Mkuu wangu mbona mnatafuta visa humu kwa kutoa miaka ilihali hakuna mahala nimeitaja hiyo miaka?. Sasa utajenga vipi Utaifa wa Taifa la Tanzania ikiwa hili neno lenyewe Tanzania halikuwepo toka siku ya Muungano wala hiyo Katiba ya nchi (mwongozo) haikutungwa siku ya Muungano? sasa kwa ufahamu wako ndio tuseme hatukuwa na Taifa hadi mwaka 1977? Jamani jaribuni kuelewa mtu anazungumza nini badala ya kutafuta makosa ambayo hayana msingi. Hivi wewe Ukizaliwa mwaka 1972 lakini ukabatizwa mwaka 1980 ina maana hukulelewa ktk mazingira ya Kikristu kwa sababu ulizaliwa kama Mchambuzi na baada ya kubatizwa ukaitwa Joseph? Hii miaka ya nini mkuu wangu ikiwa tunachoongelea hapa ni Utaifa wa nchi hii iitwayo Tanzania.Nadhani unajua kuna tofauti kubwa Kati ya tanu na CCM.
CCM ilizaliwa miaka 13 baada ya muungano (1977), kabla ya hapo, kulikuwa na TANU kwa upande wa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar. Hata katiba ya muda ya JMT kwa miaka 13 (kipindi cha 1965-77) ilitamka wazi kwamba - hadi pale tanu itakapoungana na asp, chama pekee cha kisiasa katika jamhuri ya muungano kitakuwa ni TANU.
Hivyo basi ujenzi wa huo utaifa wa Tanzania unaoujadili, ujenzi huu ulikuwa ukiendeshwa na chama cha Tanganyika (Tanu), sio CCM (chama cha muungano). Kwa maana nyingine, haupo sahihi kusema Kwamba ccm ndiyo taasisi iliyotumika kujenga utaifa wa Tanzania, unless hoja ibadilike kuwa kwamba ujenzi wa utaifa wa Tanzania ulianza mwaka 1977, na sio 1964.
Tanu ilizaliwa miaka kumi kabla ya muungano, miaka saba kabla ya uhuru. Na kama umesoma vizuri historia ya nchi yetu, Tanu iliundwa kwa madhumuni ya kuwaunganisha waafrika ndani ya Tanganyika dhidi ya mkoloni, kwa hiyo hii ilikuwa ni hatua ya mwanzo ya ujenzi wa utaifa wa Tanganyika. Tanu ilifanikiwa kujenga utaifa wa Tanganyika over and beyond udini na ukabila, na umoja na utaifa huo ndio uliofanikisha harakati za uhuru chini ya Tanu. MaSwali kwako kufuatia mafanikio ya tanu:
1. Je utaifa wa Tanganyika ulikuwa na mapungufu gani?
2. Utaifa wa tanzania ulilenga watanganyika au watu gani? Kwa maana nyingine, je, mradi wa utaifa wa tanzania ulilenga kuimarisha mapungufu ya utaifa wa tanganyika au kitu kingine?
3. Kwanini leo wale wanaohusishwa na utaifa wa tanzania ni wale wale waliohusishwa na utaifa wa tanganyika?
4. Kati ya mzanzibari na mtanganyika, ni yupi anayefupisha ndoto ya utaifa wa Tanzania ndani ya muungano?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Utaifa wetu huu umejengwa baada ya mwaka 1967 baada ya katiba ya TANU kutolewa, na haikuwa na msisitizo kiutendaji hadi mwaka 1971 baada ya kupitiswa mwongozo mpya wa TANU ambao ulikuja fuatiwa na Azimio la Arusha mwaka 1977, hivyo hatua kwa hatua ama awamu kwa awamu mikakati ilibuniwa kutokana na hali halisi iwe kwa wananchi wake ama Utaifa wetu. Nia ianweza kuwepo toka mwaka 1961 lakini ujenzi halisi wa Utaifa wetu ulianza haswa baada ya Katiba ya mwaka 1977 ambayo hadi leo ndio tunatoitumia na ndivyo mataifa wanavyotutazama kutokana na malezi ya Katiba hiyo. Yapo marekebisho mengi yamefanyika lakini maadam Mwongozo uliopo leo unatokana na katiba ya mwaka 1977 basi huu ndio UTAIFA tuloujenga hadi leo na kama tuna mapungufu yoyote ya Utaifa wetu basi unatokana na katiba hiyo!
Mimi binafsi nina hakika Nyerere anygeweza kuujenga Utaifa wa Tangantyika tofauti kabisa kama sio muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu naamini Kwa dhati Abdulrahman Babu alikuwa sababu kubwa ya siasa ya Ujamaa (1964 -1976) japo wengi wanaamini kwamba Nyerere alikuwa mjamaa hata kabla ya Uhuru. Tafadhali usianzishe ubishi mwingine maana hii ni imani yangu mimi sii lazima uikubali.
