Kuna watu huwa wanamjadili Zitto kwa Mahaba yaliyopitiliza bila kufanya tathmini ya kina (Critical Analysis). Huwa wanaijadili ACT kama vile ni NCCR + CUF against CDM, si kweli !. ACT ni genge la vijana wahuni wenye kutaka maisha mazuri kwa haraka ( Lugha nyepesi ni maisha mazuri kwa njia za ujanja ujanja).
Wapo ndugu zetu wengine humu ndani wamejisahaulisha ,wakaweka uwezo wao wa kuchambua mambo wakajivesha mabomu na kuanza kujadili post za fb za vijana wa Suprime leader. Mbaya zaidi wanafanya analysis kwa kutumia likes za fb pale Suprime Leader anapoweka habari zake hewani.
Mnapojadili ACT na huyo Suprime Leader tusisahau takwimu za kura za ubunge alizopata 2005 na 2010. Ukifanya tathmini kwa takwimu utapata majibu pia kwanini Suprime Leader anakimbia kugombea Kigoma .
Mwaka 2005 ulikuwa ni mwaka muhimu kwa siasa za Mkoa wa Kigoma. Huu ni wakati ambapo Jimbo la Kigoma Kaskazini lilimpeleka bungeni kijana wa miaka 29, huyu ni Zitto Kabwe. Zitto alipata ushindi wa asilimia 51.1 uliotokana na kura 28,198 dhidi ya mgombea wa CCM na mbunge aliyekuwa akimaliza muda wake Mayonga Halimenshi aliyepata asilimia 39.6 zilizotokana na kura 21,822.
Mwaka 2010 Zitto aligombea tena, mara hii CCM ikimleta Robinson Fulgence Lembo na CUF ikimsimamisha mgombea mwenye nguvu, Omary Mussa Nkwarulo. Matokeo yalipotangazwa Zitto Kabwe aliwashinda wapinzani wake kwa kupata kura 23,366 (asilimia 48.57), dhidi ya kura 18,352 (asilimia 38.15) za Fulgence wa CCM, huku Nkwarulo wa CUF akipata kura 4,839 (asilimia 10.06). Ukitizama utaona kuwa ushindi wa Zitto ulikuwa ukiporomoka kwa kasi kubwa, ulishuka kwa asilimia tatu ( Kura takribani 5000 zilipotea) ukilinganisha na ule wa mwaka 2005.
Sio lengo langu kubadili mada ila ACT ni Zitto bila Zitto hakuna ACT.
Mkuu , huu ujanja ujanja unaouzungumzia ndio tunaukataa na kuwafumbulia Watanzania kile kinachoonekana kama kitendawili au mauza uza
Supreme na genge waliaminisha umma, demokrasia ni ushindani, ni njia huru.
Wenye mahaba wakasema hakukuwa na tatizo supreme kuonyesha nia ya Urais wakati mgombea wake akijinadi n.k.
Ghafla mauza uza yakaaza. Within 24hr kabla ya mkutano mkuu, ikachiupuka nafasi ya u-supreme kutoka kuzimu.
Supreme akasimamishwa bila mtu. Afadhali ya CCM waliokuwa wanasimamisha mtu na kivuli, hili la supreme ilikuwa direct kick hakuna golikipa. Tukahoji, jamani wenzetu mbona mlisema demokrasia inakuwa ABCD sasa kwanini mwatenda EFCG?
Waraka ulitetewa na wanaMhaba, mkakati wa ushindi na si uhuni. Huko walikwokwenda kupora chama cha watu, hakukuwa na waraka, ilikuwa jino kwa jino. Tukauliza, mkakati mbona haufanyi kazi huko mahala tulivu?
WanaMahaba wakasema hakuna kosa kutia nia ya Urais hata kama unamgombea.
Tulipohoji, wakasema mbona Mrema alipigia CCM debe(CCM haishikiki)?
Tukauliza, wenzetu tunazungumzia huko mlikopora chama ! tunaitwa wenye chuki
Umma ukaanishwa, supreme anakwaza na ukanda. CCM wakachukua na kuifanya agenda wakichochea na udini.
Wiki zilizopita CCM wakaonekana walisingiziwa tu, wenye agenda wakajitokeza.
Wakatumia meneno matamu kuonyesha uporaji wa kanda moja dhidi ya nyingine.
Haa! wenzetu si mlituambia kuna ukanda mlikotoka? Mbona nyinyi mnahubiri kwa jasho na takwimu?
Tuleteeni takwimu tuone ukweli, WanaMahaba wakakimbia.
Tunaona wanarudi kinyemela kama unyemela wa kuingiza nafasi ya supreme wakaituondoa katika mada
Walituaminisha, katiba haichezewi! ni dhambi kubwa. Kuna vifungu vimeingizwa kupitia mlango wa uani.
Tukasema hiyo haifai tunakemea. Tukauliza lakini si nanyi mlikuwemo? Wakajibu hapana, walikuwa na waraka
Haa! tunashangaa ghafla bila kujua, tunasikia 'ladies and jandomen, We present to you the one and the only supreme leader!
Masaa 24 political landscape ikabadilika kabisa, katiba ikanyakuliwa kutoka kwa wanachama ikawa ya supreme
Tukaambiwa, hakuna shida kula sahani moja na kijani njano.
Supreme akawa na waziri wa CCM wakishambulia kanda ya kaskazini kwa jitihada zao za kujiletea maendeleo.
Wakawananga wananchi wa mikoa husika tukiambiwa siasa haina adui wa kudumu( ACT/CCM dhidi ya kanda ya kaskazini)
Nyuma ya pazia, mwenyekiti wa ACT anasema 'ukitaja UKAWA tu kwa ulimi wako' na ikatihibitika pasi shaka mi ulimi wako, utakuwa umejivua uanachama. Tukauliza wenzetu, vipi mbona mnatuacha njia panda?
Wakaendelea kutuaminisha wamekuja kizalendo, uchu na uchungu wa kulikomboa taifa. Taifa kwanza.
Nyuma ya pazia supreme anasema, majimbo anayotamani ni yale ya upinzania.
Katibu mkuu wake akisema kanda ya pwani lazima wawafumue CUF, na supreme akimalizia NCCR wafunge virago Kigoma
Tukauliza, wenzetu kwani tatizo lililotufikisha hapa tulipo ni upinzani au ni CCM.
WanaMahaba wakatujibu lazima kwanze uanze na ''soft spot'' huko kwa CCM baadaye.
Kwamba, CCM iendelee endelee hadi watakaposhika nguvu! Ndio tukahoji, hivi huu si mpini kweli!
Unaona jinsi CCM walivyopumua na kujipanga kuliangamiza taifa kwa miaka mingine, kazi zao wanafanya 'wazalendo''
Orodha ni ndefu Mwakalinga, ni ujanja ujanja wa mjini tu! Hapana, inatosha, hatuwezi kuiacha nchi ikifanywa punching bag, CCM wanapiga kutoka kushoto, ACT wanakinga bag lisiyumbe. Mh mh, huu ni mpini na ni hatari kwa ustawi wa taifa
WanaMahaba wamekimbia na takwimu za supreme leader. Hawataki kzungumzia kauli ya supreme na ACT ya kulimega taifa katika kanda kama Nigeria au Somalia. Wanatafuta vi mada wanachomeka, wakipewa hoja wanakimbia.
Tutadai takwimu tu, watake wasitake. Tutadai watuambie supreme amelenga nini kwa kauli za kulibomoa taifa kikanda
Tukikaa kimya, tutalisaliti taifa! hatuwezi kamwe!