Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Good, now that we understand each other...sasa tuendelee kuijadili mada iliyo mbele yetu; Duru za siasa: Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani.

Hii mada ilianzishwa na Nguruvi3 tarehe 11 Mei 2014, siku tano baada ya Chama cha ACT-Tanzania kupata usajili wa kudumu huku ikidaiwa kuwa Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba ni wanachama waanzilishi na mlezi wa chama akitajwa kuwa ni Zitto Kabwe. Msajili wa Vyama Jaji Mutungi alikabidhi cheti kwa kaimu Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Kadawi Limbu, katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma tarehe 6 Mei 2014.

Kwa kitendo hicho, Chama cha ACT-TANZANIA kilivunja rekodi kwa kukabidhiwa cheti chake cha usajili wa kudumu rasmi ndani ya muda mfupi kuliko wakati wowote huko nyuma mara baada ya usajili wa muda. Hali hiyo haikuwahi kutokea katika historia ya vyama vingi nchini na wengi walibaki wakijiuliza kulikoni wakikumbuka usajili wa vyama huko nyuma ulivyogubikwa na mizengwe hadi vingine kunyimwa usajili kabisa kwa hofu ya kuwa mpini kwa chama tawala.

Kwa Mujibu wa Msajili wa vyama vya siasa Nchini chama hicho kilidaiwa kupata wanachama 200 kila mkoa katika mikoa 10 Tanzania bara na visiwani na hivyo kuungana na 22 vyenye usajili wa kudumu vitakavyoshiriki katika chaguzi mbalimbali ukiwemo uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2015. Hata hivyo haikuweza kuthibitika mara moja kama uhakiki wa hao wanachama ulifanywa na ofisi ya msajili kama ulivyotakiwa.

Wakati chama cha ACT-Tanzania kinapata usajili wa kudumu, aliyedaiwa kuwa mlezi wake, Zitto Kabwe, alikuwa amefungua kesi mahakamani akipinga kufukuzwa Chadema. Ikumbukwe kuwa washiriki wa Zitto, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba tayari walikuwa wamekwishatinga huko kwa chama chao kipya. Ajabu ni kwamba chama hakikuzinduliwa kwa muda wa mwaka moja, je walikuwa wanamsubiri Supreme Leader?

Hivi tafsiri ya usaliti ukoje? Haya tuendelee...
Msome Mbowe hapa chini kiduchu.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema hawatamruhusu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Kauli ya Mbowe imetolewa siku chache baada ya Zitto kutangaza kuwa ACT ipo tayari kujiunga na Ukawa kama wanavyotaka Watanzania wakiwamo baadhi ya viongozi wa umoja huo.Alitoa kauli hiyo jana wilayani Kyerwa alipozungumza na MTANZANIA.Mbowe alisema kuwa hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM).“Hatuwezi kumruhusu Zitto na chama chake kiwe miongoni mwa Ukawa. Tukiruhusu Zitto awepo siri zote zitakuwa zikiwafikia CCM,” alisema Mbowe.Aprili 15 mwaka huu, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), kilitangaza kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la kuleta mapinduzi ya uchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya wananchi.Zitto alisema hivi sasa taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia ya kufanikisha malengo ya kukitoa CCM madarakani.

Cc; Kimweri.
 
Last edited by a moderator:
The papers confirm the transfer of financial resources from the central government to the local ones. However, that isn't a point we disagree. Is it?

Anyway the role of the central government in financing the LGAs is a Ponzi scheme. It robs Peter to pay Paul.

The point we disagree is that - while you argue that LGAs are financially strapped to an extent that they cant even affaord to pay their employees salaries, i argue that they can pay salaries but cant finance development projects, hence dependence from central government by means of subsidies to finance the later.

Can you show us from your sources that LGAs also rely on subsidies to pay salaries to their employees?
 
Msome Mbowe hapa chini kiduchu.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema hawatamruhusu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Kauli ya Mbowe imetolewa siku chache baada ya Zitto kutangaza kuwa ACT ipo tayari kujiunga na Ukawa kama wanavyotaka Watanzania wakiwamo baadhi ya viongozi wa umoja huo.Alitoa kauli hiyo jana wilayani Kyerwa alipozungumza na MTANZANIA.Mbowe alisema kuwa hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM)."Hatuwezi kumruhusu Zitto na chama chake kiwe miongoni mwa Ukawa. Tukiruhusu Zitto awepo siri zote zitakuwa zikiwafikia CCM," alisema Mbowe.Aprili 15 mwaka huu, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), kilitangaza kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la kuleta mapinduzi ya uchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya wananchi.Zitto alisema hivi sasa taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia ya kufanikisha malengo ya kukitoa CCM madarakani.

Cc; Kimweri.

UKAWA maana yake ni umoja wa katiba ya wananchi. Umoja huo ulizaliwa kutokana na CCM kuingilia mchakato wa katiba kwa kuchakachua maoni ya wananchi yaliyotolewa mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba iliyokuwa chini ya jaji warioba. Ukawa walipoona maoni na msimamo wao unapuuzwa kwa maana ya kwamba CCM haipo tayari kuingia katika maridhiano, Ukawa wakaamua kuachana na mchakato "haramu' na kurudi kwa wananchi. Zitto akiwa kama mmoja wa wajumbe wa bunge la katiba hakuwaunga mkono ukawa, badala yake akasema wazi kwamba:

1. Ukawa walikosea kutoka nje ya bunge;
2. Akaenda mbali na kuwaita ukawa 'wasaka tonge',
3. Na kwamba msimamo wao juu ya mfumo wa serikali tatu una nia ovu ya kuvunja muungano.

Zitto kwanza ajibu maswali yafuatayo:

1. Je kitendo cha ukawa kutoka nje ya bunge kilikuwa ni sahihi?
2. Je mtazamo wake kwamba ukawa ni wasaka tonge sasa umebadilika? Kwanini?
3. Mtazamo wake kwamba serikali tatu zitavunja muungano, umebadilika? Kwanini?
4. Ukawa sasa sio haramu tena bali halali?

Washirika wa Zitto kwa maana wasaliti wenzake, kitila mkumbo na mwigamba, wote waliweka wazi msimamo wao kwamba nia yao kujiunga chama kipya ni kuleta aina mpya ya upinzani, chama ambacho kitapambana na Chadema ili chama hicho kiafanikiwe kukiangamiza chadema kisiasa na kuwa chama kikuu kipya cha upinzani nchini. Ushahidi wa maneno haya upo wazi kwenye gaeti la raia mwema kupitia kitila mkumbo. Chama hicho kipya cha kupambana na Chadema sasa kinajulikana kama ACT Wazalendo. Je:

1. Zitto haoni kwamba kuna mgongano hapa kwa maana ya kwamba, dhamira ya ACT ambayo ipo wazi mchana kweupe ni kujiunga na mpinzani wake namba moja Chadema ili kuvuruga safari ya UKAWA?

2. Je, ACT haijiamini kwamba inaweza kushinda bila ya kushirikiana na ukawa?

Pia tusisahau kwamba, Zitto alishatangaza kwamba:

a) Kama wananchi ya majimbo ya Kigoma wanataka maendeleo, waipigie kura ACT kwenye majimbo yote ya Kigoma, na sio ukawa.

b) Kwamba ACT itapambana na chadema kwa gharama yoyote kunyakua ngome za Chadema DSM kwa maana ya majimbo ya Segerea, Kawe na Ubungo.

Lengo kuu la Ukawa ni kuendeleza nguvu katika ngome hizo tatu, na pia kuchukua majimbo mengine yote ya CCM DSM, yani kinondoni, ilala, temeke, Kigamboni na Ukonga. Kwa zitto, ACT haina shida na ngome hizi za CCM, lakini ina tatizo na ngome za Chadema/ukawa. Je:

Je Zitto haoni kufikia hapa, msimamo na mtazamo wake hauendani na malengo na maono ya UKAWA?
 
mchambuzi,
mkuu wala hunasababu kabisa ya kutumia UKAWA kujenga hoja ya uchaguzi kwa sababu umesema mwenyewe kuwa UKAWA niUMOJA WA KATIBA ya WANANCHI. Katiba sio Uchaguzi na wapo engi ndani ya uchaguzi huu hawakuwa members wa bunge la katiba. je, yalikuwa makosa kutoka nje ya bunge? nadhani unakumbuka hata mimi nilisema ni makosa kwa sababu kutoka kwao kuliwapa nafas CCM kufanya watakalo juu ya uadishi wa katiba ile. Sura moja ikasababisha sura zote zitokane na fikra za CCM ilihali wananchi walitaka mambo mengine mengi ya kiutawala na haki zao kama raia wa nchi hii.

Jambo jingine kubwa zaidi ni kutambua kwamba walichokitaka na haswa serikali 3 ni kutafuta nafasi za madaraka yao katika uongozi, haituhusu wananchi zaidi ya kwamba tunatambua mipaka na tofauti zetulakini haituongezei haki wala wajibu. ni changa la macho tu kwa sababu WATU wakisha ungana ukaanza kuleta chako chako changu changu ni kugawana umaskini kama alivyosema mwalimu Nyerere wakati mmoja. Hizi ni siasa za wasaka tonge, kosa la Zitto ni kusema ukweli.

3. Ni kweli serikali 3 za Jumuiya zikitumia neno la Shirikisho zingevunja Muungano. huwezi pindua maamuzi yalopitishwa na Artical of Union kwa kutotombua uhalai wake kisha mkaunda serikali 3 ndani ya Artical msoitambua. Hivyo ili itambulike inabidi kuvunja Muungano halafu iandikwe mpya kutokana na maridhiano mapya ambayo aidha iwe ni serikali 1,2 au 3.

Kama wana UKAWA wanatambua kwamba Nyerere na Karume walikuwa ni wale walozoea vya kunyonga vya kuchinja hawawezi utasemaje palikuwa na Muungano pale? Sisi wananchi tuliwasikia viongozi wa UKAWA wakiweka madai haya kiasi kwamba Jussa akatukanwa na kuitwa Mwarabu, ilifikia pabaya sana na pengine kama wangeendelea na Bunge nadhani mikono ingerushwa mule.

4. UKAWA ni jina tu limeendelea kutumiwa kwa faida ya wanasiasa wenyewe maana hakuna UMOJA hapo ni kugawana majimbo na kila mtu na chake, yale yale ya serikali 3 kutaka mambo ya muungano na yasokuwa ya Muungano. Yaani wanaungana dhidi ya CCM lakini haiwatawasaidia wananchi lolote zaidi ya kuwagawa. Hivyo Zitto kaqtoa suggestion kama kweli wana nia ya dhati sasa hivi waungane kwa lengo kubwa ni kubomoa mfumo wa kinyonyaji ili kuwaletea wananchi mapinduzi ya kiuchumi.

Fikra hizi na wazo kama hili linajenga zaidi ya kusema ati UKAWA ipo kugawana majimbo kama kwamba CCM wameisha tolewa. Jengeni hoja za kisera kwanza ili kumuondoa CCM sio kutumia Katiba ilishindikana ati kuwa sababu ya kumuondoa CCM..
 
mchambuzi,
mkuu wala hunasababu kabisa ya kutumia UKAWA kujenga hoja ya uchaguzi kwa sababu umesema mwenyewe kuwa UKAWA niUMOJA WA KATIBA ya WANANCHI. Katiba sio Uchaguzi na wapo engi ndani ya uchaguzi huu hawakuwa members wa bunge la katiba.

Kwanini Zitto anatafuta kuingia UKAWA kama umoja huu hauna rellevance yoyote na uchaguzi?
 
Mkuu Mkandara #524 naona unataka ‘kuchepuka' hayo ya katiba ya eneo lake.

Kama utayaongelea na iwe katika muktadha wa ACT na supreme kama ilivyo hoja
za Mchambuzi

Hoja unazoulizwa ni hizi

A ) Kwavile Zitto alisema ni makosa ukawa kutoka nje. Je,alitoka kufanya nini ikiwa alielewa ni makosa.
Lengo lake kutoka lilikuwakufikia matarajio gani

B ) Kwa vile Zitto alishaona UKAWA ni umoja wa wasaka tonge,lini ameona umuhimu wa kuungana na wasaka tonge? Jambo gani lime mbadilisha kushirikiana na wasaka tonge?

C ) Kwa vile UKAWA wana msimamo wa maoni ya tume ya Warioba kuhusu S3, ni vipi Zitto anayeamini S3 zitavunja muungano anaweza kukaa nao katika misimamo miwili tofauti kiasi hicho?

D ) Ni lini Zitto ametambua S3 zitavunja muungano, ikiwa alishawahi kuandika Makala magazetini akishadidia S3 hata kabla ya tume yaWarioba. Ni lini alisimama na kusema alikosea au amebadilisha msimamo

E ) Kwa vile hoja ya UKAWA ni kuongeza wabunge kwa kuimarisha waliopo na kutafuta wengine, na kwavile azma ya Zitto ni kupora maeneo yanayoshikiliwa na UKAWA kama alivyosema, ni kwa vipi Zitto anaweza kushirikiana na UKAWA katika sintofahamu hiyo?

F ) Kwa vile Zitto ameyatamani majimbo ya NCCR Kigoma,Chadema kwingineko, na kwa vile katibu mkuu wa ACT katamani majimbo ya mikoa yapwani (CUF), nini msimamo wa ACT?

Je, hizo ni kauli zao kama watu binafsi au ndio msimamo wa ACT

Na katika mazingira hayo, ACT na supreme wanawezaje kuwa washirika na si washirikina katika jitihda za kuliondoa taifa mikononi mwa wezina mafisadi wa miaka 40?
 
Last edited by a moderator:
The point we disagree is that - while you argue that LGAs are financially strapped to an extent that they cant even affaord to pay their employees salaries, i argue that they can pay salaries but cant finance development projects, hence dependence from central government by means of subsidies to finance the later.

Can you show us from your sources that LGAs also rely on subsidies to pay salaries to their employees?

The thing is some public entities are under the jurisdictions of LGAs, but the central government pay the salaries of those who work in those entities. Take for example primary schools. Who pays the salaries of primary school teachers?

Mind that primary school teachers are the largest group of public employees in any municipal. Please mention just one municipal authority that is self-sufficient to cover the salaries of teachers for one fiscal year.

Furthermore, since LGAs are non profit organizations which don't borrow money, issue municipal bonds, or receive donations, the only sources of their revenues are local taxes (15%) and subsidies from the central government (85%).

Show me one LGA that can only use 15% of its revenues to cover the salaries of its employees. Remember that salaries form the largest expense item in the operations of any public entity.
 
Katika matapeli wa kisiasa ni zitto tu unayemuona anayekufanya uamke saa kumi usiku kumjadili???

kuwa alisema hivi na leo anafanya hivi, Mbowe alisema nini juu ya CUF, NCCR na Kafulila na kafanya nini? in politics that is common..' i said in politics' kwa sababu nkulumba umeamua siasa za online na huwezi kamwe kwenda front tukakusikia kamwe huwezi kufikia level ya zitto

kuwa ni tapeli nimeuliza uthibitisho hauna......ila unasisitiza ni tapeli
Moja ya utapeli ni huu wa majuzi. Supreme alikwenda mahakamani akieleza anapigania haki na demokrasia.

Wiki mbili baada ya hukumu,anavishwa taji la supreme, anakwenda katika vyombo vya habari na kusema yeye alishiriki kuanzisha ACT

Kama alijua kuwa ni mwanachama wa ACT, mahakamani alifuata nini?

Tunajua alikwenda kulinda ubunge usogee sogee.
Hakusema analinda ubunge kama Hamad Rashid au Kafulila walivyofanya, alidanganya ameonewa akijua hakuonewa.

Utapeli mwingine wa supreme ni kukacha posho za bunge lakinikakodi ndege ya milioni 70

Leo yapo ya gharama za TANAPA ambazo hazijafafanuliwa

Hivi kuwaambia wananchi serikali 3 ndio muafaka, halafu kusema zitavunja muungano, hakuna element za utapeli mkuu

Kusema UKAWA ni wasaka tonge, kisha kusema wafanye kazi pamoja, si aina ya utapeli hata kama haujakomaa vizuri

Alposema ana majina ya Uswiss, kisha kushindwa kuyatoa, hapo si aina ya utapeli kweli

Aipochukua hoja za Kafulila zilizoungwa mkono na wabunge wengi wakiwemo CCM, na supreme kusema ni yake, huoni ka mfumo fulani kakitapeli mkuu

Orodha inaendelea, kama unahitaji tuwasiliane hapa jamvini
 
Mkuu Mkandara #524 naona unataka ‘kuchepuka' hayo ya katiba ya eneo lake.

Kama utayaongelea na iwe katika muktadha wa ACT na supreme kama ilivyo hoja
za Mchambuzi

Hoja unazoulizwa ni hizi

A ) Kwavile Zitto alisema ni makosa ukawa kutoka nje. Je,alitoka kufanya nini ikiwa alielewa ni makosa.
Lengo lake kutoka lilikuwakufikia matarajio gani

B ) Kwa vile Zitto alishaona UKAWA ni umoja wa wasaka tonge,lini ameona umuhimu wa kuungana na wasaka tonge? Jambo gani lime mbadilisha kushirikiana na wasaka tonge?

C ) Kwa vile UKAWA wana msimamo wa maoni ya tume ya Warioba kuhusu S3, ni vipi Zitto anayeamini S3 zitavunja muungano anaweza kukaa nao katika misimamo miwili tofauti kiasi hicho?

