Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Nguruvi3,

Ahali yangu naona tunarudi kule kule nilikokubainishia toka awali.

Huo mfano nilikuwekea ujue kuwa hata siku moja hamuwezi kuchangia 50/50 % kwenye muungano wenu kwa kila nchi kwani huo ndio uhalisia kutokana na eneo la nchi na idadi ya watu. Ndio maana wachumi wa nchi hizo wakaja na mapendekezo hayo.

Kumbuka kuwa JFC wamechambua kwa kina na kuja formula mbayo ndio hiyo ikiwemo 21% ya ajira katika vyombo vya muungano laazima wapewe wa Znz lakin TUNALOJADILI HAPA NI KUWEPO NA AKAUNTI YA PAMOJA YA FEDHWA ZA MUUNGANO AMBAZO ZITARATIBIWA NA KUSIMAMIWA NA JFC. Hii account itaondoa hayo malalamiko na manung'uniko yako. Kwani kwa sasa kutokana na TGK kujivika Joho la Tanzania wanawadhulumu sana wa Znz.
Mfano tunaposema mambo ya Ulinzi ni ya Muungano, ni vipi katika wizara hiyyo IWEMO JKT ambacho si chombo cha muungano. Kumbuka Znz kuna JKU. Au wizara mambo ya ndani ambacho ni chombo cha Mungano iweje kuwe na Magareza au Zimamoto ambavyo si vyombo vya muungano?. Kumbuka Znz kuna Chuo cha mafunzo na jeshi la Zimamoto.

Sasa unapopitisha Bajeti hii na kuita ya muungano huoni kuwa ukakasi umezidi hapo. Kwanini vyombo hivi vya Muungano na taasisi zake wasifate mgawo wao wa bajeti zao kupitia JFC na kutoka fedhwa zao katika Akaunti maalum ya pamoja na kuwaacha Pesa za mambo yasiyo ya muungano ziendelee kupitia katika Single Tressure Account iliyopo BOT?

sasa wasi wasi wenu ni nini?

Kumbuka mzowea vya kunyonga ...

Hakuna marefu yasiyo na ncha. Znz huru ileeeeeeeeeeeeeeeeeee

waachwe Znz wapumue

Nadhani wanajamvi wanakushangaa sana. Unaulizwa kitu kimoja unazua kitu kingine.

Maswali ni haya ndugu mchumi
Katika ajira 150,000 za polisi(mfano) wznz wangapi wameajiriwa na je hilo si sehemu ya uchumi.
Pili, kama wafadhili watatoa 60% ya misaada(mfano), hiyo 40% znz inachangia kiasi gani katika account ya pamoja?
Tatu, Je, wafadhili wakiacha kuchangia, ina maana JFC itakuwa imekufa? Na kama itakuwepo znz itachangia kiasi gani?

Haya ndiyo maswali, kama huwezi kuayajibu, stop and quit! hatuwezi kuwa na mjadala wa bla bla.
 
Nguruvi3,

Naona unajiviringisha bila kujua mwelekeo wako.

Ngoja nikurudisha katika uhalisia KWANI MARA ZOTE NAKWAMBIA UCHUMI NI TAALUMA NA WALA SIO BLA BLA. Rejea katika Bajeti ya JMTz ya mwaka huu 2014/2015. jaribu kuangalia taratibu uone ni kiasi gani Bajeti hiyo inategemea ihsan za misaada kutoka kwa wahisani na wafadhwili lakin pia Mikopo kutoka taasisi za kimataifa na mabenk na nchi wahisani?

Je nikikwambia kuwa Bajeti yenu haiwezi kutekelezeka kabisa bila wahisani kutoa misaada na kuwapa mikopo?je utabisha hata hilo. ichambue kwa kina bajeti yenu utaona hayo na kuweka majibu yako hapa.

Je unajuwa Deni lenu la Taifa mpaka kufikia April 2014?

Pole sana.
Narudia tena, sasa tufanye bajeti nzima inategemea asilimia 70 wafadhili.
Maswali ya msingi ni haya
1. Katika 30% znz inachangia nini
2. JFC inaendeshwa na mapato ya nchi au ni kutegemea misaada, na wafadhili wakaikataa, muungano utakuwa umekufa?
3. Deni la ndani la nchi, znz inachangia kiasi gani

Haya ndiyo maswali ya msingi.

Narudia kauli za Mchambuzi. Kwa mtu mchumi kama wewe, unapoelekeza kichwa chako katika misaada na mikopo inatisha na inasikitisha sana. Nilidhani ulitakiwa usaidie taifa kuona ni jinsi gani tunaweza kuendeleza nchi zetu kwa kutumia mapato yetu. Kwa masikitiko makubwa mtu aliyewahi kufanya kazi idara ya uchumi ndiye huyu! Kwanini Tanzania ni masikini ? Sina jibu

Narudia tena, hakuna nchi inayojivunia misaada. Kitendo cha wewe kjujikita katika misaada lazima ukione kama ni tatizo la ukoloni na hakika ni ujinga wa hali ya juu kudhani nchi yoyote inaendelea kwa misaada.
Hivyo badala ya kujikita katika hoja laini zinazo adulterate mjadala turudi katika uhalisia kama wananchi wa nchi huru.

Mawazo hayo ya misaada hayana tofauti na yale madai ya mabalozi. Ni lazima tubadili namna tunavyofikiri.
Kiwango chako nadhani ni juu ya hoja unazotoa, na nina imani una uwezo wa kutoa mawazo mazuri ukijitahidi.
 
Mchambuzi,

Kwanza kabisa naomba uniambie ni study gani hiyo iliyosema Znz ilikuwa inachangia 12 Milioni katika muungano bila kutaje TGK inachangia kiasi gani na vile vile Ni kiasi gani kilichokuw kinahitajika? Naomba nieleze nitafatilia kwani uchumi ni kazi zangu na kwa bahti kubwa nilikuwa Wizara ya Fedhwa Muungano kitengo cha bajeti kwa miaka 6.nitaomba unibainishie study hiyo ilifanywa na nani ili niweze itafuta.

Kuhusu alilosema Nguruvi3 la mikopo na misaada. Mimi naomba nikupe kitu live kutoka katika bajeti yenu ya Muungano ya 2014/2015. kama Ulimsikiliza na kuipitia vizuri bajeti yenu iliyosomwa jana na Bi Saada bint Salum ameweka wazi kuwa bajeti yenu ni zaidi ya 19 Trilion na makusanyo yenu yote pamoja na maduhuli yanakadiriwa kufikia chini ya 11 Trillion. Sasa hapo utaona kuna upungufu wa zaidi ya 8 Trikllion.

Na kama utazidi kuichambua zaidi utaona pasa zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ni chini ya 17% , hivyo mnategemea MIKOPO PAMOJA NA MISAADA KWA AJILI YA FEDHWA ZA MAENDELEO KWA ZAIDI YA 80%. au ujaliona hilo?

Sasa kama unajitambua au ukiwa na ilmu kidogo ya uchumi TUNASEMA BAJETI YENU NI TEGEMEZI KWA TAKRIBAN NUSU YA BAJETI MNATEGEMEA IHSAN ZA WAHISANI KWA KUWAPA MISAADA NA MIKOPO NAFUU. Sasa sijui unalielezaje hilo.

Nikirudi kwenye mada napenda nikuulize kama umepitia bajeti ya wizara ya miundombinu ya Mh Magufuri ya 2014/2015 umeona kuwa wamekopa pasa kutoka nje kwa ajili ya barabara ya Tunduru - namtumbo na nyingine kutoka Tunduru kwenda mangaka. lakin vile wanatafuta fedhwa za kukopa kukamilisha barabara ya Mbezi kupitia maramba mawili mpaka kinyerezi. sasa jiulize je barabara hizi zinahusu nini na Znz? kwanini wasikope kwa jina la TGK ili wadaiwe TGK bali wanakimbilia kukopa kwa jina la Tanzania ili Znz nao wahusike na huo mkopo? Je hii uoni kuwa ni dhulma kwa Znz?

Na uoni kuwa ujanja huu ndio unaosababisha JMTz kupata kigugumizi kutekeleza sharia zake ikiwemo hii ya Akaunti ya pamoja chini ya JFC ambayo itahusika tu na mambo ya muungano kama mambo ya ndani, Ulinzi, mambo ya nje na taasisi zake?

Kubwa la mwisho nilitaka nikupe taarifa kuwa Wizara ya fedhwa Si katika wizara za Muungano lakin ndani yake kuna BOT na TRA ambayo ni mambo ya muungano? Je uoni kuwa kuna ukakasi hapo?Lakin hata wizara ya Mao ya ndani ambayo ni ya muungano lakin ndani yake kuna magereza ambacho si kitu cha muungano? Je ukakasi huu mpaka lini?

Kuhusu hii la Utaifa nafikiri hili lipo wazi kabisa kuwa Znz ni nchi na limewekwa kabisa kisharia katika katiba ya Znz.

Nafikiri nimekukidhi kwa majibu yangu lakin kama una zaidi Bismillah

Source ya takwimu za milioni kumi na Mbili Kama wastani wa mchango wa znZ kwa mwaka kwa kipindi cha 1964-1977 ni utafiti uliofanywa na tume ya mabadiliko ya katiba, sio Lipumba Kama nilivyosema awali, niwie radhi kwa Hilo. Nina documents nyingi natumia kwa ajili ya Uzi ninaoandaa juu ya gharama za muungano, nikipata the actual document I will share accordingly.

Hoja kuhusu bajeti ya muungano kutegemea donors kwa asilimia kubwa haijibu hoja yangu ya awali. Aid has been a curse kwa nchi zetu, znZ ilitakiwa washukuru Kwamba kwa kubebwa na Tanganyika wamekwepa laana hii na badala yake wamejifunza kutoka kwa Tanzania na nchi nyingine za afrika. Cha kushangaza, nao wanataka fanya Makosa Yale Yale. Hiyo Ndio ilikuwa hoja ya msingi ambayo haujaijibu.

Kuhusu mikopo ya nje kujenga barabara ya tunduru na kwingineko, huku znZ ikilipishwa Deni lisilomhusu, kwanini unakwepa hoja Kwamba 88% ya Deni la nje la Zanzibar linadhaminiwa na Tanganyika?

Hoja ya akaunti ya pamoja:

Kuna haja ya kujadili variables Tatu kwa Wakati mmoja:

1. Mapato.
2. Matumizi.
3. Mgawanyo.

For some reasons haufanyi hivyo. Katika suala la joint finance commission, changamoto ni Mbili:

Kwa upande mmoja - serikali ya mapinduzi ya znZ inalalamika Kwamba haipati mgao unaostahili kutokana na makusanyo au Mapato ya muungano.

Kwa upande mwingine, upande wa Tanzania bara unasema Kwamba Zanzibar haichangii gharama za muungano.

Je hauoni kwa pande Mbili hizi za hoja tatizo kwa JFC lipo zaidi upande wa znZ? Mapato ya znZ ya sh. Bilioni 400, ni kiasi gani kinaenda Katika matumizi ya muungano?

Kuhusu mgao na malalamiko ya znZ, mgao wa fedha za ndani Hawana shida nao Kabisa kwani makusanyo ya muungano ni ya wote, na ya ZRA ni Yao, huku watanganyika wakiwa Hawana chao Bali cha wote. Kama vile haitoshi kudhaminiwa na Tanganyika fedha za nje by 88%, wanataka zaidi. Hawafikirii na hawajali Kabisa hiyo 88% inalipwa vipi, wanachoona ni barabara za tunduru ambazo mkopo wake unalipiwa na mtanganyika anyways. Tupe ushahidi Hapa juu ya mchango wa znZ Katika kulipa Deni la taifa kwa uwiano sawa na wanachochukua. Sioni mantiki Katika hoja Kwamba Deni la taifa ni la wote lakini kuna miradi Kama hiyo ya barabara Tanganyika ambayo ni uonevu kwa mzanzibari.

Mengine uliyojadili kuhusu mkanganyiko wa mambo ya muungano na yasiyo ya muungano ni hoja ambazo tumekuwa tukizijadili Katika muktadha wa kudai fiscal autonomy ya Tanganyika.

Mwisho nashukuru umekiri Kwamba kuna utaifa wa Zanzibari ambao Kwao ni muhimu kuliko utaifa wa Tanzania.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nimekuuliza swali la muhimu sana, unawezaje kutenganisha mamlaka ya serikali mbili? ZNZ na JMT?
Nani atakayesimamia mambo yasiyo ya muungano?
Kwasasa ndivyo ilivyo, Mkandara amesahau kuwa kufanya hivyo ni kuvaa koti la muungan
Swali lako linaonyesha bado kabisa hujanielewa.. Nimesema hivi:- katika JMT hapatakiwi kuwa na MAMBO YASOKUWA YA MUUNGANO, sasa unaposema nani atasimamia mambo yasokuwa ya muungano nakushangaa ni mambo gani hayo tena ikiwa yote yatakuwa ni ya Muungano?..

Pili mkuu lazima ufahamu mfumo naozungumzia kwanza ili upate kujenga hoja zako. Mambo yote yakisha kuwa ya Muungano ina maana sisi wote ni wahusika wa kila jambo linalotokea kwa manufaa ya Tanzania (JMT), ila kila upande watakakuwa na mamlaka kamii ya kuendesha shughuli zake kutokana na maliasili na rasilimali walizokuwa nazo. Sisi kuwa na reli haina maana haiwahusu Zanzibar, kwa sababu kuna mchango wa kodi ambao utaingia mfuko wa taifa kwa asilimia fulani, mathlan tuseme kodi ni asilimia 19, asilimia 10 ni ya Taifa na asilinmia 10 ni ya nchi (Bara).

Zanzibar nako kuna bandari na meli zake huko pia kutachangia mfuko wa Taifa kwa hiyo waziri wa fedha wa JMT anapowakilisha bajeti yake itatokaa na mapato yalokusanywa toka pande mbili. Zile asilimia 9 kwa kila Upande ndizo hazitahusiana na JMT ila kwa sehemu walizokusanya.Huu ndio muundo unaotakiwa yaani kuweze kutenganisha pato la kila nchi (upande) na pato la Taifa.

Zanzibar waendelee kuwa kama walivyo na bunge lao, serikali yao, na mahakama zao kama ilivyo ili waweze kuwa na mamlaka ya kuendesha shughuli za serikali yao na sisi tutaendelea kulitumia wizara zetu kuwa na mamlaka ya kuendesha mambo ya JMT na yale ya Tanganyika kama tunavyoweza kuendesha shughuli za wizara 22 za muungano.

Kwa hiyo wizara zote za JMT ni lazima zituhusu sote isipokuwa usichotaka kuelewa ni nani atasimamia shughuli za uendeshaji wa serikali hizi 2 yaani ya Zanzibar na Tanganyika?JMT .. hili ndio swali na majibu yake ni kutazama kwanza serikali za wenzetu zimeweza vipi kuwa namambo yote ya Muungano isipokuwa mamlaka ya shughuli za serikali yameachwa kwa nchi husika. Shughuli zote za kuendesha serkali ya Ontario zinafanywa na viongozi wa Ontario ambao hawahusiki na uendeshaji wa shughuli za majimbo mengine, lakini viongozi wa serikali ya Canada wanahusika na kila jambo linaloihusu wizara yake canada nzima.

Hata Askari Polisi wapo wa Ontario tu na wapo wa RCMP wakihusika na shughuli za Canada nzima. Hawa wenzetu wana uwezo mkubwa wa kuwa na viongozi kila nchi kila jimbo na kila kata lakini sisi sidhani kama tunahitaji viongozi wengi kiais hicho. Na pia wakati haupo nasi maana mwaka 2015 ni kesho tu tunaweza jikuta hatuna katiba na hakuna lilofanikiwa..

Na jibu langu ni kwamba kila upande utasimamia uendeshaji wa shughuli za serikali zake kama tunavyoweza leo kusimamia mambo ya muungano 22 kwa bara. Ikiwa leo waziri wa fedha wa JMT ni waziri wa fedha na mawaziri wengine 21 ni wasimamizi wa shughuli za serikali ya JMT (Tanganyika na Zanzibar) basi haitakuwa tatizo mawaziri wengine wote kusimamia shughuli zote za JMT. Sijui umenielewa?.

Labda nikupe mapendekezo yangu japo yanaweza kuwa hayapendezi.. Waziri mkuu atachaguliwa na wananchi kupitia kura za bara hivyo anakuwa kiongozi wa serikali ya bara, na rais mwenyewe ndiye atatakiwa kuwa kiongozi wa serikali ya JMT hivyo kila bunge la JMT lazima rais awe na mwakilishi kwa niaba yake (waziri ofisi ya rais) ama yeye mwenyewe kuhudhulia vikao vya bunge la JMT. Hivyo kila waziri atakaye teuliwa na rais atakuwa waziri wa serikali ya JMT, na manaibu waziri wote watakuwa wasimamizi wa serikali ya tanganyika hawa watachaguliwa na waziri mkuu (i.e Pinda).

Kwa nini nashauri hivi, ni kwa sababu tukikubali kuunda serikali ya Tanganyika ina maana tutahitaji kuwa na bunge lake pekee kwa majimbo yote sijui ni mangapi halafu tuwe na uchaguzi wa bunge la JMT, kwa hiyo tutakiwa kuwa na mawaziri wa serikali ya JMT na mawaziri wa serikali ya Tanganyika. Tutatakiwa kuwa na makazi ya mawaziri wa serikali ya tanganyika na mawaziri wa serikali ya JMT. Tutatakiwa kuwa na mabunge mawili moja la JMT na jingine la serikali ya Tanganyika na kadhalika..Kwa kuchelea kazi hii ngumu na muda tulokuwa nao leo ndio maana napendekeza tuendelee na hizi serikali 2 lakini tukubali kuweka mambo yote yawe ya Muungano. na Usimamizi wake utafanywa na watu wale wale walioko ktk madaraka leo maana tayari tuna mawaziri na manaibu karibu kila wizara ya serikali ya JMT.

Hivyo sikatai kuwa na serikali 3 hata kidogo ikiwa tu swala la kwanza litatazamwa nalo ni kuhakikisha kwamba serikali ya JMT inabeba mambo yote kuwa ni ya Muungano hakuna kisichokuwa cha Muungano isipokuwa usimamizi wake ndio kila upande utajitegemea kuendesha shughuli hizo. Mwanzo kutakuwa confusion lakini ifahamike tu ya kwamba kwa kila kodi inayokusanywa kuingia mfuko wa taifa ni pato la JMT sii la bara wala Znz na kile kinachokuswanywa kwa asilimi 9 ni pato la upande unaohusika.

Kifupi mkuu wangu ungeweza kusoma ama kuelewa jinsi gani hawa wenzetu wanaendesha serikali zao na kwamba hakuna jambo ambalo sii la Muungano isipokuwa sheria. Na ndio maana unaweza kuta jimbo moja wanaruhusu Ushoga na jingine hawaruhusu, ukakuta jimbo moja wanajiunga na Jumuiya zenye asili nao na kwingine wakajiunga na Jumuiya tofauti lakini zile za Kitaifa zinawahusu wote. Hivyo unapoisoma katiba ya Muungano wao huwa inawahusu wote. Wenye matatizo ni Zanzibar, sisi maadam katiba iitungwa kwa maslahi ya Watanganyika kama ilivyokuwa ya mwaa 1977 sioni sababu ya kuanza mwanzo kuitaka tanganyika kwa sasa hivi... Ebu pitia kipande hiki ujue nini maana ya Muungano http://www.know-britain.com/general/great_britain.html
 
Mkuu Mkandara
Nimekusoma hapo juu. Kwanza nikueleze kuwa nchi za wenzetu mifumo yao si kuwa tunaielewa kwa kuisoma, tumeishi na tunaiafahamu vema. Mfumo unaopendekeza ndio ambao Warioba alipendekeza katika rasimu ya kwanza.
Ninyi mkasema serikali itakuwa kubwa mno, majeshi matatu n.k. bila kufahamu kuwa hapo Ontario kuna RCMP, OPP, na City police kama Toronto, Durham, Peel na Vaughan. Mlikataa mfumo huo kwa kudanganywa na akina Nape, leo mnaushari tena.

Pili, suala la mambo yote ya muungano nalo unaongelea mbele-nyuma.
Tulikuwa na 22 tukielekea kuwa na yote, ukawa shuhuda wa kuvaa koti.
Leo wznz wanataka hadi uraia, unadhani tunaweza vipi katika hali iliyopo.

Tatu, kuna kitu umekitaja kama 'nchi ya bara'. Kwakukusoma unajaribu tu kukwepa jina Tanganyika, lakini maana yako ni hiyo.
Unaposema eti waziri mkuu achaguliwe na watu wa bara, huyu atakuwa kiongozi gani asiye na vyombo kama bunge, mahakama na serikali yake kama Rais wa ZNZ?

Tena unasema manaibu mawaziri ndio wafanye kazi kwa niaba ya Tanganyika. Hawa watawajibika kwa waziri mkuu.
Sijui watafanya vipi kazi ikiwa hawana nyenzo za kufanyia kazi kama bunge.

Hawa mawaziri watapata wapi fungu la kuendesha shughuli zao. Ukisema waombe JMT huoni tayari ni kuvaa koti la muungano.
It is impossible kuwa na waziri tu aliyechaguliwa na pinda asiyejua anafanya kazi kwa serikali gani.

Tena mfumo unaopendekeza ukiuangalia kw aundani ndio uliopo. Katibu mkuu wa wizara anafanya nini katika muungano?

Unachokipendekeza ndicho CCM wanapendekeza. Kwasasa wamekwama kama utakavyokwama kujibu kwasababu ni kituko kuwa na mawaziri wa muungano ukawaita wa Tangayika, wakachota fungu JMT ukalalamika wamevaa koti.
Mkandara huwezi kuwa na serikali ya Pinda tu, unakuwa na serikali ya wananchi.

Hata mantiki haikubaliani na ushauri wako. Kwanini waziri anayeteuliwa na Pinda awe naibu?
Ni naibu wa nani ikiwa ameteuliwa na waziri mkuu aliyechaguliwa. Nani yupo juu ya huyu naibu, waziri mkuu au waziri wa serikali ya muungano? Kwanini mawaziri wa znz wasiwe manaibu kama wale wa Pinda. Mkuu hapa huoni kuna tatizo kweli!

Unachosema hapa ni kuwa kutakuwa na manaibu mawaziri wanaoshughulikia nchi unayoiita ya 'bara'
Logic inakukataza usitumie Tanzania, na unajua hilo.

Mantiki inakataa kuwa hakuna naibu wa kushughulikia mambo ya bara akiwa naibu wa waziri wa muungano.

Mkuu Mkandara, unachoogopa wewe ni kuwepo kwa Tanganyika kwa woga kuwa znz haitakuwa na mteremko iliyo nao.
Huwezi kuwalaumu Watanganyika waliokubali hali hiyo kwa miaka 50. Thanks to Zanzibar waliowashtua Watanganyika.

Hapa tulipo Tanganyika haikwepeki, mtaikwepa katika maandishi kiuhalisia hamtaweza.

Na mwisho, Mkuu hatuhitaji katiba ya 2015. Tunahitaji katiba itakayobadili mwelekeo wa nchi.
Bila kujali lini itapatikana, jambo muhimu ni kufuata mantiki, kuwa wakweli na kukubali kuwa dunia inavyobadilika ndivyo tunavyopaswa kubadilika.

Leo mkuu wa Intelligence anajulikana kwa jina, na anapoishi. Huko nyuma hakuna aliyejua kuwa Kitine alikuwa chief of intelligence.

Leo FBI na CIA wana twitter account, huko nyuma hata kutaja tu ilionekane taboo.
Hii ina maana moja, mabadiliko ni jambo lisilozuilika. Na kwa suala la Tanganyika ambayo imeumia sana na huu muunga , changes are inevitable.

Any attempt to stop Tanganyika, is a step toward anarchy and xenophobia.
Zanzibar is prone and vulnerable for the same.

The situation is down the hill, spiraling at supersonic speed.
The return of Tanganyika is the only cushion Zanzibar can use in this volatile environment, otherwise, people of ZNZ will absorb the maximum heat and pay dear price.
 
Kuhusu mgao na malalamiko ya znZ, mgao wa fedha za ndani Hawana shida nao Kabisa kwani makusanyo ya muungano ni ya wote, na ya ZRA ni Yao, huku watanganyika wakiwa Hawana chao Bali cha wote. Kama vile haitoshi kudhaminiwa na Tanganyika fedha za nje by 88%, wanataka zaidi. Hawafikirii na hawajali Kabisa hiyo 88% inalipwa vipi, wanachoona ni barabara za tunduru ambazo mkopo wake unalipiwa na mtanganyika anyways. Tupe ushahidi Hapa juu ya mchango wa znZ Katika kulipa Deni la taifa kwa uwiano sawa na wanachochukua. Sioni mantiki Katika hoja Kwamba Deni la taifa ni la wote lakini kuna miradi Kama hiyo ya barabara Tanganyika ambayo ni uonevu kwa mzanzibari.

Mengine uliyojadili kuhusu mkanganyiko wa mambo ya muungano na yasiyo ya muungano ni hoja ambazo tumekuwa tukizijadili Katika muktadha wa kudai fiscal autonomy ya Tanganyika.

Mwisho nashukuru umekiri Kwamba kuna utaifa wa Zanzibari ambao Kwao ni muhimu kuliko utaifa wa Tanzania
Mkuu huyu jamaa hana hoja, anajaribu kujenga hoja zake kitoto sana.
Tumemuuliza kuwa kama bajeti ni misaada asilimia 50, je hiyo asilimia 50 iliyobaki znz inachangia kiasi gani katika muungano. Hana jibu. Tukamwambia hiyo JFC inaendeshwa kwa misaada na kama ni hivyo, wafadhili wakikataa itakuwaje? Hana jibu. Anachokifanya ni kubadili mjadala kwa mambo trivial.

Ni trivial kwasababu hawezai hata kuyatetea. Mfano, anaongelea waziri Magufu kuzungumzia barabara za Tanganyika na kwamba hizo pesa ni za kukopa kwa jina la Tanzania. Mtu huyu ambaye ni mchumi kama Mwigulu, alipaswa kwanza kuangalia bajeti ya znz kabla hajasema hayo.

1. Bajeti ya mwaka huu ni Bilioni 700. Mapato ni Bilioni 400. Angejiuliza nani anafidia bilioni 300 kwanza.

2. SMZ inapokosa mishahara na kuchukua hazina, hiyo inamsaidia nini mtu wa mwanza ili hali ni nchi jirani ya znz

3. Huyu mtu anaongelea bajeti ya magufuli ambayo ni ndogo sana. Hebu ajiulize 1.1. Trilion, bajeti ya ulinzi, znz inachangia kiasi gani. Mbona haongelei hilo na bajeti hiyo.

4. Mwezi wa kwanza JMT ilitoa bilioni 11 kwa umeme wa kwenda Pemba. Pesa hizo zimeyoka fungu gani la muungano analojua yeye. Kumbuka kuwa znz ilishindwa na kuomba msaada. Umeme wa nchi ya znz unamhusu nini mnyamwezi

5. Gharama za wale watalii pale Dodoma nani anabeba. Wabunge wa nchi ya znz wanamhusu nini myao wa Tunduru.

6. Wale wanafunzi 1700 wanaosoma bure, wanamhusu nini Mha au mhaya wa Kagera ikiwa wametoka nchi ya znz.

Orodha ni ndefu sana, tatizo ni kuwa uwezo wa kujadili kwa wenzetu ni mdogo sana.
Hiyo JFC anazungumzia misaada baada ya kujadili
1. Mapato
2. Matumizi
3. Mgawanyo

Ndiyo maana nimemwambia kama ana hoja alete au ajibu, kama hana ni vema akae kimya asivuruge mjadala.
 
Barubaru
Ili kuweka sawa mjadala, tukumbushe kuwa suala la JFC lipo katika premise hizi
1. Mapato
2. Matumizi
3. Mgawanyo

Nje ya hapo,hakuna hoja nyingine itakayoeleweka.
 
Last edited by a moderator:
Source ya takwimu za milioni kumi na Mbili Kama wastani wa mchango wa znZ kwa mwaka kwa kipindi cha 1964-1977 ni utafiti uliofanywa na tume ya mabadiliko ya katiba, sio Lipumba Kama nilivyosema awali, niwie radhi kwa Hilo. Nina documents nyingi natumia kwa ajili ya Uzi ninaoandaa juu ya gharama za muungano, nikipata the actual document I will share accordingly
.

Najuwa siku zote unapojadili jambo ni lazima ujikite kuonyesha TGK ilichangia kiasi gani na JMTz ilichangia kiasi gani? kwani kwa kutofanya hivyo utakuwa wewe mwenyewe unajiweka njia panda na kujionyesha kuwa ni mshabiki tu hua hoja muhimu hapo.
Binafsi nitashukuru sana kama utaweka uzi maalum kwani mimi nitakuwa mchangiaji mkuu katika mada hii kwani mimi si tu kushiriki katika baadhwi ya vikao hivyo vya Wizara ya Fedhwa muungano lakin pia nilikuwa kwa miaka 6 hivyo najua mengi sana. Nitasaidia kuchangia . Nakusubiri kwalo.

Hoja kuhusu bajeti ya muungano kutegemea donors kwa asilimia kubwa haijibu hoja yangu ya awali. Aid has been a curse kwa nchi zetu, znZ ilitakiwa washukuru Kwamba kwa kubebwa na Tanganyika wamekwepa laana hii na badala yake wamejifunza kutoka kwa Tanzania na nchi nyingine za afrika. Cha kushangaza, nao wanataka fanya Makosa Yale Yale. Hiyo Ndio ilikuwa hoja ya msingi ambayo haujaijibu.

Kuhusu mikopo ya nje kujenga barabara ya tunduru na kwingineko, huku znZ ikilipishwa Deni lisilomhusu, kwanini unakwepa hoja Kwamba 88% ya Deni la nje la Zanzibar linadhaminiwa na Tanganyika?

Kama nilivyobainisha hapo juu kuwa zaidi ya 42% ya Bajeti kuu ya JMTz inategemea ufadhwili kutok nje kwa njia ya mikopo na misaada. Hilo nafikiri lipo wazi. Pitia bajeti ya JMTz ya mwaka 2014/2015 inayojadiliwa hivi sana utaona wazi kabisa kuwa makisio yenu ya bejeti hiyo ni zaidi ya 19 Trilion na makusanyo yenu ni chini ya 12 Trilion, hivyo zaidi ya 8 Trilion zinategema ufadhwili huo wa misaada na mikopo. Sasa ahali yangu sijui inachobisha ni nini tena hapa? au unafikiri kuna siasa katika uchambuzi wa kiuchumi zaidi ya numbers kuonyeshwa dhwahir shahir.

Kuhusu hili la zaidi ya 88% ya deni la Znz lnadhaminiwa na TGK. Hili nafikiri imekupuruchuka rafiki yangu. Deni hilo linadhaminiwa na Tanzania. Ikimbukwe kuwa Tz ni muungano wa nchi mbili TGK na Znz. Na mas'ala yate ya mahusiano ya kimataifa yapo chini ya muungano ambao ni Tz. Hivyo Znz kutokana na makubaliano hayo haiwezi kabisa kwenda kukopa nje bila kupitia Muungano kwani wenyewe ndio wenye dhamana ya kusaidia hilo ikiwemo pamoja na kudhamini mikopo yote.

Lakin cha kukuongezea hapa vile vile kumbuka TGK inadaiwa mikopo kutoka nje mpaka kufikia 30th April 2014 zaidi ya 36 Trillion na taasisi mbalimbali za kimataifa na mataifa mbalimbali duniani. Na deni hilo lote kwa 100% limedhaminiwa na Tanzania. Je unalitambua hilo?

Hoja ya akaunti ya pamoja:

Kuna haja ya kujadili variables Tatu kwa Wakati mmoja:

1. Mapato.
2. Matumizi.
3. Mgawanyo.

For some reasons haufanyi hivyo. Katika suala la joint finance commission, changamoto ni Mbili:

Kwa upande mmoja - serikali ya mapinduzi ya znZ inalalamika Kwamba haipati mgao unaostahili kutokana na makusanyo au Mapato ya muungano.lakin kubwa zadi hapo ni Znz kulalamika kuwa TGK inakwenda kukopa nje kwa jina la Tz katika mambo yasiyo ya muungano na hivyo deni hilo kudaiwa wadau wote wa muungano huo ikiwemo Znz.(nimeongeza mimi)

Kwa upande mwingine, upande wa Tanzania bara unasema Kwamba Zanzibar haichangii gharama za muungano.

Je hauoni kwa pande Mbili hizi za hoja tatizo kwa JFC lipo zaidi upande wa znZ? Mapato ya znZ ya sh. Bilioni 400, ni kiasi gani kinaenda Katika matumizi ya muungano?

Kuhusu mgao na malalamiko ya znZ, mgao wa fedha za ndani Hawana shida nao Kabisa kwani makusanyo ya muungano ni ya wote, na ya ZRA ni Yao, huku watanganyika wakiwa Hawana chao Bali cha wote. Kama vile haitoshi kudhaminiwa na Tanganyika fedha za nje by 88%, wanataka zaidi. Hawafikirii na hawajali Kabisa hiyo 88% inalipwa vipi, wanachoona ni barabara za tunduru ambazo mkopo wake unalipiwa na mtanganyika anyways. Tupe ushahidi Hapa juu ya mchango wa znZ Katika kulipa Deni la taifa kwa uwiano sawa na wanachochukua. Sioni mantiki Katika hoja Kwamba Deni la taifa ni la wote lakini kuna miradi Kama hiyo ya barabara Tanganyika ambayo ni uonevu kwa mzanzibari.

Mengine uliyojadili kuhusu mkanganyiko wa mambo ya muungano na yasiyo ya muungano ni hoja ambazo tumekuwa tukizijadili Katika muktadha wa kudai fiscal autonomy ya Tanganyika.

Mwisho nashukuru umekiri Kwamba kuna utaifa wa Zanzibari ambao Kwao ni muhimu kuliko utaifa wa Tanzania.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Kuhusu hili la akaunti ya pamoja ya fedhwa na uchumi ya Muungano. Hii nafikiri hatuna haja ya kuijadili sana kwani ilishajadiliwa na Bunge toka mwaka 1996 tena Bnge la Muungano la JMTz na SIO baraza la wawakilishi.

Kumbuka kuwa katika Bunge la Muungano la JMTz ambalo ndanimwe kuna zaidi ya 80% ya wabunge wake wametoka Tgk iliipitia sharia hii mwaka 1996 na kuipitisha bila kikwazo chochote kutoka upande wowote wa muungano na wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala waliipitisha bila mushker wowote.

Waliichambua kwa kina sana na kuangalia kwa uzito wake malalamiko makubwa yanayotolewa na nchi zote mbili kuhusu mambo mbalimbali a kiutawala na kiuchumi na mwisho kukubaliana kuanzishwa kwa TUME YA PAMOJA ya uchumi na fedhwa ( Joint Finance Commission ) JFC na kuita wataalamu kuchambua kero hizo za muungano na kuja na mapendekezo yake Serikalini JMTz.

Bunge la Muungano la JMTz likakubali na kupitisha Katika katiba Ibara ya 133 kuhusu kuanzishwa kwa Akaunt ya pamoja ya fedhwa itakayoshughulikia mambo ya Muungano TU na akaunti hiyo ingesimamiwa na JFC na hivyo kuziacha wizara ya fedhwa TGK kujihusisha na mambo ya TGK na ile wizara ya fedhwa Znz kujihusisha na mambo ya Znz na hivyo kuondoa kero hizo za muungano kama ulivyoainisha katika bandiko lako na nyingine ambazo hujaziweka hapo.

Hiyo ni kwa ufupi sana nakukukumbusha kwa mara nyingine tena.

lakin suala la msingi hapa ni KWANINI SERIKALI YA JMTZ INAKATAA KUTEKELEZA SHARIA HII A KUANZISHWA KWA AKAUNTI YA PAMOJA FEDHWA ZA MUUNGANO CHINI YA JFC?

