoishi Tanganyika, nakuhakikishia kuwa Tanganyika ndio nchi pekee duniani iliyobeba wznz wengi.

mwaka jana tumetoa uraia mwingine kwa Warundi 162,000 na hao ni registered, unregistered wapo kwa mamia.Wataishi kwa sheria za Tanganyika, watalipa kodi Tanganyika na watahudumia Tanganyika.

Hakuna Mtanganyika anayefikiria kwenda kuishi znz kwasababu hakuna sababu za maana za kufanya hivyo.
Hivyo usitishe watu kwa mara nyingine tena, tunasema watabaki na kuishi kwa sheria za Tanganyika, watafanya kazi na kupia kodi za Tanganyika na hakutakuwa na sababu za kutumia jina la Tanzania kupora rasilimali za Tanganyika.

Mzigo wa gharama hautakuwepo na hakutakuwa na ulalamishi.

Tanganyika ndiyo salama yao, kinyume chake ni suala la muda.
 
Thank you Sir, hivyo hoja ya kwamba wengi wamezaliwa wakiwa katika utaifa wa Tanzania haina mantiki. Pili, wanaodai utaifa wa Tanganyika hawana makosa.Hakuna anayekana, ndio maana tunasema ili kuweza kuweka mambo sawa, tulivue koti la Tanzania na kuzindua Tanganyika. Tutakuwa na Tanganyika, Zanzibar na Tanzania. Hakuna atakayevaa koti hilo peke yake. Ikifika wakati wa kulihudumia kwa kufua na kupiga pasi, kila mmoja atawajibika. Kwa mengine kila mmoja ashike lake. Tutakuwa tumevua koti salama salimini Ni kweli mzanzibar hana mamlaka ya kuzngumzia jambo la Tanganyika. Mfano, wazanzibar wameondoa Bandari katika mambo ya muungano, hivi mzanzibar anaongelea bandari ya Tanganyika ili iweje. Ana masilahi gani kwasababu yake yapo znz na sisi Tanganyika hatuongelei masilahai yao. Tunapoongelea afya mzanzibar anachangia nini maana hana masialhi na afya na ndivyo kwa wizara na idara nyingine.
In fact hawapaswi hata kuwemo mule, hata yale ya muungano kama ulinzi na usalama, wanajadili nini wakati hawana mchango wowote? Mkuu tunasema wazi hata uwepo wao hauna maana zaidi ya kuzua rabsha. Sikiliza michango yao utagundua kuna tatizo, mfano, 'znz ni nchi au si nchi" Hilo ndilo wanaloona limewapeleka Dodoma.
Juzi mbunge wa znz kauliza swali kwa werema, hivi wizara ya sheria inamhusu vipi ikiwa wao wana mwanasheria wao na wizara yao na wala hawamtambui Werema au wizara husika. Wao pale Dodoma wakusanye posho na kulalala. Hawana haki na ni haramu kuongelea mambo yanayohusu nchi yetu. Wana nchi yao serikali yao na utaifa wao Mkuu wangu, si tuliongeza mambo yakawa 22 amabyo ni sawa na 47 ili tuongelee mambo kwa pamoja. Wznz wakasema yameongezwa kinyemela na hawataki. Wanataka turudi katika 11. Wakaanza hata bila majadilaino kwa kuondoa mambo yao. Leo unasema wanaonewa wakati wao wenyewe anataka mamlaka kamili. Hivi hapa mkuu huoni unavyojichanganya.

Wazanzibar wanataka mamlaka kamili, huwezi kuwa na mamlaka kamili ukiwa na mambo luluki ya muungano. Tumejaribu 22 wamekataa sasa unataka warudi kujadili mambo yasiyowahusu. Hilo halitatokea tena, kama 7 hawakubali, basi njia Nyeupee. Haruwezi kuishi na wznz ambao kazi yao kubwa ni kudai vyeo na kuomba omba huku mchango wao ukiwa ulamamishi wa kudai perememnde., This time tutakomaa nao na ahueni yao ni mambo 7, kama hataki wajiandae kwa mambo 0 na hapo sitaki hata kufikiri nini kitatokea. Well, sisi hatutaki Tanganyika kwasababu ya mdomo wao, tunataka kwasababu ni muhimu kwa ustawi na maendeleo yetu.
Huo mdomo wao sasa utawagharimu kwasababu hatarudi nyuma hadi Tanganyika izinduke. Tanganyika itazinduka ima kwa sheria au kwa njia za asili. Ninachojua ni kuwa hakuna njia ya kurudi tena miaka 50 ya kutoa peremende.
Hakuna sababu za kupanga mambo yetu wznz waende kudihdinisha. Hatuna sababu za kutumia rasilimali zetu kuwafuta machozi wznz kila wanapotaka peremende. Mwisho umetimia ni suala la muda.

Kuhusu wznz watakoishi Tanganyika, nakuhakikishia kuwa Tanganyika ndio nchi pekee duniani iliyobeba wznz wengi.
Juzi tumetoa uraia mwingine kwa Warundi 162,000 na hao ni registered, unregistered wapo kwa mamia.
Wataisgi bara kwa sheria za Tanganyika, watalipa kodi Tanganyika na watahudumia Tanganyika.

Hakuna Mtanganyika anayefikiria kwenda kuishi znz kwasababu hakuna sababu za maana za kufanya hivyo.
Hivyo usitishe watu kwa mara nyingine tena, tunasema watabaki na kuishi kwa sheria za Tanganyika, watafanya kazi na kupia kodi za Tanganyika na hakutakuwa na sababu za kutumia jina la Tanzania kupora rasilimali za Tanganyika.
Mzigo wa gharama hautakuwepo na hakuatakuwa na ulalamishi.

Tanganyika ndiyo salama yao, kinyume chake ni suala la muda.
Mkuu wangu mweee. Wewe unataka kuizindua Tanganyika ipi? maana wewe mwenyewe unakubali kuwa asilimia 95 ya mambo yanayojadiliwa ktk bunge la Muungano ni ya Tangayika? sasa kuizindua hiyo tanganyika sii hutakuwa umechukua kabisa koti na kuliweka begani?, yaani umezidiwa na joto tu lakini koti bado lako..Kinachokosekana hapa ni serikali ya Muungano ambayo kiuhalisia haipo mkuu wangu. Tangayika haipunguziwi kitu leo hii ikiwa bajeti ya serikali inayojadiliwa leo bungeni ni ile ya mambo ya Tanganyika kwa jina la Tanzania, tusichokuwa nacho ni bunge la Muungano wa kweli ambalo ndio huunda serikali kwani hawa wabunge wetu ndio hao hao Mawaziri wa serikali.. Hivyo, kama unauitaka serikali ya 3 basi omba serikali ya Muungano na bado sielewi kwa nini uitake serikali hiyo ikiwa kikwazo chetu sote wananchi tumekubaliana ni hiyo katiba ya mwaka 1977. .
 
Tunataka kuvua koti, wakati tunajadili yale ya asilimia 95 pasowepo mtu anatughasi. Wakati tunapitisha sheria zetu, hatupaswi kuzipeleka zanz kwa watu 50 wa BLW waidhinishe.

Hatutaki tutumike kwa jina la Tanzania pale wznz wanapotaka kupunzika bila kodi ua kufanya kazi.
Gharama ni kubwa na hili tutalijadili tena. ZNZ inachukua bajeti kubwa kuliko halamashuri za miji 54 na wizara 5 za muungano kwa pamoja. Hapana inatosha.

Hatutaki tuwe na watu special ndani ya nchi yetu. Sisi sote ni Watanganyika, hii habari ya asilimia 4.5 au 21 ni ubaguzi.
Kwani wznz wanamchango gani zaidi ya Sumbawanga?

Tanganyika tu ndio itatatua kitendawili na ndiyo salama ya wznz. Wakitaka tuirudishe kwa njia zetu hilo halitakuwa jambo jema kwao. Narudia tena, Tanganyika tu ndiyo salama yao.
 
Nguruvi3, mwenzetu Mkandara lazima nikiri; ananiacha hoi. Sasa kama mambo yanayojadiliwa ndani ya Bunge la Muungano asilimia 95 ni ya Tanganyika (Tanzania Bara) sasa hao wenzetu wa Visiwani wako mle wanataka wajadili kitu gani? Wakiwa kwao ndani ya bunge lao (BLW) hakuna Mtanganyika anatia pua pale; sasa kwa nini wapate taabu yote hiyo ya kupigwa na mawimbi makali wakivuka bahari ya Hindi, wanafuata nini huku? Je Mkandara kweli haoni hapa kuna kitu hakiko sawa? Haoni kwamba dawa ni kwa kila upande kuwa na bunge lake kwa mambo yake halafu ndipo liwepo bunge la wote kwa mambo ya wote. Ni hapo tu Muungano utapata japo heshima na uhalali kama wa nchi mbili ambazo kwa pamoja zimekubali kushirikiana kwa mambo yaliyoridhiwa na pande zote. Muungano wetu hauwezi ukafanikiwa kama Tanganyika itaendelea kulivaa koti la wote, koti la Muungano, huo ni usanii! Kwani Zanzibar hawalitaki koti hilo!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu ni ngumu sana kumwelewa Mkandara .
Anabadilisha position kila uchao. Ukifuatilia kwa undani ni ngumu kuelewa anatetea nini hasa.

Mkandara anasema Tanganyika imevaa koti la muungano na hivyo Zanzibar inaonewa.
Halafu Mkandara huyo huyo anasema kuna mambo yameingizwa kinyemela katika muungano. Hayakuwepo.

Tukimwambia sawa sasa tuvue koti kwa kutenga mambo ya znz na Tanganyika, anasema znz itapata hasara.
Kama ni hivyo koti gani ambalo znz inalalamika lakini haitaki livuliwe? Mkandara anabadili upepo na kusema tunawaonea sana.
Turudishe Tanganyika, hataki. Tubaki na Tanzania , anasema tunavaa koti. Nini tufanye? anashauri tuendelee kukamua wananchi wetu kodi na wznz wanemeeke ili muungano ushamiri.

Mkandara anasema, ni haki mambo yote yawe ya muungano ila utekelezaji wake uwe na mamlaka tofauti.
Akiambiwa mamlaka hizo ni zipi, anasema ni JMT na Zanzibar

Tumemuuliza JMT ni nchi gani, akasema ni Tanganyika ambayo imegeuza mamlaka yake kuwa JMT.
Tukamuuliza sasa kama Tangayika ndiyo Tanzania, koti la muungano lipo wapi?
Anajibu hapana Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar.

Akiulizwa sasa mambo ya muungano na yasiyo ya muungano unayetenga vipi Tanganika ikiwa kuna JMT na Zanzibar.
Jibu la Mkandara ni kuwa lazima yasiyo ya muungano yatengwe na ya muungano.
Tukamuuliza chombo gani kisimamie yasiyo ya muungano, akasema Tanzania bara iwe na mambo yake.

Tanzania bara si ndiyo Tanganyika? Mkandara anasema Tanganyika ilishakufa.
Tukarudi nyuma kumuuliza kama ilishakufa wapi alipata JMT yenye Tanganyika na ZNZ na kwanini Tanganyika ilifutika.
Mkuu anasema tunataka tuwe taifa moja.

Tunamuuliza lakini znz wana utaifa wao, mkandara anasema hilo si tatizo, tatizo ni utaifa wa Tanganyika.
Haa! kwanini Tanganyika iwe nongwa kama tunataka kuwa na Taifa moja?

Mkandara anasema Taifa linalojulikana ni Tanzania. Hatukuwa na utaifa wa Tanganyika kwasababu Nyerere alikuwa anaujenga. Tukamuuliza, kama muungano usingekuwepo tungekuwa taifa gani. Jibu, tungekuwa taifa la Tanganyika.

Analalamika kwanini wznz hawaruhusiwi kujadili mambo ya Tanganyika.
Katika mkanganyiko huo, amefikia mahali anasema sisi ni taifa moja na wanaotaka kuvunja muungano ni Waanzibar wa Hizbu. Mkandara hataki kukubali kuwa katiba ya znz ni ya wznz na wala haikuandikwa na Hizbu.

Katiba hiyo inasema znz ni nchi yenye serikali na utaifa wa zanzibar na si Tanzania ikiwa na vyombo kamili kama nchi huru.
Ukweli wa katiba Mkandara haugusii kabisa.

Mkandara anashauri tufunge bandari zetu ili ile ya znz ifanye kazi kwa ufanisi. Asichokisema ni kuwa bandari si suala la muungano tena na waliokimbiza ni wazanzibar hao hao anaotaka wapewe kipaumbele kwa kile wasichokitaka kushiriki.

Mkuu Mkandara anasema misaada na mikopo inaishia Tanganyika.
Asichowaambia watu ni mchango wa znz nje ya jina la Tanzania.

Asichowaambia ni kuwa znz haina bajeti ya ulinzi na usalama, mambo ya nje, mambo ya ndani, na wala haina mchango hata senti tano kuendsha muungano. Deni lote la ndani znz inawasukumia Watanganyika na haina deni la nje

Mkandara hawaelezi wasomaji kuwa bajeti ya znz ni pungufu kwa mapato yake kwa takribani 350B.
Kama haina mikopo na misaada, nakisi hiyo anafidia nani kama si hazina Dar?

Mkandara anasema, wale watalii kutoka nchi jirani ya znz wanaokuja kupiga soga Dodoma, waruhusiwe kujadili mambo ya Tanganyika. Hawaambii watu yale ya BLW yajadiliwe na Mtanganyika gani anayewakilisha.

Ninachofahamu alisema (yupo katika rekodi) kuwa znz watapata hasara, asichokisema faida ya sasa wanaipata kutoka wapi.

Ni ngumu sana kuelewa kwanini anatetea serikali 2 wakati huo huo akitaka serikali 3 na kulaani serikali 3 akisumanga katiba ya serikali 2. Ngoja tusubiri sijui kesho atakuja na msiamo upi maana keshamaliza yote na hatuelewi anasimamia wapi.
 
Tunataka kuvua koti, wakati tunajadili yale ya asilimia 95 pasowepo mtu anatughasi. Wakati tunapitisha sheria zetu, hatupaswi kuzipeleka zanz kwa watu 50 wa BLW waidhinishe.

Hatutaki tutumike kwa jina la Tanzania pale wznz wanapotaka kupunzika bila kodi ua kufanya kazi.
Gharama ni kubwa na hili tutalijadili tena. ZNZ inachukua bajeti kubwa kuliko halamashuri za miji 54 na wizara 5 za muungano kwa pamoja. Hapana inatosha.

Hatutaki tuwe na watu special ndani ya nchi yetu. Sisi sote ni Watanganyika, hii habari ya asilimia 4.5 au 21 ni ubaguzi.
Kwani wznz wanamchango gani zaidi ya Sumbawanga?

Tanganyika tu ndio itatatua kitendawili na ndiyo salama ya wznz. Wakitaka tuirudishe kwa njia zetu hilo halitakuwa jambo jema kwao. Narudia tena, Tanganyika tu ndiyo salama yao.
Kwa maneno haya kwa nini bado wewe unataka Muungano? ni rahisi sana kuwaita wao wabaguzi lakini sii lazima mtu aseme kwa mdomo wake na ninavyokusoma hapa unaonyesha wazi kuwa wewe na wenzako ni wabaguzi maana haya ulikuwa nayo siku zote ila sasa umepata sababu ya kuyatoa.

Na hii ndio hofu yangu kubwa kwa vijana kama nyie msiojua maana wala kuthamini juu ya Muungano, Mwenge wa Uhuru, Mashujaa wetu na zaidi ya yote UTU wetu kama hao kina Jussa maana hamkukulia ktk mazingira hayo.. Ni hali ambayo wazawa wa Dar husema wa kuja hawana Ustaarabu kwa maana ya mila na desturi za UTU wetu.

Nitarudia tena kusema hivi zanzibar hawana kosa lolote kuomba mamlaka kamili ya ki republic ambayo ndani ya mfumo wa Kibepari kila nchi ina mamlaka kamili ya kuendesha shughuli zake za maendeleo, unless wewe una tafsiri yako juu ya mfumo ktk Kiutawala ktk Muungano wa nchi na watu, neno la kiingereza huitwa Sub sovereign na obligation zake (SSO). Mamlaka haya ni haki ambayo wameidai na halali kwao kama nchi ndani ya JMT tukizingatia kwamba mrengo wa Ujamaa kwa taifa zima haupo tena.

Haiwezekani kabisa wao waingie Bunge la Muungano mahala ambapo ati leo mambo yote sii ya Muungano - Uliona wapi?, halafu wakisema ama kuongeza neno mnasema wanawaingilia mambo yenu!, sasa iweje hilo Bunge mliite la Muungano wakati kiuhalisia ni Bunge la Tanganyika! msianzie huko mnataka tu serikali ya tanganyika!

Huyo waziri mkuu ni waziri wa tanganyika miaka yote hata alipokuwa Salim kwa zanzbar ni ceremonial tu hii kweli haki? wakisema tumevaa koti la Muungan mnachukia na kuidai Tangayika ambayo ipo na inafanya kazi zake. Hivyo hata tukianzisha Tangayika kitakachobadilika hapa ni jina tu maana Madaraka na mamlaka ya Pinda hayatabadilika.

Sina la kuongezea mkuu wangu nyie endeleeni na hiyo UKAWA yenu ambayo kwangu miye ni Upuuzi mtupu kudai serikali kwa sababu za Kisiasa zaidi ilihali hakuna mabadiliko yoyote kwa wananchi wake ambao wameiomba Katiba mpya na kwa maslahi yao kwanza na sii ya Chadema au CUF..
 
Mkandara;9716011]Kwa maneno haya kwa nini bado wewe unataka Muungano? ni rahisi sana kuwaita wao wabaguzi lakini sii lazima mtu aseme kwa mdomo wake na ninavyokusoma hapa unaonyesha wazi kuwa wewe na wenzako ni wabaguzi maana haya ulikuwa nayo siku zote ila sasa umepata sababu ya kuyatoa
Ubaguzi kaunza mznz. Mimi kwao si Mtanzania ni Mtanganyika. Stahili yangu si kuishi ni kuchomwa moto. Siruhusiwi kujenga au kumiliki bustani. Siruhusiwi kuajiriwa au kujiajiri. Mimi ni mgeni kama Mcameroon au Mnigeria. Hata katiba yao hainitambui.Wznz ni wabinafsi, wabaguzi si mimi. Tunasema mambo yawe 7 kinyume chake, tuvenje jahazi
Na hii ndio hofu yangu kubwa kwa vijana kama nyie msiojua maana wala kuthamini juu ya Muungano, Mwenge wa Uhuru, Mashujaa wetu na zaidi ya yote UTU wetu kama hao kina Jussa maana hamkukulia ktk mazingira hayo.. Ni hali ambayo wazawa wa Dar husema wa kuja hawana Ustaarabu kwa maana ya mila na desturi za UTU wetu.
Hapana, mkuu mengine tuneyaona na tunaandika kwasababu tumeyaona. Huu muungano hauthaminiwi na hao wanaokumabia wanauthamini.
Si hao hao wamua azimio la Arusha, leo muungano wana uthamini vipi.
Si hao hao wanamwita Nyerere laanatulah, leo wanathamin vipi muungano.
Hao wznz wangekuwa na utu wangethubutu kumchoma Mtanganyika kwa moto.
Wznz wangekuwa na staraabu wangemwita Nyerere laanatulah kwa muungano wanaoutaka leo.
Wznz wangekuwa wastaarabu wangepiga kelele ilimhali wanalala na kula kwa kodi za bara.
Kuna mstaarabu tegemezi, ni kutoka wapi
Nitarudia tena kusema hivi zanzibar hawana kosa lolote kuomba mamlaka kamili ya ki republic ambayo ndani ya mfumo wa Kibepari kila nchi ina mamlaka kamili ya kuendesha shughuli zake za maendeleo
Zanzibar ni republic ya kwanza, hiyo ya pili mbona huitaji mkuu. Ni ipi hiyo?
Haiwezekani kabisa wao waingie Bunge la Muungano mahala ambapo ati leo mambo yote sii ya Muungano - Uliona wapi?, halafu wakisema ama kuongeza neno mnasema wanawaingilia mambo yenu!
mambo ya muungano wanasema tumeyaingiza kinyemela na wanayaondoa, mafuta na gesi, anga, banadari, baraza la mitihani na wanataka benki kuu pamoja na fedha, tayari wana wimbo na bendera yao, sasa Dodoma wanafanya nini
Huyo waziri mkuu ni waziri wa tanganyika miaka yote hata alipokuwa Salim kwa zanzbar ni ceremonial tu hii kweli haki?
Hawatambui katiba yetu, hawana mchango wa hali au mali achilia mawazo.
Huwezi kumlipa mtu milioni 10 kwa mwezi akidai mabalozi 3 au 4. Huyo ana mchango gani wa mawazo ya maana.
Wanadai mabalozi kwasababu hawana kingine cha kusema, wapo wapo tu. Tatizo letu si mabalozi wa znz ni umasikini, ujinga na maradhi. Hao wabunge wa kuazima kutoka nchi jirani ya znz hawana habari, wanadai mabalozi.

Huko kwao hatujaingia BLW huku kwenye mambo yetu wanafanya nini.
Hatambui katiba yetu wanataka kujadili nini.

Waje Dodoma walale wachukue posho, wasivuruge mijadala isiyowahusu.
Hata kuja Dodoma wanalipiwa. Mchango 0, mdomo 100% .

Tuwaambie ukweli tusiwafiche hawa, imefikia mahali wanataka mambo yetu yaende kwao wakaidhinishe.
Mwisho sasa, tunawaambia hivi hapo Dodoma walale hawana mchango wowote wa maana zaidi ya tafrani na kelele
wakisema tumevaa koti la Muungan mnachukia na kuidai Tangayika ambayo ipo na inafanya kazi zake. Hivyo hata tukianzisha Tangayika kitakachobadilika hapa ni jina tu maana Madaraka na mamlaka ya Pinda hayatabadilika.
Hilo koti tunataka kulibua, kikwazo ni wewe na wznz ambao hamtaki. Mkandara, hebu tueleze tunavuaje koti hilo bila Tanganyika. Kuna wakati unajichanganya saana, mara mambo yote ni ya muungano, mara tumevaa koti mara wana haki.

Wana haki ya kukataa muungano pia. Hilo waambie, muda wa kuumiza watu wetu kuhudumia nchi jirani ya znz sasa baasi.
Muda wa kulipia watu kodi wakiwa wanapunga upepo sasa baasi.
Muda wa kualika wabunge wa nchi jirani hatuhitaji. Muda wa kusomesha watoto wa jirani bure sasa basi.

Wana nchi, serikali na taifa lao, wakitaka ni 7 tu , hawataki tutaizindua Tanganyika na itawalazimu watusaidie kwa gharama zao.
Ni ghali lakini kwa faida ya Watanganyika it is mutatis mutandis
 
Ubaguzi kaunza mznz. Mimi kwao si Mtanzania ni Mtanganyika. Stahili yangu si kuishi ni kuchomwa moto. Siruhusiwi kujenga au kumiliki bustani. Siruhusiwi kuajiriwa au kujiajiri. Mimi ni mgeni kama Mcameroon au Mnigeria. Hata katiba yao hainitambui.Wznz ni wabinafsi, wabaguzi si mimi. Tunasema mambo yawe 7 kinyume chake, tuvenje jahazi
Na ndio maana nasema nyie hamfahamu zaidi ya jazba zenu. Ikiwa Muungano wetu ulikuwa wa mkataba na maazimio yake iweje usiyatazame haya kwanza Waasisi wetu walikubaliana ktk MAMBO YASIYOKUWA YA MUUNGANO kwa wakati ule na yaliorodheshwa wazi, na hivyo kutowapa Wabara milki ya ardhi Zanzibar.. Tatizo liko wapi?

Na kama unakumbuka sisi wabara tuliokuwa tukienda Zanzibar kwa passport kana kwamba Zanzibar nchi ni nyingine kabisa. Haya yalikuwa makubaliano na tukaanguka saini. Baadaye yakafanyika marekebisho kwa makubaliano vile vile tukafikia hatua ya kwamba Unaweza kwenda Znz bila pasi lakini hatujawahi gusia la ardhi iweje wewe ujiulize kuwa mali za ukoo upande wa mama pia una urithi nazo?

Maswala ya ardhi kama kweli wewe ni mpenda Muungano huu ni swala la Bara kuliweka ktk kero yake japo mimi sioni sababu kabisa ya wewe Mbara kutafuta ardhi Zanzibar wakati serikali ilijaribu sana kuwaondoa Wazanzibar huko kutokana na udogo wa ardhi iliyopo na kuwapa nafasi huku Bara. Na hata huku Bara wakati wa Ujamaa kuna wabara walohamishwa makazi yao na hata sheria ilikataza kujenga ama kununua ardhi ameneo yalotengwa kwa ajili ya kilimo ama nje ya kijiji cha Ujamaa.

Je sio nyie mnaotukataa sisi Wazawa tuishio nje ya kwamba hatutajkiwi kuwa raia wa nchi hii?.. Je sii ubaguzi huo ama kwa sababu ipi maana sisi tunaelewa ni sheria tu inayotukwaza na inaweza badilishwa! Kama tungekuwa tunafikiria kama nyie basi tungeisha kata tamaa maana wapo wajinga wanasema mtu huwezi kuwatumikia mabwana wawili sasa sielewi ni lini serikali ikawa bwana wa mwananchi? nijuavyo mimi mwananchi, mzawa ndiye bwana na serikali hunitumikia! lakini wapi mijitu haielewi wala haitaki kuelewa!

Hivyo huwezi kuwalaumu Wazanzibar ktk hilo ikiwa sote tuliafiki na kuweka masharti haya ili kutoimeza Zanzibar na pia kuondoa matatizo ya Ardhi. Binafsi nina hakika kabisa kama ingekuwa huru kwa wabara kununua ama kumiliki ardhi Zanzibar basi huu Muungano usingechukua hata miaka 10. hii ni hekima walotumia waasisi wetu am,bayo sisi vijana wa leo hatuna isipokuwa tunapima mambo kwa marefu ya mkono, hatuoni mbele zaidi.

Hapana, mkuu mengine tuneyaona na tunaandika kwasababu tumeyaona. Huu muungano hauthaminiwi na hao wanaokumabia wanauthamini.
Si hao hao wamua azimio la Arusha, leo muungano wana uthamini vipi.
Si hao hao wanamwita Nyerere laanatulah, leo wanathamin vipi muungano.
Hao wznz wangekuwa na utu wangethubutu kumchoma Mtanganyika kwa moto.
Wznz wangekuwa na staraabu wangemwita Nyerere laanatulah kwa muungano wanaoutaka leo.
Wznz wangekuwa wastaarabu wangepiga kelele ilimhali wanalala na kula kwa kodi za bara.
Kuna mstaarabu tegemezi, ni kutoka wapi
Mkuu unaabndika vitu ambavyo wewe mwenyewe inaonyesha unakubaliana navyo manaa wanaomwita Nyerere Laanatullah ndio hao mko nao bega kwa bega ndani ya UKAWA ni hao hao wengine baina yenu wanaosema na kumdhihaki Nyerere kutoka vyama vyenu vya bara. Maneno alosema Tundu Lissu hayana tofauti na kumuita Nyerere na Karume Laanatullah maana unapohoji Muunganio na hekima zao basi unawaondoa ktk watu wenye akili timamu ama Majambazi..
Kwangu miye Mikandara sioni tofauti baina ya Ntarahamwe na Boko Haram, na hivyo siwapongezi CCM wlaa UKAWA kwa sababu nyiote mnakwepa jukumu kubwa la kukubali kwamba Muungano wa nchi hauna MA MBO YASIYOKUWA YA MUUNGANO isipokuwa kwa Jumuiya ya nchi zenye Utaifa wake zinapokubaliana kuungana kwa maswala fulani tu iwe ni EAC ama EU ambako kila nchi inajitawala.

Zanzibar ni republic ya kwanza, hiyo ya pili mbona huitaji mkuu. Ni ipi hiyo?
Hiyo ya pili ni JMT ambayo ni Tangayika kama nilivyosema Joseph kujiita Yussuph haiondoi ukweli kwamba ni mtu yule yule..

mambo ya muungano wanasema tumeyaingiza kinyemela na wanayaondoa, mafuta na gesi, anga, banadari, baraza la mitihani na wanataka benki kuu pamoja na fedha, tayari wana wimbo na bendera yao, sasa Dodoma wanafanya nini
Wanaoweka madai hayo mko nao pamoja huko UKAWA, sasawaulize nyie mnafanya nini pamoja nao mkizunguka Tanganyika nzima tena mlianzia zanziobar kwa madai ya tanganyika ili iweje? Kwa mwenye kuelewa atajua wazi kwamba mnasukumwa kama gari bovu na hao Hizbulllah hamjui mnachokifanya!
Hawatambui katiba yetu, hawana mchango wa hali au mali achilia mawazo.
Huwezi kumlipa mtu milioni 10 kwa mwezi akidai mabalozi 3 au 4. Huyo ana mchango gani wa mawazo ya maana.
Wanadai mabalozi kwasababu hawana kingine cha kusema, wapo wapo tu. Tatizo letu si mabalozi wa znz ni umasikini, ujinga na maradhi. Hao wabunge wa kuazima kutoka nchi jirani ya znz hawana habari, wanadai mabalozi.

Huko kwao hatujaingia BLW huku kwenye mambo yetu wanafanya nini.
Hatambui katiba yetu wanataka kujadili nini.

Waje Dodoma walale wachukue posho, wasivuruge mijadala isiyowahusu.
Hata kuja Dodoma wanalipiwa. Mchango 0, mdomo 100% .

Tuwaambie ukweli tusiwafiche hawa, imefikia mahali wanataka mambo yetu yaende kwao wakaidhinishe.
Mwisho sasa, tunawaambia hivi hapo Dodoma walale hawana mchango wowote wa maana zaidi ya tafrani na kelele
Maswala ya Ubalozi na kadhalika ni mapungufu ya Kikatiba baada ya suisi kuachana na Ujamaa lakini haya yalikuwa makubaliano ya awali wakati tukiwa Wajamaa na serikali moja. Na hata katika makubaliano hayo tulisema rais akitoka Bara basi makamu wa rais lazima atoke Zanzibar na ndiye atakuwa rais wa Zanzibar. Hili haliwezekani leo ndani ya Utawala wa Kidemokrasia na vyama vingi hivyo usitake kuwalaumu wao isipokuwa Hii katiba tulokuwa nayo haikidhi mazingira haya. Na kama tunataka kubadilisha jambo lazima liwe na makubaliano baina ya pande 2 na sii serikali ya Tangayika kufanya maamuzi bila makubaliano.

