Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Alinda,

Nafikiri ujaelewa swali hapo ( au labda nikuandikie kwa my mother language Kiarabu labda utanielewa ...joke.)

Kifupi hayo ulioandika hapo juu ni maneno ya ZZK?
Na kama ya ZZK aliyatoa wapi? utupe reference yako?

Hilo ndilo uliloulizwa na si lingine. Kwani kuna tuhumu Lukuki mnazozitoa zinazomuhusisha ZZK kuwa ni mbaguzi na mchochezi kwa kutoa kauli hizo. sasa kinachohitajika ni ile connection baina ya maneno hayo na tamko la ZZK.

Pole sana

Barubaru umemuuliza swali la Muhimu sana huyu mwanadada Alinda, Je hayo maneno ni ya ZZK?

Kimsingi hayo ni maneno ya Adharus akielezea jinsi ZZK alivyosema, Lakini hata hivyo imeshabainika kuwa siyo Kauli ya ZZK neno kwa neno, bali inashabihiana tu.

Ndiyo maana tukasema, wamejenga hoja based on Kuambiwa, na Predetermined motive yao ni ya kudistort ujumbe wa Zitto.

Na hii ndiyo maana wanafanya cherry picking ili supposedly kauli halisi ya ZZK waifanyie Spinning!
 
..sasa kwanini wewe hutuletei kauli ya Zitto neno kwa neno?

..lakini hata ukiileta ukumbuke kwamba tayari kuna mchangiaji ameleta data za TRA ambazo zinakubalika kama rejea sahihi ya mchango wa kila mkoa ktk "keki ya taifa."

cc Mkandara, Mchambuzi, Nguruvi3, Alinda
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hapa hatuzungumzii Revenues hizi ni fedha za serikali (Taxes) sio Jumla ya pato la taifa (GDP). Kwa hiyo tulikosea toka mwanzo kudhania Zitto alitumua mapato ya kodi za seeikali kwa sababu tuliletewa taarifa nusu nusu. Sasa kwa kumsoma zaidi imegundulika wazi kwamba ni report ya HDI kuhusu Tanzania ndio chanzo cha yeye kuzungumzia swala la Umaskini nchini na mfumo mbovu wake mbovu. Maana huwezi kuanza vita ya Umaskini pasipo kuelewa changamoto zake itakuwa unabuni tu..

Ndio maana nikasema mahala fulani ya kwamba nikisema huko nyuma ya kwamba Ikiwa wewe unastahili mshahara zaidi kutokana na ufanyaji kazi yako, haina maana ninataka wafanyakazi wengine wapunguziwe mshahara yao ili ulipwe wewe bali kuonmyesha tofauti baina ya ko na wengine. Lengo sio kuleta uhasama baina ya wafanyakazi bali ni hoja ya wewe kuwa mfanyakazi bora na unayestahili mshahara mzuri zaidi, ndicho Zitto alichokuwa akizungumzia - Watu hamtaki kuelewa..
 
Najiuliza sana, Kiongozi mkuu wa chama cha ACT'wazalendo'. Msemaji mkuu wa chama, aliyejinasibu kuwa ataendesha siasa za kisasa kabisa huku akitumia njia zote za mitandao kukutangaza chama; inakuwaje hotuba zake za kukitanganza chama kwa watanzania zinakuwa adimu namna hii? Na pale zipopatikana zinakuwa zimefupishwa, zimekatwa katwa katwa? Nikweli amejitahidi (S.L) kutumia mitandao mpaka inasemekana ana Google app inayotoa habari zake (app hiyo sijaitembelea).
Kinacho nishangaza ni kwa nini Watetezi wa S.L kutokutoa ushirikiano wowote wa kuziweka wazi hotuba za S.L mtu muhimu katika siasa za ACT!!

Je. Haya yote yanatokana na Watetezi wake kukiri kimya kimya kuwa ACT ni mpini wa CCM kuumaliza upinzani na kwa namna nyingine kuwa kauli za S. L kweli zinalenga kuua umoja wa watanzania? Labda anayesemwa ni Msemaji wa ACT (sina hakika kama ni hapa JF ama sehemu nyingine) Mkuu Kapwela anaweza kutupa maelezo ya kutosha juu ya haya mambo yanayo randaranda kichwani mwangu juu ya Watetezi wa SL, SL mwenyewe, na ACT kwa ujumla.
 
Kilimanjaro imetajwa tarehe 05/04 na ndio siku hiyo hizo comment ulizozileta zilipotolewa,refer chini

Sasa Alinda kama tayari ulimsoma Zitto akiwaambia watu wasubiri amalize report nzima,miezi yote hii miwili hukwenda kusoma ili uwe na uhakika na kile unachojadili humu?mpaka leo unamjibu Barubaru ulikuwa kama hujaiona hiyo report Zitto aliyosema uisubiri, na Zitto kamalizia tarehe 7/04/,miezi miwili iliyopita.

Michango ya watu sio hoja maana tunajua watu wanaweza kutafsiri vitu tofauti kwa namna tofauti cha msingi ambacho ndio hoja ya hapa ni kwani Zitto alisemaje?je Zitto aliingiza ubaguzi?je Zitto alisema mikoa fulani inapendelewa?je alisema kuna mikoa inanyonywa?je alisema mgawanyo wa mapato ni kigezo pekee cha maendeleo?utagundua sio kweli.

KUna michango mizuri juu ya maendeleo na uchumi imetolewa humu,ni mizuri,lakini watu kwa kuwa walikuwa hawajapewa taarifa sahihi walikuwa wanajadili juu ya USAHIHI wa ZITTO au KUKOSEA KWAKE wakati hakuna kitu kama hicho,nakumbuka kuna watu mpaka wakawa wanaeleza jinsi KIlimanjaro na ARusha wanavyolipa kodi kubwa, unajiuliza kama source ni Zitto kwani Zitto alisemaje juu ya hilo?miezi miwili iliyopita.Huu ni mfano mmojawapo,kuna maeneo mengi ya aina hiyo.Hii yote ni kwa sababu msingi wa mjadala ulikuwa PROPAGANDA CHAFU.

Nadhani hii hoja inahitaji kuisha sasa.

Ni vizuri Alinda na Nguruvi mkubali tu kuwa HAIKUWA HOJA YA KWELI.Kuna mambo mengi bado tunaweza kujadili kuhusu ACT ama Zitto, tusimame kwenye UKWELI na SIO UONGO WALA PROPAGANDA.

Ni wapi Zitto kasema watu wasubiri amalizie report? Nionyeshe hili andishi..
 
Najiuliza sana, Kiongozi mkuu wa chama cha ACT'wazalendo'. Msemaji mkuu wa chama, aliyejinasibu kuwa ataendesha siasa za kisasa kabisa huku akitumia njia zote za mitandao kukutangaza chama; inakuwaje hotuba zake za kukitanganza chama kwa watanzania zinakuwa adimu namna hii? Na pale zipopatikana zinakuwa zimefupishwa, zimekatwa katwa katwa? Nikweli amejitahidi (S.L) kutumia mitandao mpaka inasemekana ana Google app inayotoa habari zake (app hiyo sijaitembelea).
Kinacho nishangaza ni kwa nini Watetezi wa S.L kutokutoa ushirikiano wowote wa kuziweka wazi hotuba za S.L mtu muhimu katika siasa za ACT!!

Je. Haya yote yanatokana na Watetezi wake kukiri kimya kimya kuwa ACT ni mpini wa CCM kuumaliza upinzani na kwa namna nyingine kuwa kauli za S. L kweli zinalenga kuua umoja wa watanzania? Labda anayesemwa ni Msemaji wa ACT (sina hakika kama ni hapa JF ama sehemu nyingine) Mkuu Kapwela anaweza kutupa maelezo ya kutosha juu ya haya mambo yanayo randaranda kichwani mwangu juu ya Watetezi wa SL, SL mwenyewe, na ACT kwa ujumla.

Hizi huwezi kuzipata maana zinamuaacha uchi.. Mwambie alete hotuba ya Shinyanga, Tabora na Kigoma.
 
Ritz, Gamba la Nyoka, Waberoya, Mkandara, Kapwela, Adharusi:

Mnawekeza sana katika kutuondoa kwenye hoja ya msingi, huku mkitamani sana tufunike kombe mwanaharamu apite. Hilo tutalikataa kwa nguvu zote. Bila ya kujalisha zitto alitoa hotuba wapi na lini, bado hoja yake ya msingi imejaa upotoshaji na uchonganishi.

Siku za nyuma, niliwahi kujadili kwamba kuangalia kila mkoa (kwa kigezo cha GDP) na mchango wa mkoa husika katika GDP ya Taifa kama kigezo cha kupima au kufafanisha kiwango cha maendeleo ya mkoa mmoja dhidi ya mkoa mwingine approach ambayo ipo ‘flawed’.
Badala yake nikjadili kwamba kigezo ambacho kinakaribiana na uhalisia wa mambo ni tax revenues. Wapo waliopinga, kwa mfano akina Mkandara kwa hoja kwamba GDP ndio kipimo sahihi zaidi. Lakini kama kawaida yao, hawakufafanua msimamo wao huo, zaidi ya kuendeleza mtazamo wa “zidumu fikra sahihi za Zitto Kabwe”.

Swali langu kwenu:

Kati ya “Government Income” (Taxes) na “National Income” (Market Value of Goods and Services Produced in an economy i.e GDP):
· Ipi inapima juhudi za maendeleo kwa vitendo zaidi? Mkandara na wenzake wanaendelea kusisitiza kwamba ni GDP. Tukiuliza Kwanini? Jibu ni kwamba Zitto kasema.
·
Nilijadili kwamba, kwa upande mmoja, PATO LA TAIFA (GDP) ni jumla ya thamani (thamani ya soko) ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa ndani ya uchumi husika. Na kwamba kwa upande mwingine, KODI ni Pato la Serikali kwa maana ya kwamba this is an income earned by the STATE. Umuhimu wa Pato is for the state to finance public expenditure kama zile ambazo mkandara anasema kwa sasa zimegeuzwa kuwa fursa badala ya haki (mfano Elimu, Afya n.k), pamoja na kugharamia masuala mengine yanayohusiana na mahitaji ya umma. The state doesn’t fund development projects via GDP!

Tofauti kubwa baina ya Tax Revenues and National Income:
1. Taxes are mandatory payments, ruled by law, lakini GDP isn’t directly ruled by law. Kwa mfano, usipozalisha vya kutosha katika shughuli zako za kiuchumi kama kilimo, ufugaji, uvuvi, hakuna Sheria inayokubana, lakini usipolipa kodi, ni kosa kisheria.
2. Taxes (by default) are the best expression of the common efforts or collective efforts of the community. Hii ni tofauti na GDP. Hakuna collective effort. Ilikuwa hivyo wakati wa vijiji wa ujamaa, na hata hivyo it didn’t work. Otherwise kwenye suala la taxes, sense of community or collectivity applies globally. Dhana hii inaendana na hoja aliyotoa Nguruvi3 awali juu ya ‘utaifa’ linapokuja suala la kutafuta maendeleo. Swali kewnu, Je:

· Mnakumbuka “Kodi ya Maendeleo”? Kwanini maendeleo yalihusishwa moja kwa moja na kodi na (sio GDP)?

Pengine Mjamaa Mkandara anaweza kutusaidia na majibu,
Ningepende niweke msisitizo hapa kwamba Zitto ni mbabaishaji na mpotoshaji kwa sababu kati ya GDP na Tax Revenues, its tax revenues that explains more directly on why there’s an income difference baina ya mkoa mmoja na mwingine. Nitafafanua:

Unlike GDP, taxation is the most effective way of financing the costs of all public goods. By public goods, maana yake ni kwamba – goods ambazo consumption (matumizi) yake yanapofanywa na mtu mmoja haipunguzi matumizi ya wengine lakini pia. Pia ni vigumu kuzuia watu wasitumie such public goods, hata kama hawajalipia. Mfano ni taa za barabarani n.k. Funds kwa ajili ya such goods zina uhusiano wa moja kwa moja na Government Income (Tax Revenues) kuliko National Income (GDP). Kwa maana hii, Zitto anaposema kwamba kuna maeneo ambayo yapo nyuma kwa sababu ya poor public services or infrastructure, anajisahau kwamba ni kwa sababu ya mapungufu kwenye Tax system na sio National Income Statistics.

Kama tulivyokwisha ona, tofauti na suala la GDP/Pato la Taifa - (yani uzalishaji wa goods and services), taxes are mandatory payments, constrained BY LAW. Kitakwimu tunaona zipo jamii kadhaa nchini ambazo hazifanyi uzalishaji wa kutosha kwa sababu mbalimbali, lakini bado maisha yao yanaendelea na hakuna anayewabugudhi au kuwaambia kwamba wanavunja sharia. Wananchi hawa wanaishia kuitwa tu wavivu, wazembe, economically challenged etc, na hakuna sheria zinazowabana. Lakini linapokuja suala la Pato la Serikali (kodi), takwimu zinatuonyesha kwamba kuna jamii ambazo zinajituma na kuchangia sana kwenye mapato ya serikali, na maendeleo ya taifa kwa ujumla, na juhudi hizi zipo constrained by LAW. Kuna masuala mengine matatu ambayo ni muhimu kuyatazama kufikia hatua hii:

Kwanza - Kodi hukusanywa kutoka kwenye jamii nzima, na main inspiration katika hili ni vitu vikuu vitatu:

· Justice.
· Efficiency.
· Effectiveness.

Again, tukitazama in practice, tunaona kwamba zipo jamii ambazo zinalipa kodi kubwa kuliko jamii nyingine, pamoja na kwamba ulipaji wa kodi ni kwa mujibu wa sheria. Je is there justice katika hili? Kwanini Zitto asijadili suala hili muhimu badala ya kutumia muda wake kuchonganisha wananchi? Kama kweli Zitto ana lengo la kuangalia viwango vya maendeleo katika jamii mbalimbali kwa maslahi ya taifa, basi anatakiwa aangalie vitu hivi vitatu kwa pamoja namely – justice, efficiency & effectiveness.

Suala la pili ni kwamba – tofauti na GDP, Kodi inaweza kutumika katika malengo mapana ya kupunguza tofauti ndani ya jamii (social and economic inequality). Swali kwa zitto na wapambe wake, je:
· Kati ya Taxes & GDP, which one is the most effective tool of curbing or reducing “income inequality”? Kwanini mchumi mahiri Zitto haoni hilo? Kwanini wafuasi wake mnashindwa kuhoji au kuona ukweli? Kwenu, kila anachosema Zitto ni “Kweli Tupu”, sisi tukipinga kwa hoja na mantiki ambazo zinaangalia utaifa kwanza, badala ya kujibu kwa hoja, mnatupatia majibu yaliyojaa matusi na shutuma kwamba tuna wivu dhidi ya supreme leader.
Suala la tatu ni kwamba – kiuchumi, GDP dynamics ni major determinant ya mapato ya kodi. Kwa mfano, GDP ikiwa kubwa, basi Mapato ya Kodi nayo yanatakiwa kuwa makubwa, na GDP ikiwa ndogo, na mapato ya Kodi pia yanatakiwa kuwa madogo. Swali – je, hivyo ndivyo hali ilivyo nchini? Haya ndio mambo ambayo Zitto anatakiwa ajadili, sio kwenda kupotosha umma na kuchonganisha watanzania. Nitajitahidi kujadili:

Ili taifa liweze kuendelea kiuchumi, Tax revenues must grow at a much faster rate than GDP. Swali – je, hivyo ndivyo hali ilivyo nchini? Kwanini tunaachia wanasiasa wetu waendelee kutudanganya huku wakipanda majukwaani na kusifia serikali ya CCM eti moja ya mafanikio yake ni kwamba leo Tanzania is in the top twenty gobally katika ligi ya kasi ya kukua kwa uchumi (GDP Growth Rate). Kwani kwa wastani, uchumi wetu (GDP) unakuwa kwa kasi ambayo kwa wastani haijapungua 6% kwa mwaka, kwa miaka zaidi ya kumi mfululizo. Swali - Je, how is the growth in tax revenues? Kama tulivyogusia kidogo, kasi yake inatakiwa iwe kubwa lakini hali haipo hivyo. Na akina Zitto wala hawana muda wa kuangalia hilo. Kwao adui namba moja ni Arusha na Kilimanjaro kwa kipimo cha GDP. Swali juu ya actual contributions (taxes) ya mikoa hii adui kwao? Hawana muda kwa sababu aidha hawajui au it doesn’t sell politically.

Tujadili kidogo dhana ya “Tax to GDP Ratio”. Mifano tutayojadili pengine itawasaidia Zitto na wapambe wake waelewe kwamba hatupo hapa kuenezea chuki dhidi yao bali kuwaelimisha na kuwaambia kwamba wasipotoshe watanzania kwa hoja na siasa nyepesi nyepesi. “Tax to GDP Ratio” ni uwiano wa makusanyo ya kodi dhidi ya pato la taifa (inaweza pia kuwa pato la mkoa). Katika mantiki ya kiuchumi, mara nyingine the higher the ratio, the more desirable and vice versa holds. Kupandisha ratio hii juu mara nyingi huwa ni mkakati wa makusudi wa kusaidia nchi au mkoa au kanda husika to cover differences in the region’s budget revenue. Tusisahau kwamba its Budget revenue ambazo ndio husaidia wananchi kupata au kusambaziwa huduma za kijamii. Huduma za kijamii haziletwi na GDP kama Mkandara na Zitto wanavyopotosha.

Katika hali ya kawaida, mapato ya kodi hayatakiwi kupanda kwa kasi ndogo kuliko pato la taifa (mkoa), kwani kasi ya mapato ya kodi ikiwa chini zaidi ya kasi ya pato la taifa, basi “Tax to GDP ratio hushuka”. Kasi ya mapato ya kodi inatakiwa iwe juu kuliko kasi ya pato la taifa, kwani hivyo ndivyo tax to GDP ratio inapanda. A higher Tax to GDP ratio is more desirable kwa ajili ya uchumi bora wenye kunufaisha maisha ya walio wengi. Again, hii ni kwa sababu huduma za kijamii ambazo mkandara anasema ni haki na sio fursa, pia huduma za kijamii ambazo zitto anazijadili kwa mtindo wa Human Development Index (HDI), zao la huduma hizi ni “Tax revenues” more directly kuliko GDP. Why? Zipo sababu nyingi lakini rahisi kabisa kuelewa ni kwamba:

Unlike GDP figures, tax revenues are tangible. Unaweza kukusanya mapato ya kodi, ukayapangia mipango na mikakati ya maendeleo and implement na kuona social progress. Lakini GDP haishikiki, its intangible, inabakia kuwa kwenye figure ya kutumia kinadharia zaidi kuliko taxes. Ni bahati mbaya sana kwamba akina Mkandara na Zitto wapo busy kuaminisha umma kwamba kila mkoa una haki ya kudai GAWIO LA GDP - nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda. Bila ya hivyo, basi Arusha na Kilimanjaro wataendelea kuwa ni wanyonyaji. How pity!

Tuangalie kidogo dhana ya Tax to GDP ratio kwa Vitendo zaidi katika muktadha wa uchumi wetu. Takwimu hizi ni za kipindi cha mwaka 2013/14.

MKOA
MAPATO YA KODI (TAX REVENUES)
PATO LA TAIFA (GDP)
TAX TO GDP RATIO
Kilimanjaro
100 billion Sh
2 trillion Sh
5%
Shinyanya
18 billion sh
1.9 trillion sh
0.9%
Kigoma
9 billion sh
900 billion sh
1%
Mwanza
118 billion sh
4 trillion sh
3%
Arusha
242 billion sh
2.1 trillion sh
11.5%
Mbeya
68 billion sh
3.2 trillion sh
2.1%
Sources: TRA/BOT/NBS

Quick Observations:
1. Katika mikoa hii mitano, Mwanza inaongoza kwa mchango wake kwa pato la taifa (GDP), lakini kwenye pato la serikali (mapato ya kodi), Mwanza ni ya pili kwa Arusha. Kama tunazungumzia maendeleo, swali langu kwa zitto na wafuasi wake akina Mkandara, Ritz et al ni, je:
· Kipi kinatakiwa kuwa chanzo cha uhakika cha mipango ya maendeleo – je ni GDP ya Mkoa au Makusanyo ya Kodi ya Mkoa? How?

2. Observation ya pili ni kwamba – Arusha inaongoza katika Tax to GDP Ratio, ikifuatiwa na Kilimanjaro. Arusha imeuzidi mkoa wa Mwanza kwa karibia mara nne. Swali linalofuata kwenu ni je, mnadhani ni kwanini? Kwa maana nyingine nyepesi:
· Katika hali ya kawaida, what explains low Tax to GDP ratio ya Kigoma na Shinyanga vis a vis Arusha na Kilimanjaro?
· Na je tofauti hii ina maana gani katika uneven regional development iliyopo?

Haya ndio masuala ambayo Zitto na wapambe wake walitakiwa kujikita zaidi kwa maslahi ya taifa badala ya kukimbilia takwimu na hoja nyepesi nyepesi zenye lengo la kujitafutia cheap popularity. Kwa mfano, mjadala ambao ungejenga utaifa na pia dhana ya collectiveness aliyojadili Nguruvi3 ungeangalia mambo kama haya kwamba:

· Sababu kwanini mikoa mingine experience low Tax to GDP ratios (kwa mfano Shinyanga na Kigoma) ni more of structural factors. Kwa mfano, inaweza kuwa kwamba vipato vya wakazi wa mikoa hii ni vya chini sana kuwawezesha kuchangia katika mapato ya kodi tofauti na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro; Zitto angeweza kabisa kuangalia suala hili kwa mtazamo huo kwa maana ya kujadili mikakati ya kuinua vipato vya wananchi badala ya kusingizia mikoa mingine iliyoendelea kwamba ndio chanzo kwanini mikoa mingine wakazi wake ni maskini.

· Zitto angeweza pia kujadili kwamba tofauti hii ya “Revenue to GDP ratio” inaweza inachangiwa na ‘high levels of informalization’ ya shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa mfano katika mikoa ya Kigoma na Shinyanga kuliko Arusha na Kilimanjaro. Kwa maana nyingine, informal sector katika mikoa ya Kigoma na Shinyana inawezekana ni kubwa kuliko Arusha na Kilimanjaro, na kwa hali hiyo, ni vigumu kwa mamlaka husika za kodi kukusanya kodi ya kutosha katika mazingira ya uchumi uliotawaliwa zaidi na informal sector.

· Zitto angeweza pia kujadili kwamba upo uwezekano kwamba mikoa ya Kigoma na Shinyanga ina mianya mikubwa na mikubwa ya kukwepa kodi (tax evasion) kuliko Arusha na Kilimanjaro, ndio maana Tax to GDP ratio zao ni ndogo zaidi.

· Vile vile inawezekana ikawa kwamba mwamko wa wananchi wa Kigoma na Shinyanga katika kuchangia kodi kwa ajili ya maendeleo yao ni mwamko mdogo kuliko ilivyo kwa Arusha na Kilimanjaro. Zitto na wenzake walitakiwa kuangalia haya kwa hoja zinazojenga na sio kubomoa umoja wetu wa kitaifa.

· Pia, Zitto alitakiwa kutumia fursa aliyonayo kujadili existence of lack of policy initiatives zenye kuziba mianya ya inayopelekea mapato mengi ya serikali kupotea kwa njia mbalimbali kama viel ufisadi, uzembe, misahama ya kodi katika sekta mbali mbali n.k.

· Hoja ya Zitto kwamba Shinyanga ina utajiri (Pamba na Madini) lakini wananchi wake wana maisha duni ni hoja ambayo haikutegemewa kutoka kwa mtu kama yeye. Anasahau kwamba alipokuwa bungeni, alikuwa ni mmoja wa wabunge waliopigania sana kufutwa kwa kodi katika sektaya Kilimo cha biashara (cash crops). Kwa maana hii, mikoa inayotegemea zao kubwa kama la Pamba haiwezi kukusanya kodi za kutosha to finance social services kwa sababu zitto alishiriki katika kufanikisha hilo akiwa bungeni.

· Zitto pia anasahu kwamba hoja yake juu ya utajiri wa madini shinyanga inapwaya, hasa pale anaposingiza umaskini wao kwa mikoa mingine kwani mikoa inayotegemea rasilimali za madini, mikoa hii haiwezi ku-raise enough revenues kutoka kwenye sekta hii kwa serikali bado imeshindwa kuja na kodi zinazowabana vizuri wawekezaji katika sekta ya madini. Zitto alitakiwa awaeleze wana shinyanga juu ya jitiada zake katika kufanikisha hilo alipokuwa bungeni, kwamba halina uhusiano wowote na wakazi wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. Isitoshe, Arusha na Kilimanjaro ni kiuchumi inategemea sana sekta za huduma kuliko Kilimo, na sekta hizi hazina misamaha ya kodi, na hii ni moja ya sababu juu ya kwanini Arusha na Kilimanjaro mapato yao ya kodi yapo juu kuliko mikoa mingi.

Mwisho:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina kauli mbiu isemayo, “Pamoja Tutajenga Taifa Letu”. Maana yake hapa ni kwamba Kigezo Cha Maendeleo ni KODI, na sio GDP.
 
Last edited by a moderator:
Ni wapi Zitto kasema watu wasubiri amalizie report? Nionyeshe hili andishi..

Samahani kwenye kipengele hiyo, niliby-pass hicho kiulizo hapo chini,nimeondoa sentensi inayohusika na sentensi yako hii.

Pia si umeona Zitto naye kachangia hapo umesoma kama kuna sehemu amesema watu wasubiri kwanza mpaka amalize report nzima?

Ebu nawe kuwa muadilifu kwenye mjadala kwa kuyafanyia kazi yaliyobaki

Kilimanjaro imetajwa tarehe 05/04 na ndio siku hiyo hizo comment ulizozileta zilipotolewa,refer chini

Miezi yote hii miwili hukwenda kusoma ili uwe na uhakika na kile unachojadili humu?mpaka leo unamjibu Barubaru ulikuwa kama hujaiona hiyo report Zitto aliyosema uisubiri, na Zitto kamalizia tarehe 7/04/,miezi miwili iliyopita.

Michango ya watu sio hoja maana tunajua watu wanaweza kutafsiri vitu tofauti kwa namna tofauti cha msingi ambacho ndio hoja ya hapa ni kwani Zitto alisemaje?je Zitto aliingiza ubaguzi?je Zitto alisema mikoa fulani inapendelewa?je alisema kuna mikoa inanyonywa?je alisema mgawanyo wa mapato ni kigezo pekee cha maendeleo?utagundua sio kweli.

KUna michango mizuri juu ya maendeleo na uchumi imetolewa humu,ni mizuri,lakini watu kwa kuwa walikuwa hawajapewa taarifa sahihi walikuwa wanajadili juu ya USAHIHI wa ZITTO au KUKOSEA KWAKE wakati hakuna kitu kama hicho,nakumbuka kuna watu mpaka wakawa wanaeleza jinsi KIlimanjaro na ARusha wanavyolipa kodi kubwa, unajiuliza kama source ni Zitto kwani Zitto alisemaje juu ya hilo?miezi miwili iliyopita.Huu ni mfano mmojawapo,kuna maeneo mengi ya aina hiyo.Hii yote ni kwa sababu msingi wa mjadala ulikuwa PROPAGANDA CHAFU.

Nadhani hii hoja inahitaji kuisha sasa.

Ni vizuri Alinda na Nguruvi mkubali tu kuwa HAIKUWA HOJA YA KWELI.Kuna mambo mengi bado tunaweza kujadili kuhusu ACT ama Zitto, tusimame kwenye UKWELI na SIO UONGO WALA PROPAGANDA.

Kumbuka sikuzote,kukiri kukosea ni ishara ya uungwana na hatushindani humu bali tunataka mjadala ubase kwenye ukweli kama wewe mwenyewe ulivyosema hapa chini.

Sasa hapa tutaelewana.. Hoja ni kujua ukweli...

Hivyo natoa wito maliza hayo yaliyobaki hapo juu,tufunge hii chapter tusonge mbele na masuala mengine.Hatuwezi kusimama hapahapa miezi yote hii,kuna mengi pia yanapaswa kujadiliwa.
 
Najiuliza sana, Kiongozi mkuu wa chama cha ACT'wazalendo'. Msemaji mkuu wa chama, aliyejinasibu kuwa ataendesha siasa za kisasa kabisa huku akitumia njia zote za mitandao kukutangaza chama; inakuwaje hotuba zake za kukitanganza chama kwa watanzania zinakuwa adimu namna hii? Na pale zipopatikana zinakuwa zimefupishwa, zimekatwa katwa katwa? Nikweli amejitahidi (S.L) kutumia mitandao mpaka inasemekana ana Google app inayotoa habari zake (app hiyo sijaitembelea).
Kinacho nishangaza ni kwa nini Watetezi wa S.L kutokutoa ushirikiano wowote wa kuziweka wazi hotuba za S.L mtu muhimu katika siasa za ACT!!

Je. Haya yote yanatokana na Watetezi wake kukiri kimya kimya kuwa ACT ni mpini wa CCM kuumaliza upinzani na kwa namna nyingine kuwa kauli za S. L kweli zinalenga kuua umoja wa watanzania? Labda anayesemwa ni Msemaji wa ACT (sina hakika kama ni hapa JF ama sehemu nyingine) Mkuu Kapwela anaweza kutupa maelezo ya kutosha juu ya haya mambo yanayo randaranda kichwani mwangu juu ya Watetezi wa SL, SL mwenyewe, na ACT kwa ujumla.
Hizi huwezi kuzipata maana zinamuaacha uchi.. Mwambie alete hotuba ya Shinyanga, Tabora na Kigoma.

Ninayo heshima kubwa kwako Tujitegemee lakini nasikitika kuwa hoja yako hii imekaa kitetesi mno, kwa namna hoja yako ilivyo unapaswa kuipeleka kwenye jukwaa la tetesi naamini utapata majibu yanayoendana na tetesi.

Tukumbuke wakati wote uzito wa jukwaa hili, JUKWAA LA GREAT THINKERS!

Dada yangu Alinda, please.
 
Kilimanjaro imetajwa tarehe 05/04 na ndio siku hiyo hizo comment ulizozileta zilipotolewa,refer chini

Michango ya watu sio hoja maana tunajua watu wanaweza kutafsiri vitu tofauti kwa namna tofauti cha msingi ambacho ndio hoja ya hapa ni kwani Zitto alisemaje?je Zitto aliingiza ubaguzi?je Zitto alisema mikoa fulani inapendelewa?je alisema kuna mikoa inanyonywa?je alisema mgawanyo wa mapato ni kigezo pekee cha maendeleo?utagundua sio kweli.

KUna michango mizuri juu ya maendeleo na uchumi imetolewa humu,ni mizuri,lakini watu kwa kuwa walikuwa hawajapewa taarifa sahihi walikuwa wanajadili juu ya USAHIHI wa ZITTO au KUKOSEA KWAKE wakati hakuna kitu kama hicho,nakumbuka kuna watu mpaka wakawa wanaeleza jinsi KIlimanjaro na ARusha wanavyolipa kodi kubwa, unajiuliza kama source ni Zitto kwani Zitto alisemaje juu ya hilo?miezi miwili iliyopita.Huu ni mfano mmojawapo,kuna maeneo mengi ya aina hiyo.Hii yote ni kwa sababu msingi wa mjadala ulikuwa PROPAGANDA CHAFU.

Nadhani hii hoja inahitaji kuisha sasa.

Ni vizuri Alinda na Nguruvi mkubali tu kuwa HAIKUWA HOJA YA KWELI.Kuna mambo mengi bado tunaweza kujadili kuhusu ACT ama Zitto, tusimame kwenye UKWELI na SIO UONGO WALA PROPAGANDA.

Zitto Kabwe Fulgence Miku Kilimanjaro na hasa mji wa moshi unanyonywa na mji wa Arusha. Hii hasa ni kwenye utalii. Kwenye Kilimo kuna potential kubwa sana ya Kilimanjaro kuchangia zaidi kwenye Pato la Taifa. Kinachonichanganya ni inakuwaje Kilimanjaro ichangie kidogo sana kwenye Pato la Taifa lakini iwe ya pili kwenye ubora wa maisha ya wananchi?

Si maneno yangu bali ni maneno ya Zitto. Pia msome Mchambuzi hapo juu alivyodadavua haya mambo..
 
Ninayo heshima kubwa kwako Tujitegemee lakini nasikitika kuwa hoja yako hii imekaa kitetesi mno, kwa namna hoja yako ilivyo unapaswa kuipeleka kwenye jukwaa la tetesi naamini utapata majibu yanayoendana na tetesi.

Tukumbuke wakati wote uzito wa jukwaa hili, JUKWAA LA GREAT THINKERS!

Dada yangu Alinda, please.

Sawa turudi kwenye hoja ya kujenga taifa soma mchango wa Mchambuzi. Unakubalina na mchambuzi?
 
Bila ya kujalisha zitto alitoa hotuba wapi na lini, bado hoja yake ya msingi imejaa upotoshaji na uchonganishi.

Badala yake nikjadili kwamba kigezo ambacho kinakaribiana na uhalisia wa mambo ni tax revenues. Lakini kama kawaida yao, hawakufafanua msimamo wao huo, zaidi ya kuendeleza mtazamo wa "zidumu fikra sahihi za Zitto Kabwe".

Swali langu kwenu:

Kati ya "Government Income" (Taxes) na "National Income" (Market Value of Goods and Services Produced in an economy i.e GDP):
· Ipi inapima juhudi za maendeleo kwa vitendo zaidi? Mkandara na wenzake wanaendelea kusisitiza kwamba ni GDP. Tukiuliza Kwanini? Jibu ni kwamba Zitto kasema.
·
Nilijadili kwamba, kwa upande mmoja, PATO LA TAIFA (GDP) ni jumla ya thamani (thamani ya soko) ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa ndani ya uchumi husika. Na kwamba kwa upande mwingine, KODI ni Pato la Serikali kwa maana ya kwamba this is an income earned by the STATE. Umuhimu wa Pato is for the state to finance public expenditure kama zile ambazo mkandara anasema kwa sasa zimegeuzwa kuwa fursa badala ya haki (mfano Elimu, Afya n.k), pamoja na kugharamia masuala mengine yanayohusiana na mahitaji ya umma. The state doesn't fund development projects via GDP!

Tofauti kubwa baina ya Tax Revenues and National Income:
1. Taxes are mandatory payments, ruled by law, lakini GDP isn't directly ruled by law. Kwa mfano, usipozalisha vya kutosha katika shughuli zako za kiuchumi kama kilimo, ufugaji, uvuvi, hakuna Sheria inayokubana, lakini usipolipa kodi, ni kosa kisheria.
2. Taxes (by default) are the best expression of the common efforts or collective efforts of the community. Hii ni tofauti na GDP. Hakuna collective effort. Ilikuwa hivyo wakati wa vijiji wa ujamaa, na hata hivyo it didn't work. Otherwise kwenye suala la taxes, sense of community or collectivity applies globally. Dhana hii inaendana na hoja aliyotoa Nguruvi3 awali juu ya ‘utaifa' linapokuja suala la kutafuta maendeleo. Swali kewnu, Je:

· Mnakumbuka "Kodi ya Maendeleo"? Kwanini maendeleo yalihusishwa moja kwa moja na kodi na (sio GDP)?

Pengine Mjamaa Mkandara anaweza kutusaidia na majibu,
Ningepende niweke msisitizo hapa kwamba Zitto ni mbabaishaji na mpotoshaji kwa sababu kati ya GDP na Tax Revenues, its tax revenues that explains more directly on why there's an income difference baina ya mkoa mmoja na mwingine. Nitafafanua:

Zitto anaposema kwamba kuna maeneo ambayo yapo nyuma kwa sababu ya poor public services or infrastructure, anajisahau kwamba ni kwa sababu ya mapungufu kwenye Tax system na sio National Income Statistics.

Suala la pili ni kwamba – tofauti na GDP, Kodi inaweza kutumika katika malengo mapana ya kupunguza tofauti ndani ya jamii (social and economic inequality). Swali kwa zitto na wapambe wake, je:
· Kati ya Taxes & GDP, which one is the most effective tool of curbing or reducing "income inequality"? Kwanini mchumi mahiri Zitto haoni hilo?

Haya ndio mambo ambayo Zitto anatakiwa ajadili, sio kwenda kupotosha umma na kuchonganisha watanzania.

Tax revenues must grow at a much faster rate than GDP. Na akina Zitto wala hawana muda wa kuangalia hilo. Kwao adui namba moja ni Arusha na Kilimanjaro kwa kipimo cha GDP. Swali juu ya actual contributions (taxes) ya mikoa hii adui kwao? Hawana muda kwa sababu aidha hawajui au it doesn't sell politically.

Tujadili kidogo dhana ya "Tax to GDP Ratio". Mifano tutayojadili pengine itawasaidia Zitto.Katika mantiki ya kiuchumi, mara nyingine the higher the ratio, the more desirable and vice versa holds. Huduma za kijamii haziletwi na GDP kama Mkandara na Zitto wanavyopotosha.

Ni bahati mbaya sana kwamba akina Mkandara na Zitto wapo busy kuaminisha umma kwamba kila mkoa una haki ya kudai GAWIO LA GDP - nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda. Bila ya hivyo, basi Arusha na Kilimanjaro wataendelea kuwa ni wanyonyaji. How pity!

· Zitto pia anasahu kwamba hoja yake juu ya utajiri wa madini shinyanga inapwaya, hasa pale anaposingiza umaskini wao kwa mikoa mingine.Zitto alitakiwa awaelewe wana shinfanya jitiada zake katika kufanikisha hilo alipokuwa bungeni, kwamba halina uhusiano wowote na wakazi wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. Isitoshe, Arusha na Kilimanjaro ni kiuchumi inategemea sana sekta za huduma kuliko Kilimo, na sekta hizi hazina misamaha ya kodi, na hii ni moja ya sababu juu ya kwanini Arusha na Kilimanjaro mapato yao ya kodi yapo juu kuliko mikoa mingi.

Huu ni mfano wa namna thread hii ilivyojengwa kwenye msingi mbovu.

Hii ni hoja nzuri sana na kuna nyingi zingine zimewekwa humu, lakin bahati mbaya kwa kuwa msingi ulipotoshwa watu wakajikita kujibu hoja ambazo hazipo na kumjibu ambaye hajauliza/hajasema.

Msome Zitto hapo chini.

.........................................................................................................................................

Zitto Kabwe

Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu

Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.

Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.

Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.

Mikoa 9 nchini ina idadi ya watu zaidi ya 2m. Dar, Mbeya, Tanga, Morogoro, Mwanza, Tabora, Kagera, Dodoma and Kigoma. Mikoa hii ina 52% ya Watanzania wote

Wakati Dar inachangia 16.93% ya katika Pato la Taifa, inaongoza kwa makusanyo ya kodi ambapo inachangia 81% ya Mapato yote ya Serikali. Kwa makusanyo ya Kodi mkoa wa pili ni Arusha na wa tatu ni Tanga.

Dar, Arusha, Tanga, Mwanza na Kilimanjaro huchangia 90% ya mapato yote ya Serikali nchini

Shinyanga inaendelea kushangaza sana. Wakati inashika nafasi ya nne kuchangia Pato la Taifa (6% of Tanzania GDP), inashika moja ya nafasi ya chini kabisa kuchangia Mapato ya Serikali ( 0.46% of total tax ). Unajua sababu? Shughuli nyingi za kiuchumi za Shinyanga hufanyika Shinyanga lakini kodi zake zakusanywa Dar es Salaam. Mfano migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, kodi zake zinalipwa Dar es Salaam

Mkoa wa Njombe ndio unaongoza kwa kuwa na watu wengi virusi vya ukimwi. 15.4% ya watu wa Njombe wenye umri kati ya 14 - 49 wanaishi na virusi vya ukimwi. Mkoa unaofuata ni Iringa wenye 10.9% ya watu wake kuwa na virusi vya ukimwi.

Dodoma, Manyara na Tanga ndio mikoa yenye watu wachache zaidi wanaoishi na virusi vya ukimwi

Mkoa wa Simiyu ndio mkoa wenye watu wachache zaidi wenye elimu ya sekondari ambapo 3.7% ya watu wa Simiyu wenye umri wa zaidi ya miaka 25 wana elimu ya sekondari. Dar es Salaam ndio mkoa wenye watu wengi zaidi wenye elimu ya Sekondari, 29%

Katika kodi zote zinazokusanywa Dar es Salaam, 75% zinatokana na forodha, 16% kodi ya mapato na 9% kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Dar inachangia 81% ya makusanyo yote ya kodi nchini. Hii inaonyesha kuwa Watanzania wengi sana hawalipi kodi. Utegemezi kwenye forodha ni hatari sana kwa uhai wa nchi yeyote.

" there appears to be a disconnect between economic growth on the one hand and human development on the other" Tanzania Human Development Report 2014

Takwimu zote ninazoweka hapa toka jana zinatoka katika Tanzania Human Development Report 2014. Taarifa imesheheni kwa kweli

Tofauti ya Kipato miongoni mwa wananchi (Inequality) ni jambo linalokosekana kabisa kwenye uchambuzi wa Taarifa ya Maendeleo ya Watu ( THDR 2014). Ninadhani moja ya hatari kubwa nchini ni kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Sifa ya sasa ya uchumi wa Tanzania ni 'kufaidisha wachache na kufukarisha wengi'
......................................................................................................................................
 
Zitto Kabwe Fulgence Miku Kilimanjaro na hasa mji wa moshi unanyonywa na mji wa Arusha. Hii hasa ni kwenye utalii. Kwenye Kilimo kuna potential kubwa sana ya Kilimanjaro kuchangia zaidi kwenye Pato la Taifa. Kinachonichanganya ni inakuwaje Kilimanjaro ichangie kidogo sana kwenye Pato la Taifa lakini iwe ya pili kwenye ubora wa maisha ya wananchi?

Si maneno yangu bali ni maneno ya Zitto. Pia msome Mchambuzi hapo juu alivyodadavua haya mambo..

He mara hii Zitto mwenye kulaumiwa kwa kusema Kilimanjaro kuinyonya shinyanga, eti anazungumzia na Kilimanjaro Kunyonywa pia.

je hii si ni ushahidi wa Wazi wa Zitto kutaka fair distribution ya keki ya taifa? na si issue ya ubaguzi?.
 
Tupe ufafanuzi hapo, kivipi unataka fair distribution na kwa vigezo vipi? tupe shule kwa uelewa wako..Lakini kabla ya hapo pata shule kutoka kwa Mchambuzi..
 
Zitto Kabwe Fulgence Miku Kilimanjaro na hasa mji wa moshi unanyonywa na mji wa Arusha. Hii hasa ni kwenye utalii. Kwenye Kilimo kuna potential kubwa sana ya Kilimanjaro kuchangia zaidi kwenye Pato la Taifa. Kinachonichanganya ni inakuwaje Kilimanjaro ichangie kidogo sana kwenye Pato la Taifa lakini iwe ya pili kwenye ubora wa maisha ya wananchi?

Si maneno yangu bali ni maneno ya Zitto. Pia msome Mchambuzi hapo juu alivyodadavua haya mambo..

Hoja ya Mchambuzi ni mfano wa nilichokuwa nakisema toka mwanzo juu ya upotoshaji uliofanyika na kuwafanya wachangiaji kusimamia kwenye MISINGI YA HOJA AMBAYO HAIPO
KUna michango mizuri juu ya maendeleo na uchumi imetolewa humu,ni mizuri,lakini watu kwa kuwa walikuwa hawajapewa taarifa sahihi walikuwa wanajadili juu ya USAHIHI wa ZITTO au KUKOSEA KWAKE wakati hakuna kitu kama hicho,nakumbuka kuna watu mpaka wakawa wanaeleza jinsi KIlimanjaro na ARusha wanavyolipa kodi kubwa, unajiuliza kama source ni Zitto kwani Zitto alisemaje juu ya hilo?miezi miwili iliyopita.Huu ni mfano mmojawapo,kuna maeneo mengi ya aina hiyo.Hii yote ni kwa sababu msingi wa mjadala ulikuwa PROPAGANDA CHAFU.

Ni vizuri Alinda na Nguruvi mkubali tu kuwa HAIKUWA HOJA YA KWELI.Kuna mambo mengi bado tunaweza kujadili kuhusu ACT ama Zitto, tusimame kwenye UKWELI na SIO UONGO WALA PROPAGANDA.

Unaweza ukaona hapo jinsi Mchambuzi ANAVYOJIKITA KUMJIBU NA KUMKOSOA ZITTO kwa HOJA AMBAZO ZITTO HAJAZISEMA.Hoja nyingi zilijikita kwenye:

1.Zitto kasema mkoa wa Shinyanga/Tabora unanyonywa na mkoa wa Kilimanjaro.

2.Zitto kasema umaskini wa Shinyanga/Tabora unatokana na mkoa wa Kilimanjaro.

3.Zitto kasema kuwa mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa.

4.Zitto kasema mgawanyo wa mapato ya serikali sio wa HAKI na ndio MSINGI PEKEE WA MAENDELEO YA WATU.

Wengine wakaenda mbali kujadili TAX/GDP kwa misingi hiyohiyo,ambayo sio ya kweli bali ni propaganda tu.Hatujawatendea haki wachangiaji wengi hapa katika hili.

Kuna hoja nyingi sana sana zimetolewa hapa lakini tumezipunguzia makali kwa kuzipersonalize kwa "mtu" na hivyo kuzipunguzia "nguvu ya hoja" yenyewe. Tumeishakosea lakini sikuzote hakuna deadline ya kujisahihisha,hatujachelewa.

Ni wakati sasa hili jukwaa lirudi kwenye nafasi yake na kujielekeza kujadili issues na sio kujadili "watu", hii ndio tofauti ya jukwaa hili na jukwaa la siasa.Hili ndilo jukwaa pekee kwa sasa ambalo watu wazima wapo comfortable kujadili/kusoma humu.Kama jukwaa hili likishindwa basi Jamiiforums imeshindwa.Tujiepushe kulifanya jukwaa hili kuwa jukwaa la propaganda/chuki/hasira zetu za kisiasa, tutapoteza maana na baadae hadhi ya jukwaa lenyewe.

Pamoja na yote kwenye mjadala huu, naomba nikiri hadharani kuwa nina heshima kubwa sana kwako Alinda,ubarikiwe sana!
 
Tupe ufafanuzi hapo, kivipi unataka fair distribution na kwa vigezo vipi? tupe shule kwa uelewa wako..Lakini kabla ya hapo pata shule kutoka kwa Mchambuzi..
Yaani nilitaka kuuliza kitu hicho hicho. Ninaongezea, mbona wanaosema kuna unfair distribution of national cake, hawaonyeshi ni wapi?

Lakini pia ina underline statement za kiongozi mkuu unless tuelezwe unfair distrtibution ipi
 
Wewe Nguruv huna haki tena ya kujadili hoja ambayo source yake ni Facebook kwa sababu huna imani nayo.

Muachie Alinda na wengine wenye kuzipa uzito source za Facebook tufanye nao mjadala, wewe Nguruv itakuwa ni sawa na kulamba matapishi yako mwenyewe kuingia ktk mjadala kwa kutumia reference usizo na imani nazo!
 
Ritz, Gamba la Nyoka, Waberoya, Mkandara, Kapwela, Adharusi:Mnawekezasana katika kutuondoa kwenye hoja ya msingi, huku mkitamani sana tufunike kombemwanaharamu apite. Hilo tutalikataa kwa nguvu zote.
My take: Njia dhaifu sana ya kujenga hoja na utetezi kwa kiongozi mkuu.

Bila ya kujalisha zitto alitoa hotuba wapi nalini, bado hoja yake ya msingi imejaa upotoshaji na uchonganishi.
My take, hoja muhimu zinataka kufunikwa na spinning ambazo nazohawazijui. Hizo zina mu expose kiongozi mkuu badala ya kumsafisha. Hatutafunikakombe hata siku moja

Mchango wa mkoa katika GDP kigezo cha kupimA/kufafanishakiwango cha maendeleo ya mkoa mmoja dhidi ya mwingine,ni approach ‘flawed'.
Swali langu kwenu:
Kati ya "Government Income" (Taxes) na"National Income" (Market Value of Goods and Services Produced in an economyi.e GDP):

Ipi inapima juhudi za maendeleo kwa vitendo zaidi?
My take: Tafadhali tuwekeeni positionyenu . Haya ndiyo madini tunayotakiwa tuyadili

PATO LA TAIFA (GDP) ni jumla ya thamani (thamani ya soko) ya bidhaa nahuduma zote zinazozalishwa ndani ya uchumi husika.
KODI ni Pato la Serikali kwa maana ya kwamba this is an income earned bythe STATE.
Umuhimu wa Pato is for the state to finance public expenditure kama zileambazo mkandara anasema kwa sasa zimegeuzwa kuwa fursa badala ya haki (mfanoElimu, Afya n.k), pamoja na kugharamia masuala mengine yanayohusiana namahitaji ya umma.The state doesn't fund development projects via GDP!

Tofauti kubwa baina ya Tax Revenues andNational Income:
1. Taxes are mandatory payments, ruled by law, lakini GDP isn't directly ruledby law. Kwa mfano, usipozalisha vya kutosha katika shughuli zako za kiuchumikama kilimo, ufugaji, uvuvi, hakuna Sheria inayokubana, lakini usipolipa kodi,ni kosa kisheria.

2. Taxes (by default) are the bestexpression of the common efforts or collective efforts of the community. Hii nitofauti na GDP. Hakuna collective effort.Swali kewnu, Je:Mnakumbuka "Kodi yaMaendeleo"? Kwanini maendeleo yalihusishwa moja kwa moja na kodi na (sio GDP)?

My take:Tafadhalini tunaomba tusikie upande mwingine una hoja gani

Ningepende niweke msisitizo, Zitto nimbabaishaji na mpotoshaji kwa sababu GDP na Tax Revenues, its tax revenues thatexplains more directly on why there's

an income difference baina ya mkoa mmoja na mwingine.
My take: Kuna hoja mbadala dhidi ya hii? Kama hakuna, je si kwelikiongozi mkuu alitumia takwimu kibubusa ili kuhadaa umma katika kujenga chuki
Madini hayo! Tusemezane
 
Back
Top Bottom