Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)





hapo hakuna hisia ni mwendo wa Fact tu..
Je hilo bandiko liko Facebook au halipo?

Je umesoma hapo juu kuna Kilmanajaro au haipo? Kama haipo je wachangiaji wanaoitaja Kili wameitoa wapi? na umemsoma Zitto mwenyewe alirudisha alichokuwa amenyofoa lakini kwa namna nyingine? (na hii ni baada ya wachangiaji kupoteza muelekeo) hiyo ni tarehe 5.4 hata kabla ya Nguvuri3 hajaleta uchambuzi wake humu.

Sasa basi kuchukua hayo maandishi ya juu, unganisha na maandishi ya Zitto aliyonyofoa na kuyarudisha, unganisha hayo maneno.. Sema ni wapi nimeongeza hata neno moja?? twende taratibu si kwa kukashifiana..
 
Nguruvi3, naona wafanya maskhala kwa sababu unapenda sana kubadilisha hoja za watu ama hukuelewa toka mwanzo na ndio maana wewe hurudisha hoja zilizopita kwa sababu toka mwanzo hukumsoma mtu ukamuelewa ama unafikiri tunasahau hoja zetu hutokana na hoja ilotangulia. Mjadala maana yake ni kutafuta nguvu ya hoja na ndio maana Hoja hujibiwa kwa Hoja.. hivyo huwezi chomoa jibu la hoja pasipo kutanguliza swali la mjadakla ulokuwepo wakati ule.

Hotuba ya Zitto kama alivyoiweka Ritz imetokana na utafiti wa report ya HDI ya Tanzania ambayo mkuu Adharusi alitangulia kutufahamisha wakati tukirumbana. Mimi na wewe tulikuwa hatufahamu Zitto kapata wapi ushahidi wa maneno aloyahutubia, tukadhani pengine ni Total reveune ya kila mkoa kama alivyotueleza Mchambuzi akitumia revenues report ya TRA akithibitisha kwamba Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa ukichangia zaidi ya Shinyanga.

Sasa kwa mwenye kuutafuta ukweli tungejiuliza WHY? why sisi tunatafuta kujua ni mkoa gani unachangia zaidi ya mwingine ikiwa sisi hatuamini katika Ukabila ama Ukanda? hatuamini katika haki ya mkoa kuchangia zaidi wanastahili mgao zaidi pia..Hadi mkatafuta kuthibitisha Kilimanjaro ilichangia zaidi ya Shinyanga? why go through all that kama hamkuamini katika hayo..Na kwa nini tulianza kuamini Mkoa wa Kilimanjaro ulichangia zaidi ya Shinyanga na kuanza kusema sababu gani Shinyanga kuwa chini? wengine wakisema Mkoa wa Shinyanga ni wavivu hawachangamkii fursa zilizopo, hawajitumi ama kushughulisha kama wana Kilimanjaro!.
Haya yote hayakuwa na Ukabila isipokuwa maelezo ya Zitto na kwamba ni wivu tu unamsumbua Zitto mliyasema haya na kadhalika.. haya oyte niliyasoma humu lakini nikayapuuza maana sikutaka kutoka nje ya mada tukaanza mkupishana ila nikasema Ukabila tunaso sisi wenyewe kwa kufikiria na kutetea mikoa yetu wakati hakuna baya lilozungumzwa.

Na Adharusi alipokuja na Ushahidi wa hotuba ya Zitto kuwa imetokana na report ya HDI ambayo inaonyesha Kilimanjaro inachangia kidogo kuliko Shinyanga (GDP) mkaanza kugeuka tena na kusoma maelezo ya mwandishi Adharusi kutafuta makosa katika hotuba hiyo ndio mkajenga hoja kwa nini Zitto kasema Hata hivyo Kilimanjaro inachangia blaa blaa blaa mkipindisha makusudi maandishi ya Adharusi yalotangulia na neno PIA ALISEMA, hii ikiwa na maana Adharusi anaelezea kile anachokumbuka pasipo mtiririko wa hotuba yenyewe ambayo Ritz kaiweka na imeonyesha alichosema Zitto ni Mkoa wa Lindi anaochangia kidogo kuliko Shinyanga.

Kilichozidi kutushangaza sisi ni kwamba Zitto hakulinganisha mkoa wa Shinyanga na Kilimanjaro isipokuwa alilinganisha Mkoa wa Shinaynga na Lindi. Sasa kama kweli nyie mngekuwa na uchungu sana wa Ukabila mngezungumzia ya mkoa wa Lindi na Shinyanga lakini wapi bado swala ni kuitaja mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wakati Zitto kaitaja mikoa zaidi ya 10. Iweje mnyofoe mikoa miwili tu ya Kilimanjaro na Arusha kujengea hoja yenu dhidi ya Zitto?.

Kwa hiyo kama unadhani Kapwela kadandia Treni basi nimetoa habari nzima kwa kifupi chake tu ili mjue sisi tumesimama wapi na nadhani kwa jinsi mnavyoitetea mikoa hiyo imetupa wasiwasi mkubwa juu ya Msimamo wa Chadema nayo imechukua ule mchezo wa CUF kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010. Na fikra hizi ndizo zimetuogopesha wengi wetu juu ya mwelekeo wa CDM baada ya uchaguzi wa mwaka 2010..

Maanake ni maelezo yenu wenyewe katika kujishtukia pindi jina likitajwa. Ni sawa na maisha ya Uswazi, mtu akisikia pembeni jina lake limetajwa - Aaaaah nani Nguruvi? - basi unaanza kununa ukidhania watu wanakusema vibaya.. Huwezi kusemwa vibaya ikiwa wewe mwenyewe unajitambua una tabia nzuri ila yule anayefikiria anasemwa vibaya ni kwa sababu anajua he is not a good person!.

Kwa hiyo mkiitwa wa Kaskazini mnachukia lakini haya majibu na utetezi wa kanda hata kabla hamjaulizwa. Hofu ya mtu anapoitaja mikoa hiyo ni tabia ile ila ambayo CDM wanapenda sana kuzungungumzia viongozi wa vyama vingine lakini usikosee ukamsema Dr.Slaa au Mbowe. Ni kosa kubwa na Usaliti kwani hawa watu ni manabii au Miungu? na Kilimanjaro a Arusha ni Peponi huku kwingine kote ni Jahanam japo zote zipo mbinguni.
 



Hiki kitu umekitoa wapi? Nimeingia katika facebook ya Zitto ya tarehe 5.4 hakuna kitu kama hiki. hebu twambie hii post umeitoa wapi. Lakini sishangai nilitemea kitu kama hiki kutoka kwako maana wewe kwa kuspinning hauna mfn.
 


JIhoji mwenyewe kama bado una credibility hiyo.

Great thinker anajadili hoja,miezi miwili.

Msingi ya hoja yake ni facebook page, vipande alivyovichagua yeye,anasimamia hivyo vipande miezi miwili, alafu eti macho yake yana makengeza sana kiasi kwamba vipande vingine vinavyokamilisha taarifa hiyo hakuviona,miezi miwili, credibility!



Inakera sana
 
Sasa Alinda na wewe unatuchanganya, wewe unasema kwenye facebook hapo awali alisema hivi

Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa, mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.

HALAFU BAADAE UNATWAMBIA KUWA ALISEMA HVI:
Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.
Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.
Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu

HIVI ALINDA KWA MACHO YA KAWAIDA UNATAKA KUTUAMBIA KUWA MABANDIKO HAYO MAWILI NI SAWA?, Huoni ommissions zozote katika bandiko la kwanza ukicompare na la pili?
 

Jihoji mwenyewe

 

Hakipo facebook?

Wewe ulikipata wapi kama hakipo facebook?

Kwa kuwa japo source ya hoja yako ni facebook nimeamua kukuunganishia taarifa nzima ya ripoti hiyo kwenye page ya Zitto.
 
Hakipo facebook?

Wewe ulikipata wapi kama hakipo facebook?

Kwa kuwa japo source ya hoja yako ni facebook nimeamua kukuunganishia taarifa nzima ya ripoti hiyo kwenye page ya Zitto.

Nimekuuliza ulicholeta umekitoa wapi?
 

Hacha hizo dana dana basi.. Nimesome hapo juu...
 
Jihoji mwenyewe

Hayo si majibu ya maswali yangu, Ni ukweli kuwa hawezi kuyajibu maana yanakutia hatiani.. mnadzidi kujiacha uchi pale mnapojaribu kumtetea kwa mabandiko yenu ya kuunga unga. Kama hutaki kujibu soma basi michango ya watu.. Sisi tumenyofoa je na hao wamenyofoa? si umemuona Zitto akirudisha kipande alichonyofoa??


nimekuuliza hivi.. hapo hakuna hisia ni mwendo wa Fact tu..
Je hilo bandiko liko Facebook au halipo?

Je umesoma hapo juu kuna Kilmanajaro au haipo? Kama haipo je wachangiaji wanaoitaja Kili wameitoa wapi? na umemsoma Zitto mwenyewe alirudisha alichokuwa amenyofoa lakini kwa namna nyingine? (na hii ni baada ya wachangiaji kupoteza muelekeo) hiyo ni tarehe 5.4 hata kabla ya Nguvuri3 hajaleta uchambuzi wake humu.

Sasa basi kuchukua hayo maandishi ya juu, unganisha na maandishi ya Zitto aliyonyofoa na kuyarudisha, unganisha hayo maneno.. Sema ni wapi nimeongeza hata neno moja?? twende taratibu si kwa kukashifiana..
 
Hakipo facebook?

Wewe ulikipata wapi kama hakipo facebook?

Kwa kuwa japo source ya hoja yako ni facebook nimeamua kukuunganishia taarifa nzima ya ripoti hiyo kwenye page ya Zitto.

Ulicholeta hakipo Facebook....Umeleta vitu vya kungaunga kukidhi matakwa yako. Na kudhihisha ilo bandiko langu kutoka Facebook pg yake linakutia hatiani..

Muulize na Adharusi bandiko lake amelitoa wapi? ingaweje naye aliedit...
 
Last edited by a moderator:


Ulichotuletea humu ndani umekitoa wapi?? ndilo swali la msingi.. Kwa nini hukuleta hivyo vipande vipande kama vilivyo? unaongopa nini kuleta vipande vipande? Wakati anaweka hivyo vipande vipande mbona hakuwambia wachangiaji wasubiri kwanza watachángia akimaliza?
 

Hakipo facebook?

Wewe ulikipata wapi kama hakipo facebook?

Kwa kuwa japo source ya hoja yako ni facebook nimeamua kukuunganishia taarifa nzima ya ripoti hiyo kwenye page ya Zitto.

Ulicholeta sijakiona Facebook labda kama ukiambia umeuga uga kukidhi matakwa yako. Kama ungekuwa muungawana ungeleta hivyo vipande vipande kama vilivyo.. Lakini huwezi fanya hivyo maana vinakutia aibu.
Hebu tujifanye kuwa mimi nilichoandika ni uongo kama unavyotaka kutuaminisha.. sasa na huyu naye kachomoa mikoa? na maelezo yangu yake yanapishana?
 
Hiki kitu umekitoa wapi? Nimeingia katika facebook ya Zitto ya tarehe 5.4 hakuna kitu kama hiki. hebu twambie hii post umeitoa wapi. Lakini sishangai nilitemea kitu kama hiki kutoka kwako maana wewe kwa kuspinning hauna mfn.
Ulicholeta hakipo Facebook....Umeleta vitu vya kungaunga kukidhi matakwa yako. Na kudhihisha ilo bandiko langu kutoka Facebook pg yake linakutia hatiani..

Nimekuuliza ulicholeta umekitoa wapi?


Sasa unasema source yako ni facebook na facebook page yenyewe hujaisoma sasa ulikuwa na moral authority gani ya kujadili miezi miwili yote hii?maana vitu vyote hivyo vipo kwenye page hiyohiyo.

WEWE ULICHOFANYA UMECHUKUA NUSU YA KIPANDE CHA KWANZA NA KIPANDE CHA NNE, vipande vingine HUJAVIONA, propaganda!

Kumbuka wakati wote hili sio jukwaa la propaganda.

Kwa sababu hutaki kwenda kujisomea basi narudia kukurahisishia kazi:
.................................................................................................................................................................
Zitto Kabwe

April 5 · Dar es Salam, Tanzania


Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu

Zitto Kabwe
April 5 · Dar es Salam, Tanzania ·
Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.

Zitto Kabwe
April 5 · Dar es Salam, Tanzania ·

Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.

Zitto Kabwe
April 5 · Dar es Salam, Tanzania ·
Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.

Zitto Kabwe

April 5 · Dar es Salam, Tanzania ·
Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.

Zitto Kabwe
April 5 · Dar es Salam, Tanzania ·
Mikoa 9 nchini ina idadi ya watu zaidi ya 2m. Dar, Mbeya, Tanga, Morogoro, Mwanza, Tabora, Kagera, Dodoma and Kigoma. Mikoa hii ina 52% ya Watanzania wote

Zitto Kabwe
April 6 · Dar es Salam, Tanzania ·
Wakati Dar inachangia 16.93% ya katika Pato la Taifa, inaongoza kwa makusanyo ya kodi ambapo inachangia 81% ya Mapato yote ya Serikali. Kwa makusanyo ya Kodi mkoa wa pili ni Arusha na wa tatu ni Tanga.

Zitto Kabwe
April 6 · Dar es Salam, Tanzania ·
Dar, Arusha, Tanga, Mwanza na Kilimanjaro huchangia 90% ya mapato yote ya Serikali nchini

Shinyanga inaendelea kushangaza sana. Wakati inashika nafasi ya nne kuchangia Pato la Taifa (6% of Tanzania GDP), inashika moja ya nafasi ya chini kabisa kuchangia Mapato ya Serikali ( 0.46% of total tax ). Unajua sababu? Shughuli nyingi za kiuchumi za Shinyanga hufanyika Shinyanga lakini kodi zake zakusanywa Dar es Salaam. Mfano migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, kodi zake zinalipwa Dar es Salaam

Zitto Kabwe
April 6 · Dar es Salam, Tanzania ·
Mkoa wa Njombe ndio unaongoza kwa kuwa na watu wengi virusi vya ukimwi. 15.4% ya watu wa Njombe wenye umri kati ya 14 - 49 wanaishi na virusi vya ukimwi. Mkoa unaofuata ni Iringa wenye 10.9% ya watu wake kuwa na virusi vya ukimwi.

Zitto Kabwe
April 6 · Dar es Salam, Tanzania ·
Dodoma, Manyara na Tanga ndio mikoa yenye watu wachache zaidi wanaoishi na virusi vya ukimwi

Zitto Kabwe
April 6 · Dar es Salam, Tanzania ·
koa wa Simiyu ndio mkoa wenye watu wachache zaidi wenye elimu ya sekondari ambapo 3.7% ya watu wa Simiyu wenye umri wa zaidi ya miaka 25 wana elimu ya sekondari. Dar es Salaam ndio mkoa wenye watu wengi zaidi wenye elimu ya Sekondari, 29%

Zitto Kabwe
April 6 · Dar es Salam, Tanzania ·
Katika kodi zote zinazokusanywa Dar es Salaam, 75% zinatokana na forodha, 16% kodi ya mapato na 9% kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Dar inachangia 81% ya makusanyo yote ya kodi nchini. Hii inaonyesha kuwa Watanzania wengi sana hawalipi kodi. Utegemezi kwenye forodha ni hatari sana kwa uhai wa nchi yeyote.

Zitto Kabwe
April 7 · Dar es Salam, Tanzania ·
" there appears to be a disconnect between economic growth on the one hand and human development on the other" Tanzania Human Development Report 2014

Zitto Kabwe
April 7 · Dar es Salam, Tanzania ·
Takwimu zote ninazoweka hapa toka jana zinatoka katika Tanzania Human Development Report 2014. Taarifa imesheheni kwa kweli

Zitto Kabwe
April 7 · Dar es Salam, Tanzania ·
Tofauti ya Kipato miongoni mwa wananchi (Inequality) ni jambo linalokosekana kabisa kwenye uchambuzi wa Taarifa ya Maendeleo ya Watu ( THDR 2014). Ninadhani moja ya hatari kubwa nchini ni kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Sifa ya sasa ya uchumi wa Tanzania ni 'kufaidisha wachache na kufukarisha wengi'
.................................................................................................................................................................

TEMBELEA HIYO PAGE KAJISOMEE MWENYEWE
 
Ndiyo maana Nguruvi3 hataki haya mambo ya Facebook.

Teh teh teh
 
Last edited by a moderator:
Danadana zipi?, wewe umetuletea mabandiko mawili tofauti ya Facebook halafu unataka kutufanya tuamini kuwa yanafanana?

Nimekwambia soma badiko langu hapo juu kutoka facebook ya Zitto na jibu maswali yangu.. Na uniambie utofauti ni ni nami nitatoa maelezo.. Ila nawe ujibu maswali yangu. Maana wewe ni mkwepaji maswali mzuri.. rejea swali la "Stahiki"
 

Sasa hapa tutaelewana.. Hoja ni kujua ukweli si kukashifiana..


Katika hilo bandiko lako la kwanza ambalo (blue) Zitto kaliedit.. wasome wachangiaji wanataja Kilimanjaro je katika hilo Bandiko kuna neno Kilmanjaro?

Msome tena Zitto akirejesha hiyo Kilimanjaro.. Naomba kwa hisani yako leta mchango ya wachangiaji katika hilo bandiko la kwanza (maana mie sina utaalamu wa mambo haya)

Katika bandiko hili hapo mwenye blue..

Pia si umeona Zitto naye kachangia hapo umesoma kama kuna sehemu amesema watu wasubiri kwanza mpaka amalize report nzima?

NB: Kwa sasa ninatoka hivyo nitarudi baadaye sana au kesho...
 
Sasa hapa tutaelewana.. Hoja ni kujua ukweli si kukashifiana..


.. wasome wachangiaji wanataja Kilimanjaro je katika hilo Bandiko kuna neno Kilmanjaro?

Msome tena Zitto akirejesha hiyo Kilimanjaro.

Kilimanjaro imetajwa tarehe 05/04 na ndio siku hiyo hizo comment ulizozileta zilipotolewa,refer chini


Sasa Alinda kama tayari ulimsoma Zitto akiwaambia watu wasubiri amalize report nzima,miezi yote hii miwili hukwenda kusoma ili uwe na uhakika na kile unachojadili humu?mpaka leo unamjibu Barubaru ulikuwa kama hujaiona hiyo report Zitto aliyosema uisubiri, na Zitto kamalizia tarehe 7/04/,miezi miwili iliyopita.

Michango ya watu sio hoja maana tunajua watu wanaweza kutafsiri vitu tofauti kwa namna tofauti cha msingi ambacho ndio hoja ya hapa ni kwani Zitto alisemaje?je Zitto aliingiza ubaguzi?je Zitto alisema mikoa fulani inapendelewa?je alisema kuna mikoa inanyonywa?je alisema mgawanyo wa mapato ni kigezo pekee cha maendeleo?utagundua sio kweli.

KUna michango mizuri juu ya maendeleo na uchumi imetolewa humu,ni mizuri,lakini watu kwa kuwa walikuwa hawajapewa taarifa sahihi walikuwa wanajadili juu ya USAHIHI wa ZITTO au KUKOSEA KWAKE wakati hakuna kitu kama hicho,nakumbuka kuna watu mpaka wakawa wanaeleza jinsi KIlimanjaro na ARusha wanavyolipa kodi kubwa, unajiuliza kama source ni Zitto kwani Zitto alisemaje juu ya hilo?miezi miwili iliyopita.Huu ni mfano mmojawapo,kuna maeneo mengi ya aina hiyo.Hii yote ni kwa sababu msingi wa mjadala ulikuwa PROPAGANDA CHAFU.

Nadhani hii hoja inahitaji kuisha sasa.

Ni vizuri Alinda na Nguruvi mkubali tu kuwa HAIKUWA HOJA YA KWELI.Kuna mambo mengi bado tunaweza kujadili kuhusu ACT ama Zitto, tusimame kwenye UKWELI na SIO UONGO WALA PROPAGANDA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…