Tunaitaka katiba hii mpya iweze kutoa nafasi za Kidemokrasia na sii kidikteta tena hivyo maadam katiba iliwanyima Wazanzibar fursa zilizokuwepo ndani ya katiba ile wanayo haki mkisheria kuitumia katiba hiyo hiyo kudai mambo haya japo yamepitwa na wakati. Hivyo kugawana umaskini hauwezi kuwa suluhisho bali kuandika katiba mpya itakayo vipa dhamana vyama vya siasa vitakavyoshinda uchaguzi kutoa mawaziri, mabalozi, jaji mkuu, mkuu wa Ulinzi na Usalama na kadhalika bila kujali anatoka wapi ili kuvipa dhamana vyombo hivyo na sii Uzawa wa mtu. Kama tuliweza kuondoa Machief na tukaweka Wabunge tena basi wasokuwa wa makabila hayo na leo tunaikubali iweje tushindwe kuondoa Uzanzibar na Utanganyika ktk mfumo huu wa Kibepari?... Nyerere na Karume wasingeweza kufikiria hivi wa sababu wao walijenga Taifa la Kijamaa na hivyo UTAIFA wetu ulitazama zaidi haki na nafasi sawa za kiutawala kupitia chama CCM na sii vinginevyo. Mwaka 1964 Ungemwambia Nyerere au Karume kuwa na vyama vingi wangekutia segelea na usahaulike, hii haina maana walikuwa wajinga isipokuwa itikadi ya kiutawala haikuruhusu mgigogoro ya Kisiasa wakati ujenzi wa UTaifa letu unaandaliwa Kijamaa.

Hilo koti tunataka kulibua, kikwazo ni wewe na wznz ambao hamtaki. Mkandara, hebu tueleze tunavuaje koti hilo bila Tanganyika. Kuna wakati unajichanganya saana, mara mambo yote ni ya muungano, mara tumevaa koti mara wana haki.

Wana haki ya kukataa muungano pia. Hilo waambie, muda wa kuumiza watu wetu kuhudumia nchi jirani ya znz sasa baasi.
Muda wa kulipia watu kodi wakiwa wanapunga upepo sasa baasi.
Muda wa kualika wabunge wa nchi jirani hatuhitaji. Muda wa kusomesha watoto wa jirani bure sasa basi.

Wana nchi, serikali na taifa lao, wakitaka ni 7 tu , hawataki tutaizindua Tanganyika na itawalazimu watusaidie kwa gharama zao.
Ni ghali lakini kwa faida ya Watanganyika it is mutatis mutandis
Mkuu mimi sijichanganyi hata kidogo ila naelewa nini haswa tatizo la Muungano wetu. Nimesema NI kuwepo kwa MAMBO YASIYOKUWA YA MUUNGANO - kwisha iwapo mambo yote tayakuwa ya Muungano haijalishi tuna serikali 1, 2 au 3 maana kila swala Bungeni la JMY litwahusu wabunge wote wa JMT. sasa ikiwa ni serikali 2 Zanzibnar watapewa mamlaka ya kuendesha shughuli zao nasi Bara tutakuwa na maswala yetu maana wabunge wetu wako ktk bunge la JMT. Kila mbunge anajihusisha na jimbo lake hivyo tutakuwa na wawakilishi hata kama itabakia tulivyo, serikali ya Pinda ni serikali ya Tanganyika haitabadilika kitu. Vivyo hivyo tukiwa na serikali 3 au 1 bado swala kubwa litakuwa kwamba mambo yote ni ya Muungano hivyo madai ya Zanzibar yatafukiwa na katiba hiyo na madai ya Tanganyika yatafukiwa vile vile.

Kuidai serikali ya Tanganyika amabayo ni serikali ya JMT ni kujivika kanzu na kibalaghashia tuonekane waswahilina kumbe hakuna lolote ila unafiki mtupu. Bunge la JMT linatakiwa kujadili maswala ya Tanzania nzima na kila mbunge ahusike kikamilifu na mustakabali wa Taifa na sioi vinginevyo.

Kama hulioni hili basi utashindwa pia kuona jinsi CCM wanavyo dominate Bunge na siasa za Vyama vingi kwa sababu katiba yetu haikufanyiwa marekebisho kuvipa vyama vingine mamlaka kamili. Linaloamuliwa Bungeni leo hii ni kwa maslahi ya CCM lakini waulize wao watakwambia mpewe nini? CCM ndio inawapa ruzuku, CCM ndio inawawezesha hata kushiriki kugombea Ubunge na pengine hata kuwepo Dodoma. Haya ni matusi makubwa sana kwa vyama vyua kisiasa lakini pia makosa sii ya Chadema wala CUF ama NCCR isipokuwa tulipoingia mfumo wa vyama vingi hatukufanya marekebisho ya kikatiba kuwapa nafasi vyama vya kisiasa kuwa na mamlaka sawa na chama tawala. Hiyo CCM yenyewe inatakiwa kujivua koti ili mambo yote ya kisiasa yawe kwa vyama vyote na sii CCM kuruhusiwa mihadhara lakini sio CUF ama Chadema.

CCM wapewe Ulinzi lakini sio vyama vinginevyo.. Leo wewe unashangaa kusikia bara tujivue koti na kwamba mambo yote yawe ya Muungano kwa sababu wewe ni sawa huyo CCM unayemlalamikia tatizo tu ni kwamba Nyani huwa haoni makalio yake..
 
Mkandara;9727598]Na ndio maana nasema nyie hamfahamu zaidi ya jazba zenu. Ikiwa Muungano wetu ulikuwa wa mkataba na maazimio yake iweje usiyatazame haya kwanza Waasisi wetu walikubaliana ktk MAMBO YASIYOKUWA YA MUUNGANO kwa wakati ule na yaliorodheshwa wazi, na hivyo kutowapa Wabara milki ya ardhi Zanzibar.. Tatizo liko wapi?
Mkandara huko nyuma suala hilo liliachwa kama lilivyo. Hakuna makubaliano ya aina yoyote. Kilichotokea siku za karibuni ni kutengeneza sheria ya kumbana Mtanganyika. Sheria mahususi kwa Mtanganyika si Mkenya aliyetoka Momba na kununua pwani, au Mtaliano aliyenunu ardhi ya beach. Ni mahususi kwa Mtanganyika.

Na kama unakumbuka sisi wabara tuliokuwa tukienda Zanzibar kwa passport kana kwamba Zanzibar nchi ni nyingine kabisa. Haya yalikuwa makubaliano na tukaanguka saini. Baadaye yakafanyika marekebisho kwa makubaliano vile vile tukafikia hatua ya kwamba Unaweza kwenda Znz bila pasi lakini hatujawahi gusia la ardhi iweje wewe ujiulize kuwa mali za ukoo upande wa mama pia una urithi nazo?
Usipotoshe, Tanganyika walisema kama znz inaweka passport na wao waje na passport. Wazanzibar wakanywea wakijua passport haimdhuru Mtanganyika kama inavyowaumiza wao. Nusu wanaishi huku na hivyo hawakuwa na chaguo ila to bow to the pressure. Hwajarudia tena upuuzi na sijui kama watarudia. Kama wanataka wajaribu.

Maswala ya ardhi kama kweli wewe ni mpenda Muungano huu ni swala la Bara kuliweka ktk kero yake japo mimi sioni sababu kabisa ya wewe Mbara kutafuta ardhi Zanzibar wakati serikali ilijaribu sana kuwaondoa Wazanzibar huko kutokana na udogo wa ardhi iliyopo na kuwapa nafasi huku Bara. Na hata huku Bara wakati wa Ujamaa kuna wabara walohamishwa makazi yao na hata sheria ilikataza kujenga ama kununua ardhi ameneo yalotengwa kwa ajili ya kilimo ama nje ya kijiji cha Ujamaa
Hatuna sababu za kuweka kero, tunataka Tanganyika tushughulike na fiscal autonomy yetu. Znz ni kisehemu kidogo sana ambacho uwepo au kutokuwepo kwake hakudhuru masilahi ya Tanganyika.

Je sio nyie mnaotukataa sisi Wazawa tuishio nje ya kwamba hatutajkiwi kuwa raia wa nchi hii?.. Je sii ubaguzi huo ama kwa sababu ipi maana sisi tunaelewa ni sheria tu inayotukwaza na inaweza badilishwa! Kama tungekuwa tunafikiria kama nyie basi tungeisha kata tamaa maana wapo wajinga wanasema mtu huwezi kuwatumikia mabwana wawili sasa sielewi ni lini serikali ikawa bwana wa mwananchi? nijuavyo mimi mwananchi, mzawa ndiye bwana na serikali hunitumikia! lakini wapi mijitu haielewi wala haitaki kuelewa!
Suala la diaspora linatakiwa liangaliwe kwa jicho la uchumi na usalama. Lakini sioni kama kuna tatizo, tatizo ni kuwa ninyi watu wa nje hamuwakilishi maoni kama erudite, au ellite. Huwezi kuvaa gwanda la kijani ili ufanikiwe. Matokeo ya kuvaa magwanda ya kijani ni kuwa inferior kwa kina Mwigulu na Membe. You must change the way of thinking, act like citizen and avoid kujikomba komba.
Hatuelewi CCM nani na wananchi ni nani. Organize yourself first

Hivyo huwezi kuwalaumu Wazanzibar ktk hilo ikiwa sote tuliafiki na kuweka masharti haya ili kutoimeza Zanzibar na pia kuondoa matatizo ya Ardhi. Binafsi nina hakika kabisa kama ingekuwa huru kwa wabara kununua ama kumiliki ardhi Zanzibar basi huu Muungano usingechukua hata miaka 10. hii ni hekima walotumia waasisi wetu am,bayo sisi vijana wa leo hatuna isipokuwa tunapima mambo kwa marefu ya mkono, hatuoni mbele zaidi.
Mkuu hatuhaitaji ardhi yao, tunataka Tanganyika tuamue hatima yetu. Huu muungano una miaka zaidi ya 10 kwasababu ya pipi na peremende. Sasa tumechoka, wenzetu kuomba omba tuu, hata siku moja hakuna hoja inayohusu umasikini, maradhi au ujinga.
Sasa basi.
 
