Ritz,
Gamba la Nyoka,
Waberoya,
Mkandara,
Kapwela,
Adharusi:
Mnawekeza sana katika kutuondoa kwenye hoja ya msingi, huku mkitamani sana tufunike kombe mwanaharamu apite. Hilo tutalikataa kwa nguvu zote. Bila ya kujalisha zitto alitoa hotuba wapi na lini, bado hoja yake ya msingi imejaa upotoshaji na uchonganishi.
Siku za nyuma, niliwahi kujadili kwamba kuangalia kila mkoa (kwa kigezo cha GDP) na mchango wa mkoa husika katika GDP ya Taifa kama kigezo cha kupima au kufafanisha kiwango cha maendeleo ya mkoa mmoja dhidi ya mkoa mwingine approach ambayo ipo flawed.
Badala yake nikjadili kwamba kigezo ambacho kinakaribiana na uhalisia wa mambo ni tax revenues. Wapo waliopinga, kwa mfano akina
Mkandara kwa hoja kwamba GDP ndio kipimo sahihi zaidi. Lakini kama kawaida yao, hawakufafanua msimamo wao huo, zaidi ya kuendeleza mtazamo wa zidumu fikra sahihi za Zitto Kabwe.
Swali langu kwenu:
Kati ya Government Income (Taxes) na National Income (Market Value of Goods and Services Produced in an economy i.e GDP):
· Ipi inapima juhudi za maendeleo kwa vitendo zaidi?
Mkandara na wenzake wanaendelea kusisitiza kwamba ni GDP. Tukiuliza Kwanini? Jibu ni kwamba
Zitto kasema.
·
Nilijadili kwamba, kwa upande mmoja, PATO LA TAIFA (GDP) ni jumla ya thamani (thamani ya soko) ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa ndani ya uchumi husika. Na kwamba kwa upande mwingine, KODI ni Pato la Serikali kwa maana ya kwamba this is an income earned by the STATE. Umuhimu wa Pato is for the state to finance public expenditure kama zile ambazo mkandara anasema kwa sasa zimegeuzwa kuwa fursa badala ya haki (mfano Elimu, Afya n.k), pamoja na kugharamia masuala mengine yanayohusiana na mahitaji ya umma. The state doesnt fund development projects via GDP!
Tofauti kubwa baina ya Tax Revenues and National Income:
1. Taxes are mandatory payments, ruled by law, lakini GDP isnt directly ruled by law. Kwa mfano, usipozalisha vya kutosha katika shughuli zako za kiuchumi kama kilimo, ufugaji, uvuvi, hakuna Sheria inayokubana, lakini usipolipa kodi, ni kosa kisheria.
2. Taxes (by default) are the best expression of the common efforts or collective efforts of the community. Hii ni tofauti na GDP. Hakuna collective effort. Ilikuwa hivyo wakati wa vijiji wa ujamaa, na hata hivyo it didnt work. Otherwise kwenye suala la taxes, sense of community or collectivity applies globally. Dhana hii inaendana na hoja aliyotoa
Nguruvi3 awali juu ya utaifa linapokuja suala la kutafuta maendeleo. Swali kewnu, Je:
· Mnakumbuka Kodi ya Maendeleo? Kwanini maendeleo yalihusishwa moja kwa moja na kodi na (sio GDP)?
Pengine Mjamaa
Mkandara anaweza kutusaidia na majibu,
Ningepende niweke msisitizo hapa kwamba Zitto ni mbabaishaji na mpotoshaji kwa sababu kati ya GDP na Tax Revenues, its tax revenues that explains more directly on why theres an income difference baina ya mkoa mmoja na mwingine. Nitafafanua:
Unlike GDP, taxation is the most effective way of financing the costs of all public goods. By public goods, maana yake ni kwamba goods ambazo consumption (matumizi) yake yanapofanywa na mtu mmoja haipunguzi matumizi ya wengine lakini pia. Pia ni vigumu kuzuia watu wasitumie such public goods, hata kama hawajalipia. Mfano ni taa za barabarani n.k. Funds kwa ajili ya such goods zina uhusiano wa moja kwa moja na Government Income (Tax Revenues) kuliko National Income (GDP). Kwa maana hii, Zitto anaposema kwamba kuna maeneo ambayo yapo nyuma kwa sababu ya poor public services or infrastructure, anajisahau kwamba ni kwa sababu ya mapungufu kwenye Tax system na sio National Income Statistics.
Kama tulivyokwisha ona, tofauti na suala la GDP/Pato la Taifa - (yani uzalishaji wa goods and services), taxes are mandatory payments, constrained BY LAW. Kitakwimu tunaona zipo jamii kadhaa nchini ambazo hazifanyi uzalishaji wa kutosha kwa sababu mbalimbali, lakini bado maisha yao yanaendelea na hakuna anayewabugudhi au kuwaambia kwamba wanavunja sharia. Wananchi hawa wanaishia kuitwa tu wavivu, wazembe, economically challenged etc, na hakuna sheria zinazowabana. Lakini linapokuja suala la Pato la Serikali (kodi), takwimu zinatuonyesha kwamba kuna jamii ambazo zinajituma na kuchangia sana kwenye mapato ya serikali, na maendeleo ya taifa kwa ujumla, na juhudi hizi zipo constrained by LAW. Kuna masuala mengine matatu ambayo ni muhimu kuyatazama kufikia hatua hii:
Kwanza - Kodi hukusanywa kutoka kwenye jamii nzima, na main inspiration katika hili ni vitu vikuu vitatu:
· Justice.
· Efficiency.
· Effectiveness.
Again, tukitazama in practice, tunaona kwamba zipo jamii ambazo zinalipa kodi kubwa kuliko jamii nyingine, pamoja na kwamba ulipaji wa kodi ni kwa mujibu wa sheria. Je is there justice katika hili? Kwanini Zitto asijadili suala hili muhimu badala ya kutumia muda wake kuchonganisha wananchi? Kama kweli Zitto ana lengo la kuangalia viwango vya maendeleo katika jamii mbalimbali kwa maslahi ya taifa, basi anatakiwa aangalie vitu hivi vitatu kwa pamoja namely justice, efficiency & effectiveness.
Suala la pili ni kwamba tofauti na GDP, Kodi inaweza kutumika katika malengo mapana ya kupunguza tofauti ndani ya jamii (social and economic inequality). Swali kwa zitto na wapambe wake, je:
· Kati ya Taxes & GDP, which one is the most effective tool of curbing or reducing income inequality? Kwanini mchumi mahiri Zitto haoni hilo? Kwanini wafuasi wake mnashindwa kuhoji au kuona ukweli? Kwenu, kila anachosema Zitto ni Kweli Tupu, sisi tukipinga kwa hoja na mantiki ambazo zinaangalia utaifa kwanza, badala ya kujibu kwa hoja, mnatupatia majibu yaliyojaa matusi na shutuma kwamba tuna wivu dhidi ya supreme leader.
Suala la tatu ni kwamba kiuchumi, GDP dynamics ni major determinant ya mapato ya kodi. Kwa mfano, GDP ikiwa kubwa, basi Mapato ya Kodi nayo yanatakiwa kuwa makubwa, na GDP ikiwa ndogo, na mapato ya Kodi pia yanatakiwa kuwa madogo. Swali je, hivyo ndivyo hali ilivyo nchini? Haya ndio mambo ambayo Zitto anatakiwa ajadili, sio kwenda kupotosha umma na kuchonganisha watanzania. Nitajitahidi kujadili:
Ili taifa liweze kuendelea kiuchumi, Tax revenues must grow at a much faster rate than GDP. Swali je, hivyo ndivyo hali ilivyo nchini? Kwanini tunaachia wanasiasa wetu waendelee kutudanganya huku wakipanda majukwaani na kusifia serikali ya CCM eti moja ya mafanikio yake ni kwamba leo Tanzania is in the top twenty gobally katika ligi ya kasi ya kukua kwa uchumi (GDP Growth Rate). Kwani kwa wastani, uchumi wetu (GDP) unakuwa kwa kasi ambayo kwa wastani haijapungua 6% kwa mwaka, kwa miaka zaidi ya kumi mfululizo. Swali - Je, how is the growth in tax revenues? Kama tulivyogusia kidogo, kasi yake inatakiwa iwe kubwa lakini hali haipo hivyo. Na akina Zitto wala hawana muda wa kuangalia hilo. Kwao adui namba moja ni Arusha na Kilimanjaro kwa kipimo cha GDP. Swali juu ya actual contributions (taxes) ya mikoa hii adui kwao? Hawana muda kwa sababu aidha hawajui au it doesnt sell politically.
Tujadili kidogo dhana ya Tax to GDP Ratio. Mifano tutayojadili pengine itawasaidia Zitto na wapambe wake waelewe kwamba hatupo hapa kuenezea chuki dhidi yao bali kuwaelimisha na kuwaambia kwamba wasipotoshe watanzania kwa hoja na siasa nyepesi nyepesi. Tax to GDP Ratio ni uwiano wa makusanyo ya kodi dhidi ya pato la taifa (inaweza pia kuwa pato la mkoa). Katika mantiki ya kiuchumi, mara nyingine the higher the ratio, the more desirable and vice versa holds. Kupandisha ratio hii juu mara nyingi huwa ni mkakati wa makusudi wa kusaidia nchi au mkoa au kanda husika to cover differences in the regions budget revenue. Tusisahau kwamba its Budget revenue ambazo ndio husaidia wananchi kupata au kusambaziwa huduma za kijamii. Huduma za kijamii haziletwi na GDP kama Mkandara na Zitto wanavyopotosha.
Katika hali ya kawaida, mapato ya kodi hayatakiwi kupanda kwa kasi ndogo kuliko pato la taifa (mkoa), kwani kasi ya mapato ya kodi ikiwa chini zaidi ya kasi ya pato la taifa, basi Tax to GDP ratio hushuka. Kasi ya mapato ya kodi inatakiwa iwe juu kuliko kasi ya pato la taifa, kwani hivyo ndivyo tax to GDP ratio inapanda. A higher Tax to GDP ratio is more desirable kwa ajili ya uchumi bora wenye kunufaisha maisha ya walio wengi. Again, hii ni kwa sababu huduma za kijamii ambazo mkandara anasema ni haki na sio fursa, pia huduma za kijamii ambazo zitto anazijadili kwa mtindo wa Human Development Index (HDI), zao la huduma hizi ni Tax revenues more directly kuliko GDP. Why? Zipo sababu nyingi lakini rahisi kabisa kuelewa ni kwamba:
Unlike GDP figures, tax revenues are tangible. Unaweza kukusanya mapato ya kodi, ukayapangia mipango na mikakati ya maendeleo and implement na kuona social progress. Lakini GDP haishikiki, its intangible, inabakia kuwa kwenye figure ya kutumia kinadharia zaidi kuliko taxes. Ni bahati mbaya sana kwamba akina Mkandara na Zitto wapo busy kuaminisha umma kwamba kila mkoa una haki ya kudai GAWIO LA GDP - nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda. Bila ya hivyo, basi Arusha na Kilimanjaro wataendelea kuwa ni wanyonyaji. How pity!
Tuangalie kidogo dhana ya Tax to GDP ratio kwa Vitendo zaidi katika muktadha wa uchumi wetu. Takwimu hizi ni za kipindi cha mwaka 2013/14.
MKOA
| MAPATO YA KODI (TAX REVENUES)
| PATO LA TAIFA (GDP)
| TAX TO GDP RATIO
|
Kilimanjaro
| 100 billion Sh
| 2 trillion Sh
| 5%
|
Shinyanya
| 18 billion sh
| 1.9 trillion sh
| 0.9%
|
Kigoma
| 9 billion sh
| 900 billion sh
| 1%
|
Mwanza
| 118 billion sh
| 4 trillion sh
| 3%
|
Arusha
| 242 billion sh
| 2.1 trillion sh
| 11.5%
|
Mbeya
| 68 billion sh
| 3.2 trillion sh
| 2.1%
|
Sources: TRA/BOT/NBS
Quick Observations:
1. Katika mikoa hii mitano, Mwanza inaongoza kwa mchango wake kwa pato la taifa (GDP), lakini kwenye pato la serikali (mapato ya kodi), Mwanza ni ya pili kwa Arusha. Kama tunazungumzia maendeleo, swali langu kwa zitto na wafuasi wake akina
Mkandara,
Ritz et al ni, je:
· Kipi kinatakiwa kuwa chanzo cha uhakika cha mipango ya maendeleo je ni GDP ya Mkoa au Makusanyo ya Kodi ya Mkoa? How?
2. Observation ya pili ni kwamba Arusha inaongoza katika Tax to GDP Ratio, ikifuatiwa na Kilimanjaro. Arusha imeuzidi mkoa wa Mwanza kwa karibia mara nne. Swali linalofuata kwenu ni je, mnadhani ni kwanini? Kwa maana nyingine nyepesi:
· Katika hali ya kawaida, what explains low Tax to GDP ratio ya Kigoma na Shinyanga vis a vis Arusha na Kilimanjaro?
· Na je tofauti hii ina maana gani katika uneven regional development iliyopo?
Haya ndio masuala ambayo Zitto na wapambe wake walitakiwa kujikita zaidi kwa maslahi ya taifa badala ya kukimbilia takwimu na hoja nyepesi nyepesi zenye lengo la kujitafutia cheap popularity. Kwa mfano, mjadala ambao ungejenga utaifa na pia dhana ya collectiveness aliyojadili
Nguruvi3 ungeangalia mambo kama haya kwamba:
· Sababu kwanini mikoa mingine experience low Tax to GDP ratios (kwa mfano Shinyanga na Kigoma) ni more of structural factors. Kwa mfano, inaweza kuwa kwamba vipato vya wakazi wa mikoa hii ni vya chini sana kuwawezesha kuchangia katika mapato ya kodi tofauti na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro; Zitto angeweza kabisa kuangalia suala hili kwa mtazamo huo kwa maana ya kujadili mikakati ya kuinua vipato vya wananchi badala ya kusingizia mikoa mingine iliyoendelea kwamba ndio chanzo kwanini mikoa mingine wakazi wake ni maskini.
· Zitto angeweza pia kujadili kwamba tofauti hii ya Revenue to GDP ratio inaweza inachangiwa na high levels of informalization ya shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa mfano katika mikoa ya Kigoma na Shinyanga kuliko Arusha na Kilimanjaro. Kwa maana nyingine, informal sector katika mikoa ya Kigoma na Shinyana inawezekana ni kubwa kuliko Arusha na Kilimanjaro, na kwa hali hiyo, ni vigumu kwa mamlaka husika za kodi kukusanya kodi ya kutosha katika mazingira ya uchumi uliotawaliwa zaidi na informal sector.
· Zitto angeweza pia kujadili kwamba upo uwezekano kwamba mikoa ya Kigoma na Shinyanga ina mianya mikubwa na mikubwa ya kukwepa kodi (tax evasion) kuliko Arusha na Kilimanjaro, ndio maana Tax to GDP ratio zao ni ndogo zaidi.
· Vile vile inawezekana ikawa kwamba mwamko wa wananchi wa Kigoma na Shinyanga katika kuchangia kodi kwa ajili ya maendeleo yao ni mwamko mdogo kuliko ilivyo kwa Arusha na Kilimanjaro. Zitto na wenzake walitakiwa kuangalia haya kwa hoja zinazojenga na sio kubomoa umoja wetu wa kitaifa.
· Pia, Zitto alitakiwa kutumia fursa aliyonayo kujadili existence of lack of policy initiatives zenye kuziba mianya ya inayopelekea mapato mengi ya serikali kupotea kwa njia mbalimbali kama viel ufisadi, uzembe, misahama ya kodi katika sekta mbali mbali n.k.
· Hoja ya Zitto kwamba Shinyanga ina utajiri (Pamba na Madini) lakini wananchi wake wana maisha duni ni hoja ambayo haikutegemewa kutoka kwa mtu kama yeye. Anasahau kwamba alipokuwa bungeni, alikuwa ni mmoja wa wabunge waliopigania sana kufutwa kwa kodi katika sektaya Kilimo cha biashara (cash crops). Kwa maana hii, mikoa inayotegemea zao kubwa kama la Pamba haiwezi kukusanya kodi za kutosha to finance social services kwa sababu zitto alishiriki katika kufanikisha hilo akiwa bungeni.
· Zitto pia anasahu kwamba hoja yake juu ya utajiri wa madini shinyanga inapwaya, hasa pale anaposingiza umaskini wao kwa mikoa mingine kwani mikoa inayotegemea rasilimali za madini, mikoa hii haiwezi ku-raise enough revenues kutoka kwenye sekta hii kwa serikali bado imeshindwa kuja na kodi zinazowabana vizuri wawekezaji katika sekta ya madini. Zitto alitakiwa awaeleze wana shinyanga juu ya jitiada zake katika kufanikisha hilo alipokuwa bungeni, kwamba halina uhusiano wowote na wakazi wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. Isitoshe, Arusha na Kilimanjaro ni kiuchumi inategemea sana sekta za huduma kuliko Kilimo, na sekta hizi hazina misamaha ya kodi, na hii ni moja ya sababu juu ya kwanini Arusha na Kilimanjaro mapato yao ya kodi yapo juu kuliko mikoa mingi.
Mwisho:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina kauli mbiu isemayo, Pamoja Tutajenga Taifa Letu. Maana yake hapa ni kwamba Kigezo Cha Maendeleo ni KODI, na sio GDP.