Unajua mnapo laumu mtu juu ya jambo inatakiwa kwanza mjipime wenyewe. kwa sababu mnapenda kunilaumu mimi kumuamini
Ritz wakati nyie wenyewe hamna nukuu halisi ya hotuba ya Zitto akiwa Shinyanga, hata nyie sielewi mliipata wapi japo nilikubali mloyaandika kama hotuba ya Zitto na tukajadili nikitoa mfano wa hotuba ya Mbowe vile vile akiwa Shinyanga. Kama mnapinga aloyaandika
Ritz vizuri wekeni hotuba halisi na tuonyesheni link yake maana unapotaka Ritz atoe Link inawabidi nanyi katika madai yenu mtoe Link ya madai yenu kuwa ndio halali.
Nimejaribu kupitia hotuba yake ilowekwa humu JF sikuona mahala wameiweka hotuba kamili kama mlivyosema. Maelezo ya mkutano huo haya
Hapa, na ukisoma imeelezwa kwa ufafanuzi mzuri sana. Nje ya hapo nachukua maelezo yenu (iwe wewe au Ritz) na kuyajengea Hoja maana tupo ktk mjadala. Sikuwepo Shinyanga na wala sikuiona Hotuba hiyo. Na unaposema ati Zitto hakuitaja mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kwa bahati mbaya ni swala lako wewe kukataa ukweli maana kama kuna ukweli katika maelezo yake kuna ubaya gani. Ubaya ni kutunga kitu ambacho hakina Ukweli na ukweli tumeupata HDR kuwa takwimu zipo kama alivyoonyesha
Mchambuzi takwimu za TRA siwezi kumpinga kwa sababu ati kwa sababu sio zake kanukuu TRA.
Kosa ni pale anaposema kitu ambacho sii kweli. HDR wametuonyesha takwimu zao na mchango wa Shinyanga iweje kuitaja mikoa hiyo iwe tatizo? mngependa aitaje mikoa gani na isingekuwa tatizo ikiwa fikra zenu hazikujenga hoja ya Ukabila. Je, kwa fikra hizo hizo mlokuwa nazo angesema Shinyanga inachangia kuliko Dodoma lakini Dodoma wanapewa zaidi isingekuwa Ukabila dhidi ya Wagogo?. Au Dodoma kidogo haina nguvu ya hoja kuliko mikoa mloitaja?
Nauliza:- Kwa nini mnafikiria ni Ukabila kuitaja Arusha na Kilimanjaro kama sio lengo lenu kuhakikisha ACT haikubaliki Arusha na Kilimanjaro kwa kuzua fitna hii mapema. Maana sioni sababu zaidi ya kwamba nyie ndio wenye nia ya kuichafua ACT isipate wanachama mikoa ambayo Chadema inaweka ngome yake. Ama nyie wenyewe mna hisia za ukbaila na mpo tayari kuilinda mikoa yenu dhidi ya maneno yyote yanayohusu Mikoa hiyo au Chadema, maana rahisi kwenu kuizungumzia vibaya Kigoma na ACT lakini isiwe Kilimanjaro na Chadema - Kwa nini? kama watanzania kwanini mnakuwa na mipaka ktk nchi hii kuzungumziwa.
Maswala ya Zitto kuwa Supreme huo ni mtazamo wenu kwa sababu hata Mbowe alikuwa na ambition toka nimjue na kafika mbali kwa juhudi zake na sii kuyataka madaraka tu bali he worked for it. Dr.Slaa pia nimeonyesha huko nyuma na wengine wengi tu wameingia katika Siasa kwa nguvu kubwa wakitaka kuwa watu fulani na wamefanikiwa wengine imebuma. Kwa hiyo kila mtu ana malengo yake, Ningependa sana kuwa tajiri isipokuwa sioni njia rahisi na halali lakini kama ipo na pasipo kukiuka sheria why not follow that right path hata kama kuna watu wataona wivu.
Mkandara,
Tatizo lenu (
Waberoya,
Ritz,
Adharusi,
Zakumi et al) mnabeba maneno ya Supreme leader
Zitto kama ALPHA na OMEGA. Mmebanwa, sasa mnahama kutoka Zitto KAYASEMA, sasa mnamtetea kwa hoja kwamba zitto KAYASOMA. Pamoja na ujanja ujanja wenu huu, bado hoja zenu pamoja na zitto zimetawaliwa na mapungufu, na huo ndio msingi wetu wa hoja. Sasa mnatulazimisha tuachane na hoja ya Zitto KASEMA, na badaka yake tujadili hoja ya zitto "KASOMA". Sawa, twende huko huko kwa supreme leader Zitto KASOMA.
Fine, Zitto Kasoma 'Tanzania Human Development Report 2014'. Katika sehemu ya utangulizi wa ripoti hii, sehemu moja INASOMEKA hivi:
"This report argues that,
economic growth, while welcomed and necessary, is not sufficient. Rather than focusing on the mere expansion of output, Tanzania needs to emphasize the importance of changing qualitative features of production that occur through the growth process."
Wajuzi wa ukalimali watatusaidia na tafsiri hapa. Vinginevyo hapa tunagundua kwa urahisi tu kwamba Zitto alisoma, hakuelewa. Hii ni kwa sababu, hakuwa na muda wa kusoma kwa undani na kuelewa jinsi gani ripoti ALIYOSOMA inajihami juu ya mapungufu yaliyopo. Kwa msomi, hasa wa hulka ya zitto, ilitakiwa aelewe mapema kabisa kwamba kila ripoti ina limitations zake na huwekwa wazi kabisa. Lakini badala yake, msomi na mchumi zitto akakimbilia kwenye sehemu yenye takwimu ili aweze kuwahi mikutano yake ya kilaghai na kibaguzi.
Huko nyuma, nilimwambia
Zakumi haya haya kwamba GDP as a measure isnt sufficient to lead us into conclusion ya Zitto. Zakumi akabisha na kuhamia kwenye hoja kwamba kiongozi bora ni yule mwenye uwezo wa ujanja ujanja wa maneno ya kisiasa. Kwa maana nyingine, zakumi akahalalisha ulaghai , ubaguzi na utapeli wa zitto kwa hoja kwamba siasa is supreme to everything rationality, objectivity, and common sense. Je hadi hapa:
* Hamuoni kwamba ni wazi zitto hakusoma ripoti yote na kuielewa kabla ya kutumia katika ziara zake za kitapeli na kibaguzi?
*Hamuoni kwamba Zitto anapingana na ripoti aliyosoma kwa maana ya kwamba he's prematurely leading us into conclusion za kutugawa na kutupotosha?
Kwa uwazi kabisa, ripoti inatuonya kwamba tusipagawe na dhana ya expansion of output (GDP) kufikia hitimisho juu ya tofauti ya maendeleo baina ya eneo moja na eneo lingine. Lakini zitto hilo hana muda nalo, anadhania watanzania wote ni wajinga tu wa kulishwa takwimu ambazo hazija fanyiwa uchambuzi ili zikiwasilishwa, zijenge badala ya kubomoa. Lakini mbaya zaidi, na nyie mnadandia makosa hayo hayo. Kwa kweli inasikitisha sana.
Ripoti ALIYOSOMA Supreme Leader Zitto inahimiza juu ya umuhimu wetu kama taifa kujikita zaidi on "qualitative features of production" kuliko "quantitative features" (GDP). Na hii imekuwa ni moja ya sehemu muhimu sana ya hoja zetu kupinga uropokaji, ubaguzi na upotoshaji wa Zitto Kabwe mbele ya umma.
Ebu tazame hitimisho la ripoti ILIYOSOMWA na Zitto:
["...while HDI and MPI are useful measures of human development, they are by no means adequate for explaining the contradictions between economic growth and slow trends in poverty reduction or raised living standards. The chapter extended the discussion of human development beyond the attributes of HDI and MPI to include population dynamics, particularly the vital components of the human lifecycle, namely fertility, age at marriage, mortality and migration, and the implications of these for achieving human development. The chapter argued that achieving quality aspects of growth and income would require policies and strategies that address the qualitative ingredients needed to achieve qualitative growth."]
Hapa tunaona wazi jinsi gani HDI inajadiliwa kuwa ni dhaifu. Mkandara yeye haoni hilo, anachoona ni ALICHOSOMA Zitto. Nukuu hii inaenda mbali zaidi na kujadili masuala ambayo tuliyagusia, hasa suala la idadi ya watu kwa mapana na marefu yake. Hitimisho hapo ni kwamba kufanikisha quality growth and income inawezekana kwa kuhusisha qualitative ingedients suala ambalo litapelekea qualitative growth. Hizi qualitative ingedients,
Nguruvi3 na wengine wamezijadili kwa kina, hasa jinsi gani mikoa ya Kilimanjaro na Kagera wamezifanyia kazi, hivyo kuvuna matunda yao kwa kupiga hatua kubwa kimaendeleo.