Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Hapana si kweli kuwa kila jambo lazima kuwe na wingi wa wabunge.
Suala la katiba ni la kitaifa na linapaswa kuamuliwa kwa kuangalia mustakabali huo.

Huwezi kusema bunge limeitishwa haraka kwasababu ya vita basi lazima maamuzi yafanyike katika misingi ya vyama. Huo si utaifa.

Suala la katiba halikupaswa kusimamiwa na wabunge waliopo. Ukifuata taratibu utaona lilipaswa kuwa na mkutano wa kitaifa kwanza halafu uchaguzi wa wabunge ambao si hawa wa bunge la JMT

Tukiendekeza wabunge tunapoteza utaifa. Hata wabunge wanawajibu wa kuwajibisha serikali kwa manufaa ya wapiga kura.

Unachosahau ni kuwa wabunge wakiapa hufanya hivyo kwa niaba ya waliowachagua na waliowakataa. Mbunge ni mwakilishi wa watu wote.
Hakuna mbunge mnwakilishi wa CCM Ludewa, Muheza au Kigoma.

Hesabu bado zina matatizo. Wana namba lakini kuna factors zinaozhusiana na namba.
Leo tunajua sahihi zimeghushiwa, mkataba halisi itabidi uje.

Wabunge wa CCM unaodhani ni wengi ndio hao hao walipitisha katiba ya znz ya 2010 siyo bungeni bali katika chama chao ambao wao ni sehemu ya uongozi.

Nani atajaribu kuondoa znz kama si nchi. Nani atawashawishi Watanganyika wabebe mzigo tena. Yes, wanaweza kufanikiwa lakini mwaka 2016 tutaandika katiba tena.
Hawatakuwa na suluhu kama walivyoshindwa miaka 50.
 
kufanikiwa lakini mwaka 2016 tutaandika katiba tena.
Hawatakuwa na suluhu kama walivyoshindwa miaka 50.

Mkuu hapa unamaanisha nini 2016 kuna kipi kitakacho tokea? Nadhani wewe sio mmoja katika wale wanaodhani kwamba kuna mabadiliko kuelekea 2015 election? Hili pia nimeshalijadili kwamba mwaka 2010 mimi nilisimama hapa nikasema CCM is dead nani anaetaka mzoga wake, lakini mwaka jana nikasema nafuta maneno yangu. CCM wataongoza hii nchi kwa muda wa miaka 10 mingine baada ya hapo labda tena labda duru ya siasa inaweza kugeuka, kama tuu upinzani utajitambua.
 
Hjajelewa hoja yangu, nimetumia 2016 kuonyesha kuwa tutakuwa tunaandika katiba kila baada ya miaka 4.

Kitakachochagiza si vyama au uchaguzi. Kuna nguvu itakayotoka kwa wananchi ambao kila siku wanapata uelewa wa katiba. Safari ya uelewa bado ni ndefu lakini wanaelewa. Nguvu hiyo ndio itakayolazimisha uandikaji wa katiba nyingine.
 
Mchambuzi, umeelezea vizuri sana labda kuna kitu kimoja kwa watu wengi wenye kudai "ratification haikufanyika" wanashindwa kukikubali au kukielewa. Ratification haikufanywa na Baraza la Wawakilishi kama wengi wanavyotaka. Isingewezekana kufanywa na BLW kwa sababu moja kubwa tu; halikuwepo.

Chombo kilichofanya ratification ni Baraza la Mapinduzi la Zanzibar. Sasa, watu wengi kwa makosa tu wanafikiria kuwa Baraza la Mapinduzi (Revolutionary Council) ni kama Bunge au Baraza la Wawakilishi. Watu wengi hawajui kuwa pamoja na mabadiliko mbalimbali Baraza la Mapinduzi (BLM) na BLW si kitu kile kile.

Sasa, swali linaweza kuulizwa: Je Baraza la Mapinduzi lilikuwa na nguvu ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wananchi wa Zanzibari? Jibu ni lazima useme "ndiyo" kwani ukisema "hapana" utajikuta kuwa maamuzi mengi yaliyofanywa baada ya Mapinduzi na yanakubaliwa na kusherehekewa na WAzanzibari wengi leo hii yalifanywa na BLM na si BLW.

Kitu ambacho wasomi wetu wengi hawajakifanyia kazi ya kutosha ni hili la BLM na nafasi yake katika utawala wa Zanzibar kabla ya mabadiliko ya 1984 na baadaye.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, mimi ni miongoni mwa hao wanaodai kuwa ratification haikufanyika kwa upande wa Zanzibar!.

Kwa kuanzia naomba ufanye rejea kipengele hiki cha "Articles of the Union"
Naomba nijiquote
Wanabodi,

Kuna hatari kubwa kwa Bunge Maalum La Katiba, kupelekewa "The Act of Union" na kudanganywa eti hizo ndizo "The Articles of Union!", wakati kiuhalisia, hivyo ni vitu viwili tofauti!.

Hati za Muungano zilizotokana na "Makubaliano ya Muungano, wengine wakiita ni Mkataba wa Muungano!, yaani "Articles of The Union!", ni ule uliosainiwa April, 22 1964 Mjini Zanzibar,

The Articles were agreed and signed on 22 April 1964 by Presidents Nyerere of Tanganyika and Karume of Zanzibar on behalf of their respective countries. (KWA KUSHUHUDIA HAPA Julius K. Nyerere, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na abeid Karume, Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wametia saini nakala mbili za mkataba huu, hapa Zanzibar siku ya tarehe Ishirini na mbili ya mwezi Aprili, 1964)

Makubaliano hayo, yaliweka kipengele mahsus hiki,

VII) Mkataba huu utahitaji kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.

Ni kufuatia kipengele hicho, ndipo Bunge la Tanganyika lilitunga sheria ya Muungano, na sheria hii ndio yenye saini ya Msekwa na Chief Adam Sapi Mkwawa!

Hili suala la hati halisi za Muungano nimelizungumza
Hapa-Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu?!

Na Hapa-Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu?!.

Na Hapa-Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?!.

Na Hapa-Jee Wajua Kuwa Kuna Uwezekano Tanzania Sii Nchi Halali Kisheria?!.

Pasco
Hapo kwenye Bold ndicho kipengele kinachozungumzia "ratification".

Kwenye mada yangu hii,
Nimesema ratification ni takwa la kisheria!, its a legal process!, inafanyikwa kwa maandishi!.
Kabla ya Mundane, Zanzibar ilikuwa ni sovereign state yenye kiti chake UN!. Muungano ni "mkataba wa kimataifa" based on "Hati za Muungano" ambazo ni international instruments!. Ili kuzipa hati hizo, nguvu ya kisheria na uhalali wa kisheria to act on Zanzibar, ilibidi hati hizo zifanyiwe "ratification process" ili ziwe applicable kwenye domestic laws za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kwa kuzitungia sheria ya Muungano kama Tanganyika walichofanya ile siku ya Tarehe 25/04/1964 kwenye Bunge la Tanganyika!.

Hakuna legal process yoyote iliyofanyika Zanzibar ku ratify hizo "Articles of The Union" kwa mujibu wa kipengele cha VII cha Hati za Muungano!. Wakati wa Muungano hakukuwa na BLW, bali BLM, sheria zote za BLM zinaitwa Decrees!, hakuna Decree yoyote iliyofanywa na BLM ku ratifay muungano!.

Hata hivyo, pamoja na kukosekana hiyo ratification, kwenye mada yangu ile nimesema Muungano ni halali!, umehalalishwa by performance!.

8. Pamoja na kutokuwepo ratification, Jee Muungano ni halali?....

20.Kupitia hoja hizo na nyingine ambazo sikuzitaja, Mimi Pasco wa JF, kwa Mamlaka niliopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya Kifungu cha "Freedom of Expressions", Sasa Natamka Wazi kuwa Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Haukuwa Ratified Properly in Zanzibar!. Ila pia Nasisitiza, Muungano Huu ni Halali, japo ulikosa uhalali kwa njia ya Expressly in Zanzibar, umepata uhalali huo Impliedly!.

Natanguliza shukrani.

Pasco.
Kitu kikubwa katika ratification ni hitaji la kisheria, hufanywa kisheria!, likifanyika vinginevyo vyovyote vile, hata kama ni kwa nia njema, kama halijakidhi matakwa ya kisheria, halijafanyika!, hivyo hakuna ratification yoyote ya muungano iliyofanyika Zanzibar!.

Kufuatia kutofanyika ratification hiyo, hakumaanishi muungano sio halali, no way, muungano ni halali ila Wanzanzibar wakiamua wenyewe kwa ridhaa yao kuwa hawautaki tena muungano!, they can just walk away, bila any legal obligations kwa sababu hawakuuratify in the first place!.

Kuna mahali niliufananisha na ndoa ya mkeka!, mwanamke kabakwa bila ridhaa yake, baada ya kubakwa katulia ndani ya ndoa hiyo ya ubakwaji kwa miaka 50!, kitendo tuu cha kutulia ndani ya "dhana ya ndoa", kinahesabika ndio "consent" yenyewe!, kwa vile hakusaini shahada yoyote ya ndoa!, siku akiichoka ndoa hii, hahitaji kuomba talaka!, she can just walk away peacefully!.

Pasco
 
SHAMSA NAHODHA VUAI
ASHINDWA KUELEWA CHANZO CHA MUUNGANO
HAJASOMA MKATABA WA MUUNGANO LICHA YA KUWA WAZIRI KIONGOZI

Katika utetezi wa hoja ya kamati yake Shamsa vuai Nahodha anasema mkataba wa muungano ulitamka kuhusu serikali mbili, ya JMT na SMZ.

Katika hali ya kushangaza Shamsa hakueleza mkataba anaozungumzia ni upi.
Mchambuzi katika bandiko hili https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/635645-siri-ya-hati-ya-muungano-na-njama-za-kuuficha.html ameeleza na kuonyesha kwa nyaraka hatua azilizotumika kuanzia siku ya muungano hadi jina la Tanganyika linatoweka.

Katika uzi huo, Mchambuzi kaonyesha bila shaka kuhusu Tanganyika ilivyofutwa kwa seria ya mwaka 1967, kutengenezwa kwa Tanzania bara na Zanzibar kwa katiba ya mwaka 1977, kujiondoa taratibu kwa katiba ya znz ya 1984 hadi kuondoka kabisa katika muungano kwa katiba ya 2010.

Bandiko hilo lina vielelezo na tarehe ya kila tukio.
Shamsi anaposimama na kusema muungano ulikusudia mataifa mawili, ni ushahidi kuwa waziri kiongozi wa znz hajui muungano ulianza na kumalizwa vipi.
Pengine maana Nahodha anadhani bado kuna muungano.

Katika malalamiko ya wznz moja ni lile la kukiukwa kwa mkataba wa muungano.
Nahodha anapaswa kusimama na kutetea kama mzanzibar.

Baada ya kutimuliwa uwaziri wa ulinzi, Nahodha alikimbilia znz na kusema yeye ni 'znz kwanza'
Hieleweki hiyo znz kwanza anawezaje kuipata chini ya kivuli kizito cha Tanganyika.

Nadhani Nahodha alipaswa kwenda maktaba na si bunge la katiba. Kwa mtu wa hadhi ya waziri kiongozi kutoa hoja laini, urojo kama alizotoa, hilo linatosha ni ushahidi kuwa majadiliano ya muungano ni magumu.
Ugumu ni pale wanapokuwepo watu wanaoishi kwa hisia na wasiojua hasa wanataka nini.

Tusemezane
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, mimi ni miongoni mwa hao wanaodai kuwa ratification haikufanyika kwa upande wa Zanzibar!.

Kwa kuanzia naomba ufanye rejea kipengele hiki cha "Articles of the Union"
Naomba nijiquote

Hapo kwenye Bold ndicho kipengele kinachozungumzia "ratification".

Kwenye mada yangu hii,
Nimesema ratification ni takwa la kisheria!, its a legal process!, inafanyikwa kwa maandishi!.
Kabla ya Mundane, Zanzibar ilikuwa ni sovereign state yenye kiti chake UN!. Muungano ni "mkataba wa kimataifa" based on "Hati za Muungano" ambazo ni international instruments!. Ili kuzipa hati hizo, nguvu ya kisheria na uhalali wa kisheria to act on Zanzibar, ilibidi hati hizo zifanyiwe "ratification process" ili ziwe applicable kwenye domestic laws za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kwa kuzitungia sheria ya Muungano kama Tanganyika walichofanya ile siku ya Tarehe 25/04/1964 kwenye Bunge la Tanganyika!.

