Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Msome Mbowe hapa chini kiduchu.Good, now that we understand each other...sasa tuendelee kuijadili mada iliyo mbele yetu; Duru za siasa: Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani.
Hii mada ilianzishwa na Nguruvi3 tarehe 11 Mei 2014, siku tano baada ya Chama cha ACT-Tanzania kupata usajili wa kudumu huku ikidaiwa kuwa Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba ni wanachama waanzilishi na mlezi wa chama akitajwa kuwa ni Zitto Kabwe. Msajili wa Vyama Jaji Mutungi alikabidhi cheti kwa kaimu Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Kadawi Limbu, katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma tarehe 6 Mei 2014.
Kwa kitendo hicho, Chama cha ACT-TANZANIA kilivunja rekodi kwa kukabidhiwa cheti chake cha usajili wa kudumu rasmi ndani ya muda mfupi kuliko wakati wowote huko nyuma mara baada ya usajili wa muda. Hali hiyo haikuwahi kutokea katika historia ya vyama vingi nchini na wengi walibaki wakijiuliza kulikoni wakikumbuka usajili wa vyama huko nyuma ulivyogubikwa na mizengwe hadi vingine kunyimwa usajili kabisa kwa hofu ya kuwa mpini kwa chama tawala.
Kwa Mujibu wa Msajili wa vyama vya siasa Nchini chama hicho kilidaiwa kupata wanachama 200 kila mkoa katika mikoa 10 Tanzania bara na visiwani na hivyo kuungana na 22 vyenye usajili wa kudumu vitakavyoshiriki katika chaguzi mbalimbali ukiwemo uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2015. Hata hivyo haikuweza kuthibitika mara moja kama uhakiki wa hao wanachama ulifanywa na ofisi ya msajili kama ulivyotakiwa.
Wakati chama cha ACT-Tanzania kinapata usajili wa kudumu, aliyedaiwa kuwa mlezi wake, Zitto Kabwe, alikuwa amefungua kesi mahakamani akipinga kufukuzwa Chadema. Ikumbukwe kuwa washiriki wa Zitto, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba tayari walikuwa wamekwishatinga huko kwa chama chao kipya. Ajabu ni kwamba chama hakikuzinduliwa kwa muda wa mwaka moja, je walikuwa wanamsubiri Supreme Leader?
Hivi tafsiri ya usaliti ukoje? Haya tuendelee...
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema hawatamruhusu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Kauli ya Mbowe imetolewa siku chache baada ya Zitto kutangaza kuwa ACT ipo tayari kujiunga na Ukawa kama wanavyotaka Watanzania wakiwamo baadhi ya viongozi wa umoja huo.Alitoa kauli hiyo jana wilayani Kyerwa alipozungumza na MTANZANIA.Mbowe alisema kuwa hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM).Hatuwezi kumruhusu Zitto na chama chake kiwe miongoni mwa Ukawa. Tukiruhusu Zitto awepo siri zote zitakuwa zikiwafikia CCM, alisema Mbowe.Aprili 15 mwaka huu, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), kilitangaza kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la kuleta mapinduzi ya uchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya wananchi.Zitto alisema hivi sasa taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia ya kufanikisha malengo ya kukitoa CCM madarakani.
Cc; Kimweri.
Last edited by a moderator: