Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #561
Hakuna ku balance, uzi ni mpini wa CCM ambao ni ACT. Mandelezo ya uzi ni kauli chafu na hatarishi dhidi ya taifa na utaifa.Ndio maana nikasema mwanasiasa anaruhusiwa kusema kweli pale inapohitajika maadam lengo lake ni kuufikisha ujumbe pasipo kutafsirika vibaya..Wote Mbowe na Zitto wamefurahiwa na wakazi wa mji huo na wamewapa pongezi wewe/mimi nani wa kutafsiri kuwa hotuba zao zimejaa ukabila.
Tueleweshe kwanza, kauli za Zitto zilikuwa sahihi kwa kuangalia ukweli wa takwimu na hoja?
Ni kweli kuwa Kilimanjaro na Arusha ndio chanzo cha matatizo ya Mwanza na Shinyanga?
Tunachopigania hapa ni kuondoa kizazi cha wanasiasa matapeli. Hawa akina supreme ni matapeli wanaochipukia.
Hatuwezi kukaa kimya tukiwaona wanakomaa katika utapeli.
Miaka 50 ya matapeli inatosha, sasa ni muda wa kusema, mh supreme leader siasa zako za kulitumbukiza taifa katika xenophobia unaziacha nyumbani kwako. Tanzania ni yetu sote, kuchonganisha mikoa ni jambo la hatari sana.
Ni hatari anayotengeneza supreme lazima ipingwe, ikemewe.
Hatutaweka kalamu chini hadi pale taifa na umma utakapokuwa salama!