2. Utaifa wa Tanganyika haukuwa na tatizo lolote zaidi ya kwamba kila penye nia kuna malengo. Uhuru wa Tanganyika haukuwa na malengo ya wananchi wa Tanganyika tu, bali ni hatua moja ya UHURU wa nchi zote za Kiafrika kwa lengo la kuunda TAIFA wao. Hivyo unachoweza kusema leo pengine ni kwamba fikra hizo zimepitwa na wakati ama azma hiyo isingewezekana. baada ya kujua kwamba MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO. Lakini huwezi kufikiria ya leo kuyaweka mwaka 1964 ama 1977 wkaati wao waasisi wetu waliweka nia ya kuwa na TAIFA moja wakianza kwa hatua ya nchi jirani (wazo la Nyerere).
Kama lisingekuwepo wazo la kuunda Umoja wa nchi huru za Kiafrika kama jumuiya ya Utaifa wa nchi hizo pengine Tanganyika ingekuwa tofauti lakini haikuwa na hawezi kuwa maaa tayari leo tyuna nchi inayoitwa Tanzania. Kuna hata habari ya kwamba TaNGANYIKA TULIKUWA TAYUARI KUAHIRISHA uHURU WETU IILI SISI NA kENYA NA uGANDA tupate Uhuru siku moja na pengine kuunda TAIFA moja lakni haikuwezekana hivyo mimi na wewe hatuwezi kubashiri Tanganyika huru wlala Utanganyika kwa leo.
3. Hao wanaohusishwa na Utanzania ndio wale wale wa Utanganyika ni kina nani hao maana wauliza swali wakati jibu lake unalo wewe. Hawa watu wanahusishwa kivipi?
4. Anayefupisha ni yule asiyependa kusikia akilaumiwa naye ni sisi Watanganyika. Ni kweli tulimelivaa koti la Muungano, na maneno haya yanatuuma sana japo ni kweli tupu. Waswahili wanasema Ukweli unauma, hivyo badala yetu kukana kulivaa koti ebu turudi nyuma na tufikiri tena wakati huu bunge likiendelea na kukubali kwamba kweli tumelivaa koti la Muungano.
Wee siikiliza kwa makini bunge liitwalo la Muunano, utakuta karibu mambo yote yanayojadiliwa humo ni mambo ya Tanganyika na Mzanzibar akiinuka tu na kuhoji basi atashambuliwa kana kwamba hana mamlaka ya kuzungumza pale. Sasa tujiuklize hao wabunge wa Zanzibar wnaafanya nini pale Bongeni Dodoma ikiwa asilimia 90 kama sio 95 ya mambo yote yanayojadiliwa mule ni ya Tanganyika! Hata vyama vya wapinzani nao vile vile kama hawatakiwi utadhani bunge hilo ni kikao cha wanaCCM na sii bunge la Muungano. Hivyo ni kama tuna serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar, mnachotakiwa kuomba ni serikali ya Muungano ambayo kiuhalisia HAIPO.
Halafu wakiona wameonewa ktk hilo wakaitaka Zanzibar yao tunaanza kusema wao ndio wanataka kuvunja Muungano! haya sii ndio yale ya ndoa ambayo mwanamke ashirikishwe tu kwa mambo ya Jikoni? Bibie akiuliza tu maswala ya kazi au biashara anaambiwa wewe unataka nini, Unalishwa bure, unalala bure kazi yako iko jikoni na kitandani kaa kimyaa!. Kisha huyo mke akiomba talaka basi yeye ndio anayetaka kuivunja ndoa, hii mkuu tumeitoa wapi?
Kwa nini tunaendekeza mila chafu kama hizi ambazo leo hii wap[o baikna yetu wanaopinga kabisa Mwananke kudai haki zake kama mzazi! tena mkitumika lugha nya kwamba Nyerere aliilazimisha ndoa hii pasipo kushauriana na wengine jambo ambalo ni Uongo mkubwa ulotungwa na wale waliokuwa upande wa pili (Hizbu).
Zanzibar wamedai nchi yao kutokana na sisi tunavyo wa abuse, na huwezi kushindana na mwanamke kwa matusi ndio maana tunazidi kuchukia. Wazanzibar mdomo wanao na wanajua sana jinsi ya kutuchokonoa haswa pale panapo
wauma na sasa mnafikia kutaka kuandika hiyo talaka pasipo kujua kwamba tumezaa watoto wengi na ile child support itakula kwetu na sii kwa Zanzibar. Kuna Wzanzibara wengi bara kuliko population yao huko makwao na karibu kila familia Zanzibar ina ndugu zake bara hivyo wao wanaweza kuishi bara lakini sisi hatutaweza..