Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Mkuu Mkandara nadhani tuwe honest.

Nilishasema kuwa Waraka ulikuwa childish move, hiyo haina maana naunga mkono kinyume chake.
Ninasimama kwenye hoja kwanza, kama ninavyosimama sasa na kusema Kitila kuteua viongozi ni makosa yale yale aliyokataa na haonekani kujifunza . Nasimama kusema, siasa za Kitila hazilingani na nafasi yake kijamii.
Nasimama kusema kama alivyosema Alinda , wajitokeze wafanye mambo bila kutufanya wajinga.

Kitila alipoandika kuhusu ACT tulijua anaandaa nini, sasa anakuja na njama za kumuokoa ZZK ktuoka katika kesi kiana kwa kusema anamshawishi ili hali tunajua lao moja. Kitila aliyekataa ZZK kushiriki waraka sasa anatuambia kuhusu ushiriki wake.

Kibaya ni utezui wa ZZK kuwa mwenyekiti kama CEO, akiamini Mhusika Mkuu (MM) aliyetakiwa kuwa mwenyekiti sasa anateuliwa kuwa mwenyekiti. Phwee . Angalia nafasi ya hawa jamaa katika jamii halafu angalia uzito wa siasa zao.

Msome Alinda 37, Mchambuzi 38
 
Hakuna anayekataa kwamba CCM kimechoka, kama wapo, basi hawaelewi umuhimu & role ya vyama vya siasa katika maendeleo ya nchi. Socially, politically, economically, CCM is sick, weary and irreparably tainted. The party is no longer fit to govern our nation, and without an alternative, its really frightening to think about what the future holds for our nation.

Vinapojitokeza vyama kama chadema, vyama hivi vinatoa matumaini mengi kwa wale watafuta "mbadala". Chadema chini ya watu kama zitto, kitila etc kilikuwa kinazidi kujijenga kama chama mbadala, siku hadi siku, huku input ya watu hawa ikiwa ni kubwa sana bila ya kujalisha ni nani walikuwa pale juu kwenye uongozi. Ni kama vile watu hawa wakaanza kuona kwamba mchango wao hatuuthamini au umma hauoni kwa vile tu hawapo juu kwenye uongozi wa chama. Hii sio kweli, wananchi wengi sana walitambua mchango wao. Hawakufanya utafiti kabla ya kuandaa mapinduzi yao. Laiti wangefanya utafiti, wangeona ukweli upo wapi, wangekuwa na subira, na demokrasia na haki ingefuata mkondo wake siku moja kwani chama ni watu, sio mtu mmoja mmoja.

All that said and done, chadema kimevurugwa, na wengi tumerudi tena kuanza kutafuta chama mbadala. Baadae tukasikia kwamba wavurugaji wa chadema wameanzisha chama chao. Sasa kwanini tusihoji ili tuone kama chama hiki kipya ni mbadala wetu wa kweli?

Zoezi letu halitaishia na kina Kitila tu, na kila tukisikia juhudi za watu wakijaribu kuleta chama mbadala, our scrutiny becomes of essence kwani tuna kiu kubwa sana for an alternative party. Unfortunately, in ACT, so far we see nothing but "the same alternative" in the offering. Ni kwa mantiki hii, hoja zetu zinaonekana kama vile zinalenga kushambulia watu badala ya chama. Lakini Ukweli unabakia kuwa "chama ni watu".

Mwisho, kwa wale wanaodhania tumeanza this scrutiny na ACT peke yake watembelee profile zetu, watakutana na mijadala mizuri sana na mwenyekiti wa CCK ambae ni mdau humu na aliwasilisha katiba yake ili kuomba mawazo ya wadau. Kitila anashindwa nini kufanya hivyo humu or elsewhere na badala yake anaona jambo muhimu kwa sasa ni kumteua zitto uenyekiti na kuwekeza katika kuchukua wanachama wa chama kile kile (chadema)? Hapa ana maanisha kwamba wanachadema hawapo kule kwa misingi ya sera na itikadi bali mvuto wa zitto. Ushahidi wa hili upo pale anapotanguliza jina la zitto badala ya sera na itikadi ya ACT kuvutia wanachama.
Kitila Mkumbo, wewe ni mdau humu na tunajua unatusoma. Kwa vile umekubali kwamba ccm ni chama kinachokufa, na kwa vile ni chama chenye wanachama wengi kuliko vyama vyote combined, mbadala wa kweli (ACT) ulitakiwa ulenge watu hao, sio wanachama wa chadema kwani pamoja na madhaifu yake, chadema bado ni mbadala kwa wananchi wengi. Wewe kuja na mkakati wa kuleta mbadala for both chama tawala na chama kikuu cha upinzani kwa wakati mmoja ni udhaifu mkubwa sana kimtazamo na kimkakati. Njia hii haiwezi fanikisha ujenzi wa upinzani bali itabomoa upinzani. Lakini Iwapo utafanikisha, basi mwisho wake utakuwa Ni ACT kuwa chama dola, kitu ambacho umejadili Kwamba hakifai kwa demokrasia yetu changa.






Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Tukasema kuwa yale ya Mrema hatuhitaji yatokee tena.
Nimeonyesha NCCR na TLP kama mbadala
CUF Maalim na CUF Hamad Rashid
CUF Maalim na CUF chausta
Kitila kutanguliza jina la mtu na siyo sera 'zilizomvutia' ni kurudisha kule kule kwa akina Mrema, Seif,Hamad na Mapalala

Watu hawataki scrutiny wanataka kupokea ujio tu tena ukiambatanishwa na majina makubwa.

Kuhusu mchango wa akina ZZK na Kitila, hakika subira ni jambo muhimu sana katika maisha yetu.
Hawa watu walikubalika katika siasa za chama chao na ilikuwa suala la muda tu wangeongoza. Tatizo ni subira.

Kuhusu suala la kutanguliza jina, hiyo likuwa ni 'psychology' ya kuwaambia watu yule mwenyekiti wenu mnayemtaka sasa anahamia huku, jiandaeni mje. At the same time ilikuwa kumteua katika nafasi ya ueneyekiti wa chama asichojua sera zake bila kufuata kanuni za demokrasia.

Kitila, sera za chama zinatungulia na zinabaki kuwa za chama, wanachama wanafuata na huondoka ikibidi.
Huwezi kujenga chama kwa msingi wa jina, siyo mbadala ni udhaifu.

Kugawana wanachama na CDM hakuondoi tatizo tulilo nalo la papa kuogelea katika bahari kuu kwa raha zake.
Ulipaswa kuwavuta wanachama kutoka pande zote kwa sera, na pengine ungewapata mbadala wengi wa CCM kuliko mbadala wa CDM ambao wapo wapo tu.
 
Katika hili mimi nitapenda niseme machache tu,

Kwanza ni sifu sera ya chadema Juu ya uongozi kwa vijana wake na matarajio yao,

Utaratibu wakuandaa vijana kuja kuwa viongozi ni sera thabiti na tanzu kabisa katika uga wa siasa za leo ambazo zipo kwenye kizio cha siasa za kiuchumi baada ya kutoka kwenye siasa za ukombozi na maendeleo.

Zitto ni miongoni mwa vijana wa mwanzo na angekuwa muhitimu wa mwanzo wa sera ya kuandaliwa kuwa kiongozi,

Na niseme wazi katika siasa za vijana, itachukua miongo kadhaa kuzaliwa mtu wa aina ya Zitto katika ardhi ya Tanzania,

Ujio wa Chama kiitwacho ACT binafsi ninalaaani kwa nguvu zote, sio ninalani kwakuwa chama kipya kimekuja, laa hasha, bali ninalaani kwakuwa kimekuja katika misingi ya kupambana na upinzani na sio kupambana na chama tawala ili kishike dola,

Nilishalieza hapa mazingira ya ujio wake kwa maana ya usajili wake na uongozi wake na namna kilivyo na mafungamano tata.





Yaliyotokea kwake ni sehemu ya mapito ya siasa za kiafrika na za kiswahili,

Ninaisifu na kuishukuru kamati kuu ya Chadema kwahatua madhubuti dhidi ya Zitto na wenzake.
 
Mkuu, mimi kwenye kauli ya chama kina wenyewe wanaofanya kazi usiku na mchana halafu hao hao anaowasema siyo wenye chama anageuka tena na kuwasema waanzilishi wa ACT ndiyo imenishangaza sana.

Nimemuuliza swali dogo tu kama hawa binadamu wangehamia TLP and CUF angesema wanauwa CHADEMA?.

