Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #381
Mkuu, hoja ya misaada na mikopo ni ya ajabu sana.Definitely hoja ya pili.
Ibara ya 133 ya katiba inaelekeza serikali Mbili zilizopo kuchangia gharama za muungano, Zanzibar kwa miaka zaidi ya 20 sasa haichangii moja kwa moja Bali kupitia Mapato ya muungano of which kimsingi ni Mapato ya Tanganyika.
Mwisho wazanzibari wanasahau Kwamba masuala ya misaada na mikopo haipo Katika katiba ya jmt, hivyo hayatambuliki kisheria. Sasa Kujadili Kwamba JFC Ipo kwa Mujibu wa Sheria (which is correct) lakini hapo hapo kusingizia suala la mikopo na misaada kwa znZ Kama kikwazo cha JFC kutekeleza majukumu yake ya kikatiba Wakati masuala ya fedha za nje (mikopo na misaada) sio masuala ya muungano, lakini pia hayapo kisheria ni kukosa umakini wa hoja
Hivi znz wanaweza kujivunia mikopo? Kwa uchumi wa Bilioni 400, wakiwa hawana assets, wanataraji nje ya muungano wangeweza kukopa kiasi gani.
Ukweli wasioukubali ni kuwa katika asilimia 88 ya dhamana ya mikopo ya znz, hakuna senti tano inayoingia katika muungano. Wakati huo huo, mikopo ya Tanganyika inaingia katika JMT na wao kunufuaika bila strings attached. Huu ni ukweli ambao hawautaki.
ZNZ haina deni la ndani hata siku moja. Deni hilo linabebwa na Mtanganyika
Ukweli mwingine ni kuwa kwa uchumi wa bilioni 400, nje ya muungano hiki ni kisiwa kinachoweza kununulika.
Hiyo misaada wataipata sana, lakini mwisho wa siku watapigwa bei. Huo ni ukweli wasioutaka kuusikia.
Hili la JFC ni hoja ya kitoto sana. Huwezi kuwa na account ya pamoja ukiwa na uchumi wa trilioni 10 mwenzako akiwa na bilioni 400. Hata kama tutasema account hiyo ichangiwe kwa 1/8 znz na 7/8 bado znz ni tatizo.
Mishahara tu kwa mujibu wa waziri wao wa fedha inachukua nusu ya bajeti. Kipi walichobaki nacho cha kuchangia account ya pamoja ya JFC?
Suala la misaada ni la kipuuzi na ni wapuuzi tu wanaoweza kujivunia hilo.
Account ya pamoja kama inaendeshwa kwa misaada, hii maana yake misaada ikishindwa kupatikana basi hakuna account hiyo.
Kwamba, wznz mchango wao katika account ya pamoja ni misaada na mikopo. Kwamba, wana hesabu ndege aliyeko mtini kama mali yao. Katika mlo wao, hawafikirii kutafuta bali ndege walioko mtini ni assets zao. Wenzetu hao!
Ni kituko na ukosefu wa fikra kudhani kuwa ni fahari kukopa IMF kuliko kupewa bure.
Kwamba, wznz wanajivunia sana misaada na mikopo kutoka washington na Paris Club.
Huu kama si ukoloni wa akili ni wendawazimu.
Nilidhani nchi za Afrika zilitakiwa ziondokane na minyororo ya misaada, kumbe kuna watu wanaamini misaada na mikopo ni jambo muhimu sana kwa ustawi wao achilia mbali ustawi wa muungano.
Kwa upande mwingine, jambo hili la muungano limetokea mahali pazuri.
Watanganyika wengi hawakuwa na fahamu kusuhu namna walivyobeba mzigo,uzito na ugumu wa mzigo huo.
Leo lazima Watanganyika watafute fiscal autonomy ya kuamua mambo yao zaidi ya kuwa na account ya pamoja.
Account ya pamoja ni kuendelea kuhalialisha mzigo. Hawa watu wasioweza kulipa bili ndogo ya umeme, wanawezaje kuchangia account hiyo. Account ya pamoja ni ujinga, huwezi kuchukua rasilimali za Mtanganyika ukaziweka katika account na kudai ni zetu na znz. Narudia tena kwa bilioni 400, znz itachangia nini yarabi, japo ijenge barabara moja tu
Ukiangalia kwa undani, mbali ya ardhi na watu, kifedha makusanyo ya kodi za Kariakoo ni makubwa kuliko SMZ.
Kwa mwaka mapato ya kariakoo ni zaidi ya bilioni 500, nyingi kuliko ya znz.
Nadhani SMZ ilitakiwa iwe na JFC na account ya pamoja na soko la kariakoo na si Tanganyika.
Hata kwa akili za kawaida tu, Ilala ni kubwa kicuhumi kuliko znz.
Leo wanasema eti JFC haifanyi kazi kwasababu Tanganyika inataka kuiba bilioni 400 za mwaka za Zanzaibar!!!
Matatizo yote yana suluhu moja, Tanganyika izinduke, iamue mipango yake na taratibu zake bila kushirikisha znz.
Znz nao wawe na mambo yao yasiyohusu ushirika na Tanganyika.
Hapo Tanganyika itajivua lawama za kitoto na znz itatafuta mshirika wa kuchangia bilioni 400 sawa sawa.
Watanganyika wanapaswa kuona kile wasichokiona kwa macho mawili. Mzee Mwanakijiji anakauli yake kuwa kupe hakusumbui akiwa mgongoni hadi ndigana itakapokuangusha.
Labda kwa Watanganyika, tuwaeleze kitu kimoja. Kama tuamua kuchangia mambo ya muungano japo kwa 1/8 znz na 7/8 Tanganyika, znz haitaweza kuendesha serikali ya muungano kwa wiki mbili tu. I mean bila kuondoa hata senti tano katika bilioni 400,znz haina uwezo wa kuendesha au kuchangia JMT.
Hawa ndio wanataka account ya pamoja! ni tatizo gani?
Hatuhitaji JFC na Zanzaibar kwasababu haina maana yoyote. Hatuwezi kuchukua kodi zetu tukazweka kwenye kapu ili kila mmoja aliyenawa na asiyenawa mikono achote. Huko ni kuwanajisi walipa kodi wa Tanganyika.