SAMUEL SITTA NA UFUFUO WA TANGANYIKA
SEHEMU YA PILI
Katika sehemu ya kwanza, tulijadili kwamba hoja ya G55 ilikuja katika versions tatu tofauti na sio moja kama wengi wanavyofikiri. Ufahamu juu ya ukweli huu ni muhimu ili kujua jinsi gani serikali ilifanikiwa kuidhibiti hoja hii (tofauti na mkakati wa ccm uliotumia hoja kwamba serikali tatu haikuwa ni sera ya ccm).
Baada ya kujadili hizi versions za Hoja ya G55,ni muhimu kujikumbusha matukio kadhaa yaliyojiri kipindi kile:
Kati ya tarehe 30 july siku ambayo hoja ya G55 ilipoibuliwa kwa mara ya kwanza, na tarehe 24 agosti 1994 ilipokuwa adopted na bunge, zanzibar ilijitoa OIC. Pakatokea pia makubaliano kwamba rais wa znz ataacha kuwa makamo wa rais wa jmt na badala yake kutakuwa na makamu rais ambae atakuwa running mate wa urais wa muungano na atatokea pande tofati wa muungano na ule anaotokea rais; Mwalimu nyerere alihutubia wabunge huku waziri wa sheria na katiba, samuel sitta akiahidi kuandaa chapisho la government white paper juu ya muungano kwa mujibu wa version ya tatu ya hoja ya G55 ambapo umma ungekaribishwa kuchangia mawazo juu ya mfumo wa muungano, hasa suala la kuirudisha Tanganyika; mikakati yote hii ililenga kuanza ipunguza nguvu motion ya G55 lakini ni dhahiri kwamba kuna Limit ya kiwango cha viongozi kuweza chakachua historia. Umma ukifikia sehemu ukasema "sasa imetosha", suala ambalo chama kiliweza dhibiti kwa miaka hamsini kinaweza badilika kwa nguvu ya umma ndani ya siku chache tu;ushahidi wa hili kwa nchi za wenzetu upo wazi;
Tutazame implications za hoja ya G55:
Professor shivji katika kitabu chake titled "let the people speak: Tanzania down the road to neo-liberalism" anasema kwamba:
Ili kuelewa vyema version ya tatu ya G55, kuna haja ya kujadili kwanza versions 1&2. Shivji anasema kwamba version ya kwanza ambayo ililenga kuanzisha serikali ya tanganyika ilikuwa na unresolvable constitutional and political problems; constitutional problem ya kwanza ni kwamba ile motion ilikuwa ni motion binafsi iliyohoji mfumo wa muungano; kwa maana hii, chini ya ibara ya 98(1) ya katiba ya JMT (1977), ingehitajika robo tatu ya kura ya wabunge wote ili kupitishwa, na possibly robo tatu ya wabunge wa znz na bara (rejea ibara ya 98(1b) ya katika ya JMT 1977, kwa vile motion ililenga marekebisho ya katiba ya nchi(jmt). Katika mazingira yale, shivji anasema kwamba hoja isingeweza kupita kwani kura zisingetosha.
Tatizo la pili la version ya kwanza ni kwamba - kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ingelazimu zaidi ya 70% ya katiba ya JMT (1977) kuandikwa upya; hili lisingewezekana kwani ingekuwa ni karibia sawa na kuandika upya katiba kwani moja ya nguzo kuu za katiba ya jmt (1977) ni mfumo wa serikali mbili, na isitoshe, bunge lile halikuwa na mamlaka ya kufanyia mabadiliko katiba ya jmt kiasi cha kugusa its basic structure (hasa mfumo wa muungano);
Na tatu, mabadiliko ya makubwa ya katiba hasa kuirudisha Tanganyika yangewezekana tu kwa kupitia uandikishaji wa katiba mpya ya JMT; na bunge la jmt (pamoja na rais) halikuwa na nguvu za kikatiba kuandika katiba mpya, nguvu hiyo ingetakiwa itokane na bunge la katiba ambalo mamlaka yake na nguvu zake inatakiwa zitoke moja kwa moja kwa wananchi; katika hili shivji anasema kwamba:
In a republic, the people are the ultimate sovereign and possess the powers to constitute a government for themselves. A constituent assembly therefore is a higher body than the parliament
Kwahiyo, hoja inayofuatia ni kwamba - attempt yoyote ya kubadilisha mfumo wa muungano kwa kufanyia marekebisho katiba ya JMT ingekuwa unconstitutional kwa vile ni kinyume na mkataba wa muungano (1964).
Kulikuwepo tatizo lingine la kisiasa kuhusiana na version ya kwanza ya hoja ya G55. Kwa mfano, je nani aliwapa wabunge mamlaka ya kubadilisha mfumo wa jamhuri ya muungao? Kwani wakati wanachaguliwa, walichaguliwa kwa misingi ya katiba ya katiba ile ile ya 1977. Kwa maana hii, iwapo walikuwa wanahisi katiba ile ilikuwa na mapungufu kimfumo, basi utaratibu wa kikatiba wa kufanikisha hili ulihitaji kuhusisha wananchi ili watumie mamlaka waliyonayo kufanya mabadiliko haya kwani sio serikali wala bunge la JMT vilikuwa na mamlaka makubwa zaidi ya wananchi katika kufanikisha jambo lile; hali hii ikapelekea adoption ya Version ya pili na ya tatu;
Ni dhahiri kwamba wabunge walibaini mapungufu tajwa hapo juu ambayo yalikuwepo ndani ya version ya kwanza; kwahiyo wakaja na version ya pili kurekebisha tatizo hili (rejea huko juu), hasa kwa kuja na nyongeza juu ya kura ya maoni/referendum; hivyo version ya pili ikakatua tatizo pungufu la version ya kwanza na sasa kuwa hoja ambayo inasimama na ipo sahihi "legally and politically"; version hii ya pili kimsingi ilikuwa na mambo muhimu yafuatayo:
Wabunge kama wawakilishi wa wananchi wanaona kwamba kuna mapungufu ya kimsingi ya mfumo wa serikali mbili ambao umezaa malalamiko ya pande zote za muungano na kwamba njia sahihi ya kurekebisha tatizo hili ni kwa kurudisha serikali ya Tanganyika, hivyo kuufanya muungano kuwa ni wa serikali tatu - ya muungano, na mbili zinazosimamia masuala je ya muungano katika kila nchi shiriki - serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar. Kwahiyo wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wanapendekeza kwa wananchi hoja hii ili wao ndio wawe na maamuzi ya mwisho; kwa mantiki hii, hoja ya G55 ikaelekeza serikali kuandaa "referendum" ambapo, serikali ingeleta bill bungeni na kuipa serikali mamlaka ya kufanya referendum na kuweka sawa mchakato wa kufanikisha zoezi hili;
Bunge na BILL ya referendum:
Simple majority kwa kanuni za wakati ule zingepitisha version ya pili ya G55 na ingekuwa haijaenda kinyume na mkataba wa muungano, 1964; hivyo kisheria hali ingekuwa sawa; kisiasa - pia hali ingekuwa sawa kwani kimsingi, kilichokuwa kitokee ni wawakilishi wa wananchi (wabunge) kurudisha suala hili fundamenta back to the people/demos;
Katika hali hii, issa shivji alipata kuandika kwamba:
...Now many people have misunderstood and others have deliberately mispresented, the significance and content of a referendum. The kind of referendum on the union structure proposed in the second version of necessity is inseparable from a number of other constitutional questions.
...As I have already argued, if three governments are accepted, we would require a new Constitution. The new constitution clearly couldn't stop at simply providing for three governments. The principles which guide the government or governments;its powers; and structure, etc, all would have to be discussed; all this would have to be done afresh in the light of our history; the current circumstances;the utter legal inadequacy of the present constitution and its doubtful political legitimacy and so on; in short we would have to discuss the whole issue of crystallising a national consensus and establishing a new constitutional order.
The most democratic way of doing it would ofcourse be by a process of national debate preceeding a national referendum; this would mean we would have to consider seriously the calling of a national conference followed by a constituent assembly followed by a referendum on the new draft constitution;
For these reasons, for the powers-that -be, the issue of referendum is an opening up of a "Pandora's Box. No wonder the word had an electric effect on the party (CCM) and state machinery. And no wonder too that some compromises had to be made so long as a "referendum" was kept out.
Mikakati ya kuua hoja ya kura ya maoni ikapelekea kuzaliwa wa version three ya G55 huku mchakato ukiratibiwa kikamilifu na ccm na serikali yake, na waziri wa sheria na katiba wa wakati huo, akiwa ni Samuel Sitta.
Itaendelea...
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums