Nimesha wambieni kuwa hapa tunazungumzia UCHUMI, kila mkoa una mapungufu yake na kiongozi bora ni yule anayeyaona mafungufu hayo kwa ngazi zote. Hakuna mtu asoliona la Shinyanga kukosa maji mkoa mzima isipokuwa kwenye miradi ya dhahabu, leo hii 2015 mji wa Shinyanga bado hauna maji, huwezi sema hili ni tatizo la nchi nzima. Na kibaya zaidi ni pale Shinyanga inayochangia mfuko wa Taifa kwa kiasi kikubwa ndio mkoa hawana maji wakati tuna mikoa ina umeme hadi vijijini tokana na mipango ya maendeleo ya serikali kuu.Mkuu hanayebisha kuwa mfumo wetu ni mbovu, hilo liko wazi, tunachobisha/au ambacho hatuelewi je huu mfumo mbovu ni kwa ajili ya baadhi ya mikoa tu au ni Tanzania nzima?
Unasema haki ya Elimu ni ukweli uliowazi kuwa elimu yetu Tanzania nzima ni mbovu, Mtoto aliyemaliza darasa la saba Geita hana tofauti na mtoto aliyemaliza darasa la saba Mtwara au Afya hali ya hospital zetu sote zinazohudumiwa na serikali ni mbovu iwe ni DAr, iwe ni Mwanza.. Na hili ni wa ajiri ya viongozi wetu ambao wao hawatumii hizi huduma, watoto wao wako English medium, wakiugua wanapelekwa India hivyo basi ni vigumu kuona tatizo kama huko nje, utaona tatizo pale uwepo ndani ya tatizo na hapo ndipo utaweza kupata wazo ya kulitatua.
Hebu tuchukulie mfn mdogo tu wa elmu yetu ya darasa la saba, Baada ya miaka 7 ya mtoto kukaa shule, anafanyiwa mtihani, huu mtihani wa siku moja/au wa masaa 4 mpaka 8 unatosha kumuamulia maisha ya huyu mtoto, kwamba wewe umefeli hivyo utabaki nyumbani hivyo basi.. Na viongozi wetu wanaona ni jambo la kawaida kabisa mtoto mdogo mwenye miaka 13 mpk 15 kuhukumu maisha yake ya mbeleni kwa mtihani wa siku moja tu. Huyu mtoto hapewi nafasi nyingine ya kusema ngoja ajaribu tena au kama serikali kuweka utaratibu wa watoto wote ambao hawakuweza kupata maksi za kuendelea na masomo ya O level basi warudie masomo yao kwa uangalizi wa walimu maalum au hata kupelekwa shule za ufundi iwe kwa lazima au kwa hiyari hapana, huo ndio unakuwa mwisho wa safari yake. Halafu hawa hawa viongozi do wenyewe wa kwanza kuanza kuwakashfu hawa watu kuwa ni "wanywa viloba" Sasa unategemea nini unapomuacha mtoto wa miaka 13 ajiamulie maisha yake mwenyewe? Hizi ndizo akili za viongozi wetu.
Tuna waziri wa watoto na jinsia, tuna waziri wa elimu na msululu mrefu sasa sijui wakifika ofisini huwa wanafanya nini?
Hivyo basi tatizo si mikoa, tatizo si kupendelewa au vyovyote vile manvyofikiria, tatizo ni viongozi wasio na maono ya mbeleni.
Tukienda kwenye ile dhana ya mkoa unachangia sana ni lazima uwe na maendeleo, swli litakuja na ninafahamu hutaweza kulijibu nalo ni je ile mikoa ambayo uchangiaji wake ni mdogo si haki wao kuwa na maendeleo? Kwamba nini
Lindi iwe na maendeleo hali Shinyanga hawana? (nitafurahi sana kupata ufafanzi wako)
Ofcourse ni lazima Tanzani nzima tuwe na maendeleo, tutakuwa na maendeleo pale ambapo tutawapa watu elimu, Elimu ndo mama wa kila kitu bila Elimu hakuna maendeleo hata leo ukiamua kuchukua mgao wa Tanznia nzima nakuwapelekea wana Shinyanga kama hawana elimu watabaki hivyo hivyo. Ukiangalia mkoa wa Shinyanga una fursa si kwa madini peke yake bali hata kwa wafungaji, Tanzania kuna soko kubwa la maziwa ya Ngómbe na nyama au hata nchi za jirani tu kinachotakiwa ni watu wapewe Elimu ya ufugaji bora, wajifunze ujasiriamali,wajengewe barabara ili waweza kusafirisha bidhaa zao ndani ya miaka 5 Shinyanga utakuwa mkoa mwingine kabisa. (maana dhahabu wameishaamu kuwapa ndugu zako Wakanada)(husinipe za uso lakini:A S wink🙂
Kwa maana hiyo utaona hapa tatizo si mgao wa Kili au Arusha tatizo ni viongozi wetu ambao wanawaze miaka 5 ya ubunge na nafasi za upendeleo na baada ya hapo wao kwao ndo mwisho wa Tanzania, hawafahamu Tanzania itakuwa hata baada ya miaka 500 ijayo.
Nitoke nje ya mada:
Ushuhuda: Mimi si mkazi wa Dar, kuna kipindi nilikuja kikazi, basi jamaa yangu yuko maeneo ya Goba, yaani hali niliyokuta Dar ilikuwa ni kihama maana nilikuwa ninatoka nyumbani saa 12 asubuhi kurudi ni saa 5 usiku hali kazi ilikuwa inaisha saa 10 jioni (sasa sijui kama ni ugeni au la).
Ila kituko cha mwaka ni pale ndege ya kwenda Mwanza ilikuwa inaondoka saa 7mchana, tulitoka Goba saa 3 asubuhi (private car) tulifika Airport saa 5asubuhi mwenyeji wangu nilimwabia kuwa hana haja ya kusubiri anaweza kuondoka tu, basi akawa amenishusha na kurudi Goba, ndege yangu iliondoka Dar saa 7 ilikuwa inachukua masaa mawili hivyo tulifika Mwanza saa 9mchana, kutoa mizigo na kusalimiana na watu wa hapa na pale (Airporrt) nilifika nyumbani saa 10jioni. Sasa nimefika ninampiga mwenyeji wangu kuwambia nimefika salama cha "ajabu aliniambia yeye hajafika labda baada ya dkkama 20 ndo atakuwa nyumbani, nilimuuliza umepitia sehemu? alijibu ni foleni hajapita sehemu yeyote.. nikasema nini?
Niliwaza hivi hawa viongozi wetu wanawaza nini? kama kutoka Airport kwenda Goba mtu anatumia masaa 5 hali itakuwaje baada ya miaka 20 au 50? Ila cha ajabu hakuna viongozi anayeumizwa na swala la foleni. watu wanapoteza muda mwingi ambao ungetumika katika ujezi wa Taifa au katika familia zao katika foleni. Viongozi kimya.
Nimeandika ya hapo juu kukuonyesha kuwa tatizo letu kama nchi ni viongozi ambao wamechoka kufikria, ambao hawana mawazo mapya, hawana mikakati yoyote ya kututoa hapa na kutupeleka pale. Wanaongoza kwa mazoea tu, wanafikiri miaka 50 iliyopita si miaka 50 ijayo. SWali ni kama wameshindwa kutatua haya maswala madogo madogo je wataweza maswala makubwa? jibu kila mtu analo.
Tusitoane macho, umasikini wetu si wa ajili ya watu wa mkoa fulani bali ni kwa ajili ya viongozi wabovu waliochoka kufikiria, wanaofikiri matumbo yao na familia zao. Hebu angalieni wabunge wanalipwa mil230 kwa kazi gani waliyoifanya? hivi hizi mil 230 zingepelekwa katika majibu na kutengezea ajira kwa vijana wetu walau vijana 50 tu kila jimbo iwe ni kilimo, ufugaji. ufundi na nk je ndani ya miaka 50 tungekuwa wapi? Hayo mashangingi wanayokopeshwa wangekuwa wanakuposha wakulima matreta ndani ya miaka 5 Tanzania ingekuwa ni aina gani?
Hivyo basi tusitoane macho, matatizo ya mtu wa Geita hayasababishwi na mkoa wa Iringa.. Labda mtu atuletee hapa takwimu za kudhibitisha hivyo.
Alinda utanisamehe sana kaitka hili maana ni watu wa Kaskazini tu ndio wanapingana na hoja ya Zitto na sielewi kwa sababu gani, kama ushahidi ama madai yenu yangetolewa na watu wa mikoa mingine ningewasikiliza lakini kwa jinsi ilivyo inaonyesha watu wa Kaskazini hawataki kuambiwa ukweli. Ni mjadala wazi lakini binafsi yangu naona kama kuna ukweli msopenda uzungumzwe.
Hivyo maana mimi nimemwelewa Zitto na kwa bahati nzuri sana ni muumini wa UJAMAA pengine itakuwa bora sana kama nikisema Tanzania watu wote ni maskini! japo naelewa sio kweli maana kuna matajiri tena wa nguvu na serikali hii CCM ndio inyojenga madaraja wa watu walokuwa nacho na wasokuwa nacho! Sasa kina nani wasokuwa nacho hapo tena ukitaka ugonvi mwingine ukiwataja matajiri pasipo kuwasifia, hata viongozi wa CCM watasema nao ni maskini!. Ukisema kuna MAFISADI utaulizwa kina nani…..
Waswahili wanasema:- Kila mtu anataka kwenda peponi, lakini hakuna mtu anayetaka kufa! hiyo peponi utaipata vipi..
Last edited by a moderator: