Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Alinda:

Ufafanuzi: nadhani katika posti yangu nimesema unachukia, sijasema unamchukia mkenya au unawachukia wakenya. Kuchukia na kuwachukia ni vitu viwili tofauti japokuwa shina la neno ni moja. Kuna watanzania wengi wanachukia nafasi za kazi kuchukuliwa na wageni lakini hawachukii wageni wenye nafasi hizo.

Kabla hatujasonga mbele ni lazima tusawazishe hii sintofahmu, hivyo basi bado nasisitiza hakuna sehemu nilipoandika neno "chuki" iwe kwa wakenya au kwa nafasi za kazi zinazochukuliwa na wakenya.. SIjaandika kitu cha namna hii kama papo nionyeshe.. Niko radhi kuomba msamaha.

Ritz Inawezekana kabisa alisema hivyo, Ila kwa bahati mbaya sikuweza kusiliza hiyo RFA au youtube. Ila hapa kinachojadiliwa ni kitu alichoandika mwenyewe na kutaka watu tujadlili..

Waweza kwenda katika kwenda kwenye Facebook yake.. Ndo nimetoa kila kitu huko... Na katika kuweka msititizo kitu cha kujadili ndo alikuja na hayo maandishi "

Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7."

Hayo si maneno yangu au ya mwana ukumbi yeyote ni maneno ya Zitto katika Facebook wall yake..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu , hayo unayosema ndiyo yangewezesha taifa kusongambele.

Shinyanga na Mwanza wakifanikiwa taifa ,imefanikiwa.

CCM haijawezakutumia fursa hizo, Supreme leader anaona wananchi wa K’njaro na Arusha ndiotatizo

Frustration zake haziwezi kuvumiliwa akitumbukiza chuki naubinafsi. Zitakemewa.
Siasa za ulaghai hapana
Mkuu tupanue mnakasha kidogo msome kiduchu mwanaukumbi mwenzetu.

NasDaz
Unaelekea hauna ufahamu wa masuala ya kiuchumi na matokeo yake umetaka kutafsiri hoja hiyo ya-Zitto-kisiasa... inaelekea unadhani anai-dis CHADEMA, kwamba, kwavile inahusishwa na Mkoa wa Kilimanjaro lakini bado mkoa huo una mchango mdogo katika pato la taifa! Nature ya Mkoa wa Kilimanjaro na aina ya watu wake inashawishi hali hiyo kutokea na kwa maana nyingine, shughuli za kiuchumi kwa Mkoa wa Kilimanjaro zina direct effect kwa watu wake. Ukitoa Mlima K'njaro, sidhani kama Mkoa una mradi mkubwa wa kitaifa kama ilivyo kwa machimbo ya madini! Lakini pamoja na kutokuwa na miradi mikubwa ya kitaifa, watu wake ni wahangaikaji, watafuta pesa ambazo largely zina-affect mifuko yao kwa kuwa ni shughuli binafsi!Kimsingi, hoja ya Zitto hapo ni kwamba, mfumo wetu wa uchumi hauna direct positive effect kwa wananchi wake na ndio maana, mkoa kama Shinyanga pamoja na kuchangia asilimia kubwa ya pato la taifa lakini maendeleo ya watu wake bado ni duni... hii ikionesha wazi kwamba there's no multiplier effect kwenye sekta ya madini! Katika mazingira ya kawaida, kwenye fairness in economic activities, basi ingetarajiwa kwamba, Shinyanga iwe na maendeleo makubwa zaidi ya watu wake kuliko Lindi ambayo contribution yake kwenye pato la taifa is only 1.89%! Hii maana yake ni nini? Kumbe Lindi pamoja na kuchangia kidogo sana kwenye GDP lakini shughuli za kiuchumi mkoani humo zina direct effect kwa wananchi wa kawaida tofauti na Shinyanga! Na hili wala halihitaji shahada ya uchumi kulifahamu, WHY? Shughuli kubwa ya kiuchumi kwa Mkoa wa Lindi ni kilimo cha ufuta na korosho na kwa maeneo mengine ( ya Lindi) ni pamoja na nazi!! Kiasi kikubwa cha mauzo ya ufuta, korosho na nazi yanaenda moja kwa moja kwa wakulima/wananchi tofauti na mauzo ya dhahabu!
 
Last edited by a moderator:
Ritz Inawezekana kabisa alisema hivyo, Ila kwa bahati mbaya sikuweza kusiliza hiyo RFA au youtube. Ila hapa kinachojadiliwa ni kitu alichoandika mwenyewe na kutaka watu tujadlili..

Waweza kwenda katika kwenda kwenye Facebook yake.. Ndo nimetoa kila kitu huko... Na katika kuweka msititizo kitu cha kujadili ndo alikuja na hayo maandishi "

Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7."

Hayo si maneno yangu au ya mwana ukumbi yeyote ni maneno ya Zitto katika Facebook wall yake..

Alinda.

Watu wameamua Kuspin Kauli ya Zitto. Zitto ametoa statstic za mikoa zaidi ya kumi,nyie mmeamua kuchomoa mikoa miwili tu ya Kilimanjaro na Arusha, ili kumbambikizia Zitto dhana ya Ukabila. Hizi ni siasa za maji taka.
 
Last edited by a moderator:
Kuna uwezekano katoa clarification huko face book

Mkandara atakuwa shahidi mzuri tu kwasababu kuanzia jukwa lasiasa hadi hapa, yeye ni kinara wa hoja husika.

Msome hapo juu, '' Shinyanga inachangia Zaidi haipati stahiki, Kilimanjaro inachangia kidogo inapata stahiki''

Mwenzako team Adharusi kaja na data kabisa

Nashangaa hukuona hayo yote. All in all,tunajua alifanya shambulio la kisiasa dhidi ya mikoa ya kaskazini
Mkuu tafadhali, mimi nimesikia malalamiko yenu, nikataka kueleweshwa kwani alisema nini. Mkaja na haya maneno nami nikasema sioni ubaya hata kama ameitaja Kilimanjaro kwa sababu mwanasiasa yeyote unapozungumzia hoja lazima awe na mifano hai ili kujenga hoja yake. Na sikasisitiza hata Mbowe aliposema Wasukuma bado sikutafsiri vibaya iwapo lengo lake lilikuwa kuonyesha unyonyaji dhidi ya jamii hiyo. na nikaendelea kutoa mifano hata ya wanawake na kadhalika lkn wapi bado hamkutaka kuelewa.

Sisi wenyewe hujiuliza Kwa nini Tanzania masikini hali tulipata Uhuru sawa na nchi kama Singapore au Maleysia, wakati hao wenzetu hawana maliasili nyingi kama sisi?. Japo ni swali la kujiuliza lakini jibu lake lipo ama linaangukia wananchi wenyewe au Utawala mbovu. Ili kuwaondoa wananchi unaweza onyesha mchango wao ktk pato la taifa hivyo unabakia na moja tu la Uongozi Bora!. Hapa Maleysia ama Singapore hazihusiki, ni mifano hai inayokupa uwezekano wa kuwepo sababu ndani za kutoendelea kwetu.

Na ndivyo nilivyoelewa mimi, Zitto kaweza kufanya siasa za Kiitikadi, kuonyesha mfumo mbovu wa kiutawala na hivyo wananchi wachague chama chenye dhamira ya kweli ktk kubadilisha maisha yao. Mimi nadhani kwa sababu nyie mmezeoa siasa za majitaka basi kila kitu lazima kitafsirike katika misingi hiyo - Kutafuta mchawi.

Hii habari ya Siasa za kiitikadi ni ngeni kwenu na itawapa shida sana kuelewa pasipo kutenganisha hisia zenu maana kwenu siasa ni WATU. Ukimsema Mbowe au Dr.Saa umeua Chadema, Ukiwasema Wachagga una maana Chadema, Ukiwasema Waislaam ni CUF, Ukimsema Zitto unaua ACT, hizi ndizo siasa tulojengwa nazo kwa miaka 20 ilopita. Kumbe wenzetu wameondoka katika siasa hizo na kuchukua hatua nyingine kabisa ya kutumia ITIKADI na SERA kufafanua ukombozi ktk falsafa nzima ya UJAMAA wa Demokrasia.
 
Mkandara , kama kuna kundi lisiloguswa, una jukumu kama raia kuonyesha matatizo yaliyopo na wanajamvi watajumuika nawe.

Nakushauri uanzishe uzi kama huu ili tuchangie huko. Sisi tumeonyesha mfano kuwa pale tusipokubaliana napo tutaweka wazi. Hivyo una nafasi ya kufanya hivyo bila ku-adulterate mjadala, kuupindisha ili kuondoa ukweli unaomkabili supreme

Supreme leader anawajibika kwa kauli zake za uchochezi, za kutaka kuvuruga taifa.

Tunajua historia yake ni kuleta sintofahamu ndani ya vyama vya siasa. Inapovuka mipaka na kuingia katika utaifa, hatutakaa kimya.

Nawe pia usikae kimya kama wapo wanaotenda kinyume. Lakini pia usitake ku insinuate habari zako katika uzi usiohusika

Pili, kumwita supreme leader siyo sisi. Chama chake kinamtambua kama kiongozi mkuu.

Unless uje na tafasiri nyingine supreme leaderni tafsiri halali.

Ni kama vile Kim II sung(Grate leader), Kim Jong (Dear leader).

ACT wana mfumo kama huo, ambako Anna ni Mwenyekiti na Zitto ni supreme leader.

Kwa maneno mengine, ni kama Iran ambako kuna Rais wa nchi na kiongozi mkuu wa nchi kama Khomeni au Khemenei

Neno supreme leader lina maana kiongozi mkuu. La sivyo tuambie kiongozi mkuu kwa lugha ya kigeni anaitwa nani, nasi tutaheshimu

Supreme leader anaweza kuota ndoto zote bila kikwazo aukizuizi.

Ndoto zake zisielekee kuligawa na kulivuruga taifa kwa misingi ya ukanda.

Huko tutaingilia kati ndoto hizo kwani zitakuwa si ndoto bali njozi.

Tunajua njozi zinaweza kuwa na matokeo mabaya na hatutapenda matokeo hayo katika taifa letu.

Anaweza kufanya siasa hizo anakojua si Tanzania. Hatuta kaa kimya kamwe!

Chama cha supreme hakiwezi kulinganishwa na maono ya Nyerere.Tungekuomba umwache mzee Nyerere apumzike kwa Amani. Nyerere alipigania taifa,supreme anapigania kugawa nchi. Usifaninishe kichuguu na mlima Kilimanjaro

Hatuna wivu wala majungu, maneno anayesema mwenyewe. Waraka waliandika wenyewe, na sasa yupo katika rekodi akieneza siasa za kushambulia mikoa ya kaskazini dhidi ya kanda ya ziwa. Hatuwezi kukaa kimya wananchi wakichonganishwa na genge dogo lisilifokia watu 10 lenye kueneza uongo, uzushi na unafiki. Hatutakaa kimya asilani
Haya bado unaendelea na tabia yako ya USupreme yaani unataka kuchaguliwa watu ya kuandika. Kwa nini nianzishe mada nyingine wakati wewe unaweza andika lolote utakalo na huambiwi kaanzishe mada? Hivi kuanzisha mada humu JF inakupa nguvu ya kuambia watu waandke nini?.. Hii ndio tabia yenu na mnashindwa kujitazama wenyewe lakini wepesi sana kuchambua wengine..mada inahusu ACT kuwa mpini wa CCM hili la Supreme umelitoa wapi na kulifanya ndio mada? kwa nini wewe usianzishe mada nyingine tuijadli...