Kumbuka kuwa tunapoita Sharia maana yake imejadiliwa kwa kina sana na Serikali yenyewe kabla kupelekwa muswada Bungeni na baadae wawakilishi wa wananchi Bungeni kwa maana WABUNGE tena zaidi ya 80% kutoka TGK kuijadili kwa kina sana na kuikubali na kisha Rais wa JMTz kuitia saini yake kuwa Sharia na sasa kusubiri tu utakalezaji wake.

Tujiulize KWANINI SERIKALI YA JMTZ INAPATA KIGUGUMIZI KUTEKELEZA SHARIA HIYO?

lakin nafikiri tungeanzia hapa katika mada hii. KWANINI SERIKALI YA JMTz ilipeleka muswada huu (wa Akaunti ya pamoja ya fedhwa za muungano kusimamiwa na JFC) Bungeni na wabunge wa JMTz kuujadili na kuupitisha?

Nasubiri jibulako hapa.

Cc. Pasco
 
Mkandara;9801304]Pili mkuu lazima ufahamu mfumo naozungumzia kwanza ili upate kujenga hoja zako. Mambo yote yakisha kuwa ya Muungano ina maana sisi wote ni wahusika wa kila jambo linalotokea kwa manufaa ya Tanzania (JMT), ila kila upande watakakuwa na mamlaka kamii ya kuendesha shughuli zake kutokana na maliasili na rasilimali walizokuwa nazo. Sisi kuwa na reli haina maana haiwahusu Zanzibar, kwa sababu kuna mchango wa kodi ambao utaingia mfuko wa taifa kwa asilimia fulani, mathlan tuseme kodi ni asilimia 19, asilimia 10 ni ya Taifa na asilinmia 10 ni ya nchi (Bara).

Zanzibar nako kuna bandari na meli zake huko pia kutachangia mfuko wa Taifa kwa hiyo waziri wa fedha wa JMT anapowakilisha bajeti yake itatokaa na mapato yalokusanywa toka pande mbili.
Zile asilimia 9 kwa kila Upande ndizo hazitahusiana na JMT ila kwa sehemu walizokusanya.Huu ndio muundo unaotakiwa yaani kuweze kutenganisha pato la kila nchi (upande) na pato la Taifa.
Mkuu Mkandara , mfumo unaopendekeza ni ule wa HST ambapo 13% ingawanywa kati ya majimbo na serikali kuu.

Tulianza kuwa na mfumo huo, Wazanzibar wakalalamika na sasa hivi TRA inakusanya mapato znz na kuyaacha huko huko.
Mapato ya Tanganyika ndiyo yanatumika katika muungano ikiwemo kufidia bajeti ya znz, bill zake na deni la nje na ndani.
Iweje leo uone Mtanganyika ndiye 'tatizo' na kutia macho yako upofu wa chanzo halisi cha tatizo?

Unashangaza unapotumia neno kila upande. Kuna upande mmoja tu mkuu ambao ni znz. Upande wa pili hauna eneo ndiyo maana kila mara unasema wznz wananyonywa na JMT. Tunachotaka ni kuwa na pande mbili zinazoeleweka na si kufikirika.

Kwa sasa znz ina mapato ya 400 Bilioni. Je, huduma zitagawanywa kwa kuzingatia kigezo gani ili znz ione haionewi?

Nakushangaa mkuu unavyobadili position. Ni wewe Mkandara upo katika rekodi ukikosoa rasimu ya kwanza ya katiba iliyokuwa na serikali kuu yenye mambo mengi ya pamoja. Ulisema serikali ya shirikisho itakuwa kubwa sana na hakuna sababu za kuwa na viongozi wengi na gharama kubwa. Leo unapendekeza kile kile ulichokikataa awali tena ukimsumanga Warioba. Unasema hayo ni mawazo na si maoni yake, kumbe basi yalikuwa na mantiki sana hukusema.

Unaosema Tanganyika itumie wizara za muungano kufanya mambo yake, nawe kama barubaru mnakwepa ukweli mchungu. Utawezaje kufanya mambo katika ofisi ya muungano ukakwepa koti la muungano?
Unawezaje kufanya kazi ukiwa huna structure. Kwamba, anaamka mtu asubuhi na kufanya mambo ya Tanganyika hata kama hatumjui. Hakuna structure inayo define mambo yalivyo.

Wakati unashauri kuwa na ofisi za Tanganyika katika ofisi za muungano, unakimbia upande wa pili na kusema Tanganyika imevaa koti.

Labda nikuulize, kuna tatizo gani Zanzibar ikawa na mambo yake kama ambavyo Tanganyika itakuwa nayo?
Nini ulazima wa Tanganyika kutokuwepo hadharani. Kimantiki unakubali uwepo wa Tanganyika, lakini hutaki kutaja hilo, nini hekma yako kuficha ukweli huo.
 
Last edited by a moderator:
Barubaru
Ili kuweka sawa mjadala, tukumbushe kuwa suala la JFC lipo katika premise hizi
1. Mapato
2. Matumizi
3. Mgawanyo

Nje ya hapo,hakuna hoja nyingine itakayoeleweka.

Nguruvi3,

Ahali yangu unanung'unika saaaaaana bila kujua hata muh'tadhwa wenyewe umesimamia wapi.

Labda nikusaidie kidogo hapo. Hayo ulioeleza hapo juu ndio msingi mkubwa sana wa Kero za Mvungano wenu. Na ndio yanayojengewa hoja na kila nchi katika kuthibitisha hoja zao. Kumbuka hayo yanaweza jengewa hoja katika sehemu kuu tatu:
1. mapato ya makusanyo ya ndani
2. mapato kutokana na misaada
3. mapato kutokana na Mikopo

Lakin pia matumizi ya kila nchi katika muungano na mgawanyo wake kwa stahiki husika kwa kila nchi mshirika wa muungano wenu.

Mambo hayo ndio yaliokuwa chachu kwa Serikali a JMTz kuandaa muswada na kuupeleka Bungeni mwaka 1996 ili ukajadiliwe na wabunge wa Muungano ambao zaidi ya 80% wanatoka TGK nao kwa pamoja wakaupitisha na Rais wa JMTz enzi hizo Mh Mkapa akaridhia na kuwa sharia ya kuanzishwa kwa JFC.

Sasa laazima uelewe kuwa JFC haikupitishwa na BLW Znz au kupitishwa kwa mlango wa nyuma. Na moja ya majukumi yake yamewekwa katika Katiba ya Muungano ya JMTz ibara ya 133 , na SIO katiba ya Znz katika. kuelekeza kuanzishwa kwa akaunti ya pamoja ya fedhwa za muungano na akaunti hiyo itasimamiwa na kuratibiwa na JFC.

Sasa labda nikuulize,

KWANINI SIRIKALI YA JMTz ilipeleka muswada wa kuundwa kwa JFC Bungeni? Na kwanini wabunge wa JMTz ambao zaidi ya 80% wanatoka Tanganyika walipitisha muswada huo na hatimaye kuwa sharia?

Kwanini Serikali ya JMTz inapata kigugumizi kutekeleza sharia hiyo iliyopitishwa na Bunge na kuridhiwa na Rais wake wa JMTz?

Naomba kama majibu yako hapa.

Cc mzee mwanakijiji, Pasco, Ritz, Bobuk, Gombe sugu, The Big Show

Narudia tena, sasa tufanye bajeti nzima inategemea asilimia 70 wafadhili.
Maswali ya msingi ni haya
1. Katika 30% znz inachangia nini
2. JFC inaendeshwa na mapato ya nchi au ni kutegemea misaada, na wafadhili wakaikataa, muungano utakuwa umekufa?
3. Deni la ndani la nchi, znz inachangia kiasi gani

Haya ndiyo maswali ya msingi.

Narudia kauli za Mchambuzi. Kwa mtu mchumi kama wewe, unapoelekeza kichwa chako katika misaada na mikopo inatisha na inasikitisha sana. Nilidhani ulitakiwa usaidie taifa kuona ni jinsi gani tunaweza kuendeleza nchi zetu kwa kutumia mapato yetu. Kwa masikitiko makubwa mtu aliyewahi kufanya kazi idara ya uchumi ndiye huyu! Kwanini Tanzania ni masikini ? Sina jibu

Narudia tena, hakuna nchi inayojivunia misaada. Kitendo cha wewe kjujikita katika misaada lazima ukione kama ni tatizo la ukoloni na hakika ni ujinga wa hali ya juu kudhani nchi yoyote inaendelea kwa misaada.
Hivyo badala ya kujikita katika hoja laini zinazo adulterate mjadala turudi katika uhalisia kama wananchi wa nchi huru.

Mawazo hayo ya misaada hayana tofauti na yale madai ya mabalozi. Ni lazima tubadili namna tunavyofikiri.
Kiwango chako nadhani ni juu ya hoja unazotoa, na nina imani una uwezo wa kutoa mawazo mazuri ukijitahidi.

Nguruvi3,

Awali ya yote. napenda nikusaidie mambo machache hapa.

Deni la ndani ya nchi yenu ni LAAZIMA KILA MTU ALIPE KILE ALICHOKOPA. Znz wameainisha katika bajeti yao 88% ya deni lao limedhaminiwa na Muungano. Hivyo Znz watatakiwa walilipe hilo.

Na vile Deni la TGk ambalo mpaka kufikia 30th April 2014 walikuwa wanadaiwa zaidi ya 36 Trilion li laazima lilipwe na TGk wenyewe ingawa deni hilo limedhaminiwa na Muungano.

Kila mtu abebe furushi lake mwenyewe.

Tukija hili la bajeti zenu na taaluma yangu ya Uchumi. nafikiri nililiweka wazi kabisa kule katika uzi tulijadili sana na wewe wenye anuani ya KWANINI 21% YA AJIRA ZA MUUNGANO ZIPELEKWE ZNZ?

Lakin kwa faida ya wengine katika Uzi huu. Mimi binafsi sipendezwi na najua katika nadharia yoyote ya kiuchumi mfumo mnaotumia katika BAJETI zenu umepitwa na wakti. Mfumo mnaotumia ni CASH bajeti yaani mnaweka makadirio yenu ya mapato na matumizi kwa mwaka kisha kupitisha bajeti hizo. sasa inapokuja katika utekelezaji wake yaani makusanyo yenu yanakuwa hapa na yanatoka taratibu sana kiasi cha kufanya miradi yenu ya maendeleo kukwama.

mathalan mwaka 2013/2014, Ni kiasi cha 28% to 32% cha makadirio ya matumizi ya wizara zenu ndio yaliweza kupatikana kwa mwaka mzima. Na utaona pesa hizo walizopata zilitumika katika kulipa Mishahara, Chai, mafuta na matengenezo ya magari ya wakuu, Posho za safari na semina na uendeshaji wa Afisi. Ukitazama kwenye miradi ya maendeleo hakuna hata wizara moja iliyoweza kutekeleza zaidi ya 8% ya makadirio yake.

Na hata bajeti ya mwaka huu 2014/2015 ipo the same. Sioni kama mna nia ya dhati kujikwamua katika kujiondoa na huu UTEGEMEZI katika bajeti zenu kwani hakuna target maalum na mikakati maalum katika kujiondoa kwalo. Matokeo yake ukijitazama kiuchumi mnaona wazi kuwa mfumo huo wa CASH najeti utazidi kuwaweka masikini na kuzidi kuwa watu wa kutembeza bakuli ili kukidhi bajeti zenu.

Nilibainisha kidogo tu ili mjikwamua mnatakiwa muende kwenye CAPITAL BAJETI. Hii maana yake baada ya kutengeneza bajeti zenu Serikali inakwenda kukopa pesa hizo katika taasisi mbalimbali za kimataifa na kuzilipa wizara kwa wakti. Hili litasaidia sana wizara na idara za Serikali kutekeleza mipango yake kwa wakti na bila kusuasua na kupunguza ghara za miradi kukwama na kuongezeka thamani. Lakin katika mfumo huu Serikali itatumia makusanyo yake ya ndani na nje kulipia mikopo katika taasisi hizo.

Kubwa ninaloweza kubainisha mfumo wa capita bajeti unahitaji zaidi uzalendo, uwajibikaji na ubunifu mkubwa vyanzo vya mapato na usimamizi mzuri wa matumizi ya Serikali.

nafikiri nitakuwa nimekujibu kwa mara nyingine tena. lakin kama una suala lolote basi Bismillah

CC: JokaKuu

Mkuu ni ngumu sana kumwelewa Mkandara .
Anabadilisha position kila uchao. Ukifuatilia kwa undani ni ngumu kuelewa anatetea nini hasa.

Mkandara anasema Tanganyika imevaa koti la muungano na hivyo Zanzibar inaonewa.
Halafu Mkandara huyo huyo anasema kuna mambo yameingizwa kinyemela katika muungano. Hayakuwepo.

Tukimwambia sawa sasa tuvue koti kwa kutenga mambo ya znz na Tanganyika, anasema znz itapata hasara.
Kama ni hivyo koti gani ambalo znz inalalamika lakini haitaki livuliwe? Mkandara anabadili upepo na kusema tunawaonea sana.
Turudishe Tanganyika, hataki. Tubaki na Tanzania , anasema tunavaa koti. Nini tufanye? anashauri tuendelee kukamua wananchi wetu kodi na wznz wanemeeke ili muungano ushamiri.

Mkandara anasema, ni haki mambo yote yawe ya muungano ila utekelezaji wake uwe na mamlaka tofauti.
Akiambiwa mamlaka hizo ni zipi, anasema ni JMT na Zanzibar

Tumemuuliza JMT ni nchi gani, akasema ni Tanganyika ambayo imegeuza mamlaka yake kuwa JMT.
Tukamuuliza sasa kama Tangayika ndiyo Tanzania, koti la muungano lipo wapi?
Anajibu hapana Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar.

Akiulizwa sasa mambo ya muungano na yasiyo ya muungano unayetenga vipi Tanganika ikiwa kuna JMT na Zanzibar.
Jibu la Mkandara ni kuwa lazima yasiyo ya muungano yatengwe na ya muungano.
Tukamuuliza chombo gani kisimamie yasiyo ya muungano, akasema Tanzania bara iwe na mambo yake.

Tanzania bara si ndiyo Tanganyika? Mkandara anasema Tanganyika ilishakufa.
Tukarudi nyuma kumuuliza kama ilishakufa wapi alipata JMT yenye Tanganyika na ZNZ na kwanini Tanganyika ilifutika.
Mkuu anasema tunataka tuwe taifa moja.

Tunamuuliza lakini znz wana utaifa wao, mkandara anasema hilo si tatizo, tatizo ni utaifa wa Tanganyika.
Haa! kwanini Tanganyika iwe nongwa kama tunataka kuwa na Taifa moja?

Mkandara anasema Taifa linalojulikana ni Tanzania. Hatukuwa na utaifa wa Tanganyika kwasababu Nyerere alikuwa anaujenga. Tukamuuliza, kama muungano usingekuwepo tungekuwa taifa gani. Jibu, tungekuwa taifa la Tanganyika.

Analalamika kwanini wznz hawaruhusiwi kujadili mambo ya Tanganyika.
Katika mkanganyiko huo, amefikia mahali anasema sisi ni taifa moja na wanaotaka kuvunja muungano ni Waanzibar wa Hizbu. Mkandara hataki kukubali kuwa katiba ya znz ni ya wznz na wala haikuandikwa na Hizbu.

Katiba hiyo inasema znz ni nchi yenye serikali na utaifa wa zanzibar na si Tanzania ikiwa na vyombo kamili kama nchi huru.
Ukweli wa katiba Mkandara haugusii kabisa.

Mkandara anashauri tufunge bandari zetu ili ile ya znz ifanye kazi kwa ufanisi. Asichokisema ni kuwa bandari si suala la muungano tena na waliokimbiza ni wazanzibar hao hao anaotaka wapewe kipaumbele kwa kile wasichokitaka kushiriki.

Mkuu Mkandara anasema misaada na mikopo inaishia Tanganyika.
Asichowaambia watu ni mchango wa znz nje ya jina la Tanzania.

Asichowaambia ni kuwa znz haina bajeti ya ulinzi na usalama, mambo ya nje, mambo ya ndani, na wala haina mchango hata senti tano kuendsha muungano. Deni lote la ndani znz inawasukumia Watanganyika na haina deni la nje

Mkandara hawaelezi wasomaji kuwa bajeti ya znz ni pungufu kwa mapato yake kwa takribani 350B.
Kama haina mikopo na misaada, nakisi hiyo anafidia nani kama si hazina Dar?

Mkandara anasema, wale watalii kutoka nchi jirani ya znz wanaokuja kupiga soga Dodoma, waruhusiwe kujadili mambo ya Tanganyika. Hawaambii watu yale ya BLW yajadiliwe na Mtanganyika gani anayewakilisha.

Ninachofahamu alisema (yupo katika rekodi) kuwa znz watapata hasara, asichokisema faida ya sasa wanaipata kutoka wapi.

Ni ngumu sana kuelewa kwanini anatetea serikali 2 wakati huo huo akitaka serikali 3 na kulaani serikali 3 akisumanga katiba ya serikali 2. Ngoja tusubiri sijui kesho atakuja na msiamo upi maana keshamaliza yote na hatuelewi anasimamia wapi.

Nguruvi3,

Mengine tu imenibidi nicheke kwani naona ni manung'uniko yako ya kila siku lakin ukiiambiwa ianzishwe akaunti ya pamoja na fedhwa ya nchi hizo kwa mambo ya muungano tu unaruka maili 200 na kuanza kuleta assumptions na utabiri wa Al Marhum Sheikh Yahya sasa sijui unaogopa UWAZI wa hilo au kupata pa kunun'gunika tu kama kawaida yako.

Nilipo RED.

hapo nilitaka nkusaidie kidogo. Bajeti kuu ya Znz kwa mwaka 2014/2015 ni takriban 710 billion na makusanyo yao a ndani yanakadiriwa kufikiwa 400 Billion.

Lakin vile vile bajeti ya JMTz 2014/2015 ni zaidi ya 19 Trilion na makusanyo yao ya ndani wanayokusudia kukusanya ni chini ya 12 Trilllion. Hivyo utaona kuna MAPUNGUFU YA ZAIDI YA 7 TRILION.

Labda nikuulize suala la kizushi hapa.

TGK itapata wapi 350 B kuwapa Znz kusaidia bajeti yao wakti wenyewe wana upungufu wa zaidi ya 7 Trilion?

Hivi unafikiri bajeti ya Ulinzi na usalama, mambo ya nje na na mambo ya ndani kwa Znz inaweza kufikia nusu ya bajeti kuu ya Znz ambayo ni takrib 700 B.

Cc😡Mag3,@ Ngongo
 
Barubaru, ili ku cc wadau Wengine, weka alama ya @ bila space Kabla ya kila jina la mhusika, Vinginevyo hawezi ona the mention. Nitarejea kwenye hoja zako nyingine.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
.

Najuwa siku zote unapojadili jambo ni lazima ujikite kuonyesha TGK ilichangia kiasi gani na JMTz ilichangia kiasi gani? kwani kwa kutofanya hivyo utakuwa wewe mwenyewe unajiweka njia panda na kujionyesha kuwa ni mshabiki tu hua hoja muhimu hapo.
Binafsi nitashukuru sana kama utaweka uzi maalum kwani mimi nitakuwa mchangiaji mkuu katika mada hii kwani mimi si tu kushiriki katika baadhwi ya vikao hivyo vya Wizara ya Fedhwa muungano lakin pia nilikuwa kwa miaka 6 hivyo najua mengi sana. Nitasaidia kuchangia . Nakusubiri kwalo.

Kama nilivyobainisha hapo juu kuwa zaidi ya 42% ya Bajeti kuu ya JMTz inategemea ufadhwili kutok nje kwa njia ya mikopo na misaada. Hilo nafikiri lipo wazi. Pitia bajeti ya JMTz ya mwaka 2014/2015 inayojadiliwa hivi sana utaona wazi kabisa kuwa makisio yenu ya bejeti hiyo ni zaidi ya 19 Trilion na makusanyo yenu ni chini ya 12 Trilion, hivyo zaidi ya 8 Trilion zinategema ufadhwili huo wa misaada na mikopo. Sasa ahali yangu sijui inachobisha ni nini tena hapa? au unafikiri kuna siasa katika uchambuzi wa kiuchumi zaidi ya numbers kuonyeshwa dhwahir shahir.

Kuhusu hili la zaidi ya 88% ya deni la Znz lnadhaminiwa na TGK. Hili nafikiri imekupuruchuka rafiki yangu. Deni hilo linadhaminiwa na Tanzania. Ikimbukwe kuwa Tz ni muungano wa nchi mbili TGK na Znz. Na mas'ala yate ya mahusiano ya kimataifa yapo chini ya muungano ambao ni Tz. Hivyo Znz kutokana na makubaliano hayo haiwezi kabisa kwenda kukopa nje bila kupitia Muungano kwani wenyewe ndio wenye dhamana ya kusaidia hilo ikiwemo pamoja na kudhamini mikopo yote.

Lakin cha kukuongezea hapa vile vile kumbuka TGK inadaiwa mikopo kutoka nje mpaka kufikia 30th April 2014 zaidi ya 36 Trillion na taasisi mbalimbali za kimataifa na mataifa mbalimbali duniani. Na deni hilo lote kwa 100% limedhaminiwa na Tanzania. Je unalitambua hilo?

Kuhusu hili la akaunti ya pamoja ya fedhwa na uchumi ya Muungano. Hii nafikiri hatuna haja ya kuijadili sana kwani ilishajadiliwa na Bunge toka mwaka 1996 tena Bnge la Muungano la JMTz na SIO baraza la wawakilishi.

Kumbuka kuwa katika Bunge la Muungano la JMTz ambalo ndanimwe kuna zaidi ya 80% ya wabunge wake wametoka Tgk iliipitia sharia hii mwaka 1996 na kuipitisha bila kikwazo chochote kutoka upande wowote wa muungano na wabunge wa upinzani na wale wa chama tawala waliipitisha bila mushker wowote.

Waliichambua kwa kina sana na kuangalia kwa uzito wake malalamiko makubwa yanayotolewa na nchi zote mbili kuhusu mambo mbalimbali a kiutawala na kiuchumi na mwisho kukubaliana kuanzishwa kwa TUME YA PAMOJA ya uchumi na fedhwa ( Joint Finance Commission ) JFC na kuita wataalamu kuchambua kero hizo za muungano na kuja na mapendekezo yake Serikalini JMTz.

Bunge la Muungano la JMTz likakubali na kupitisha Katika katiba Ibara ya 133 kuhusu kuanzishwa kwa Akaunt ya pamoja ya fedhwa itakayoshughulikia mambo ya Muungano TU na akaunti hiyo ingesimamiwa na JFC na hivyo kuziacha wizara ya fedhwa TGK kujihusisha na mambo ya TGK na ile wizara ya fedhwa Znz kujihusisha na mambo ya Znz na hivyo kuondoa kero hizo za muungano kama ulivyoainisha katika bandiko lako na nyingine ambazo hujaziweka hapo.

Hiyo ni kwa ufupi sana nakukukumbusha kwa mara nyingine tena.

lakin suala la msingi hapa ni KWANINI SERIKALI YA JMTZ INAKATAA KUTEKELEZA SHARIA HII A KUANZISHWA KWA AKAUNTI YA PAMOJA FEDHWA ZA MUUNGANO CHINI YA JFC?

Kumbuka kuwa tunapoita Sharia maana yake imejadiliwa kwa kina sana na Serikali yenyewe kabla kupelekwa muswada Bungeni na baadae wawakilishi wa wananchi Bungeni kwa maana WABUNGE tena zaidi ya 80% kutoka TGK kuijadili kwa kina sana na kuikubali na kisha Rais wa JMTz kuitia saini yake kuwa Sharia na sasa kusubiri tu utakalezaji wake.

Tujiulize KWANINI SERIKALI YA JMTZ INAPATA KIGUGUMIZI KUTEKELEZA SHARIA HIYO?

lakin nafikiri tungeanzia hapa katika mada hii. KWANINI SERIKALI YA JMTz ilipeleka muswada huu (wa Akaunti ya pamoja ya fedhwa za muungano kusimamiwa na JFC) Bungeni na wabunge wa JMTz kuujadili na kuupitisha?

Nasubiri jibulako hapa.

Barubaru, Kama ambavyo umekuwa unajadili, uhusiano wa kifedha baina ya serikali ya muungano na serikali ya mapinduzi ya znZ ni uhusiano uliopo kikatiba (ibara za 133 n 134). Lakini Kama nilivyojadili, na Kama alivyosisitiza Nguruvi3, ni lazima suala hili liangaliwe kwa 3D: Mapato, gharama, uchangiaji. Bila ya kufanya hivyo mjadala utajaa siasa, malalamiko na upotoshaji.

Sasa Kujibu hoja yako, ni lazima uelewe Kwamba kutekeleza masuala ya muungano, ni lazima kuangalia kwa pamoja mambo makuu mawili: gharama za kuendesha muungano na upatikanaji wa Mapato ya kuendesha muungano. Nilijadili jinsi gani znZ Hawana shida na masuala ya fedha za ndani ya muungano kwani wanabebwa na kodi Za mtanganyika. Kwa mfano, Mapato ya muungano ni haya:

1. Kodi ya Mapato kwa Watu binafsi na mashirika. Hapa tunajua Kabisa Kwamba over 80% ya kodi au Mapato haya yapo upande wa Tanganyika. Mapato ya vyanzo hivi ni karibia shillingi trillioni 2.5.

2. Ushuru wa forodha ni chanzo cha pili. Zanzibar mwaka huu wa fedha imekusanya shillingi bilioni 64.5 tu, na Mapato haya hayaketwi Katika kapu la muungano, tofauti na Mapato ya Tanganyika kutoka ushuru wa forodha ambayo ni takriban shillingi trillioni moja. Hapa pia kumbuka hoja yangu ya awali jinsi gani 75% ya Mapato ya Tanganyika yalivyogeuzwa kuwa ni Mapato ya kugharamia muungano.

3. Chanzo cha Tatu cha Mapato ya muungano ni ushuru wa bidhaa zinazozalishwa nchini. Katika hili, tunajua wazi Kabisa Kwamba uzalishaji karibia wote unafanyika Tanganyika. Mapato ya kodi hii ni Kama shillingi trillioni 1.5. Kama Sikosei, znZ waliwahi lalamika juu ya kodi hii kutozwa kwa bidhaa zinazokuwa consumed Kwao, na kodi hii haikatwi tena kwa bidhaa produced bara but consumed in znZ.

Nadhani hadi Hapa unaona wazi Kabisa Kwamba ingawa Mapato haya yanaitwa - vyanzo vya muungano, Ukweli ni Kwamba ni vyanzo vya Tanganyika ambavyo Ndio vinagharamia muungano huku Zanzibar ikiwa haina mchango wowote wa maana. Sasa Unaposema Kwamba Tanganyika inachukua mikopo nje kwa jina la Tanzania ambalo linajumuisha znZ na Kwamba mikopo hiyo inaendesha mambo ya Tanganyika huku mzanzibari nae akilipishwa, Hapa Inakuwa Vigumu kukuelewa.

Kwa haya Mapato ya ndani, znZ wapo Kimya, lakini kwa suala la mikopo na misaada ya nje Ndio wanapigania Kelele. Swali langu kwako, je:

• Zanzibar wanataka access to mikopo na misaada ili wawe in a good position kuchangia gharama za muungano au kwa matumizi nje ya muungano?

Umejadili sana suala la JFC, hivyo basi tuliangalie lilivyo kwa Mujibu wa katiba ya jmt(1977). Ibara za 133 na 134 za katiba zimetoa maelekezo juu ya gharama za muungano pamoja na upatikanaji wa Mapato kuchangia uendeshaji wa muungano. Ibara ya 133 unasema hivi:
"Serikali ya jamhuri ya muungano itatunza akaunti maalum itakayoitwa 'akaunti ya fedha ya pamoja', na ambayo itakuwa ni sehemu ya mfuko wa hazina ya serikali ya jamhuri ya muungano ambapo kutawekwa fedha yote itakayochangwa na serikali Mbili kwa kiasi kitakachokubaliwa na tume ya pamoja ya fedha kwa Mujibu wa Sheria iliyotungwa na bunge, kwa madhumuni ya shughuli za jamhuri ya muungano kwa mambo ya muungano iliyotungwa na bunge"

Maswali kwako:

• Ni kipi ambacho Tanganyika inatakiwa ibebe lawama hapo? Katiba inataka serikali Mbili zichangie, Mbona ni serikali ya Tanganyika pekee ndiyo inabeba mzigo?

1. Zanzibar wanategemea kuchangia gharama za muungano kwa vyanzo vipi vya Mapato? Mikopo na misaada? Kwani kwa Mapato yake ya ndani ya shillingi bilioni 400, Leo tunajua znZ hawezi changia gharama za muungano kwa uwiano sawa na anachopatiwa na Tanganyika ambazo ni gharama za mtanganyika kwa njia ya kodi.

Hapa Nguruvi3 kakuuliza, je nje ya misaada na mikopo hakuna muungano? Haujaja na majibu yanayoeleweka.

2. Kwa Wakati wote wa mgogoro unaouzuia JFC isifanye kazi iliyokusudiwa, ni Serikali Ipi inachangia muungano? Katika majibu yako, kumbuka Yale Mapato ya muungano Kule juu kwa Mujibu wa katiba.

]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara
Nimekusoma hapo juu. Kwanza nikueleze kuwa nchi za wenzetu mifumo yao si kuwa tunaielewa kwa kuisoma, tumeishi na tunaiafahamu vema. Mfumo unaopendekeza ndio ambao Warioba alipendekeza katika rasimu ya kwanza.
Ninyi mkasema serikali itakuwa kubwa mno, majeshi matatu n.k. bila kufahamu kuwa hapo Ontario kuna RCMP, OPP, na City police kama Toronto, Durham, Peel na Vaughan. Mlikataa mfumo huo kwa kudanganywa na akina Nape, leo mnaushari tena.

Pili, suala la mambo yote ya muungano nalo unaongelea mbele-nyuma.
Tulikuwa na 22 tukielekea kuwa na yote, ukawa shuhuda wa kuvaa koti.
Leo wznz wanataka hadi uraia, unadhani tunaweza vipi katika hali iliyopo.

Tatu, kuna kitu umekitaja kama 'nchi ya bara'. Kwakukusoma unajaribu tu kukwepa jina Tanganyika, lakini maana yako ni hiyo.
Unaposema eti waziri mkuu achaguliwe na watu wa bara, huyu atakuwa kiongozi gani asiye na vyombo kama bunge, mahakama na serikali yake kama Rais wa ZNZ?

Tena unasema manaibu mawaziri ndio wafanye kazi kwa niaba ya Tanganyika. Hawa watawajibika kwa waziri mkuu.
Sijui watafanya vipi kazi ikiwa hawana nyenzo za kufanyia kazi kama bunge.

Hawa mawaziri watapata wapi fungu la kuendesha shughuli zao. Ukisema waombe JMT huoni tayari ni kuvaa koti la muungano.
It is impossible kuwa na waziri tu aliyechaguliwa na pinda asiyejua anafanya kazi kwa serikali gani.

Tena mfumo unaopendekeza ukiuangalia kw aundani ndio uliopo. Katibu mkuu wa wizara anafanya nini katika muungano?

Unachokipendekeza ndicho CCM wanapendekeza. Kwasasa wamekwama kama utakavyokwama kujibu kwasababu ni kituko kuwa na mawaziri wa muungano ukawaita wa Tangayika, wakachota fungu JMT ukalalamika wamevaa koti.
Mkandara huwezi kuwa na serikali ya Pinda tu, unakuwa na serikali ya wananchi.

Hata mantiki haikubaliani na ushauri wako. Kwanini waziri anayeteuliwa na Pinda awe naibu?
Ni naibu wa nani ikiwa ameteuliwa na waziri mkuu aliyechaguliwa. Nani yupo juu ya huyu naibu, waziri mkuu au waziri wa serikali ya muungano? Kwanini mawaziri wa znz wasiwe manaibu kama wale wa Pinda. Mkuu hapa huoni kuna tatizo kweli!

Unachosema hapa ni kuwa kutakuwa na manaibu mawaziri wanaoshughulikia nchi unayoiita ya 'bara'
Logic inakukataza usitumie Tanzania, na unajua hilo.

Mantiki inakataa kuwa hakuna naibu wa kushughulikia mambo ya bara akiwa naibu wa waziri wa muungano.

Mkuu Mkandara, unachoogopa wewe ni kuwepo kwa Tanganyika kwa woga kuwa znz haitakuwa na mteremko iliyo nao.
Huwezi kuwalaumu Watanganyika waliokubali hali hiyo kwa miaka 50. Thanks to Zanzibar waliowashtua Watanganyika.

Hapa tulipo Tanganyika haikwepeki, mtaikwepa katika maandishi kiuhalisia hamtaweza.

Na mwisho, Mkuu hatuhitaji katiba ya 2015. Tunahitaji katiba itakayobadili mwelekeo wa nchi.
Bila kujali lini itapatikana, jambo muhimu ni kufuata mantiki, kuwa wakweli na kukubali kuwa dunia inavyobadilika ndivyo tunavyopaswa kubadilika.

Leo mkuu wa Intelligence anajulikana kwa jina, na anapoishi. Huko nyuma hakuna aliyejua kuwa Kitine alikuwa chief of intelligence.

Leo FBI na CIA wana twitter account, huko nyuma hata kutaja tu ilionekane taboo.
Hii ina maana moja, mabadiliko ni jambo lisilozuilika. Na kwa suala la Tanganyika ambayo imeumia sana na huu muunga , changes are inevitable.

Any attempt to stop Tanganyika, is a step toward anarchy and xenophobia.
Zanzibar is prone and vulnerable for the same.

The situation is down the hill, spiraling at supersonic speed.
The return of Tanganyika is the only cushion Zanzibar can use in this volatile environment, otherwise, people of ZNZ will absorb the maximum heat and pay dear price.
Mkuu wangu kama umenisoma vizuri nashukuru japo bado huelewi ya kwamba mimi sipingi mapendekezo yote ya RASIMU ya Warioba isipokuwa tunapinga swala la kukubaliana na kundi la wahaini kina Jussa linalotaka kwanza marekebisho mapya ya muungano uwe wa Mkataba.
The Act ratifies the Articles of Union between the Republic of Tanganyika and the People's Republic of Zanzibar, provides for the government of the United Republic and of Zanzibar, makes provision for the Modification and Amendment of the Constitution and Laws of Tanganyika for the purpose of giving effect to the Union and the said Articles, and for matters connected therewith and incidental thereto.
This Act and the Law of Zanzibar entitled the Union of Zanzibar and Tanganyika Law, 1964, may be together cited as the Acts of Union of Tanganyika and Zanzibar.
Source:Bofya

Hivyo, sisi wananchi toka mwanzo wa kijiwe hiki hukio Nyenzo, BCS na Jambo, tuliomba KATIBA mpya ambayo kisheria inaruhusiwa na shria za muungano wenyewe ili kuimarisha Muungano na sii swala la kugusa tena Artical of Union ili kujenga nguzo na sheria mpya za Muungano. Hivyo nimesema sii mara moja ila mara 100 kidogo ya kwamba Katiba iliyopo haitoshelezi mahitaji ya wananchi ktk 1. Ujenzi wa demokrasia nchini (vyama vingi) na 2. Uchumi na maendeleo ya wananchi wake 3. Kulinda haki miliki ya wazawa ktk Uraia (Elimu ya Uraia) maana hadi leo tunachanganya Uzawa na Uraia.

Haya ni ndio baadhi tu ya mambo MUHIMU ninayo yakumbuka tulokuwa tukizungumzia kwa miaka mingi sana ilopita hapa JF japo kuna kundi la Wazanzibar ambao miaka yote wamekuwa wakiutazama Muungano huu kama ni KUTAWALIWA kutokana na kwamba nchi yao haina mamlaka ya Kirepublic (semi - sovereignity), hivyo kuifanya Tanganyika kuvaa koti la Muungano yaani Tanganyika ina mamlaka kamili ya kirepublic (semi sovereignity) ndani ya jina la serikali ya JMT (Joseph anaitwa Yussuph)

Swala la Tanganyika limejitokeza majuzi tu tena baada ya rasimu ya Warioba! Halikuwepo na wala halijawahi kuwa tatizo isipokuwa nyie UKAWA ndio mmezalisha hoja mpya mkijua fika kwamba Tanganyika ipo.. Ni ubishi tu wa kuzaliwa! lakini ukweli ni kwamba kinachokosekana kiuhalisia ni serikali ya JMT kwa sababu hakuna mahala popote duniani serikali ya Muungano ina mambo yasokuwaya muungano. hata kwa Malakia mambo yote yapo chini yake isipokuwa mamlaka ya usimamizi wa shughuli za serikali ndio amekabidhiwa waziri mkuu, lakini Malkia ana wawakilishi wake (Governor general) ambao ndio ndio wenye executive power ktk mambo yote japo in practice Prime minister ndiye mwenye mamlaka ya kiutendaji Mfano tazama kipengele hiki kinasemaje (The Canadian Constitution Act (1867) places executive power in the Queen. However, in practice this power is exercised by the prime minister and his ministers)

Mimi kama mwana Jamii nilitazama madai yao na kuukubali ukweli huo kwa sababu ni kweli Tanganyika iitaka kujiunga na jumuiya yoyote haina haja ya swala hilo lijadiliwe wala kupata idhini ya Zanzibar isipokuwa tunatumia jina la JMT kwa faida ya Tanganyika. Ni kweli tumejiunga na jumuiya kibao za Kimataifa iwe za hapa Afrika au za nje na Zanzibar wameshindwa kujiunga kutokana na wao kutokuwa TAIFA.. Kwa ufupi hata hiyo timu ya Taifa Stars, wachezaji wake ni kutoka Bara!

Kwa maana mimi ni binadamu na mwenye kufikiri nje ya Box na mwelewa, nimekubaliana na ukweli huu ya kwamba hapa hakuna serikali ya JMT..ndio ukweli lazima tuukubali, hivyo tunapoidai serikali 3, basi serikali hiyo iwe ni ile ya JMT maana hii ndiyo haipo!. Ukweli ni kwamba Tanganyika tunaye waziri mkuu Pinda, na Zanzibar walikuwa naye Shamsi Vuai sijui sasa hivi nani. Swali linakuja, Je ni nani waziri mkuu wa serikali ya JMT? Haya yote yanatokana na mkanganyiko wa MAMBO YASIYOKUWA/ na YA MUUNGANO. haipaswi kuwa hivyo maana ikiwa mambo yote yatakuwa ya Muungano Pinda angekuwa waziri mkuu wa JMT (Tanganyika na Zanzibar) ktk hali hii tulokuwa nayo leo.

Sasa wewe unataka kujua kama tukifanya mambo yote yawe ya Muungano nani atakuwa waziri mkuu wa Tanganyika? Unaona kumbe unajua na kukubali kwamba Pinda ni waziri mkuu wa Tanganyika hivi sasa na tukibadilisha katiba, Tanganyika itakosa waziri mkuu, hivyo arguement yako yote ni kwa maslahi ya bara na sii Tanzania - Tanganiyka kwanza!

Mkuu kinachotakiwa ni kurekebisha mambo haya ili yawe ya Muungano ama kila upande uwe na nafasi sawa ktk ushiriki wake. Hivyo napingana na Rasimu ya Warioba pale inapotoa jawabu la swala hili ni Kuunda serikali 3 ambazo hiyo serikali kuu itakuwa na MAMBO 7. Hapa kwenye mambo 7, ndipo napopingana na rasimu ya Warioba na ninapopingana na mfumo wa serikali 2 wa CCM kwa sababu pia imeshikilia kuwepo kwa mambo ya Muungano na yasiyokuwa ya Muungano. Mimi nasimama kivyangu na kusema hakuna MAMBO YASOKUWA YA MUUNGANO hivyo sehemu ya 2 ibara ya 3 ya katiba iliyopo ifutwe.

Hivyo basi kama Warioba atanambia ya kwamba tunaunda serikali 3 lakini MAMBO YOTE NI YA MUUNGANO, Swadakta nitakubaliana naye ila kutakuja kipengele cha muda, kutoelewana juu ya serikali hii ya JMT iweje, kutokubali juu ya Tanganyika maana hata wewe hukubali kwamba tumevaa koti la Muungano. Sisi tunatumia jina la Kondoo (JMT) japo wanachokisema Wazanzibar ni kwamba Tanganyika ni kama mbwa mwitu alovaa ngozi ya Kondoo ndani ya zizi hili la Muungano. Hii haina maana tumvue Mbwa mwitu ngozi hiyo ili ajulikane kama ni mbwa mwitu bali wanataka ktk zizi la Kondoo pasiwepo Mbwa mwitu, nyie mnataka Mbwa mwitu ajitokeze na kuwa mbwa mwitu hao Kondoo wanafanya nini ktk kundi la Mbwa mwitu. Ubishi wa iaina hii hatutakuwa na mwisho wala kupatiwa ufumbuzi kwa sababu ni Ujinga mtupu kuuendekeza!.

Kilichopo ubaoni ni kuunda hiyo serikali na haswa serikali inayotakiwa kuundwa ni serikali ya JMT kwa sababu wabunge wote waliopo leo Bungeni haswa kwa majimbo ya bara ambao ni mawaziri ni viongozi wa Tanganyika sii JMT! na ndio maana wanajadili miswada asimilia 95 ya maswala ya bara. Hii ndio imeleta utata kwa wananchi wengine (wabara) kuuliza hao Wazanzibar wanafanya nini Dodoma kujadili maswala ya Bara? hivyo Tanganyika ipo kiuhalisia isipokuwa kisichokuwepo ni bunge la JMT. Sijui umenielewa?.. hapa mimi na wewe tunazungumzia hali halisi na sii hisia zetu za Utanganyika na Uzanzibar.

Kwa hiyo basi kama kweli tunahitaji serikali 3 basi serikali inayotakiwa ni serikali ya JMT ambayo mambo yote yatakayo jadiliwa humo ni ya TAIFA letu na wabunge wote watahusika na maswala yote. Serikali hiyo itahusika na mambo yote ya Tanzania nzima na sii kuwa na waziri mkuu kama Pinda ambaye hatambuliwi Zanzibar kutokana na kwamba yeye ni waziri mkuu anayefanya kazi bara, ama Vuai wazir kiongozi wa Zanzibar hivyo kuwafanya viongozi hawa kuwa ni mawaziri wakuu wa Bara na visiwani - Hakuna waziri mkuu wa JMT. Sijui umenielewa?...

Mwisho, mkuu wangu, lazima tukubali kwamba Wazanzibar wana Point japo hawajui jinsi ya kuwakilisha malalamiko yao ila ukweli upo ktk matendo yetu. Ni sawa na mtu anayejiita Muislaam ilihali hafuati ibada za dini. Ukweli ni kwamba toka Malecela 1993, Msuya 1994 -1995) Sumaye 1995 -2005) Lowassa 2005 -2008 na Pinda huyu hawa wote wamekuwa mawaziri wakuu wa Tanganyika na sii mawaziri wakuu wa JMT...That is the fact.

Na wamekuwa hivyo kwa sababu baada ya mageuzi ya Kisiasa nchini (kuwa na vyama vingi) yalotanguliwa na mageuzi ya Kiuchumi mwaka ya 1984 hatukufanya marekebisho makubwa ya mamlaka ya uongozi ambao unakwenda sambamba na mabadiliko hayo. Swala sio tena rais akitoka bara basi makamu lazima atoke Zanzibar, swala sii Mtanganyika akishika wadhifa huu basi Mzanzibar naye ashike wadhifa ulee. Hii ni dunia ya jamii moja, haina ubaguzi wala upendeleo wa Kikabila ama rangi maana ukiwauliza watu Mzanzibar ni nani hawajui isipokuwa watakuja na tafsiri ya sura zao mpya. Je Mzanzibar ni mzawa wa Zanzibar hata kama anaishi Bara? Je, Mzanzibar ni mwenye nasaba yake Zanzibar? ni Mpemba, Mngazija au yule wa makabila ya asili ya Zanzibar!. Mtanganyika ni nani? na nini tofauti baina ya raia na mzawa!. Yote haya ni mawazo finyu ya watu walopitwa na wakati na tukiwaendeza tu basi Tutaharibu kila kitu mbele yetu na huu Muungano hautaweza kusimama tena.
 
Barubaru, Kama ambavyo umekuwa unajadili, uhusiano wa kifedha baina ya serikali ya muungano na serikali ya mapinduzi ya znZ ni uhusiano uliopo kikatiba (ibara za 133 n 134). Lakini Kama nilivyojadili, na Kama alivyosisitiza Nguruvi3, ni lazima suala hili liangaliwe kwa 3D: Mapato, gharama, uchangiaji. Bila ya kufanya hivyo mjadala utajaa siasa, malalamiko na upotoshaji.

Sasa Kujibu hoja yako, ni lazima uelewe Kwamba kutekeleza masuala ya muungano, ni lazima kuangalia kwa pamoja mambo makuu mawili: gharama za kuendesha muungano na upatikanaji wa Mapato ya kuendesha muungano. Nilijadili jinsi gani znZ Hawana shida na masuala ya fedha za ndani ya muungano kwani wanabebwa na kodi Za mtanganyika. Kwa mfano, Mapato ya muungano ni haya:

1. Kodi ya Mapato kwa Watu binafsi na mashirika. Hapa tunajua Kabisa Kwamba over 80% ya kodi au Mapato haya yapo upande wa Tanganyika. Mapato ya vyanzo hivi ni karibia shillingi trillioni 2.5.

2. Ushuru wa forodha ni chanzo cha pili. Zanzibar mwaka huu wa fedha imekusanya shillingi bilioni 64.5 tu, na Mapato haya hayaketwi Katika kapu la muungano, tofauti na Mapato ya Tanganyika kutoka ushuru wa forodha ambayo ni takriban shillingi trillioni moja. Hapa pia kumbuka hoja yangu ya awali jinsi gani 75% ya Mapato ya Tanganyika yalivyogeuzwa kuwa ni Mapato ya kugharamia muungano.

3. Chanzo cha Tatu cha Mapato ya muungano ni ushuru wa bidhaa zinazozalishwa nchini. Katika hili, tunajua wazi Kabisa Kwamba uzalishaji karibia wote unafanyika Tanganyika. Mapato ya kodi hii ni Kama shillingi trillioni 1.5. Kama Sikosei, znZ waliwahi lalamika juu ya kodi hii kutozwa kwa bidhaa zinazokuwa consumed Kwao, na kodi hii haikatwi tena kwa bidhaa produced bara but consumed in znZ.

Nadhani hadi Hapa unaona wazi Kabisa Kwamba ingawa Mapato haya yanaitwa - vyanzo vya muungano, Ukweli ni Kwamba ni vyanzo vya Tanganyika ambavyo Ndio vinagharamia muungano huku Zanzibar ikiwa haina mchango wowote wa maana. Sasa Unaposema Kwamba Tanganyika inachukua mikopo nje kwa jina la Tanzania ambalo linajumuisha znZ na Kwamba mikopo hiyo inaendesha mambo ya Tanganyika huku mzanzibari nae akilipishwa, Hapa Inakuwa Vigumu kukuelewa.

Kwa haya Mapato ya ndani, znZ wapo Kimya, lakini kwa suala la mikopo na misaada ya nje Ndio wanapigania Kelele. Swali langu kwako, je:

• Zanzibar wanataka access to mikopo na misaada ili wawe in a good position kuchangia gharama za muungano au kwa matumizi nje ya muungano?

