Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Mkuu maswali mengine ni mujaribu sana, sidhani kama matokeo rasmi baada ya uchakachuzi yatakuwa sawa na hitaji lako, bilashaka umeuliza hayo matokeo kwa maksudi fulani
Hapana mkuu mimi nilisema ktk miscalculation za CCM, Dr.Slaa aliondoka CCM baada ya kushindwa na Qorro uchaguzi wa ndani CCM, wao wakarukia na kusema hapana Dr. Slaa alimshinda Qorro lakini CCM wakafanya mizengewe wanaCCM wakamwambia uahamie chama chochote cha Upinzani wakampa kura zao. Mimi nikasema kama hayo ni kweli ebu nipeni hizo takwimu za maoni ya wanaCCM maana najua hakuna kiti hicho. Basi tu hawataki kukubali kwamba Dr.Slaa alihama CCM kutokana na kutoelewana na viongozi wake. Na naweza kuziweka hoja zao hapa ukajisomea mwenyewe..
 
Duh ama kweli kazi tunayo. Nyie na hasa JokaKuu alipinga hoja yangu kwamba Dr.Slaa aliondoka CCM kwa kutoelewana na uongozi (baada ya jina lake kukatwa) na kuhamia Chadema. Yeye anasema Dr.Slaa alimshinda Qorro na wewe ukaongezea kusema Alishinda kura za maoni ila CCM wakamfanyia mizengewe akaaambiwa na wanachama ahamie chama chochote watampa kura zao.

Ndipo nikaulizia takwimu za maoni ya wana CCM jimbo la Karatu yaloonyesha Dr.Slaa alimshinda Qorro! ugumu wa swali hili nini?
Mkuu naona kidogo hali imekuwa dhofla, unachanganya nani kasema nini

Nimehoji, hivi Qorro hakushindwa na kuteuliwa kama mgombea akiwa mshindi wa pili?

Mkuu usi paste maneno, tulizana kabiliana na hoja maana bado tunasubiri hoja na takwimu za supreme.
Huku kwingine ni kama tunatafuna karanga tukikusubiri ulete mlo.
 
Kuna watu huwa wanamjadili Zitto kwa Mahaba yaliyopitiliza bila kufanya tathmini ya kina (Critical Analysis). Huwa wanaijadili ACT kama vile ni NCCR + CUF against CDM, si kweli !. ACT ni genge la vijana wahuni wenye kutaka maisha mazuri kwa haraka ( Lugha nyepesi ni maisha mazuri kwa njia za ujanja ujanja).

Wapo ndugu zetu wengine humu ndani wamejisahaulisha ,wakaweka uwezo wao wa kuchambua mambo wakajivesha mabomu na kuanza kujadili post za fb za vijana wa Suprime leader. Mbaya zaidi wanafanya analysis kwa kutumia likes za fb pale Suprime Leader anapoweka habari zake hewani.

Mnapojadili ACT na huyo Suprime Leader tusisahau takwimu za kura za ubunge alizopata 2005 na 2010. Ukifanya tathmini kwa takwimu utapata majibu pia kwanini Suprime Leader anakimbia kugombea Kigoma .

Mwaka 2005 ulikuwa ni mwaka muhimu kwa siasa za Mkoa wa Kigoma. Huu ni wakati ambapo Jimbo la Kigoma Kaskazini lilimpeleka bungeni kijana wa miaka 29, huyu ni Zitto Kabwe. Zitto alipata ushindi wa asilimia 51.1 uliotokana na kura 28,198 dhidi ya mgombea wa CCM na mbunge aliyekuwa akimaliza muda wake Mayonga Halimenshi aliyepata asilimia 39.6 zilizotokana na kura 21,822.

Mwaka 2010 Zitto aligombea tena, mara hii CCM ikimleta Robinson Fulgence Lembo na CUF ikimsimamisha mgombea mwenye nguvu, Omary Mussa Nkwarulo. Matokeo yalipotangazwa Zitto Kabwe aliwashinda wapinzani wake kwa kupata kura 23,366 (asilimia 48.57), dhidi ya kura 18,352 (asilimia 38.15) za Fulgence wa CCM, huku Nkwarulo wa CUF akipata kura 4,839 (asilimia 10.06). Ukitizama utaona kuwa ushindi wa Zitto ulikuwa ukiporomoka kwa kasi kubwa, ulishuka kwa asilimia tatu ( Kura takribani 5000 zilipotea) ukilinganisha na ule wa mwaka 2005.

Sio lengo langu kubadili mada ila ACT ni Zitto bila Zitto hakuna ACT.
 
By JokaKuu Mkandara,

..naomba nikusahihishe kidogo.

..Dr.Slaa alishinda ktk kura za maoni za CCM huko Karatu.

..sasa CCM wakamfanyia mzengwe kwa kukata jina lake na kumpa ushindi mgombea aliyeshika nafasi ya pili.

..wananchi waliokuwa wakimuunga mkono Dr.Slaa wakamwelekeza achague chama kingine watamuunga mkono. Dr akahamia CDM and the rest is history.

..Dr.Slaa hakupewa nafasi za uongozi haraka kama ulivyoeleza. alikaa bungeni na michango yake mle ndiyo iliyopelekea yeye kupewa nafasi za uongozi CDM.

..pamoja na hayo, huyu mzee wa watu ana uwezo na ni mpambanaji kwelikweli. hakuna shaka kwamba ametoa mchango mkubwa sana ktk kuijenga CDM.[/QUOTE Mkandara ukiangalia profile yake yupo kuanzia
Dah mkuu wangu ama kweli sikuwezi. haya rudi kasome bandiko lako la #655 na kule kwenye Duru - Matukio ya Dunia, soma umeandika nini sitopenda kuweka vitu ambavyo unajua umekosea sasa unatafuta pa kutokea...
 
Haya na hilo jibu lake la pili ktk marekebisho yake akidai Dr. Slaa hakupanda haraka ukweli huu hapa na kutoka site ya Chadema:-

POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
CHADEMA Secretary General 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu
Constituency) 1995 Todate
CHADEMA Member of National Executive
Committee 1995 –

Chama Cha Mapinduzi – CCM Secretary Foreign Branch(Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
 
Ok, nafasi ya vice na katibu mkuu inapatikanaje? Hebu nikumbushe maana sijui katiba yao inasemaje
 
Kuna watu huwa wanamjadili Zitto kwa Mahaba yaliyopitiliza bila kufanya tathmini ya kina (Critical Analysis). Huwa wanaijadili ACT kama vile ni NCCR + CUF against CDM, si kweli !. ACT ni genge la vijana wahuni wenye kutaka maisha mazuri kwa haraka ( Lugha nyepesi ni maisha mazuri kwa njia za ujanja ujanja).

Wapo ndugu zetu wengine humu ndani wamejisahaulisha ,wakaweka uwezo wao wa kuchambua mambo wakajivesha mabomu na kuanza kujadili post za fb za vijana wa Suprime leader. Mbaya zaidi wanafanya analysis kwa kutumia likes za fb pale Suprime Leader anapoweka habari zake hewani.

Mnapojadili ACT na huyo Suprime Leader tusisahau takwimu za kura za ubunge alizopata 2005 na 2010. Ukifanya tathmini kwa takwimu utapata majibu pia kwanini Suprime Leader anakimbia kugombea Kigoma .

Mwaka 2005 ulikuwa ni mwaka muhimu kwa siasa za Mkoa wa Kigoma. Huu ni wakati ambapo Jimbo la Kigoma Kaskazini lilimpeleka bungeni kijana wa miaka 29, huyu ni Zitto Kabwe. Zitto alipata ushindi wa asilimia 51.1 uliotokana na kura 28,198 dhidi ya mgombea wa CCM na mbunge aliyekuwa akimaliza muda wake Mayonga Halimenshi aliyepata asilimia 39.6 zilizotokana na kura 21,822.

Mwaka 2010 Zitto aligombea tena, mara hii CCM ikimleta Robinson Fulgence Lembo na CUF ikimsimamisha mgombea mwenye nguvu, Omary Mussa Nkwarulo. Matokeo yalipotangazwa Zitto Kabwe aliwashinda wapinzani wake kwa kupata kura 23,366 (asilimia 48.57), dhidi ya kura 18,352 (asilimia 38.15) za Fulgence wa CCM, huku Nkwarulo wa CUF akipata kura 4,839 (asilimia 10.06). Ukitizama utaona kuwa ushindi wa Zitto ulikuwa ukiporomoka kwa kasi kubwa, ulishuka kwa asilimia tatu ( Kura takribani 5000 zilipotea) ukilinganisha na ule wa mwaka 2005.

Sio lengo langu kubadili mada ila ACT ni Zitto bila Zitto hakuna ACT.
Mkuu , huu ujanja ujanja unaouzungumzia ndio tunaukataa na kuwafumbulia Watanzania kile kinachoonekana kama kitendawili au mauza uza

Supreme na genge waliaminisha umma, demokrasia ni ushindani, ni njia huru.

Wenye mahaba wakasema hakukuwa na tatizo supreme kuonyesha nia ya Urais wakati mgombea wake akijinadi n.k.
Ghafla mauza uza yakaaza. Within 24hr kabla ya mkutano mkuu, ikachiupuka nafasi ya u-supreme kutoka kuzimu.

Supreme akasimamishwa bila mtu. Afadhali ya CCM waliokuwa wanasimamisha mtu na kivuli, hili la supreme ilikuwa direct kick hakuna golikipa. Tukahoji, jamani wenzetu mbona mlisema demokrasia inakuwa ABCD sasa kwanini mwatenda EFCG?

Waraka ulitetewa na wanaMhaba, mkakati wa ushindi na si uhuni. Huko walikwokwenda kupora chama cha watu, hakukuwa na waraka, ilikuwa jino kwa jino. Tukauliza, mkakati mbona haufanyi kazi huko mahala tulivu?

WanaMahaba wakasema hakuna kosa kutia nia ya Urais hata kama unamgombea.
Tulipohoji, wakasema mbona Mrema alipigia CCM debe(CCM haishikiki)?
Tukauliza, wenzetu tunazungumzia huko mlikopora chama ! tunaitwa wenye chuki

Umma ukaanishwa, supreme anakwaza na ukanda. CCM wakachukua na kuifanya agenda wakichochea na udini.
Wiki zilizopita CCM wakaonekana walisingiziwa tu, wenye agenda wakajitokeza.

Wakatumia meneno matamu kuonyesha uporaji wa kanda moja dhidi ya nyingine.

Haa! wenzetu si mlituambia kuna ukanda mlikotoka? Mbona nyinyi mnahubiri kwa jasho na takwimu?

Tuleteeni takwimu tuone ukweli, WanaMahaba wakakimbia.
Tunaona wanarudi kinyemela kama unyemela wa kuingiza nafasi ya supreme wakaituondoa katika mada

Walituaminisha, katiba haichezewi! ni dhambi kubwa. Kuna vifungu vimeingizwa kupitia mlango wa uani.
Tukasema hiyo haifai tunakemea. Tukauliza lakini si nanyi mlikuwemo? Wakajibu hapana, walikuwa na waraka

Haa! tunashangaa ghafla bila kujua, tunasikia 'ladies and jandomen, We present to you the one and the only supreme leader!
Masaa 24 political landscape ikabadilika kabisa, katiba ikanyakuliwa kutoka kwa wanachama ikawa ya supreme

Tukaambiwa, hakuna shida kula sahani moja na kijani njano.

Supreme akawa na waziri wa CCM wakishambulia kanda ya kaskazini kwa jitihada zao za kujiletea maendeleo.

