Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Toka zamani Zitto anatunia hizi data lakini ajabu sasa anazitumia na ACT - Wazalendo anaonekana msaliti msome kiduchu hapa chini.Alinda, tumeshawishiwa kuwa data za Mchambuzi hazifai. Tukaomba halisi kwa mujibu wao
Wameleta za HDI, Mchambuzi kazifinyanga finanyanga hakuna jibu.
Mkandara anasema Zitto alisoma tu katika mkutano, asilaumiwe
Zitto.
Hali ya Taifa hili ni mbaya sana. Na tusipoangalia, Taifa hili tutalipeleka shimoni kabisa. Tangu mwaka 2007, Asilimia 38% ya watanzania wamedumaa akili kutokana na lishe duni. Maana yake nini? Maana yake katika kila watanzania 100, watanzania 38 wamedumaa akili, hawafikiri vizuri kutokana na lishe duni. Lishe duni ni indicator ya ufukara. Kama madiwani wa CCM ni watanzania wa kawaida, basi katika kila madiwani 10, madiwani 4 wamedumaa akili. Au katika kila wabunge 10( wa CCM lakini), wabunge 4 wamedumaa akili kama wanatoka familia za kawaida. Hivyo hivyo kwa mawaziri wa serikali ya CCM, kwamba inawezekana katika kila mawaziri 10, mawaziri 4 wamedumaa akili. Pengine ndio sababu wamekuwa wanasaini mikataba mibovu ya kifisadi.Kwahiyo tarehe 24, Mei, Ukichagua CCM, maana yake ni kwamba unaunga mkono mwenendo wa serikali ya CCM kusababisha watanzania 4, katika kila watanzania 10 wawe waendelee kudumaa akili. Na ukimpigia kura Magessa wa CHADEMA, maana yake ni kwamba, unapinga , unakasirishwa na mwenendo huu. Jamani taarifa hizi hatuzitungi sisi! Wala hatuziandai sisi. Ni taarifa za serikali. Ukisoma taarifa ya serikali ya Hali ya Umasikini na Maendeleo nchini (Pverty & Human Development 2007).
Nadhani umeishaelewa wapi Zitto anapozipata hizo data lakini najua haiwezi kukubali utaendelea kurusha ngumi hewani mpaka mwisho.
Last edited by a moderator: