Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Shukran sana hiyo Lindi hawana haja nayo maana haiko kaskazini? ama kweli wameipania ACT wakati ni kizazi chao wenyewe, unajua ni kama mzazi alokataa mimba hutunga kila mbinu kuikana japo anajua kuwa yeye ndiye haswa aloitia mimba. Utasikia mbona pua yake kama ya Hussein yule unayesema siku zote kuwa rafiki tu. Mkataa mimba siku zote huwa yeye ndiye mwenye sababu.
 
Mtu yeyote makini, mwenye kujenga hoja za Kishawishi, Kutumia lugha za kuudhi, na vijembe vilivyopitiliza ni dalili ya Chuki. Mfano Nguruvi3, Kila mara anatumia jina la maadui wa Zitto kisiasa kumdhihaki. Tazama jina la dhihaka analotumia la "Supreme Leader", au wakati mwingine akitumia neno " Supreme", Ni dhahiri kwa mtu aliyegreat thinker, yeye angejikita kwenye kujenga hoja, badala ya "ad hominem attacks", "name calling" au character assasination.
 

Ninakumbushia maswali yangu page 55 no.#1088 ... tupe darasa na sisi tufaidike.
 
Tunachouliza sisi kwa nini mmenyofoa Kilimanjaro na Arusha tu, wakati Zitto katumia maneno hayo hayo kwenye mikoa mingineyo tazama hutoba yake hapa halafu tazama ulipochukua la Shinyanga kuwa mkoa maskini wewe umelipachika wapi?

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake. Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.

Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora.
Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.

Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%).
Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.

Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%.
Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.
 

Hivi kuna takwimu gani zinazoonyesha TRA kuna wachaga wengi kuliko makabila mengine? Pili kama hawa wachaga wanasifa za kuajiriwa tatizo liko wapi? NI sekta gani hapa nchini unapokwenda ukakuta mlinganyo wa makabila? au dini? na kama kila sekta kuna watu wa kabila fulani wengi kuliko makabila mengine kwanini iwe TRA tu? Nenda Mamlaka ya Pamba Mwanza kule ni wasukuma tupu tena hata mle ofisi lugha inayotumika ni kisukuma lakini hakuna mtu anayelalamika maana ni watanzani wenzetu, waliajiriwa kutoka na sifa zao si kabila yao sasa hapo tatizo ni nini?
Yaani unataka tufike wakati wa kuajiri tuangalie kabila la mtu si sifa za mtu? Hivi huko kwenye duani ya kwanza unapoishi ndivyo wanavyoajiri kwa kuangalia makabila (hivi wana makabila huko kweli) na kuwa kufanya hivi kweli Tanzania yetu inaweza kupiga hatua kwenda mbele?

(Nje ya topic) NImekuwa nikijiuliza hasa kuwa mchaga ni nani? ni yule mtu mwenye jina la kichaga? au ni yule mtu alizaliwa Kagera na wazazi ambao ni wachaga ila huyu mtu anafahamu kihaya, anaishi mila na desturi za kihaya, hajawahi kwenda uchagani zaidi ya kusikia simulizi? au ni yule aliyezaliwa uchagani, akajifunza mila na desturi za kichaga, kaongea kichaga ingawaje wazazi wake ni wahaya? Swali langu hapa Mchaga ni yupi?? (hili swali ni kwa kila mtu atakayependa kunipa ufafanuzi haliusiani na topiki iliyo mbele yetu)
 
Hii hotuba si ya kweli, maneno yamefichwa.

Tumemuuliza aliyeileta kama inafanana na ile nyingine, wote wakakimbia. Maneno yameongezwa na kupunguzwa

Tukirudi nyuma, Mkandara hupaswi kutumia hotuba yoyote ile zaidi ya ile uliyosikia mwenyewe iliyokuwa na maneno
'' Kilimanjaro inachangia kidogo inapasta stahiki, Shinyanga inachangia sana haipati stahiki''

Tumekuuliza ni stahiki gani Kilimanjaro inapata? Ni stahiki gani Shinyanga haipati

Hivyo usibabaike kwa kutumia hotuba ziliazoandikwa kwa kuhaririwa.

Soma ile ya Adharusi halafu linganisha na hiyo unayosema. Usiturudishe kule tuliko acha.

Tetea hotuba yako au nenda katika maneno aliyonukuu Alinda katika twits

Pili, video iliyoletwa imekatwa pale Kilimanjaro ilipotajwa, why? Nini kinafichwa

Tatu, Kilimanjaro na Aeusha hazipo katika top list ya kuchangia au maendeleo. Neno ''hata hivyo'' limetumika kwa maana gani.

Nne, kwanini Zitto amechomoa Kilimanjaro(9) , Arusha(7) na kuacha mikoa iliyo mbele ya hiyo. Ni kigezo gani alitumia

Nne, Zitto alishawahi kusema Kigoma na Kilimnajaro zinatofautiana kwa maendeleo hivyo watu waisogope EAC
Zitto hakuwahi kusema Dar au Lindi, bali alikwenda moja kwa kule anakolenga. Safari hii kaingiza na Arusha. Ukweli huu ni mchungu lakini lazima usemwe. Kuendelea kulinda uhuni ni kuliangamiza taifa. Taifa kwanza mtu baadaye

Mnavyozidi kuleta utetezi dhaifu ndivyo mnazidi kufungua 'pandora box'

Ukweli unabaki pale pale Kiongozi mkuu wa ACT( naambiwa nisutumie kiingereza) alilenga mikoa ya kaskazini katika kutaka kuwavuta wapiga kura ya kanda ya ziwa na kati

Hapo ndipo tunasema,tatizo la ACT si CCM
Si mpini tu bali pia ACT ni tatizo la umoja wa kitaifa, chimbuko la ukanda na kutaka kuleta siasa za ukabila
 
Kwamba Zitto analigawa taifa ni lugha itakayokuudhi,hata hivyo ndiyo lugha sahihi anayopaswa kuambiwa. Hatuwezi kusema analijenga taifa wakati ana dissect taifa vipande vipande, anaingiza chuki miongoni mwa wana jamii. Soma nyuzi zote zilizomhusisha Zitto na kauli zake, utaona jinsi watu wanavyotukanana kwa maneno machafu. Hiyo huoni kama tatizo, tatizo ni pale anapoitwa supreme.
Labda tutamwita kiongozi mkuu ingawa ukweli unabaki pale pale kwa kiingereza ni supreme leader.

Tunarudia tena, hatuwezi kuwa loyal kwa mtu, tunakuwa loyal kwa nchi.
Leo tunaambiwa anajenga ujamaa wa Mwalimu . Lini Nyerere alisimama na kuligawa taifa vipande vipande kama kiongozi mkuu.

Njia njema ya kumsaidia ni kumweleza ajitokeze, ima atoe ufafanuzi au aombe radhi. Hakuna short cut

Ni bora tukabaki wajinga tukisimamia ukweli, kuliko kuwa wajanja tukilisaliti taifa kwa sababu ya mtu au watu
 
Alinda , kuna swali la ziada

'' Mikoa iliyowezeshwa'

Tunauliza mikoa iliyowezeshwa ni ipi, imewezeshwaje na kwa rasilimali gani ukilinganisha na mikoa mingine
 
Last edited by a moderator:


Mkandara ninakuheshimu sana, sipendi kusingiziwa kitu ambacho sijafanya na sipendi kumsingizia binadamu mwenzangu kitu ambacho hajafanya.. Hivyo basi mimi sikuchomoa kitu chochote... Labda nijieleze kwa ufasaha na ni matumaini utanielewa..

Ni hivi, hicho nilichoquote nimekitoa kwa Adharusi, na hicho ndicho ZItto alichokuwa ameandika katika Facebook yake tarehe 5.4, Baada ya kuandika hivyo kulitokea mjadala mkali kwenye Facebook yake kuhusu hayo aliyoyandika, pia hiyo hoja ikaletwa humu JF kama alivyoileta Adharusi kutoka Facebook ya Zitto, humu mjadala ulikuwa mkali na katika kumbukumbu zangu na wewe ulikuwa miongoni mwa wachangiaji ukawa unasema ni kweli Shinyanga haipati stahiki yake.

Baada ya mjadala kuwa mkali, wa uchonganishi, wa matusi kwa wa wachaga (maana humu watu wamekalirishwa kuwa KLM/Arusha ni wachaga) ZItto alifuta hiyo "Shinyanga"/alifanya "Editing" na kusomeka kama inavyosomeka sasa.. Kwa kudhibitisha hilo unaweza kwenda katika wall ya Zitto na utakuta kinachojadiliwa hakiendani na mada husika.. Utakuta kuna "Shinyaga"lakini katika mada ya Zitto hakuna neno "Shinyanga"

Pia kumbuka wakati Zitto anafanya Editing za kisiri siri watu tulishaanza kujadili na kama nilisema hapo juu kuwa wewe ni miongoni mwa waliokuwa unajadili katika jukwaa la siasa huku ukisisitiza kuwa Shinyanga hawapati stahiki yao..

Sasa basi swali kwako ni kwanini ulisema Shinyanga hawapati stahiki yao? Kumbuka wewe ulikuwa active sana kuhusu hii mada si jukwaa la siasa si jukwaa hili hivi kweli wewe Mkandara ulijipinda kuandika kitu husichokuwa na uhakika nacho?

Hivi kweli tumefika stegi hii ya kuwa ukishindwa hoja huja na uongo uongo? Sisi humu ni watu wazima, tunashughuli zetu, tuna familia zetu ambazo zinatutegemea hivi kweli tumeshindwa kufanya kitu cha maana sisi na familia zetu mpaka tuanze kumsingiza Zitto? Uliwahi kusema kuwa ZItto na Mbowe unawafahamu ni marafiki zako/au watu wako wa karibu hebu wasiliana na Zitto muulize kama kilichoandikwa ni kweli ama si kweli!

Naomba siku nyingi kabla huajandika tuhuma kwa mtu jaribu kufanya utafiti kidogo ili kujua nani kasema nini, wapi na lini. Hivyo ndivyo nifanyavyo kabla sijaandika kitu basi ufanya uchunguzi kwanza maana sipendi kabisa kumsingizia mtu kitu ambacho hajafanya, na kitokea kwa bahati mbaya nimefanya hivyo basi uwa ni mwepesi wa kuomba msamaha na hivi ndivyo nilivyo lelewa na ndivyo inavyoilea familia yangu...
 
Last edited by a moderator:
Kwanza ninakuomba ufahamu tu ya kwamba niliyoandika hapo juu ilikuwa kielelezo cha malalamiko ya WATU ambayo hayatakiwi kupuuzwa na serikali wala wanasiasa kwa kuhofia Ukabila ikiwa kweli Ukabila umetumika. Hii ni katika kukuonyesha tu ya kwamba yapo maswala mwanasiasa hutakiwi kuyaepa kwa sababu unahofia watu watatafsiri vibaya. na kwa bahati mbaya wewe umeshanitafsir vibaya makusudi kwa sababu zako mwenyewe.

Ikiwa wananchi wanalalamika kuhusu Ukabila na wakataja kabila fulani hakuna kosa ikiwa kweli Ukabila umetumika kuajiri wafanyakazi. na hakuna ubaya kuzungumzia Upendelea mahala ambapo unaona umetumika maadam uwe na ushahidi wa kitendo hicho kutumiwa. Na nikatoa mfano kuwa TRA imelalamikiwa kuwa na Wachagga wengi, sio mtazamo wangu mimi isipokuwa nimeandika malalamiko ya wananchi na pia Nimetoa mfano wa Bima na Wanyakyusa.

Lakini wewe umechagua la Wachagga kuwa hoja ya msingi japo hii yote ni mifano ya malalamiko yalowahi kutokea. Hukuona tatizo katika mfano wa Wanyakyusa ukachukua wa Wachagga WHY? Halafu wewe umetoa mfano wa Mamlaka ya Pamba Mwanza kujaa Wasukuma na wala usitupe sifa za kuajiriwa kwao isipokuwa umetumia neno ni Watanzania kama sifa. Ili wewe ujue kuna wasukuma tu ina maana ulifikiria kwanza kabila lao na sii Watanzania kwa hiyo dukuduku ulikuwa nalo hizo sababu unazijenga baada ya. Hivyo hapa sikuelewi kabisa unachojaribu kujenga kama hoja yako maana ubaya wangu kusema Wachagga wakati wewe umeona kwa macho yako Wasukuma wengi Mamlaka ya Pamba!.

Na kuhusu Utoaji wa Ajira hata Ulaya kuna Racism, wapo watu walokosa ajira kwa sababu ni rangi zao ama asili yao. Ubaguzi ni Ubaguzi tu uwe kwa kabila, dini, jinsia, Nationality kwa sababu Ubaguzi upo duniani na ndio sababu ya kuupiga vita, huwezi kupiga vita kitu kisichokuwepo. Na hizo sifa unazozungumzia hata kama zipo kwa mwenye Ubaguzi hatazitazama ila sifa ya Kibaguzi ndio alotumia yeye.

Nadhani una tatizo sana na mtu kusema Wachagga, pengine nimefanya kosa ningetumia kabiila jingine lakini nilichoandika ni mambo yalokwisha tokea nchini ambayo yamedai Ukabila kutumika katika utoaji ajira. Na huwezi kutumia takwimu kuhalalisha Ukabila kwa sababu inaweza kuwa mtu mmoja tu ukamwezesha kwa sababu ya Ukabila au ukamtenga mtu mmoja tu kwa sababu ya Ukabila. Kwa hiyo tuelewane kwanza maana naona tunatoka nje ya mada kwa sababu nimeandika kitu kilichowahi kuzungumzwa imekuwa nongwa!.
 

Kufanya editing katika wall ya mtu, ni haki yake, Mara ngapi sisi watumiaji wa JF tumefanya editing katika hoja zetu tunazoposti hapa?. Kuna sababu nyingi za kufanya editing, mojawapo ni kuongezea nyama katika hoja yako ili ueleweke vizuri.

Nilitegemea mngekuwa na utu na uungwana kidogo, basi hoja zenu zingebase katika post ya Zitto iliyo latest.
Lakini ukiachilia wall ya Facebook, Zitto ameirudia hoja hii majukwaani, huku akifanya comparison ya mikoa mbalimbali. Lakini nyinyi hamtaki mnafanya cherrypicking ya kile mnachokipenda ili kumharibia taswira yake mbele ya umma.

Tena Zitto amekuwa muungwana sana katika wall yake ya Facebook, anatolerate mawazo ambayo ni kinzani kwako, ana uwezo wa kufuta comment zote ili kuficha motive yake, lakini kwa kuwa hana nia mbaya, basi anaziacha tu, ili iwe sehemu ya mjadala.

Hoja ya Zitto ipingwe kwa hoja mbadala, tusijifanye sisi ni akina kalumanzira, kujua yaliyomo katika moyo wa mtu.
 
Last edited by a moderator:

Mkandara umesema wachaga/wanyakyusa mie nikachagua wachaga kujenga hoja yangu.. kosa langu ni lipi?
Hivi tumefika hali hii ya kutaka kuchagulia hata cha kuongea? kweli? Kwamba katika hoja kama kuna wachaga na kabila lingine basi mtu harusiwi kutaja wachaga na kama akitaja ni kosa au ni lazima usema kwa nini wachaga?

Kuhsu wasukuma hebu nisome vizuri nilichoandika.."Nimesema maana ni wenzetu (Yaani watanzania wetu) na wameajiriwa kutoka na sifa zao. (Yaani sifa zilizokuwa zinatafutwa katika hizo nafasi ndizo ziliwabeba) sijui umenipata hapo?

Kuhusu Canada nimekuuliza na Canada wanauliza wewe ni mcanada wa Torroto au sijui ni wapi? kama unavyoshauri tufanye? au wanaajiri kutoka na sifa ya mtu alizonazo? (hapa ninamaanisha Mcanada awe ni mweusi/mweupe) na kama kuna ubaguzi je huo ubaguzi unakufurahisha? na kama haufurahii huo ukabila mbona unataka na sie tuajiri kwa minajiri ya ukabila?
 
Hapana Bibie sasa naona unanisingizia miye kwa sababu nilipoingia katika mada hii hapakuwepo na nukuu yoyote iwe ya FaceBook wala hapa JF isipokuwa tuliulizana HOTUBA ya Zitto Shinyanga kuwa alisema Kilimanjaro wanaidhulumu Shinyanga (kwa maneno yenu wenyewe). Mchambuzi akaja na takwimu za TRA kutuonyesha hakuna dhulma. Sasa unaposema mimi nasema uongo wakati sijaiona hiyo ya FaceBook humu unanitia wasiwasi kama kweli tupo pamoja ktk mjadala huu maana hata hili neno dhulma mmekuja nalo nyie wenyewe.

Nukuu ya Adharusi pekee niliyoiona mimi ni ile nilolinganisha na hotuba ya Zitto aloitoa Ritz na kusema hata yeye kachambua kutokana na mjadala maana aliongezea neno Zitto pia alisema... (Ina maana kuna third party hapa anayenukuu maneno ya Zitto According to na sio Zitto mwenyewe). Kwa maana ya kwamba kuna ongezeo la hotuba aloiacha nyuma. Hivyo hakuwa na mpangilio kama hotuba yenyewe. Hata baada ya kupata Hotuba kamili bado umeleta swali ambalo unajua kabisa umetoa maneno ya chini ukayaweka na Kilimanjaro na Arusha. Kwa hiyo pengine mimi ndiye nilikuwa najadili kitu tofauti kabisa maana nilikuwa katika hotuba yake Shinyanga na sii FB.

Kama Zitto aliandika hivyo FB mngeweka hapa nukuu ile tukaijadili hivyo maadam huna itakuwa vigumu kwangu mimi kujadili kitu ambacho sijakiona wala hakipo katika mada hii. Utanisamehe kama unaona nimekukosea lakini ukweli ni kwamba tunajadili tu yale tulokuwa nayo hapa na marekebisho yangu yametokana na mjdala huu sio wa FB.
 
Sikuchagulii isipokuwa wewe ndiye umeniuliza miye. kama utaniuliza mimi kwa ku limit jibu liwe kuhusu wachagga nina haki ya kuuliza maana swala hapa lilikuwa watu kuzungumzia Ukabila, ukachagua moja na kulishikilia hilo hilo kuonyesha bado kuna hisia za chuki za watu na wachaga wakati nilichosema miye ndio lugha alotumia Zitto. Nimetaja watu wanalalamikia Ukabila nikatoa mifano miwili wewe ukachomoa mmoja unaohusu wachaga na kuniuliza maswali, wakati huo huo wewe ukawasema Wasukuma kwa lugha ile ile na huoni kosa ndio maana nashangaa!

Haswa wanauliza kama wewe ni mkazi wa Ontario, Toronto na sehemu gani. Kuna kazi unaweza kuzikosa kwa sababu huna Usafiri, unakaa mbali, rangi, lugha, urefu na kadhalika kwao hizi zote ni sifa za kuajiriwa inategemea na kazi yenyewe. Zipo nafasi za kazi hutoka kwa ajili ya wanawake tu, walemavu tu, mashoga tu na hata weusi tu ili kuwawezesha kundi hilo la jamii baada ya kuachwa nyuma. Wenzetu wanatambua haya na huyafanyia kazi pasipo kuficha uchafu uvunguni..
 
Nguruvi3.

Hamna mtu aliyekimbia mimi nipo wewe kama Supreme Leader wa ili jukwaa umetoa tamko kwa wafuasi wako wanipuuze sasa hivi unasema tumekimbia wote daah!!!

Ngoja nirudi ukumbini!
 
Last edited by a moderator:


Kwanza hakuna kitu kinachoitwa Hotuba ya Zitto Shinyanga.. maana hayo aliyoleta Ritz hatufahamu aliyatoa wapi.. Zaidi ya kutwambia alimsikiliza yeye mwenyewe Mwanza..

Pili Kama wewe haukuona alichokuwa kaandika ZItto, na kwa bahati mbaya hatukuweza kukitoa Facebook na kukileta humu ndani haiondoi ukweli kuwa kilicholetwa na adharusi ndicho alichosema na ndicho kilisomwa na watu wengi na kuleta matusi kwa watu wa KLM/Arusha waliopata maendeleo yao kwa nguvu zao wenyewe.


tatu nafikiri hata wewe umeona kosa la Zitto ndo maana unajaribu kutuaminisha/kubadili mjadala kuwa "mnalisha/hakusema.. Na kama umeona hili basi unakubalina na hoja ya Nguvuri3 kuwa Zitto ni mchonganishi.

Na hata kwenye utetezi wenu sikuona mtu wa kumtoa Zitto katika tope aliloingia mwenyewe, zaidi ya mbona hata fulani alisema hivi... au sisi ni wabaguzi ndo maana umechomoa hiyo mikoa na. nk

NNe.. Ukweli ndio huo ukubali au ukatae lakni hicho ndicho alichoandika tarehe 5.4 Hakuna anayeongelea hotuba ya Shinyanga maana hakuna mwenye hotuba ya Shinyanga wala ya Tabora (zaidi ya kipande ambacho kinamuweka katika tope zaidi) na hakuna mwenye hotuba ya Mwanza....

Ushauri:Siku nyingine kabla hujaanza kuandika kitu chochote jaribu kufanya uchunguzi kufahamu kama unachojadili kinahusu nini, kimetoka wapi, na kimetoka kwa nani ni kweli humu mtu akisema hivi na nk.
 
Mkuu Mkandara.

Huyu Alinda anasema wamenza kumjadili Zitto toka tarehe 5 uongo kumbukumbu zipo humu kwenye huu uzi.

Post ya kwanza ya kujadili hotuba ya Zitto ameanza kuandika Nguruvi3 tarehe 19 leo hii wanatuambia walianza kudili twits za Zitto toka tarehe 5.

Alinda ebu tukumbushe hizi twits mlizoanza kujadili na Nguruvi3 zipo page ya ngapi.
 
Last edited by a moderator:


Haya basi hiyo si shida...
 
Mkuu Mkandara.

Hebu wasome watu wazima wapo radhi kusema uongo ili malengo yao yatimie.

Hapa Nguruvi3 na Alinda wanasema toka tarehe 5 walikuwa wanajadili kauli ya Zitto.

Teh teh teh
 
Last edited by a moderator:

Hivi kuna takwimu gani zinazoonyesha TRA kuna wachaga wengi kuliko makabila mengine? Pili kama hawa wanyakyusa wanasifa za kuajiriwa tatizo liko wapi? NI sekta gani hapa nchini unapokwenda ukakuta mlinganyo wa makabila? au dini? na kama kila sekta kuna watu wa kabila fulani wengi kuliko makabila mengine kwanini iwe BIMA tu? Nenda Mamlaka ya Pamba Mwanza kule ni wasukuma tupu tena hata mle ofisi lugha inayotumika ni kisukuma lakini hakuna mtu anayelalamika maana ni watanzani wenzetu, waliajiriwa kutoka na sifa zao si kabila yao sasa hapo tatizo ni nini?
Yaani unataka tufike wakati wa kuajiri tuangalie kabila la mtu si sifa za mtu? Hivi huko kwenye duani ya kwanza unapoishi ndivyo wanavyoajiri kwa kuangalia makabila (hivi wana makabila huko kweli) na kuwa kufanya hivi kweli Tanzania yetu inaweza kupiga hatua kwenda mbele?

(Nje ya topic) NImekuwa nikijiuliza hasa kuwa mchaga ni nani? ni yule mtu mwenye jina la kinyakyusa? au ni yule mtu alizaliwa Kagera na wazazi ambao ni wanyakyusa ila huyu mtu anafahamu kihaya, anaishi mila na desturi za kihaya, hajawahi kwenda unyakyusani zaidi ya kusikia simulizi? au ni yule aliyezaliwa unyakyusani, akajifunza mila na desturi za kinyakyusa, kaongea kinyakyusa ingawaje wazazi wake ni wahaya? Swali langu hapa Myakikyusa ni yupi?? (hili swali ni kwa kila mtu atakayependa kunipa ufafanuzi haliusiani na topiki iliyo mbele yetu)


Mkandara haya nimefuta wachaga na kuandika wanyakyusa kama ulivyotaka.. Je kuna kilichobadilika?

Naomba uonyeshe ungwana na ujibu maswali yangu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…