Hakuna legal process yoyote iliyofanyika Zanzibar ku ratify hizo "Articles of The Union" kwa mujibu wa kipengele cha VII cha Hati za Muungano!. Wakati wa Muungano hakukuwa na BLW, bali BLM, sheria zote za BLM zinaitwa Decrees!, hakuna Decree yoyote iliyofanywa na BLM ku ratifay muungano!.

Hata hivyo, pamoja na kukosekana hiyo ratification, kwenye mada yangu ile nimesema Muungano ni halali!, umehalalishwa by performance!.

Kitu kikubwa katika ratification ni hitaji la kisheria, hufanywa kisheria!, likifanyika vinginevyo vyovyote vile, hata kama ni kwa nia njema, kama halijakidhi matakwa ya kisheria, halijafanyika!, hivyo hakuna ratification yoyote ya muungano iliyofanyika Zanzibar!.

Kufuatia kutofanyika ratification hiyo, hakumaanishi muungano sio halali, no way, muungano ni halali ila Wanzanzibar wakiamua wenyewe kwa ridhaa yao kuwa hawautaki tena muungano!, they can just walk away, bila any legal obligations kwa sababu hawakuuratify in the first place!.

Kuna mahali niliufananisha na ndoa ya mkeka!, mwanamke kabakwa bila ridhaa yake, baada ya kubakwa katulia ndani ya ndoa hiyo ya ubakwaji kwa miaka 50!, kitendo tuu cha kutulia ndani ya "dhana ya ndoa", kinahesabika ndio "consent" yenyewe!, kwa vile hakusaini shahada yoyote ya ndoa!, siku akiichoka ndoa hii, hahitaji kuomba talaka!, she can just walk away peacefully!.

Pasco
Pasco,
mkuu wangu mbona wsomi nyie mnachanganya sana madawa? nani kasema nchi ili iwe nchi inahitaji kiti chake UN? Zanzibar ilikuwa nchi hata kabla ya kupata Uhuru, swala la kupewa kiti UN kinahusiana na utawala uliopo kuhalalisha na kukubaliwa na mataifa. Hivyo kuna nchi ambazo ni soverign lakini hazina kiti UN kwa sababu utawala wake hautambuliwi kimataifa.

Unajua mkuu wangu swala hili la Muungano wa Yanganyika na Zanzibar mnataka sana kulifanya la kikanisa yaani kuna utaratibu maalum wa ndoa hii,hivyo mtu akifanya ndoa ya mkeka haina uhalali kwa sababu tu mzungu huitambua ndoa ya aina ya kanisani.

Nitarudia kusema kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kipekee na hamuwezi kuuweka ktk mafunzo ya elimu ama shirikisho kama m wajumbe wengi wanavyodai. Muungano wetu umetokana na historia ya nchi zetu ambayo haifanani na shirikisho lolote iwe la Marekani ama Uingereza, Egypt na kadhalika toka tamaduni, mila na mazingira yake. Hivyo kutumia mifano ya sijui Marekani kuwa ni federation basi nasi tuwe hivyo inawapotosha wananchi. Mbona watu hawaitazami RUSSIA ambayo iliunda federation wakaingia ktk civil war, hadi mkombozi Lenin alipoingia na mapinduzi na kuunda Muungano (UNION) ya USSR ambayo tumeyaona matokeo baada ya mzee Goba kufikiri anaweza kutatua mahitaji ya wananchi na nchi yake kikatiba kwa kutumia kero za wananchi badala ya Russia ina mahitaji gani yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi.

Sasa leo hii mnadai ratification ili hali baraza la Mapinduzi la wajumbe 10 ndilo pia lilikuwa baraza la mawaziri na unaweza fanyia utafuiti utagundua kwamba0 mawaziri wote wa baraza hilo ndio walokuwa viongozi wa kwanza wa baraza la mawaziri wa Tanzania. Sasa iweje hawa watu wachukue majukumu ya kuwa mawaziri ktk baraza jipya la serikali ya muungano lakini huklo nyuma hawakuwahi kuukubali muungano wenyewe? wengine wanadai ati mwanasheria hakuwa Mzanzibar, sasa kweli mnataka kunambia huko Afghanstan ambako mwanasheria mkuu alikuwa Taliban na muumini wa sharia law ndiye alotakiwa kumuapisha rais Karzai?

Sina maana ya kwamba mwanaseria yule alikuwa muumini wa sheria za utawala wa Sultan lakini bado kabisa Zanzibar ilikuwa na sheria zilizowatenga weusi na huyo mwanasheria akitafsiri sheria hizo dhidi ya weusi. Kwa hiyo ni sawa kwenu mwanasheria huyo huyo alowakandamiza weusi, atumiwe hata baada ya Mapinduzi? Jamanui mwanasheia ni kama sheikh au Padre tu anaweza wafungisha ndoa watu na ikatambuliwqa kisheria, tatizo lisemwe ktk usajili wa ndoa hiyo na kina nani waloikubali ndoa. Zanzibar mpya ilizaliwa siku ya Mapinduzi na hakika Serikali, Mahakama na Bunge la Zanzibar kwa wakati huo wa mapinduzi halikuwa tena Utatu mtakatifu. Zanzibar mpya ilizaliwa na mambo mapya kwa maana ya kwamba baada ya mapinduzi ingewezekana kabisa Zanzibar ingevuliwa uanachama UN na kutotambuliwa kimataifa ilihali sisi ni wamoja muungano ulikuwa lazima.

Mkuu wangu sababu za kuunda muungano huo wa kipekee na uloweza kudumu hadi leokwa miaka 50 ni nyingi sana kama kuna kiongozi yeyote aloweza kuzama ndani ya muungano huo. Labda niseme tu ya kwamba kila napowasoma humu, hujenga fikra za kwamba humu kuna waumini tu sawa na Waislaam na Wakristu wanaotumia imani zao kujenga hoja dhidi ya ndoa ya Mkristu na Muislaam mkijiuliza ni sheria gani ya ndoa imetumika?maana haiswihi! Je, wengine mnatumia sheria za kiislaam kutoikubali na wengine mnatumia sheria za kikristu kutoikubali vile vile lakini nyote mmeshindwa kuelewa kwamba kinachowaunganisha nyie nyote kuwa na hoja moja ni hiyo IMANI yenu ya Utanganyika na Uzanzibar. Tanzania yetu haina dini, kabila wala mila na desturi za wazungu maana ilizaliwa kwa historia yetu sisi na sii ya Marekani wala Egypt.