Kifupi Chadema na watu kama nyie mna tabia za Al - Shabab, Usipokuwa nasi wewe ni adui yetu, usiposilimishwa utauawa kisiasa. Ukiwa nasi hata kama sio muumini una haki zaidi. Mnapenda kutunga sheria za kujilinda wenyewe na kwamba nyie ni chaguo la Mungu na kwa nguvu zake mtashinda. Hizi siasa za Kimungu Mungu huku mkiwa hukumu watu wengine kama kwamba nyie ndio wasafi kusema kweli mimi zinanitisha sana maana unapompa Binadamu madaraka ya kumtumia Mungu basi jua atakuja na Utume wake - New world Order.
 
Mkandara,

..ni kweli mwanasiasa anatakiwa kujenga hoja kwa mifano hai.

..sasa mfano hai ambao Zitto alipaswa kuutumia kule Shinyanga ni kueleza matatizo yaliyoko ktk sekta za pamba, ufugaji, na wachimbaji madini wadogo-wadogo.

..mimi sikubaliani kabisa na hii habari ya kulinganisha mkoa mmoja vs mwingine, au kulinganisha jamii moja vs nyingine kwa namna ile alivyofanya Zitto.

..hapa Tz kuna umasikini mkubwa sana. vilevile uelewa wa wananchi wetu siyo mkubwa kiasi hicho. hii habari ya kulinganisha jamii moja vs nyingine inaweza kuleta chuki kuliko kutatua matatizo yaliyopo.

NB:

..kuna mahali eti tunaambiwa Lindi ni mkoa wa kumi kwa maendeleo. mimi nadhani taarifa hizi zinadhihirisha kwamba Tanzania hakuna maendeleo. period.

cc Ritz, Alinda, Mchambuzi, Nguruvi3
 
Mkuu Zitto anafahamu haya isipokuwa Zitto anazungumzia pia mikabtaba mibovu ya serikali ni sehemu ya mchango wa wananchi wa Shinyanga kuwa na maisha duni. Kiuchumi amechukulia GDP na matunda yake kayaona ktk HDI. Haina maana anawazungumzia Watu wa Kilimanjaro, Dar au Arusha isipokuwa anaonyesha uwezekano wa mkoa huo kuwa bora zaidi.

Wewe hukubaliananinkwa sababu unaamini katika kuficha ukweli. Mimi nakubali na napokea hoja yoyote hata kama ina madai ya Ubaguzi ndani yake yazungumziwe kama yalivyo maana tukumbuke tunapigana na UBAGUZI wa aina yoyote iwe dini, kabila gender na kadhalika na inapotokea ni muhimu kusema wazi na hata kulinganisha ili watu waone unachokieleza. Ubinafsi pekee ndio hutengeneza hisia za kujificha nyuma ya pazia japo ukweli upo. Nawaomba tu kina Nguruvi3 wasinielewe vibaya naposema haya wakaunganisha na Zitto maan tunazungumzia Transparency.

Kwa mfano, inakuwaje sisi rahisi kuzungumzia swala la Apartheid na utawala wa Makaburu tukasema kwa kutumia takwimu za Kimataifa kuwa Huko South au Zimbabwe, Wananchi weusi ni asilimia 90 lakini wanamiliki asilimia 30 tu ya Ardhi wakati wazungu walokuwa asilimia 10 wanamiliki asilimia 70. Tulifanya hivyo ili kueleza Ukweli na sio kuuficha kwa sababu nia na lengo ilikuwa kuondoa Ubaguzi huo sio kuchokonoa ili wanawanchi wachukiane maana tayari Ubaguzi ulikuwepo na ulitokana na mfumo wa Kibaguzi, haikuwa wananchi wazungu ndio wenye makosa isipokuwa Utawala wa South na Mandela alipopigania Uhuru wao alitaka USAWA katika muundo.

Kuna Mifano ya takwimu juu ya Tanganyika na Zanzibar unafikiri kuitumia kunaleta Udini baina ya bara na visiwani au kuna ukweli ambao wananchi wanatakiwa kuijua. Kuna tatizo gani kuizungumzia kwa nia safi pasipo watu kuanza kufikiria Udini ama Ukabila ikiwa watu wenyewe hawana hisia hizo?..

Tuachane na hayo, kinachonitisha mimi katika swala hili ni mtu kukataa matumizi ya mifano kama hii ina maana mnakataa ukweli fulani kwa kuficha jambo fulani, na mnapotetea jambo kama hili inanipa wasiwasi na nyie ya kwamba mpo tayari kuficha ukweli ili kulinda maslahi yenu japo siyajui. Shinyanga na Kilimanjaro ni mikoa wa Tanzania kote kuna wakazi wa makabila -Wachagga, Wasukuma na makabila mengine mengi tu wanaishi mikoa hiyo, hakuna mkoa wa kabila fulani hili limeshaondoka, iweje nyie muanze kufikiria kuitaja Kilimanjaro inahusiana na Uchagga na Shinyanga ni Wasukuma?.. Huoni kama nyie ndio mna tatizo la Ukabila ulojificha.
 
Kabla hatujasonga mbele ni lazima tusawazishe hii sintofahmu, hivyo basi bado nasisitiza hakuna sehemu nilipoandika neno "chuki" iwe kwa wakenya au kwa nafasi za kazi zinazochukuliwa na wakenya.. SIjaandika kitu cha namna hii kama papo nionyeshe.. Niko radhi kuomba msamaha.

I have treated this debate as a contact sport. Naona nimekuchezea rafu na sikukutendea haki. Niwie radhi na naomba msamaha.
 
Mkandara,

..hoja ya Zitto ni kwamba kuna dhuluma inayofanywa na Kilimanjaro na Arusha dhidi ya Shinyanga.

..sisi tukasema hilo siyo kweli. wachangiaji wenzetu,particularly Mchambuzi, wamempinga kwa hoja na data.

..ndiyo maana sisi wengine ktk kumsaidia, tukasema hoja hiyo inaweza kujadilika bila kusukumiana lawama baina ya jamii moja vs jamii nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara,

..ni kweli mwanasiasa anatakiwa kujenga hoja kwa mifano hai.

..sasa mfano hai ambao Zitto alipaswa kuutumia kule Shinyanga ni kueleza matatizo yaliyoko ktk sekta za pamba, ufugaji, na wachimbaji madini wadogo-wadogo.

..mimi sikubaliani kabisa na hii habari ya kulinganisha mkoa mmoja vs mwingine, au kulinganisha jamii moja vs nyingine kwa namna ile alivyofanya Zitto.

..hapa Tz kuna umasikini mkubwa sana. vilevile uelewa wa wananchi wetu siyo mkubwa kiasi hicho. hii habari ya kulinganisha jamii moja vs nyingine inaweza kuleta chuki kuliko kutatua matatizo yaliyopo.

NB:

..kuna mahali eti tunaambiwa Lindi ni mkoa wa kumi kwa maendeleo. mimi nadhani taarifa hizi zinadhihirisha kwamba Tanzania hakuna maendeleo. period.

cc Ritz, Alinda, Mchambuzi, Nguruvi3

Jokakuu:

Katika posti zilizotangulia inaonyesha kuwa Mbowe alisema maneno kama hayo ya Zitto. Tofauti iliyopo inaonyesha kuwa Zitto alilinganisha na kanda ya kaskazini. Na hivyo kauli yake kuwa na negative connotation kwa baadhi ya watu, ukichukulia jinsi talaka yake na CDM ilivyokuwa na migogoro.

Kama Zitto angesema kuwa Shinyanga haipati mapato kama mikoa au kanda zingine (bila kutaja majina), huu mjadala usingekuwepo. Au maneno hayohayo aliyosema angeyasema akiwa ndani ya CDM, longolongo lisingetokea.

Swali linalokuja je uhuru wake wa kujieleza unaanzia na kunaishia wapi?

Tumehamua kufuata western democracy, ni lazima tukubali faida na hasara zake. Kuna wanasiasa watakuwa edgy and controversial.
 
Mkandara,

..hoja ya Zitto ni kwamba kuna dhuluma inayofanywa na Kilimanjaro na Arusha dhidi ya Shinyanga.

..sisi tukasema hilo siyo kweli. wachangiaji wenzetu,particularly Mchambuzi, wamempinga kwa hoja na data.

..ndiyo maana sisi wengine ktk kumsaidia, tukasema hoja hiyo inaweza kujadilika bila kusukumiana lawama baina ya jamii moja vs jamii nyingine.

Jokakuu:

You are implying kuwa Zitto alisema hivyo. Na ingekuwa kweli kama Tanzania ingekuwa na mikoa mitatu tu: Shinyanga, Arusha na Kilimanjaro. Lakini kwa sababu Tanzania ina mikoa zaidi ya 25, Shinyanga haiwezi kudhulumiwa na Arusha na Kilimanjaro pekee yake.
 
Mkandara,

..hoja ya Zitto ni kwamba kuna dhuluma inayofanywa na Kilimanjaro na Arusha dhidi ya Shinyanga.

..sisi tukasema hilo siyo kweli. wachangiaji wenzetu,particularly Mchambuzi, wamempinga kwa hoja na data.

..ndiyo maana sisi wengine ktk kumsaidia, tukasema hoja hiyo inaweza kujadilika bila kusukumiana lawama baina ya jamii moja vs jamii nyingine.
JokaKuu.

Hiyo siyo hoja ya Zitto unafanya makusudi kuchagua mikoa miwili, Zitto kaelezea mfumo mzima ametaja mikoa mingi msome.

Zitto.
Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu.
 
Last edited by a moderator:
Mkandara,

..hoja ya Zitto ni kwamba kuna dhuluma inayofanywa na Kilimanjaro na Arusha dhidi ya Shinyanga.

..sisi tukasema hilo siyo kweli. wachangiaji wenzetu,particularly Mchambuzi, wamempinga kwa hoja na data.

..ndiyo maana sisi wengine ktk kumsaidia, tukasema hoja hiyo inaweza kujadilika bila kusukumiana lawama baina ya jamii moja vs jamii nyingine.
Ikiwa hotuba ya Zitto ni hiyo hapo juu aloiweka Ritz ebu nifafanulie ni wapi kasema Dhulma inafanywa na mikoa hiyo na sio mfumo (mrengo) wa serikali tawala, pengine mimi sielewi!
 
Mkuu tafadhali, mimi nimesikia malalamiko yenu, nikataka kueleweshwa kwani alisema nini. Mkaja na haya maneno nami nikasema sioni ubaya hata kama ameitaja Kilimanjaro kwa sababu mwanasiasa yeyote unapozungumzia hoja lazima awe na mifano hai ili kujenga hoja yake. Na sikasisitiza hata Mbowe aliposema Wasukuma bado sikutafsiri vibaya iwapo lengo lake lilikuwa kuonyesha unyonyaji dhidi ya jamii hiyo. na nikaendelea kutoa mifano hata ya wanawake na kadhalika lkn wapi bado hamkutaka kuelewa.

Sisi wenyewe hujiuliza Kwa nini Tanzania masikini hali tulipata Uhuru sawa na nchi kama Singapore au Maleysia, wakati hao wenzetu hawana maliasili nyingi kama sisi?. Japo ni swali la kujiuliza lakini jibu lake lipo ama linaangukia wananchi wenyewe au Utawala mbovu. Ili kuwaondoa wananchi unaweza onyesha mchango wao ktk pato la taifa hivyo unabakia na moja tu la Uongozi Bora!. Hapa Maleysia ama Singapore hazihusiki, ni mifano hai inayokupa uwezekano wa kuwepo sababu ndani za kutoendelea kwetu.

Na ndivyo nilivyoelewa mimi, Zitto kaweza kufanya siasa za Kiitikadi, kuonyesha mfumo mbovu wa kiutawala na hivyo wananchi wachague chama chenye dhamira ya kweli ktk kubadilisha maisha yao. Mimi nadhani kwa sababu nyie mmezeoa siasa za majitaka basi kila kitu lazima kitafsirike katika misingi hiyo - Kutafuta mchawi.

Hii habari ya Siasa za kiitikadi ni ngeni kwenu na itawapa shida sana kuelewa pasipo kutenganisha hisia zenu maana kwenu siasa ni WATU. Ukimsema Mbowe au Dr.Saa umeua Chadema, Ukiwasema Wachagga una maana Chadema, Ukiwasema Waislaam ni CUF, Ukimsema Zitto unaua ACT, hizi ndizo siasa tulojengwa nazo kwa miaka 20 ilopita. Kumbe wenzetu wameondoka katika siasa hizo na kuchukua hatua nyingine kabisa ya kutumia ITIKADI na SERA kufafanua ukombozi ktk falsafa nzima ya UJAMAA wa Demokrasia.

Tatizo unaowaambia kina Nguruvi3 wameamua kwa makusudi kumlisha maneno Zitto au wameamua kufugia Nywele vichwa vyao
 
Last edited by a moderator:
Ikiwa hotuba ya Zitto ni hiyo hapo juu aloiweka Ritz ebu nifafanulie ni wapi kasema Dhulma inafanywa na mikoa hiyo na sio mfumo (mrengo) wa serikali tawala, pengine mimi sielewi!
Pamoja na juhudi za kututoa kwenye mada ya Nguruvi3 inayosema; Re: Duru za siasa: Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani, naomba nikuulize Mkandara, kwa nini unaamini hayo ndiyo maneno aliyoyatamka Supreme Leader akiwa Shinyanga? Sijui kwa nini leo umwamini Ritz kwa kutoa nukuu anayodai ni ya Zitto...huu ushikaji umeanza lini! Kabla sijarudi kwenye mada na mimi naomba nikukumbushe kidogo onyo lililotolewa na Kamati ya Usaliti chini ya Samson Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo, nanukuu;

Mkakati wa Mabadiliko2013 said:
Udhaifu wa tunayemtaka:

Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu.

Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake.

Mkuu Mkandara, mtu anayeongelewa hapa ni huyo huyo aliyekuwa anatengenezewa njia ili siku akitua chamani moja kwa moja atawazwe kuwa Kiongozi Mkuu (hata katiba ilikuwa inamsubiri!). Hapo tahadhari inatolewa jinsi asivyokuwa na busara na alivyo mwepesi katika kutoa matamshi bila kufikiria madhara yake katika jamii. Lakini kama nilivyotahadharisha hapo mwanzo haya tuyaache turudi kwenye mada iliyoko mezani...Re: Duru za siasa: Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani!

Supreme Leader hakuitaja mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kwa bahati mbaya, aliitaja kwa kukusudia lakini kama kawaida yake hakuzingatia ni jinsi gani matamshi yake yangepokelewa katika jamii. Ni katika mikakati hiyo hiyo aliwaita wana UKAWA wasakatonge bila kufikiria athari zake kwa watu wanaopigania mabadiliko ya kweli katika nchi hii. Yeye alichokusudia ni kuzidi kuwafurahisha wale ambao alikuwa na hakika wangempigia vigelegele kwa matamshi yake hayo...nasikia sasa anajuta, kasahau majuto ni mjukuu!
 
Mkuu Mkandara , the more supreme’s zelotes open up, they expose him in precarious situation.

Hayo maneno si ya supreme leader. Tangu mjadala uanze jukwaa la siasa ulikoshiriki vema hadi wakati huu, hujawahi kutumia maneno ‘stahiki’

Unachokifanya ni spinning inayoonyesha ulivyotekwa na fikra za ulaghai kama supreme, wanasema ‘disingenuous’’

Umetaja K’njaro na Shinyanga ili kupunguza wigo wa eneo supreme aliloshambulia .

Tuweke rekodi sawa, supreme alishambulia K’njaro na Arusha kutokea
Shinyanga na Mwanza. No more no less

Tutayatumia maneno yako kukuonyesha twisting haimsaidii supreme

1 ‘’Shinyanga wanachangia sana hawapewi stahiki,Kilimanjarowanachangia kidogo wanapewa stahiki’’
Tunarudia kusisitiza haya si maneno yake,lakin tuyajadili kama ulivyoyaumba

Historia : Tume ya Kamala ikikusanya maoni (EAC)kushirikisha Burundi na Rwanda, Zitto alisema bungeni ‘Msiogope EAC,MbonaKilimanjaro wameendelea kuliko Kigoma?

Ukisoma kauli yake(kwa mujibu wako) Supreme leader anasema K’njaro inapata stahiki, Shinyanga haipati stahiki(ukiondoa Arusha) ili kupunguza wigo wa ‘’shambulio’’ la kisiasa alilofanya

Tunakuuliza, kwanini alisema K’njaro inapata stahiki yake?

Je,alikuwa na takwimu za kuthibitisha hilo? Kwanini alitumia K’njaro na si mikoa 6 iliyoko mbele ya K’njaro?

Ni stahiki gani inayopata ambayo Shinyangahaipati?

Je, hii si historia ya chuki dhidi ya K’njaro kama alivyoanza wakatiwa EAC?

Tungependa wewe na Zitto mtuonyeshe stahiki zipi na kiwango gani ambazo Shinyanga inanyimwa na Arusha/K’njaro zinapata.

Ndio maana tunasema, kadri mnavyoleta utetezi usio na mashiko, mnamweka mahali pabaya kisiasa.

Leo tunajua kumbe Zitto ana data zinazoonyesha K’njaro inapata stahiki dhidi ya Shinyanga, na wala si Sumbawanga, Tabora au Lindi

Mnajribu kutuonyesha ‘attack’ ya Zitto-ACT dhidi ya mikoa ya kaskazini ni ya kukusudia kabisa.

kwa hiyo ndo unajidili ACT? badili kichwa cha habari kiwe Zitto
 
Mkuu Nguruvi3 ACT bado ni mpini wa CCM kumaliza wapinzani? Maana naona zile mbwembwe za mpini zimepungua ghafla au ndo unajipanga kuja na kasi,ari na nguvu mpya??

Ila swali letu bado liko pale pale pesa ya kuendesha mkutano mkuu wa chama, pesa za kuzunguka mikoa 11 zilitoka wapi?

Pamoja na zunguka mikoa 11 waliweza kupata wanachama 7000tu.. Kwangu mimi hii ni idadi ndogo sana ukiangalia umaarufu wa Zitto, nguvu zlizotumika kutangaza chama chake, watu walivyokuwa wanajaa katika mikoni yake nilitegemea idadi kubwa zaidi ya hii.

Hii si dalili nzuri kwa kijana mdogo kama Zitto kupata mwitikio mdogo kiasi hiki. Sijui ngoja tuone katika uchaguzi mkuu ni vipi ACT itapanda chati.

7000 kwako ni ndogo,ila ACT kwao ni mafanikio,mlivyo na Nongwa ingetokea amepata wanachama million tano bado mngeZoZa hamna jema nyinyi,kumbuka thread ilianza kabla ya Zitto hajapewa kadi ACT
 
Ikiwa hotuba ya Zitto ni hiyo hapo juu aloiweka Ritz ebu nifafanulie ni wapi kasema Dhulma inafanywa na mikoa hiyo na sio mfumo (mrengo) wa serikali tawala, pengine mimi sielewi!
Mkandara, rangi yako inazidi kunawiri. Unakumbuka jukwaa lasiasa ulijadili nini?
Adharusi, unakumbuka jukwaa la siasa ulijadili nini?Duru ulileta nini?

Hiyo siyo hotuba ya Zitto. Wabe ambaye ni right handman wa supreme aje hapa atueleze nini alisema Zitto

Tuna rekodi zenu nyote. Ritz hayo si maneno ya Zitto , ni sawa nay ale ya ‘Kilimanjaro inachangia kidogo inapata stahiki, Shinyanga Zaidihaipati stahik'' Tulielezwa na Lieutenant wa Zitto.

Hivyo tuna info za kutosha kuhusu hotuba ile iliyozua vurugu kule jukwaa la siasa, na right handmen wa Supreme wote wanajua hiyo si hotuba. Usipotoshe umma.
Tunarekodi za kutosha JF njooni mthibitishemaneno ya Ritz
 
Back
Top Bottom