Kuna haja ya kuelewa jinsi gani Tanganyika ilitutoka ili tuweze kujua tutaizinduaje. Nitajaribu kujadili suala hili.
Ningependa nianze mchango wangu kwa hoja za
Nguruvi3 kwa kugusia kidogo hili la Pinda na Tanganyika ingawa nguruvi3 ameliweka katika muktadha wake vizuri sana.
Pinda amekuwa waziri mkuu kwa miaka sita sasa na kwa mtazamo wangu he's the worst prime minister our country eve had. Katika miaka yake sita kama waziri mkuu, amefanya nini la maana, hasa katika kutatua kero za muungano au for that matter, kuuboresha? Mwalimu nyerere alikerwa sana na kitendo cha waziri mkuu wa wakati ule (John Malecela) kumshauri vibaya rais wa JMT Ali Mwinyi juu ya sakata la G55 na Tanganyika. Hakika mwalimu angekuwepo leo, angekerwa sana na waziri mkuu kushindwa kumshauri vizuri rais wa sasa juu ya udhibiti wa zanzibar kuvunja katiba ya JMT.
Suala la pili nalopenda kujadili ni kwamba: mkataba wa muungano (1964) ndio nguzo kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinyume na mkataba wa muungano na pia kinyume na katiba ya muda ya 1965, katiba ya JMT (1977) ambayo inatumika hadi leo haitoi kauli ya wazi ya kuunda serikali ya Tanganyika na haimpo madaraka rais wa muungano au kiongozi mwingine yoyote kuendesha na kusimamia mambo ndani ya Tanganyika (tanzania bara?), mambo ambayo hayapo ndani ya muungano. Nape na CCM wanataka kuendeleza tatizo hili au kasoro hii, na pengine tuwaulize kwamba je, kwanini mkataba wa muungano ulitamka juu ya uundwaji wa serikali ya Tanganyika? Kwanini hilo liliendelea kutamkwa ndani ya katiba ya muda (1965)? Je hili lilikuwa ni kosa la bahati mbaya? Ni dhahiri hili lilifanywa kwa makusudi kuiondoa Tanganyika for good. Kama alivyojadili nguruvi3, leo hii, Rais wa JMT na Serikali ya JMT ndio vyombo vinavyohusika na uendeshaji wa serikali ya Tanganyika na hali hii imekuwepo tangia siku muungano ulipozaliwa 1964. Wakati vyombo hivi viwili vilipewa madaraka kamili na mkataba wa muungano (1964) na Katiba ya muda ya JMT (1965) ili kutekeleza jukumu hili la msingi kabisa, katiba ya JMT ya mwaka 1977 haikutamka juu ya madaraka hayo ya kusimamia na kuendesha Tanganyika. Kwa maana hii, hatua na maamuzi yote yaliyochukuliwa na marais wa JMT na hata leo (Kikwete) kuhusu mambo yasiyokuwa ya muungano (ya Tanganyika au tuite Tanzania bara), hayana nguvu za kisheria, wala za kikatiba. Hili ni tatizo kubwa sana kwani ndio vimefanya Tanzania ionekane ni Tanganyika na Tanganyika ni Tanzania machoni mwa wananchi wengi. Mbaya zaidi, hali hii inachangia sana watu wengi kuja na hoja kwamba hakuna haja ya kuwa ba serikali zaidi ya moja kwa nchi nzima ya tanzania.
Tukiangalia sakata la G55 kidogo - hoja binafsi juu ya Tanganyika ililenga kurekebisha kosa hili na kulikuwa na hoja ya msingi na ndio maana bunge na rais walipitisha hoja hii kwa maslahi ya muungano na taifa kwa ujumla. Lakini kinyume chake, uamuzi huu ukapingwa na hoja kuwa watered down kwa maelezo kwamba chama hakikuwa kimebadilisha sera yake ya mfumo wa serikali mbili. Swali linalofuatia ni je- CCM kilipata wapi wapi madaraka ya kuingilia mambo ya kikatiba wakati mkataba wa muungano haukutaja chama chochote cha siasa? CCM ya leo ya kina nape inapata wapi madaraka ya kuingilia mambo ya kikatiba ya nchi wakati huu wa mfumo wa vyama vingi vya siasa? Taifa letu litaelekea wapi iwapo vyama vya kisiasa vitakuwa vinaingilia suala la katiba bila ya nguvu ya kisheria na kikatiba? CCM inataka kulipeleka wapi taifa letu?
JINSI KATIBA YA JMT ILIVYOKIUKA MKATABA WA MUUNGANO NA JINSI CCM ILIVYOSHIRIKI KUIZIKA TANGANYIKA.
Katiba ya 1977 ibara ya (1)
Inasema kwamba Tanzania ni jamhuri huru iliyoungana. Ikumbukwe kwamba awali katika mkataba wa muungano na pia katiba ya muda ya 1965, Tanzania haikutajwa, badala yake - Jamhuri ya Muungano Tanganyika na Zanzibar.
Ibara ya (2) juu ya nchi shiriki inataja nchi hizo kuwa ni Tanzanoa Bara na Zanzibar, again kinyume na mkataba wa muungano, na katiba ya muda 1965.
Tume ya warioba imejaribu kuja na ufumbuzi juu ya kasoro hii kubwa, tena sio kwa kubuni bali kwa kurudi kwenye legal foundation of the union - mkataba wa muungano, lakini badala ya kupongezwa, inatukanwa, wakiwepo makada wa ccm.
MUHIMU:
Muswada wa Katiba ulipelekwa bungeni april 25 1977 na kupitishwa siku hiyo hiyo kuwa katiba ya JMT bila hata kushirikisha umma. Katiba hii ikakiuka mkataba wa muungano kwa kila namna, lakini muhimu kuliko yote, kutoweka uendeshaji wa serikali ya Tanganyika kwa mujibu wa katiba. Kasoro hii inaweza kuonekana ni ndogo sana kama anavyojadili Pinda lakini sio suala dogo kwani linaonyesha dhahiri uingiliaji wa chama CCM katika katiba wakati kimsingi CCM sio mshiriki wa asili wa Muungano. Ndani ya katiba ya 1977, CCM ikajipa mamlaka ya "kuunda na kuvunja katiba". Kwa hali hii, CCM inahalalishia vyama vingine vikiingia madarakani vije na katiba zinazokidhi mahitaji ya vyama husika vya siasa. Hii ni hatari kwa muungano na taifa kwa ujumla.
Nirudie swali tena, kwanini Katiba ya 1977 haikutaja utawala wa Tanganyika, moja ya nchi shiriki za muungano? Mkataba wa muungano uliweka wazi kwamba hadi hapo katiba mpya ya JMT itakapokuwa tayari na kupitishwa na bunge:
*Katiba ya Tanganyike itumike kwa ajili ya JMT lakini irekebishwe ili ieleze uwepo wa serikali ya zanzibar.
*vile vile chini ya mkataba wa muungano, ikakubalika kwamba katika kipindi hicho cha mpito, Jamhurri ya muungano iwe inasimamia Tanganyika. Kipindi cha mpito kilikuwa ni mwaka mmoja ambapo mkataba wa muungano uliagiza kwamba mchakato wa Katiba mpya ya JMT uanze. Ibara ya 4 ya mkataba wa muungano inasema hivi:
...na hilo bunge lililotajwa na rais litakuwa na mamlaka juu ya mambo hayo kwa ajili ya jamhuri ya muungano, hii ni ziada juu ya mamlaka kuhusiana na mambo yote yanayohusiana na Tanganyika
Mwaka 1965, katiba ya muda iliweka wazi juu ya kipindi cha mpito (mwaka mmoja, sio 12) kwa kusema:
12(1) Mamlaka yote ya serikali juu ya mambo ya muungano kuhusu na mengine yote ndani ya tanganyika yamewekwa chini ya rais
Pia ibara ya 49 ya katiba ya muda (1965) inasema:
Mamlaka ya kutunga sheria juu ya mambo yote yalio ya muungano na mambo mengine yote ndani na juu ya Tanganyika yanawekwa chini ya bunge.
Ilitarajiwa kwamba sheria za kudumu juu ya masuala yote yasiyo ya muungano zingefuata muda sio mrefu. Tanganyika kama moja ya nchi shiriki za muungano ilitakiwa kupewa haki zake kuhusu masuala yasio ya muungano kama ilivyopewa zanzibar. Baada ya nchi kukaa na katiba ya muda kwa miaka karibia 13 badala ya mwaka mmoja tu kama mkataba ulivyoelekeza kiwe ni kipindi cha mpiti, Katiba ya 1977 ikaja na mambo ya ajabu kabisa. Katiba hii iliacha kabisa kuiweka Tanganyika, kwa mfano, juu ya serikali inasema
Mamlaka ya serikali ya jamhuri ya muungano kuhusiana na jamhuri ya muungano na mambo yote ya muungano yanawekwa mikononi mwa rais
Fananisha maneno haya na yale ya hapo juu kwenye katiba ya 1965 na mkataba wa muungano 1964.
Na kwa upande wa znz, katiba ya JMT 1977 ikatamka:
Kutakuwa na serikali ya zanzibar inayojulikana kama serikali ya mapinduzi ya zanziba ambayo itakuwa na mamlaka katika zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya muungano kwa mujibu wa masharti ya katiba hii
Wapi mamlaka ya Tanganyika katika suala hili? Ndio nape na ccm wanakuja na hoja kwamba serikali mbili zitatatua mgogoro baada ya kushindwa kwa miaka 50? Kwa dawa gani, baraza la wawakilishi la Tanzania bara litakalozaa mabunge matatu ndani ya serikali mbili? How pathetic!
Ibara ya (3) ya katiba ya 1977 ilileta confusion kubwa sana, hasa kipengele kilichosema:
Chama ndicho chenye madaraka ya mwisho katika mambo yote kwa mujibu wa katiba hii na katiba ya chama.
Pia inasema:
Shughuli zote za vyombo vya serikali ya muungano zitatekelezwa kwa mujibu wa matakwa ya chama.
Tunabaki kujiuliza, je, chama kiliingiaje katika suala la muungano?
Kama alivyojadili nguruvi3, Sio tu ccm, bali hata ASP na TANU havikuhusika katika kuleta muungano 1964. Uamuzi huu ulikuwa ni wa marais wawili kwa kutumia mamlaka yao kama wawakilishi wa wananchi. Isitoshe, nchi ilikuwa bado ndani ya mfumo wa vyama vingi (vilifutwa 1965). Mkataba wa muungano ulifanya kwa makusudi kabisa kutohusisha vyama vya siasa na huu unatakiwa ndio uwe msingi wa katiba yoyote tutakayotunga (JMT na Tanganyika). Mkataba wa muungano haukuja na dhana ya kushika hatamu, dhana ambayo ccm ambayo sio tu kwamba haikutajwa kwenye mkataba, pia haikuwepo kama chama cha siasa lakini baadae kikaja kujichukulia mamlaka yote ya muungano kama vile kilihusika kwa namna yoyote. Swali linalojirudia ni je, kama mkataba haukutaja vyama, viliingia vipi?
Itaendelea...
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums