Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Nimesha wambieni kuwa hapa tunazungumzia UCHUMI, kila mkoa una mapungufu yake na kiongozi bora ni yule anayeyaona mafungufu hayo kwa ngazi zote. Hakuna mtu asoliona la Shinyanga kukosa maji mkoa mzima isipokuwa kwenye miradi ya dhahabu, leo hii 2015 mji wa Shinyanga bado hauna maji, huwezi sema hili ni tatizo la nchi nzima. Na kibaya zaidi ni pale Shinyanga inayochangia mfuko wa Taifa kwa kiasi kikubwa ndio mkoa hawana maji wakati tuna mikoa ina umeme hadi vijijini tokana na mipango ya maendeleo ya serikali kuu.
Alinda utanisamehe sana kaitka hili maana ni watu wa Kaskazini tu ndio wanapingana na hoja ya Zitto na sielewi kwa sababu gani, kama ushahidi ama madai yenu yangetolewa na watu wa mikoa mingine ningewasikiliza lakini kwa jinsi ilivyo inaonyesha watu wa Kaskazini hawataki kuambiwa ukweli. Ni mjadala wazi lakini binafsi yangu naona kama kuna ukweli msopenda uzungumzwe.

Hivyo maana mimi nimemwelewa Zitto na kwa bahati nzuri sana ni muumini wa UJAMAA pengine itakuwa bora sana kama nikisema Tanzania watu wote ni maskini! japo naelewa sio kweli maana kuna matajiri tena wa nguvu na serikali hii CCM ndio inyojenga madaraja wa watu walokuwa nacho na wasokuwa nacho! Sasa kina nani wasokuwa nacho hapo tena ukitaka ugonvi mwingine ukiwataja matajiri pasipo kuwasifia, hata viongozi wa CCM watasema nao ni maskini!. Ukisema kuna MAFISADI utaulizwa kina nani…..

Waswahili wanasema:- Kila mtu anataka kwenda peponi, lakini hakuna mtu anayetaka kufa! hiyo peponi utaipata vipi..
 
Last edited by a moderator:

Sasa labda nikuulize swali, Ukosefu wa maji mkoani Shinyanga unashababishweje na mikoa mingine?

Na je ni watu gani wa Kaskazini wanaopingana na Zitto? Hapa tupate ufafanuzi kidogo maana mambo ya mafumbo mafumbo huwa naona ni umbeya tu.. Sema fulani na fulani ambaye anatoke Kaskazini anapingana na Zitto?
 
Alinda , kama kawaida, wanachomeka hisia zao. La watu wakaskazini ni kutuondoa katika mjadala.
Na mbele ya safari utasikia mengine! wanajaribu kuchomeka tunawajua

Ukisoma hoja za Mkandara, inasikitisha,nyuzi zote zilizohusiana na kauli za kiongozi mkuu amechangia! kasahau kuwa mjadala mzito uliozua hisia kali za ukabila katika jamii umeendelea kutokana na kauli hatarishi za kiongozi mkubwa


Mkandara, Kiongozi mkuu yupo katika rekodi akisema ' Tusiogope EAC kwababu kuna tofauti ya maendeleo kati ya Kigoma na Kilimanjaro'' Leo tukiangalia takwimu zao wenyewe K'njaro haipo katika top 6.

Ni wazi kauli ile aliitoa wakati ule tukampa benefit of doubt, leo tukiangalia nyuma hakuna shaka kauli ile ni mwendeleo wa anayosema sasa. Tumeondoa benefit of doubt na sasa yupo on spot! tunammulika kwasababu mbegu anayopanda ni hatari na ni mbaya sana

Kauli ya kuchangia na maendeleo hawaelezi inawiana vipi. Adharusi nimemuuliza kidogo sana kakimbia anasubiri wiki inayokuja kurudi na tuhuma. Mkandara atufafanulie tusioelewa, uhusiano wa kuchangia pato na maendeleo.

Ukimsikiliza Kiongozi mkuu, aliitaja mikoa ya K'njaro na Arusha mwanzoni. Ukiangalia takwimu zake, mikoa hiyo haipo katika orodha ya juu. Hivi kwanini asiseme Dar ipo juu kwa maendeleo, ameenda kutoa kauli ya jumla mikoa miwili ipo juu bila kuonyesha nafasi zake.

Na mwendelezo huo huo ndio sasa anautumia kushambulia Singida na Iringa kama midomo mirefuuu.

Hakuna shaka chuki yake ni dhidi ya mikoa fulani. Hilo halihitaji degree lipo wazi kila mtu anayetumia akili analiona.

Na wala hakuna tatizo kama atakuwa na chuki na maeneo asiyotaka.

Tatizo ni pale anapotumbukiza mbegu za eneo fulani kuonewa na eneo jingine.
Hilo ndilo lililipelekea mauaji ya Kimbari Rwanda, anapaswa kuyajua na si Kinyume chake

Marekani wakipoingia Iraq, walitamka, ni muda sasa serikali itakayoundwa iwashirikishe Shia walionewa na Sunni (Saddam)
Walifanya hivyo waungwe mkono bila kujua wanatumbukiza mbegu ya chuki.

Leo Marekani ana wakati mgumu wa kuleta maridhiano na nchi imevurugika kwa sectarian war.

Ndiyo hatari anayopanda huyu mtu, kwa kusema maendeleo ya sehemu mojani matokeo hasi au chanya ya eneo jingine.

Kuendelea kutetea upuuzi(Ignorance) wa aina hii ni kuleta madhara makubwa sana katika taifa

Kama Shinyanga haina maji, Arusha inahusika vipi na tatizo hilo?

Na kama kuchangia kunakwenda sambamba na maendeleo, basi Kigoma itakuwa wapi?

Halafu wanaotumbukiza mbegu za chuki wanarudi na kutamba tumejenga barabara.
Sasa akina Mkandara watueleze kama kuchangia unastahili kupewa zaidi, Singida, Kigoma watakuwa hali gani?

Halafu hawajiulizi kwanini Lindi yenye maendeleo kwa mujibu wao, ipo juu ya Shinyanga na ipo chini katika uchangiaji.
Je mfano mzuri ulikuwa upi, huu wa Lindi au ule wa kuendelea kombo mikoa ya kaskazini.

Kisiasa hatuna tatizo , anaweza kuamua maeneo ya kufanya siasa zake.

Kitaifa kuna tatizo, huyu mtu anayechomeka ubaguzi na hisia zisizo na ukweli na mbegu chafu ya ukabila hataishia hapo.
Akimaliza ukanda na ukabila, atarukia agenda nyingine. Tusipomkemea ataua taifa

Tumkemee ili tuwe salama. Nchi zilizokumbwa na matatizo hazikuanza siku moja.

Tuliona Serbia na Bozinia. Mbegu zikipandwa ka mfano huu huu tunaouona. Zikachanua na kisha kutoa matunda

Leo tunaambiwe 'shut up and dance' taifa likiselelea katika siasa za hatari. Jamani tukemee
 
Nani alosema unasababishwa na mikoa mingine ama nyie ndivyo mlivyotafsiri hotuba ya Zitto..

Nakuomba itafute hotuba Obama leo hii katka azishi ya yule mchugaji SC halafu nambie wewe umeelewaje..

NB: Upo msemo mujini:- Watu wa Kaskazini = Wafuasi wa CDM...
 
Mimi nafikiri Nguruv na Mwenzie Alinda wameshaelewa, Tukisema watu wa Shinyanga tunazungumzia Watanzania, na Ikisemwa watu wa Arusha inazungumzia Watanzania..Wote wana haki sawa na Stahili zao mbele ya Serikali na kwa mujibu wa hoja ya Zitto Stahili hiyo inabidi ibase katika uchangiaji katika pato la Taifa.
Wenye hoja wanaipinga hoja ya Zitto kwa hoja mbadala. Wasio na hoja wanamlisha maneno Zitto eti anaibagua mikoa ya Kaskazini. Huu ni mtizamo usio sahihi, na kulishana maneno.

Sijaona mahali katika kauli ya Zitto akizungumzia kuwa Kabila fulani limenyimwa haki, Au kabila fulani limependelewa, Hicho kitu hakipo.

Leo hii Watanzania wanaishi sehemu zote za nchi hii, Kwa hiyo Serikali ikipanga mipango mibovu katika sehemu fulani, wanaoathirika ni Watanzania wote!

Alinda na Nguruv, Msitake kuyapa maneno ya Zitto Tafsiri yenu mnayoipenda wenyewe!
 

Nani alosema unasababishwa na mikoa mingine ama nyie ndivyo mlivyotafsiri hotuba ya Zitto..

Labda tupe maana ya haya maneno`:

"Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa, mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.


Ukimaliza tufafanulie hapa ulimanisha nini?


Husisahau na hapa:

Hayo si maneno yetu ni maneno yako wewe.Sasa tueleze ukosefu wa maji Shinyanga unasababishwaje na mikoa mingine?


Nakuomba itafute hotuba Obama leo hii katka azishi ya yule mchugaji SC halafu nambie wewe umeelewaje..

Hatuongelei siasa za Obama na US tunaongelea siasa za Tanzania na Zitto. Hivyo sioni umuhimu wa hotuba ya Obama.

NB: Upo msemo mujini:- Watu wa Kaskazini = Wafuasi wa CDM...

Kwahiyo na wewe unaamini kuwa Chadema ni chama cha Kaskazini na watetezi wote wa Chadema ni wakaskazini, na wale wanaomkosoa Zitto ni watu wa Kaskazini?

Sasa nikuulize swali uliwahi kusema kuwa Zitto alikuwa rafiki yako katika Facebook, na baada ya kumkosa alikutoa katika marafiki zake wa Facebook. Je wakati unamkosoa ulikuwa mkaskazini?

Kwa mantiki ile ile ya "Msemo wa mjini" tuamini ACT ni chama cha Waha na wewe unamtetea Zitto kwa vile wewe ni Mha? na kama sivyo unapata wapi ujasiri wa kuongea hizi pumba? (sorry kwa hilo neno lakini sina neno lingine zaidi ya pumba)
 
Tunatumia hoja zenu wenyewe kukuonyesha wapi tatizo lilipo.

Soma Hayo ni maneno ya Zitto mwenyewe kutoka kwa mashabiki wake.

Tueleze kulikuwa na sababu zipi za kuzungumzia uchangiaji wa pato la taifa

Kulikuwa na sababu zipi za kuongelea maendeleo ya taifa vs uchangiaji wa pato la taifa

Tueleze nafasi ya Kilimanjaro, Arusha katika maendeleo ni ipi, zaidi ya kusema kwa ujumla 'maendeleo zaidi''

Tunakusubiri


Halafu kumbuka
Kiongozi mkuu alishawahi kusema 'Tusiogope EAC kwasababu tofauti ya maendeleo ipo nchini kati ya Kigoma na Kilimanjaro''
Soma vizuri kauli hiyo, huo ndio ulikuwa mwanzo wa shambulio kuelekea kaskazini. Ndio alikuwa katika spring board na sasa tunaona

Unapounganisha na kauli zake za sasa, unawezaje kutushawishi kuwa hana Inda na kinyongo na wananchi wa mikoa hiyo!!!!

Hakuongelea utaifa, alivchokuwa anakifanya ni kutafuta namna ya kutumbukiza hisia. Ukisoma jukwaa la siasa vijana wametutakana kama hawana akili nzuri. Utadhani ni Wacamerom na Wana Nigeria.

Ni kauli tu za mtu mmoja ambaye angeweza kutoka na kuweka sawa.
Alikaa kimya! Je, hakuna sababu za kuamini kuwa ilikuwa makusudi?

Halafu silkilza video ya kiongozi mkuu '' Kuna dhambi mtu wa Kigoma kuwa mwenyekiti wa chama""
Hivi hii kauli inachembe ya Utanzania kweli! Kwamba sasa tunachagua viongozi kimikoa.

Hivi kuna mtanzania kweli anaweza kusema hayo! I mean mtanzania mwenye uchungu na nchi hii, anaweza kusema hayo!

Wengine tunapata taabu sana kuamini kama wote ni wazawa na wazalendo wa nchi hii.
Kama hatuwezi kukemea mambo rahisi yanayobomoa taifa kama haya kuna shaka.

Wahutu na Watusi walianza hivi hivi! anajua zaidi. Inashangaza hamuoni hatari hiyo.

Tunaweza ku import mitumba ya nguo na magari, hili la hatari na umoja wa nchi, hapana! ni letu sote tusimame pamoja

Tusikubali ku import matatizo, hapana! tuwaambie hatukubali
 
Pamoja na utetezi hafifu wa wafuasi wa Supreme Leader, nafikiri ujumbe umefika na nina hakika mlengwa hatarudia tena kutoa kauli ya kichochezi kama hiyo alioitoa akiwa Shinyanga. Ambalo halikunishangaza ni kwamba watu wale wale ambao kwa makusudi wanaituhumu Chadema kwa Ukabila/Ukanda ndio hao hao wanatetea kauli za kibaguzi za Supreme Leader. Nachukua nafasi hii kuwashukuru wote mliosimama kidete kulaani hiyo kauli na naomba hata siku moja tusiwafumbie macho watu wanaotaka kutugawa Watanzania kiimani, kikanda na kikabila. Tanzania bila unafiki na undumilakuwili inawezekana, Tanzania bila CCM inawezekana na Tanzania bila wasaliti wa mabadiliko inawezekana.
 
 
Wewe mtetezi wa nani wa Criminal Mbowe?
 
Hawa watu Alinda na Nguruv wanachekesha kweli, Kauli ya Adharus kuhusu aliyoyasema Zitto WANAIKUBALI Lakini Kauli ya Ritz kuhusu aliyoyasema Zitto WANAIKATAA!

Tukiwauliza basi na nyinyi Leteni Ya Kwenu kwa Kadri mlivyomsikia Zitto Mwenyewe Akizungumza kuhusu hiyo Mikoa ya Shinyanga, Arusha, Dar es salaam HAWANA

NGOJA NIMUULIZE NGURUV, JE NI KWA NINI UNADHANI KAULI YA ADHARUS NI NUKUU HALISI YA ALIYOYASEMA ZITTO, LAKINI NUKUU YA RITZ SIYO NUKUU HALISI YA ALIYOYASEMA ZITTO, NAOMBA NA USHAHIDI WA MAJIBU YAKO
 






Ukiwa muongo husiwe msahaulifu. Hayo ni maneno yako mwenyewe.
 




Ukiwa muongo husiwe msahaulifu. Hayo ni maneno yako mwenyewe.
Sasa ulichokisema umetaka kuonyesha nini ya kwamba pale nimeandika Watu wa mikoa mingine wangesema! CDM inajulikana ngome yake ipo Kasikazini na ndivyo ilivyo licha ya hivyo nimesema sijui sababu ya kuwaita watu wa kaskazini maana uliuliza baada ya mimi kulitumia neno hilo ukataka kujua maana yake haswa ukisema ni fumbo, sasa umekuja na tafsiri yako mwenyewe kumbe tayari ulikuwa na tafsiri yako.

Hata hao CUF tunajua ngome yake ipo Zanzibar hivyo wakiitwa Wazanzibar kwa maana ya wafuasi wa CUF.. Inaeleweka kwetu tunaotaka kuzungumza kwa lugha hiyo, wala haina maana hakuna wana CUF bara. Ni siasa mlizochagua wenyewe kuzifuata baada ya kujinasibisha na Ukabila/Ukanda hivyo sisi wengine tumejitoa katika kundi hilo maana tunajua ndicho kinachoimaliza Chadema. Kiwalacho kii nguoni mwao!
 

Hayo si maneno ya Adharusi ni maneno ya Zitto aliyoandika katika ukurasa wake wa Facebook tarehe 5.April.

Lakni sikushangai mtu mzima kama wewe unapokuja kukana kitu ulichoandika wewe mwenyewe tena hata kabla ya wino haujakauta.
Na uzuri ni kuwa hata nyie umnahitisha kwa hoja ile ile kuwa huu ni ubaguzi mnaona kitu kile kile tuonacho sie, ila mnajiriwadha wa kupindisha ukweli kuwa hayo maneno yamekotka kwetu. Nafikiri huu ni ujumbe kwa boss wenu kuwa alichoongea hata nyie wafuasi wake hamna hoja ya kupingana na sie labda mnachoweza ni kupindisha uongo uwe ukweli na kwa hili hamatafaikiwa. Maana maandishi yalikuwa facebook, watu walisoma, watu walimpiga wazi wazi.

.

Nimekwambia unipe maana ya hiyo paraghaf:Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa, mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.

Hayo mengine ni bla bla tu.


Ala wewe vipi lakini?...Kila siku unataka sana kunichangulia maneno ya kuandika, kwa nini lakini? una tabia gani mbovu ya kuamrisha watu wazima waseme nini wanapoongea na wewe kama vile sisi ni watoto wadogo au unaongea na mwanao hapa.


Huu upuuzi huwa sijibu hizi ni ligi za akina "laki si pesa" mie nilishatoka huko. pole


[
Hatuongelei Zitto kufukuzwa au la tunachoongelea ni kauli za Zitto: Je uchangiaji wa pato la taifa unahusikaje na maendeleo katika mikoa husika? Na je ni kweli wakati wanakigoma wanapigwa mabomu kwa kuchangua vyama vya upinzani mikoa ya Iringa, Arusha na Singida walikuwa wanakumbatia watawala? Hayo ni maswali niliyokuuliza zaidi ya mara 7 ila mpaka sasa wewe ni maelezo marefuuuuu za Mbowe na Zitto au ya Chadema na Zitto.

.

Alaa mara hii umesahau ulichosema? Nanukuu "NB: Upo msemo mujini:- Watu wa Kaskazini = Wafuasi wa CDM..."
Jaribu kuwa na aibu basi unaandika kitu na kukikana?

..

Husipindishe maneno wewe ni mtu mzima soma kwa makini nilichoandika.. Nimeuliza swali baada ya wewe kuandika hivi:
NB: Upo msemo mujini:- Watu wa Kaskazini = Wafuasi wa CDM..."

Na mie nikakuuliza hivi:
Kwahiyo na wewe unaamini kuwa Chadema ni chama cha Kaskazini na watetezi wote wa Chadema ni wakaskazini, na wale wanaomkosoa Zitto ni watu wa Kaskazini?

Sasa nikuulize swali uliwahi kusema kuwa Zitto alikuwa rafiki yako katika Facebook, na baada ya kumkosa alikutoa katika marafiki zake wa Facebook. Je wakati unamkosoa ulikuwa mkaskazini?

Kwa mantiki ile ile ya "Msemo wa mjini" tuamini ACT ni chama cha Waha na wewe unamtetea Zitto kwa vile wewe ni Mha? na kama sivyo unapata wapi ujasiri wa kuongea hizi pumba? (sorry kwa hilo neno lakini sina neno lingine zaidi ya pumba)

Sasa niambie ni wapi niliposema ACT ni chama cha Waha??? Acha siasa za uongo uongo, jenga hoja bila kumtungia mtu kitu ambacho hajasema. Ni kweli uliowazi kuwa wewe huwa unapenda siasa za ubaguzi na kwa hili tumekuwa tukikupuuzia. ni wewe uliyechomeka Wachaga na TRA, ni wewe uliyechomeka Chadema na wachaga, ni wewe uliyechomeka wanyakyusa na (sijui na shirika gani la umma hata sikumbuki maana kwangu ulikuwa ni upuuzi) Unaposhindwa hoja ujaribu hoja za kibaguzi..



Upuuzi sijibu.
 

""utanisamehe sana kaitka hili maana ni watu wa Kaskazini tu ndio wanapingana na hoja ya Zitto na sielewi kwa sababu gani, kama ushahidi ama madai yenu yangetolewa na watu wa mikoa mingine ningewasikiliza lakini kwa jinsi ilivyo inaonyesha watu wa Kaskakazini hawataki kuambiwa ukweli. Ni mjadala wazi lakini binafsi yangu naona kama kuna ukweli msopenda uzungumzwe.
Aliyeandika haya ni wewe si watu wengine.

Nilipokuuliza unamaana gani wa watu wa kaskazini wanaopinga na Zitto nawe ulisema:

NB: Upo msemo mujini:- Watu wa Kaskazini = Wafuasi wa CDM...?

Kwenye blue unazidi kulikoroga.. Ila kwa vile mie si shabiki wa siasa za kugawa watu..ngoja nipuuzie huo ujinga uloandika hapo.
 
Alinda,
Kama ni upuuzi hata miye nimeuona wako tokazamani lakini niliendelea kukujibu kwa hiyo bota tukomee hapa..
 
Mimi nafikiri Nguruv na Mwenzie Alinda wameshaelewa, Tukisema watu wa Shinyanga tunazungumzia Watanzania, na Ikisemwa watu wa Arusha inazungumzia Watanzania
..

Mkambiwa someni kabla ya kujadili hamtaki, bila kusoma na kuelewa kinachoongelewa kwa kweli mnatia aibu. maana mnapinga na sisi wakati mnaongea kitu kile kile ambacho tumeongea tangu pg.no. 15. Hakuna aliyeongea mambo ya kabila fulani, labda upande wa pili wa akina mkandara.

Wote wana haki sawa na Stahili zao mbele ya Serikali na kwa mujibu wa hoja ya Zitto Stahili hiyo inabidi ibase katika uchangiaji katika pato la Taifa. !


Kwenye msitari mmoja kuna maneno yanayopingana. Hapo kwenye nyekundu ndo hoja yetu ya msingi. na kwenye blue hivi ukianza kutoa stahiki kwa vigezo vya uchangiaji wa pato la taifa huoni kuwa kutajenga matabaka katika taifa moja? maana hapa kutakuta mikoa ya Dar, Mwanza Kil na nk ndo yenye maendeleo zaidi na mikoa kama Kigoma, Lindi na nk ni masikini wa kutupwa? Na je ikitokea mtu wa Shinyanga akakuuilza kwanini watu wa Kagera wajengewe barabara hali wanachangia kiasi kidogo katika pato la taifa na sisi tunaochangia sana hatuna umeme utawajibu je?

Wenye hoja wanaipinga hoja ya Zitto kwa hoja mbadala. Wasio na hoja wanamlisha maneno Zitto eti anaibagua mikoa ya Kaskazini. Huu ni mtizamo usio sahihi, na kulishana maneno.!

Hoja ya mbadala ni ipi? maana wanao pinga sijaona mtu yeyote aliyekuja na hoja badala ile bla bla za Chadema walifanya kakosa kumfukuza Zitto..


Haya tumeyaongelea sana huko nyuma


QUOTE=Gamba la Nyoka;13116459]Alinda na Nguruv, Msitake kuyapa maneno ya Zitto Tafsiri yenu mnayoipenda wenyewe![/QUOTE]


"Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa, mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.
 


Hii ndo nukuu halisi kutoka katika facebook ya Zitto ya tarehe 5. April. Na hiki ndo tunachojadili.

"Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa, mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.
 
Alinda,
Kama ni upuuzi hata miye nimeuona wako tokazamani lakini niliendelea kukujibu kwa hiyo bota tukomee hapa..

Na huu ndo ungwana.. Kuliko kuongopa mchana kweupe na kukana andishi lako bora kukaa kimya...
 
Mkuu wangu huu mpini ni hatari hawautaki hata kuusikia upitie tena kiduchu.

Zitto.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.


Wamehamia Facebook sasa hivi ndiyo wanajadili halafu hawataki kabisa watu wengine waongee habari zingine lakini wao ruksa kuja na habari za Goba.

Halafu ni marufuku kumsema vibaya Criminal Mbowe lakini Zitto ruksa kumsema upendavyo.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…