Wakawananga wananchi wa mikoa husika tukiambiwa siasa haina adui wa kudumu( ACT/CCM dhidi ya kanda ya kaskazini)

Nyuma ya pazia, mwenyekiti wa ACT anasema 'ukitaja UKAWA tu kwa ulimi wako' na ikatihibitika pasi shaka mi ulimi wako, utakuwa umejivua uanachama. Tukauliza wenzetu, vipi mbona mnatuacha njia panda?

Wakaendelea kutuaminisha wamekuja kizalendo, uchu na uchungu wa kulikomboa taifa. Taifa kwanza.

Nyuma ya pazia supreme anasema, majimbo anayotamani ni yale ya upinzania.
Katibu mkuu wake akisema kanda ya pwani lazima wawafumue CUF, na supreme akimalizia NCCR wafunge virago Kigoma

Tukauliza, wenzetu kwani tatizo lililotufikisha hapa tulipo ni upinzani au ni CCM.

WanaMahaba wakatujibu lazima kwanze uanze na ''soft spot'' huko kwa CCM baadaye.
Kwamba, CCM iendelee endelee hadi watakaposhika nguvu! Ndio tukahoji, hivi huu si mpini kweli!

Unaona jinsi CCM walivyopumua na kujipanga kuliangamiza taifa kwa miaka mingine, kazi zao wanafanya 'wazalendo''

Orodha ni ndefu Mwakalinga, ni ujanja ujanja wa mjini tu! Hapana, inatosha, hatuwezi kuiacha nchi ikifanywa punching bag, CCM wanapiga kutoka kushoto, ACT wanakinga bag lisiyumbe. Mh mh, huu ni mpini na ni hatari kwa ustawi wa taifa

WanaMahaba wamekimbia na takwimu za supreme leader. Hawataki kzungumzia kauli ya supreme na ACT ya kulimega taifa katika kanda kama Nigeria au Somalia. Wanatafuta vi mada wanachomeka, wakipewa hoja wanakimbia.

Tutadai takwimu tu, watake wasitake. Tutadai watuambie supreme amelenga nini kwa kauli za kulibomoa taifa kikanda

Tukikaa kimya, tutalisaliti taifa! hatuwezi kamwe!
 
Ok, nafasi ya vice na katibu mkuu inapatikanaje? Hebu nikumbushe maana sijui katiba yao inasemaje
Nguruvi ndugu yangu, sasa imekuwa ya Katibu mkuu wakati nimesema alipanda ngazi ya uongozi haraka iweje urukie katibu wakati alianza kuwa Makamu wa Mwenyekiti 1998 miaka mitatu tu baada ya kujiunga. Aliingia Kamati kuu mara tu baada ya kuchukua Karatu. Iweje uchague lilokuwa mbali ukaacha ya karibu wakati huko nyuma umefanya upotoshaji wa nguvu juu ya bandiko langu.

Nia na lengo langu toka mwanzo ilikuwa kuonyesha jinsi chama kinavyoweza fanya miscalculation zake wakidhani wamemshusha mtu kumbe ndio wamempaisha. Sikuwa na maana mbaya lakini mlivyokuja kama kwamba nasema Uongo maneno mengi wakati ukweli upo wazi kabisa.
 
Dr.Slaa aliondoka CCM baada ya kushindwa na Qorro uchaguzi wa ndani CCM, wao wakarukia na kusema hapana Dr. Slaa alimshinda Qorro....

Basi tuseme upo sahihi, tunaomba utuwekee hapa takwimu zako kudhibitisha ushindi wa Patrick Qorro dhidi ya Dr. Slaa kura za maoni CCM 1995 jimbo la Karatu.

Vinginevyo tukiangalia the big picture, Qorro lost twice to Slaa kupitia kura za wananchi wa Jimbo la Karatu. Thats the bottom line.
 
Nguruvi ndugu yangu, sasa imekuwa ya Katibu mkuu wakati nimesema alipanda ngazi ya uongozi haraka iweje urukie katibu wakati alianza kuwa Makamu wa Mwenyekiti 1998 miaka mitatu tu baada ya kujiunga. Aliingia Kamati kuu mara tu baada ya kuchukua Karatu. Iweje uchague lilokuwa mbali ukaacha ya karibu wakati huko nyuma umefanya upotoshaji wa nguvu juu ya bandiko langu.

Nia na lengo langu toka mwanzo ilikuwa kuonyesha jinsi chama kinavyoweza fanya miscalculation zake wakidhani wamemshusha mtu kumbe ndio wamempaisha. Sikuwa na maana mbaya lakini mlivyokuja kama kwamba nasema Uongo maneno mengi wakati ukweli upo wazi kabisa.
Nilielewa kuwa ulilenga kuonyesha jinsi Slaa alivyopaa kuwa 'supreme' akama supreme alivyokwea ngazi kutoka nowhere na kuwa supreme. Anyway hilo liishe

Vipi umefanikiwa kupata takwimu alizotumia supreme leader kule Mwanza na Shinyanga?
 
Hapana mkuu mimi nilisema ktk miscalculation za CCM, Dr.Slaa aliondoka CCM baada ya kushindwa na Qorro uchaguzi wa ndani CCM, wao wakarukia na kusema hapana Dr. Slaa alimshinda Qorro lakini CCM wakafanya mizengewe wanaCCM wakamwambia uahamie chama chochote cha Upinzani wakampa kura zao. Mimi nikasema kama hayo ni kweli ebu nipeni hizo takwimu za maoni ya wanaCCM maana najua hakuna kiti hicho. Basi tu hawataki kukubali kwamba Dr.Slaa alihama CCM kutokana na kutoelewana na viongozi wake. Na naweza kuziweka hoja zao hapa ukajisomea mwenyewe..

Nilisema hapo awali kuwa kwenye siasa unaruhusiwa kusema kauongo lakini kauongo kawe na mfananofanano na ukwelli.. Sasa wewe unachotaka kutuaminishwa ni kuwa Dr. Slaa alishindwa na Qorro kweli? Hivi kaka yangu umeshindwa hata ku"google" tu mbona ni kitu cha sekunde? Ni kweli hakuna idadi ya kura si kwa Jokakuu tu bali hata wewe nikikwambia leta hudhibitisho kuwa Qorro alimshinda Dr. Slaa huna.

Pamoja na hayo nimeleta ushahidi husio na takwimu kutoka kwa Mh. Wasira

alivyosema tarehe 19. Nov 2014 mjini Arusha nanukuu
"CCM Mkoa wa Arusha ina historia ya kupoteza uchaguzi kutokana na mgawanyiko unaosababishwa na matokeo au mchakato wa kura za maoni. Mwaka 1995, Jimbo la Karatu lilinyakuliwa na Chadema kupitia Dk Willibrod Slaa baada ya vikao vya uteuzi kupuuza maoni ya wananchi kupitia kura za maoni kwa kumteua Patrick Quorro badala Dk Slaa aliyeshinda kura za maoni."

Chanzo Wasira: Ubora wa mgombea muhimu kuliko chama 2015

Pia hapa kuna maoni ya Prof. Kitila Mkumbo katika gazeti la Raia mwema la tarehe 29.Oct.2014 anasema hivi "
Kisiasa, tunaweza kusema Dk. Slaa ni zao la ujinga na ubabe wa viongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Aliingia rasmi katika siasa za kitaifa mwaka 1995 alipogombea ubunge kupitia CCM na kushinda kura za maoni lakini jina lake liliondolewa kwa kile ambacho yeye anakieleza kwamba “jina liliondolewa kimizengwe kwa msingi kwamba hakuwa mwenzao”.
Baada ya kunyang’anywa ushindi wake katika kura za maoni, Dk. Slaa aligombea kupitia CHADEMA na kushinda. Alikuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfufulizo kutoka mwaka 1995 hadi mwaka 2010 alipogombea urais

- See more at: Raia Mwema - Dk Willibrod Peter Slaa: Muadilifu na mchapa kazi mwenye nakisi ya hekima na weledi

Hao na wengine wengi tu kama uki"google" wanaelezea kitu kile kile alichoelezea Jokakuu.. Sasa sijui unataka nini ili uamini kuwa Dr. Slaa alishinda kura za maoni na si Qorro?
 
Basi tuseme upo sahihi, tunaomba utuwekee hapo takwimu zako kudhibitisha ushindi wa Patrick Qorro dhidi ya Dr. Slaa kura za maoni CCM 1995 jimbo la Karatu.
Alaaa sasa imekuwa mimi? jamani mseme nyie hamna jibu mnataka mimi niwape kura za maoni? Watu wanazua mengi tu mkuu kwanza fahamu hii habari ya kura za maoni ya wanachama ilianza lini? 1995 Ndio uchaguzi wa kwanza wanachama wengi walikuwa CCM na wachache NCCR wangeweza vipi kuchukua maoni ya wanachama wa CCM wakati ule hata mfumo wenyewe bado. Watanzania kwa usanii achana nao..
 
Alaaa sasa imekuwa mimi? jamani mseme nyie hamna jibu mnataka mimi niwape kura za maoni? Watu wanazua mengi tu mkuu kwanza fahamuhii habari ya kura za maoni ya wanachama ilianza lini? 1995 Ndio uchaguzi wa kwanza karibu wanachamai wengi walikuwa CCM na wachache NCCR wangeweza vipi kuchukua maoni ya wananchama wakati ule. Watanzania kwa usanii achana nao..

Mkandara nisome hapo juu.. Swala la kura ya 1195 lilikuwepo na ndo unaona hata Wasira analalamika jinsi CCM walivyovurunda hasa kwa Karatu ni kitu ambacho CCM wanakijutia mpaka leo.
 
Nilisema hapo awali kuwa kwenye siasa unaruhusiwa kusema kauongo lakini kauongo kawe na mfananofanano na ukwelli.. Sasa wewe unachotaka kutuaminishwa ni kuwa Dr. Slaa alishindwa na Qorro kweli? Hivi kaka yangu umeshindwa hata ku"google" tu mbona ni kitu cha sekunde? Ni kweli hakuna idadi ya kura si kwa Jokakuu tu bali hata wewe nikikwambia leta hudhibitisho kuwa Qorro alimshinda Dr. Slaa huna.

Pamoja na hayo nimeleta ushahidi husio na takwimu kutoka kwa Mh. Wasira

alivyosema tarehe 19. Nov 2014 mjini Arusha nanukuu
"CCM Mkoa wa Arusha ina historia ya kupoteza uchaguzi kutokana na mgawanyiko unaosababishwa na matokeo au mchakato wa kura za maoni. Mwaka 1995, Jimbo la Karatu lilinyakuliwa na Chadema kupitia Dk Willibrod Slaa baada ya vikao vya uteuzi kupuuza maoni ya wananchi kupitia kura za maoni kwa kumteua Patrick Quorro badala Dk Slaa aliyeshinda kura za maoni."

Chanzo Wasira: Ubora wa mgombea muhimu kuliko chama 2015

Pia hapa kuna maoni ya Prof. Kitila Mkumbo katika gazeti la Raia mwema la tarehe 29.Oct.2014 anasema hivi "
Kisiasa, tunaweza kusema Dk. Slaa ni zao la ujinga na ubabe wa viongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Aliingia rasmi katika siasa za kitaifa mwaka 1995 alipogombea ubunge kupitia CCM na kushinda kura za maoni lakini jina lake liliondolewa kwa kile ambacho yeye anakieleza kwamba "jina liliondolewa kimizengwe kwa msingi kwamba hakuwa mwenzao".
Baada ya kunyang'anywa ushindi wake katika kura za maoni, Dk. Slaa aligombea kupitia CHADEMA na kushinda. Alikuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfufulizo kutoka mwaka 1995 hadi mwaka 2010 alipogombea urais

- See more at: Raia Mwema - Dk Willibrod Peter Slaa: Muadilifu na mchapa kazi mwenye nakisi ya hekima na weledi

Hao na wengine wengi tu kama uki"google" wanaelezea kitu kile kile alichoelezea Jokakuu.. Sasa sijui unataka nini ili uamini kuwa Dr. Slaa alishinda kura za maoni na si Qorro?
Anafahamu wazi nani alishinda. Anachotaka ni kwa kura ngapi, hatujui kama hilo linaweza kubadili mwelekeo wa hoja kwa namna yoyote.

Hapa ni kuendeleza kamjadala ka pembeni,tunamsubiri akimaliza atuletee takwimu alizotumia supreme leader kule Mwanza/Shinyanga. Mkandara yupo katika rekodi akizungumzia suala hilo halina makosa na ni ukweli tu.

Aliomba takwimu, Mchambuzi kazimwaga! tukaambia zimetoka katika makabarasha yaliyoliwa na panya.

Sasa mpira upo kwake, tunaomba takwimu za supreme leader kuthibitisha uporaji unaofanywa na kanda ya kaskazini dhidi ya kanda ya Ziwa au kati au yoyote ile
 
Alaaa sasa imekuwa mimi? jamani mseme nyie hamna jibu mnataka mimi niwape kura za maoni? Watu wanazua mengi tu mkuu kwanza fahamu hii habari ya kura za maoni ya wanachama ilianza lini?

Mkuu, unasimamia wapi? Je unatuambia kwamba mwaka 1995 hapakuwa na utaratibu wa kura ya maoni? Au unatuambia kwamba Qorro alimshinda Slaa kura ya maoni 1995?

1995 Ndio uchaguzi wa kwanza wanachama wengi walikuwa CCM na wachache NCCR wangeweza vipi kuchukua maoni ya wanachama wa CCM wakati ule hata mfumo wenyewe bado. Watanzania kwa usanii achana nao..

Kwahiyo kura ya maoni ilianza 2000? 2005? 2010?

Na vipi kuhusu hoja za Alinda #691
 
Mkandara nisome hapo juu.. Swala la kura ya 1195 lilikuwepo na ndo unaona hata Wasira analalamika jinsi CCM walivyovurunda hasa kwa Karatu ni kitu ambacho CCM wanakijutia mpaka leo.
Sio kweli, sisi wenyewe tulikuwa CCM, Kila jimbo vikao vya chama walipendekeza majina mawili halafu, makao makuu wanachagua moja kati yao. Jina linalorudi ndilo linapewa dhamana ya chama.

CCM kwa miaka yote wamechukua mfumo wa MTU Anayekubalika kwa mtazamo wa makao makuu kama wanavyotaka kufanya UKAWA. Hii ndio hoja yangu mimi kuwa Kamati kuu inaweza fanya makosa ya kudhani mtu fulani sio Jembe kumbe ndio akawamaliza na Dr.Slaa ni mfano bora kabisa.
 
Nguruvi ndugu yangu, sasa imekuwa ya Katibu mkuu wakati nimesema alipanda ngazi ya uongozi haraka iweje urukie katibu wakati alianza kuwa Makamu wa Mwenyekiti 1998 miaka mitatu tu baada ya kujiunga. Aliingia Kamati kuu mara tu baada ya kuchukua Karatu. Iweje uchague lilokuwa mbali ukaacha ya karibu wakati huko nyuma umefanya upotoshaji wa nguvu juu ya bandiko langu.

Nia na lengo langu toka mwanzo ilikuwa kuonyesha jinsi chama kinavyoweza fanya miscalculation zake wakidhani wamemshusha mtu kumbe ndio wamempaisha. Sikuwa na maana mbaya lakini mlivyokuja kama kwamba nasema Uongo maneno mengi wakati ukweli upo wazi kabisa.

Mzee mwenzangu kwa heshima uliyonayo humu jamvini wakati mwingine naogopa kupingana na wewe. Hoja ya ndugu yetu Nguruvi3 ni kwambwa Kina Mkumbo walikimbia CDM (walijifukuzisha) kutokana na mfumo kandamizi wa kupeana vyeo (kama unavyotoa mfano wa Dr. Slaa-kwa tafsri yako).

Hoja ni kwamba kwanini wanafanya waliyoyapinga CDM!
Ndio maana nawaona kama Genge la wahuni.
 
Last edited by a moderator:
Sio kweli, sisi wenyewe tulikuwa CCM, Kila jimbo vikao vya chama walipendekeza majina mawili halafu, makao makuu wanachagua moja kati yao. Jina linalorudi ndilo linapewa dhamana ya chama.
Baada ya CCM mkaenda wapi? Na leo mpo wapi?

CCM kwa miaka yote wamechukua mfumo wa MTU Anayekubalika kwa mtazamo wa makao makuu kama wanavyotaka kufanya UKAWA. Hii ndio hoja yangu mimi kuwa Kamati kuu inaweza fanya makosa ya kudhani mtu fulani sio Jembe kumbe ndio akawamaliza na Dr.Slaa ni mfano bora kabisa.
Alinda kajadili hilo, tunasubiri counter argument yenye mashiko. Vinginevyo kwa hoja hii, maana yako ni kwamba Dr Slaa alimshinda Qorro kwa vigezo vyote.
 
Mkuu, unasimamia wapi? Je unatuambia kwamba mwaka 1995 hapakuwa na utaratibu wa kura ya maoni? Au unatuambia kwamba Qorro alimshinda Slaa kura ya maoni 1995?

Kwahiyo kura ya maoni ilianza 2000? 2005? 2010?

Na vipi kuhusu hoja za Alinda #691
Nimesema hapakuwa na kura za maoni ya WANACHAMA wa CCM 1995 kwa mgombea Ubunge. Kama Wasira kasema hivyo na Dr. Kitila waombeni hizo kura za maoni za majina yalopitishwa na wananchi kwa kila jimbo. Sii lazima zitakuwepo?.. Leo hii mimi naweza kuzua haya haya juu ya Zitto na Mbowe miaka ijayo na watu wakaamini ya kwamba Zitto alikubalika Chadema kuliko Mbowe ktk kinyang'anyiro cha Mwenyekiti.

Ukweli ni kwamba Jina la Dr.Slaa lilikatwa kama walivyokatwa wengine ktk Uchaguzi iwe wa wabunge au rais ama uchaguzi nyinginezo kabla ya kuwafikia wanachama au wananchi..Unajua kuna watu wanaamini hata uchaguzi wa JK umetokana na kura za maoni ya wanachama 2005.
 
Nimesema hapakuwa na kura za maoni ya WANACHAMA 1995. Kama Wasira kasema hivyo na Dr. Kitila waombeni hizo kura za maoni yalopitishwa na wananchi kwa kila jimbo. Sii lazima zitakuwepo?.. Leo hii mimi naweza kuzua haya haya juu ya Zitto na Mbowe miaka ijayo na watu wakaamini ya kwamba Zitto alikubalika Chadema kuliko Mbowe ktk kinyang'anyiro cha Mwenyekiti.

Ukweli ni kwamba Jina la Dr.Slaa lilikatwa kama walivyokatwa wengine ktk Uchaguzi wa rais ama uchaguzi nyinginezo kabla ya kuwafiia wanacham au wananchi..Unajua kuna watu wanaamini hata uchaguzi wa JK umetokana na kuza za maoni ya wananchi..

Unataka kutulaghai hapa. Hivi unajua maana ya dhana ya "kura ya maoni"? Kura hii ilikuwepo 1995 na hata kabla, tofauti ni kwamba composition ya vikao vya maamuzi ilikuwa sio kama ya leo hii ambapo chama kimejaribu kupanua zaidi wigo wa demokrasia.
 
Back
Top Bottom