Maswala ya Ubalozi na kadhalika ni mapungufu ya Kikatiba baada ya suisi kuachana na Ujamaa lakini haya yalikuwa makubaliano ya awali wakati tukiwa Wajamaa na serikali moja. Na hata katika makubaliano hayo tulisema rais akitoka Bara basi makamu wa rais lazima atoke Zanzibar na ndiye atakuwa rais wa Zanzibar. Hili haliwezekani leo ndani ya Utawala wa Kidemokrasia na vyama vingi hivyo usitake kuwalaumu wao isipokuwa Hii katiba tulokuwa nayo haikidhi mazingira haya. Na kama tunataka kubadilisha jambo lazima liwe na makubaliano baina ya pande 2 na sii serikali ya Tangayika kufanya maamuzi bila makubaliano.
Mkuu Mkandara , kuna mambo mengi muhimu sana ya kushughulikia. Hii hoja ya mabalozi ni kukosa cha kuzungumza na ndiyo maana tunawaambia walale hotelini maana hawana mchango wowote

Hao mabalozi unaosema, wanahudumiwa na Tanganyika.
Nje ya muungano znz haiwezi kuwa na balozi 30, hata hizo 4 watakazokuwa nazo zitakuwa si balozi ni nyumba za watu.

Kuendesha ubalozi si lele mama ni gharama.Hawa wasioweza kulipa umeme kuanzia utotoni hadi wanajukuu hawawezi kuhudumia balozi 30.

Lakini basi leo kukiwa na mabalozi 30 kutoka znz, je hiyo itakuwa imeondoa umasikini wa wavuvi wasioweza kununua mita 3 za nyavu.

Wavuvi wanaotegemea waitaliano wanunue pweza kwa sh 200. Mabalozi watawasaidia vipi.
Hii ni thinking ya kiwango cha chini sana ndio maana tunasema wenzetu hawana la kuzungumza.

Lakini pia lazima wznz waelewe kuwa kuzungumza si kudai tu, lini wao waliwahi kzungumzia gharama za muungano.Hawazungumzii kwasababu hawajui posho zao pale Dodoma zinatoka wapi.
Makubaliano hakuna kuhusu mabalozi, na kama yapo kuwajibika kwake kukoje?

Halafu unanishangaza sana, Mkandara naona huu uzi umekuchanganya saana.
Unaposema kila jambo likibadilishwa lazima kuwe na pande mbili tena ukisota vidole Tanganyika, nikuulize
1. Katiba ya 2010 kulikuwa na mazungumzo ya pande 2?
2. Kuondoa gesi na mafuta kulikuwa na mazungumzo
3. Kuanzisha baraza lao la mitihani kulikuwa na mazungumzo
4. Kuweka sheria za kuzuia ajira kwa Mtanganyika, kulikuwa na mazungumzo
5. Kuondoa bandari na anga, kulikuwa na mazungumzo?
6. Kuanzisha IMO huku wakiiba ada kutoka Tanzania maritime kulikuwa na mazungumzo?
7. Kupiga wabara marufuku kumiliki ardhi, kulikuwa na mazungumzo?
9. Kudhalilisa katiba ya JMT, kulikuwa na mazungumzo?

Yaani wznz wakifanya uhuni na ujuha ni halali kabisa.
Ndiyo haya ya kuchagua wanafunzi kwa kutumia uzanzibar na si academic qualification.

Wanaokota tu mitaani. Hawana uchungu kwasababu hawalipi ada au mikopo kwasababu ni wznz.

Wanapewa nafasi 21 asilimia si kwasababu ya sifa, kwasababu tu ni wznz eti ni halali kwao na ni halali kwetu kuwa na wafanyakazi wanaoajiriwa kwa sifa ya uzanzibar na si jambo jingine.
Tunaongozwa hata na viazi kwasababu tu wao ni watu wanatakiwa upendeleo maalumu

Haya sasa yanafika mwisho, Watanganyika wanasema wanataka Tanganyika yao, kama wznz watahitaji msaada basi ni 7 tu. Nje ya hapo vunja jahazi kila mtu na njia yake, ile ya znz nyeupeee...!

Kama wznz hawatakubali kurejea Tanganyika, tutairudisha kwa gharama kubwa za wznz.
Trust me, inakuja.
 
nimekusoma na naendelea kukusoma na kutambua chuki ulokuwa nayo juu ya Muungano huu na ndio sababu sintokubakliana na watu wenye fiktra na mtazamo huu. Lengo na nia yebnu sii kuwa na Muungano bali kujitenga na hawa watu waitwao Wazanzibar. Kesho itakuwa Wasukuma na nadhalika maana toka nimefika hapa Mujini nimeona jinsi hiki kizazi kipya kinavyojisikia,.. Ni watu walopoteza kabisa mila na tamaduni na kujiona wao wanajua kuliko kila mtu, wao ni wazungu weusi Kidhungu kwa kila neno la Kiswahili. Hakuna salaam wala kuamkuana kama tulivyolelewa sisi isipokuwa kama mnajuana. Hakua Ujirani wala udugu hivyo sikushangai.

Hao Wazanzibar unaowachukia kwa namna moja wako wamoja zaidi yetu sisi. Kwao Mzanzibar sii kabila wala rangi ila Uzawa na wapo wenyeji, wangazija, Mashiraz, na hata Wachina wakipendana kama jamii moja na wanaipenda lugha yao ya Kiswahili na tamaduni zao mbali kabisa na imani yao ya dini> hii ndio nchi yenye Identity sio sisi mijitu imetoka huko Uswekeni imeingia mjini na kupelekwa kusoma nje basi imerudi na elimu ya Ubwana. Kwa Mtanganyika kama sii wa makabila 120 ya Tanganyika basi wewe sii Mtanganyika na haiwezekana hata Mhindi alozaliwa Kariakoo akapewa haki sawa na Mchagga au Mnyakyusa.

Nakusihi sana usiwe ktk kundi hili na hiyo UKAWA yenu ni chombo cha hawa watu wanaofikiria wao wanaijua sana Tanganyika wakati hawana walijualo zaidi ya kuzaliwa ktk ardhi hii. Nawaomba sana wewe na hasa vichwa vya hapa kijiweni kutokubali kutumiwa na haya makundi ya Kisiasa ambayo kwao wana malengo yao binafsi kutokana na eklimu zao za maskini akipata.

Mkuu Mchambuzi na Nguruvi3 jitahidini sana kusoma alama za wakati kwa sababu hyo Tanganyika yenyewe ndani ya mfumo huu uliopo iwe hata serikali 3 pasipo kuubaidlisha na kupata mfumo mpya utakao ondoa mamlaka ya utekelezaji shughuli za serikali toka mikononi mwa hiyo serikali kuu ya CCM au Tanganyika ili shughuli hizo ziwe za majimbo, basi itakuja siku tokea vita kubwa baadaye maana mbali kabisa na Zanzibar wananchi wa Mtwara, Mara, Shinyanga, Arusha na kadhalika watachoka pia kubebana na watakuja na sababu hizi hizi za kutoiona faida ya serikali ya Tanganyika ama TANGANYIKA muitakayo.

Nimeyatazama haya tokana na kauli zenu wenyewe (nimewasoma na kelewa kina cha fikra zenu) na kutambua kwamba hakuna kitu Utaifa wala Uzalendo, watu tunaishi kwa chuki na hasira za maskini jeuri. Nitasema la mwisho ya kwamba sio tu Tanganyika imevaa koti la Muungano bali hata huu mkoa wa Dar es Salaam itakuja siku watu wataona mkoa huu ama jiji hili umevaa koti la Tanganyika, na utakuja nambia na kukumbuka maneno yangu.
 
Tafuta video ya Yahya Kassim utaelewa kuwa Watanganyika wapo salama baada ya wzaznzibar kuwatenga.Yahya amesema wazi kuwa muungano ukifa na wao wataondoka, tena kasema 'wallahi nanyi mnaondoka kule'' Tafuta video.

Msimamo wa wznz ni mamlaka kamili, kwasasasa wznz wale wale waliokuwa wanamtusi Nyerere laanatullah hawajui wamtusi nani maana lanataulah inageuga kwa Jumbe.Leo wanadai mkataba wa muungano wa Pemba na Unguja.

Kugawanyika kwa wznz kuhusu suala la muungano kuna jibu moja, nje ya muungano hakuna cha dini wala nini.Unajidanganya unaposema dini yao ni moja, Somalia wana dini na koo zinazofanana kuliko wznz.
Leo wamesambaratika.
Hujaishi znz, kuna ubaguzi mkubwa wa kinafiki, misikiti inaendeshwa kwa rangi, kama washirazi, n.k

Nasema hivi huu uzi umekuchanganya, fikiria haya, Seif Idd, Mohamed Khatib, Pandu Kificho, Shamsa Vuai, Asha Bakari. Waangalie hao wanapigania nini halafu uangalie Jusa, Seif Hamad, wanapigania nini.
Mkandara hujui kuna wanaosema mapinduzi DAIMA na wasemao Mapinduzi zii.

Watanganyika ni wamoja sana usianze kutisha watu kama CCM na prof Shivji wanavyofanya.
Kwamba ustawi wa Tanganyika unategemea kulisha watu wanaoshinda wamelala.
Hata kudanganya hamuwezi jamani!

Miaka 50 tumeishi kama Watanzania, leo wenzetu wanjiita wazanzibar tena wakitubagua bila haya, soni au aibu. Miaka 50 wenzetu haataki Utanzania wanataka kutumia jina la utanzania, kulala na kupunga upepo kwa gharama za watu wetu. Miaka 50 hawataki kuitwa Watanzania leo Mkandara anasema ni wenzetu.
Mznz si Mtanzania, ni raia wa nchi jirani na anapaswa kuangaliwa kwa jicho hilo kuanzia makazini, mashuleni hata mitaani. Si mwenztu kesha tukana, hatuna sababu za kujipendekeza

Mimi naona fahari nikilipa kodi yangu ikaenda Musoma, Lindi au Songea kujenga bara bara, au kusomesha watoto wa huko. Hao ni Watanganyika wenzangu. Nimeenda Mtimbira baada ya wiki nikapewa eneo la kulima na kiwanja cha kujenga. Nilikuwa Musoma pale Nyakatende nikapewa eneo la kujenga.
Nilikuwa Tabora Isevya nikauliza tu tayari nikapewa eneo la kujenga. Hao ni wenzangu.

