Wanabodi,
Kwanza lazima kwanza tufahamu siasa ni kitu gani kisha ndio tujenge hoja zetu kwa maudhui (content) yanayolingana na siasa haswa tunapolijadili swala hili la Upinzani. Kwanza kabisa kuwepo kwa vyama vya Upinzani ni jambo jema sana maana sisi sote hatuwezi kufikiri sawa, hatuwezi kuwa na mahitaji sawa, mazingira tamaduni na kadhalika vyote hivi vinachangia katika tofauti zetu na vyote hivi huchangia utetea wa kisiasa katika kila tunachokiona kuwa ni haki na fursa ya wananchi katika ujenzi wa USAWA baina yao. Kwa hiyo kila mtu atautazama USAWA huo kutoka upande wake, kutoka kundi la kijamii yake wamepungukiwa nini ambacho wengine wanafaidika nacho ilihali wao ni jamii moja.
Chimbuko la kisiasa haswa limetokana na KUTETEA haki za watu wako kutokana na mfumo ama muundo wa kisheria unao wanyima haki na fursa zilizopo iwe ya kitamaduni, mila, desturi au mafao stahiki kutokana na mazingira wanayoishi kushiriki sawa na makundi mengine. Na imekuwa hivyo kwa miaka kiasi kwamba hata mbunge huwakilisha matakwa ya watu wake mbele ya mtazamo mpana wa Kitaifa. UTETEZI wa kundi la wanyonge kama mfano dhidi ya Udhalilishaji hata siku moja haiwezi kuwa ni Ubaguzi.
Na kutokana na tofauti hizi za kimazingira na tamaduni, rasilimali watu hujenga hisia za matabaka baina yao ambazo zinaweza kulijenga taifa ama kulibomoa ikiwa SIASA SAFI hazikutumika kuwa kigezo na mahala pa kufikiwa muafaka baina ya makundi haya ya kijamii ili kuunda UMOJA wa kudumu kwa kuzingatia yale yanayowaunganisha na sii yale yanayowatenganisha maana changamoto kubwa ya Utaifa ni USAWA baina ya wahusika katika mambo Yanayowaunganisha kwani hakuna Umoja wa kudumu unaoweza kupatikana kwa mambo yasowaunganisha maana hayana maslahi ya pamoja.
Sasa leo hii tukipuuza usawa tukajenga hoja ambazo zinapuuza ukweli wa kisiasa kwa sababu tu leo tunaishi kwa mazoea ambayo hayana USAWA, ali mradi kila mmoja kulinda fursa na haki walonazo kwa makusudi kabisa huu huitwa UJINGA kwa maana ya IGNORANCE. Wakoloni na Makaburu walikuwa na Ujinga (Ignorance) kwa sababu hawakutaka kujielimisha katika usawa walitetea fursa zao kwa hoja zinazopinga Usawa wa binadamu hautokani na haki ama fursa sawa kwa wote bali nani anastahili haki na fursa hizo ka vigezo vyao. Hata tawala wa Kiimla na kidikteta zilitumia UJINGA huo kutotazama USAWA wa binadamu kama kigezo kikubwa cha kujenga UMOJA wa KITAIFA.
Hivyo basi kutokana na Ujinga (ignorance) ndivyo harakati za fikra pevu za mageuzi hutokea, vyama vya UPINZANI (RESISTANCE) vikajitokea kutetea HAKI na FURSA hizo katka mazingira na nafasi zile zile zilizokandamizwa na UJINGA. Kwa hiyo vyama vya Upinzani asili yake ni kutokubaliana na hali iliyopo ya Utawala unaowanyima wananchi haki na fursa sawa kwa wote - As they say resistance is to refuse to comply with something..
Kwa karne za zamani, Upinzani waliingia msituni kwa sababu haikuwa HAKI wala halali kupingana na Utawala na matokeo yake upinzani ukawa wa siri na kujificha misituni. Upinzani ukazua vita na mauaji ya pande mbili zilizopingana kutetea kile kile walochukuwa wakiamini ni halali ya kila upande. Sasa Ujio wa vyama vya Upinzani kisasa ni ujenzi mpya wa vita baina ya jamii badala ya kuingia msituni na kupigana mapanga, ikawekwa sheria ya Upinzani kupitia mabaraza yetu na sheria zikatungwa kwa kuzingatia mazungumzo (dialogue) baina ya makundi yanayotofautiana kiitikadi (utetezi wa haki na fursa) kwa njia ya AMANI pasipo kupigana vita ama kujenga chuki baina yaa..
Kifupi nachotaka kusema hapa, Kila mwanasiasa ni lazima kwanza atetee watu wake, jamii yake kwa kusimamia haki na fursa zilizopo pale ambapo usawa umepotoshwa. Viongozi wote wa Kimataifa na wengine wameitwa mashujaa ni kwa sababu walianza na kutetea watu wao, kisha kupanua wigo zaidi kwa kadri na jinsi jamii hiyo inavyokubaliana. Hao Kina Abraham Lincorn, John MacDonald, Churchill, Mkwawa, Marealle, Nyerere, Nkrumah, Mandela hadi viongozi wa leo kina Harper, Cameron, Obama wanaweza tu kuitwa viongozi bora ikiwa wameweza kwanza kuwatetea USAWA wa haki na fursa kwa makundi yote yaloijenga JAMII hiyo kuwa Taifa moja.
Sasa huwezi sema leo ati kwa sababu Mandela alipingana na Utawala wa makaburu ambao dhahiri watu weupe walipendelewa basi ni mchonganishi kwa sababu ati aliwataja wazungu dhidi ya weusi akiwa yeye mweusi. Huwei sema Nyerere alikuwa mbaguzi kwa sababu alipingana na Wakoloni walotawala nchi za Afrika kwa sababu wazungu ama waarabu pia walizaliwa Afrika. hapa tutakuwa tunapotosha content kwa makusudi kwa sababu kinachogombaniwa ni mfumo ama muundo unaowakandamiza wengine kwa kutumia vigezo hivyo hivyo.
UJINGA ni pale hao Wakoloni, Makaburu na Waarabu walipokataa na kutetea nafasi zao ya kwamba kulikuwepo USAWA baina yao na weusi wakijenga hoja zinazowabagua wanyonge na kustahili haki na fursa walozopewa kwa sababu ya asili yao. Hata siku moja mtu anayelia kwa UNYONGE hawezi kuwa yeye mbaguzi bali mbaguzi ni yule mwenye nguvu na uwezo wa kushinikiza kuendelea kuwakandamizi ama kupinga matakwa ya wengine katika kuwapa nafasi sawa katika haki na fursa.
Hivyo napowasikia watu wa kaskazini wakiendelea kutetea Ubora wao na kwamba wao ni zaidi isipokuwa hawa kina Zitto wanaopigania fursa na haki sawa kwa mikoa mingine ndio wabaguzi inanishangaza sana na najitahidi sana kuwasoma hawa watu wanaojivunia na kutetea MIKOA yao, wakitumia jina la makabila yao kama wanatengwa kwa sababu wana mafanikio zaidi ili waendelee kufaidika na muundo wa kiutawala uliopo inanipa sura na picha wa wazungu wabaguzi naoishi nao kila siku hapa nilipo. Well anyway sitowalaumu sana maana siasa pia ni kutetea U Mangimeza!
Ebu msome huyu jamaa hapa:-
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Ukristo walijenga makanisa na shule.Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupatafedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1, 2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote.
Ni vema pia kusema kUwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu.
Inanishangaza..