Sitaki kuwaharibia mjadala lakini kuna kitu sijakielewa vizuri
Mkandara kuna sehemu umeandika kuwa Kodi si pato la Taifa bali ni pato la Serikali. Na hapo umeandika kuwa kodi ni sehemu ya pato la Taifa. Swali langu ni je kuna tofauti kati ya Kodi pato la taifa na kodi pato la serikali? Maana mie kwangu mie tunapongelea kuhusu kodi sioni tofauti kati ya serikali na taifa. Ufanunuzi wako tafadhali.
Swali la pili kwako na
Mchambuzi
Tusema wanakijji wamelima shamba lao la mihogo na kuvuna mihongo yenye thamani ya mil.20, hizi mil 20 zitahesabika katika pato la Taifa!? (kama nimeelewa vizuri) Lakini hawa wanakijiji hizo mil. 20 wasipozilipia kodi labda kwa sababu ya msamaha ua ukwepaji kodi.. Je likapokuja swala la "gawio" katika maendeleo ya shughuli za jamii, je mgao utalenga hizo mil 20 au utalenga mchango wao wa kodi/ushuru?
(natumaini mtalielewa ili swali maana hizi taaluma zinawenyewe sisi wengine ni kuchota elimu tu)
Alinda,
Mfano wako ni mzuri sana kutusaidia kuliweka suala hili sawa pengine for good. Wanakijiji wakilima na kuvuna mihogo yenye thamani ya soko ya shillingi milioni 20, huo utakuwa ni mchango wao kwa pato la mkoa na hata taifa (GDP). Na hiyo itatoa fursa kwa PATO LA SERIKALI (KODI) kupatikana kupitia tozo katika muktadha wa huo uzalishaji wa mihogo.
Tukirudi kwa wakulima hawa wa Mihogo - If its a business case, watatoa gharama zote na kubakisha faida. Wakulima hawa watakuwa na uhuru wa kutumia Faida itakayobakia kwa jinsi watakavyoamua, hata wakiamua kuachana na kilimo chao na kula mtaji wote. Lakini lipo jambo muhimu hapa, nalo ni kwamba moja ya gharama katika uzalishaji wa bidhaa na huduma, tena gharama ambayo ipo kwa mujibu wa sheria, ni KULIPA KODI, unless kuna tax exemption ambayo pia nayo lazima iwe kwa mujibu wa sheria. Kwahiyo kama sehemu ya gharama za uzalishaji wa bidhaa (mihogo kwa mfano), wakulima hawa watalazimika kulipa kodi kabla ya kupiga mahesabu ya Faida ya jasho lao. Swali linalofuata ni je:
· Kwanini Kulipa kodi ni kwa mujibu wa sheria?
Ni kwa sababu, katika taifa au uchumi wowote ule, zipo aina mbili ya Goods namely - Public goods and Private goods. Awali tulijadili maana ya public goods na kwanini zinaitwa hivyo, kwa mfano taa za barabarani (security lights), traffic lights, bus station, national defense system, light house (for ships) n.k. Bidhaa hizi (Public goods) zina two main features namely (1) Non Excludable and (2) Non-Rivalrous. Kwa maana nyingine, in order for a good to qualify as a "public good", it must be non-excludable and non-rivalrous. Ni such feature ndio hupelekea umuhimu wa serikali kugharamia provision of such goods. Kwanini? Mfano mzuri ambao hutumiwa in classical economics ni light house(Mnara wa meli). Tuujadili mfano huu:
Mnara wa meli ni "non-excludable" kwa sababu its impossible kuzuia meli zisitumie au zisifaidike na mnara husika hata kama hazikuchangia katika kugharamia ujenzi wa mnara huo. Lakini pamoja na hayo, kwa usalama wa meli, abiria na mizigo, meli zote lazima zitumie na zifaidike na mnara huo. Mnara wa meli vile vile ni Non‐rivalrous kwa sababu kama tayari meli nyingi zinafaidika na mnara uliopo, hakuna extra cost itakayotokea kwa kuruhusu meli nyingine kufaidika nan a mnara husika. Hii ni tofauti na Private goods kama mkate, boksi la juisi ambazo zote ni rivalrous good kwa sababu the more these are provided to someone or to some people itahitaji more and more goods to be produced vinginevyo kutakuwa na shortage. Kwa private goods, such chaarcteritics ndio zinatoa incentives za kuzizalisha na kusambaza kibiashara. Lakini for public goods, the fact kwamba ni non excludable and non-rivalrous, uzalishaji au provision yake by private sector huwa haina tija. Lakini kwa vile such goods ni muhimu sana, serikali lazima iingie gharama kwa maslahi ya taifa. Gharama za serikali katika jambo hili ni KODI, na sio GDP.
Nimetoa mfano huu kwa makusudi. Tukichukulia wananchi wa Shinyanga, Arusha n.k, wote wana mahitaji kama haya mengi tu ambayo bila ya ushiriki wa serikali, provision of such goods haitakuwepo, na italeta a huge crisis. Tukitumia mfano wa wakulima wa Mihogo, iwapo wakulima wa Mihogo uliowatolea mfano wanazalisha zao hili lenye market value tuseme ya T.sh 2,000,000, sasa ili mazao yaweze kufika Sokoni, watalazimika kutumia barabara. Barabara ni moja ya Public Goods, whether ni barabara chini ya Tanroads au zile chini ya Manispaa husika. Katika hali ya kawaida, wakulima hawa watahitajika kulipa kodi ya aina Fulani ili serikali iweze kuendelea kugharamia matumizi ya barabara husika na wakulima hawa lakini pia na watumiaji wengine. Provision of such services ndio maana halisi ya KEKI YA TAIFA. Na uwepo wa Fedha kugharamia mahitaji haya ndio maana hali ya SUNGURA MKUBWA au SUNGURA MDOGO, kule kwenye mijadala Bungeni.
Mgao halali kwa Wananchi?!!?
Mgao kwa wananchi maana yake ni kugawana kwa keko ya taifa. Kugawana kwa keki ya taifa maana yake ni uwepo wa sungura mkubwa na sio mdogo. Sungura hapa maana yake ni MAPATO YA KODI, Not GDP. Kwahiyo katika hali ya kawaida, mgao wa serikali kwa wananchi husika ni lazima utokane na michango ya wananchi husika kwenye PATO LA SERIKALI (KODI), ili wananchi hao wapate huduma wanazostahili. Vinginevyo kama wakulima hawa wamevuna mihogo yenye thamani ya shillingi milioni 20 (na huu ndio mchango wao kwa PATO LA TAIFA/GDP), lakini wakatumia pato hilo kugawana kwa matumizi binafsi na kukwepa kodi, wakulima hao watakuwa na uhalali gani wa kudai kwamba hawapati keki ya taifa? Ndio maana kodi ipo kwa mujibu wa sheria, na upatikanaji wa huduma za kijamii (keki ya taifa) ni lazima iendane na mchango wa wananchi au mkoa husika katika mapato ya serikali.
Ndio maana shughuli za uzalishaji zinatozwa kodi. Shughuli zote za uzalishaji (GDP Output) ambazo hazilipi kodi na kufanya hivyo kinyume cha sheria, maana yake ni kwamba mapato yake yanaenda kwenye mifuko ya wazalishaji kwa matumizi ambayo hayahusu umma bali maisha binafsi. Jamii ya aina hiyo haina uhalali wa kulalamika kwamba wanakosa keki ya taifa. Ndio maana suala la kodi katika demokrasia zilizokomaa ni suala muhimu sana katika chaguzi kuu. Mara nyingi, ceteris paribus, wananchi huwa more concerned zaidi with how their taxes are being spent kuliko suala la GDP.