Wakati Ukawa inaundwa, Zitto alikuwa ni Mwanachama wa Chadema.
Zitto alikuwa anaamini katika itikadi, falsafa, na malengo ya Chadema. Akiwa Chadema, kama mwanachama,
aliapa kuwa mwaminifu kwa chama, na kwa maneno yake, katika nyakati tofauti, alisema kwamba adui wa maendeleo ya watanzania ni chama cha Mapinduzi.
Baada, Zitto akaanza unduminakuwili, na hapa ndio akaanza kutuacha tumeduwaa tusijue la kufanya kwani, akiwa bado mwanachama wa Chadema, akaanza kushutumu UKAWA kwamba wanataka kuvunja muungano. Akaanzea kusema kwamba UKAWA sio lolote bali ni wasaka tonge. Leo kapata tonge lake la supreme leader, sasa anageuka na kusema kwamba yupo tayaru kuungana na Ukawa, lakini tatizo ni kwamba uongozi wa Ukawa unamzuia kufanya hilo. Hivi kweli inaingia akilini kumkubalia kiongozi wa chama cha upinzani kinachopambana na upinzani kujiunga na movement ambayo awali alisema kwamba movement husika itavunja muungano, na kwamba ni kundi la wasaka tonge??
Tukirudi kwenye hoja ya zitto juu ya UKAWA kuwa na nia ya kuvunja muungano, je ni kwanini zitto alisema hivyo? Ni kwa sababy moja tu, nayo ni kwamba UKAWA uliamua kuungana na wananchi, UKAWA uliamua kuegemea kwenye maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya. Zitto kama mwanachama wa Chadema aliwahi kuunga mkono serikali tatu. Kwa hoja yake kwamba UKAWA utavunja muungano, wakati ukweli ni kwamba moyo wa katiba mpya ni muundo wa Muungano:
· Je tutakuwa tunakosea kusema kwamba zitto alianza kutumika na CCM?
· Je tutakuwa tunakosea kusema kamba ni wazi alikuwa na mpango wa kuivuruga chadema?
Mkiwa kama wafuasi wa zitto, huwa mnaamini sana uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja na kuwasilisha takwimu. Swali kwenu -
Mkandara,
Ritz,
adhurusi et al:
· Je,
Zitto aliposema kwamba hoja ya UKAWA juu ya serikali tatu inalenga kuvunja muungano, Zitto alifanya utafitihuu wapi? Lini? Na alitumia methodology gani kufikia hitimisho hilo?
Mkandara, tafadhali tusaidie katika hili.
Tuangalie masuala mengine muhimu:
Tume ya Nyalali ilikuja na utafiti kupitia kura ya maoni kwamba wananchi walio wengi (80%) walitaka mfumo wa chama kimoja uendelee, huku walio wachache (20%) wakipendelea mfumo wa vyama vingi vya siasa uanzishwe nchini Tanzania. Tatizo ni kwamba wapo wasioelewa kwanini maoni ya wachache yalichukuliwa badala ya maoni ya wengi. Ni hivi - kweli ni kwamba, ukisoma kwa undani juu ya maoni yale (80/20), utagundua mara moja kwamba wananchi walitoa conditions za kuendelea na mfumo wa chama kimoja, conditions ambazo hazingeweza kutekelezeka chini ya chama kimoja, na kuendelea kungangania mfumo huo bila kutekeleza conditions za wananchi, CCM ingekufa mapema zaidi. Mwalimu aliona hilo, hivyo akashauri busara itumike.
Tangia kurudi kwa mfumo wa vyama vingi, CCM imeshindwa kutekeleza mambo mengi sana kwa wananchi, na kufikia hatua kwamba wananchi wengi hivi sasa wamekuwa wakililia sana kuiangusha CCM, hasa ikizingatiwa kwamba kuimarika kwa upinzani (hasa Chadema) kumewapa matumaini mapya. Wakati Chadema ipo katika peak ya mafanikio kuelekea safari hiyo, anatokea kiongozi mmoja wa chadema zitto na kuanza kuvuruga mafanikio hayo. Mara kutoa kauli hii, mara kutoshiriki harakati zile, mifano hai ipo wazi mingi sana. Baada ya kushindwa njam zake ndani ya Chadema, amehamia ACT, chama ambacho wenzake waliotangulia walishaweka wazi tena kwa maandishi kwenye gazeti la Raia Mwema kwamba kunahitajika chama kipya cha upinzani kwenda kupambana na Chadema. Sio na CCM, CUF, NCCR, au vyama vingine, bali CHADEMA.
Katika hali kama hiyo, wananchi wakikutana na wapinzani wa upinzani, wapinzani wanaoifanyia kazi CCM, tena kwa kauli zao wenyewe, kwa maandishi yao wenyewe, kwa vitendo, wananchi hawa wanakatishwa sana tamaa kwani viongozi wa aina ya zitto wanawacheleweshea mageuzi waliyoyatafuta kwa muda mrefu sana, harakati ambazo zimepelekea wengi kupoteza kazi zai, maisha yao, viungo vyao, mali zao, n.k.
Tumalizie kwa kuchambua baadhi ya hoja za Zitto MPYA wa ACT:
1. Siku ya uzinduzi wa ACT Wazalendo,
Zitto alisema kwamba amejiunga na ACT kwa kuwa chama hicho kinaendana na kitu ambacho amekuwa anakipigania kwa miaka yake yote ya kisiasa. Kitu hicho ni maslahi ya taifa.
Mkandara,
Ritz, et al, je ni maslahi yepi hayo ambayo Chadema haikuyapigania?
2. Zitto akazidi kusema kwamba ACT ni chama pekee ambacho kinakubaliana na itikadi na falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea na kwamba chama hicho kimeamua kurudisha Azimio la Arusha, azimio ambalo liliasisiwa na Mwalimu Nyerere.
· Je, itikadi ya Ujamaa ipo kwenye rasimu mpya (tume ya warioba) ya katiba?
· Au ACT imepanga kuja na amendments za katika ikitwaa madaraka?
· Wananchi gani wamesema wanataka kuendelea na ujamaa kama itikadi? Kwa utafiti upi?
· Je, sio sahihi kusema kwamba ACT inaiga ujamaa wa CCM ili iwe rahisi kwa vigogo wa CCM kuhamia ACT bila kuonekana wasaliti wa itikadi ya chama cha mapinduzi? Kumbuka, Ujamaa na mfumo wa muungano wa serikali mbili ndio nguzo kuu za kufanya mwanachama wa ccm aonekane kwamba ni mwaminifu kwa chama cha mapinduzi,
3. Zitto akaendelea kusema kwamba amejiunga na ACT kwa vile ni chama pekee ambacho kinaamini katika uadilifu, chama ambacho pia kimeweka wazi miiko ya maadili ya uongozi na pia kuhakikisha kwamba viongozi wote wa ACT wanakubaliana na hayo na wamesaini juu ya hayo.
· Je kwake yeye, maadili ni nini, kutangaza hadharani mali ulizokuwa nazo? Je hiyo inatosha? Vipi kuhusu kujibu tuhuma za kupokea rushwa, hiyo sio sehemu ya maadili? Zitto hajajibu tuhuma lukuki dhidi yake.
4. Zitto akazidi kusema kwamba kwenye ACT, hakujengwi mtu, badala yake kinajengwa chama. Kinachounganisha wanachama wote wa ACT ni vitu vikuu viwili undugu wao na uzalendo wao.
· Supreme leadership structure inalenga kujenga nini kama sio mtu?
· Kama nguzo kuu za ACT ni ungudu na uzalendo, kwanini Zitto anaenda kinyume na misingi hiyo kwa kuanza kuwagawanya wananchi kwa njia ya ukabila na sehemu walipotoka, hasa Kilimanjaro na Arusha?
5. Zitto akaambia wananchi pia kwamba kati ya mafanikio yake akiwa mbunge, amefanikiwa kuiangusha serikali ya CCM mara nyingi, huku akitaja suala la buzwagi, escrow n.k.
· Kama anamzungumzia Waziri Karamagi, huyu aliondolewa na kashfa ya Buzwagi au Richmond?
· Hoja ya buzwagi iliibuliwa na nani kati yake na gazeti la -----------?
· Sakata la escrow, kati yake na Kafulila, nani ndiye mwasisi wa hoja hii? Kwanini mwishoni aliamua kujiunga na upande wa hoja wa Chenge, ambae alikuwa ni mtuhumiwa?
Kwa kweli, katika hoja zote za Zitto, hakuna hata moja hapo juu ambayo ina ukweli. Vinginevyo,
Ritz,
Mkandara,
adhurusi, tuelimisheni, pengine hatuna ufahamu.
Vinginevyo, tunachosikia kutoka kwenu sana sana ni hoja redundant kwamba Zitto ameonewa, na amehamia ACT kwa sababu amefukuzwa Chadema, hivyo ameenda ACT kusimamia na kupigania maslahi ya taifa.
Ndugu zangu, tukubaliane katika ukweli ufuatao:
· Zitto amejiunga ACT baada ya dhamira yake na wenzake ya usaliti dhidi ya Chadema, kugundulika.
· Zitto amejiunga na ACT kutokana na tuhuma dhidi yake juu ya kuhujumu Chadema kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi.
· Zitto alishtukiwa mapema kwamba alikuwa anatumika kukivuruga chadema. Kwahiyo, kilichomvua uanachama Zitto ni kanuni, taratibu, na katiba ya chadema. Haya ya Kanuni, taratibu, katiba, yote zitto alikuwa anayajua vyema. Na hata siku anaenda mahakamani kuweka pingamizi, alikuwa anajua hatima ya mwanachama kutafuta suluhu mahakamani ni nini, kwamba bila ya kujalisha kama angeshinda au angeshindwa kesi, uanachama wake ulikuwa umefika kikomo.
Maswali kwenu:
· Iwapo Zitto asingefukuzwa Chadema, JE angeondoka na kwenda ACT?0
· Iwapo itikadi na falsafa ya chadema kwake ilikuwa ni tatizo, kwanini aliendelea kutafuta haki mahakamani, haki ndani ya chama ambacho itikadi na falsafa zake haziendani na ndoto yake?