Mkuu Mkandara, recognition ya mataifa inafanywa na UN!. Tanzania imetambuliwa UN as a United Republic based on its presentation ya ile NV (Note Verbale) ya Chief Erasto Mang'enya. Kwenye NV hiyo ilisema "Artcles of Union ziko attached!, in reality, no arctles were attached!, ndio maana kwenye hoja yangu nimesema Tanzania ni taifa "De Facto" not "De Jure!"!.
Karibu sana Bongo!,
Siku ukiwa mjini, katika pita pita yako, pitia Mtaa wa Mkwepu, ule wa pale mbele ya Club Billicanas, ukitokea upande wa Billcanas kuelekea Round About ya Azam, hapo katikati kuna vijiofisi vingi vingi vya uchochoroni. Moja ya viofisi hivyo imebandikwa bango la PPR!, sukuma huo mlango wa bati, ndani utanikuta!.
Ila kabla hujaja nijulishe ili niazime kiti ofisi ya jirani, vinginevyo utasisima!.
Most welcome!.
Karibu Sana!.
Pasco.
Mkuu wangu shukran sana ila nataka kuuliza hivi! ikiwa kweli recognition ya mataifa hufanywa na UN, kwa nini basi mnataka kuichambua tena recognition ya Tanzannia ambayo tayari ilikwisha pitishwa? kwa nini swala hili lisipelekwe UN kwenyewe kuuliza Uhalali wa Tanzania.
Pili, kama nilivyosema UN huzitambua tu nchi ambazo zinakubaliana na masharti waloweka UN, hii haina maana ya kwamba nchi ambazo hazitambuliwi na UN sio nchi na kuwepo kwake sio halali. Haya ndio maswala yanayoturudisha ktk mgogoro wa nchi kama Palestine na Kosovo japo zipo nchi nyingi tu ambazo sii wanachama wa UN kutokana na sababu maalum aidha ya madai ya nchi nyingine kuwa sehemu ya nchi hiyo sms mtawala wake hakubaliki. Hivyo uhalali wa nchi ni kutokana na kura za wanachama wa nchi na sio matakwa ya wananchi wenyewe. Leo hii rais wa Ukraine ni kionmgozi wa KKK na tayari UN wameisha mkubali.
Hivyo tunaiona hatari hapa ya kupotosha ukweli kwamba kuzungumzia swala la Muungano wa Taanzania kwa kutumia vifungu vya sheria za UN, na sidhani kama tunajenga ila tunatafuta sababu za kutaka serikali 3 kwa kuirudia historia badala ya kueleza kwa nini tunahitaji serikali 3.. UN ni chombo kilichoanzishwa kwa maslahi ya nchi zote duniani kuepukana na kuzitambua nchi zinazokiuka haki za binadamu. Hakuna zaidi ya hilo na msingi wa mwongozo wake wote ni kuhusu haki za binadamu kutokana na historia ya vita vya kwanza.i
Hivyo basi, sidhani ni akili kwa mtoto alozaliwa na wazazi wawili kuanza kuitazama hati ya ndoa ya wazazi wake ili kuthibitisha kwamba ndoa baina ya baba yake na mama yake haikuwa halali na hivyo anataka kujitenga na ndugu zake! Ni kwa kutumia vigezo gani vya kuhalallsha ikiwa UN wenyewe walishapitisha? dio nauliza uhalali gajni maana nijuavyo miye kitanda kakizai haramu na hakuna kitu MTOTO WA HARAMU maana haramu ni kitendo kilichofanywa na wazazi wenyewe.
Ndio kusema huwezi kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maisha yako kwa kutazama kwanza ndoa ya wazazi wako, matatizo ni yako na haiwezekani mtoto akarekebisha ile ndoa ya wazazi kwa kuchapisha cheti kipya cha Kanisa au msikiti wakati wazazi wake hawakuwa wa imani moja. Kusema kweli ni ujinga mkubwa kurudia kuutazama asili ya Muungano wetu kama shirikisho wakati haikuwa shirikisho. Ni upumbavu mwingine kujaza hoja ikiwa wengi ya wabunge wetu hawafahamu kiini cha ujenzi wa muunganoi huu.
Ndio kusema kwamba inaonyesha wabunge wetu na viongozi wetu wengi hawafahamu kabisa muundo wa muungano wetu na hati yake kwa sababu Nijuavyo mimi hakuna maswala yasokuwa ya Muungano kwa bara. HAKUNA ila wanasiasa wetu wamekuja badilisha mengi mwaka 1984. Serikali zilikuwa 2 ile ya Zanzibar na nyingine ni ya Muungano ambapo shughuli zote za Tanganyika zilipelekwa ktk serikali ya Tanzania.
Ni mgawanyo tu wa kazi na shughuli za serikali sio upande ubeeb msalaba wake. Hivyo hapakuwa na maswala yasokuwa ya muungano ktk katiba ya Tanzania isipokuwa kwa kuanisha yale yasokuwa ya Muungano kwa Zanzibar na ndio maana Wabunge wa Zanzibar kitaifa walikuwepo bungeni wakati wakijadili maswala yasiyokuwa ya muungano. Ama hawa wanaobisha watuambie kwa nini wabunge wa Zanzibar walihudhuria vikao bunge la muungano ktk maswala yasokuwa ya muungano?.
Hivyo basi madai ya Zanzibar kuhusu ugawanaji wa pato la Taifa ni halali kabisa hata kama mchango wao ni mdogo. Na hakuna nchi niijuayo mimi ambayo ina wizara zisizokuwa za muungano ktk mapato yake - Hakuna! ila nayaona TZ, tena basi bila kujua kwamba ni mfumo huu ndio tatizo kubwa la Muungano wetu, mfumo unaotugawa ktk mapato ya nchi kuwa sii ya muungano BIG MISTAKE!
Nijuavyo mimi kila nchi iliyopo ktk muungano husema ama kutumia hili neno mamlaka kamili kwa maana ya kwamba wao wenyewe wanapanga mipango ya uendeshaji wa wizara husika makusanyo ya kodi na kadhalika lakini haihusiani kabisa na ugawanaji wa mapato. Mfano kama Jesh la Polisi huko Marekani na Canada Polisi wa Zanzibar hana mamlaka tanzania Bara na yule wa Bara hana mamalaka Zanzibar isipokuwa kwa idhini maalum kutoka chombo cha Kitaifa.
Mamlaka kamili ni kuwezeshwa kuchagua na kuendesha mipango ya maendeleo ya sehemu husika na sio ktk kugawana Umaskini (mapato) hakuna kitu hivyo. Kila nchi hukusanya pato lake na kuchangia mfuko wa Taifa.Serikali kuu huchukua panga lake moja kwa moja kwa asilimia ilowekwa, Hivyo sisi Bara tuzalishe zaidi ya Zanzibar bado asilimia sawa itakatwa kuchangia mfuko wa Taifa.
Nitarudia kusema hivi ikiwa wakati wa Muungano Zanzibar ilikuwa na raia laki 3 wakati ssisi tulikuwa na millioni 11 ni kipi kimebadilka leo tukiwa na watu 40 bara na Znz ina Million 2? piga mahesabu maana wanasema mfumo ule umepitwa na wakati.. wakati upi?.
NNe, ikiwa leo Znz ni watu millioni 2 wakachangia Bil 2 ilihali Tanzania bara yenye watu mil 40 ikachangia Bil 40 kwa nini watu wanasema Znz inachangia kiasi kidogo sana wakichukua Bil. 2 dhidi ya Bil.40 pasipo kuitazama population na asilimia zake?..
Mwisho mkuu nitakutembelea nikipata muda maana nimekamatwa ipaswavyo na maswakla ya mujini. inabidi nimalize hizi shughuli kabla ya kugeuza!