D ) Ni lini Zitto ametambua S3 zitavunja muungano, ikiwa alishawahi kuandika Makala magazetini akishadidia S3 hata kabla ya tume yaWarioba. Ni lini alisimama na kusema alikosea au amebadilisha msimamo

E ) Kwa vile hoja ya UKAWA ni kuongeza wabunge kwa kuimarisha waliopo na kutafuta wengine, na kwavile azma ya Zitto ni kupora maeneo yanayoshikiliwa na UKAWA kama alivyosema, ni kwa vipi Zitto anaweza kushirikiana na UKAWA katika sintofahamu hiyo?

F ) Kwa vile Zitto ameyatamani majimbo ya NCCR Kigoma,Chadema kwingineko, na kwa vile katibu mkuu wa ACT katamani majimbo ya mikoa yapwani (CUF), nini msimamo wa ACT?

Je, hizo ni kauli zao kama watu binafsi au ndio msimamo wa ACT

Na katika mazingira hayo, ACT na supreme wanawezaje kuwa washirika na si washirikina katika jitihda za kuliondoa taifa mikononi mwa wezina mafisadi wa miaka 40?
Kwa sababu vitu hivi viwili havihusiani na kama kweli wana nia ya dhati wakubali kuungana kwa masharti ya kuvunja mfumo wa kinyonyaji ili kuwaletea wananchi mapinduzi ya Kiuchumi (Sera). Hivyo anaondoa priority zao na kutanguliza mahitaji ya Wananchi mbele, jambo ambalo UKAWA hawana na hawatakubali kwa sababu linawaondoa katika dhamira zao - Kusaka tonge.

Mimi naamini Zitto kasema hivyo kuwapima tu akielewa haiwezekani, na kisiasa kajisafisha yeye kuonekana sii mkorofi bali wao maana anajua nia na lengo kuu la UKAWA ni kugawana majimbo, hoyo Katiba imetumika tu kama nyenzo walobakia nayo kisiasa. Nitasema tena acha Zitto mimi mwenyewe nawafikiria hivyo na kama kweli wana nia ya dhati wazungumzie wao watawafanyia nini wananchi tofauti na CCM. Waseme itikadi zao, sera zao kama hazitakuwa na ahadi sawa na zile zile za CCM maana hawazungumzii kuubomoa mfumo uliopo. Katiba haijengi Itikadi wala Sera za vyama, sasa wanaitumia katiba ya nini ktk kutafuta kura za wananchi?
 
wakuu wa mnakasha kuna maswali kadhaa najiuliza, hivi ni kwanini Kiongozi mkuu anapata support kubwa toka kwa viongozi wa CCM? (mfano Mh. Mwigulu Nchemba alimlilia sana KM alivyofukuzwa uanachama)
lakini pia kuna wajumbe wa mnakasha huu hapo kabla walikuwa watetezi wakubwa wa serikali ya CCM na CCM kwa ujumla kama huyu Ritz , imekuaje sasa wamekuwa watetezi wakuu wa Kiongozi Mkuu (KM)? lini walitangaza kuhamia ACT-wazalendo?
Mkuu Zimwi likujualo….
Waswahili wa Pemba….

Hata Team EL imeshaona fursa eneo hilo, ndio maana wanasema mzee akikatwa

jina nyumbani, lazima teamEL itachepuka!

Unakumbuka enzi za Yanga na Pan Africa?

Zumbe, Zumbe! Usitafutie watu chuki
 
Kwani Chadema hawampi support Warioba ambaye hadi leo yuko CCM? au mnategemea naye kujiunga Chadema maana huwezi kisia kitu ikiwa wewe hufikirii hivyo!
 
Kwani Chadema hawampi support Warioba ambaye hadi leo yuko CCM? au mnategemea naye kujiunga Chadema maana huwezi kisia kitu ikiwa wewe hufikirii hivyo!
Yeah, pamoja na CUF, NCCR naakina Maria Sarungi na wenzake!
 
Yeah, pamoja na CUF, NCCR naakina Maria Sarungi na wenzake!
Wewe unafikiri hakuna watu wa CUF, NCCR wanampa support Zitto au hao kina Maria Sarungi pamoja na ukorofi wake. Watu wanajua Zitto mkorofi lakini anasimamia nini penye haki..Na hata miye nampa sipport kubwa Warioba kwa kazi aloifanya japo sikubaliani na muundo wa serikali zake, mengineyo safi kabisa, nampa support Slaa japo ana mapungufu yake, Nampa support Mbowe naye ana mapungufu yake ila sijafikia kuwaamini kabisa.

Nisowaamini ni Jussa, Mbatia na Maalim Seif japo siwachukii kwa hiyo utaona kumsifia mwanamke uzuri wake haina maana unamtaka wewe.
 
Wanabodi,

Mnajua swala la Uchumi wa nchi ni pana sana na hatuwezi kaa hapa tukabishana juu ya pato la taifa na revenue kwa kutumia takwimu maana undani wa vitu hivi unaweza kutupa picha tofauti kabisa. Unaweza soma Tax revenue za mahala ukasema safi na kujisifia lakini in real terms tax hizo ni kubwa na zinawakandamiza wananchi na kuwanufaisha wengine. Tanzania yetu ni mfano mzuri sana wa mfumo mbovu kabisa wa uwekezaji na ukusanyaji taxes. Sijapata kuona kusema kweli ni maajabu ya Firaun kuona nchi tajiri lakini wananchi wake maskini wa kutupwa..

Na kwa huu mtindo wa CCM kuwapa wageni nafuu lakini ukawashindilia wananchi na kodi za asilimia 20 hadi 30 kama sales tax sii mrengo mzuri kabisa na ndio maana binafsi yangu nimesimama katika Ujamaa ambao unadai kodi sawa kwa wote. Halafu basi Tanzania yetu wananchi wanatozwa tax hata kabla ya kupigiwa mahesabu ya manunuzi vs mapato au faida na hasara.

Zipo biashara zinachukua hadi mwaka ndio unaweza kuyaona matunda yake lakini utakandamizwa na tax hadi ukubali kushindwa mwenyewe. Yaani mtu akiuza Tsh. millioni 3 anafuatwa kulipa tax zake, pasipo kutazama huyu mtu kalipa tax kiasi gani ktk matumizi na manunuzi ya mali hizo jambo ambalo huku wenzetu ndivyo wanavyopiga mahesabu. U pay taxes unaponunua na U receive taxes unapouza - tofauti yake ndio unalipa/pwa.

Bongo sivyo hata kama biashara nzima ni hasara kwako, wao wanakuja na kutazama tu machine yao imesema umeuza kiasi fulani lipa kodi kiasi hiki na what about nilizolipa kununulia mali na matumizi? Yaani mwenye biashara analipa kodi mara mbili pasipo kujua na TRA wanafurahia na kupongezwa kwa makusanyo yao. Kwa hiyo, hii nchi yetu hii maisha yanazidi kuwa magumu kwa sababu zimejengwa hila kwa wajanja kupata penyo za kufisadi na walalahoi kuendelea kuumia. Huwezi jenga uchumi kwa njia za panya hata kidogo utawaumiza wengi na hakuna bora litakalo fanyika isipokuwa kwa mwenye kutumia njia hizo hizo za panya ndiye atafaidika na kuitwa mjasiriamali wa mwaka!

Mkandara umenikumbusha mbaali sana suala la SALES TAX.

Hakika mfumo huo wa Sales Tax hautumiki pahala popote duniani zaidi ya TRA ya Tanzania. Na huo ndio unaoleta mgogoro mkubwa sana baina ya wafanyabiashara wa huko Tz na mashine za EFD za TRA. Kwani mashine hizo zimewekwa katika mfumo wa kukata kodi ya mauzo bila kujua mtu huyo amenunua bidhaa ile kwa kiasi gani na amelipia Tax kiasi gani kabla ya kuiweka dukani na kuiuza.

Nimefurahishwa sana na upembuzi wako.

Thanx

Mimi naamini Zitto kasema hivyo kuwapima tu akielewa haiwezekani, na kisiasa kajisafisha yeye kuonekana sii mkorofi bali wao maana anajua nia na lengo kuu la UKAWA ni kugawana majimbo, hoyo Katiba imetumika tu kama nyenzo walobakia nayo kisiasa. Nitasema tena acha Zitto mimi mwenyewe nawafikiria hivyo na kama kweli wana nia ya dhati wazungumzie wao watawafanyia nini wananchi tofauti na CCM. Waseme itikadi zao, sera zao kama hazitakuwa na ahadi sawa na zile zile za CCM maana hawazungumzii kuubomoa mfumo uliopo. Katiba haijengi Itikadi wala Sera za vyama, sasa wanaitumia katiba ya nini ktk kutafuta kura za wananchi?

Hapo kwenye nyekundu.. Nilisema kuwa Zitto ni mnafiki na ni muongo.. Ninashukuru kwa kuona huo unafiki wake na ulaghai wake kwa wananchi.

Tuchukulie ulichosema ni kweli je Zitto anafanya huo unafiki kwa faida ya nani? na huu ulaghai laghai kwa wananchi mpaka lini na kwa nini?

Ifike wakati wanasiasa wasimamie wanachoamini sio huu ulaghai laghai kwa wananchi majukwaani unasema ili na moyoni unapingana na ulichokisema.. na huyu ndo Zitto yaani haamini hata anachokisema mwenyewe.. Leo wasaka tonge, kesho nitaka kujiunga nao, kesho kutwa matatizo yangu na Mbowe yasipelekwe kwenye vyama...

Na kwa bahati mbaya sana viongozi wa Chadema wameangukia katika siasa zake... Cha muhimu ni kum-ignore tu kwani wakiendelea kucheza naye watapoteza muda wao.. Yeye kama Zitto hana cha kupotea kama ningekuwa kiongozi wa Chadema nimgemuacha abwabwaje bwabwaje na bila shaka angechoka na kuacha mwenyewe..
 
Zakumi kamuuliza Mchambuzi kuhusu utapeli wa Zitto. Mkandara kaja na ushahidi wa utapeli.
Anasema kuwa Zitto alikuwa ana wapima UKAWA.

Huo ndio ule utapeli wa kwenda mhakamani akijua hakuna kinachompeleka.
Sasa anacheza na akili za UKAWA, huku wale wafuasi wa kundi la I la Zitto wakiendelea kuamini anachosema bila chembe ya shaka.

Kundi la Pili hawaamini kabisa na wala hawana shaka

Kundi la tatu ndilo lina mashaka yanayopungua kila siku.
Mkandara, mtu aliye na mashaka na Zitto akisoma kauli yako tu ataondoa mashaka na kuelekea kundi la Pili.

Alinda, unafiki ni tabia ya mtu, inaweza kupuliziwa utuli kwa muda tu, mwisho wa siku tabia ni tabia tu inarudi katika mkondo wake sawia.
 
Hapana sio kweli kabisa kwa sababu ulaghai wa kisiasa ni jambo jema hata wale wanaotangaza nia ya Urais wengi wao wanajua hawatashinda, ila basi tu ni katika kujisafisha na kujua nafasi zao kisiasa zimesimama wapi. Huwapimi wananchi bali unatazama nafasi yako kwao na kama kweli wanaamini katika mageuzi unayotaka kuwapelekea.

Unafiki upo katika mifumo yenyewe maana unawekwa kona ambayo huna jinsi isipokuwa kushambulia na haitakiwi kuwekana kona. Zitto kasema viongozi hao ni wasaka tonge na kawapa mtihani kama kweli wao sio wasaka tonge watakubali mabadaliko hayo akijua hawawezi maana sio lengo lao toka mwanzo.

Kama wangekuwa sio wasaka Tonge wangekubali hata pasipo kumtumia yeye kubadilisha siasa zao wakaungana kuwa kitu kimoja badala ya kugawana majimbo halafu wakasema:- UKAWA tumeungana ktk kubadilisha mfumo mzima wa CCM ili kuwaletea wananchi mapinduzi ya Kichumi.. sii lazima yatumike maneno hayo lakini ukweli ni kwamba hawawezi...hata miye hapa najua hawawezi kutenga tofauti zao hata kidogo ila wote wana interest zao. Kwa hiyo unafiki ni kuusema Ukweli?

UKAWA hawazungumzii UCHUMI hata kidogo ni WATU tu.. Nimeisikia hotuba ya Slaa akiwa Marekani nikasema kwa nini hotuba kama hizi hatuzisikii nyumbani.. Ni ukweli usopingika na UKAWA lazima wafahamu kwamba wananchi sio wajinga sana kutotambua mbivu baina na mbichi..
 
Zakumi kamuuliza Mchambuzi kuhusu utapeli wa Zitto. Mkandara kaja na ushahidi wa utapeli.
Anasema kuwa Zitto alikuwa ana wapima UKAWA.

Huo ndio ule utapeli wa kwenda mhakamani akijua hakuna kinachompeleka.
Sasa anacheza na akili za UKAWA, huku wale wafuasi wa kundi la I la Zitto wakiendelea kuamini anachosema bila chembe ya shaka.

Kundi la Pili hawaamini kabisa na wala hawana shaka

Kundi la tatu ndilo lina mashaka yanayopungua kila siku.
Mkandara, mtu aliye na mashaka na Zitto akisoma kauli yako tu ataondoa mashaka na kuelekea kundi la Pili.

Alinda, unafiki ni tabia ya mtu, inaweza kupuliziwa utuli kwa muda tu, mwisho wa siku tabia ni tabia tu inarudi katika mkondo wake sawia.

Wananchi wanazidi kujawa na hofu kutokana na unafiki wa Zitto. Upo ushahidi ulio wazi kwamba ACT ilishapitisha azimio la kukataa kata kata kujihusisha na UKAWA. Ndio maana pengine Mkandara ametoboa siri kwamba zitto anachofanya ni kuchezea tu umma akili. Kwani haiwezekani mwenyekiti wa ACT Taifa - Anna, akapiga marufuku wanachama wake kujihusisha na UKAWA bila ya kufuata katiba, kanuni, taratibu na itifaki za chama chake cha ACT. Haiwezekani. Mwenyekiti Anna hawezi kutoa amri hiyo bila ya kupata idhini ya Supreme Leader Zitto. Kwa mantiki hiyo, Mkandara yupo sahihi kabisa kutoboa siri kwamba anachofanya Zitto ni utapeli na usanii tu wa kisiasa kwa wananchi. Kiongozi wa aina hiyo hafai kupewa dhamana ya kuongoza mabadiliko katika taifa letu. Wananchi wanatafuta mabadiliko hawana muda na mzaa mzaa wa kisiasa. Zitto, yeye anaendesha siasa zake kimzaa mzaatu.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, mbali ya kada wa ACT Mkandara kuwa sahihi kwamba Zitto anachofanya ni utapeli kwa wananchi, pia Mwenyekiti wa ACT, Anna nae yupo sahihi kwani Katiba ya ACT inasema kwamba:

"...kwa mujibu wa kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yoyote ambaye atasaidia kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wa chama kingine, atakuwa amepoteza uanachama wake".

Tunahitaji nini zaidi kuamini kwamba Zitto ni tapeli na msanii wa kisiasa?

Au pengine Zitto hajasoma katiba ya chama chake cha ACT juu ya jinsi gani mwanachama anaweza kupoteza uanachama? Inawezekana Zitto hana muda wa kusoma na kuelewa katiba za vyama ambavyo yeye ni mwanachama kwani hata alipokuwa Chadema, Katiba ya chadema iliweka wazi kabisa kwamba ikitokea mwanachama akaenda kutafuta suluhu mahakamani badala ya ndani ya chama, mwanachama huyo atakuwa amepoteza uanachama wake moja kwa moja bila ya kujalisha matokeo ya kesi mahakamani. Pamoja na hilo kuwa wazi ndani ya katiba ya Chadema, zitto bado akaenda mahakamani kinyume na katiba ya chama chake cha zamani, Chadema.

Kwanini zitto aaminiwe?
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

  • Wananchi wanazidi kujawa na hofu kutokana na unafiki wa Zitto. Upo ushahidi ulio wazi kwamba ACT ilishapitisha azimio la kukataa kata kata kujihusisha na UKAWA. Ndio maana pengine Mkandara ametoboa siri kwamba zitto anachofanya ni kuchezea tu umma akili. Kwani haiwezekani mwenyekiti wa ACT Taifa - Anna, akapiga marufuku wanachama wake kujihusisha na UKAWA bila ya kufuata katiba, kanuni, taratibu na itifaki za chama chake cha ACT. Haiwezekani​

Nime quote sehemu hii ndogo ili nipate kukueleza kwamba Zitto hakuwa nje ya Katiba, wala kanuni za ACT kwa sababu masharti aloyatoa ndio lengo la ACT nayo ni - Kufumua mfumo wa KINYONYAJI uliopo ili kuwaletea wananchi mapinduzi ya kiuchumi. Sasa Zitto analijua hili kwamba UKAWA hawawezi kuufumua mfumo uliopo wa Kinyonyaji ila wanataka kuuboresha na hivyo malengo yao hayapo sawa. Kwa maana nyingine niseme hivi ACT haiwezi kuungana na UKAWA kwa sababu UKAWA hawaamini katika UJAMAA...Zitto kawapa UKAWA mtihani ambao hawawezi kuupokea kutokana na masharti yake yanaegemea mrengo wa ACT..
 
Hapa bado unazunguka mkuu. Hoja ni kuwa kauli ipi ni sahihi?

1. Mwenyekiti Anna anasema ukitamka tu UKAWA tayari umeshapoteza uanachama
2. Zitto anasema, wapo tayari kuungana na UKAWA

Kama Chair Anna Mghirwa yupo sahihi kwa mujibu wa katiba ya ACT, na supreme leader yupo sahihi kwa mujibu wa katiba ya ACT kama msemaji wa chama, ni kauli ipi ipo sahihi?
 
Back
Top Bottom