Umejadili sana suala la JFC, hivyo basi tuliangalie lilivyo kwa Mujibu wa katiba ya jmt(1977). Ibara za 133 na 134 za katiba zimetoa maelekezo juu ya gharama za muungano pamoja na upatikanaji wa Mapato kuchangia uendeshaji wa muungano. Ibara ya 133 unasema hivi:
"Serikali ya jamhuri ya muungano itatunza akaunti maalum itakayoitwa 'akaunti ya fedha ya pamoja', na ambayo itakuwa ni sehemu ya mfuko wa hazina ya serikali ya jamhuri ya muungano ambapo kutawekwa fedha yote itakayochangwa na serikali Mbili kwa kiasi kitakachokubaliwa na tume ya pamoja ya fedha kwa Mujibu wa Sheria iliyotungwa na bunge, kwa madhumuni ya shughuli za jamhuri ya muungano kwa mambo ya muungano iliyotungwa na bunge"

Maswali kwako:

• Ni kipi ambacho Tanganyika inatakiwa ibebe lawama hapo? Katiba inataka serikali Mbili zichangie, Mbona ni serikali ya Tanganyika pekee ndiyo inabeba mzigo?

1. Zanzibar wanategemea kuchangia gharama za muungano kwa vyanzo vipi vya Mapato? Mikopo na misaada? Kwani kwa Mapato yake ya ndani ya shillingi bilioni 400, Leo tunajua znZ hawezi changia gharama za muungano kwa uwiano sawa na anachopatiwa na Tanganyika ambazo ni gharama za mtanganyika kwa njia ya kodi.

Hapa Nguruvi3 kakuuliza, je nje ya misaada na mikopo hakuna muungano? Haujaja na majibu yanayoeleweka.

2. Kwa Wakati wote wa mgogoro unaouzuia JFC isifanye kazi iliyokusudiwa, ni Serikali Ipi inachangia muungano? Katika majibu yako, kumbuka Yale Mapato ya muungano Kule juu kwa Mujibu wa katiba.

]

Sent from my iPhone using JamiiForums

Mchambuzi,

naona unazidi sana kujichanganya kwa hili suala la kuanzishwa kwa JFC na kazi zake. Kwani hayo aliyouliza Nguruvi3 pamoja na manung'uniko yako mbaona yalishajadiliwa tayari toka 1996 na Bunge la Muungano na kukubaliwa na kisha raisi wa JMTz aliridhia na kuwa sharia.

sasa kama unataka mjadala zaidi mimi naona TUIJADILI SHARIA HIYO ya kuundwa JFC na majukumu yake lakin TUSIPINGE UTEKELEZAJI WAKE.

Labda nikupe zaidi kuwa JFC ipo kisharia na kuna afisi zao na wafanyakazi kibao wapo pale Sukari House Dar. Lakin kubwa kama unapitia Bajeti ya wizara ya Fedhwa kitabu cha matumizi utaona kuna MATUMIZI MAALUM YANATENGWA NA KUOMBEWA PESA KWA AJILI YA UENDESHAJI WA JFC. Je umepitia bajeti ya 2014/2015 ya JMTz hususan kitabu cha matumizi na kuona wametengewa kiasi gani mwaka huu? KILA MWAKA WANATENGEWA PESA KWA KAZI AMBAZO HAWAZIFANYI KUTOKANA NA SERIKALI YA JMTz kusuasua kuwapa majukumu yao

Sasa kama mumekubali hata kuitengea bajeti kamili hii JFC na wakti huo huo hamtaki kuipa majukumu yake kisharia ya kutunza na kuratibu akaunti ya pamoja na fedhwa za Muungano je huoni kuwa ni ifisadi huo.

Je amuoni kuwa mnawalipa watu mishahara na shahiki nyingine bila kufanya kazi zili mlizokusudiwa hamuoni kuwa ni UFISADI HUO.

Lakin suala langu kwako lilikuwa la msingi sana. JE KWANINI BUNGE LA JMTZ NA SERIKALI YA JMTZ WALITUNGA SHARIA NA KUIPITISHA LAKIN WANAPATA KIWEWE KATIKA KUITEKELEZA?

Kumbuka kukataa au kusuasua kuwapa majukumu yao JFC inakula kwenu kwani kila siku watu wanaruka hewani na kuzunguka bila kazi. Nakumbuka mwaka uliopita niliwaona Mbabane Swaziland wafanyakazi sita wakiwa study tour ya mwezi mmoja na nilisafiri nao mpaka South Afrika kutalii kidogo. Mola awape nini.

Mnatafuta mchawi wa uchumi wenu badala ya kuangalia maamuzi na utekelezaji wa maamuzi yenu

Hocuspocus! Anachronism.

Umeambiwa discussion iwe katika premise ya , Mapato, matumizi na Mgawanyo. Wewe unaleta hadithi ziszizo na maana za watu 6 wanaotalii. Hao sita sio sawa na wale 81 wanaokuja Dodoma katika bunge lisilowahusu.

Kama huna hoja juu ya JFC, please quit. Unaharibu na kuchafua sana majadiliano. Thanks for contribution
 
Kuhusu hoja ya Muungano wenu hili ni jambo gumu sana kujadili hususan michango ya wadau katika muungano. Kwani hakuna chombo sahihi kinachoweza kusema nani achangie kiasi gani na kwa nani.

kama hao 81 wanakuuma je umechukua hatua gani zaidi ya kunung'unika tu bila kuchukua hatua ya Ziada. na kuna mengi mnajipendekeza kwa Znz ili kuulinda Muungano wenu huku mkiwabana kiuchumi na kuwadhulumu haki zao katika muungano wenu.

lakin hata wewe kama kuna mtu anajitokeza kukusaidia mzigo wako utakuwa na sababu gani kumkatalia. Chukulia mfano ni hivi juzi tu Mh magufuri ametoa wataalamu wake waende kuzitathmini barabara za mji mkongwe Znz ili wazijenge kwa lami wakti bara bara zenyewe zina lami iliowekwa muda mrefu. sasa unataka Znz wawakatalie?

Kumbuka ukijipendekeza utakufa na mzigo wako. LAKIN MWIBA MKUU WA KUONDOSHA MGOGORO HUU NI KUANZISHWA KWA AKAUNTI A PAMOJA YA FEDHWA ZA MUUNGANO. Kwa kupitia akaunti hii atajulikana nani anachangia nini lakin pia matumizi ya kila mtu na kulinda uwiano wa mapato na matumizi hayo.

kama mchumi nina khofu kubwa Znz kubebeshwa deni la 36 Trilion zilizokopwa na TGK wakti wao wamepewa kiduchi kisichofikia hata 2% ya fedhwa hizo tena kwa masimango makubwa.

Kwa hili la kutunga Sharia na kuiacha kuitekeleza Mimi kama mchumi naona kuna SIRI kubwa kwa TGK kuonekana wanavyoidhurumu Znz na kuibana kiuchumi na kimapato.

waachwe Znz wapumue.

Pole sana ahali yangu kwa spining zako

Nguruvi3,

Mengine tu imenibidi nicheke kwani naona ni manung'uniko yako ya kila siku lakin ukiiambiwa ianzishwe akaunti ya pamoja na fedhwa ya nchi hizo kwa mambo ya muungano tu unaruka maili 200 na kuanza kuleta assumptions na utabiri wa Al Marhum Sheikh Yahya sasa sijui unaogopa UWAZI wa hilo au kupata pa kunun'gunika tu kama kawaida yako.

Nilipo RED.

hapo nilitaka nkusaidie kidogo. Bajeti kuu ya Znz kwa mwaka 2014/2015 ni takriban 710 billion na makusanyo yao a ndani yanakadiriwa kufikiwa 400 Billion.

Lakin vile vile bajeti ya JMTz 2014/2015 ni zaidi ya 19 Trilion na makusanyo yao ya ndani wanayokusudia kukusanya ni chini ya 12 Trilllion. Hivyo utaona kuna MAPUNGUFU YA ZAIDI YA 7 TRILION.

Labda nikuulize suala la kizushi hapa.

TGK itapata wapi 350 B kuwapa Znz kusaidia bajeti yao wakti wenyewe wana upungufu wa zaidi ya 7 Trilion?

Hivi unafikiri bajeti ya Ulinzi na usalama, mambo ya nje na na mambo ya ndani kwa Znz inaweza kufikia nusu ya bajeti kuu ya Znz ambayo ni takrib 700 B
Barubaru , kuna wkati unachafua sana mijadala kwa hoja zako zisizolingana na usomi au umri. Tunakuomba tafadhali kama huna cha kujadili basi ukae kimya.

JFC tumekuambia inajadilika katika premise hizi, Mapato, matumizi, Mgawanyo.
Siku tatu hujaweza kusema chochote cha maana kama mchumi, badala yake unaleta trivial and useless story za watu 6 kusafiri kwenda south.

Kamuulize waziri Aboud na waziri wa fedha wa znz wapi nakisi ya BL350 inatoka. Kamuulize Lissu aliyeeleza fedha za bajeti zinatoka wapi. Kamuulize Pandu Kificho aliyezungumzia fedha za bajeti ya znz zinatoka wapi.

Katika mapato ya B400 gharama za ulinzi na usalama za znz ni zaidi ya nusu ya hizo. Hata siku moja hutasikia mznz akisema ulinzi na usalama pamoja na mambo ya ndani yasiwe ya muungano.

Kuna deni la ndani ambalo linabebwa na Tanganyika. Kumbuka SMZ mishahar tu inachukua zaidi ya nusu ya bajeti kulingana na waziri Mzee.

In short huna arguement za maana kama msomi kiwango cha Daktari. Please tunashukuru kwa mchango wako na tunakuomba usivuruge mijadala. Ahsante sana kwa mchango wako, tukikuhitaji tutakualika, kwasasa tunakushukuru sana
 
Watetezi wa Zanzibar wanakwepa Ukweli Kwamba:

1. Serikali ya muungano imekuwa ikigharamia mambo ya muungano kutokana na Mapato ya muungano lakini pia na Mapato yasiyo kuwa ya muungano kwa upande wa Tanzania bara/Tanganyika. Kwa upande wa Zanzibar, serikali hii haichangii moja kwa moja Kama Tanganyika, badala yake inachangia kupitia Mapato ya muungano ambayo yanakusanywa na serikali ya jamhuri ya muungano, of which zaidi ya 75% ni Mapato ya Tanganyika.

2. Kwa miaka 50, bajeti ya JMT haitenganishi vyanzo vya Mapato na matumizi kwa utaratibu wa mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika. Tunapozungumzia bajeti ya Tanzania, maana yake ni bajeti ya serikali moja - inayoshughulikia muungano (tanganyika na Zanzibar) huku znZ ikiwa na bajeti yake (fiscal autonomy) na vipaumbele vyake. Kwa upande wa Tanganyika, bajeti yake ni hiyo hiyo ya muungano Katika kapu moja. Kuwa na bajeti
Moja - ya Tanganyika na muungano inaathiri sana vipaumbele vya Tanganyika. Wazanzibari Hawaoni hili.

Given yote haya na niliyojadili awali,
Kati ya hoja hizi Mbili, ipi holds more water?

•Hoja ya kwanza ni ya znZ ambao wanalalamika hawapati mgao unaostahili kutokana na Mapato ya serikali ya muungano.

•Hoja ya pili ni ya upande wa Tanganyika Kwamba Zanzibar haichangii kuendesha muungano.

Definitely hoja ya pili.
Ibara ya 133 ya katiba inaelekeza serikali Mbili zilizopo kuchangia gharama za muungano, Zanzibar kwa miaka zaidi ya 20 sasa haichangii moja kwa moja Bali kupitia Mapato ya muungano of which kimsingi ni Mapato ya Tanganyika.

Mwisho wazanzibari wanasahau Kwamba masuala ya misaada na mikopo haipo Katika katiba ya jmt, hivyo hayatambuliki kisheria. Sasa Kujadili Kwamba JFC Ipo kwa Mujibu wa Sheria (which is correct) lakini hapo hapo kusingizia suala la mikopo na misaada kwa znZ Kama kikwazo cha JFC kutekeleza majukumu yake ya kikatiba Wakati masuala ya fedha za nje (mikopo na misaada) sio masuala ya muungano, lakini pia hayapo kisheria ni kukosa umakini wa hoja.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom