Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Kabla hatujafika huko tupe hotuba iloinukuu maneno hayo tuyasome sote maana inaonyesha kuna sintofahamu juu ya hotuba hiyo. Kila mtu anasema lake hivyo ili tuwe mstari mmoja yaweke maneno ya Zitto yanayoonyesha kuwa mikoa fulani huinyonya Shinyanga!

..wewe si ndiye uliyekuwa ukimtetea kwamba anasema ukweli? kuhusu hiyo dhuluma na unyonyaji.

..hii siyo thread ya kwanza mimi na wewe kujadili kile alichokisema Zitto kwa wananchi wa Shinyanga.
 
..wewe si ndiye uliyekuwa ukimtetea kwamba anasema ukweli? kuhusu hiyo dhuluma na unyonyaji.

..hii siyo thread ya kwanza mimi na wewe kujadili kile alichokisema Zitto kwa wananchi wa Shinyanga.
Mkuu usitake kubadilisha kauli yangu. Nionyeshe mahala popote niliposema kauli yoyote inahusu mikoa hiyo kuidhulumu Shinyanga maana wewe ndio ulokuwa ukisema nami nikipinga. Nikakupa hadi mfano wa Umaskini wetu ukizungumziwa tukaitaja Singapore au Malaysia kuwa haina maana Singapore inahusika na mjadala isipokuwa Singapore ni mfano tu unaotumika. Nikaupa hata Apartheid. Leo tunaweza kupima wizara ya ELIMU dhidi ya ULINZI kama kuna viashirio lakini haina maana wizara ya ulinzi inaidhulumu wizara ya Elimu huu ndio mtazamo wangu ktk swala hilo.

Hii hadithi ya kwamba Zitto aliitaja mikoa hiyo kwa dhumuni la kuleta Ukabila inatokana na mwenye kuisoma awe kajenga fikra kwamba Kilimanjaro ni mikoa ya Wachagga ama Chadema hasa mlalamikaji akiwa na mahusiano na sehemu hizo kwa sababu katika sentesi hiyo kuna mikoa ya Dar, Arusha na Kilimanjaro lakini wamechomoa mkoa mmoja tu kuonyesha chuki ya Zitto kwa Wachagga. na ndio mjadala ulotuweka hapa muda wote huu tukatoka katika mada yenyewe.

Mara ngapi humu tumezungumzia Tanganyika na Zanzibar, nikawa against wazo la utengano na mkweli kutetea UMOJA wetu dhidi ya wale wanaofikiria Utengano wa kikabila iwe Mzanzibar au Mtanganyika? Nimeyasoma maoni mangapi humu yanayodhihirisha fikra za UMIMI ya kwamba Zanzibar inabebwa na Tanganyika?

Nikapingana na dhana hiyo kwa kusema tusilaumiane sisi bali tulaumu mfumo uliopo kuwa ndio mbovu na hata mapendekezo yanayotolewa yatajenga uhasama zaidi? Kisha nikajenga hoja ya kile kinachotakiwa kufanyika maana kiuchumi serikali ndiye mjenzi wa msingi kwa policies na miundombinu kama chachu ya Economic Transiformation. Watu hawawezi kubadilisha nchi wala mkoa pasipo serikali kwanza kuwa na mfumo bora wa kiuchumi na ktk ubora wake ndio maana wachumi husema ili tuendelee tunahitaji WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA haya sio maneno ya Mwalimu ila ni elimu ya Uchumi ambayo wengi wanafikiri mwalimu ndiye mwanzilishi wake lakini ndio kiini cha fikra zozote za muundo wa Utaifa, vyama vingi, uwajibikaji, uadhilifu, uwazi na uzalendo wa kila Taifa duniani.
 
..kuna maneno vs hoja.

..hoja nzima ya Zitto inajenga dhana kwamba kuna mikoa na jamii fulani zinadhulumu mikoa na jamii nyingine.

cc Mkandara, Nguruvi3, TRUVADA
Mkuu kwa faida ya Wanaukumbi unaweza kutuwekea hayo maneno ya Zitto kayasemea wapi tuwekee nukuu zake kiduchu!!

Samahani lakini...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa faida ya Wanaukumbi unaweza kutuwekea hayo maneno ya Zitto kayasemea wapi tuwekee nukuu zake kiduchu!!

Samahani lakini...
Wakuu ebu pitieni mchango wa Bi. Azza Hilal Hamad kuhusu Shinyanga akiwa bungeni Hapa.
 

Mkandara,

Tatizo lenu (Waberoya, Ritz, Adharusi, Zakumi et al) mnabeba maneno ya Supreme leader Zitto kama ALPHA na OMEGA. Mmebanwa, sasa mnahama kutoka Zitto KAYASEMA, sasa mnamtetea kwa hoja kwamba zitto KAYASOMA. Pamoja na ujanja ujanja wenu huu, bado hoja zenu pamoja na zitto zimetawaliwa na mapungufu, na huo ndio msingi wetu wa hoja. Sasa mnatulazimisha tuachane na hoja ya Zitto “KASEMA”, na badaka yake tujadili hoja ya zitto "KASOMA". Sawa, twende huko huko kwa supreme leader Zitto “KASOMA”.

Fine, Zitto Kasoma 'Tanzania Human Development Report 2014'. Katika sehemu ya utangulizi wa ripoti hii, sehemu moja “INASOMEKA” hivi:

"This report argues that, economic growth, while welcomed and necessary, is not sufficient. Rather than focusing on the mere expansion of output, Tanzania needs to emphasize the importance of changing qualitative features of production that occur through the growth process."

Wajuzi wa ukalimali watatusaidia na tafsiri hapa. Vinginevyo hapa tunagundua kwa urahisi tu kwamba Zitto alisoma, hakuelewa. Hii ni kwa sababu, hakuwa na muda wa kusoma kwa undani na kuelewa jinsi gani ripoti ALIYOSOMA inajihami juu ya mapungufu yaliyopo. Kwa msomi, hasa wa hulka ya zitto, ilitakiwa aelewe mapema kabisa kwamba kila ripoti ina limitations zake na huwekwa wazi kabisa. Lakini badala yake, msomi na mchumi zitto akakimbilia kwenye sehemu yenye takwimu ili aweze kuwahi mikutano yake ya kilaghai na kibaguzi.

Huko nyuma, nilimwambia Zakumi haya haya – kwamba GDP as a measure isn’t sufficient to lead us into conclusion ya Zitto. Zakumi akabisha na kuhamia kwenye hoja kwamba kiongozi bora ni yule mwenye uwezo wa ujanja ujanja wa maneno ya kisiasa. Kwa maana nyingine, zakumi akahalalisha ulaghai , ubaguzi na utapeli wa zitto kwa hoja kwamba siasa is supreme to everything – rationality, objectivity, and common sense. Je hadi hapa:

* Hamuoni kwamba ni wazi zitto hakusoma ripoti yote na kuielewa kabla ya kutumia katika ziara zake za kitapeli na kibaguzi?
*Hamuoni kwamba Zitto anapingana na ripoti aliyosoma kwa maana ya kwamba he's prematurely leading us into conclusion za kutugawa na kutupotosha?

Kwa uwazi kabisa, ripoti inatuonya kwamba tusipagawe na dhana ya expansion of output (GDP) kufikia hitimisho juu ya tofauti ya maendeleo baina ya eneo moja na eneo lingine. Lakini zitto hilo hana muda nalo, anadhania watanzania wote ni wajinga tu wa kulishwa takwimu ambazo hazija fanyiwa uchambuzi ili zikiwasilishwa, zijenge badala ya kubomoa. Lakini mbaya zaidi, na nyie mnadandia makosa hayo hayo. Kwa kweli inasikitisha sana.

Ripoti ALIYOSOMA Supreme Leader Zitto inahimiza juu ya umuhimu wetu kama taifa kujikita zaidi on "qualitative features of production" kuliko "quantitative features" (GDP). Na hii imekuwa ni moja ya sehemu muhimu sana ya hoja zetu kupinga uropokaji, ubaguzi na upotoshaji wa Zitto Kabwe mbele ya umma.

Ebu tazame hitimisho la ripoti ILIYOSOMWA na Zitto:


["...while HDI and MPI are useful measures of human development, they are by no means adequate for explaining the contradictions between economic growth and slow trends in poverty reduction or raised living standards. The chapter extended the discussion of human development beyond the attributes of HDI and MPI to include population dynamics, particularly the vital components of the human lifecycle, namely fertility, age at marriage, mortality and migration, and the implications of these for achieving human development. The chapter argued that achieving quality aspects of growth and income would require policies and strategies that address the qualitative ingredients needed to achieve qualitative growth."]

Hapa tunaona wazi jinsi gani HDI inajadiliwa kuwa ni dhaifu. Mkandara yeye haoni hilo, anachoona ni ALICHOSOMA Zitto. Nukuu hii inaenda mbali zaidi na kujadili masuala ambayo tuliyagusia, hasa suala la idadi ya watu kwa mapana na marefu yake. Hitimisho hapo ni kwamba kufanikisha quality growth and income inawezekana kwa kuhusisha ‘qualitative ingedients’ suala ambalo litapelekea ‘qualitative growth’. Hizi ‘qualitative ingedients’, Nguruvi3 na wengine wamezijadili kwa kina, hasa jinsi gani mikoa ya Kilimanjaro na Kagera wamezifanyia kazi, hivyo kuvuna matunda yao kwa kupiga hatua kubwa kimaendeleo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa faida ya Wanaukumbi unaweza kutuwekea hayo maneno ya Zitto kayasemea wapi tuwekee nukuu zake kiduchu!! Samahani lakini...
Ritz , kama ninakumbuka, ulisema umesikiliza hotuba yote ya Zitto viwanja vya furshisha, Je ni kweli ulisikiliza au ulisoma? Na ilikuwa lini hiyo?
 
 
Wakuu Ritz na Mkandara, naona mnakomalia nilipopata nukuu nilizozitoa na kufikia hatua ya kunituhumu kama muongo na mpika habari; hapa chini nanukuu taarifa ya Supreme Leader aliyoitoa tarehe mosi mwezi wa tatu mwaka 2010 kwa waandishi wa habari akijibu habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika Gazeti la Mwananchi na The Citizen ya leo Jumatatu, Tarehe 1/3/2010 kuna habari ya kwamba ninatafakari kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. Nimeona ni vema nitoe taarifa rasmi juu ya jambo hili.

Nimeunda kamati ya uchunguzi (Exploratory Committee) ya watu watatu kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina juu ya jimbo gani nigombee Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka 2010. Majimbo ambayo nimeomba wayaangalie ni pamoja na
Kigoma Kaskazini (ukiondoa kata ya Mwandiga ambayo imependekezwa kukatwa na kupelekwa Jimbo la Kigoma Mjini na hivyo kuondoa zaidi ya wapiga kura 15, 000 kutoka jimbo la Kigoma Kaskazini la sasa), Kigoma Mjini, Kahama, Kinondoni na Geita.

Nimeelekeza kufanyike utafiti (survey) wa kina ili nitakapofikia kufanya maamuzi nifanye maamuzi kutokana na taarifa za kutosha. Tutatumia wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya utafiti huo katika majimbo hayo na pia kwa ajili wa uchambuzi wa hali ya kisiasa na kutoa mapendekezo.


Ninatarajia kutangaza rasmi Jimbo nitakalogombea Ubunge mnamo siku ya Jumapili tarehe
28/3/2010.

Naomba ifahamike kuwa bado sijafanya uamuzi rasmi na kwamba uamuzi wangu utazingatia taarifa ya uchunguzi, ushauri wa viongozi wa chama changu (CHADEMA) na matarajio yangu ya kisiasa ya baadae. Ni muhimu kusisitiza kuwa nikiwa Mtanzania nina haki ya kugombea Ubunge mahala popote nchini.

Uamuzi wowote nitakaoutoa utazingatia kwa kiasi kikubwa sana umuhimu wa kujenga mfumo imara wa demokrasia ya vyama vingi na hasa kuwa na Bunge imara lenye wabunge wengi wa kambi ya upinzani.



(imesainiwa)

ZZK.

1/3/2010


Yawezekana kwamba hata haya majigambo ya Zitto msiyapokee wala kuyakubali kama kweli aliyatoa ila narudia kutoa tahadhari niliyoitoa hapo awali kuwa JF kwa kumbu kumbu haina mfanowe. Ndio maana ninaporudi nyuma na kumsoma Mkandara mara nyingi nabaki mdomo wazi kwa mshangao nikijiuliza kwa nini anakuwa msahaulifu kiasi hicho. Hapa tunaushuhudia ulaghai live na bila chenga wa shujaa wenu Supreme Leader Zitto Zuberi Kabwe nuru, dira na taa ya ACT.

Jibu wanalolitoa wapenzi wa Supreme Leader ni kwamba hata wengine wameshawahi kusema hadharani mipango yao ya kugombea ama Ubunge au hata Uraisi. Kweli amnyimae punda adesi, kampunguzia mashuzi...ni wapi kwa mfano Mh. Mbowe amewahi kudai amepokea barua ya maombi kutoka Mwanza, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Ukerewe n.k wakimgombania awawakilishe na kujikuta anaunda kamati imshauri agombee jimbo gani! Huu kama si ulaghai ni nini?
 
Last edited by a moderator:
Ritz , kama ninakumbuka, ulisema umesikiliza hotuba yote ya Zitto viwanja vya furshisha, Je ni kweli ulisikiliza au ulisoma? Na ilikuwa lini hiyo?
Nimeisilikiza na kuisoma pia hapa JF jukwaa la siasa sijui wewe mwenzagu ulisikiliza au ulisoma?
 

Mag3.

Sijakuelewa kwenye ili bandiko lako kosa la Zitto ni lipi? Siku hizi Citizen wana makala za kiswahili nilikuwa sifahamu.
 
Last edited by a moderator:
Mag3.
Sijakuelewa kwenye ili bandiko lako kosa la Zitto ni lipi? Siku hizi Citizen wana makala za kiswahili nilikuwa sifahamu.
Yaani hata hata uungwana tu wa kuniomba radhi kwa kuniita mzee muongo na mpika maneno hauna Ritz! Hakika hata huko tunakoelekea sijui kama tutafika, how sad...!
 
Last edited by a moderator:
Yaani hata hata uungwana tu wa kuniomba radhi kwa kuniita mzee muongo na mpika maneno hauna Ritz! Hakika hata huko tunakoelekea sijui kama tutafika, how sad...!
Mkuu uungwana upi unataka nikufanyie wakati Habari zako zinajichanganya jisome hapa chini.

Mag3

By February 2010:
Hadi sasa nimekwishapokea maombi mengi kutoka kwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni, Kahama, Geita, Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini ili niwawakilishe bungeni," alisema Zitto.

Hata hivyo, Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hadi sasa bado hajafanya uamuzi rasmi wa jimbo gani kati ya hayo atakwenda kugombea.


Hii habari yako ya mwanzo tofauti na hii uliyokuja nayo kutoka kwenye Mwananchi.
Angalia tarehe zako unaweza kweli kuchanganya February na March.
 
Last edited by a moderator:
Yale yale ya Mkandara, kuhamisha goli mnaposhikwa pabaya. Mwananchi waliandika habari tarehe 28 February 2010, Citizen wakairudia kwa Kiingereza kesho yake siku ambayo Zitto pia alitoa taarifa kwa Waandishi wa habari. What's so hard to understand here? Shame on you guys!
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na yote habari zako bado zipo tofauti habari niliyokupinga mwanzo maandishi yake mbona hayapo kwenye hiyo habari mpya hizi habari zote ulizokuja nazo ni za kiswahili.
 
Last edited by a moderator:
Nimeisilikiza na kuisoma pia hapa JF jukwaa la siasa sijui wewe mwenzagu ulisikiliza au ulisoma?
Je,hiyouliyosoma na kuisikiliza inafanana na hii hapa chini?

 
Je,hiyouliyosoma na kuisikiliza inafanana na hii hapa chini?

Umeniuliza swali nimekujibu na mimi pia nimekuiliza swali nijibu ndiyo utaratibu sasa wewe kazi yako kuuliza maswali wenzako tu au wewe ndiyo supreme leader wa ili jukwaa jibu swali langu.

Hotuba ya Zitto uliisikia wapi wapi au uliisoma wapi?

Kisha tuendelee na mpini...
 
Nimeisikia redioni na kuisoma JF
Tuendelee hapa chini
Nimeisilikizana kuisoma pia hapa JF jukwaa la siasa sijui wewe mwenzagu ulisikiliza auulisoma?
Je,hiyouliyosoma na kuisikiliza inafanana na hii hapa chini?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…