Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #361
Nadhani wanajamvi wanakushangaa sana. Unaulizwa kitu kimoja unazua kitu kingine.Nguruvi3,
Ahali yangu naona tunarudi kule kule nilikokubainishia toka awali.
Huo mfano nilikuwekea ujue kuwa hata siku moja hamuwezi kuchangia 50/50 % kwenye muungano wenu kwa kila nchi kwani huo ndio uhalisia kutokana na eneo la nchi na idadi ya watu. Ndio maana wachumi wa nchi hizo wakaja na mapendekezo hayo.
Kumbuka kuwa JFC wamechambua kwa kina na kuja formula mbayo ndio hiyo ikiwemo 21% ya ajira katika vyombo vya muungano laazima wapewe wa Znz lakin TUNALOJADILI HAPA NI KUWEPO NA AKAUNTI YA PAMOJA YA FEDHWA ZA MUUNGANO AMBAZO ZITARATIBIWA NA KUSIMAMIWA NA JFC. Hii account itaondoa hayo malalamiko na manung'uniko yako. Kwani kwa sasa kutokana na TGK kujivika Joho la Tanzania wanawadhulumu sana wa Znz. Mfano tunaposema mambo ya Ulinzi ni ya Muungano, ni vipi katika wizara hiyyo IWEMO JKT ambacho si chombo cha muungano. Kumbuka Znz kuna JKU. Au wizara mambo ya ndani ambacho ni chombo cha Mungano iweje kuwe na Magareza au Zimamoto ambavyo si vyombo vya muungano?. Kumbuka Znz kuna Chuo cha mafunzo na jeshi la Zimamoto.
Sasa unapopitisha Bajeti hii na kuita ya muungano huoni kuwa ukakasi umezidi hapo. Kwanini vyombo hivi vya Muungano na taasisi zake wasifate mgawo wao wa bajeti zao kupitia JFC na kutoka fedhwa zao katika Akaunti maalum ya pamoja na kuwaacha Pesa za mambo yasiyo ya muungano ziendelee kupitia katika Single Tressure Account iliyopo BOT?
sasa wasi wasi wenu ni nini?
Kumbuka mzowea vya kunyonga ...
Hakuna marefu yasiyo na ncha. Znz huru ileeeeeeeeeeeeeeeeeee
waachwe Znz wapumue
Maswali ni haya ndugu mchumi
Katika ajira 150,000 za polisi(mfano) wznz wangapi wameajiriwa na je hilo si sehemu ya uchumi.
Pili, kama wafadhili watatoa 60% ya misaada(mfano), hiyo 40% znz inachangia kiasi gani katika account ya pamoja?
Tatu, Je, wafadhili wakiacha kuchangia, ina maana JFC itakuwa imekufa? Na kama itakuwepo znz itachangia kiasi gani?
Haya ndiyo maswali, kama huwezi kuayajibu, stop and quit! hatuwezi kuwa na mjadala wa bla bla.