Hata hivyo mkuu wangu niko mujini fanya tuonane...maana nimesilikiza bunge na zioja vyake nashindwa hata kucheka, kulia ama kununa. By the time bunge hili linakwisha serikali ya Tz itakuwa katika deficit ya ajabu na wala msije shangaa!
 
Pasco,
mkuu wangu mbona wsomi nyie mnachanganya sana madawa? nani kasema nchi ili iwe nchi inahitaji kiti chake UN?
Mkuu Mkandara, recognition ya mataifa inafanywa na UN!. Tanzania imetambuliwa UN as a United Republic based on its presentation ya ile NV (Note Verbale) ya Chief Erasto Mang'enya. Kwenye NV hiyo ilisema "Artcles of Union ziko attached!, in reality, no arctles were attached!, ndio maana kwenye hoja yangu nimesema Tanzania ni taifa "De Facto" not "De Jure!"!.

Hata hivyo mkuu wangu niko mujini fanya tuonane...maana nimesilikiza bunge na zioja vyake nashindwa hata kucheka, kulia ama kununa. By the time bunge hili linakwisha serikali ya Tz itakuwa katika deficit ya ajabu na wala msije shangaa!
Karibu sana Bongo!,
Siku ukiwa mjini, katika pita pita yako, pitia Mtaa wa Mkwepu, ule wa pale mbele ya Club Billicanas, ukitokea upande wa Billcanas kuelekea Round About ya Azam, hapo katikati kuna vijiofisi vingi vingi vya uchochoroni. Moja ya viofisi hivyo imebandikwa bango la PPR!, sukuma huo mlango wa bati, ndani utanikuta!.

Ila kabla hujaja nijulishe ili niazime kiti ofisi ya jirani, vinginevyo utasisima!.

Most welcome!.
Karibu Sana!.

Pasco.
 
Mkuu Mkandara, recognition ya mataifa inafanywa na UN!. Tanzania imetambuliwa UN as a United Republic based on its presentation ya ile NV (Note Verbale) ya Chief Erasto Mang'enya. Kwenye NV hiyo ilisema "Artcles of Union ziko attached!, in reality, no arctles were attached!, ndio maana kwenye hoja yangu nimesema Tanzania ni taifa "De Facto" not "De Jure!"!.

Karibu sana Bongo!,
Siku ukiwa mjini, katika pita pita yako, pitia Mtaa wa Mkwepu, ule wa pale mbele ya Club Billicanas, ukitokea upande wa Billcanas kuelekea Round About ya Azam, hapo katikati kuna vijiofisi vingi vingi vya uchochoroni. Moja ya viofisi hivyo imebandikwa bango la PPR!, sukuma huo mlango wa bati, ndani utanikuta!.

Ila kabla hujaja nijulishe ili niazime kiti ofisi ya jirani, vinginevyo utasisima!.

Most welcome!.
Karibu Sana!.

Pasco.
Mkuu wangu shukran sana ila nataka kuuliza hivi! ikiwa kweli recognition ya mataifa hufanywa na UN, kwa nini basi mnataka kuichambua tena recognition ya Tanzannia ambayo tayari ilikwisha pitishwa? kwa nini swala hili lisipelekwe UN kwenyewe kuuliza Uhalali wa Tanzania.
Pili, kama nilivyosema UN huzitambua tu nchi ambazo zinakubaliana na masharti waloweka UN, hii haina maana ya kwamba nchi ambazo hazitambuliwi na UN sio nchi na kuwepo kwake sio halali. Haya ndio maswala yanayoturudisha ktk mgogoro wa nchi kama Palestine na Kosovo japo zipo nchi nyingi tu ambazo sii wanachama wa UN kutokana na sababu maalum aidha ya madai ya nchi nyingine kuwa sehemu ya nchi hiyo sms mtawala wake hakubaliki. Hivyo uhalali wa nchi ni kutokana na kura za wanachama wa nchi na sio matakwa ya wananchi wenyewe. Leo hii rais wa Ukraine ni kionmgozi wa KKK na tayari UN wameisha mkubali.

Hivyo tunaiona hatari hapa ya kupotosha ukweli kwamba kuzungumzia swala la Muungano wa Taanzania kwa kutumia vifungu vya sheria za UN, na sidhani kama tunajenga ila tunatafuta sababu za kutaka serikali 3 kwa kuirudia historia badala ya kueleza kwa nini tunahitaji serikali 3.. UN ni chombo kilichoanzishwa kwa maslahi ya nchi zote duniani kuepukana na kuzitambua nchi zinazokiuka haki za binadamu. Hakuna zaidi ya hilo na msingi wa mwongozo wake wote ni kuhusu haki za binadamu kutokana na historia ya vita vya kwanza.i

Hivyo basi, sidhani ni akili kwa mtoto alozaliwa na wazazi wawili kuanza kuitazama hati ya ndoa ya wazazi wake ili kuthibitisha kwamba ndoa baina ya baba yake na mama yake haikuwa halali na hivyo anataka kujitenga na ndugu zake! Ni kwa kutumia vigezo gani vya kuhalallsha ikiwa UN wenyewe walishapitisha? dio nauliza uhalali gajni maana nijuavyo miye kitanda kakizai haramu na hakuna kitu MTOTO WA HARAMU maana haramu ni kitendo kilichofanywa na wazazi wenyewe.

Ndio kusema huwezi kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maisha yako kwa kutazama kwanza ndoa ya wazazi wako, matatizo ni yako na haiwezekani mtoto akarekebisha ile ndoa ya wazazi kwa kuchapisha cheti kipya cha Kanisa au msikiti wakati wazazi wake hawakuwa wa imani moja. Kusema kweli ni ujinga mkubwa kurudia kuutazama asili ya Muungano wetu kama shirikisho wakati haikuwa shirikisho. Ni upumbavu mwingine kujaza hoja ikiwa wengi ya wabunge wetu hawafahamu kiini cha ujenzi wa muunganoi huu.

Ndio kusema kwamba inaonyesha wabunge wetu na viongozi wetu wengi hawafahamu kabisa muundo wa muungano wetu na hati yake kwa sababu Nijuavyo mimi hakuna maswala yasokuwa ya Muungano kwa bara. HAKUNA ila wanasiasa wetu wamekuja badilisha mengi mwaka 1984. Serikali zilikuwa 2 ile ya Zanzibar na nyingine ni ya Muungano ambapo shughuli zote za Tanganyika zilipelekwa ktk serikali ya Tanzania.

Ni mgawanyo tu wa kazi na shughuli za serikali sio upande ubeeb msalaba wake. Hivyo hapakuwa na maswala yasokuwa ya muungano ktk katiba ya Tanzania isipokuwa kwa kuanisha yale yasokuwa ya Muungano kwa Zanzibar na ndio maana Wabunge wa Zanzibar kitaifa walikuwepo bungeni wakati wakijadili maswala yasiyokuwa ya muungano. Ama hawa wanaobisha watuambie kwa nini wabunge wa Zanzibar walihudhuria vikao bunge la muungano ktk maswala yasokuwa ya muungano?.

Hivyo basi madai ya Zanzibar kuhusu ugawanaji wa pato la Taifa ni halali kabisa hata kama mchango wao ni mdogo. Na hakuna nchi niijuayo mimi ambayo ina wizara zisizokuwa za muungano ktk mapato yake - Hakuna! ila nayaona TZ, tena basi bila kujua kwamba ni mfumo huu ndio tatizo kubwa la Muungano wetu, mfumo unaotugawa ktk mapato ya nchi kuwa sii ya muungano BIG MISTAKE!

Nijuavyo mimi kila nchi iliyopo ktk muungano husema ama kutumia hili neno mamlaka kamili kwa maana ya kwamba wao wenyewe wanapanga mipango ya uendeshaji wa wizara husika makusanyo ya kodi na kadhalika lakini haihusiani kabisa na ugawanaji wa mapato. Mfano kama Jesh la Polisi huko Marekani na Canada Polisi wa Zanzibar hana mamlaka tanzania Bara na yule wa Bara hana mamalaka Zanzibar isipokuwa kwa idhini maalum kutoka chombo cha Kitaifa.

Mamlaka kamili ni kuwezeshwa kuchagua na kuendesha mipango ya maendeleo ya sehemu husika na sio ktk kugawana Umaskini (mapato) hakuna kitu hivyo. Kila nchi hukusanya pato lake na kuchangia mfuko wa Taifa.Serikali kuu huchukua panga lake moja kwa moja kwa asilimia ilowekwa, Hivyo sisi Bara tuzalishe zaidi ya Zanzibar bado asilimia sawa itakatwa kuchangia mfuko wa Taifa.

Nitarudia kusema hivi ikiwa wakati wa Muungano Zanzibar ilikuwa na raia laki 3 wakati ssisi tulikuwa na millioni 11 ni kipi kimebadilka leo tukiwa na watu 40 bara na Znz ina Million 2? piga mahesabu maana wanasema mfumo ule umepitwa na wakati.. wakati upi?.

NNe, ikiwa leo Znz ni watu millioni 2 wakachangia Bil 2 ilihali Tanzania bara yenye watu mil 40 ikachangia Bil 40 kwa nini watu wanasema Znz inachangia kiasi kidogo sana wakichukua Bil. 2 dhidi ya Bil.40 pasipo kuitazama population na asilimia zake?..

Mwisho mkuu nitakutembelea nikipata muda maana nimekamatwa ipaswavyo na maswakla ya mujini. inabidi nimalize hizi shughuli kabla ya kugeuza!
 
Mkuu Mkandara, recognition ya mataifa inafanywa na UN!. Tanzania imetambuliwa UN as a United Republic based on its presentation ya ile NV (Note Verbale) ya Chief Erasto Mang'enya. Kwenye NV hiyo ilisema "Articles of Union ziko attached!, in reality, no articles were attached!, ndio maana kwenye hoja yangu nimesema Tanzania ni taifa "De Facto" not "De Jure!"!.

Karibu sana Bongo!,
Siku ukiwa mjini, katika pita pita yako, pitia Mtaa wa Mkwepu, ule wa pale mbele ya Club Billicanas, ukitokea upande wa Billcanas kuelekea Round About ya Azam, hapo katikati kuna vijiofisi vingi vingi vya uchochoroni. Moja ya viofisi hivyo imebandikwa bango la PPR!, sukuma huo mlango wa bati, ndani utanikuta!.

Ila kabla hujaja nijulishe ili niazime kiti ofisi ya jirani, vinginevyo utasisima!.

Most welcome!.
Karibu Sana!.

Pasco.

Pasco,

Hapo nilipowekea rangi ni mawazo yako, ambayo hujayathibitisha. UN hawafanyi mambo yao kiswahili swahili kuwa uwaambie articles ziko attached lakini ukawa hujaziattach halafu wakakaa kimya, kungekuwa na follow memo kutoka ofisi ya Katibu mkuu kuulizia ziko wapi articles hizo. Kwa vile hujaweza kuonyesha kuwa Umaja wa mataifa uliulizia articles hizo, basi usieneze hisia zako binafsi bila kuwa na ushahidi. Nakala ya cover page inayoonekana kwenye website ya UN siyo kuwa ndilo lililokuwa dossier lote liliwasilishwa huko. Kulikuwa na documents nyingi kuoneysha kuwa serikali mpya ya Muungano inakubaliana na wajibu wa iliyokuwa Tanganyika na iliyokuwa Zanzibar kwa pamoja, yaani itatakeleza mikataba yote ambayo iliingiwa na nchi hizo kabla ya kuungana.
 
Mkuu Kichuguu, kanisome hapa [h=3]Jee Wajua Kuwa Kuna Uwezekano Tanzania Sii Nchi Halali ...[/h]
[h=3]Bunge Maalum Lapigwa Changa la Macho!? Lapewa"Act of .[/h]
Pasco.
 
Huko ulikonituma kupasoma niliwahi kupasoma zamani sana. Hisia zako ulizoweka kule bado unaziendeleza hata wakati huu ambapo bunge linafanya kazi ya muhimu kwa future ya nchi hii. Hebu angalia ulivyoliza swali conjecturally

"Hivyo msingi mkuu wa Taifa la Tanzania ni zile hati ambazo zimeelezwa kuwasilishwa na lile tangazo la Balozi, swali ni jee Hati hizo, ziliwasilishwa?, kwanini hazikuwasilishwa?, bila hati hizo Tanzania bado ni taifa?. Uhalali wa Tanzania kama Taifa bila hati ukoje?.

