Unajua wewe huwa mgumu sana kusoma kitu ukaelewa.. Msome tena Mchambuzi alichoeleza juu ya Mwenyekiti Anna alisema nini baada ya neno BILA YA...Hapa bado unazunguka mkuu. Hoja ni kuwa kauli ipi ni sahihi?
1. Mwenyekiti Anna anasema ukitamka tu UKAWA tayari umeshapoteza uanachama
2. Zitto anasema, wapo tayari kuungana na UKAWA
Kama Chair Anna Mghirwa yupo sahihi kwa mujibu wa katiba ya ACT, na Zitto yupo sahihi kwa mujibu wa katiba ya ACT kama msemaji wa chama, ni kauli ipi ipo sahihi?
Labda utapeli mkubwa upo UKAWA ambao wanadai Umoja wa Katiba ya Wananchi halafu wanachagua watu wa kuingia kama vile katiba ya Warioba wameihodhi wao. Mkuu unaweza tumia lugha yoyote kukashifu mtu ama kitu lakini ukweli tunaujua. Mlisema kwanza Zitto atahamia NCCR - haikuwa, Zitto atahamia CCM - haikuwa, Zitto anapeleka habari TISS wakati Slaa anapokea habari toka TISS. Ni kosa kubwa kuwasiliana na TISS ni Uhaini..kweli?
Yaani kuema kweli CDM walikosea sana kutafuta awamu ya tatu kwa nguvu za kisiasa wakati ukweli umekuja jitokeza kuwa wao ndio wana matatizo. Binafsi yangu Kamati kuu kuendelea na muhula wa 3, halfu kesho wakichukua nchi ndio waachie Uongozi wa chaa ni kujihakikishia nafasi za juu wao tu kila hatua ya maendeleo ya Chama.
Na ndio maana sishangai sana pale Slaa alipotaka mshahara mkubwa kuacha kugombea Ubunge iii awe katibu mkuu wa chama. Aliweka masharti ambayo Chadema haikuwa na jinsi wakati kina Mbowe na Ndesa walitumia fedha yao toka mfuko kukisimamisha chama..Mkuu kuna upuuzi upuuzi unafanyika Chadema inahitaji sana moyo kuuvumilia.