Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)



Kitu cha kwanza: ACT sio mali ya Limbu, ingawaje alianzisha. Ni mali ya wanachama. Na wanachama ndio wenye kauli kuliko mwenyekiti.

Pili: Wanachama wana haki ya kubadilisha muundo wa chama. Na haki hiyo hiko extended hata kwa wanachama waliojiunga leo au jana. Hivyo Zitto alipojiunga na ACT alikuwa na haki zake za uanachama.

Tatu: Kuwa mwanzilishi sio sababu ya mtu kutotimuliwa. Hivyo usijenge hoja kwamba waanzilishi walitimuliwa.

Nne: Katiba za vyama vya siasa sio sheria ya nchi. Zinabadilishwa kwa mapenzi ya wanachama. Hivyo matukio ya ndani ya chama hayamuhusu mtu asiye mwanachama. Kama unataka kujihusisha jiunge na chama.
 

Du, haki ya wanachama wawili Kitila na Mwigamba?
Mkuu haya ni majibu ya jazba na kiburi kwa kukwepa hoja za msingi.
 
Mkuu kabla sijajibu hoja zako, hebu tupe takwimu alizotumia Zitto kufikia hitimisho kuwa wananchi wa kanda fulani wanawapora wa kanda nyingine. Kama hiyo kauli si sawa, basi tupe kauli yake sahihi na takwimu alizotumia.

Twende taratibu mkuu


Nguruvi3:

Kwanini unaomba twakimu wakati maswali mengi tu unaogopa kuyajibu? Kwenye zaidi ya posti tatu nimekuuliza kwanini mnaona uzito kukemea ubaguzi wa kidini, kikabila, kikanda unaofanya wa viongozi wa juu wa vyama vya kisiasa, wafanyabiashara au viongozi wa serikali?

Je nikienda TRA, BOT, Usalama wa Taifa, nitapata takwimu zinazoonyesha diversity ya nchi au watu walipata ajira kwa juhudi na sio kubebwa?

Unahusisha matamshi ya Zitto na matukio ya Rwanda. Matatizo ya Rwanda hayakutokea kwa sababu ya siasa tu. Yalikuwa mpaka kwenye muundo wa ajira.

Kwanini watanzania wanachagua rais kutoka makabila madogo na sio makabila makubwa? Kwanini mhaya ana nafasi ndogo sana ya kuwa rais?

Najua hii posti utaacha kuijibu.
 

Mkuu wewe ni mdini na mkabila, ni wapi katiba ya nchi imesema mhaya hawezi kuwa rais wa nchi hii?
Unaweza kutoa ushahidi wa ubaguzi wa kidini, kikabila na kikanda unaofanywa na viongozi wa juu wa kisiasa ukiacha kiongozi mkuu wa ACT?
 
Ok, tueleze amesema nini kwa ufasaha. Pili, tuletee zile data alizotumia kwa hoja ya kwanza.

Nisome kwa umakini Nguruvi3 magie3 Mchambuzi
Naeleza kilichosemwa na Zitto na source ya Takwimu alizozizotoa
Source ya Takwimu alizotoa Zitto zinatoka Tanzania Human Development Report 2014(THDR 2014).
Nanukuu maelezo ya Zitto
"Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa,pia akasema Mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.(Sijaona Zitto aliposema Arusha,Kilimanjaro zinapora utajili wa Shinyanga) kinachofanywa na Nguruvi3 nikuleta uchochezi na chuki ili watu wa Arusha na KLM wamchukie Zitto,na ikiwezekana wamletee fujo,ili aje aandike si tulisema...narudia tena ulistahili ban kwa kupotosha kwa lengo unalolijua mwenyewe
Mchambuzi nawe naomba usome maelezo ya Zitto hapo chini,maana wewe unataka Zitto ataje CCM
" Zitto akasisitiza ndio mana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi,huwezi kuwa na mkoa unashika nafasi ya 4 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namna 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu,Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi,ina Ng'ombe na Pamba.Tunavita moja tu,kufanya Mapinduzi ya mfumowetu was uchumi kutoka mfumo wa kinyonyaji na kifisadi na kujenga uchumi shirikishi,pia Zitto aligusia Takwimu za watu wenye elimu ya sekondari simiyu ni 3.7%, na Dar ni 29% inaongoza nchi mzima
Wapi Zitto kasema Arusha,Kilimanjaro,zinaipokonya Shinyanga,bora weredi wenu mngeonyesha kujadili Takwimu(THDR2014).Kuliko kumlisha maneno Zitto kwa Chuki zenu bila sababu
 
Last edited by a moderator:

Kwa hapa nitamuomba nguvuri3 kwa ruhusa yake nitoke nje ya mada iil kutoa maelezo ya ufahamu wangu juu ya mfumo dume...
 
Last edited by a moderator:

Unachowasilisha hapo juu ni kile kile ambacho tumekuwa tunakipinga kwamba ni ulaghai, upotoshaji na ubaguzi unaofanywa na Supreme Leader Zitto dhidi ya watanzania. Aidha ulipitwa na majibu yetu juu ya hoja hii au unadhania tumesahau tulichosema. Ili kujikumbusha, bofya hapo chini:

https://www.jamiiforums.com/great-t...wa-ccm-kumaliza-upinzani-22.html#post12577398

Nadhani laptop yako uliyoacha ikwiriri sasa umeipata na upo tayari kuchambua takwimu husika.
 

Nimeelewa kuwa kazi yenu kupotosha maneno,nilichosema Laptop nimeacha Dar,na Mimi Nipo Lindi..wapi nilisema nimeacha Laptop Ikwiriri..mlisema mnataka kujua Zitto katoa wapi Takimwi nimewapa jibu hilo katoa Tanzania Human Development Report 2014,na nimesema Zitto alisemaje nikamnuu,ulihoji kwanini Zitto ajaitaja CCM,nikajibu yeye anazungumzua mfumo sio Chama,juzi tena tumemsikia Lema anasema Zitto hawezi isema vibaya CHADEMA mlitaka afanye mnayowaza nyie
majibu mmeyapata na mmeelewa,naomba mniambie wapi Zitto kasema mikoa ya Arusha,KLM inainyosha Shy
 

..mimi nilikuwa nazungumzia sababu za Dr.Sla/a kutimkia CDM mwaka 95.

..nilieleza kwamba mwaka 95 Dr.Sla/a alikuwa mshindi wa kwanza na Patrick Qorro[r.i.p] alikuwa mshindi wa pili ktk kura za maoni kwa jimbo la Karatu.

..sasa CCM-NEC wakamteua Patrick Qorro kusimama kwa tiketi ya CCM. Matokeo yake Dr.Sla/a akajiengua chama hicho na kujiunga na CDM.

..baada ya kusema hayo Mkandara akanidai nilete ushahidi wa matokeo ya kura ya maoni za CCM ya mwaka 95. Mimi nikwambia ni vigumu kwangu kufanya hivyo, nikwambia the best I could do ni kuleta maelezo hayo toka glob inayoheshimika ya huyu jamaa wa Mbulu-Karatu-Hanang.

..nadhani mpaka hapo tuko pamoja sasa.

cc Mkandara, Nguruvi3, zumbemkuu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbona unanichagulia maneno ya kuandika? Mada hii inahusu ACT mbona wamzungumzia Zitto? na sababu yangu kumzungumzia Lema imehusiana na maneno yake mwenyewe juu ya ACT na Zitto, halafu wewe unaweka ukomo watu waandike juu ya nini? Kama huu sio U Supreme kwa sababu tu wewe umeanzisha mada hii, utawezaje kuwa na audesity ya kusema wengine.
 

Mchambuzi mmeomba data mmeletewa na Mkuu Adharusi kakuwekea na source kuwa Zitto alipozipata "Tanzania Human Development Report" bado hautaki unaita ulaghai.

Mkuu wakati mwingine jifunzeni kusoma vitu msivyovipenda.

Mbona data zako ulizoleta watu hawajasema ulaghai.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara.

Bahati nzuri ndugu yetu hapa ukumbini Mkuu Adharusi kutulitea ushahidi wa takwimu alipozipata Zitto lakini Mchambuzi hataki anaita ulaghai ngoja tumsubiri Nguruvi3 maana kapiga sana kelele akiomba hizo takwimu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu huo sio Ushahidi ni hearsay ya mwana Blog ambaye kasikia pia kutoka kwa watu. Na wapo walosema Dr.Slaa aligombea Babati na kuchujwa huko ndio akaenda NCCR kuomba kugombea Babati wakamkatalia akajiunga na Chadema meaning Chadema ilikuwa option yake ya tatu. Hivyo kwa mwenye kuutaka ukweli nadhani angeulizwa mwenyewe au viongozi wa CCM.

Nachokisema 1995 CCM walikuwa wakichuja watu kutafuta anayekubalika kutokana na ushindani wa NCCR ulokuwepo. Hapa Mkapa inasemekana alishindwa ktk kuraza maoni ya wanachama, ati Mwalimu ndiye akampandisha hadi akashinda lakini ukiwauliza wanachama wa CCM wapige kura nchi nzima tusijue kuna upigaji kura wa wanachama wa CCM kumtafuta mgombea Urais wanayempenda?
 
Mkuu Mkandara.

Bahati nzuri ndugu yetu hapa ukumbini Mkuu Adharusi kutulitea ushahidi wa takwimu alipozipata Zitto lakini Mchambuzi hataki anaita ulaghai ngoja tumsubiri Nguruvi3 maana kapiga sana kelele akiomba hizo takwimu.
Sawa kabisa sasa inajulikana kwamba Zitto alitumia GDP kuonyesha jinsi mfumo mbovu wa mikataba unavyoweza kuwagharimu wananchi wa Shinyanga. kama nilivyosema toka zamani Chadema ilikuwa sera yao kuhakikisha mikoa hiyo inafaidika na maliasili zilizopo sasa nashangaa sana kusikia leo wanalalamika juu ya kutajwa Kilimanjaro wakati walikuwa wakizungumzia Mtwara na Lindi dhidi ya Dar sijui ilikuwa dhidi ya wazaramo?

Na toka lini watu wakafikiria kwamba unapoisema Kilimanjaro una maana Wachagga? Je, isije kuwa kweli ndivyo wanavyo fikiri kuwa Kilimanjaro ni ya wachagga na haitakiwi kuzungumziwa! wamekuwa kama Wayahudi ukisema ubaya wa serikali na Utawala wao tayari ni Anti- Semitic kwa sababu wao wenyewe wanaamini Israel is for Jews only!
 

..hili ni jambo dogo sana kwa mimi na wewe kuvutana na kujaza server ya watu hapa.

..naomba tumalize mvutano huu kwa kukubaliana kwamba Dr.Sla/a alikuwa CCM halafu akahamia CDM.

..baada ya kujiunga CDM alishinda ubunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo.

cc Adharusi, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara.

Bahati nzuri ndugu yetu hapa ukumbini Mkuu Adharusi kutulitea ushahidi wa takwimu alipozipata Zitto lakini Mchambuzi hataki anaita ulaghai ngoja tumsubiri Nguruvi3 maana kapiga sana kelele akiomba hizo takwimu.
Alicholeta Adharusi si takwimu. Chukua zile za Mchambuzi uweke sambamaba na za Adharusi! Mlima na Kichugu

Yaani imetia uvivu kujadili takwimu zake ndio maana tumeamua kukaa kimya.
Hivi unaweza kusema Dar inachangia 9% na K'njaro 1% ukaja na conclusion kweli! real!

Ndio maana tunapiga kelele, supreme si kuwa anapotosha tu bali anaharibu uwezo wa vijana kufikiri
 
Hapana mkuu hakuna ukomo, tunajaribu kuzuia watu 'wasichepuke''

Wamejaribu kusema supreme asijadiliwe, wengine wakaingiza escrow na wengine gas na mafuta, kahawa n.k. katika kuhakikisha tunaondoka katika mada ili kumnusuru supreme na hoja nzito mbele ya meza yake

Hapa hakuna u-supreme, ukitaka u-supreme lazima uteuliwa na jopo masaa 24 (siri kali) kisha utawazwe kupitia mkutano mkuu. I mean unatangazwa na kutawazwa hapo hapo.
 
Mkuu wewe ni mdini na mkabila, ni wapi katiba ya nchi imesema mhaya hawezi kuwa rais wa nchi hii?
Unaweza kutoa ushahidi wa ubaguzi wa kidini, kikabila na kikanda unaofanywa na viongozi wa juu wa kisiasa ukiacha kiongozi mkuu wa ACT?

Also the constitution doesn't stipulate that the presidency should alternate between Christians and Muslims? Does it. The answer is no. The question now is why the country elects a muslim president after a christian and vice versa? Is this by design or by coincidence? The truth of the matter is it's by design.

The constitution of any country is as good as the people who follow it. What's more, the constitution alone can't describe every aspect of the society or daily routines of individuals. For instance, you don't wake up every morning thinking about following the constitution. As a matter of fact many Tanzanians don't understand the importance of the constitution. So for the constitution work, it's to be complemented by social norms. Currently, our social norms say that a Haya can't be a president even though there are a good number of qualified Hayas out there.

Likewise, the social norms in CDM say Zitto couldn't be a chairman of the party. Call me name anything you want, but that is the truth.

With regard to ACT, it is a social group too. They will create or probably they have already created their social norms too.

The entire debate we are having here isn't about the violation of the constitution or laws, but rather the social norms. The constitution of Tanzania doesn't say anything about the distribution of wealth and Zitto is entitled to say that Shinyanga isn't getting its share of the deal.

The guardians of social norms will say Zitto is playing divisive politics. Some of us who love red-meat politics we say bring it on.
 
Kijana kaweka asilimia akisema ni takwimu. Hakuna analysis nyingine aliyoona bali kutupa namba tu kwavile kasikia kutoka kwa supreme

Hapa napata nguvu sana ya kupambana na ulaghai, maana kizazi kinavia, kina 'najisiwa' na kudhalilishwa

Ukimuuliza afafanue kwa mistari miwili, hawezi. Maana hajui hata 9.6 imepatikana kutokana na nini
Yeye kameza tu kutoka kwa supreme. Huyu supreme ni hatari kwa ustawi wa taifa

Hapo kijana amaamini ni kweli Shinyanga inaporwa kwa mujibu wa supreme
Kakwepa hoja za supreme kaumba umba maneno.

Tusichoke ama sivyo kizazi kitaangamia mikononi mwa malaghai!
 
Mchambuzi,

..hii mada yako naomba umshirikishe jamaa mmoja anaitwa Kapwela.

..tuliwahi kujadili hizi fitina za Zitto Kabwe lakini hatukuelewana, nadhani wewe umeelezea vizuri sana ukisaidiwa na data.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…