Hilo swali ni conjecture ambayo unaijibu kwa hypothesis usiyothibitisha. Mambo ya aina hii hayastahili kuumiza vichwa vya watanzania kweni ndiyo yanayochangia kuwachanganya akili wabunge wetu wasiokuwa makini na kuishia kuzungumza mambo ya kuhisi tu. Binafsi ningeiona hii ni hoja ya maana iwapo ungethibitisha kuwa hati hazikupelekwa, na hivyo kurtusaidia kuelewa kuwa UN siyo chombo makini.
 
Wakuu zangu naangusha kitu kizito sana naomba mchango wenu ktk mjadala utakao fuatia. Nitauita - AJIZI NYUMBA YA UMASKINI na sii NJAA!
 
UPOTOSHAJI TULIOUSEMA NDIO HUU

Baadhi wa wachangiaji wamesema ni kitu kigumu kuunganisha majeshi ya nchi tatu na hilo litapelekea jeshi kutawala.

Ukisoma rasimu ya katiba, jeshi ni moja na ni miongoni mwa mambo 7.
Rasimu haikusema kutakuwa na jeshi la znz wala la Tanganyika au muungano.

Mambo yaliyoachwa kwa serikali ya washirika ni jeshi kama ulinzi na usalama na mengine.
Ni jambo la kushangaza kuona waziri anasimama na kutetea hoja ya majeshi matatu.

Hii ni dalili kuwa hoja zimekwisha na sasa ni vitisho kwa wananchi.
Hoja kama ya gharama imezungumzwa lakini hakuna anayekuja na gharama za serikali mbili kuonyesha utofauti na tatu.

Wazungumzaji wa upande wa serikali 2 wamejikita katika kusema 'ni nzuri' wala hawaonyeshi uzuri upo wapi.

Ni hao ndio waliomnanga Warioba na tume na sasa hawana majibu yatokanayo na rasimu.
Hili litabaki kuwa tatizo kwa kukosa majibu.

Katika mambo yanayoshangaza ni kuona wajumbe wa znz wakitetea mfumo wa serikali 2.
Hii ni baada ya kubaini kuwa mfumo huo tofauti na wanavyoaminishwa, unawafaidisha.

Kwa bahati mbaya, Wajumbe wa Tanzania hawawezi kutetea Tanganyika kwasababu ni Watanzania isipokuwa wachache wa upinzani na wenye weledi.

Uppotoshaji utaendelea na tutasikia mengi.
Ukweli kwamba hoja za Warioba hazijibiwi unaeleza kazi nzito na nzuri ya tume.

Tunauliza wajumbe, tuonyesheni uzuri wa serikali 2
Kinyume cha hapo Watanganyika wajiandae na miaka mingine ya kulipia gharama za nchi jirani.
Zigo hilo walipitishe kwa watoto wao mapema bila kusita.

Bila Tanganyika huru, Tanzania stable haipo.

Tusemezane
 
Upotoshaji sasa unaenda mbali zaidi. Waziri Lukuvi akimwakilisha waziri mkuu anaenda kanisani kusema kwamba wanaodai mamlaka kamili zanzibar wana agenda ya kislamu - jamani, huu sio uchochezi? Damu zikimwagika Lukuvi atapona "the hague" kweli?

Mbona mkataba wa muungano (1964) uliweka wazi suala la mamlaka kamili kwa pande zote juu ya masuala nje ya kumi na moja ya muungano? Mamlaka kamili na udini yanaingiaje?

Viongozi wanafikia hatua ya kusema kwamba serikali tatu zikipita, ccm itakabidhi madaraka ya nchi kwa jeshi (Lukuvi ananukuliwa kanisani), hivi bado kuna haja ya Rais kumwacha ndani ya baraza la mawaziri katika nyakati hizi ambapo nchi inaelekea kwenye machafuko?

Ama kweli hiki ni Kiwewe cha Tanganyika. CCM inajua kwamba kwa vile ilikataa Tanganyika, haitapata kura za urais wa Tanganyika, kwani mgombea wake ataomba kura kuongoza kit gani wakati yeye na chama chake walikikataa? Mgombea wa ccm zanzibar nae hatopita kwani zanzibar ilihitaji Tanganyika (serikali tatu) ili iwe na mamlaka kamili juu ya masuala nje ya muungano. Urais wa muungano pia kwa ccm utakuwa mashakani.

Kiwewe mara nyingine mwisho wake huwa ni kifo.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu mchambuzi ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa tunaona upuuzi huku bara na visiwani.

Angalia clip hii

Kimsingi kinachoongewa ni upuuzi na jazba jazba kwa kuwa hakuna substance, lakini ukikusanya yote unaona wazi kuwa hawa jamaa wanasema kuwa hakuna haja ya serikali mbili au tatu...wanataka tugawane mbao za jahazi. Which in my opinion will make a lot of economic sense to mainland. Kuna jamaa mmoja aliyevaa shati la bluu anaonekana kama Hitler.

https://www.youtube.com/watch?v=x8AOlS67rYQ&sns

cc nguruvi3, Mzee mwanakijiji, Barubaru, jmall, murutongore, anna tibaijuka, kichuguu, mkandara, pasco
 
KIWEWE CHA KUZINGUKA TANGANYIKA SASA DHAHIRI
WANAMAZINGAOMBWE WAISHIWA MBINU
KIKWETE ALIWEKA TAIFA REHANI, TUNAKOELEKEA KUBAYA, JK KUBEBA 'DAMU'

Mbinu zote kuanzia hatua ya kwanza ya kukimbia mkutano wa kitaifa, kupeleka mswada hovyo, kumtumia Rais na Mwenyekiti kubadilisha maoni ya tume n.k. zimeonekana kushindikana.
Ukweli unabaki kuwa maoni na kauli za wananchi hazina budi kusikilizwa.

Katika hali ya kiwewe cha kuzinduka kwa Tanganyika, Serikali kupitia CCM wameanza upotoshaji.
Upotoshaji kama nao umegonga mwamba. Wananchi hawaelewi , wanazidi kuchanganyikiwa

Kwa mfano, CCM iliyojaa mapapa ya ufisadi imepata wapi huruma za kulalamikia gharama za serikali 3?

CCM inaulizwa kama 3 ni gharama, na ilijulikana uwezekano wa 1,2,3 na mkataba ulikuwepo, kulikuwa na haja gani ya kuunda tume iliyotumia mabilioni ya pesa yaliyowatia wananchi gharama?

Wananchi wanahoji,maoni waliyoambiwa watoe yana maana gani kama hayafanyiwi kazi?
Wanauliza, miaka 50 haikuwezekana, je,bora kuendele akubahatisha kwa miaka mingine 50 ijayo?

Wananchi wanauliza kama hakuna serikali 3 kwasasa, na Rais anasema yapo mambo yasiyo ya muungano yameondolewa na yanazidi kuondolewa, mambo hayo ni ya nani na yanapelekwa wapi?

Maswali kama hayo na mengine yanawatia CCM kiwewe kwasababu hawana majibu rasmi zaidi ya kupotosha na kubabaisha. Hakuna mchangiaji wa rasimu aliyeweza kueleza kinagaubaga mapato ya JMT ya leo yanatoka wapi kiasi cha kudhani serikali ya shirikisho haitakuwa na mapato rasmi.

Kutokana na kiwewe hicho tumemsikia Rais akimnanga mzee Warioba, hakutueleza nini atafanya na kwa mbinu gani tofauti na miaka 50 iliyopita.

Rais akaenda mbali hata kulishirikisha jeshi, jambo ambalo si sahihi.
Wanajeshi kwa sheria zilizopo hawapaswi kuwa wanasiasa au kuwafungaminisha na siasa

Rais alifanya hivyo ili kujenga hofu kwa wananchi, bila kujua anakaribisha tatizo lingine kwa upande wa pili na anakiuka miongozo ya nchi ambayo yeye ndiye 'custodian'

Endapo Kikwete anaogopa jeshi lisiingilie mambo ya nchi, iweje uchaguzi wa mwaka 2010, kama Amir jeshi mkuu aliruhusu mnadhimu wa jeshi kuingia kati uchaguzi?
Mbona rais hakuonyesha wasi wasi wa jeshi kuingilia mambo ya kisiasa ambayo ni ya raia?

Lakini kubwa zaidi ni la hivi majuzi ambapo waziri Lukuvi akiwa mwakilishi wa serikali alisimama kanisani na kutoa msimamo wa serikali 2.
Hii ni mbinu dhaifu na dalili za wanamazingaombwe kuishiwa na hoja.

Ni mbinu hatari sana kwasababu wanasiasa siku zote husema 'dini na siasa havichanganyiki'
Leo wapi Lukuvi amepata ushujaa wa kuchanganya mambo hayo?

Hakuna shaka ametumwa na serikali ambayo mkuu wake ni Rais Kikwete.
Lengo lake kuu ni kuwagawa wananchi ili mgawanyo huo utoe mafao kwa CCM.

Lukuvi ameenda bungeni kutetea msimamo wake ambao ni wa serikali.
Utetezi wake umeongeza 'sensitization' katika mambo ya dini.

Kikwete amesahau mvutano ulikokuwepo miaka ya karibuni kuhusu mambo ya dini. Tunamshukuru mungu Watanzania ni waelewa vinginevyo tungekuwa na hadithi tusiotaka hata kuitaja.

Leo Kikwete anamtuma waziri aende kanisani kutafutwa kuungwa mkono.

Hivi akitokea kiongozi mwingine akaenda Jamatini au msikitini kufikisha ujumbe kama wa Lukuvi, kiongozi huyo atakuwa amekosea wapi na atahukumiwa na sheria ipi ambayo haimgusi Lukuvi au serikali iliyomtuma?

Hivi Kikwete haoni yanayotokea Nigeria na Afrika ya kati, na wala hakujifunza kwa yale ya Kenya aliyokwenda kusuluhisha?

Kwabahati mbaya sana, Watanzania ni watu wa ajabu.
Badala ya kuangalia walipojikwaa, wao huangalia walipoangukia.

Lukuvi hana hatia, ni mjumbe aliyetumwa na serikali ya Kikwete.
Hadi sasa serikali ya Kikwete imekaa kimya bila kumwajibisha ikielewa Lukuvi ni mjumbe tu.

Tatizo si Lukuvi, tatizo ni serikali ya JK iliyomtuma Lukuvi katika nyumba za dini.
Siku zijazo kikwete hatakuwa na maadili ya kiroho(moral authority) ya kukemea uovu ndani ya nyumba za ibada.
Swali atakalokutana nalo ni moja, Mbona Lukuvi aliposema ilikuwa jambo zuri na kawaida?

Ni kwa mtazamo mpana tunaweza kusema, kwa lolote lile litakalokuwa na madhara(mungu aepushe) kwa damu ya Watanzania hakika Lukuvi hana hatia, ni njiwa tu aliyepeleka salamu.

Mwenye kubeba dhamana ya matatizo yanayotengenezwa na serikali ya JK ni JK.
Hilo akae akijua na hakika hatakuwa na mahali pa kujitetea.

Ndio maana inasemwa, Tanganyika inaleta kiwewe. Mazingaombwe sasa mbinu zimekwisha na hatari inayotengenezwa na JK atakayebeba dhamana hiyo ni JK.

Waswahili husema mjumbe hauawi, mwacheni Lukuvi apeleke barua kama tarishi, muulizeni mwenye ujumbe, njia anayolipeleka taifa ina heri?

Tusemezane.

Usikose Duru za siasa: UKAWA wanavyobabaika, historia ya juisi ya maembe kujirudia.

Anna Tibaijuka Dr.F.Ndugulile Nape Nnauye HKigwangalla John Mnyika Bongolander zumbemkuu Mzee Mwanakijiji Mag3 Mkandara Mchambuzi Kichuguu Kimweri Kichuguu Pasco Andrew Nkumbi Zakumi JokaKuu Zitto Kabwe AshaDii Mkuu wa chuo Ritz
 
Kama hatauta mumunya maneno naweza kusema this is one of lowest points in our politics, by any means it should not be brought to worshiping places. Leo sitalaumu mwenyekiti wa CUF akituma wajumbe wake misikitini, au mwenyekiti na NRA akianza kueneza siasa misikitini. Inaonekana wazi kabisa kuwa tunachosema hakifai tunakifanya wenyewe.

Lakini vile vile ni aibu sana kwa kanisa kumruhusu mtu kama Lukuvi kwenda madhabahuni na kutumia madhabahu kama uwanja wa siasa. Tunapolaumu content ya aliyosema Lukuvi, tusisahau kuwa Kanisa limefanya kosa kubwa sana, na linatakiwa kukemewa kwa kushiriki kuvunja sheria za nchi.
 
haya yanawezekana kwa kuwa huko madhabahuni kumejaa wanasiasa na si wachungaji wa kondoo wa bwana. Umeshawahi ona wapi dini ikahusishwa kwenye kuandaa mustakabali wa taifa kwa kigezo cha moral authority?leo hii acceptance ya Wachungaji ni part and parcel ya approval process za wanasiasa wetu.

Anachokifanya Lowasa kwenye makanisa kimetazamwa mpaka kimeonekana ni kitu cha kawaida na si tatizo.But, as we always comment humu kwenye jukwaa. JK is Tanzania "Achilles heel" whether he likes it or not.
The buck stops with the president. And, so far he has passed it on to God Knows where so many times, it has stopped being funny.
This "Katiba" will define Kikwete Legacy, and am not the only one who thinks the chap doesn't really care how-positive or negative.
 
It is the lowest in deed!
Mkuu haya hayakuanza leo, tofauti na zamani, sasa yamerasimishwa.
Huko nyuma kulikuwa na juhudi za kuhakikisha dini zinatumika kwenye mambo ya 'moral' siku hizi dini zinatumiwa na morons.

Kikwete amebadili mwelekeo wa taifa hili kuelekea njia mbaya kwa kiasi kikubwa.
Kitu kinachotia maudhi sana, hawa viongozi wa dini wapo mstari wa mbele kukemea uhalifu.

Wakishaondoka kukemea uhalifu wa vibaka na machangudoa wanarudi kwenye makasiri yao kuzungumzia uhalifu mwingine na wanasiasa wakiwa na glass za chai na juisi, wakipanga namna ya 'kuteka' waumini wao huko misikitini na makanisani.

Binafsi simalaumu Lukuvi hata kidogo, yeye ametumwa na kama ujuavyo elimu yake haimruhusu kwenda kinyume na maagizo. Maisha yake yanategemea kutumwa na alichofanya ni kubeba ujumbe hata kama ujumbe huo utakuwa ni samadi au baruti.
Kazi ya Lukuvi ni kutua mzigo at the destination as one piece.

Tuangalie ujumbe alioubeba umetoka kwa nani.
Ujumbe alioutoa umetoka serikalini ambako mkuu wake ni Rais.

Hivyo ujumbe ni wa Rais, ndiye tunayepaswa kumuuliza kama ujumbe huo una heri na nchi hii au umelenga kutengeneza 'bomu' JK anadhani likilipuka akiwa Msoga Chalinze atakuwa salama!

Hapa nakubaliane nawe kuwa kanisani limefanya makosa na linashusha hadhi yake ya kukemea uovu kwani linaimarisha uovu.

Lakini pia, mlizinzi wa watu na mali zao kwa mujibu wa katiba yetu naye kapeleka ujumbe kanisani ambao lengo lake na mwisho wake ni tatizo kwetu.

Huyu tumwambie, Rais kama unategemea kustaafu, tuachie nchi yetu salama huko unakopeleka taifa ni kubaya

haya yanawezekana kwa kuwa huko madhabahuni kumejaa wanasiasa na si wachungaji wa kondoo wa bwana. Umeshawahi ona wapi dini ikahusishwa kwenye kuandaa mustakabali wa taifa kwa kigezo cha moral authority?leo hii acceptance ya Wachungaji ni part and parcel ya approval process za wanasiasa wetu.

Anachokifanya Lowasa kwenye makanisa kimetazamwa mpaka kimeonekana ni kitu cha kawaida na si tatizo.But, as we always comment humu kwenye jukwaa. JK is Tanzania "Achilles heel" whether he likes it or not.
The buck stops with the president. And, so far he has passed it on to God Knows where so many times, it has stopped being funny.
This "Katiba" will define Kikwete Legacy, and am not the only one who thinks the chap doesn't really care how-positive or negative.
Mkuu nilikemea sana kitendo cha Samwel Sitta kwenda kuwaona Pengo na Mufti Simba.
Nilisema hawa ni sehemu ya jamii hivyo wapewe nafasi kama watu wngine na si kuwapa kipaumbele cha maamuzi ya kisiasa.

Nilikemea sana kitendo cha Lipumba kuzungumza Msikitini si kwa maudhui tu bali kama kiongozi wa kisiasa.

Nipo katika rekodi nikikemea Pengo kujiingiza katika comment za mambo ya muungano.
Pengo, ni kadinali wa ajabu, anapenda sana kujishirikisha katika siasa pengine tofauti na wazee kama Rugambwa waliokuwa wanajishughulisha sana na mambo ya kiimani kuliko siasa.

Hili la kanisa kumwalika Lukuvi ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana.
Nasimama kusema wazi kanisa lililomwalika Lukuvi kufikisha ujumbe wa Kikwete linahubiri kitu gani cha maana? Nasema hivyo kwasababu kama hilo kanisa halioni hatari inayotengenezwa na wanasiasa sijui linaona hatari gani nyingine katika jamii.

Hawa akina EL, Samwel Sitta walikuwa kambi moja ya mtandao.
Wanaujua udhaifu wa mkuu wetu kikamalifu.
JK ameachia hali hii kwa muda na nachelea kusema hana uwezo wa kuizuia bali kuipa uhalali tu.

Lukuvi hana kosa, yeye ni tarishi, ametumwa na Serikali ya JK kwenda kuchochoe hisia.
Tunayepaswa kumuuliza ni JK, je , huko ndiko alipoamua kulitosa taifa?

Hivi kesho Kikwete atasikilizwa na nani kukitokea mambo mabaya yanayohusisha dini?
Nani anaweza kumtuhumu mwenzake katika boti inayozama wakiwa wote ni abiria?

Kikwete anapata wapi moral authority ya kuzuia matatizo siku zijazo ikiwa ameshaondoa heshima ya kufanya hivyo?

Jamani, tusimshambulie Lukuvi, mwenye ujumbe huo ni Kikwete ambaye ni mkuu wa Serikali.
Tumuulize JK taifa lipo njia sahihi au limekwenda off road?

Na huko kwenye mitaro, na madaraja linakoelekea nani atalikwamua?
Ndivyo alivyoamua kuliacha taifa katika matatizo makubwa namna hii.

The buck stops with President, hakuna namna kikwete atakwepa lawama, tuhuma au maswali kuhusu haya ya Lukuvi.

Lukuvi ameshasema ametumwa na serikali ambayo mkuu wake ni JK.
Tumeusikia ujumbe wa JK kanisani, aliyeupeleka ni Lukuvi
 
Back
Top Bottom