Kama aliweza kumtuhumu kuwa Mh. Zitto alikuwa anafahamu waraka ulioandikwa na Dr. Kitila, kwa nini kwa sasa asijenge tena mazingira hayo hayo na kusema Mh. Zitto anafahamu kila jambo linaloendelea ndani ya ACT, hii ni pamoja na kuzielewa katiba na taratibu na sera za ACT.

Yaani CHADEMA inawambia haiwataki na haitaki huduma zao katika jamii halafu tena inaanza kuhofia uwepo wao katika siasa?. Mbona hii ni kali katika siasa!.

Huku ndiyo kunakosemwa, kuogopa vivuli vyao!.
 
Alinda , hapa ndipo kwenye hoja zinazozungumziwa.

Mwanzo tulisikia kunahitajika mbadala wa CCM na CDM, tulifahamu jitihada zilikuwa mbioni. Hakukuwa na tatizo.Shughuli zikaendeshwa kuanzisha chama, hilo halina tatizo. Inafahamika !

Tatizo likajitokeza pale Kitila alipokwenda katika vyombo vya habari.
Niweke sawa, hakuna tatizo la Kitila kutangaza kujiunga na chama cha ACT.

Lakini basi yeye akiwa amejificha na tukijua anafanya hivyo, hakupaswa kwenda mbali zaidi na kutufanya mazuzu.

Kumshawishi Zitto hakuhitaji tangazo kwasababu ''wanashea maono sawa'

Tangazo limewekwa makusudi kabisa ili
1. Kumwezesha Zitto kutoka mahakamani kwa kisingizio cha kushawishiwa tukijua wazi alikwenda ili aende kwenye BMLK (Hapa wawili wanaficha 'uwazi' na wanacheza na karata dah! siitaji.

2. Kuwatangazia wafuasi wa Zitto mwito wa kujiunga na ACT bila kuwa muwazi kama ulivyosema. Hakuna tatizo pia kama Zitto ana watu wake, lakini hilo halikufanywa kwa njia za uwazi na ukweli.

Tukizangatia andiko lake la kifo cha CCM na CDM kuwa mbadala hivyo kunahitajika mbadala zaidi hakuna shaka lengo lake si kupambana na CCM.

3. Kitila hakutangaza sera za chama hicho anachomshauri mwenzake ahamie.
ZZK hajui hata sera au katiba lakini anashawishiwa ajiunge na chama.
Lakini basi, Kitila japo angeanza na kusema anamshauri zzk aondoe kesi ili kujiunga na ACT japo watu wangeelewa elewa hivyo hivyo! la hasha

4. Kubwa lao ni kumtangaza ZZK katika nafasi ya uenyekiti hata kabla ya chama hakijapata katiba. Hii ndio lowest point ya Kitila na inaondoa doubt yoyote iliyokuwepo.

Alinda, hakuna uwazi walioulilia siku nyingi kupitia waraka, kinachofanyika ni kutaka kugeuza wananchi kama mazuzu.

Tunasema , hapana, Kitila tanganza sera, vuta watu kwa hoja, maono na mipango.
Cheap politics kwa dunia ya sasa na nafasi yako katika jamii hazifai.

Huu si mwanzo mzuri na kitendo cha kufakamia matapishi si dalili njema kwa ustawi wa demokrasia na maendeleo ya nchi hii.

Kitila na ZZK ni raia wema wa nchi hii na wana haki zote, lakini wasitumie elimu au siasa za kizamani kutaka kupotosha umma kana kwamba hatujui, ni mazuzu.

Tangazeni sera, omyesheni uwazi, kila la heri. Wakivuka mstari tutawaambia bila haya.
Siasa za unafiki kwa nusu karne zimetufikisha hapa, bado tu tuendelee kumeza!

 
Last edited by a moderator:
Kifupi ni hivi, ZZK amepitia majaribio mengi sana na siku zote hakuaminiwa iwe na chama au watu binafsio. Kibaya ni kwamba watu hawataki kusikia Ukweli, hivyo ZZK aseme lolote lile hataaminika. Na kama akifuata hayo uloyasema ndio atachukiwa mara 10 maana hataaminika kwanza na kisha atatungiwa hadith mpya! Usaliti wa ZZK unaoekana tu kwa sababu tunaamini ya mwanzo pasipo ushahidi ila kauli ya watu kama Tundu Lissu anajisikia mno na kuutaka Umaarufu kuliko watu wote Chadema.

Kama nakumbuka vizuri Hata Chadema kuna wakati iliandaa nafasi za uongozi kwa watu fulani kutoka CCM ambao wao wenyewe Chadema waliwafuata japo yawezekana leo viongozi wa Chadema wanaweza kukataa. Ni mikakati ya Chama na siwezi kusema hayo yalitokea kwa sababu ya Ukaribu baina ya Mbowe na watu hao ama Dr.Slaa na watu hao. Wapo walosimama hadharani na kukana na wapo walosimama na kukubali baada ya kujiunga na Chadema lakini bado ukweli utasimama ya kwamba UMAARUFU wa mtu ni silaha ya vyama vingi nchini ktk kukijenga na kila chama kinafanya mchezo huo. Haitakiwi kuwa hivyo, lakini ndivyo Tulivyo!

Swala la ZZK, Kwanza hayo maswali uloyaorodhesha tayari yanaelemea upande wa KUTOAMINI lolote kama ilivyokuwa ktk swala la Waraka. Napiokusoma tayari nakuona unaamini nini na ndio maana unaona Undumia kuwili wa Zitto lakini usiuone wa wabunge wa CCM wanaotetea pia maslahi ya wananchi. Yawezekana ZZK alishafuatwa na kina Kitila lakini kwa nini atangaze? hivi kweli itakuwa akili kwa mwanasiasa ambaye anasubiri hukumu kudai kwamba amefuatwa na waasisi wa ACT ili kujiunga na chama hicho? Ili iweje na atapendwa kweli ndani ya chama chake maana siasa sio Mpira!

Je, unajua ni mara ngapi Mbowe kafuatwa na vyama vingine? unajua ni mara ngapi Dr.Slaa kafuatwa sasa ukishajua kwamba hawa viongozi hawakuwahi kutangaza habari hizo utawahukumu vipi? Ama niseme unajua ni viongozi gani wa nje, Chadema imewahi kuwafuata wajiunge hao nao ni wasaliti wa vyama vyao? Hivi kweli Dr.Slaa aliisaliti CCM alipohamia CDM ama ilikuwa haki yake!

Hata kama ingelikuwa mimi ndiye ZZK na ktk nafasi aliyopo na nikafuatwa na Kitila ama iwe nahusika na mpango wa kuanzishwa kwa ACT sina sababu ya kumuomba mtu yeyote ruksa ikiwa hawa watu wanadai hawanitaki ni swala la muda tu, hawakuniamini pindi niliposema Ukweli wangu na wanahaha sasa kusikia vijimambo! ZZK kaapa kwa miungu wote anaowafahamu kuhusu waraka, kuhusu kuhusika na waraka ama mpango wa kukisaliti chama lakini hakuaminiwa ila wameaminiwa wale walosoma tu waraka japo sii mashahidi, ama watunzi wa waraka huo.

ZZK ni sawa na mfungwa alohukumiwa Kifo kwa kosa la jinai ambalo halina Ushahidi isipokuwa sura na mienendo yake imehukumiwa. Sasa huyu mfungwa akifanya mpango wa kutoroka Jela, kweli yeye atakuwa msaliti wa sheria kandamizi asubiri uamuzi wa viongozi wasiomtaka. Sii hawa hawa walituaminisha kuwa Kiongozi Sitta amefuatwa na viongozi wa Chadema kumtaka ajiunge ili kuongeza nguvu ya chama hasa baada ya kuenguliwa kiti cha U spika na akadai hatafanya hivyo hadi apewe Nafasi ya kugombea Urais!. Kuna habari millioni tulozisikia humu JF kuhusu vioongozi mbali mbali lakini hili la ZZK limewashinda kumeza, kutokana na Umaarufu wake unawasumbua watu. Mimi sielewi kwa nini ZZK akiwa maarufu inawasumba watu na sielewi zaidi kwa nini watu wanachukia ZZK kuwa na marafiki wakati Mbowe pia ana marafiki tena wanafiki ndio wengi zaidi. Sisi wa Mujini tunawajua hawa watu wachumia tumbo dada.

Wapo watu wana akili ya Kitumwa zinazowaweka duniani, kazi yao kila siku ni kujipendekeza kwa mwenye nacho waonekane wao waaminifu na wema sana kumbe wanafiki tu upande wa pili, kazi yao kutwa kumpa sifa kiongozi juu ya umahiri wake, Uzuri wake, umakini wake, busara zake, uongozi wake na wengine hadi kuwa makuhadi wake ili mradi tu hawa watu wapate kula ya siku. Usidanganywe na hizi habari za mtaani dada wenye mitaa hiyo tupo! Leo hii hakuna Uzalendo wa Chama ndani ya Chadema ila kuna Uzalendo wa viongozi na nidhamu ya woga kama ilivyo CCM. Kama wewe sii kambi ya Lowassa utakuwa na wakati mgumu sana kupeta kisiasa. Madongo anayopigwa kina Membe, Makamba, Mwandosya, Salim, Warioba yote yana malengo nje kabisa ya uzalendo!

Zilikuwepo habari za Lowassa, kina Mpendazoe na wengine wengi ambao walikuja kuunda chama cha CCJ. Walimsema hadi Mzee Mwanakijiji kuwa mmoja wa waasisi wa chama hicho lakini hata siku moja hukunisikia mimi nikiwahukumu watu hao kwa habari za mitaani na wala sii hoja maana kila Mtu ana haki yake ya URAIA. Pamoja na Yote hayo uliwasikia CCM wakiyabebea bango? sidhani walifanya subira, wakaheshimu haki za hao watu kujiunga nna chama chochote wakiopendacho na baadaye ukweli ukajitokeza nani mwenzao na nani msaliti.

Jamani tuache habari za mipasho na zile hadith za kwamba Muislaam akiingia kanisani basi kesha fanya shiriki ni lazima asilimu upya na wala ZZK sio mbwa kaingia msikitini bali binadamu anayetakiwa kuheshimiwa kwa haki zake za Kiraia kuchagua chama ama kujiunga na chama chochote aklipendacho na kwa wakati wake. Dini ni swala la Kiimani ya roho na sii jengo, rosali wala joho. Viongozi wetu wengi wanavaa majoho na mikufu mizito kifuani lakin ndani kutupu - wasikudanganye!!

Tazama pia tofauti baina ya wapenzi wa Chadema na CCM, ilipotokea fununu za Mh.Sitta na hata Sumaye hakuna mtu aloibebea mbeleko, kama upepo ilikuja na ikapita, leo Mh.Sitta bado yuko CCM aliaminika na anaaminika wala CCM hawakuibebea njuga kwa sababu wao kama Chama wana sheria, kanuni na utaratibu wao na sii kufuata habari za magazetini ama watunzi wa hekaya wa JF. Kitu gani kimejitokeza ktk dunnia ya leo hii na kimefanya watu tuaminishwa dhambi kuwa sii haramu bali choice ya Mtu. Tazama leo ukiupinga sana utawala dhalimu wa Kibepari utaitwa Terrorist. Ukweli nikwamba UONGO unaaminika zaidi kuliko UKWELI na ukitaka kujua Uongo ni upi na nukweli ni upi fuata manenmo yangu. UONGO hauna mwisho, ila UKWELI huwa na MWISHO. Uongo siku zote lazima uendelee kutungiwa uongo tofauti na Ukweli ambao uksha toka hakuna cha kuongeza!

Ukipingana ana mfumo wao (kiuchukmi) utafungiwa wewe milango yote kama Zimbabwe, Cuba na Korea Kaskazini na hata marafiki wako watapigwa chapa usoni wasionekane karibbu yako ili mradi wewe uonekane umeshindwa kiuchumi na kila siku picha za maisha magumu ya wananchi wako zitawekwa ukurasa wa mbele. Hizo sheria, kanuni na taratibu zao ktk kulinda maslahi ya makampuni makubwa ambayo hayakuipewa nafasi ya kupenyeza ktk nchi hizo.

Kifupi Ukiona rais yeyote anasifiwa sana na nchi za magharibi, basi jua ya kwamba huyo rais ndiye Mbwiga kuliko wote ktk kulinda maslahi tya nchi yake. Na ukisikia hapendwi jua ya kwamba huyu anajjali zaidi maslahi ya nchi yake maana NCJHI ni kwa Mapana ya RASILIMALI zake.i
 
Ni wewe unayehimiza tusijadili Watu lakini hoja zako zote hapo juu zinabebwa na Watu.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu Mkandara:

Nini kilikuvutia na kuwa mfuasi au mfuatiliaji wa karibu wa siasa Za chadema?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ni wewe unayehimiza tusijadili Watu lakini hoja zako zote hapo juu zinabebwa na Watu.



Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu mimi nawazungumzia watu kwa sababu ndio mada yenyewe mloiweka na kuwataja kwa majina yao na sii kinyuma. Nna hata hao wengine nilowataja nimefanya hivyo ili kutoa Mifano na reaction zenu juu ya swala kama hilo na sii vinginevyo. Unaponiona mimi namzungumzia mtu fulani basi ujumbe wangu unakwenda direct kwake iwe ni swali ama ushauri na sii kuanzisha taarabu!

Swali lako la Pili, nilivutiwa na Chadema kutokana na imani kwamba Chadema imejipanga vema kufanya mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi wakichukua dhamana ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI na sii Mabwanyeye. Nilijiunga na Chadema kwa sababu niliamini kuwa UFISADI ndio adui mkubwa wa maendeleo ya Mtanzania na Chadema walichukua fursa hiyo kuupiga vita. Nilikuwa na bahati kuwa karibu na baadhi ya viongozi wake kupitia jukwaa hili la JF, nikawasikia kauli zao, nikasikia malengo yao na kikubwa zaidi walikuwa haribu sana na wananchi wakikubali kuipokea mawazo ya wananchi na hata kukosolewa hapa hapa JF.

Nina mashaka sana kama isingekuwa kijiwe hiki cha JF, mahala nilipoweza kuwasoma hawa viongozi na kuwahoji wakati wanatangaza sera za chama, hakika isingekuwa rahisi mimi kujiunga na chama hiki. Lakini baada tu ya chama kupata Umaarufu, kenge nao wakajiunga ktk kundi la Mamba wakiitwa Wapiganaji.Vingozi wenyewe hawakuwa na shida tena na jukwaa hili kwa sababu maskini akipata makalio hulia bwataaa! ndio kafika. Huu ndio mwanzo wa ukweli kujitokeza kama hivi leo unawaona?. Kupitia haya nikawaasa sana viongozi na hata wanachama wa CDM humu humu JF bila kujua kwamba WATU wengi ktk siasa hutafuta UMAARUFU kama hatua ya kwanza, umaarufu ambao utazijenga CV kisiasa ambayo kwao ni Ajira! Leo hii wako wapi?

Mtu yeyote anayejiunga siasa kwa sababu ya ajira, akaomba saana kura zenu ktk majanvi mbalimbali, akajieleza kwa maneno meengi matamu na kufokea sana mabaya mwogope! maana akisha ingia ndani basi ndiye wa kwanza kulilia posho mishahara, Uheshimiwa na kuwaweka ndugu na wake zao ktk nafasi za uongozi. Ukisha ona vile basi jua chama kimeshaingiliwa na walokuwa na moyo haswa wa kukijenga chama na wazalendo wataonekana wachawi kwani nguvu ya pesa siku zote hu control media! Usikubali kuamini yanayoandikwa ktk magazeti na Blogspot maana hii ni biashara na pesa ndio huzungumza kwanza.

Mkuu miomi bado sijakata tamaa na nina hakika kama ningekuwa Kiogozi basi ningewekwa ktk kundi nla ZZK maana ndivyo Tulivyo lakini ukweli naujua mwenyewe. Sikubali kudanganywa na Ngongoto hawa, kama Mbayuwayu nitachanganya na za kwangu!
 

Swadakta Ndugu Mkandara, maneno yako haya ni Mujarrabu kabisa katika mada hii.

Chadema ya 2008 ni tofauti kabisa na Chadema ya 2014, Chadema ya sasa inaendeshwa kwa hoja nyepesi nyepesi, viongozi wasio na nidhamu ya utendaji, wenye ujuaji mwingi (Lissu et al), wenye kusigina katiba ya chama bila hofu yoyote, majungu na wivu wa kisiasa , imekuwa chadema ya watu wasio na uwezo wa kuibua hoja nzito za Kitaifa, chama kisichojali haki za wanachama wake na hivyo kufanya timuatimua isiyo na kichwa wala miguu!

Kiufupi Chadema must reform, ni lazima kirudishe imani kwa wananchi, la sivyo kitajifia kifo cha mende!
 
Haya mh tumekusikia na tunashukuru kwa maoni yako.

Tunaomab turudi kwenye mada, hapa hatuongelei umaarufu wa CCM au udhaifu wa CDM

Tunaongelea ACT/Kitila na uteuzi wa Mwenyekiti Zitto
 
Dr Kitila Mkumbo , ningeshauri ufuate nyao za Nyakarungu. Yeye kasema wazi kama chama cha 'uwazi' kilivyo. Nyakarungu hakuficha hisia na fikra zake. Kaweka wazi kabisa lazima wapambane na wapinzani wenzao. kumbuka, hayo si maneno ya duru za siasa, ni maneno ya mwanachama mwandamizi.

Nyakarungu kaiba kauli ya sera tofauti na ya Dr aliyeamua kukimbilia uteuzi wa mwenyekiti.
Hakuna shaka Nyakarungu anajibu hoja ingawa amekimbia kujumika nasi.

Dr Kitila, Political science na public relation ni muhimu kwa sasa kuliko uteuzi wa mwenyekiti.
Nyakarungu analeta damage uliyoanzisha akijua anafanya damage control wakati akifanya damage zaidi




cc Ng'wamapalala Mkandara JingalaFalsafa Mchambuzi
 
Mkuu, Nguruvi3

Huyo Nyakarungu ndiyo nani?.

Mwanachama Mwandamizi ndiyo nini?.

ACT ina verified name hapa JF na kupitia Verified name ndiyo tunaweza kujadili content zake kwa sababu haya aliyoleta ni mawazo yake binafsi kama yalivyo mawazo yako.
 
Last edited by a moderator:

Nyakarungu ni msemaji wa ACT?, ana wadhifa gani ndani ya ACT?. Mleta mada,hata kama ni propaganda "haribifu" dhidi ya hiki chama kipya, mbona zinakosa mashiko?.

Kupambana na ACT kwa hoja hiyo ni O.K, lakini kuichafua ACT ukitegemea kuinusuru CHADEMA au chama chochote wala hakusaidii, infact wala hakuwasaidii Watanzania katika kupanua wigo wa demokrasia!
Waswahili walisema Chema chajiuza, Kibaya chajitembeza!. CHADEMA walitake for granted imani ya wananchi wapenda mabadiriko, matokeo yake wakajiona the "untouchable invinsibles", sasa inaonekana wananchi wamepata mmbadala, tusiwakatishe tamaa kwa technique za "fear mongering"!
 

Hapo kwenye nguzo ya TANO, hoja ya Nguruvi3 ipo bayana.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Yoote uloandika ni jinsi wewe unavyofikiria ni kutuweka sawa kisaikologia ukitumia dhana, bao au ramli. Ulichoacha hapa kusema ni Mimi Nguruvi3 nadhani huyu Kitila ana nia kadhaa wa kadhaa na unadhani ZZK ni mhusika maana hakuna ushahidi wowote ktk maelezo yako. Na hakuna mtu anayekataa dhana inayoelekea ukweli, lakini kwa vile mnatumia nguvu kubwa sana kuelezea jambo hili inasimama katika uONGO.

Katika elimu ya saikologia hiyo hiyo unayotumia hapa husema kwamba - UONGO SIKU ZOTE HAUNA MWISHO lakini UKWELI UNA MWISHO.
Yaani anayesema uongo ataendelea kuongopa maana hakluna ukweli na ili aonyeshe ni kweli itabidi azidi kuongopa lakini enye ukweli jambo huisha palepale.Hii habari ya Kitila na Zitto imekuwepo kwa muda mrefu sana na kila siku inatungiwa hadith ni ktk kuashiria kuna UONGO zaidi ya Ukweli maanake kama yangekuwa na ukweli basi haya maswala yangekwisha siku nyingi. Na kibaya zaidi hadith hii inafanana sana na sinema ya waraka kaiasi kwamba inaonyesha mtunzi wa tamthiria hii ni yule yule - wetu James Hadley Chase!

Hivyo maadam uongo huu unaendelea kutungiwa UONGO.ili ubakie kuwa kama ukweli inanilazimu kutowaamini kwa lolote m,naloandika. Nisichofahamu ni dhamira yenu maana sii ZZK wala Kitila watakao athirika, hawa wnaa maisha yao na wataendelea kuishi kamawalivyokuwa Chadema lakini mimi mlalahoi hii mistari mnayoendelea kuitunga kama nyimbo za Diamond ndio inanipa wasiwasi kama mnayo nia nzuri na hawa watu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…