Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Alinda, tumeshawishiwa kuwa data za Mchambuzi hazifai. Tukaomba halisi kwa mujibu wao

Wameleta za HDI, Mchambuzi kazifinyanga finanyanga hakuna jibu.

Mkandara anasema Zitto alisoma tu katika mkutano, asilaumiwe
Toka zamani Zitto anatunia hizi data lakini ajabu sasa anazitumia na ACT - Wazalendo anaonekana msaliti msome kiduchu hapa chini.

Zitto.

Hali ya Taifa hili ni mbaya sana. Na tusipoangalia, Taifa hili tutalipeleka shimoni kabisa. Tangu mwaka 2007, Asilimia 38% ya watanzania wamedumaa akili kutokana na lishe duni. Maana yake nini? Maana yake katika kila watanzania 100, watanzania 38 wamedumaa akili, hawafikiri vizuri kutokana na lishe duni. Lishe duni ni ‘indicator’ ya ufukara. Kama madiwani wa CCM ni watanzania wa kawaida, basi katika kila madiwani 10, madiwani 4 wamedumaa akili. Au katika kila wabunge 10( wa CCM lakini), wabunge 4 wamedumaa akili kama wanatoka familia za kawaida. Hivyo hivyo kwa mawaziri wa serikali ya CCM, kwamba inawezekana katika kila mawaziri 10, mawaziri 4 wamedumaa akili. Pengine ndio sababu wamekuwa wanasaini mikataba mibovu ya kifisadi.Kwahiyo tarehe 24, Mei, Ukichagua CCM, maana yake ni kwamba unaunga mkono mwenendo wa serikali ya CCM kusababisha watanzania 4, katika kila watanzania 10 wawe waendelee kudumaa akili. Na ukimpigia kura Magessa wa CHADEMA, maana yake ni kwamba, unapinga , unakasirishwa na mwenendo huu. Jamani taarifa hizi hatuzitungi sisi! Wala hatuziandai sisi. Ni taarifa za serikali. Ukisoma taarifa ya serikali ya Hali ya Umasikini na Maendeleo nchini (Pverty & Human Development 2007).

Nadhani umeishaelewa wapi Zitto anapozipata hizo data lakini najua haiwezi kukubali utaendelea kurusha ngumi hewani mpaka mwisho.
 
Last edited by a moderator:
Zitto hajui uchumi basi, Ni mbabaishaji mbali Ya kuwa mlaghai na mbaguzi. Tukijikita Katika ukweli unaojitokeza kwamba Zitto hajui uchumi, je:

Matatizo yetu Ni volume of output (GDP) contribution Ya sekta Ya Madini au mapato Ya Kodi katika sekta Ya Madini? Tanzania sasa Ni top three in terms of output Ya mining sector in Africa. Tanzania sasa inavutia wawekezaji wakubwa kutoka kila pande ya dunia Kuja kuwekeza Kwenye mining sector, lakini kwa kauli yako japo juu hence Ya supreme zitto, hilo Ni tatizo. Nini kigumu kujua kwamba Kilio Chetu Ni low revenues and not large output Ya sekta Ya Madini?

Kwa kweli mnasikitisha sana na mchumi wenu uchwara Zitto Kabwe.
Inawezekana kweli Zitto hajui uchumi lakini hizi takwimu siyo zake msome hapa chini.

Zitto
Takwimu zote ninazoweka hapa zinatoka katika Tanzania Human Development Report 2014. Taarifa imesheheni kwa kweli.

Sasa wewe Mchambuzi mchumi mzuri uliobobea ni kupambana na Tanzania Human Development Report 2014.
 
Last edited by a moderator:
Barubaru

Na mimi naomba nikupe pole, maana na wewe ni hodari wa kutanguliza pole kabla ya kutoa hoja.

Kama ungekuwa mchumi mahiri kama unavyotuambia hapa, ungekuwa unafahamu kwamba DSM ni major "commercial capital" nchini Tanzania, na moja ya the largest commmercial capitals in East and Central Africa. Hata mwanafunzi wa "commerce" wa kidato cha kwanza anaelewa implication ya suala hili kiuchumi ni nini. Ebu tuangalie definition rahisi tu inayokuja 'google'. Inasema hivi:

"Commerce is the activity of buying and selling, especially on a large scale. The system includes legal, economic, political, social, cultural and technological systems that are in operation in any country or internationally."

Nikuulize, je:

1. Hadi hapo hauoni kwamba just from the definition, DSM lazima iongoze in terms of GDP and Tax revenues?
2. Hata bila ya hiyo definition, whats so hard for you to come into agreement kwamba majority of activities nchini - industrial, services (financial, telecommunications, real estate etc), zipo DSM kuliko sehemu nyingine yoyote nchini?
3. Whats so hard to understand kwamba large tax payers in Tanzania, their economic activities are based in DSM kuliko sehemu yoyote ile?

Look at these facts:

*About 40% of Large tax payers wapo DSM, huku Arusha ikiwa na 2.5%, Mwanza 1.2%, na kwa Zitto Kigoma 0.1%.
*Large tax payers contribute about 40% of total revenues collected by TRA countrywide.
*Large tax payers contribute about 70 % of total domestic revenues in Tanzania (TRA and Non TRA based revenues).

Hadi hapa hauoni kwamba wewe, zitto na wafuasi wengine ni wababaishaji tu?

Mchambuzi,

Nashukuru sana kwa ufafanuzi wako ambao kwa upeo wako katika nyanja hii naona umekomea hapo.

Sasa mimi nilitaka kukupa zaidi na zaidi ujue kuhusu Dar. Kiuchumi tunapopata DATA hizo za Makusanyo ya KODi kama mlivyoziainisha. Suala la kwanza tunajiuliza Kwanini Dar imekuwa ya Kwanza katika makusanyo?. Hapo hatuangalii kama ni major Commecial capital au ni mji wa kawaida tu. Kwani ukiendelea zaidi utajiuliza kwanini Dar iwe major Commercial Capital na isiwe Mtwara au Mwanza?

Sasa kwa kukusaidia Zaidi , Nakubaliana kabisa na wewe Dar ni mji maarufu wa Kibiashara lakin ili mji uwe na swifa hiyo ni laazima kuwe na viashiria. Sasa kwa upande wa Dar kupata Swifa hiyo inatokana na mambo haya hapo chini.
1. Uwepo wa Bandari.
2. Kuwepo na Umeme wa Uhakika (Ingawa umeme huo unatokea morogoro (Kidatu)) na maji yanayotokea Ruvu Pwani
3. Kuwepo na International Airport.
4. Kuna miundombinu mizuri ya Barabara (japo kwa sasa kuna foleni kubwa sana ambazo kiuchumi tunasema zinaponguza pato la taifa lenu)
5. Kuna miundombinu mizuri ya majengo japo haipo katika mipangilia mizuri ya town planning.

Mchambuzi kama utaangalia zaidi na kwenda mbali zaidi kuangalia katika Dar ni eneo gani linalokusanya zaidi basi utaona makusanyo makubwa ya Dar yanatoka bandarini iwe kwa kupokea au kusafirisha mizigo. Uwepo wa viwanda na wafanyabiashara wakubwa hapo Dar umesababishwa na viashiria nilivyovitaja hapo juu. Ukaribu kutoka bandarini na nishati ya umeme ya uhakika na miundombinu.

Nilivyo vianisha hapo juu ndivyo vinavyoifanya Dar iwe Ni old Commercial capital na mapato yake japo yanaongoza kwa Tz lakin yanazidi kushuka kutokana na poor town planning ambazo zinasababisha foleni nyingi.
Na hayo makusanyo unayoona makubwa yanatokana na bandari yenyewe , viwanda na sehemu ndogo sana wafanyabiashara.

SASA nikiitazama Mtwara.

Huu ni mji ambao bado haujajengeka na Serikali yenu kama itakuwa makini wanaweza kufanya mengi hapo kwa gharama nafuu ikiwa pamoja na kuwa na proper planning kwani kuna viashiria vyote vya kuweza kuufanya mkoa huu upande kiuchumi kuliko ilivyo dar.
1. Upo location nzuri yenye kuvutia sana

2. Kuna Bandari nzuri kubwa yenye kina kirefu
3. Kuna Umeme wa uhakika wa Gas unaotoka Mtwara hapo hapo.
4. Ardhwi nzuri yenye rutba na inayofaa kwa kilimo.

Hivi juu ndivyo vinavyovutia wafanyabiashar/ wawekezajia kuja kuwekeza katika sekta ya viwanda vikubwa na kilimo na hili ndilo eneo lenye makusanyo makubwa sana sio tu Tz bali nchi yoyote yenye bandari.

Kinachohotajika kwa mtwara ni
1. Good town planning inayoweza kutenganisha maeneo ya viwanda, maafisi ya utawala kwa maana Serikali, maeneo ya Maghala na maeneo ya makazi. Kifupi kitaalamu tunasema wanatakiwa wawe na setellite cities katika makaazi kama walivyofanya Kampala Uganda.

2. Kuweka Internatinal Airport.

3. Miundombinu ya barabara na Reli mizuri ili kuwezesha mizigo ya Msumbiji, Zambia, Malawi na DRC Congo. ikiwemo mizigo local ya mikoa ya mbeya, songea, iringa, rukwa, lindi na pwani kupitia hapo.

Hapo viwanda vingi vitakwenda huko na vile vile wafanyabiashara wengi watakimbilia huko na kuiacha Dar sababu kubwa Dar kuna uchelewashaji unaofanya na mamlaka za Serikali kama TRA, Bandari wenyewe LAKIN KUBWA FOLENI WAKATI WA USAFIRISHAJI.

Na hivyo hivyo upande wa Tanga kama itaimarishwa Bandari yao mizigo kama ya Uganda, Burundi na hata Rwanda itapitia huko na kupunguza mzigo kwa Dar.

sasa ndio nikakwambia MTWARA kama mtaacha siasa zenu hizo na kujikita kwenye maamuzi sahihi ya kufufua uchumi wenu na kuimarisha mapato yenu ya ndani basi ndani ya miaka 5 MTWARA ina nafasi kubwa sana ya kukusanya zaidi kuliko Dar.

Kifupi hakuna mji unazaliwa au kutokea kuwa Commercial Capital bila kuwa na viashiria na vivutio vinavyowekwa na mamlaka yenye dhamana.

nakumbuka wakt nipo wizara ya fedhwa huko Tgk katika mmoja wa mikutano yetu wakti wa vugu vugu la kuhamishia makao makuu Dodoma niliwahi kusema kuwa hilo haliwezekani kwa sababu ya geographia yake na na hakuna viashiria na hata ukiweka vivutio basi mtatumia gharama kubwa sana na kwa wakti ule nchi ya Tz haikuwa na fedhwa hizo. Jiulize je makao makuu Dodoma yamekuwa? je unajuwa kwanini haiwezekani?

Mchambuzi, Uchumi ni somo pana sana linalotaka ujikite kwenye kujenga hoja na kusasambua kiumakini sana kwani wachumi Dunia nzima tunaamini hakiwezi kuwa kitu bila kuundwa na kusimamiwa kiumakini.

Nilicho kupa ni kiduchu lakin kama utataka darsa zaidi basi Bismillah.

Pole sana ahali yangu.

Je wanaolima, kodi zao (kutoka sekta ya kilimo) zinachangia kiasi gani katika total tax revenues za nchi? Kilimo hivi sasa accounts for less than 30% of GDP, unataka kutuaminisha nini hapa.

Kama wewe kweli ungekuwa ni mchumi mahiri, ulitakiwa uone ni jambo jema sana kwa uchumi wa nchi kupunguza kutegemea sekta ya kilimo in terms of output and revenues na badala yake kuhamia sekta nyingine kwani hayo ndio maendeleo, na ndio msingi wa kutengeneza mapinduzi ya viwanda.

Bandari (kwa maana ya Tanzania Ports Authority) ni miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini aka Large Tax Payers kwa mujibu wa TRA. Lakini mchango wa mapato ya TPA katika hawa large tax payers sio zaidi ya 15%. Kwahiyo ni kweli bandari ina makusanyo makubwa lakini sio kweli kwamba TPA (directly) ndio inayoifanya DSM kuwa kinara katika mapato ya Kodi.

Ni viwanda vipi vilivyopo DSM ambavyo vinategemea bandari ya DSM kuuza bidhaa nje?

Pamoja na hayo yote, kwanini TPA badi iwe na mchango usiozidi 15% katika total ya large tax payers?

Mchambuzi,

Nafikiri nimekujibu mengi sana katika bandiko langu la juu.

Lakin kwa kukusaidia zaidi kuwa Dar bila bandari ungekuwa mji duuni sana kwani hakuna vyanzo vyake kama mkoa vya umeme, hakuna vyanzo vya maji, Hata Reli ya kati na ile ya Tazara isingejengwa kwani zimejengwa ili ziweze kusafirisha mazao kutoka bara kwenda ughaibuni na hata kulete vipuri na mitambo kutoka ughaibuni kuingia dar.

Hata hayo makampuni ya mawasiliano na mengine yasingekuwepo bila kuwepo na viashiria vizuri vya uwekezaji na location nzuri ya Dar yenye kubebwa na uwepo wa bandari.

Hebu fikiria bila bandari ile Port Access Road (siku hizi mandela Road) ingesheheni malori pale.

Jaribu kutofautisha TPA na TRA kwani hizi ni taasisi tofauti kabisa. Mimi ninachobainisha ni makusanyo ya TRA bandarini na sio malipo ya TPA kama kodi kwa TRA.

Kumbuka kuwa kuna malipo ya Transit goods hapo bandarini ambapo TRA wanakusanya na vile vile kuna mizigo inayoishia Tz ambapo vile vile TRA anakusanya kodi yake. Vile vile kuna malori ya kubebea mizigo, containers na hata mizani za kupimia mizigo etc.

Ndio maana nakususutiza kuwa uchumi ni sehemu pana sana unahitaji kufikiri zaidi na kuwa mbunifu ili uone mchango wa bandari.

Narudia tena tofautisha makusanyo ya TRA kwa bidhwaa zinazopita bandarini na malipo ya TPA kama kodi kwa TRA.

Kama utahitaji darsa zaidi kwa hapo basi Bismillah.

Pole sana.

Shukran sana Dr Barubaru ili darsa lako hata yule mtu mwenye elimu ya chini kabisa anakuelewa.

Ahsanta.
 
Last edited by a moderator:
Shukran sana Dr Barubaru ili darsa lako hata yule mtu mwenye elimu ya chini kabisa anakuelewa.

Ahsanta.

Ahsantum yaa akhuy Ritz.

Nimekuja jana nipo Tz nitakuwepo kwa wiki nzima Insh'Allah na insh'Allah ijumaa nitaipata mitaa ya nyumbani Upanga masjid Maamur upanga mtaa wa malik.

Ahali yangu nawapa pole sana kwa hadhwa ya foleni. Jana nilipofika mchana kutoka airport mpaka kwangu mtaa wa Mfaume Upanga tulitumia masaa zaidi ya matatu. Hakika hii ni muswiba mkubwa kwa uchumi wa nchi na utendaji kazi wa wakusanya kodi na walipa kodi.

Mahandaki kila barabara niliyopita na ubabaishaji au uvunjifu wa sharia za barabarani ni jambo la kawaida sana na limezoeleka. Traffic wote wamekuwa wakusanya kodi kwani wana vitabu vya invoice na wanasimamia hilo badala ya kuilimisha na kuonya madereva wao wamesimamia kutoza faini.

Kweli Tz kazi ipo. Nitakutafuta jioni tupate barza kidogo na kahwa.

Ijumaa njema

Hayo ni matunda ya Serikali sikivu ya ccm anayoishabikia huyo Ndugu yako katika imani.
 
Hayo ni matunda ya Serikali sikivu ya ccm anayoishabikia huyo Ndugu katika imani.

Matola.

Mie kama mchumi sijapatapo kuona SERA au mikakati ya chama chochote cha siasa kilichosajiliwa Tz chenye kuweelezea mikakati yake na Dira yake kuinua uchumi wa Tanzania. Zaidi ya kuandika mambo kisiasa ambayo hayawezi kutekelezeka.

Sasa nakuomba niwekee SERA ya chama chochote hapa barzani na mkakati wake kutatua kadhwia hizi ili tuzijadili kwa kina.

Ahsantum na ijumaa njema

Nikisoma hoja za Mchambuzi , Barubaru , nguvuri3 , Mkandara hoja #433 , #439 na #440 Zakumi na wengineo wote mnakubaliana kuwa maendeleo hayapimwi kwa GPD tu bali kwa kuangalia zaidi Tax Revenues, Historia ya eneo fulani, mwamko, idadi ya mashule, idadi ya watu, hosp na nk. na katika uchambuzi yakinifu wa mchambuzi amesema kuwa GPD inapatikana kwa kuchukua jumla ya uzalishaji kugawanya na idadi ya watu. Hivyo basi kila mtu anaelewa kama GPD ni kigezo pekee cha maendeleo basi mikoa yoote yenye wakazi wachache ingekuwa imepiga hatua mbele kimaendeleo kuliko mikoa yenye watu wengi.

Hivyo basi kama tunakubaliana kuwa GPD si kigezo cha kuangalia maendeleo katika mikoa yetu, basi tutakuwa tunakubali kuwa Zitto alifanya makosa kutoa mfn ya Arusha na Kilimanjora kuwa inamaendeleo kuliko Shinyanga kwa vile tu Shinyanga wanachangia zaidi katika pato la Taifa.

Na kama tunakubalina na hili basi hapa ndipo hoja ya nguvuri3 inaposimama kuwa pamoja na kuwa Zitto ni mchumi mzuri lakini anatumia lugha za kilaghai kufarakanisha watu. Labda kama Zitto au Adharusi wana maelezo tofauti na haya.. Natumaini Adharusi pindi atakapopata nafasi atakuja kutoa ufafanuzi ni nini Zitto alikusudia na kujibu maswali yangu no.#767
Nadhani hata wewe hukuelewa vizuri swala hili kwa sababu GDP ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yoyote au hata biashara, labda nifananishe kuwa GDP ni sawa na Gross sales za biashara yako. Unapouza zaidi ina maana unapanuka kibiashara na maendeleo ya Biashara yanaweza kuwa source ya maendeleo yako. Lakini tu itategemea hizo Gross sales tunazozungumzia ni zako wewe, au wewe ni dalali ktk franchize ambayo unalipwa commission ya mauzo. Kuna tofauti kubwa katika GDP ikiwa mauzo hayo ni mali yako au sii yako.

Kwa hiyo biashara pasipo kuuza huwezi kusema kuna maendeleo katika biashara hiyo. Na Revenues ni Mapato ya ndani ya serikali ambayo hutumiwa gharama za kuendesha utawala. Hivyo kama utachukua Revenues kama chanzo cha maendeleo utakuwa unakosea kwa sababu Revenues zinaiwezesha serikali kukidhi matumizi yake na mengine ya mihimili na mashirka. Ni sawa na Mshahara wako unapotoa fedha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani haiwezi kuwa chanzo cha mapato yako.

Maendeleo yako hutokana na mafanikio ya biashara zaidi na ni katika biashara hiyo unategemea fedha itoke kukidhi mahitaji ya nyumbani. Kwa hiyo Source ni biashara yako sio fedha unazokata kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Na ndivyo ilivyo katika Revenues yaani pasipo Revenues za kutosha serikali hukosa fedha za kujiendesha kiasi kwamba huanza kukopa nje ili kuendesha shughuli zake. Toka Rais na wizara zake, idara zake hadi mtumishi wa chini wa serikali, Bunge na Mahakama, mashirika ya umaa n.k wote hawa wanategemea Revenues ktk kugharamia matumizi ya usimamizi wa shughuli zao.

GDP inachangia sana Maendeleo ikiwa wamiliki wa mambo yote yanayohusu GDP ni raia ama mashirka yanayozalisha yapo registered nchini kama mashirika ya ndani na sio ya nje ili mzunguko wa fedha utokee nchni. Kwa hiyo utaona kwamba shirika kama Barrick ni changa la macho, yaani wana mauzo makubwa yanayohesabika lakini sisi hatuna chetu ndani. Sisi ni sawa na watu wenye shamba la kukodisha. Barricks kaja kulima akilipa kodi ya pango tu lakini mapato na faida yote ya biashara yake haituhusu. Mauzo ya baaricks yanalipwa tuseme RBC bank ya Canada nayo inakopesha mashirka ya Canada ktk biahsara zao na mzunguko wa pato la Barrick (trickle down) unakuwa upo Canada zaidi sio Tanzania.

Na tunapodai mikataba mibovu ni kwa sababu ilitakiwa sisi tufaidike. Siku hizi ukitaka shamba utaambiwa katika mavuno mwenye shamaba anataka kisu chake, Ukitaka kujenga nyumba mwenye kiwanja atataka mkataba unaompa maghorofa yake, ile habari ya kuuza umekwisha kwa sababu watu wamegundua umuhimu wa kuwa na viwanja au shamba. Sisi kama taifa bado kabisa hatujafikia kuthamini maliasili tulizojaaliwa na pengine hatujiamini kwamba itafika siku tutaweza kuijenga nchi yetu wenyewe.

That's Why Mwalimu Nyerere alikataa nakusema Tuyaache madini ardhini hati vijana wangu watakapo kuwa tayari kuyachimba lakini vijana wenyewe ndio hawa. Kwa hiyo GDP ina mchango mkubwa katika maendeleo kama mauzo hayo yatatokana na sisi. Kwa nchi maskini kama yetu yenye mtaji mdogo mauzo makubwa higher the GDP inatuonyesha tunapanuka kibiashara na hivyo kuwa na fedha zaidi ya kujipanua, kufungua miradi mingine na hata kuvutia wafanyabiashara zaidi kama watu wanavyokimbilia China. Na kila tunavyopanuka ndivyo jamii inavyoendelea maana GDP hu trickle hadi kwako wewe na mimi..
 
Zitto hajui uchumi basi, Ni mbabaishaji mbali Ya kuwa mlaghai na mbaguzi. Tukijikita Katika ukweli unaojitokeza kwamba Zitto hajui uchumi, je:

Matatizo yetu Ni volume of output (GDP) contribution Ya sekta Ya Madini au mapato Ya Kodi katika sekta Ya Madini? Tanzania sasa Ni top three in terms of output Ya mining sector in Africa. Tanzania sasa inavutia wawekezaji wakubwa kutoka kila pande ya dunia Kuja kuwekeza Kwenye mining sector, lakini kwa kauli yako japo juu hence Ya supreme zitto, hilo Ni tatizo. Nini kigumu kujua kwamba Kilio Chetu Ni low revenues and not large output Ya sekta Ya Madini?

Kwa kweli mnasikitisha sana na mchumi wenu uchwara Zitto Kabwe.
Mkuu kuwa top producer wakati mali sio yako haitusaidii kitu sisi tunakula ruzuku tu tofauti kabisa na tunachozungumzia hapa. GDP ni total sales za Tanzania haijalishi mwenye mali hizo ni mwenyeji wa ndani au wa nje, sasa ukija gundua kwamba Barricks na mashrika mengine yote ya madini sio mashirika ya ndani unagundua kwamba sisi tumepangisha tu Ardhi pasipo kuthamini dhahabu yenyewe. Mzunguko wa mapato ya Barricks unaenda ijenga Canada ambako wanalipa kodi vile vile na kuwekeza fedha zao katika mambo mengine ndani ya Canada, madini yetu yanaifaidisha Canada kuliko Tanzania.

Kinachovunwa toka shamba hili na kuuzwa itakuwepo record ya mauzo na ndiyo GDP ya kwamba shamba la Tanzaniai hutoa dhahabu ya Tsh Billioni 300 kwa mwezi, lakini sii zetu ni za Barricks shirika la nje tulomkodishia. Sisi tunafaidika na kodi tulopatana nao. Kwa nini hatukuwa na ubia ama kodi kubwa badala yake tumewapoa msamaha ndizo sababu sio Shinyanga tu bali nchi nzima tumeliwa..
 
Alinda.

Hapa nilitaka nikupe darsa kiduuuchu kuhusu masuala yako hapo juu.

Uchangiaji wa mkoa katika pato la Taifa hauhusiani kabisa na maendeleo ya mkoa. Bali Maendeleo ya nchi yote yanawekwa katika Vipaumbele vya nchi husika na hivyo ndivyo vinavyotoa dira ya bajeti ya mwaka au kipindi fulani ya nchi.

Nadhani hata wewe hukuelewa vizuri swala hili kwa sababu GDP ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yoyote au hata biashara, labda nifananishe kuwa GDP ni sawa na Gross sales za biashara yako. Unapouza zaidi ina maana unapanuka kibiashara na maendeleo ya Biashara yanaweza kuwa source ya maendeleo yako. Lakini tu itategemea hizo Gross sales tunazozungumzia ni zako wewe, au wewe ni dalali ktk franchize ambayo unalipwa commission ya mauzo. Kuna tofauti kubwa katika GDP ikiwa mauzo hayo ni mali yako au sii yako.

Hapa mnazidi kunichanganya ukichukua maelezo ya Barubaru na maelezo yako Mkandara ni tofauti..
Je uchangiaji wa pato la taifa hausiani na maendeleo ya mkoa?
Na je uchangiaji wa pato la taifa linausihana na maendeleo ya Taifa lakini si maendeleo ya mkoa?

Hapa naomba ufafanuzi wenu maana sijui nishike lipi..

Pia Mkandara Umesema hivi; "Mkuu umemamiza ubishi kwa takwimu hizi ila na wewe umekosea kusem GDP maana hiz ni real contribution za mikoa kwa TRA na ndizo nilizokuwa nazisubiria sio GDP maana GDP ni uongo na uzushi mtupu ambao hauna ukweli ktk pato la Taifa maana fedha nyingi zinakwenda nje. Nakumbuka vizuri sana kuwa mchango wa dhahabu ktk pato la Taifa ni chini ya asilimia 2, kama alivyosema JK wakati fulani..Kwa hiyo umenionyesha wazi kuwa Kilimanjatro inachangia zaidi ya Shinyanga wala sii kidogo tofauti ni kubwa sana.

Hapa inabidi tumuombe Zitto atueleze takwimu zake. Nashukuru kwamba umekuja na namba zinazothibitisha ukweli na ndicho nachokitaka miye...na siowezi kubishana juu la hili, pengine huyu Zitto alitumia GDP kama kielelezo au atuambie katumia takwimu gani?

Sasa hapa ulikuwa unamaanisha nini. Maana nilifikiri unasema GPD si kigezo cha maendeleo katika mikoa husika au nimekupata vibaya?

Halafu katika pandiko no. 439

Uliandika hivi Mkuu hadi hapa nimekubaliana na kina
Mchambuzi katika swala la Kilimanjaro na itanipa shaka juu ya sababu ya hoja ya Zitto juu ya matamko yake. Ila swala la Mtwara kusema kweli halihusiani na mchango zaidi ya mahala gani na kwamba hakuna mgao sawa - sidhani. Yawezekana pia mauzo ya gas yanafanyika Dar na collection ya TRA inaonekana Dar zaidi kwa sababu mashirika ya usambazaji gas nchini yapo Dar na ndio yenye kuchangia pato la Taifa.

Last edited by Mkandara; 27th April 2015 at 22:47.

Hapa ulimaanisha nini kusema unakubaliana na Mchambuzi? naomba ufafanuzi pia.

Pamoja na hayo nashukuru wa shule yako. katika mandiko lako hapo juu..
 
Sasa kinachokuchanganya kipi hapa. Labda niweke tafsiri zake kwa Kiingereza kama walivyoeleza wadhungu.

1. GDP is the monitary value of all the finished goods and services produced within a country's borders in a specific time period, though GDP is usally calculated on an annual basis. (The value of its output minus the value of goods that are used up in producing it)

2. National income (Pato la taifa) is the total value a country's final output of all new good and servics produced in one year. Understanding how national income is created is the starting point of macroeconomics.

3. Tax Revenue is the income that is gained by the government through taxation..

Kwa hiyo tunapojadili Pato la Taifa nazungumzia actual value kama vile Net income na GDP ni gross sales.. ndivyo mimi huchukulia tu kama mfano japo havifanani maana Kitaifa hizi hesabu huwa ni makadirio ya kukusanya hutazamia mbele, hata hiyo bajeti yetu hutegemea kukusanya kisia kadhaa (makadirio) wakati hatuna fedha hizo mfukoni. ila huchukulia mapato na matumizi yalopita mwaka jana kama kigezo cha kujenga strategies kwa matumaini ya mbele.
 
Wanaukumbi.

Inawezekana tunachanganya hivi vitu viwili.

1) Jumla ya Pato la Taifa-(Gross Domestic Product - GDP) ni kipimo cha jumla ya pato la utajiri ambalo linapatikana nchini katika muda maalum. Kwa maneno mengine Pato la Taifa ni tathmini ya bidhaa zote na huduma ambazo zinaundwa na zinabadilishwa kwa fedha. Kama jumla ya thamani ya bidhaa na huduma mwaka huu ni asilimia 1% zaidi kuliko ya mwaka jana basi ukuaji wa pato la utajiri ni asilimia 1%. Lakini jumla ya pato la taifa (GDP) huacha kazi zingine za thamani ambazo zingeweza kujumuishwa – kwa mfano, uendeshaji wa kaya na familia kwa kupata nishati rahisi na maji, na pia watu kujenga nyumba zao kwa kutumia vifaa vya asilia na ustawishaji wa vyakula kwa ajili ya matumizi yao.

2) Jumla ya Pato la Taifa-(GNP) ni sawa na jumla ya pato la taifa lakini unaongezea biashara ya ndani na biashara ya nje.
 
Nadhani unaona concept ilivyo ngumu kwa watu wa kawaida, sasa fikiria mwanakijiji, GDP anaweza kudhani ni mshahara wa mwezi na hatuwezi kumlaumu. Kwa mantiki hiyo GDP ikitafsiriwa ni 'mshahara' na hao wanavjiji, kauli ya supreme inajenga taswira gani

That being said and done, swali linakuja. Hivi supreme leader alitumia data zipi na je ujumbe wake ulikusudia nini?

Je, ailikuwa sahihi yeye kusoma takwimu tu kama alivyodai Mkandara?
 
Sasa kinachokuchanganya kipi hapa. Labda niweke tafsiri zake kwa Kiingereza kama walivyoeleza wadhungu.

1. GDP is the monitary value of all the finished goods and services produced within a country's borders in a specific time period, though GDP is usally calculated on an annual basis. (The value of its output minus the value of goods that are used up in producing it)

2. National income (Pato la taifa) is the total value a country's final output of all new good and servics produced in one year. Understanding how national income is created is the starting point of macroeconomics.

3. Tax Revenue is the income that is gained by the government through taxation..

Kwa hiyo tunapojadili Pato la Taifa nazungumzia actual value kama vile Net income na GDP ni gross sales.. ndivyo mimi huchukulia tu kama mfano japo havifanani maana Kitaifa hizi hesabu huwa ni makadirio ya kukusanya hutazamia mbele, hata hiyo bajeti yetu hutegemea kukusanya kisia kadhaa (makadirio) wakati hatuna fedha hizo mfukoni. ila huchukulia mapato na matumizi yalopita mwaka jana kama kigezo cha kujenga strategies kwa matumaini ya mbele.

Asante sana Mkandara

Sasa nimeelewa nini maana ya GPD na nini maanaya pato la Taifa.

Sasa swali langu Je uchangiaji wa pato la taifa unachangiaje maendeleo ya mikoa husika?
 
Asante sana Mkandara

Sasa nimeelewa nini maana ya GPD na nini maanaya pato la Taifa.

Sasa swali langu Je uchangiaji wa pato la taifa unachangiaje maendeleo ya mikoa husika?
Kwanza nianze kwa kusema kwamba nilikuwa namjibu Mchambuzi alipokuwa akitumia Revenues kama Pato la taifa dhidi ya GDP hivyo nadhani ndio maana ukachanganyikiwa.

Pato la taifa kama GNP nadhani kipande hiki kitakusaidia zaidi maana itakuwa maelezo marefu sana Bofya
 
Last edited by a moderator:
Alendi:

Hiyo definition ni GDP au GDP per capital? Ufafanuzi. Sisi wengine shule tulikimbia.

Kuhusiana na maneno ya Zitto, wengi hapa mko trained kuchambua facts. But you have to understand that politics isn't about facts, but narratives. Those who control narratives always win.

Mkuu Zakumi ni GDP per capital.. Asante kwa kuona hilo..

Mwanasiasa ni lazima upime kauli zako kabla hujapanda jukwaa kuhutubia, tena basi linapokuja swala la maneno yako kuleta utengano/uchonganishi baina ya watu fulani na watu fulani ni lazima "nasisitiza tena ni lazima uwe na "fact" ili kuweza kutetea hoja zako pindi uteremkapo kutoka juwaani na watu kuomba ufafanuzi kama ilivyo hapa leo, la sivyo unaweza kuleta mfatafuruku usio na lazima kwa taifa.

Mathalani baada ya Zitto kuutubia na kutoa hizo takwimu humu humu JF katika jukwaa la siasa, Mjadala ulikuwa mkali sana kuna watu walienda mbali na kutukana wachaga kuwa ni mafisadi, wanapendelea mikoa yao (maana kwao Kilimanjro na Arusha ni wachaga)wamejazana katika ofisi za serikali hivyo wanapeleka pesa zote mikoni mwao badala ya mikoa husika na nk.

Sasa je ni kweli kuwa maendeleo yanaangaliwa kwa jicho moja tu la Pato la taifa? Na je ni kweli watu wa Kilimanjaro na Arusha wanahitaji lawama kwa vile tu wao ni "wachakarikaji?" je kulikuwa na ulazima kuhubiri hizi chuki zisiso na umuhimu wowote?
Viongozi wa siasa ni lazima kuwatia moyo wananchi wanaojaribu kujiletea maendeleo na kuhamasisha mikoa ambayo hiko nyuma kimaendeleo kuiga watu mazuri ya ile mkoa iliyopiga hatua. Si vizuri kuwasimanga kwa jitihada zao.
 
Hapana sio kosa la Zitto ni kosa la sisi kuelewa, yaani tunarukia mambo pasipo kuyaelewa wala kupima kwanza. Sasa tazama basi wakati Zitto alizungumzia HDI kutokana na pato la Taifa sisi tukaenda moja kwa moja ktk Revenues na GDP wakati ni mchanganuo tofauti kabisa. Kwa kutazama mchango wa Shinyanga katika Pato la Taifa (National Income) Zitto kaweza kutupa data zinazoonyesha Shinyanga wapo chini wakati wanachangia zaidi, hivyo ni msukumo kwa wananchi kuelewa haja ya kufumua mfumo uliopo na kuweka mfumo ulokuwa bora zaidi.

Pengine swali la kumuuliza Zitto, katika muundo wa ACT na Ujamaa, serikali yake ingeweza vipi kuhakikisha Shinyanga wanafaidika zaidi kwa mchango wao maana kumbukeni nchi zote za Magharibi majimbo yalochangia zaidi hufaidika zaidi na mchango wao, na majimbo mengine huwezeshwa zaidi ili nao wachangie zaidi ktk miradi inayoongeza Productivity na hivyo kukiuza pato la taifa.

Hakuna loser, ndio maana nikamwambia nguruvi ya kwamba ukiomba ongezeko la mshahara kutokana na uzalishaji wako haina maana unataka mtu mwingine apunguziwe mshahara kwa sababu tu umetaja jina lake kuwa na pato zaidi yako. Au ni kuzua uadui baina yenu hii akili ni ya Kibongo tu siku zote tunaogopana. Lakini ni lazima mtu utumie kigezo baina yako na wafanyakazi wengine na ndivyo madai ya wanawake kuhusu mishahara sawa na wanaume haina maana kuwa mshahara wa wanaume utakatwe ili wanawake walipwe..Ni kutoelewa tu kwa watu.
 
Bado unakwepesha swali, ni uhusiano gani uliopo kati ya hayo unayosema, na aliyosema supreme leader kwa kuangalia mgawanyo wa pato la taifa, maendeleo, Shinyanga Vs Kilimanjaro/Arusha

Nadhani ukisoma maandiko yako utaona kuwa unachikiongelea nii mfumo kama taifa. Maelezo ya supreme yanaongelea ukanda zaidi yakionyesha wapo wanaochangia zaidi na kupata kidogo na wapo wanachangia kidogo na kupata zaidi.

Ndio msingi wa swali la kwanza hapo juu, onyesha uhusiano huo kwanza

Pili, ni wananchi wangapi wanaweza kuelewa kwa mtazamo wako as opposed na maelezo ya Supreme leader
 
Mkuu Zakumi ni GDP per capital.. Asante kwa kuona hilo..

Mwanasiasa ni lazima upime kauli zako kabla hujapanda jukwaa kuhutubia, tena basi linapokuja swala la maneno yako kuleta utengano/uchonganishi baina ya watu fulani na watu fulani ni lazima "nasisitiza tena ni lazima uwe na "fact" ili kuweza kutetea hoja zako pindi uteremkapo kutoka juwaani na watu kuomba ufafanuzi kama ilivyo hapa leo, la sivyo unaweza kuleta mfatafuruku usio na lazima kwa taifa.

Mathalani baada ya Zitto kuutubia na kutoa hizo takwimu humu humu JF katika jukwaa la siasa, Mjadala ulikuwa mkali sana kuna watu walienda mbali na kutukana wachaga kuwa ni mafisadi, wanapendelea mikoa yao (maana kwao Kilimanjro na Arusha ni wachaga)wamejazana katika ofisi za serikali hivyo wanapeleka pesa zote mikoni mwao badala ya mikoa husika na nk.

Sasa je ni kweli kuwa maendeleo yanaangaliwa kwa jicho moja tu la Pato la taifa? Na je ni kweli watu wa Kilimanjaro na Arusha wanahitaji lawama kwa vile tu wao ni "wachakarikaji?" je kulikuwa na ulazima kuhubiri hizi chuki zisiso na umuhimu wowote?
Viongozi wa siasa ni lazima kuwatia moyo wananchi wanaojaribu kujiletea maendeleo na kuhamasisha mikoa ambayo hiko nyuma kimaendeleo kuiga watu mazuri ya ile mkoa iliyopiga hatua. Si vizuri kuwasimanga kwa jitihada zao.
Supreme leader hakuwa na facts mkononi. Alikuwa na hisia kutokana na matatizo ya kisiasa.
Alikuwa na hasira kutokana na mahasimu wake. Alichokifanya supreme sidhani kama ni bahati mbaya, ni makusudi

Lengo lake lilikuwa kuwauta watu kisiasa kwa kuwashawishi kuwa huko kwingine waliko ni kwa 'wabaya' wao.
Ukisoma data za HDI, ni dhahiri ali target mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Hakufanya comparison kati ya mikoa 1-6 na Shinyanga na Mwanza, bali miko hiyo miwili na 7 na 9 ambayo ni target yake.

Mijadala ulikuwepo katika jukwaa la siasa kwa muda ukivuruga watu katika lines za ukabila na ukanda.

Of course kisiasa hilo lilimsaidia supreme kufikia sehemu ya lengo lake, kitaifa ni kosa kubwa sana.

Akiwa kiongozi, supreme ana jukumu la kuwaleta Watanzania katika ''common interest'' na si kuwagawa kama alivyofanya.

Na wala hakuchukua hatua za kusahihisha matatizo na usumbufu aliouleta.

Alifanya hivyo akiamini kuwa kanda fulani ni muhimu kwake kisiasa bila kujua impact katika taifa kwa ujumla

Ukisoma uzi huu, mwanzo tumeangalia maendeleo kwa ufupi na kueleza tofauti zinaweza kutokana na nini.
Mkandara na watetezi wenzake hakuna hata mmoja aliyejitokeza kusema bandiko hilo halikuwa sahihi.

Wanatambua kuwa zipo factos zinazochangia maendeleo kama historia, kijiografia, kiuchumi n.k

Wancahokifanya sasa hivi ni kufunika uvundo, ndio maana wamefikia kusema 'Zitto amesoma tu data' mkutanoni asilaumiwe.

Kwamba, akiwa mwanasiasa mwenye ushawishi, ni haki yake kutupa uchafu katika jamii na avumiliwe tu.

Hapa tupo kumwajibisha kwa kauli zake, kumekemea katika kuligawa taifa na kuchochea chuki miongoni mwa Raia

Tunaweza kuona watu wanaoelewa bado wanatatizika katika masuala haya.

Hivi ilikuwa sahihi kwenda kusema Kilimanjaro na Arusha wanachangia kidogo wanapata zaidi ya Shinyanga na Mwanza wanaochangia sana na kupata kidogo akiwa na HDI mkononi! kutibitisha kile alichojaribu kukipa picha ya uonevu

Wangapi wanajua kutafsiri takwimu hizo ambazo watetezi wake hawawezi kuzitetea hapa jamvini

Hatuonyeshwi uhusiano katika ya kuchangia, kugawanywa, maendeleo, na mikoa husika.

Tunapewa utetezi laini 'Alisoma data tu' kama anaimba mashairi, tumwache aendelee kuvuruga taifa!
 
Back
Top Bottom