Wazanzibar si wenzetu, wametukataa, wana utaifa, nchi na kila kitu chao.
Wanatuchoma moto na kutuona ni watu waovu zaidi ya Waitaliano na Wambombasa.

Mtanganyika ndiye adui wa mzn ndio maana tunasema, wao kama nchi jirani tunaweza kuishi kwa makubaliano, sasa ni 7 tu, kama hawataki njia nyeupee! Hatutaki tena kuvaa koti wala kuishi kwa kukamua ndama asiye na kiwele

Leo Mkandara anaungana na wznz kusema wananyonywa. Hivi uchumi wa bilioni 400 nani mwenye akili timammu anaweza kwenda kunyonya.

Mambo ni 7 tu kama Tanganyika na nchi jirani, kinyume chake watatusaidia kuirudisha Tanganyika kwa gharama zao ambazo ni kubwa. Trust me, gharama zitakuwa kubwa
 
Mkandara mara nyingi amejenga hoja za kuwatuhumu Watanganyika kama chanzo cha matatizo ya muungano.
Yupo katika rekodi akisema kilichosababisha znz iandike katiba ya 2010 ni uonevu wa Watanganyika.

Mkandara anasema muungano inabidi mambo yote yawe ya muungano.
Maelezo haya yaweza kumweleza Mkandara wazanzibar wanasemaje kutokana na kauli zake

Kwa hisani ya gazeti la Nipashe
Shemejiye Karume sasa ajiunga CU
Alipata kuwa Waziri akavuliwa uanachama CCM
Aliyekuwa mwakilishi wa CCM wa jimbo la Kiembe Samaki, Mansour Yusuf Himid, ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF).

Himid aliyewahi kuwa Waziri mwandamizi chini Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) chini ya Rais Ali Mohammed Shein na hapo kabla chini ya Rais Mstaafu wa Amani Karume, alifukuzwa uanachama wa CCM Agosti 26, mwaka jana kwa madai ya kukisaliti chama chake.

Himid anayedaiwa kuwa ni shemeji yake Rais Karume, baada ya kuweka bayana azma hiyo, alisema katika uchaguzi mkuu wa mwakani anakusudia kugombea kiti cha jimbo hilo kupitia CUF.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa CUF mjini hapa mwishoni mwa wiki, alisema atawashauri vijana wampigie kura Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad,ili awe Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

"Mimi ni mpenzi wa Maalim Seif Sharif na kura yangu anayo na nitashirikiana na wezangu kuzitafuta kura za ziada ili awe Rais wa Zanzibar, "alisema Himid.

Alieleza kuwa bidhaa zikiwa nyingi sokoni mteja ana haki ya kuchagua iliyo bora, hivyo ana imani kuwa CUF ndilo kimbilio la Wazanzibari ili kuifanya nchi hiyo iwe na mamlaka kamili.

Alisema moja ya sababu ya kufukuzwa CCM ni kusema ukweli na kusimamia maridhiano ya wananchi kwa kutaka muundo wa serikali tatu na kusema Muungano uliopo wa serikali mbili hauna heshima kwa Wazanzibari na taifa lao.

"Mimi nisiwe kigeugeu, nasema kuwa Muungano huu hauna heshima hata kidogo, Zanzibar tunahitaji mamlaka kamili ili kujiendesha kiuchumi," alisema Himid na kuongeza kuwa Muungano wa nchi na watu siyo mbaya, lakini muundo uliopo wa serikali mbili haufai kwani Zanzibar itaendelea kuwa mtumwa chini ya muundo huo.

'
Kabla ya hatua hiyo alikuwa anatoa kauli mbalimbali za kutaka Zanzibar imiliki rasilimali zake hasa gesi na mafuta badala ya kuwa jambo la Muungano.

Kabla ya kufukuzwa uanachama alipata kuwa Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 na kuchaguliwa tena kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili mwaka 2010 hadi 2013 alipoondoshwa kwenye nafasi hiyo kuwa Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum kwa muda wa miezi mitatu hadi aliopofukuzwa CCM.

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, katika mkutano huo alisema kiu ya Wazanzibar ni mamlaka kamili ya dola.Alisema maridhiano ya SUK hayakuwa tu kuwaunganisha Wazanzibari, lakini pia lengo lilikuwa kuyarejesha mamlaka kamili ya Zanzibar.

Akizungumzia kuhusu mchakato wa katiba, Jussa alisema hawatakubali rasimu ambayo haitazingatia matakwa ya Wazanzibari ambayo ni muundo wa serikali tatu ili bendera ya Zanzibar ipepee katika Umoja wa Mataifa (UN).

Pia alisema suala la uraia na uhamiaji Zanzibar ni muhimu kwani ni kisiwa hivyo lazima kuwe na udhibiti wa wageni kutoka nje ya Zanzibar na kila Mzanzibari kuwa na paspoti ya nchi hiyo.

MANSOUR NI NANI HASA
Mansour aliteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Rais Karume mwaka 2000 na kuteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Waziri wa Maji, Nishati Ujenzi na Ardhi hadi mwaka 2005.

Mwaka 2005 alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Kiembe Samaki kupitia CCM, nafasi ambayo amedumu nayo hadi sasa. Mwaka huo aliteuliwa na Rais Karume kuwa Waziri wa Maji, Nishati Ujenzi na Ardhi hadi mwaka 2010.

Kati ya 2005 -2010 alikuwa Mweka Hazina wa CCM Zanzibar wadhifa ulimpa fursa ya kuwa Mjumbe wa NEC na Kamati Kuu ya CCM. Mwaka 2010 hadi mwaka 2012, alikuwa Waziri wa Kilimo na Rasilimali.

Ilipofika 2009 alikuwa mstari wa mbele kuushutumu Muungano kuwa ni chanzo cha kudorora kwa Zanzibar huku akiendesha kampeni juu ya suala la mafuta kutokuwa la Muungano.

Mwanasiasa huyo ni mtoto wa Mkuu wa Kwanza wa Jeshi la Zanzibar baada ya Mapinduzi, Brigedia Jenerali Yussuf Himid.

Amekuwa akisimamia maridhiano ya Wazanzibari na Umoja wa Kitaifa akiwa mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Maridhiano aliyoshiriki kikamilifu kuyaanzisha mwaka 2009.

Pia ni miongoni mwa Wazanzibari walio mstari wa mbele kutetea muundo wa Muungano, utakaoipa Zanzibar mamlaka kamili ya dola.
CHANZO: NIPASHE
Katika hali kama hii Mkandara anaamini tunaweza kuwa na mambo ya pamoja ya muungano.
Kitendo cha wznz kuomba uraia wao bado Mkandara anakiita 'republic' akipaka mafuta kuwa hata mikoa na wilaya zinaweza kujitegemea kama znz inavyotaka.

Hivi Mkandara, hawa wanaotaka bendera ipepee UN unawezaje kutuambia walifanya marekebisho ya katiba yao kwasababu ya kuudhiwa na Watanganyika? Hawa wanaotaka uraia wao unawezaje kuwaita Watanzania?

Katika mazingira ya namna hii, Mkandara na wenzetu wangine wanaamini serikali 2 zitatatua tatizo.
Kila siku wanapewa lakini wanazidi kudai, na hainekani wametosheka. Je, tuendelee namna hii kwa miaka mingapi.
Mkandara na CCM watueleze watawezaje kukabiliana na kuleta maridhiano na watu waioutambua utanzania kama hawa?
Mkandara, bado unaamini S2 ni muafaka au una hoja mbadala?
 
Last edited by a moderator:
Mkandara mara nyingi amejenga hoja za kuwatuhumu Watanganyika kama chanzo cha matatizo ya muungano.
Yupo katika rekodi akisema kilichosababisha znz iandike katiba ya 2010 ni uonevu wa Watanganyika.

Mkandara anasema muungano inabidi mambo yote yawe ya muungano.
Maelezo haya yaweza kumweleza Mkandara wazanzibar wanasemaje kutokana na kauli zake

Kwa hisani ya gazeti la Nipashe Katika hali kama hii Mkandara anaamini tunaweza kuwa na mambo ya pamoja ya muungano.

Mkuu wangu nimesema sana juu ya hii lakini wewe bado uko sawa kabisa na hao Waznaniabr unaowasoma.
Nyote hamufahamu maana hivyo sii rahisi kuijua maana ya MUUNGANO. Na sii rahisi pia kukubaliana na mimii kwa sababu mnashindwa kutenganisha maneno haya mawili - MAMBO YA MUUNGANO na SHUGHUILI ZA SERIKALI. Ukiweza kuinielewa mimi ktk utenganisho wa haya maswala mawili basi itakupa urahisi wewe kunifahamu mimi kwanza kisha tunaweza kuyatazama madai ya hao viongozi wa Zanzibar ukajua mimi nimesimama wapi.

Nimesema wala sii mara moja ya kwamba MAMBO YOTE ni YA MUUNGANO kwa maana ya kwamba hakuna jambo ambalo haliihusu Tanganyika ama Zanzibar. Nikakupa mifano ya wanandoa ya kwmaba hakuna jambo baina ya bwana na Bibi ambalo halimhusu mwenza Hivyo kuende;lea kuyaweka mambo yasokuwa ya Muungano wakati kisiasa na kiuchumi tumebadilika ni makosa makubwa ya kwanza katika hatua za Transformation tulochukua.

Pili, Napozungumzia MAMLAKA KAMILI nasema hivi, haya mamlaka ni halali yao ZnZ, kwa sababu serikali ndani ya muungano wa kibepari inatakiwa kuwa na MAMLKA KAMILI ya utekelezaji wa shughuli zake. Hivyo maadam tuna serikali ya Zanzibar ni haki yao kudai mamlaka kamili ambayo hawakupewa toka tumeingia Ubepari na vyama vingi mwaka 1993, bado nchi yetu inatumikia siasa za Ujamaa na Kujitegemea ambapo serikali Kuu ya CCM na Tanganyika ndio yenye mamlaka hayo.

Hivyo kuwepo kwa Wazanizbar ndani ya serikali kuu haina maana mfumo wa Kijamaa umebadilika - hapana bado tunaendela na mfumo wa Kijamaa kiutawala. Hivyo napozungumzia mamlaka kamili nazungumzia haki ya utekelezaji wa shughuli za serikali yao na sii nje ya utekelezaji kama navyoomba mamlaka kamili kwa TISS au serikali za Mikoa, majimbo, Mamayor, serikali za mitaa na kadhalika mamlaka ya serikali hizi lazima yawe wazi na wapewe mamlaka kamili.

Na hata hao Wazanzibar wanaopewa madaraka ktk serikali ya JMT wengi wao ni wakazi wa Bara wengine ni wazawa wa bara hivyo tunachokijenga hapa ni Ukabila wa makazi (Uzanzibar vs Utanganyika) na sii uzawa haswa, Hivyo basi unaponisoma mimi nikiandika Mamlaka kamili huwa nazungumzia mamlaka ya kuendesha shughuli za serikali na sio Mamlaka kamili ya Zanzibar kuwa Taifa huru, lenye bendera yake UN kama Kenya au Uganda na tuwe na muungano wa mkataba.

Hili sikubaliani nalo kabisa kwa sababu naielewa Historia ya nchi yetu, Mapinduzi na napingana sana na hizi siasa za SISI vs WAO ambazo zinaenezwa na kundi la Maalim Seif na Jussa ambao ni kizazi cha Hizbu ktk kujenga Utengano wa Uzanzibar a Utanganyika. na ndio maana nasisitiza wabunge lazima wawe wakazi wa sehemu wanayogombea hivyo Mbara kama anaishi Zanzibar ataitwa Mtanzania wa visiwani na Mzanzibar anayeishi bara ataitwa Mtanzania wa bara. Ni hatua kubwa ya transition ktk transformation ya Utaifa wetu ktk mfumo huu ubepari.

Tatu,
Mkuu wangu watu kama Himid wapo na wataendelea kuwepo kwa sababu sisi Watanganyika hatutaki kuwapa mamlaka kamili ya serikali ya Zanzibar kuendesha shughuli zake. Ni sawa na Mume anayetaka kwenda hata sokoni na Mkewe, kujua marafiki zake kila siku kuchunguza namba za simu zake na kadhalika. Sisi bara ni sawa na mume mwenye wivu ulopitiliza kila kitu lazima kipitie na kubarikiwa na serikali ya JMT ambayo inaongozwa na bunge la JMT ambalo asilimia 95 ya mambo yake ni kuhusu Tanganyika. Bado unashindwa vipi kuliona hili isipokuwa watu kama Himid ndio wanaokufanya wewe ufikirie kuitoa talaka.

Unachotakiwa wewe ni kufikiria kwa nini Himid kafikia kusema hivyo? Je muungano wa nchi nyingine serikali kuu humiliki rasilimali zote au ni kila nchi humiliki rasilimali hizo?.. sasa ikiwa sisi Bara tuynamiliki migodi yote ya Geita, Bulyanhuru na kadhalika iweje swala la Znz kuwa wamiliki wa rasilimali zao iwe shida kwetu kukubali Je sababu haswa nini nini? umejiuliza hivyo? sidhani. Nenda huko majuu iwe UK, Canada au USA kila nchi mshirika ni wamiliki wa rasilimali zao ila huchangia mfuko wa Taifa kwa asilimia sawa bila kutazama nani kaweka zaidi ya nani! Mfamo Canada kila province ni wamiliki wa rasilimali zao na huchangia asilimia 8 ya kila transaction ya fedha ktk mauzo au ununuzi ktk makusanyo ya kodi kwa ajili ya mfuko wa Taifa. Na hakuna jambo ambalo sii la Muungano wa Canada hakuna, japo mafuta ni ya Alberta lakini yanawahusu WaCanadian wote kwa mchango wake wa asilimia 8 ktk mfuko wa Taifa na kutoa ajira kwa Wacanadanian wote waishio Alberta na nje bila ubaguzi wa rangi ama uzawa.

Kila province (nchi) ina mamlaka kamili kuendesha shughuli zake japo mambo yote ni ya Muungano, kila Premier (RC), Mayor ana mamlaka kamili kama Premier au Mayor na kila kiongozi wa serikali yake ana mamlaka kamili ktk serikali hiyo ambayo yote yame orodheshwa very clear kiutawala - hakuna kuingiliana shughuli wala urasimu wa kutupiana mizigo na kuweka njia za ufisadi. Sio sisi ambao bado tumeubeba mzigo wa Ujamaa na hatutaki kuuvua mgolole japo tupo dunia nyingine kabisa na hatutaki kuambiwa makosa yetu. Leo sisi bara tunayo mamlaka kamili ya kuendesha shughuli zote kwa kutumia bunge la JMT na serikali ya JMT iweje tunakataa Zanzibar wasiwe za mamlaka ya kusimamia tu maendeleo yao isipokuwa kwa idhini ya bara. Huyo Meya mwenyewe hana mamlaka kamili isipokuwa tuna mkuu wa Mkoa RC na sijui DC

Ukweli ni kwamba hatuna Bunge la JMT ila tuna bunge la Yanganyika na serikali ya Tanganyika. Iwapo Pinda ni Waziri mkuu ambaye ni mwakilishi wa serikali ktk bunge la JMT ambalo asilimia 95 hujadili mambo ya bara utasemaje kuwa huyu ni waziri mku wa JMT. lakini ikiwa mambo yote ni ya Muungano Pinda atatakiwa kujibu waswali yote yanayohusiana na maswala yote ya Muungano. Iwe Elimu au Ufungaji isipokuwa kila nchi itaendesha shughuli zake toka mfuko wake na pande watakaloomba toka mfuko wa Taifa.

Hivyo ndio kusema hapa hakuna muungano isipokuwa tuna jina la Muungano (Tanganyika kuvaa koti la Muungano) Wewe nambie ni lini maswala ya Zanzibar kama sehemu ya tanzania yamejadiliwa bungeni na ukamuona Pinda akitoa majibu? zaidi utasikia Ubishi na kuanza matusi makubwa makubwa juu ya Utanganyika na Uzanzibar. Utasikia kina NYIE vs SISI toka kwa wajumbe wote wa CUF na CCM na hivyo binafsi yangu sioni tofauti baina ya Ntarahamwe na Al Shabab!

Unachonishangaza wewe ni pale unapoamini kuwa muungano huu haufai lakini unataka serikali 3 ambazo bado zinaendeshwa na Muungano usioutaka. labda wewe nifahamishe mimi vizuri unaposema unataka serikali 3, hizi serikali 3 zitaweza vipi kuondoa matatizo ya Muungano uliopo pasipo kuathiri UMOJA wetu maana niaminivyo dawa ya kidonda sii kuukata mguu, bali unatafuta kilichosababisha kuwepo kiidonda kisha unatafuta tiba ya virusi hivyo isije kuwa ambukizi kwa jamii. Na ndivyo navyowatazama watu kama Maalim Seif na Jussa.
 
Mkandara mara nyingi amejenga hoja za kuwatuhumu Watanganyika kama chanzo cha matatizo ya muungano.
Yupo katika rekodi akisema kilichosababisha znz iandike katiba ya 2010 ni uonevu wa Watanganyika.

Mkandara anasema muungano inabidi mambo yote yawe ya muungano.
Maelezo haya yaweza kumweleza Mkandara wazanzibar wanasemaje kutokana na kauli zake

Kwa hisani ya gazeti la Nipashe Katika hali kama hii Mkandara anaamini tunaweza kuwa na mambo ya pamoja ya muungano.
Kitendo cha wznz kuomba uraia wao bado Mkandara anakiita 'republic' akipaka mafuta kuwa hata mikoa na wilaya zinaweza kujitegemea kama znz inavyotaka.

Hivi Mkandara, hawa wanaotaka bendera ipepee UN unawezaje kutuambia walifanya marekebisho ya katiba yao kwasababu ya kuudhiwa na Watanganyika? Hawa wanaotaka uraia wao unawezaje kuwaita Watanzania?

Katika mazingira ya namna hii, Mkandara na wenzetu wangine wanaamini serikali 2 zitatatua tatizo.
Kila siku wanapewa lakini wanazidi kudai, na hainekani wametosheka. Je, tuendelee namna hii kwa miaka mingapi.
Mkandara na CCM watueleze watawezaje kukabiliana na kuleta maridhiano na watu waioutambua utanzania kama hawa?
Mkandara, bado unaamini S2 ni muafaka au una hoja mbadala?

Nguruvi3,

Kwa kusikia malalamiko ya wananchi wa pande zote za muungano na ili kuondosha mashaka na kutoaminiana katika mas'ala ya muungano wenu ndipo Serikali ya JMTz ikatengeneza Tume ya pamoja a Wataalamu wa uchumi na fedhwa ili uondoa mtafaruku huo

Tume hiyo ya pamoja ya uchumi na Fedhwa (JFC) iliundwa kisharia kabisa chini ya Sharia za JMTz ya 1996 Kwa mujibu wa Katiba ya JMTz ibara ya 133 Tume hiyo ilipewa mamlaka moja wapo ni kutunza fedhwa za muungano katika akaunt maalum na kutumika katika wizara na taasisi za muungano tu lakin pia kusimamia migawanyo ya rasilimali zitokanazo na Muungano huo.

Rasilimali hizo zipo nyingi lakin kubwa hapo ni mapato kama uchangiaji, Misaada na mikopo na vile vile mfumo wa mgawanyo wake kwa nchi husika

Sasa tujiulize kuna Siri gani sharia hio yya mwaka 1996 mpaka leo hijatekelezwa ya kuwa na AKAUNT YA PAMOJA YA MAMBO yA MUUNGANO TU Ili kupunguza zogo lako hapa barzani?
 
Mkandara,
Ahasante, na nitarudi kwa kina katika hoja zako.
Ninachotaka kukuambia ni kuwa mara nyingi sana nimesema huu muungano haupo. Sababu kubwa ni kuwa znz wameshajitoa katika muungano, kisheria na kijamii. Uwepo wao katika muungano ni for convinience tu ili wapate peremende lakini si uzalendo.
Leo mznz hataki kuitwa Mtanzania , bado Mkandara anaamini hawa ni wenzetu wa taifa moja.

Utaifa wa Tanzania ni wa Tanganyika, haumhusu mznz na kwa msingi huo hata uwepo wa wznz bungeni Dodoma ni kutokana na njaa zao tu, hawapaswi kuwa sehemu wasiotaka kuwepo. Dhiki inawasukuma, na katika siku za karibuni imedhaihirika wznz hawana tena nguvu ya muungano. Wanaambiwa njia nyeupe na wanakaa kimya hatusikii tena zile ngebe zao.

Ninaposema serikali 3, nina maana tuwe na mambo 7 tu kutokana na mazoea ili kuwasaidia wznz.
Bascially katika muungano wa aina yoyote znz haiwezi kuwa na mafao kwa Tanganyika.

Ni tegemezi kutokana na kanuni za asili, kimazingira, kijaamii, kiuchumi na kijiografia.
Hawana sababu za kusema tumeungana, wanatakiwa waseme tumeungwa.

Kama hayo 7 tunayotaka kuwasadia mafakir hayana maana kwao, hewala, njia nyeupeee.
 
Joint Finance Commission iliundwa kwa lengo la kushauri serikali Mbili za muungano juu ya sharing of revenues and expenditures, na fiscal relations kwa ujumla. Mgogoro mkubwa upo kwenye suala Zima la "shared expenditures", kizingiti kikubwa cha joint finance commission kutekeleza kazi yake ni upande huu wa "shared expenditures" kuliko upande wa "shared revenues". Kwa mtazamo wako, kwanini Hali Ipo hivyo? Kwa maana nyingine - je kwanini kikwazo kikubwa kwa JFC kipo zaidi kwenye suala la matumizi ya muungano (uchangiaji wa gharama za kuendesha muungano) kuliko kwenye suala la Mapato?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nguruvi3,

Kwa kusikia malalamiko ya wananchi wa pande zote za muungano na ili kuondosha mashaka na kutoaminiana katika mas'ala ya muungano wenu ndipo Serikali ya JMTz ikatengeneza Tume ya pamoja a Wataalamu wa uchumi na fedhwa ili uondoa mtafaruku huo

Tume hiyo ya pamoja ya uchumi na Fedhwa (JFC) iliundwa kisharia kabisa chini ya Sharia za JMTz ya 1996 Kwa mujibu wa Katiba ya JMTz ibara ya 133 Tume hiyo ilipewa mamlaka moja wapo ni kutunza fedhwa za muungano katika akaunt maalum na kutumika katika wizara na taasisi za muungano tu lakin pia kusimamia migawanyo ya rasilimali zitokanazo na Muungano huo.

Rasilimali hizo zipo nyingi lakin kubwa hapo ni mapato kama uchangiaji, Misaada na mikopo na vile vile mfumo wa mgawanyo wake kwa nchi husika

Sasa tujiulize kuna Siri gani sharia hio yya mwaka 1996 mpaka leo hijatekelezwa ya kuwa na AKAUNT YA PAMOJA YA MAMBO yA MUUNGANO TU Ili kupunguza zogo lako hapa barzani?
Kwanza, njoo umjibu Mchambuzi hapo juu

Pili, tueleze kwa muundo wa sasa ni zipi wizara na taasisi za muungano tu.
Tatu, tueleze ni zipi rasilimali za pamoja za muungano
Nne, nini chanzo cha mapato cha account hiyo
Tano, kwanini kusimamia mgawanyo na si kusimamia ukusanyaji wa mapato.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara,
Ahasante, na nitarudi kwa kina katika hoja zako.
Ninachotaka kukuambia ni kuwa mara nyingi sana nimesema huu muungano haupo. Sababu kubwa ni kuwa znz wameshajitoa katika muungano, kisheria na kijamii. Uwepo wao katika muungano ni for convinience tu ili wapate peremende lakini si uzalendo.
Leo mznz hataki kuitwa Mtanzania , bado Mkandara anaamini hawa ni wenzetu wa taifa moja.

Utaifa wa Tanzania ni wa Tanganyika, haumhusu mznz na kwa msingi huo hata uwepo wa wznz bungeni Dodoma ni kutokana na njaa zao tu, hawapaswi kuwa sehemu wasiotaka kuwepo. Dhiki inawasukuma, na katika siku za karibuni imedhaihirika wznz hawana tena nguvu ya muungano. Wanaambiwa njia nyeupe na wanakaa kimya hatusikii tena zile ngebe zao.

Ninaposema serikali 3, nina maana tuwe na mambo 7 tu kutokana na mazoea ili kuwasaidia wznz.
Bascially katika muungano wa aina yoyote znz haiwezi kuwa na mafao kwa Tanganyika.

Ni tegemezi kutokana na kanuni za asili, kimazingira, kijaamii, kiuchumi na kijiografia.
Hawana sababu za kusema tumeungana, wanatakiwa waseme tumeungwa.

Kama hayo 7 tunayotaka kuwasadia mafakir hayana maana kwao, hewala, njia nyeupeee.
Nguruvi3 mkuu wangu wee..Inakuumiza kichwa Mzanzibar kutojiita Mtanzania wakati amebeba passport ya Tanzania? ameshiriki kupiga kura za kuchagua viongozi wake wa serikali zote, na hata wengine wameajiriwa na serikali ya JMT kulisha familia zao. Hawa watu unawaamini kweli? mtu kama Jussa kama kweli anaamini ktk Uzanzibar si angekuwa msituni badala ya kuwepo Dodoma kila bunge maana hautambui Muungano wetu!

Hawa watu wanatafuta tu umaarufu wa kisiasa ni muhimu sana uwasome watu kama hawa hasa wanapokuwa majukwaani. Yule Maalim Seif yuko wapi? kapewa cheo na unyapala sasa hivi ni mshirika mkubwa wa JMT tena anapenda ukubwa kupindukia kesha sahau wenzake. Muondoe hapo utamsikia kesho akilalama upya, tumewazoea watu hawa ni wakati muafaka wa kufyata midomo yao kwa kufanya mambo yote ni ya Muungano!.

Labda nikukumbushe tu ya kwamba hata huku Majuu wapo watu wanajitambulisha kwa nchi zao. Mquebec hajiiti Mcanada na hata Mscotish hajiiti Muingereza wala British, haya ni maswala ya kawaida kabisa ktk miungano ya nchi kuunda Taifa kwa sababu mara nyingi maamuzi ya kuungana nchi hufanywa na watawala kutokana na historia ya nchi hizo. Sisi tulozaliwa baada ya muunganmo ndio tunaokuja na hoja nzito dhidi ya Muungano bila kufahamu ya kwamba historia ndio ilowalazimu wao kuungana kutokana na WATU, ARDHI na USALAMA wa nchi hizo. Factors hizi haziondoki kirahisi kama jinsi watu wengi wanavyofikiria.

Unaposema tuwe na mambo 7 tu huu ni muungano wa aina gani? Je, Unawezaje kuwa na serikali ya Tanganyika pasipo kuwa na nchi yake na kama itakuwepo hii tanganyika itakuwa na mihimili mingapi na itachukua muda gani kuiandaa. Je hiyo Tanganyika itakuwa na bunge lake? halafu ndio tuwe na bunge la Muungano ambalo Wazanzibar pia hawalitaki isipokuwa kujiunga na bunge la EAC walitakalo!. Je, Unapokubali mambo 7 ya muungano haitakuwa muunganosawa na huo wa jumuiya ya EAC, hivyo unahitaji nini kuwa na mkataba mpya na Zanzibar wakati tunaweza tu kuvunja huu uliopo na tukakutana huko Arusha sijui Nairobi kisha tuanze ya Kagame vs JK!

Pili, Uksha unda serikali ya Tanganyika utahitaji kuwa na bunge la Tanganyika hivyo utaanzisha uchaguzi mpya wa wabunge utakao chukua miezi na kisha utunzi wa katiba ya tanganyika ambayo itapitia changamoto kama hizi tena. YYaani ni mlolongo wa maswali wa mambo ambayo yanaiweka katiba mpya tuitakayo kapuni.

haya nipe majibu ya haraka kuhusu haya:-
1.Bunge la Tanganyika litawakilishwa na vyama gani? maana CUF ni chama cha visiwani na Chadema chama cha bara kama wasemavyo wanasiasa, Je ni sheria ipi itakayo wazuia CUF na vyama vya visiwani kugombea bara au Chadema na vyama vya bara kugombea Visiwani?

2. Hiyo CCM itaruhusiwa kugombea upande gani Zanzibar au bara wakati kina wanachama kila upande au nacho ni chama cha bara? na kama hakitaruhusiwa kugombea Zanzibar, mgombea wa chama hicho atakuwa na mahusiano gani na CCM ya bara? au vitaanzishwa vyama vipya pande zote? nini mipaka ya vyama vilivyopo upande wa pili (ili Znz) wasione wanaingiliwa ktk mambo yao.

Wakuu zangu, hivi kweli haya yote mmeyafikiria au mnasema tu ili mradi mnaitaka Tanganyika! na mkisha ipata Tanganyika kweli bado mtakubali kuwa na hayo mambo 7? au nilichosema mimi ndio rahisi kabisa. Kumbuka tu ya kwamba Mambo yote yakiwa ya Muungano, tunawalazimisha kina Jussa kuufyata. hakuna swala la Uzanzibar wala Utanganyika ila Utanzania hata kama watajiita Wazanzibar nawe unaweza kujiita Mtanganyika na ukaipeperusha bebdera ya tanganyika juu ya paa la nyumba yako.

Hii ni Identity tu ktk mfumo wa Kiutawala na pride ya uzawa, kama tulivyokuwa tukifanya sisi na makabila yetu. Utakapo itumia vibaya hiyo pride against others hapo ndipo utakuwa umevunja sheria, otherwise ni jambo jema tu kaa vile mataifa yatakavyo peperusha bendera zao huko Brazil kuanzia hiyo kesho..
 
Back
Top Bottom